Mwenyezi Mungu alinielekeza kwenye Njia ya Kupata Utakaso

10/01/2020

Na Gangqiang, Marekani

Nilikuja Singapore peke yangu mnamo mwaka wa 2007 ili kujaribu kujipatia riziki. Singapore kuna joto sana mwaka mzima, kwa hivyo nilikuwa nikiloa chepe kwa jasho kila siku kazini. Palikuwa na taabu, na zaidi ya hayo nilikuwa mahali ambapo sikupajua kabisa bila jamaa au marafiki wowote—maisha yalihisi ya kuchosha na ya taabu sana. Siku moja mnamo Agosti, nilipokea kijikaratasi chenye matangazo ya injili nilipokuwa njiani kutoka kazini ambacho kilisema: “Lakini Mungu wa neema yote, ambaye ametuita kwa utukufu wake wa milele kupitia kwa Kristo Yesu, baada ya nyinyi kuteseka kwa muda mfupi, atawakamilisha, atawaimarisha, atawapa nguvu, na atawapumzisha” (1 Petro 5:10). Nilihisi ukunjufu moyoni mwangu nilipokuwa nikiyasoma maneno haya. Baada ya hapo, nilienda kanisani na kaka mmoja, ambapo mapokezi yenye shauku kutoka kwa kina ndugu, ambao waliulizia ustawi wangu, yalinifanya nihisi ukunjufu wa familia ambao sikuwa nao kwa muda mrefu. Macho yangu yalitokwa na machozi ghafla—nilihisi kama tu kwamba nilikuwa nimekuja nyumbani. Kuanzia wakati huo, kwenda kanisani kila Jumapili kulikuwa jambo la lazima kwangu.

Nilibatizwa mwezi huo wa Desemba, nikaingia rasmi kwenye njia ya imani. Katika ibada moja ya kanisa, nilimsikia mhubiri akisoma kutoka sura ya 18, aya ya 21 hadi 22 katika Mathayo: “Kisha Petro akakuja kwake, na kusema, Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba? Yesu akasema kwake, sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba.” Niliposikia haya, niliwaza moyoni mwangu: “Msamaha na uvumilivu wa Bwana Yesu unawezaje kuwa mkubwa hivi? Yeye huwasamehe watu sabini mara saba. Laiti wanadamu wangeweza kufanya hivi, basi kusingekuwa na kugombana, ila upendo na ukunjufu pekee!” Niliguswa sana na maneno ya Bwana, na nikaamua kutenda kulingana na mafundisho Yake.

Miaka miwili au mitatu baadaye, bosi wangu alinikabidhi madaraka ya kusimamia eneo la ujenzi, kwa hivyo nilitia bidii zangu zote kazini na nikacha kuhudhuria mikutano mara kwa mara kama ilivyokuwa. Baadaye nilitambulishwa na rafiki kwa Bw. Li, mfadhili wa biashara, na tukaanzisha kampuni ya ujenzi pamoja. Nilifurahi sana, na niliazimia kuanza kufanya kazi kwa bidii kabisa. Kisha niliingia kabisa katika hekaheka za pesa na nikaacha kabisa kwenda kanisani kwenye mikutano. Nilitaka miradi ifanyike vizuri ili nipate sifa za wengine kwa ustadi wangu, kwa hivyo nilidai mengi zaidi kutoka kwa wafanyakazi. Niliwakemea kila nilipoona kuwa walikuwa wamefanya kitu ambacho hakikuwa sahihi au hakikufikia matakwa yangu. Kiongozi wa timu mara nyingi alibubujikwa na machozi kwa sababu ya tabia yangu mbaya. Wafanyakazi waliogopa kila waliponiona na hata walijificha. Hata watu ambao walikuwa marafiki wazuri hawakuwa wema kwangu na hawakutaka kuwa na imani kwangu tena. Kuona jambo hili kulihuzunisha sana. Bwana Yesu hutufunza tuwasamehe wengine sabini mara saba, na tumpende jirani yetu kama tunavyojipenda. Hata hivyo, sikuwa nimetia hayo katika vitendo hata kidogo, hata mara moja. Kwa hivyo huko kulikuwaje kuwa Mkristo? Nilijua kuwa nilikuwa nikitenda dhambi na mara nyingi nilimwomba Bwana, nikikiri na kutubu. Niliamua kubadilika. Lakini kila wakati jambo lilipotokea, bila kujijali bado nilitenda dhambi. Nilichukizwa sana.

Mnamo Agosti mwaka wa 2015, tulisimamisha shughuli za biashara kwa sababu kampuni hiyo haikuwa ikifanya vizuri, na nikarudi nyumbani. Huku nikiwa mwenye huzuni na taabu, nilikunywa tu pombe na kucheza kamari kila siku. Mke wangu aliponiambia kwamba nilipaswa kuacha kunywa pombe, nilimpigia tu kelele: “Ni pesa zangu, nilizichuma, na nitazitumia jinsi ninavyotaka….” Hakukuwa na kitu ambacho angefanya, kwa hivyo aliketi tu pale na kulia. Kila wakati nilipoonyesha hasira yangu, nilihisi kujuta na nilijichukia, lakini sikuweza kujidhibiti kabisa. Kufikia wakati huo nilikuwa nimepoteza kabisa uzuri wote wa Mkristo; tabia na mwenendo wangu vilikuwa sawa kabisa na vya mtu asiyeamini.

Katika uchungu na kutojiweza kwangu, nilirudi kanisani kuhudhuria mikutano tena. Katika kipindi hicho, nilikuwa nikimwomba Bwana Yesu kila wakati: “Eh, Bwana! Nimefanya mambo mengi ambayo sikutaka kuyafanya, nimeyasema mambo mengi yanayowaumiza wengine. Nimekuwa nikiishi katika dhambi na kuasi dhidi Yako. Kila mara ninapotenda dhambi, mimi hujuta na kujichukia sana, lakini siwezi kujidhibiti kabisa! Mimi hukiri dhambi zangu usiku, lakini mchana mimi hurudia tena njia zangu za zamani na kutenda dhambi tena. Ee Bwana! Nakusihi Uniokoe, naweza kufanya nini ili kuacha dhambi?”

Siku ya Mwaka Mpya wa mwaka wa 2016, nilienda kwenye nchi ya Marekani—nilikuwa nimekuja jijini New York kuchuma pesa kiasi. Niliendelea kwenda kanisani wakati ambapo sikuwa na kazi na nikajiunga na kikundi cha waombaji, nikisoma Biblia na kusali pamoja na ndugu wengine. Kule, nilifahamiana na dada mmoja anayeitwa Qinglian. Siku moja, Dada Qinglian alinipigia simu akisema kwamba kulikuwa na habari njema aliyotaka kushiriki nami. Nilisema, “Habari ipi njema?” Alisema, “Kuna mmisionari atakayetutembelea. Je, unataka kwenda kumsikia akiongea?” Nikasema, “Vyema! Wapi?” Kisha akanipangia wakati wa kwenda nyumbani kwake.

Nilienda nyumbani kwa Dada Qinglian siku hiyo. Ndugu wengine kadhaa walikuwapo, na baada ya kukutana na kusalimiana, sote tulianza kujadiliana kuhusu Biblia. Ushirika wa Dada Zhao ulikuwa wenye kutia nuru na kuadilisha sana kwangu. Kisha nikamwambia juu ya hali yangu ya kila siku ya kutenda dhambi na kukiri, na uchungu wa kutoweza kuepuka dhambi, na nikatafuta msaada wake. Katika ushirika, alisema kwamba hata baada ya sisi kuanza kumwamini Bwana, bado tunatenda dhambi wakati wote, na kwamba kuishi maisha katika mzunguko usioisha wa kutenda dhambi mchana na kukiri usiku, kamwe kutoweza kuepukana nao, hakukuwa tatizo lililonitatiza mimi pekee. Badala yake lilikuwa tatizo ambalo waumini wote walikuwa nalo. Kisha Dada Zhao akatutaka tutazame video ya masimulizi fulani ya maneno ya Mungu. Maneno hayo yalikuwa haya: “Kubadilisha tabia ya mwanadamu huanza na maarifa ya kiini chake na kupitia mabadiliko katika mawazo yake, asili, na mtazamo wa akili—kwa njia ya mabadiliko ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndio mabadiliko ya kweli yatapatikana katika tabia ya mwanadamu. Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili, kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu).

Niliguswa sana, nikifikiri, “Si yanazungumza kunihusu? Mimi huwaangalia wengine kwa dharau kila wakati, nikiwakaripia kwa ajili ya hili au kuwakemea kwa ajili ya lile. Sina maadili na mantiki, na nimepoteza salio lolote la adabu takatifu.” Maneno haya yote yalipenya ndani yangu kabisa. Sikuwa nimesoma kitu kama hicho hapo awali, wala sikuwa nimesikia mhubiri yeyote akihubiri mahubiri ya aina hiyo. Nilikuwa nimehuzunishwa na kutenda dhambi kwangu kwa mara kwa mara, lakini bado sikuwa nimeweza kujitenga na vizuizi vya dhambi. Maneno haya yalinionyesha njia ya kuacha dhambi, na nilishangaa: Haya yameandikwa vizuri sana. Ni nani ambaye aliweza kuyaandika?

Dada Zhao aliniambia kuwa hili lilikuwa neno la Mungu, kwamba Bwana Yesu alikuwa tayari amerudi katika mwili, na kwa sasa Alikuwa akifanya kazi ya kuwahukumu na kuwasafisha watu kupitia neno Lake katika siku za mwisho. Sikuthubutu kuamini masikio yangu kabisa. Ni muumini yupi asiyetamani kurudi Kwake? Ghafla niliposikia habari hii ya kurudi kwa Bwana, nilifurahi sana kiasi kwamba sikujua la kufanya: Je, Bwana alikuwa amerudi kweli? Nilimwomba kwa shauku aendelee na ushirika wake. Dada Zhao alisema, “Bwana Yesu kwa kweli amerudi, na Yeye ni Mwenyezi Mungu—Kristo mwenye mwili katika siku za mwisho. Ameonyesha ukweli wote ili kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu, na Ameanza kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Atatuokoa kabisa kutoka kwa utawala wa Shetani, ambao tumefungwa na asili yetu ya kishetani na tunaoishi katika dhambi ambayo hatuwezi kujiongelesha. Mwishowe tutapata wokovu kamili na kupatikana na Mungu. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alitekeleza kazi ya ukombozi tu; Alitukomboa kutoka dhambini na Akasamehe dhambi zetu ili tusije tukalaaniwa tena chini ya sheria. Ijapokuwa Bwana alitusamehe dhambi zetu, hakusamehe asili yetu ya kishetani au tabia zetu za kishetani. Kiburi, ujanja, ubinafsi, ulafi, uovu, na tabia nyingine potovu bado zimo ndani ya mwanadamu. Hivi ni vitu ambavyo vina kina zaidi na ni kaidi zaidi kuliko dhambi. Ni hasa kwa sababu tabia hizi za kishetani na asili ya kishetani hazijatatuliwa ndiyo tunaendelea kutenda dhambi bila kujijali, na hata tunatenda dhambi ambazo ni kubwa zaidi kuliko kukiuka sheria. Kwa mintarafu ya Mafarisayo wakati ule, je, si sababu ya wao kumpinga na kumlaani Bwana, hadi kufikia wakati ambapo walimsulubisha Yesu, ni kwamba asili ya mwanadamu yenye dhambi haikuwa imetatuliwa? Kwa kweli, sote tunatambua hili sana kwa sababu sisi wenyewe tunadhibitiwa na tabia hizi potovu. Kwa hivyo, sisi husema uongo mara nyingi, hutenda kwa udanganyifu, tu wenye kiburi, na huwakaripia wengine kwa lengo la kujionyesha tu bora. Tunajua wazi kuwa Bwana anataka tuwasamehe wengine na tupende jirani yetu kama tunavyojipenda, na bado hatufanyi hivyo. Watu hufanyiana njama, hushindania umaarufu na faida, na hawawezi kuelewana kwa amani. Wakati wa magonjwa, misiba ya asili au iliyosababishwa na mwanadamu, bado tunamlaumu Mungu, na hata tunamkana au kumsaliti Mungu. Ukweli huu unaonyesha kuwa tusipotatua asili yetu ya kishetani na tabia za kishetani, basi kamwe hatutaweza kuepuka maisha haya ya mviringo wa kutenda dhambi na kukiri, kisha kukiri na kutenda dhambi. Kwa hivyo, ili kumwokoa mwanadamu kabisa toka dhambini, ni muhimu kwa Mungu kufanya hatua ya kazi Yake ya hukumu na utakaso ili kutatua asili yetu yenye dhambi. Hivi pekee ndivyo tunavyoweza kutakaswa na kuokolewa kabisa na Mungu, na kupatikana na Yeye. Hebu tusome maneno machache yaliyoteuliwa kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu na utafahamu.”

Dada Zhao alifungua kitabu cha neno la Mungu na kuanza kusoma: “Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). “Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Dada Zhao alisema katika ushirika: “Sasa kwa kuwa tumesoma maneno haya ya Mungu, tunaelewa ni kwa nini kila wakati sisi hufungwa na asili yetu ya kishetani na hatuwezi kujiondolea dhambi, siyo? Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu alifanya kazi ya ukombozi tu, si kazi ya siku ya mwisho ya kuhukumu, kusafisha, na kuwaokoa watu kabisa. Kwa hivyo bila kujali jinsi tunavyokiri dhambi zetu na kutubu, jinsi tunavyojaribu kujishinda, jinsi tunavyofunga na kusali, hatutaweza kufanikisha kuwa huru kutokana na dhambi. Hiyo inamaanisha kwamba ikiwa tunataka kuachana na utumwa na udhibiti wa asili yetu yenye dhambi, kupitia tu kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu bado hakutoshi. Lazima tukubali kazi ya hukumu inayofanywa na Bwana Yesu aliyerejea. Hii ni kwa sababu kwa kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, Mungu anaonyesha vipengele vingi vya ukweli ili kuhukumu na kufunua asili ya kishetani ya kumpinga na kumsaliti Mungu. Anafunua tabia ya Mungu yenye haki, takatifu, isiyokosewa, Akiwaruhusu mwanadamu aone waziwazi ukweli wa kupotoshwa kwake kwa kina na Shetani kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, kujua kwa kweli tabia ya Mungu yenye haki ambayo haivumilii kosa la mwanadamu, kukuza moyo wa kumcha Mungu, na hivyo kubadilisha na kusafisha tabia ya kishetani ya mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Katika kuadibu kwa Mungu na hukumu Yake adhimu na yenye ghadhabu tunamwona Mungu uso kwa uso. Kama upanga wenye sehemu mbili zenye makali, neno la Mungu hupenya mioyoni mwetu, huonyesha asili yetu ya kishetani ya kumpinga na kumsaliti Mungu na hata tabia zetu potovu ndani kabisa ya mioyo yetu ambayo sisi wenyewe hatuna njia ya kuzifichua. Linatufanya tuone kwamba kiini cha asili yetu kimejawa na tabia za kishetani kama kiburi, majivuno, ubinafsi, uovu, udanganyifu, na ujanja, kwamba sisi hatuna mfanano wa kibinadamu hata kidogo, na kwamba sisi tu mfano wa Shetani kabisa. Ni wakati huo tu ndipo tunaposujudu mbele za Mungu, tukianza kujichukia na kujilaani. Wakati huo huo, pia tunatambua kwa kina kuwa neno lote la Mungu ni ukweli, lote ni ufunuo wa tabia ya Mungu na vile vile maisha ya Mungu ni nini. Tunaona kwamba tabia ya Mungu yenye haki haivumilii kosa, na kwamba kiini kitakatifu cha Mungu hakitachafuliwa. Matokeo yake ni kukuza moyo wa kumcha Mungu; tunaanza kufuatilia ukweli kwa nguvu zetu zote na kutenda kulingana na neno la Mungu. Tunapokuja kuelewa ukweli polepole, tutazidi kuwa na ufahamu zaidi kuhusu asili yetu na tabia ya kishetani, na tutapata utambuzi zaidi na zaidi. Ufahamu wetu kumhusu Mungu utaongezeka pia. Tabia zetu za ndani zenye upotovu zitasafishwa polepole na tutaokolewa kutoka kwa vifungo vya dhambi. Tutapata kuachiliwa kwa kweli na kuishi kwa uhuru mbele za Mungu. Haya hasa ndiyo matokeo yaliyofanikishwa ndani ya wanadamu kupitia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa hivyo inaweza kuonekana kuwa kazi ya ‘ukombozi’ katika Enzi ya Neema na kazi ya ‘kumwondolea mwanadamu dhambi’ katika siku za mwisho ni hatua mbili tofauti za kazi. ‘Ukombozi’ ulikuwa tu Bwana Yesu kuchukua dhambi za wanadamu badala yao na kuwaruhusu wanadamu waepuke adhabu ambayo walipaswa kupata kwa ajili ya dhambi zao. Lakini hiyo haikumaanisha kuwa watu hawakuwa wenye dhambi, sembuse kwamba hawatatenda dhambi tena au kwamba walitakaswa kabisa. Kwa maana ‘kumwondolea mwanadamu dhambi’ ni kufichua kabisa asili ya wanadamu yenye dhambi ili tuweze kuishi bila kutegemea asili yetu potovu tena, ili tuweze kufanikisha mabadiliko katika tabia yetu ya maisha na kutakaswa kabisa. Kwa hivyo, ni kwa kukubali tu kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho tu ndiyo tabia zetu potovu zinaweza kumalizwa kabisa, ndiyo tunaweza kuepuka ushawishi wa Shetani na kuokolewa, kuongozwa katika ufalme wa Mungu na kupata ahadi na baraka za Mungu.”

Niliposikia neno la Mungu na ushirika wa kina dada, nilihisi kwamba vililingana kabisa na hali halisi na vilikuwa vya vitendo kabisa. Nilikumbuka miaka yangu mingi nilipokuwa mtu wa imani: Sio tu kwamba nilisema uongo na kudanganya mara kwa mara, lakini pia nilikuwa na kiburi na bila simile, fidhuli na asiye na mantiki, na kaidi. Watu ambao walinifanyia kazi waliniogopa na walikaa mbali nami, na hata nyumbani kwangu mke na binti yangu waliniogopa kidogo pia. Hakuna mtu aliyetaka kunifungulia moyo wake na hata sikuweza kumpata rafiki wa karibu wa kumwamini. Jambo hilo lilikuwa chungu na nilihisi kutojiweza. Hata ingawa nilisoma Biblia na kusali, kukiri dhambi zangu kwa Bwana, na hata kujidharau mara kwa mara, niliendelea kufanya mambo yale yale mabaya. Sikuweza kujibadilisha hata kidogo. Mtu kama mimi ambaye hufanya dhambi na kumpinga Bwana kila wakati anahitaji sana kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho! Bwana Yesu sasa amerudi—Yeye ni Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Leo, kuwa na nafasi ya kusikia sauti ya Mungu na kujifunza kwamba Bwana Yesu amekuja tena kuwasilisha ukweli na kufanya kazi ya kuhukumu, kusafisha, na kumwokoa mwanadamu, kwa kweli nina bahati mno! Dada huyo aliona kwamba nilijaa hamu, kwa hivyo alinipa nakala ya kitabu cha neno la Mungu: Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu. Niliikubali kwa furaha na nikaazimia kutenda imani yangu katika Mwenyezi Mungu kwa kweli!

Nilisoma maneno mengi ya Mungu baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Nilisoma kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu, siri ya kupata mwili, maana ya jina la Mungu na hadithi ya kweli kuhusu Biblia Takatifu, na pia jinsi washindi wanavyofanyizwa, jinsi ufalme wa Kristo unavyofanikishwa, jinsi matokeo ya mwisho na hatima ya kila aina ya mtu vitakavyoamuliwa, na vipengele vingine vya ukweli, nikipata ufahamu fulani kuvihusu polepole. Pia nilipata imani zaidi katika Mungu.

Mwanzoni, nilipoyasoma maneno ya Mungu ambayo yanahukumu na kumfunua wanadamu kwa ukali sana, nilihisi kuhuzunishwa na kutotulia na nilikuwa na maoni kiasi juu ya maneno hayo; nilihisi kuwa maneno ya Mungu yalikuwa makali sana. Yeye hawezi kuwa mpole kidogo? Mungu akimhukumu mwanadamu kwa njia hii, basi si mwanadamu amelaaniwa? Anawezaje kuokolewa kwa kweli? Baadaye, nilisoma katika neno la Mungu: “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli). “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema, ‘Kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu?’ Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Kutoka kwa maneno ya Mungu niligundua kuwa Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho kupitia kuonyesha ukweli, na kwamba Yeye huhukumu, hufichua na kulaani vikali tabia potovu za mwanadamu, asili ya kishetani, na vitendo viovu ambavyo humpinga Mungu. Yeye hufanya hivi ili tuone waziwazi ukweli wa upotovu wetu, tuelewe kabisa kiini cha tabia zetu potovu, na tujue asili yetu ya kishetani na chanzo cha upotovu wetu. Hii ndio njia pekee tunayoweza kujidharau na kuukana mwili. Aidha, ni kwa sababu tu Mungu anaonyesha tabia Yake yenye haki, uadhama na ghadhabu kupitia hukumu na kuadibu Kwake ndiyo tunaweza kuona haki na utakatifu Wake, na pia kuona waziwazi uchafu, ubaya na uovu wetu. Mungu pia hufanya hivi ili tujue asili yetu ya kishetani na ukweli wa upotovu wetu. Mungu asingemhukumu mwanadamu kwa ukali sana, Mungu asingefichua upotovu wa mwanadamu kwa kulenga kiini cha jambo lile, na Asingefichua tabia Yake adhimu na yenye haki, basi sisi wanadamu, ambao tumepotoshwa sana na Shetani, tusingeweza kutafakari juu yetu sisi wenyewe au kujijua. Tusingeweza kujua ukweli wa upotovu wetu au asili yetu ya kishetani. Iwapo hali ingekuwa hivyo, basi tungewezaje kuacha asili yetu ya dhambi na kutakaswa? Kutoka kwa matokeo yaliyofanikishwa na maneno makali ya Mungu tunaweza kuona kwamba upendo wa kweli wa Mungu kwa mwanadamu na bidii anayotia ili kumwokoa mwanadamu vimo ndani yamo. Kadiri ninavyozidi kuyasoma maneno ya Mungu, ndivyo ninayozidi kuhisi jinsi kazi ya hukumu ya Mungu ilivyo ya ajabu sana. Kazi ya Mungu ni ya vitendo sana! Ni hukumu kali ya Mungu pekee ndiyo inayoweza kumtakasa, kumbadilisha na kumwokoa mwanadamu. Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ndiyo tunayohitaji!

Kwa sababu ya asili yangu ya kiburi na ya kujidai kupita kiasi, niliponena na wengine niliwakaripia mara nyingi kwa njia ya kujionyesha kuwa bora, na katika vitendo vyangu nilipuuza kanuni. Nilipenda kuwalazimisha wengine wanisikilize kila mara na nilikuwa na mazoea ya kujionyesha. Mara kadhaa kwenye mikutano, nilitoa ushirika juu ya jinsi nilivyokuwa nimeshughulikia matatizo katika kitengo changu cha kazi, jinsi nilivyokuwa nimewakaripia wafanyakazi ambao hawakuwa wamefuata maagizo na nikawadhibiti, na pia jinsi ambavyo mke na binti yangu walifanya kile nilichowaambia. Hasa nilipofanya ushirika juu ya maneno ya Mungu, nilisema mambo kama, “Naamini kifungu hiki cha maneno ya Mungu kinamaanisha hivi,” na “hivi ndivyo ninavyofikiri.” Ndugu fulani aliona kuwa kila wakati nilikuwa nikifichua tabia ya kiburi na ya kujidai pasipo mimi kujua. Alinionyeshea jambo hili kwenye mkutano, akisema kwamba kusema na kutenda kwa njia hii kulikuwa dhihirisho la kiburi, kujidai, na kutokuwa na mantiki. Ikiwa mtu yeyote angenifunua jinsi hapo zamani, na mbele ya watu wengi sana, bila shaka ningetoa sababu za kupinga na kumkanusha mara moja. Lakini wakati huo, nilichagua kuwa kimya bila kubishana au kutoa hoja ya kuthibitisha usahihi wangu, kwa sababu nilikumbuka maneno haya kutoka kwa mahubiri: “Ukisema kila wakati ‘Nadhani’ katika kila mada unayokutana nayo, basi, ni vyema uache maoni yako. Nakusihi uache maoni yako na utafute ukweli. Tazama maneno ya Mungu yanasema nini. ‘Maoni’ yako si ukweli! … Una kiburi na wewe hujidai sana! Unapokabiliwa na ukweli, huwezi hata kuacha au kukana fikira na mawazo yako mwenyewe. Hutaki kumtii Mungu hata kidogo! Kati ya wale wanaofuata ukweli kwa kweli na ambao wana moyo unaomcha Mungu kwa kweli, ni nani ambaye bado husema ‘Nadhani’? Msemo huu tayari umeondolewa, kwa maana kwa kusema hivyo mtu hudhihirisha tabia ya kishetani” (“Mahubiri na Ushirika Kuhusu Neno la Mungu ‘Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano Unaofaa na Mungu’ (III)” katika Mahubiri na Ushirika XIV). Ushirika huu ulinikumbusha kuwa, kila nilipokutana na suala, maneno kama “nadhani,” “nadumisha,” na “naamini” kwa kawaida yalikuwa kwenye midomo yangu, kila wakati nikianza na neon “mimi”, na mimi mwenyewe nilikuwa na kauli ya mwisho katika kila kitu. Niliamini kuwa niliweza kung’amua mambo mimi mwenyewe, na niliweza kuyashughulikia matatizo. Siku zote niliwafanya wengine kufanya kama nilivyosema na kunitii. Kwa kujiona kuwa mkuu sana kila wakati, je, huko hakukuonyesha waziwazi tabia ya majivuno? Kile ambacho kaka huyo aliniambia wakati alipoonyesha tabia yangu kilikuwa kweli kabisa, na napaswa kukikubali. Mambo ambayo niliyaamini yalitokana na fikira na mawazo yangu, yalitoka kwa Shetani, na kwa kweli hayakuwa ukweli. Nilifikiria jinsi ambavyo, iwe nyumbani, kazini, au kati ya wenzangu, nilikuwa nikitenda kila wakati kama kwamba nilikuwa nambari ya kwanza. Iwapo mtu yeyote hakunisikiliza au alifanya jambo ambalo halikupatana na maoni yangu, nilikasirika na kumkaripia. Ukweli kwamba nilikuwa na uwezo wa kufunua mambo haya ilimaanisha kwamba hakukuwa na nafasi ya Mungu moyoni mwangu, kwamba sikumheshimu Mungu kama mkuu, lakini badala yake nilijiheshimu kuwa mkuu. Hivyo ndivyo nilivyonena na kutenda kwa kawaida, nikithibitisha jinsi nilivyo na tabia ya kiburi sana!

Baadaye nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno! Kutatua matendo yao maovu, lazima kwanza watatue matatizo ya asili yao. Bila mabadiliko katika tabia, haitawezekana kuleta suluhu ya kimsingi kwa shida hii(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kila neno lililonenwa na Mungu ni ukweli—nilisadikishwa kabisa. Nilifikiri juu ya jinsi nilivyokuwa nikiwakaripia wengine kwa njia ya kujionyesha kuwa bora katika maeneo ya ujenzi, miongoni mwa wenzangu, na nilipokuwa nyumbani. Yote haya yalikuwa mimi kutawaliwa na asili yangu ya kishetani na ya kiburi; haikusababishwa na mimi kuwa mtu mwenye hasira, au kwa sababu nina hamaki au kukosa kujizuia. Nilijiamini kuwa na ubora na talanta na wezo wa kupata mema, jambo ambao lilitia nguvu kiburi changu na ikawa desturi ya maisha yangu, kwa hivyo nilijiona kuwa bora kuliko wengine. nilimwangalia kila mtu kwa dharau, nilidhani kuwa nilikuwa bora kumliko kila mtu mwingine na niliwatalawa watu wengine kila wakati. Nilikuwa nimepata chanzo cha dhambi yangu na kuona matokeo yenye hatari ya kuacha tabia yangu ya kishetani na potovu bila kutatuliwa. Na kwa hivyo nilijitahidi kutafuta na kusoma maneno mengi ya Mungu yanayohukumu na kufichua asili ya kiburi ya mwanadamu, na nilitafakari juu yangu kwa kulinganisha. Kupitia maneno ya Mungu ya hukumu na kufunua na pia ushirika wa ndugu mikutanoni, nilianza kupata ufahamu wa kina kuhusu asili yangu ya kiburi. Niliona kuwa kwa kweli sikuwa bora kumliko mtu mwingine yeyote, na kwamba uwezo wangu na utajiri wote vilikuwa vimetolewa na Mungu, kwa hivyo sikuwa na kitu cha kujivunia. Mungu asingenikirimia hekima na busara, Mungu asingenibariki, ningefanya nini kwa kujitegemea? Kuna watu wengi sana wenye talanta duniani; kwa nini wao hufanya kazi kwa bidii na kukurupuka katika maisha yao yote lakini wakaishia kuwa mikono mitupu? Pia nilipata njia ya kutatua asili yangu yenye kiburi ndani ya maneno ya Mungu, ambayo ilikuwa kukubali kupogolewa na kushughulikiwa zaidi na ndugu, kukubali hukumu, kuadibu, majaribio na usafishaji zaidi wa Mungu, kutafakari juu yangu mimi mwenyewe kwa kuzingatia maneno ya Mungu, kufikia kujifahamu na kujichukia kwa kweli, na kutotenda tena kulingana na tabia yangu ya kishetani bali kutenda kwa kufuatana na maneno ya Mungu. Baadaye nilipitia hali nyingi za kuhukumiwa na kuadibiwa, kupogolewa na kushughulikiwa, na nilipata vipingamizi vingi na hali nyingi za kutofaulu. Ufahamau wangu kuhusu asili yangu ya kishetani na kiini kipotovu uliongezeka polepole, na pia nilipata ufahamu wa kina kuhusu ukuu, haki na utakatifu. wa Mungu. Kadiri nilivyozidi kujua haki na utakatifu wa Mungu, ndivyo nilivyozidi kuona uchafu wangu mwenyewe, hali ya kuwa duni, kutokuwa na maana na hali ya kudharaulika. Vitu ambavyo nilifikiria kuwa muhimu hapo awali au nilivyojivunia, nilihisi wakati huo kwamba havikustahili hata kutajwa. Muda mfupi baadaye, tabia yangu ya kiburi ilianza kubadilika. Yeyote aliyesema kitu ambacho kilikuwa sahihi—kina ndugu, wenzangu, au familia yangu—nilikikubali. Sikuongea tena na wengine kwa lengo la kujionyesha kuwa bora, lakini nilitenda kwa unyenyekevu na sikupuuza tena kanuni. Wakati wowote suala lilipoibuka nilijadili na wengine, na nilitenda kulingana na pendekezo la yeyote lililokuwa sahihi. Polepole, uhusiano wangu na wale walio karibu nami ulianza kufanywa kuwa kawaida. Nilikuwa na amani na furaha moyoni mwangu, na nilihisi kuwa mwishowe nilikuwa nikiishi kwa kudhibitisha mfano kidogo wa mwanadamu.

Kwa kusoma neno la Mungu kila wakati na kuishi maisha ya kanisa, nilizodo kuhisi jinsi ilivyokuwa vozuri kwa kweli kwamba niliweza kukubali kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Niliona kwa kweli kuwa singekuwa na njia ya kutatua tabia yangu ya upotovu. Ni kupitia tu hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu ndiyo nimebadilishwa na kusafishwa pole pole. Katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, mimi huwaona ndugu wengi wakifanya kazi kwa bidii katika kufuatilia ukweli, na kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mwenyezi Mungu. Wakati wowote mtu anapofichua upotovu, wengine huonyesha na kila mtu husaidiana. Sisi sote hujitafakari na kujijua kwa kuzingatia maneno ya Mungu, na tunatafuta ukweli ili kutatua upotovu wetu. Watu wote hujizoeza kuwa watu waaminifu na kuwa safi na wazi; tunakubali na kutii ushirika wowote unaolingana na ukweli na tabia zetu potovu zinazidi kubadilika. Maneno ya Mwenyezi Mungu kweli yanaweza kuwatakasa na kuwabadilisha watu. Mungu mwenye mwili amekuja miongoni mwetu, Yeye binafsi huonyesha maneno Yake ili kuhukumu na kutusafisha, na Anatuongoza kuachana na dhambi na kuokolewa kabisa—tuna bahati nzuri sana! Nilipofikiri kuhusu waumini wote wa kweli ambao wanangojea kurudi Kwake bila subira, ambao wanatamani kutupa vifungo vya dhambi na kutakaswa, lakini wanaoishi kwa uchungu bila njia ya kufuata, nilimwomba Mungu na nikafanya uamuzi: “Natamani kuhubiri injili Yako ya ufalme kwa watu wengine ili waweze kuwa kama mimi, kufuata nyayo Zako na kuanza kuitembea njia ya utakaso na wokovu kamili!”

Iliyotangulia: Kukutana na Bwana Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nimekaribisha Kurudi Kwa Bwana

Na Chuanyang, Vereinigte StaatenMajira ya baridi kali ya mwaka wa 2010 huko Amerika yaliniacha nikihisi baridi sana. Kando na baridi kali...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp