Kuinuka licha ya kushindwa

24/01/2021

Na Fenqi, Korea ya Kusini

Kabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi zangu na kuileta familia yangu heshima. Baadaye, nilifanya mtihani wa kuingia katika shule ya kuhitimu, na kisha nikawa wakili. Nilihisi kila mara kwamba nilikuwa bora kuwaliko wengine. Kwa hivyo, bila kujali nilipokwenda, nilijaribu kuringa siku zote, nikiwatarajia wengine wakubaliane nami katika kila kitu na kufanya mambo kulingana na kile nilichosema. Wakati huo, sikugundua hii ilikuwa aina ya tabia ya kiburi. Nilihisi kwamba kwa kweli nilikuwa mtu mzuri sana. Baada ya kuanza kumwamini Mungu, kupitia kusoma neno la Mwenyezi Mungu, nilitambua hatimaye tabia yangu ya kiburi na nikaona kwamba mbali na kuwa na tamaa ya makuu, pia nilikuwa mwenye majivuno na mwenye kujidai sana. Wakati mwingine, nilipoongea au kufanya mambo, sikuyajadili na mtu mwingine yeyote, na nilisisitiza kufanya mambo jinsi nilivyotaka. Hata ingawa nilipata kujielewa kiasi, nilihisi kwamba haya hayakuwa matatizo makubwa. Nakumbuka wakati mmoja nilisoma katika neno la Mungu, “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu,” na “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu.” Nilizingatia mstari huu, “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu.” Hivyo, vipi kuhusu watu wa ubinadamu mzuri? Au watu wanaomtii Mungu? Je, tabia zao bado zinahitaji kubadilika? Je, tabia iliyobadilika inamaanisha nini hasa? Nilidhani kwamba tulikuwa tukimwamini Kristo, na Kristo ni Mungu wa vitendo, kwa hivyo, je, kumwamini Kristo hakupaswi kumaanishi kumtii Kristo? Kwa hivyo, kumtii Kristo kunamaanisha kulingana na Kristo. Hasa nilipofikiria jinsi nilivyoacha kazi yangu na kuacha familia yangu, jambo ambalo lilikuwa mimi kuchagua kujitumia kwa ajili ya Mungu, niliwaza, je, hii haikuwa ishara ya mimi kumwamini Kristo na kulingana na Kristo? Lakini wakati huo, sikujua, na sikuelewa kwamba nilitakiwa kufanikisha mabadiliko katika tabia yangu ya maisha ili nilingane na Kristo, kwa hivyo nilitekeleza wajibu wangu kwa sababu ya shauku kuu. Sikujua pia kuingia katika uzima kulikuwa nini, na sikujua mabadiliko ya tabia yalikuwa nini. Unaweza kusema sikuwa na uzoefu wa maisha hata kidogo. Je, nilikuja kupata ufahamu wa kweli lini? Ni baada ya mimi kupitia kupogolewa na kushughulikiwa vikali sana ndipo nilitafakari juu yangu mwenyewe na nikaona kuwa asili yangu kwa kweli ilikuwa ya kiburi sana. Sikujua jinsi ya kutafuta ukweli au kulenga kutenda neno la Mungu mambo yaliponitendekea, na sikuwa na utiifu kwa Mungu hata kidogo. Unaweza kusema kuwa, kimsingi sikuwa mtu ambaye alilingana na Kristo. Baada ya kupitia kupogolewa na kushughulikiwa, hatimaye nilipata kujua kwa kweli Mungu alimaanisha nini Aliposema, “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu.

Mnamo 2014, kwa sababu nilimwamini Mungu, niliteswa na serikali ya CCP na nikalazimika kukimbilia ughaibuni. Baada ya kufika ughaibuni, ndugu zangu waliona kuwa nilijitumia kwa shauku kuu na nilikuwa mwenye ubora mzuri wa tabia, kwa hivyo walinichagua kama kiongozi wa kanisa, na wakapendekeza mara nyingi kwamba nishiriki katika matukio fulani na kuhojiwa na wanahabari. Lakini mambo haya yalianza kuwa mtaji wangu. Tayari milikuwa na kiburi, na nikiwa na mtaji huu, nilizidi kuwa na kiburi kupita kiasi. Nilihisi kwamba kanisa halingeendelea bila mimi, na kwamba nilikuwa nikifanya kazi muhimu. Ndugu zangu walipotaka kujadili nami kuhusu masuala ambayo niliona kuwa madogo sana, sikutaka kujisumbua nayo na nilidhani kuwa walikuwa wakilalamika bure. Iwapo waliendelea kuniuliza juu ya hayo, niliudhika. “Kwa nini unaniuliza kuhusu mambo madogo kama haya? Je, mambo haya ni ya maana? Yashughulikie wewe mwenyewe.” Na kama waliuliza zaidi, basi, sauti yangu ilibadilika papo hapo na kuwa ya kuuliza na kukosoa, na hata niliwakaripia kana kwamba nilikuwa mwema zaidi. Kwa kweli, nilipowatendea ndugu zangu kwa njia hii, hata mimi mwenyewe nilihisi kwamba haikufaa. Nilihisi kwamba nilikuwa nikiwaumiza kwa namna fulani. Lakini lazima uelewe kwamba kwa kuishi ndani ya tabia hiyo ya kiburi, nilikuwa nimepoteza ubinadamu wote. Hata kule kujisuta kidogo kulitoweka. Hivi ndivyo nilivyotenda kazini na maishani. Katika kila kitu nilichofanya katika wajibu wangu, nilitaka kuwa na kauli ya mwisho. Nilipojadili mambo na kina ndugu na kusikia maoni au mapendekezo ambayo sikuyapenda, niliwakemea papo hapo bila kufikiri na niliyadunisha maoni yao kana kwamba hayakufaa. Nilitaka mambo yote yawe kama vile nilivyotaka. Pia sikuwaambia wafanyakazi wenzangu kuhusu matatizo mara nyingi ili wajadili na kutafuta kwa sababu nilidhani baada ya kufanya wajibu wangu kwa muda, nilikuwa nimepata uzoefu wa kutosha wa kusuluhisha matatizo kwa kuyachambua na kuyachunguza, na kwamba wafanyakazi wenzangu hawakujua kazi hiyo, kwa hivyo hawakuelewa kabisa. Nilidhani, nikizungumza nao, hawataweza kuongeza kitu chochote, wala kuelewa mambo vyema zaidi kuniliko. Nilidhani kupitia mchakato wa majadiliano kulikuwa upotezaji wa wakati, kwamba kulikuwa tu kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati. Kwa hivyo niliacha kutaka kufanya kazi nao polepole. Wakuu wangu walipogundua kuhusu kazi yangu, niliudhika sana, na sikutaka kukubali usimamizi au mapendekezo ya watu wengine. Wakati huo, nilihisi kwa kweli kuwa hali yangu haikuwa sawa. Ndugu zangu pia walinionya, wakisema, “Una kiburi na unajidai sana, na hutaki kufanya kazi na yeyote. Unakataa kukubali usimamizi na mapendekezo ya wengine katika wajibu wako na kazi yako, na hutaki mtu yeyote aingilie kazi yako.” Maonyo haya na msaada huu kutoka kwa wafanyakazi wenzangu kwa kweli vilikuwa upogoaji na ushughulikiaji wa aina fulani, lakini nilivipuuza. Nilihisi kwamba, hata ingawa nilikuwa na kiburi, sikuwa nimefanikisha kuingia katika uzima, na sikuwa nimepata mabadiliko yoyote, Bado nilikuwa nikifanya wajibu wangu, kwa hivyo hili halikuwa tatizo kubwa. Sikuchukulia muawana na maonyo ya ndugu zangu kwa uzito. Niliyapuuza. Nilidhani tabia yangu ya kiburi, au asili yangu ya kishetani, havikuwa vitu ambavyo ningebadilisha kwa ghafla sana. Kwa hivyo, niliwaza, huu ni mchakato wa muda mrefu, na kwamba kwa sasa napaswa kushughulika na kazi yangu na kutekeleza wajibu wangu vizuri.

Lakini, tunapoishi ndani ya tabia ya kiburi, haimaanishi kwamba hatuhisi chochote. Moyo wangu ulihisi mtupu sana wakati huo. Wakati mwingine, baada ya kumaliza kazi, nilitafakari na kujiuliza, “Ninapofanya kazi au baada ya kumaliza, nimepata ukweli gani? Je, nimepata kuingia katika kanuni gani? Je, tabia ya Maisha yangu imebadilika kwa namna fulani?” Lakini sikuwahi kufanikisha chochote. Kwa nini? Kwa sababu kila siku nilikuwa nikipania na kujichosha ili kumaliza kazi yangu, na kila nilipokuwa na mengi mno ya kufanya, nilijawa na hasira na kukata tamaa. Ilikuwa kana kwamba kitu kimoja pekee kingenichochea nishindwe kabisa kujizuia. Nilipomwomba Mungu, nilikuwa nikifanya hivyo kwa namna isiyo ya dhati. Sikuwa na la kumwambia Mungu kutoka moyoni. Wala sikupata mwangaza au nuru yoyote kutoka katika kula na kunywa maneno ya Mungu. Wakati huo nilihisi mtupu sana na mwenye wasiwasi sana. Nilihisi kwamba kadiri nilivyozidi kutekeleza wajibu wangu, ndivyo nilivyozidi kuwa mbali na Mungu, na sikuweza kumhisi Mungu moyoni mwangu. Niliogopa kutelekezwa na Mungu. Kwa hivyo, nilienda mbele za Mungu upesi na kuomba: “Mungu! Siwezi kujiokoa, na siwezi kujidhibiti, kwa hivyo nakuomba Uniokoe.” Muda mfupi baadaye, kupogolewa na kushughulikiwa kulinijia ghafla.

Wakati mmoja, ndugu ambaye ni kiongozi wa juu wa kanisa alipouliza kuhusu kazi yangu, aligundua tatizo katika jinsi nilivyosimamia utumiaji wa pesa za kanisa. Aligundua kuwa nilipoamua jinsi ya kutumia pesa hizi, sikuwa nimejadili na wafanyakazi wenzangu au kikundi cha uamuzi. Aliniambia, “Hili ni suala la gharama za kanisa. kwa nini hukujadili na wafanyakazi wenzako au kikundi cha uamuzi? Je, huu ni uamuzi ambao unaweza kufanya mwenyewe?” Nilihisi kwamba hapakuwa na lolote ambalo ningeweza kusema ili kujibu swali la ndugu huyo. Wakati huo, sikujua kabisa jinsi ya kumjibu ndugu huyo. Kwa nini? Sikujua sababu kabisa, kwa sababu sikuwahi kufikiria hilo. Baadaye, nilianza kukumbuka. Katika kipindi hicho, kwa sababu nilikuwa nikiishi ndani ya asili yangu ya kiburi, sikuwa na hisia yoyote ya kawaida hata kidogo, sikujua kwamba wajibu wangu ulikuwa agizo la Mungu kwangu, na kwamba nilipaswa kuutekeleza kulingana na kanuni na nitafute ukweli. Sikujua kwamba nilifaa kujadili na kuamua mambo pamoja na wafanyakazi wenzangu na kikundi cha uamuzi. Sikupambanua hilo kwa sababu niliishi katika tabia yangu ya kiburi. Na hata sikujua hilo kamwe. Hata nilidhani kwamba hili lilikuwa jambo ambalo nilielewa, na kwamba sikuhitaji kutafuta au kulichunguza. Ndugu huyo alinishughulikia kwa kusema, “Wewe ni mwenye kujidai na una kiburi, na huna busara yoyote. Sadaka hizi zilitolewa kwa Mungu na watu Wake wateule, na zilipaswa kutumiwa kulingana na kanuni. Sasa sadaka zimefujwa, kwa hivyo lazima tugawe jukumu kulingana na kanuni.” Sikumjibu lolote, lakini bado nilihisi ndani yangu kwamba nilikuwa sahihi. Sikuwa nimeiba sadaka, nilikuwa nimezitumia wakati wa kufanya kazi ya kanisa, hivyo kwa nini niwajibikie hilo?

Baada ya hapo, viongozi wetu wakuu walikuja kanisani kukutana nasi, na walifanya ushirika na kuchambua tatizo langu kwa kutumia maneno ya Mungu. Wakati huo, mimi pia nilitumia maneno ya Mungu kueleza kujielewa kwangu, lakini moyoni mwangu, nilijua kuwa nilikuwa nikitumia ushirika huu juu ya neno la Mungu kuonyesha tu uasi, kutoridhika, na ukosefu wa ufahamu ambao ulikuwa umeongezeka moyoni mwangu. Nilihisi kwamba nilifanya kazi kwa bidii licha ya kutopokea shukrani yoyote. Viongozi wangu waliona kwamba sikuwa na ufahamu wa kweli kuhusu asili yangu, kwa hivyo baada ya kutafuta makubaliano ya ndugu zangu, waliniachisha kazi kama kiongozi wa kanisa papo hapo. Sikuhisi majuto sana wakati huo kwa kweli. Lakini baada ya hapo, viongozi walianza kuchunguza kwa makini kila kipengele cha gharama, na wakati huo, niligundua hatimaye kwa kweli kulikuwa na matatizo fulani. Hasara zilipozidi kuongezeka na jumla kuongezeka, zilizidi kile nilichoweza kulipa, na nilianza kuhofia. Nilianza kukumbuka uamuzi wangu wa kutumia pesa hizo na mtazamo wangu wa kutupilia mbali na kupuuza, na nilianza kujuta na kujichukia kwa kweli. Sikuwahi kufikiri kwamba kutegemea asili yangu ya kishetani katika wajibu wangu kungelisababishia kanisa hasara kama hiyo. Nilipokabiliwa na ukweli, sikuweza kujizuia kuhisi aibu, baada ya kujivuna sana. Nilitaka tu kujizaba kofi usoni. Sikuamini kwamba hayo yalikuwa mambo ambayo nilikuwa nimeyafanya kwa kweli.

Baadaye, nilimsikiliza ndugu huyo akifanya ushirika. Nitawasomea maelezo niliyoyaandika wakati huo. “Leo, kuna viongozi na wafanyakazi ambao wameamini katika Mungu kwa miaka 10 au 20, lakini kwa nini hawatendi ukweli hata kidogo, lakini badala yake wao hufanya vitu vile wanavyotaka? Je, hawatambui kuwa fikira na mawazo yao si ukweli? Kwa nini hawawezi kutafuta ukweli? Wanajitumia bila kuchoka, wakitekeleza wajibu wao kuanzia alfajiri hadi jioni bila hofu ya kazi ngumu au uchovu, lakini kwa nini bado hawana maadili baada ya kumwamini Mungu kwa miaka mingi sana? Wao hufanya wajibu wao kulingana na maoni yao, wakifanya chochote wanachotaka. Wakati mwingine mimi hushtuka ninapoona wanachofanya. Wao kwa kawaida huonekana kuwa wazuri kabisa. Si waovu, na wao huongea vizuri. Ni vigumu kufikiri kwamba wana uwezo wa kufanya mambo kama hayo ya kudharauliwa. Katika masuala muhimu kama haya, kwa nini wasitafute au kuomba ushauri? Kwa nini wanasisitiza kufanya watakavyo na kuwa na kauli ya mwisho katika mambo? Je, hii si tabia ya kishetani? Ninaposhughulikia mambo muhimu, mimi mara nyingi huzungumza na Mungu, na kumtafuta na kumwomba msaada. Wakati mwingine Mungu husema mambo ambayo hayapatani na mawazo yangu, lakini lazima nitii na kufanya mambo jinsi atakavyo Mungu. Katika masuala muhimu, sithubutu kutenda kulingana na mawazo yangu. Je, ni nini kitakachotokea nikifanya kosa? Ni bora kumwacha Mungu afanye uamuzi. Kiwango hiki cha msingi cha kumcha Mungu ni kitu ambacho viongozi na wafanyakazi wote wanapaswa kuwa nacho. Lakini nimegundua kuwa viongozi na wafanyakazi wengine ni mafidhuli. Wanadai kufanya mambo yote watakavyo. Tatizo ni lipi hapa? Kwa kweli ni hatari wakati ambapo tabia zetu hazijabadilika. … Kwa nini nyumba ya Mungu huunda vikundi vya uamuzi? Kikundi cha uamuzi ni watu kadhaa tu ambao hujadili, huchunguza, na kuamua jambo pamoja ili kuepuka makosa au hasara zozote kubwa. Lakini watu wengine hukwepa vikundi vya uamuzi na hufanya vitu kwa njia yao. Je, wao si Shetani ibilisi? Yeyote ambaye hukwepa vikundi vya uamuzi na kufanya mambo kwa njia yake ni Shetani ibilisi. Bila kujali ni kiongozi wa ngazi ipi, ikiwa yeye hukwepa vikundi vya uamuzi, hawasilishi mipango ili iidhinishwe, na hufanya kazi pekee yake, basi yeye ni Shetani ibilisi, na lazima aondolewe na kufukuzwa” (Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha). Kila neno la ushirika wa ndugu huyo lilipenya moyoni mwangu. Labda ndugu wengine hawajui msingi wa matatizo haya, lakini nilijua kuwa maneno yote aliyosema yaliongea juu yangu, na alifunua kabisa hali yangu. Nilimposikia ndugu huyo akisema kwamba watu kama hawa ni Shetani ibilisi ambao lazima waondolewe na kufukuzwa, nilipigwa na bumbuazi ghafla. Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimehukumiwa kifo. Niliwaza, “Nimefikia mwisho wangu. Sasa sitaokolewa kikamilifu kamwe, huu ndio mwisho wa maisha yangu ya kumwamini Mungu—imani yangu katika Mungu imekwisha.” Wakati huo, niliogopa sana. Niliona kila mara kwamba Mungu alinijali sana. Nilikuwa na elimu na kazi nzuri, wajibu ambao nilitekeleza katika nyumba ya Mungu ulikuwa muhimu sana, na ndugu zangu waliniheshimu, kwa hivyo nilijiona kama mtu wa pekee sana kwa Mungu. Nilidhani kwamba nilikuwa mtu muhimu wa kufundishwa katika nyumba ya Mungu. Sikuwahi kufikiri kwamba ningechukiwa na kuondolewa na Mungu kwa sababu nilikuwa nimeikosea tabia ya Mungu. Kuanzia wakati huo, nilianza kuhisi kwamba tabia ya Mungu ni ya haki na haivumilii kosa lolote, kwamba nyumba ya Mungu hutawaliwa na ukweli na haki, na kwamba haimruhusu mtu yeyote ajihusishe na mwenendo mbaya. Kanisani, tunapaswa kutekeleza wajibu wetu kulingana na kanuni na kutafuta ukweli, si tu kufanya lolote tutakalo au hata kutenda tutakavyo. Nilidhani kwamba, kwa kuwa nilikuwa nimesababisha maafa na kutumia sadaka za kanisa ovyovyo, nilikuwa nimeikosea tabia ya Mungu, na hakuna mtu ambaye angeweza kuniokoa. Ilibidi tu nisubiri kuondolewa na nyumba ya Mungu.

Katika siku zilizofuata. kila asubuhi nilipofungua macho yangu, nilihisi hofu kuu, na nilikata tamaa kabisa hata sikuwa na nguvu ya kutoka kitandani. Nilihisi kwamba sikujua pale nitakapokuwa baadaye, kwamba kosa nililofanya lilikuwa kubwa sana, na kwamba hakuna mtu ambaye angeniokoa. Nilikwenda tu mbele za Mungu, kumwomba Mungu, na kumwambia yaliyokuwa moyoni mwangu. Nilimwambia Mungu, “Mungu, nilikosea. Sikuwahi kufikiria mambo yataishia hivi. Hapo zamani sikukujua, na sikukucha moyoni mwangu. Nilikuwa mwenye majivuno na kujidai mbele Yako, nilijihusisha na mwenendo mbaya, na sikuwa na hisia kabisa, na kwa hivyo leo ninapitia kupogolewa, kushughulikiwa, kuadibiwa, na kuhukumiwa huku. Naiona tabia Yako ya haki. Natamani kutii na kujifunza mafunzo kutokana na hali hii. Nakusihi Mungu, Usiniache, kwa sababu siwezi kuishi bila Wewe.” Katika siku zilizofuata, niliendelea kuomba kwa jinsi hii. Asubuhi moja, nilisikia wimbo wa maneno ya Mungu. “Lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema, ‘Bila kujali kinachofanyika, yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu. Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi. Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa na kwa kunipangia aina hii ya mazingira. Lazima nisiache matamanio na azimio langu. Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani, na ni sawa na kujiangamiza. Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu.’ Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao. Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo, na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika(“Azimio Linalohitajika ili Kufuatilia Ukweli” Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliposikia wimbo huu wa maneno ya Mungu, nilihisi kwamba nilikuwa nimepata tumaini la kujiokoa. Niliuimba tena na tena, na kadiri nilivyozidi kuuimba, ndivyo nilivyozidi kupata nguvu moyoni mwangu. Niligundua kuwa nilifunuliwa, nilipogolewa, na nikashughulikiwa kwa njia hii kwa sababu Mungu alitaka nijijue ili niweze kutubu na kubadilika, si kwa sababu Mungu alitaka kunifukuza na kuniondoa. Lakini sikumjua Mungu, nilimwelewa Mungu visivyo, na nikajihadhari dhidi ya Mungu, na kwa hivyo niliishi katika hali hasi ya kukata tamaa kabisa kwa sababu nilidhani Mungu hakunitaka. Lakini siku hiyo niliona neno la Mungu na nikagundua kwamba mapenzi ya Mungu hayakuwa kama nilivyofikiria hata kidogo. Mungu alijua kimo changu cha kiroho kilikuwa kichanga mno, na Alijua kwamba nitakuwa hasi na dhaifu katika hali hizi, na hata nitapoteza dhamira yangu ya kutafuta ukweli. Na kwa hivyo Mungu alitumia maneno Yake kunifariji na kunitia moyo na kunifanya nitambue kwamba watu wanahitaji kufuatilia ukweli kila mara, bila kujali hali. Watu wanaposhindwa na kuanguka, au tunapopogolewa na kushughulikiwa, yote haya ni hatua muhimu katika mchakato wa kuokolewa kikamilifu. Almradi tuweze kutafakari juu yetu wenyewe na kujijua, na tuweze kutubu na kubadilika, basi baada ya kupitia hatua hizi, tutapata ukuaji wa maisha. Mara nilipofahamu haya, nilihisi kwamba sikumuelewa Mungu visivyo tena, na kwamba sikujihadhari dhidi ya Mungu sana. Nilihisi kwamba bila kujali kile ambacho Mungu anapanga na kutayarisha, kwa kweli vyote ni vya faida kwangu, na kwamba Mungu alikuwa Akiwajibikia maisha yangu. Kwa hivyo, nilijipa moyo na nikajitayarisha kukabiliana na chochote ambacho kingetokea.

Bila shaka, pia nilijituliza na kutafakari tena. Kwa nini nilikuwa nimeshindwa na kuanguka vibaya sana? Je, chanzo cha kushindwa kwangu kilikuwa nini? Ni baada tu ya kusoma neno la Mungu ndipo mwishowe nilielewa. Neno la Mungu linasema, “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno! Kutatua matendo yao maovu, lazima kwanza watatue matatizo ya asili yao. Bila mabadiliko katika tabia, haitawezekana kuleta suluhu ya kimsingi kwa shida hii(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Hapo zamani, nilikiri kuwa na kiburi kinadharia, lakini sikuwa na ufahamu wa kweli kuhusu asili yangu, hivyo bado nilijipenda, nikiishi ndani ya fikira na mawazo yangu. Nilihisi kwamba nilikuwa na kiburi kwa sababu nilistahili kuwa hivyo, na ndiyo sababu, ndugu zangu walipojaribu kunipogoa, kunishughulikia, na kunisaidia, nilipuuza. Nilipuuza kabisa. Lakini niliposoma neno la Mungu, nilielewa hatimaye kwamba asili yangu ya kiburi na majivuno ilikuwa chanzo cha ukaidi na upinzani wangu kwa Mungu. Ilikuwa mfano halisi wa tabia ya kishetani. Watu wanapoishi ndani ya asili kama hiyo ya kiburi na majivuno, wakifanya uovu na kumpinga Mungu huwa bila hiari. Nilikumbuka jinsi nilivyojipenda kila mara tangu nilipoanza kutekeleza wajibu wa kiongozi wa kanisa. Nilidhani kuwa ningefanya chochote, kwamba nilikuwa bora kuliko kila mtu, na nilitaka kufanya nipendavyo. Si hayo tu, lakini nilitaka kuchukua madaraka na kuongoza kazi ya kikundi changu chote na kuwafanya ndugu zangu wafanye kile nilichotaka. Sikuwahi kufikiria kuhusu iwapo mawazo na maamuzi yangu yalikuwa sahihi, au ikiwa yalikuwa na ubaguzi, au iwapo yangesababisha hasara kwa kazi ya kanisa hadi nilipomsikia ndugu huyo akisema kwamba mambo yalipomtendekea, alimuuliza Mungu, kwa sababu aliogopa kufanya kitu kibaya, na kwamba alitenda baada tu ya kupokea jibu kamili kutoka kwa Mungu. Ndugu huyo ambaye ni kiongozi wa juu wa kanisa ni mtu aliye na ukweli, ambaye ana moyo unaomcha Mungu na ambaye hufanya mambo kulingana na kanuni. Lakini hathubutu kujiamini kikamilifu. Mambo yanapomtendekea, anamuuliza Mungu na anamruhusu Mungu aamue. Kiongozi wa kanisa, anahitaji kutafuta ukweli katika mambo yote kumliko mtu yeyote. Lakini sikumtafuta Mungu wala kuwa na moyo umchao Mungu. Kila mambo yaliponitendekea, nilitegemea fikira na mawazo yangu yanielekeze na nikachukulia mawazo yangu kuwa ukweli. Nilijiona kuwa mwadilifu na muhimu. Je, huo si mfano halisi wa tabia ya kishetani? Nilikuwa tu kama malaika mkuu aliyetaka kuwa sawa na Mungu. Na hilo lilikuwa jambo ambalo liliikosea tabia ya Mungu sana! Mara baada ya kuelewa mambo haya, nilihisi kwamba asili yangu ya kiburi na majivuno iliogofya. Ilinifanya niishi bila hisia, ilinisababisha nifanye mambo mengi ambayo yaliwadhuru watu na kumkosea Mungu, na ilinifanya niishi kama mtu katili. Lakini Mungu ni mwenye haki. Je, Mungu angewezaje mruhusu mtu kama mimi, aliyejawa kabisa na tabia ya kishetani, achakure na kuvuruga kazi ya nyumba ya Mungu? Kwa hivyo, nilistahili kuachishwa wajibu wangu wa uongozi, nilikuwa nimejisababishia hayo. Niligundua kuwa katika miaka yote ambayo nilimwamini Mungu, nilikuwa nikitegemea vipaji vyangu, na fikira na mawazo yangu kufanya kazi yangu, na nilitafuta ukweli mara chache. Kwa hivyo baada ya wakati huo wote, sasa nusura sikuwa na uhalisi wa ukweli, na kwa kweli nilikuwa nimedhoofika kiroho na wa kuhurumiwa. Niliwaza, kwa nini siwezi kutafuta ukweli? Kwa nini kila wakati mimi hufikiri kuwa maoni na uamuzi wangu ni sahihi? Hii kwa kweli ilithibitisha kwamba sikuwa na nafasi ya Mungu moyoni mwangu, sembuse kuwa na moyo umchao Mungu. Kufunuliwa na Mungu katika wajibu wangu leo kwa kweli kulikuwa kumbusho na onyo la Mungu kwangu, na kama singebadilika mwisho wangu ungekuwa kuondolewa na kupelekwa kuzimuni. Mara nilipoelewa mambo haya, nilihisi kwamba kuhukumiwa, kurudiwa, kupogolewa, na kushughulikuwa na Mungu kwa kweli ni upendo na ulinzi wa Mungu kwa watu na yote hayo yana nia njema za Mungu. Mungu huwahukumu na kuwarudi watu si kwa sababu Anawachukia, bali kuwaokoa kutokana na ushawishi wa Shetani na tabia zao za kishetani. Na mara nilipofahamu hili, nilihisi kana kwamba kumwelewa Mungu visivyo kulipungua na sikutahadhari sana dhidi ya Mungu. Nilihisi pia kwamba bila kujali Mungu atanipangia hali gani katika siku zijazo, zitakuwa na mamlaka na mipango ya Mungu, na ninatamani kuzitii.

Wajibu wangu ulikuwa na kazi ya ufuatiliaji niliyohitaji kukamilisha, na nilihisi kwamba Mungu alikuwa Akinipa fursa ya kutubu, kwa hivyo nilihisi kwamba nilipaswa kutekeleza wajibu huu wa mwisho vizuri. Baada ya hapo, wakati wa kutekeleza wajibu wangu, nilipojadili kazi yangu na kina ndugu, sikuthubutu tena kutegemea tabia yangu ya kiburi na kufikiri kuwa mimi nilikuwa sahihi na kumfanya kila mtu mwingine anisikilize. Badala yake, niliwaruhusu ndugu zangu watoe maoni yao na mwishowe niliamua la kufanya kwa kupima maoni ya kila mtu. Bila shaka, maoni yetu yalipotofautiana, bado niliweza kuwa na kiburi na majivuno, niliendelea kushikilia maoni yangu, na kutokuwa radhi kukubali maoni na ushauri wa wengine. Lakini nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nimeshindwa, nimeanguka, na kupogolewa na kushughulikiwa, na nikahisi hofu, na kisha nilikwenda mbele za Mungu kuomba. Nilijikana kimakusudi, na baada ya hapo nilitafuta ukweli na kanuni kwa moyo uliomcha Mungu pamoja na ndugu zangu. Nilihisi salama sana nilipotekeleza wajibu wangu kwa njia hii, na uamuzi wangu uliweza kustahimili uchunguzi mkali. Na niliposhirikiana na ndugu zangu, niligundua kuwa maoni yangu mengine yalikuwa ya upendeleo. Kufanya ushirika na ndugu zangu, na kisha kuchunguza mambo, angalau kwangu, katika maswala yanayohusu ukweli, kanuni, na utambuzi, kulisaidia sana. Hasa nilipoona jinsi ambavyo mambo yalipowatokea kina ndugu, waliweza kumwomba Mungu, kutafuta, na kufanya ushirika, na hawakujiamini kwa urahisi, nilijiuliza kwa nini sikutafuta ukweli na nilijiamini kwa urahisi? Niliona kuwa kiburi na majivuno yangu vilinifanya niwe na uwezo wa kufanya lolote. Nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na sikuwa bora kuwaliko ndugu zangu. Ni baada tu ya hapo ndipo niligundua pengine nilikuwa na maarifa zaidi kidogo zaidi kuliko ndugu zangu, lakini ndani ya roho yangu, sikuweza hata kufananishwa nao. Sikuwa na moyo umchao Mungu zaidi kuwaliko. Kuhusiana na hili, kina ndugu walinipiku kabisa. Na nilipoona hayo, niligundua kuwa kila mmoja wa ndugu zangu alikuwa na uwezo fulani, na ilikuwa tofauti na jinsi nilivyowaona ndugu zangu hapo zamani. Nilihisi kwamba ndugu zangu kwa kweli walikuwa bora kuniliko, na sikuwa na chochote cha kujigamba, kwa hivyo nilianza kuepuka matatizo, na niliweza kupatana na ndugu zangu na kufanya kazi nao vizuri. Nilipomaliza kazi ya kufuatilia, nilisubiri kwa utulivu uamuzi wa kanisa kuhusu jinsi ya kunishughulikia. Sikuwahi kutarajia kwamba ndugu yule angeniambia kwamba alikuwa ameona bado nilikuwa na uwezo wa kuendelea na kutekeleza wajibu wangu baada ya kupogolewa na kushughulikiwa, na nilikuwa nimepata uelewa juu yangu mwenyewe, na kwa hivyo alisema nitaruhusiwa kuendelea na wajibu wangu. Alionyesha pia matatizo kadhaa yaliyokuwa katika utendaji wa wajibu wangu. Nilipomsikia ndugu huyo akisema nitaruhusiwa kuendelea na wajibu wangu, wakati huo, hakukuwa na lolote ambalo niliweza kusema ila shukrani kwa Mungu. Shukrani kwa Mungu! Nilihisi kwamba baada ya kupitia haya, baada ya kupata kufunuliwa, baada ya kupata kupogolewa na kushughulikiwa vikali sana, hatimaye nilikuwa na ufahamu fulani kuhusu asili yangu ya kishetani. Lakini gharama ilikuwa ya juu sana. Kwa sababu nilikuwa nimetegemea tabia yangu potovu na ya kishetani katika wajibu wangu, nilikuwa nimesababisha hasara kwa kanisa, na kulingana na kanuni, nilipaswa kuadhibiwa. Lakini Mungu hakunitenda kulingana na makosa yangu, lakini badala yake Alinipa nafasi ya kuendelea na wajibu wangu. Mimi mwenyewe nilishuhudia huruma na uvumilivu wa Mungu wa ajabu!

Kila wakati ninapokumbuka tukio hili, najutia hasara nilizolisababishia kanisa kwa sababu ya kutegemea asili yangu ya kishetani katika wajibu wangu. Pia nakubaliana kabisa na maneno ya Mungu, “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu.” Lakini, hata zaidi, nahisi kwamba kuadibiwa, kuhukumiwa, kupogolewa, na kushughulikiwa na Mungu ni ulinzi mkubwa na upendo wa Mungu wa dhati kwa wanadamu wapotovu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mabadiliko ya Mwigizaji

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda...

Masumbuko Makali ya Milele

“Roho zote ambazo zimepotoshwa na Shetani ziko chini ya udhibiti wa miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa...

Jinsi ya Kuuchukulia Wajibu Wako

Na Zhongcheng, Uchina Mwenyezi Mungu anasema, “Mahitaji ya msingi ya imani ya mtu kwa Mungu ni kuwa ni sharti awe na moyo mwaminifu, na...

Pambano la Kuwa Mtu Mwaminifu

Mwenyezi Mungu anasema, “Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp