Ni Nani Anayesema Tabia Ya Kiburi Haiwezi Kubadilishwa

24/01/2021

Na Zhao Fan, Uchina

Sasa nitasoma maneno ya Mwenyezi Mungu: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu). Maneno ya Mungu ni ya vitendo sana! Bila sisi kuhukumiwa, na kupogolewa na kushughulikiwa na maneno haya, hatuwezi kubadilisha tabia zetu za kishetani au kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida. Nilikuwa mwenye kiburi sana. Siku zote nilihisi kama kwamba mimi ni bora kuliko wengine kazini kwangu kwa hivyo nilidhani walipaswa kunisikiza. Kiburi hiki kilifichuliwa mara kwa mara baada ya kumgeukia Mungu. Siku zote nilitaka kuwa na kauli ya mwisho na nilimkaripia kila mtu kwa kumsimanga. Hii liliwadhuru kina ndugu zangu. Ni kupitia tu kwa Mungu kutuhukumu na kutupogoa, ndipo nilipata ufahamu fulani wa kiburi change na niliweza kutubu na kujichukia. Baadaye, nilianza kunyenyekea wakati nikifanya kazi na watu wengine katika wajibu wangu. Nilijifunza kuchukua maoni ya watu na kutafuta ukweli na niliishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.

Zamani mnamo 2015 nilichaguliwa kutumikia kama kiongozi wa kanisa. Na nilihisi furaha sana. Niliwaza, “Mimi kupigiwa kura na watu wengi sana kanisani kunaonyesha kuwa mimi ndiye bora hapa. Nitalazimika kufanya bidii ili wajibu huu utimizwe ili ndugu waone walifanya uchaguzi muwafaka.” Kwa hivyo nilijishughulisha sana kila siku; kila nilipomwona ndugu akiwa na shida, nilijaribu haraka kutatua suala hilo kwa kutumia maneno ya Mungu. Wakati fulani ulipita, na maisha yetu ya kanisa yalikuwa yameboreka kidogo. Kulikuwa na kazi nyingi ya kufanywa, lakini niliweza kuisimamia vizuri sana. Wakati niliona kuwa maisha katika kanisa letu yalikuwa bora zaidi kuliko yalivyokuwa katika makanisa mengine, nilifurahi sana. Punde viongozi walipoona kuwa kazi ya kanisa letu ilikuwa inaendelea vizuri, waliyafanya makanisa mengine yaige tulichokuwa tukifanya. Aidha, kanisa lilikuwa na kazi fulani muhimu, walitaka nishiriki. Na nikawaza, “Hata viongozi wananiheshimu sana na kusifu ujuzi wangu; inaonekana kama kwamba talanta yangu siyo mbaya sana—kwa kweli ni bora kuliko ya wengi!” Muda si muda, nilikuwa nimeanza kuwa mwenye majivuno sana. Nilihisi tu kwamba ningeweza kufanya kila kitu. Kwa hivyo wafanyakazi wenzangu walipotoa maoni yoyote, sikuyazingatia sana; kwa sababu nilihisi kuwa nilikuwa bora kuwaliko. Walipokosa kufanya kile nilichotaka, sikuweza kujizuia na niliwakaripia. Wakati mmoja, dada mmoja ambaye nilikuwa nikifanya kazi naye alikuwa na swali la kujibu. Kisha alinijia kulijadili. Niliwaza, “Kuna nini cha kujadili? Hili si swali gumu; hiyo ndiyo sababu nilikuacha ulijibu. Ikiwa huwezi hata kusuluhisha hili, basi ni dhahiri huwezi kazi hii. Laiti ingekuwa mimi, ningetatua hili.” Kwa hivyo nilisema kwa sauti ya kiburi, “Usijisumbue. Nitalijibu.” Alihisi kukandamizwa na mimi. Na tangu wakati huo hakuthubutu kuniomba msaada. Wakati mwingine, nilimuunga mkono Dada Wang kwa ajili ya wajibu fulani. Dada Chen alisema, “Wajibu huu ni muhimu sana; tunahitaji kujua vyema tabia ya kawaida ya Dada Wang ili tuwe na uhakika. Nilikasirishwa kidogo na jambo hilo. Niliwaza, “Nimefanya kazi ya aina hii mara nyingi hapo zamani, unafikiri sielewi? Isitoshe, nimemjua kwa muda mrefu, kwa hivyo maswali ni ya nini? Nikiimuliza kila mtu juu yake, si hilo litachelewesha mambo?” Kwa hivyo nilimwambia, “Acha kupoteza muda. Acha tu tusonge mbele.” Kuona nilivyokuwa nikisisitiza, alinyamaza. Niliona alikuwa amezuiwa kidogo wakati huo lakini sikujali tu. Kwa hivyo, ndugu alipokuwa na maoni, kila mara nilihisi ni kama hayakuwa mazuri sana, kwa hivyo nilitumia visingizio vya kila aina kukataa maoni yake, na kisha niliyaonyesha maoni niliyopendelea, na kumfanya kila mtu afanye nilivyosema. Kwa muda, wote walizuiwa na mimi, na wakati wa kujadili kazi, walionekana kunyamaza. Baadaye, sikuweza kuzungumza nao hata kidogo, nikihisi kwamba ilikuwa kawaida tu, kupoteza muda. Kwa hivyo mimi nilifanya wajibu wangu katika hali ya majivuno na nikazidi kuwa bila subira na kuwa dikteta.

Wakati mmoja, nilipoona kulikuwa na kiongozi wa timu ambaye hakuwa akifanya wajibu wake vizuri, nilidhani hakuwa na uwezo na alihitaji kubadilishwa. Nilijua kwamba nilipaswa kujadili na wafanyakazi wenzangu. Lakini niliwaza: “Si lazima nijadili nao. Wote wataishia kukubaliana nami hata hivyo.” Kwa hivyo nilimbadilisha kiongozi wa timu. Baada ya hapo, niliwaambia wafanyakazi wenzangu jinsi nilivyoshughulikia jambo hilo. Na kisha Dada Chen akasema, “Hata ingawa kumekuwa na masuala na kiongozi huyo, yeye ni mtu anayefuatilia ukweli; ni kwamba tu hajakuwa muumini kwa muda mrefu, haelewi ukweli mwingi na ana upungufu lakini hii ni kawaida. Tunaweza kumsaidia kwa kufanya ushirika. Kumbadilisha sasa kunaenda kinyume na ukweli.” Sikushawishika hata kidogo, kwa hivyo nikasema, “Nilimbadilisha kwa sababu hakuweza kufanya kazi ya vitendo kabisa. Nimewahi kushughulikia jambo la aina hii hapo awali. Wewe unajua nini?” Kuona kwamba sikutingisika, aliacha kuongea. Kisha wafanyakazi wenzangu walikwenda kukadiria ili waelewe jambo hilo. Waligundua kwamba sikuwa nimelishughulikia inavyofaa, na wakamrudisha kiongozi huyo wa timu. Kazi ya timu hiyo ilivurugwa kutokana na wajibu kubadilishwa huku na huku, nilihisi aibu wakati huo. Niliweza kuona sikuwa nikitenda kulingana na kanuni. Lakini bado sikujitafakari, au kutafuta ukweli.

Mwezi mmoja baadaye, kanisa lilikuwa na kazi muhimu, na mtu anayefaa angechaguliwa kutoka katika kikundi chetu cha wafanyakazi wenza. Nilipata msisimko sana; nikihisi kwamba katika suala la uzoefu wa kazi, nilikuwa bora kuliko wengine, nilidhani watanipigia kura. Kwa mshangao wangu, matokeo yalionyesha kuwa, sikuwa na sifa zilizohitajika. Sikupata kura zozote. Moyo wangu ulivunjika na nilihisi ulimwengu wangu ukiporomoka. Hili linawezekanaje? Mbona sikuchaguliwa? Walikosa utambuzi? Nilitaka sana kujua kwa nini, kwa hivyo niliuliza mapungufu yangu yalikuwa yapi. Nilipomwona Dada Zhou akisita, nilimwambia, “Ikiwa umeniona nimepungukiwa, hebu tuzungumze juu ya hilo.” Hapo ndipo alipopata ujasiri wa kusema, “Nahisi kuwa wewe ni mwenye kujidai sana, na hukubali maoni ya watu wengine. Na wewe hutuamuru kila wakati, na kila wakati nikiwa na wewe nahisi mwenye kuzuiwa.” Kisha dada mwingine akaongezea juu ya hilo, “Nimezuiwa na wewe pia. Wewe ni mwenye kiburi kweli, na wewe hutudharau. Kama kwamba wewe pekee ndiwe unayeweza kufanya kazi ya kanisa, na unafikiri, kwamba hakuna mtu mwingine aliye na uwezo unaokaribia wako….” Dada Chen kisha akasema, “Ninahisi kuwa wewe una majivuno, hutafuti ukweli au kukubali maoni ya mtu yeyote, na unafikiria unayo kauli ya mwisho. Wewe huamua mambo peke yako mara nyingi….” Mmoja baada ya mwingine, dada niliofanya nao kazi wote walisema nilikuwa nikiwazuia. Niliwaza, “Nyote mnasema mimi nina kiburi na huwazuia; kwa nini hamkubali kuwa hamuwajibiki katika kutimiza wajibu wenu? Sawa basi. Kuanzia sasa, nitakaa kimya. Ninyi fanyeni tu kile mnachotaka.” Jioni hiyo, sikuweza kulala. Niligaagaa na kugeuka kitandani. Siku zote nilijifikiria kuwa mfanyakazi hodari. Sikufikiria nilikuwa mbaya sana. Sikuwahi kufikiria waliona hivyo, kwamba nilikuwa mwenye kiburi, na nilikosa mantiki. Nani angefikiria walihisi kuzuiwa na wenye uchungu. Nilianza kukasirika sana. Kila mtu alinichukia sana, kiasi kwamba nilihisi kama panya wa mitaani, aliyechukiwa na kukataliwa kwa dharau. Mungu kamwe hangemwokoa mtu kama mimi. Nilianza kuwa hasi. Katika uchungu wangu, nilimwomba Mungu bila kukoma. Nilisema, “Mungu, nina uchungu mwingi sana. Sijui cha kufanya kuhusu hili. Tafadhali, nipe nuru ili niweze kuelewa mapenzi Yako….”

Asubuhi iliyofuata, niliwasha kompyuta yangu na nikasikiliza maneno ya Mungu: “Kutofaulu na kuanguka mara nyingi si jambo baya; na kufunuliwa pia si jambo baya. Iwe umeshughulikiwa, kupogolewa, au kufunuliwa, lazima ukumbuke hili wakati wote: Kufunuliwa hakumaanishi kuwa unashutumiwa. Kufunuliwa ni jambo zuri; ni fursa bora zaidi kwako kupata kujijua. Kunaweza kuuletea uzoefu wako wa maisha mabadiliko ya mwendo. Bila hilo, hutamiliki fursa, hali, wala muktadha wa kuweza kufikia ufahamu wa ukweli wa upotovu wako. Kama unaweza kujua vitu vilivyo ndani yako, vipengele hivyo vyote vilivyofichika ndani yako ambavyo ni vigumu kutambua na ni vigumu kufukua, basi hili ni jambo zuri. Kuweza kujijua mwenyewe kweli ndiyo fursa bora zaidi kwako kurekebisha njia zako na kuwa mtu mpya; ni fursa bora kwako kupata maisha mapya. Mara tu unapojijua mwenyewe kweli, utaweza kuona kwamba ukweli unapokuwa maisha ya mtu, ni jambo la thamani kweli, na utakuwa na kiu ya ukweli na kuingia katika uhalisi. Hili ni jambo zuri sana! Kama unaweza kunyakua fursa hii na ujitafakari mwenyewe kwa bidii na kupata ufahamu wa kweli kujihusu kila unaposhindwa au kuanguka, basi katikati ya uhasi na udhaifu, utaweza kusimama tena. Mara tu unapovuka kilele hiki, basi utaweza kuchukua hatua kubwa mbele na kuingia katika uhalisi wa ukweli(“Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliguswa sana na maneno ya Mungu, kiasi kwamba machozi yangu yalizidi kutiririka. Nilihisi kwa kuweka mazingira haya, kuwafanya ndugu wanishughulikie kwa ukali, Mungu hakuwa akiniondoa au kuniaibisha. Badala yake, kwa kuwa kweli nilikuwa mwenye kiburi, Mungu alikuwa akitumia hili kama mwito kunilazimisha nijitafakari, nitubu na nibadilike. Mungu alikuwa akiniokoa. Nilipogundua hili, nilihisi huru, na nikamwelewa Mungu. Nilimwomba, nikiwa tayari kujitafakari na nipate kujijua.

Kisha nilitafuta maneno fulani ya Mungu ambamo Anaongea juu ya kiburi cha mwanadamu. Mungu anasema, “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno!(“Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo wanavyozidi kuwa na uelekeo wa kumpinga Mungu. Tatizo hili ni kubwa kiasi gani? Siyo tu kwamba watu wenye tabia ya kiburi humfikiria kila mtu mwingine kuwa duni kuwaliko, lakini lililo baya zaidi, wao hata huwa na mtazamo wa udhalilishaji kwa Mungu. Hata ingawa, kwa nje, watu wengine wanaweza kuonekana kana kwamba wanamwamini Mungu na kumfuata, hawamchukulii kama Mungu hata kidogo. Wao huhisi sikuzote kuwa wanamiliki ukweli na wanajipenda mno. Hiki ndicho kiini na chanzo cha tabia ya kiburi, na hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, tatizo la kiburi lazima litatuliwe. Kuhisi kuwa wewe ni bora kuliko wengine—hilo ni jambo dogo. Suala la muhimu ni kwamba tabia ya kiburi ya mtu humzuia mtu kumtii Mungu, sheria Yake, na mipango Yake; mtu kama huyo daima huhisi kuwa na uelekeo wa kushindana na Mungu kuwatawala wengine. Mtu wa aina hii hamchi Mungu hata kidogo, sembuse kumpenda Mungu au kumtii(Ushirika wa Mungu). Nilipokuwa nikisoma maneno ya Mungu, nilikuwa na wasiwasi na mwenye hofu pia. Nilikuwa nikiishi katika kiburi, nikiwadhuru na kuwazuia watu, na pia kwanza kabisa, hakukuwa na nafasi ya Mungu moyoni mwangu, nilikuwa na uwezekano wa kumpinga wakati wowote. Nilifikiria juu ya wajibu wangu kama kiongozi, nilidhani nilikuwa na ubora fulani wa tabia, kwamba nilikuwa mwerevu na nilijifikiria kuwa mtu wa maana. Nilipokuwa nikifanya kazi pamoja na wengine, siku zote nilihisi mkubwa, kwa hivyo niliwazuia na kuwaamuru. Mtu alipokuwa na wazo, sikuwahi kutafuta kanuni za ukweli. Nilidhani kwamba kwa kuwa nilikuwa na uzoefu na niliweza kuona mambo vizuri, ningeweza kuwafanya watu wafanye kile nilichotaka. Ilikuwa ni kama niliyaona maoni yangu kama ukweli, kama kiwango, kwa hivyo kila mtu mwingine alipaswa kuyaona hivyo pia. Lilikuwa jambo la kutisha kufikiria nilikuwa nimewazuia wengine kwa kiwango kwamba hawakuweza kujieleza. Lakini sikujua kabisa, hata nikidhani wengine walikuwa pamoja nami. Kujidai kwangu sana kulinifanya nijiweke juu ya kina ndugu zangu, kiasi kwamba nilimbadilisha kiongozi wa timu bila kushauriana nao. Dada yangu alipoibua suala hili, nililikataa na nikabishana. Niliona nilikuwa mwenye kiburi sana. Sikumcha Mungu hata kidogo, wala sikufikiria ikiwa iliinufaisha kazi ya nyumba ya Mungu. Nilikuwa nimetenda tu peke yangu, kidikteta, nikiiumiza nyumba ya Mungu, kuvuruga kazi ya kanisa kwa asili yangu ya kiburi na kuwadhuru vibaya sana kina ndugu zangu. Huko kulikuwaje kutimiza wajibu wangu? Nikikumbuka hilo, nilidhani kwamba niliwajibikia kazi yangu, lakini kwa kweli nilikuwa dikteta nikijaribu kuridhisha tamaa yangu ya mamlaka. Nilikuwa nikimpinga Mungu tu! Baadaye, nilijiuliza tena na tena: Nilikuwaje mwenye kiburi sana, nikienenda kwenye njia ya kufanya uovu? Ni kwa kutafakari tu ndiyo niligundua kwamba sumu za kishetani zilinidhibiti, kama vile “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake, “ kiasi kwamba tangu nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikimwamuru kila mtu. Nilijaribu kila wakati kuwafanya wengine wanisikilize, wanizingatie na kunizunguka. Nilihisi hiyo ndiyo iliyokuwa njia pekee ya kujitokeza na kuishi namna hiyo kulikuwa kwa thamani. Sasa najua kwamba ni kwa sababu kila wakati nilikuwa nikiishi kwa kufuata sumu hizi za kishetani kwamba kiburi changu kilikithiri, na sikuwa na ubinadamu. Siyo tu kwamba nilikuwa nimewazuia na kuwadhuru watu, lakini pia nilikuwa nimeivuruga kazi ya kanisa. Ni hapo tu ndipo niligundua imani kama vile “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake,” hizo ni sumu za Shetani. Ni ovu na za upuuzi na zinaweza tu kutupotosha na kutudhuru. Nilikuwa nikifikiri kila mara kwamba kuwa bora na kusifiwa lilikuwa jambo la kufurahia. Kisha mwishowe nikaona kuwa kuishi kwa kufuata sumu za kishetani kulinifanya niishi kama zimwi. Hakuna aliyetaka kunikaribia. Watu walinidharau na pia Mungu alinidharau. Haya yalikuwa matunda machungu ya kuishi kwa kufuata sumu za Shetani! Nilifikiria kuhusu jinsi malaika mkuu alivyokuwa mwenye kiburi kupindukia, akijaribu kuwa sawa na Mungu. Hili liliikosea tabia ya Mungu, kwa hivyo Mungu alimlaani, na akamtupa hewani. Nilikuwa mwenye kiburi, nikawazuia wengine, nikiwataka wanisikilize, si hii ilikuwa tabia sawa na ile ya malaika mkuu? Mwishowe niligundua jinsi lilivyokuwa jambo la kutisha kuishi na tabia kama hiyo. Kama Mungu hangenionyesha nilichokuwa nikifanya, bado ningekuwa nikitumia kiburi changu kutimiza wajibu wangu. na ningesababisha hata madhara zaidi, mwishowe niikosee tabia ya Mungu. Mara tu nilipofahamu hatimaye, nilimwomba Mwenyezi Mungu: “Mungu, sitaki tena kuishi katika kiburi. Natamani kutafuta ukweli ili nitatue kiburi changu, na nitubu kweli.”

Kisha nikasoma kifungu hiki, “Asili ya kiburi hukufanya uwe mbishi. Watu wanapokuwa na tabia hii ya ubishi, je, si wana uelekeo wa kuwa wakaidi? Basi je, unawezaje kutatua ukaidi wako? Unapokuwa na wazo, unaliibua na kusema unachofikiri na kuamini kuhusu jambo hili, kisha, unawasiliana na kila mtu kulihusu. Kwanza, unaweza kueleza zaidi kuhusu maoni yako na kutafuta ukweli; hii ndiyo hatua ya kwanza kutia katika vitendo ili kushinda tabia hii ya ukaidi. Hatua ya pili hufanyika watu wengine wanapotoa maoni tofauti—unaweza kufanya nini ili kujizuia kuwa mkaidi? Lazima kwanza uwe na mtazamo wa unyenyekevu, upuuze kile unachoamini kuwa ni sahihi, na umwache kila mtu awe na ushirika. Hata kama unaamini kwamba njia yako ni sahihi, hupaswi kuendelea kuisisitiza. Kwanza kabisa, hayo ni maendeleo ya aina fulani; inaonyesha mtazamo wa kutafuta ukweli, wa kujinyima, na wa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Unapokuwa na mtazamo huu, wakati huo huo ambapo hushikilii maoni yako, unaomba. Kwa kuwa hujui kutofautisha mema na mabaya, unamruhusu Mungu afichue na kukuambia jambo bora na linalofaa kufanywa ni lipi. Kila mtu anapojiunga katika ushirika, Roho Mtakatifu anawaletea nyote nuru(Ushirika wa Mungu). Katika maneno ya Mungu nilipata njia ya kutenda: Nilijifunza kuwa bila kujali chochote, lazima nidumishe uchaji na utii kwa Mungu. Lazima niombe na kutafuta ukweli, kisha nijadili na kufanya ushirika na kina ndugu ili tuweze kuamua pamoja. Hata kama nadhani niko sahihi, lazima nijinyime na kujikana kwa kudhamiria, niwasikilize kina ndugu zangu, na nione ni nini kitakachokuwa adilifu na cha manufaa zaidi kwa kanisa. Katika mkutano baada ya hapo, nilijiweka wazi kwa kina ndugu zangu na nikaomba msamaha kwa jinsi nilivyowadhuru na kuwazuia. Hawakulalamika juu ya hilo. Walizungumza na mimi wazi wazi na nilihisi utulivu. Katika majadiliano ya kazi baada ya hapo, niliwauliza wengine watoe maoni yao; na maoni yalipoibuka, tulifanya ushirika pamoja hadi tukubaliane. Polepole, kila mtu aliacha kuhisi kuzuiwa na mimi na hali ilizidi kuwa ya amani.

Siku moja, nilikuwa nikijadili kazi na dada mmoja. Alisema kwamba alikuwa amewaandikia viongozi barua kuhusu baadhi ya shida ndani ya kanisa, akiwaambia juu ya masuala ambayo tulikuwa nayo katika wajibu wetu, na jinsi tulivyoyapitia. Hili lilifanya tabia yangu ya kiburi ijitokeze. Na nikawaza, “Inatosha kwamba tunazizungumzia, kwa nini uandike barua?” Nilipokuwa karibu kumnyamazisha, nilikumbuka jinsi nilivyokuwa mwenye kiburi sana hapo awali. Kila wakati niliwataka wengine wanisikilize hivyo kila mtu alihisi kuzuiwa, na sikuwa nikiishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Kwa hivyo nilijitelekeza na nikamwomba Mungu, kutotaka kuishi kwa kufuata kiburi changu, lakini nitende ukweli. Kisha niligundua jinsi lilivyokuwa jambo kubwa kwamba dada huyu alichukua jukumu la kuwasiliana na viongozi wetu. Kwa hivyo niliamua kumsaidia kuandika barua. Mara tu nilipogundua hili, sauti yangu ilikuwa ya upole ghafla na niliweza kuwasiliana naye kuhusu masuala tuliyokuwa nayo na kusikiliza maoni yake. Katika sehemu zingine nilidhani alikuwa amekosea, lakini nilijizuia kumhukumu. Kwa hivyo nilitafuta kabla ya kuzungumza. Kisha nikagundua kuwa baadhi ya mambo aliyosema sikuwa nimewahi kuyafikiria hapo awali. Nilihisi aibu kidogo. Niliona tu jinsi nilivyokuwa mwenye kiburi, nikiwazuia kina ndugu ili wasiweze kufanya kazi yao katika wajibu wao. Kwa kweli, wote walikuwa na uwezo. Wasingekuwa hapo wakifanya kazi pamoja nami, nisingeweza kutimiza wajibu huo. Baada ya hapo, tuliandaa muhtasari wa masuala hayo pamoja na baada ya kuilainisha barua hiyo, tuliituma. Baada ya hapo, katika kutekeleza wajibu wetu, kila ambapo asili yangu ya kiburi ilijidhihirisha, nilimwomba Mungu na kujikana kwa kudhamiria, nikifanya ushirika na wengine zaidi. Ushirikiano wetu ulikuwa bora zaidi na nilihisi mwenye raha na mtulivu zaidi. Kufanya wajibu wangu kwa njia hiyo kulifanya nihisi vizuri sana. Mtu mwenye kiburi kama mimi kubadilisha kidogo kweli lilikuwa tunda la kupitia hukumu ya Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuinuka licha ya kushindwa

Na Fenqi, Korea ya Kusini Kabla ya kumwamini Mungu, nilifundishwa na CCP, na sikufikiria chochote ila jinsi ya kufaulu kutokana na juhudi...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp