Ni Nani Aliye Kizuizi kwenye Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni?

24/12/2019

Na Meng’ai, Malaysia

Mwaka ambao mume wangu alifariki, nilikata tamaa sana, na zaidi ya hayo nilikuwa na mzigo ulioongezeka wa kuwalea watoto wangu. Shida ilikuwa imetokea ghafla katika maisha yangu, lakini nilikuwa na upendo wa Bwana pamoja nami siku zote na, kwa msaada wa ndugu, nilifaulu kupita katika wakati huu mgumu. Ili kulipisha upendo wa Bwana, niliendelea kutoa michango na kulihudumia kanisa, na nimekuwa nikifanya hivyo kwa zaidi ya miaka thelathini. Katika wakati huu, nimepitia kusitawi kwa kanisa na nikaona tukio tukufu la kueneza injili ya Bwana Yesu. Nimeshuhudia pia ukiwa na kutojiweza kanisani. Nilikumbuka wakati ambapo Roho Mtakatifu alianza kufanya kazi kubwa kanisani kwa mara ya kwanza, wakati ambapo tulifurahia na kupata faida kubwa kutokana na kusikiliza mahubiri ya mchungaji. Kulikuwa na upendano kati ya ndugu kana kwamba sote tulikuwa familia moja, na kila mtu aliungana katika kueneza injili na kumshuhudia Bwana. Baadaye, bila kujua kile kilichotokea, hakukuwa tena na mwanga wowote katika kile mchungaji huyo alichohubiri. Ilikuwa kama kwamba kila kitu kilikuwa hadithi ile ile ya zamani tu iliyorudiwa tena na tena, na waumini hawangeweza kupata lishe au riziki yoyote kabisa. Imani yao na upendo wao ulififia polepole, na kulikuwa na watu wachache zaidi waliohudhuria mikutano. Sisi ambao tulishiriki katika huduma pia tulikuwa tu tukifanya kazi kwa njia isiyo ya dhati. Sote tulitenda kulingana na matakwa ya watu kwenye huduma na si kumhudumia Mungu hata kidogo, lakini badala yake tulijitolea mbele ya watu wengine na kujaribu kuwafurahisha. Nilijua kuwa huduma ya aina hii haikulingana na mapenzi ya Mungu, na kwa hivyo jambo hili lilikuwa la kusikitisha sana kwangu. Pia nilihisi kutojiweza, pasipo kujua jinsi ya kutembea kwenye njia iliyokuwa mbele yangu. Kwa hivyo nilitumaini zaidi Bwana arudi haraka iwezekanavyo, ili shida hizi zote zitatuliwe.

Nilipokuwa tu nikihisi kuchanganyikiwa, mnamo mwaka wa 2016 nilichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Nilisoma sehemu kubwa ya neno la Mwenyezi Mungu na nikasikiliza yale ambayo ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu walishiriki na kile walichoshuhudia, na mwishowe nikaelewa kuwa Bwana Yesu alikuwa amepata mwili zamani na akaja ulimwenguni kuonyesha maneno Yake na kutekeleza kazi ya hukumu ya siku za mwisho kuanzia kwa nyumba ya Mungu, na Alikuwa akifanya yote haya ili kuwatakasa kabisa na kuwaokoa wanadamu na kuwaleta wanadamu katika ufalme wa mbinguni. Neno la Mwenyezi Mungu lilidhihirisha siri ya kurudi kwa Bwana ambako nilikuwa nimefikiria kuhusu kwa miaka mingi sana. Nilielewa kuwa kurudi kwa Bwana kuligawanywa katika aina mbili za majilio ya siri na ya kuja hadharani. Bwana kwanza anakuwa mwili kama Mwana wa Adamu katika majilio ya siri ili kuonyesha maneno Yake na kumhukumu na kumtakasa mwanadamu, na kufanyiza kundi la washindi kabla ya maafa. Maafa makubwa yatakaposhuka, Atawatuza wema na kuwaadhibu waovu, na Atakuja hadharani, Akionekana kwa mataifa yote na watu wote. Wakati huo, kazi ya Mungu mwenye mwili wakati wa ujio wa siri tayari itakuwa imekamilika, na wote wanaopinga na kulaani kazi ya Mungu katika siku za mwisho watapatwa na maafa na kulia sana na kusaga meno. Ndugu pia walishiriki nami ukweli kama vile hatua tatu za kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu, umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu, na jinsi Mungu atakavyofanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Wakati huo nilielewa ni kwa nini hapo awali, katika kulihudumia kanisa, hatukuwa na mwongozo wa Mungu, na kwa nini hakukuwa na njia ya sisi kusonga mbele katika kusoma Maandiko, sala, na masomo ya Biblia. Nilielewa ni kwa nini hatukuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu. Mungu alikuwa tayari amefanya kazi mpya, Akihitimisha Enzi ya Neema na kuleta Enzi ya Ufalme. Roho Mtakatifu hakuwa akifanya kazi tena ndani ya makanisa ya Enzi ya Neema, kwa hivyo roho za watu zilikuwa zimefifia na kuwa giza, bila furaha yoyote au kuridhika, na hawakuweza kupata riziki yoyote katika maisha yao ya kiroho. Ni kwa msaada wa mwongozo na mwelekeo wa Mungu ndiyo niliweza kutambua sauti ya Mungu katika neno la Mwenyezi Mungu, na nilikubali kwa furaha kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Baadaye, ndugu walishiriki nami mara kwa mara neno la Mwenyezi Mungu. Kutazama filamu, video za densi za kwaya, na video za muziki zilizotolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu kulinipa riziki kubwa, na nilimshukuru Mungu kwa dhati kwa kuniongoza hadi mbele ya kiti Chake cha enzi. Nilifurahia kuchungwa na kulishwa na neno la Mungu, na niliingia katika maisha ya furaha kamili ya kuishi uso kwa uso na Mungu.

Siku moja, mke wa mmoja wa wachungaji kanisani alinitumia ujumbe ghafla, akisema: “Kwa nini ulipenda chapisho la Umeme wa Mashariki? Vile vile uliruhusu lichapishwe kwenye kalenda yako ya matukio, na kufanya hivyo kunapingana na mapenzi ya Bwana. Wakazi wetu wa parokia wakiona chapisho kuhusu Umeme wa Mashariki, na wapendezwe na maneno ya Mwenyezi Mungu, wote wataenda kusoma kuhusu Umeme wa Mashariki, halafu tutafanya nini? Huna budi kutowasiliana na watu kutoka Umeme wa Mashariki tena. Unapaswa kufuta habari yao ya mawasiliano mara moja….” Nilijibu: “Sinema, nyimbo, na video za muziki za injili za Kanisa la Mwenyezi Mungu zote ni nzuri, na nimepata mengi kutoka kwazo. Napaswa kuzipenda!” Nilitaka kutuma ujumbe zaidi kwa mke wa mchungaji, lakini kabla hata ya kumaliza kuandika ujumbe wangu, alisema mambo mengi akimshambulia na kumshutumu Mwenyezi Mungu, na kulikashifu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Niliona kuwa hakuwa na hamu yoyote ya kuchunguza suala hili kubwa la kurudi kwa Bwana, lakini alitoa maoni na maneno ya kushutumu ambayo aliona kwamba yalifaa. Sikutaka kuzungumza naye kuhusu jambo hili tena, kwa hivyo nilibadilisha mada.

Siku chache baada ya tukio hili kutokea, Mchungaji Yang alikuja kunitafuta ili tuzungumze. Baada ya kutaniana, Mchungaji Yang aliniuliza, “Je, umechunguza kikundi chochote kingine cha dini mtandaoni?” Sikujua kwa nini Mchungaji Yang aliniuliza swali kama hilo, na nikasema, “Marafiki zangu kwenye Facebook ni wa madhehebu mengi tofauti, na nikifikiri kwamba makala wanayochapisha ni sahihi na mazuri, mimi hujaribu kuyaelewa kila wakati na kuona ikiwa yana nuru yoyote mpya. Je, unadai kwamba ni vibaya kufanya hivi?” Mchungaji Yang aliniuliza tena, “Je, ulibadili dini na kuwa wa dini ya Umeme wa Mashariki miaka miwili iliyopita? Kwa nini unataka kuchunguza Umeme wa Mashariki? Pia, wewe huenda mara kwa mara kumtafuta fulani (dada ambaye alikuwa amekubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, ambaye picha zake zilikuwa zimechapishwa na ambaye alikuwa ameshutumiwa na kuachwa na mchungaji wa kanisa lake la asili)? …” Niliposikia mfululizo wa maswali kutoka kwa Mchungaji Yang, nilianza kukasirika, na nikasema, “Kanisa la Mwenyezi Mungu ni zuri, na ndani yake kuna ukweli na kazi ya Roho Mtakatifu. Nitafuata mahali popote palipo ukweli na kazi ya Roho Mtakatifu, na hii ni sawa kabisa. Hakuna nuru mpya katika kanisa letu, na roho yangu imetiwa giza na haiwezi kupata chakula chochote huko. Nataka kutafuta kanisa ambalo lina kazi ya Roho Mtakatifu, ambapo maisha yangu yanaweza kupokea lishe ya ukweli. Mafundisho ya Umeme wa Mashariki yananivutia, na maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli. Yananiruhusu nipate riziki. Sikukosea kuchunguza Umeme wa Mashariki, nina uhuru wa kufanya hivyo.” Mchungaji Yang alisema, “Kile ambacho watu kutoka Umeme wa Mashariki wanahubiri kinakiuka mipaka ya Biblia, na hakuna maneno mengine ya Mungu isipokuwa yale ambayo yamo ndani ya Biblia. Ikiwa wanayohubiri yanapotoka kutoka kwa Biblia, basi si sahihi.” Nikasema, “Wakati mmoja nilisikia mhubiri akisema vivyo hivyo, na nilikuwa na maoni kama hayo. Lakini baada ya kusoma neno la Mwenyezi Mungu, na kusikia kile ambacho ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu walishiriki, nimekuja kujua kuwa maoni haya ni fikira na mawazo yetu wenyewe. Hayapatani kabisa na ukweli na hayalingani na ukweli. Mungu anajumuisha vyote, na Mungu ni mwingi wa hekima. Tunawezaje kuwekea mipaka maneno na kazi ya Mungu kwenye Biblia tu? Biblia inasema: ‘Na pia kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya, ambayo, yote yakiandikwa, ninafikiri kwamba hata dunia yenyewe haingetosha vitabu hivyo ambavyo vitaandikwa’ (Yohana 21:25). Tunaweza kuona hapa kwamba maneno na kazi ya Mungu iliyorekodiwa katika Biblia ni finyu sana. Si kila kitu ambacho Bwana Yesu alisema wakati huo kiliandikwa katika Biblia, sembuse maneno yaliyosemwa na Bwana aliyerejea. Aidha, kazi ya Mwenyezi Mungu imejengwa juu ya msingi uliowekwa na Bwana Yesu. Kazi ya Mwenyezi Mungu na ile ya Bwana Yesu ni kazi ya Mungu mmoja….” Mchungaji Yang hakusikia neno hata moja nililosema na hakuwa na shauku ya kutafuta na kuchunguza. Aliendelea tu kusema mambo yanayompinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu, na akaniuliza, “Ulipataje habari kuhusu tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu? Una vitabu vyao? Umehubiri kazi ya Mwenyezi Mungu kwa mtu mwingine yeyote? Umeihubiri kwa watoto wako? Nipe majina ya watu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu….” Alitaka pia nisihudhurie mkutano pamoja na watu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Iwapo singemsikiliza na niendelee kuwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu, basi angenifukuza kutoka kanisani, hangeniruhusu tena niende katika kanisa lolote na angeniharibia jina langu kabisa. Nilishtushwa na Mchungaji Yang niliyemwona mbele yangu. Mchungaji Yang, ambaye alikuwa mwenye tabia nzuri na mnyenyekevu kila wakati, na kila wakati aliongea maneno ya upole sana, alikuwa amebadilikaje na kuwa mtu katili asiye na busara? Nilimwambia, “Ni haki yangu kuchunguza ukweli, na hakuna aliye na haki ya kuingilia jambo hili. Kwa mintarafu ya ikiwa mafundisho ya Umeme wa Mashariki ni njia ya kweli au la, lazima kwanza usihukumu na kushutumu bila kufikiria. Unaweza kwenda kuchunguza mwenyewe kwenye tovuti ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambamo wana maudhui mengi. Kuna kila aina ya vitabu vya maneno ya Mungu. Nenda ukajionee mwenyewe ikiwa neno la Mwenyezi Mungu ni sauti ya Bwana Yesu aliyerejea….” Mchungaji Yang hakuweza kabisa kusikiliza kile nilichokuwa nikisema, lakini aliendelea tu kupinga na kushutumu. Alinitishia, akisema lazima niachane na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kadiri alivyozidi kuzungumza, ndivyo Mchungaji Yang alivyozidi kuvuka mpaka. Nilikasirika sana na kumwambia, “Bwana Yesu alisema: ‘Msihukumu, ili msihukumiwe. Kwani kwa ile hukumu mhukumuyo, mtahukumiwa(Mathayo 7:1-2). Ikiwa hujawahi kuchunguza maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu, basi unawezaje kutoa hukumu na maoni yoyote ya kushutumu kama utakavyo? Unapotenda hivi, je, ni kwa njia inayomcha Bwana? “Mchungaji Yang aliona kwamba sikuwa nikimsikiliza na kwamba nilikuwa nimemkanusha, na kwa hivyo hakusema kitu kingine chochote.

Katika siku zilizofuata, Mchungaji Yang alianza kunichunga. Jambo hili lilinitia wasiwasi sana, na nilipoteza pia uhuru wangu wa imani. Kanisani, kulikuwa na kijia kimoja tu cha ukumbi kilichotenganisha ofisi ya Mchungaji Yang na yangu. Aliendelea kutembea ofisini kwangu kuona nilichokuwa nikijishughulisha nacho, na wakati mwingine alisema kuwa alikuwa akienda chooni kisha akanitazama akiwa kwenye ushoroba. Siku moja, dada wawili wa Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuja ofisini kwangu kuzungumza. Mara dada walipoondoka, Mchungaji Yang alienda kumtafuta msaidizi wangu. Msaidizi wangu baadaye aliniambia kwamba Mchungaji Yang alikuwa amemwuliza watu hawa wawili walikuwa kina nani, na kwa nini walikuwa wamekuja…. Mchungaji Yang alinichunga siku nzima kana kwamba alikuwa akimchunga mhalifu. Jambo hilo lilinifanya nihisi kukandamizwa sana na bila uhuru kabisa. Siku moja, sikuenda kanisani, na nilikuwa nikishiriki na ndugu wengine katika mkutano uliokuwa mtandaoni. Wakati huo huo, nilipokuwa nikiandika mihtasari ya mkutano sebuleni kwangu, Mchungaji Yang ghafla alitokea nyuma yangu (mlango ulikuwa wazi kidogo, na mtu yeyote aliyekuja angeingia chumbani) akasema, “Unafanya nini? Unaandika nini?” Niliruka juu kwa mshtuko kwa ajili ya sauti ya ghafla na isiyotarajiwa. Nilihisi mpweke moyoni kwa kusumbuliwa naye kwa njia kama hiyo, na bila kujali nilichofanya sikuweza kurudi katika hali ya utulivu. Nilimchukia sana, na nikawaza: “Kuchunguza njia ya kweli katika imani ya mtu katika Mungu ni sawa na sahihi, na ni haki ambayo Mkristo anapaswa kuwa nayo.” Roho Mtakatifu hakuwa akifanya kazi tena ndani ya kanisa letu, na wakazi wote wa parokia walikuwa hasi, dhaifu na waliofifia katika roho. Waliishi katika mazingira ambayo yalikuwa yamezama kwenye giza, na nilikuwa nikitafuta kanisa ambamo Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi. Je, ilikuwaje makosa kutafuta nyayo za Mungu? Kwa nini alitaka kunichunga? Kwa nini hakuniacha?

Sio tu kwamba mchungaji alikuwa akinifuatia na kunisumbua, lakini pia mzee mmoja wa kanisa hata aliniita ili kunisumbua. Aliniambia: “Kile ambacho watu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu huhubiri kimekiuka mipaka ya Biblia. Ikiwa unaamini katika Bwana, huwezi kumsaliti Bwana, ambaye amekupa wema mwingi sana. Huwezi kuwa bila na dhamiri….” Nilijibu vikali, “Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu mmoja, na bila shaka sijamsaliti Bwana Yesu kwa kumwamini Mwenyezi Mungu. Naenda kwa kasi sawa na nyayo za Mwanakondoo….” Hata hivyo, bila kujali jinsi nilivyojaribu kueleza hayo, mzee wa kanisa alikuwa sawa na mchungaji. Isipokuwa kusema mambo ya kushutumu na kukufuru, na kunizuia kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, hakusikiza neno hata moja la yale niliyoshiriki au kushauri. Sikutaka kuzungumza naye tena, kwa hivyo nilifikiria tu kisingizio cha kukata simu. Lakini yule mzee wa kanisa hakuniacha. Aliendelea kupiga simu ili kunisumbua na akasema kwamba, kwa ajili ya imani yangu katika Mwenyezi Mungu, nilikuwa nimesahau neema ya Bwana na nilikuwa nimemsaliti. Nilikumbuka kilichosemwa katika Ufunuo: “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo(Ufunuo 14:4). Kwenye msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, Mwenyezi Mungu anatekeleza hatua ya kazi ya kuhukumu na kuwatakasa watu kupitia maneno, na kukubali kwangu kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kulionyesha wazi kuwa nilikuwa nikienda kwa kasi sawa na nyayo za Mwanakondoo. Mtu yeyote angewezaje kusema kuwa nilikuwa nikimsaliti Bwana Yesu? Mwanzoni, Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi, watu ambao walikuwa wamemwamini Yehova waliacha sheria na wakakubali injili ya ufalme wa mbinguni ambayo ilikuwa ikihubiriwa na Bwana Yesu. Walimfuata Bwana Yesu, lakini je, walikuwa wamesahau wokovu wa Yehova? Je, huu ulikuwa usaliti kwa Yehova? Si huu ni uongo? Baada ya haya kutukia, mchungaji kwa mara nyingine alinitumia ujumbe mtandaoni akimtukana, kumpinga, na kumshutumu Mwenyezi Mungu. Kusoma maneno ya kutisha kama hayo kulinifanya nihisi kuchukizwa na kukasirika tena. Ni Shetani tu aliyekuwa na uwezo wa kutamka kufuru kama hii, na wakiwa na vyeo vyao kama viongozi kanisani, ilikuwaje kwamba hawakuwa na hofu ya Mungu hata kidogo na walithubutu kusema kila aina ya kufuru? Ilinikumbusha maneno ya Bwana Yesu: “Ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja(Mathayo 12:32). Kumkufuru Mungu ni dhambi kubwa na mbaya! Nilihisi hofu iliyolimatia kwa niaba yao, lakini bila kujali nililosema, walifunga tu masikio yao na wakakataa kusikia chochote. Waliendelea tu kushutumu, kupinga, na kukufuru. Sikuweza kuelewa tu: Mzee wa kanisa na mchungaji wote walikuwa na maarifa ya Biblia na walikuwa wamesoma theolojia, na maneno ya Mwenyezi Mungu yalizungumzwa kwa uwazi sana, kwa nini ilikuwa kwamba hawangetafuta au kuchunguza maneno Yake? Kwa nini walisisitiza kabisa kumshutumu na kumpinga Mwenyezi Mungu?

Huku nikizingatia swali hili, nilienda kuwatafuta ndugu wa Kanisa la Mungu Mwenyezi. Dada Lin alishiriki nami, akisema, “Kwa mintarafu ya ni kwa nini mzee wa kanisa na mchungaji hawatafuti wala kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, lakini badala yake wanamhukumu na kumpinga kwa hasira, Mwenyezi Mungu alifunua asili na chanzo cha tatizo hili. Mwenyezi Mungu asema ‘Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia). ‘Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?(“Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Wakati ambapo Bwana Yesu alikuwa amekuja kufanya kazi Yake kwa mara ya kwanza, Alizongwa na lawama na upinzani wa hasira wa viongozi wa Kiyahudi—makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo. Mwishowe, walimsulibisha Bwana Yesu. Mababu wa Mafarisayo walimwamini Mungu na walikuwa stadi wa sheria. Kwa hivyo kwa nini walimkataa na kumlaani Bwana Yesu, na kumsulubisha msalabani? Tunaweza kuona kutoka katika neno la Mungu kwamba hii ilitokana na asili yao ya kishetani ya kuwa wabishi, wenye kiburi, na kutotii ukweli. Bwana Yesu alionyesha ukweli mwingi, na hawakuutafuta au kuuchunguza, badala yake walifuata mitazamo yao wenyewe. Imani yao katika Mungu ilitegemea tu fikira na mawazo yao wenyewe, na walifafanua Biblia kwa kunukuu aya nje ya muktadha. Hii iliwafanya wawe vipofu, na kutopata nuru yoyote kutoka kwa Mungu. Hawakujua kazi ya Roho Mtakatifu, na hawakuelewa ukweli, wala hawakuweza kuelewa sauti ya Mungu. Hii kwa kweli ilisababisha maneno ya Biblia yatimie: ‘Kwa kusikia mtasikia, na hamtaelewa; na kutazama mtatazama, na hamtaona: Kwani mioyo ya hawa watu imekuwa mizito, na masikio yao hayasikii vizuri, na wameyafunga macho yao(Mathayo 13:14-15). Wachungaji na wazee wa kanisa miongoni mwa watu wa dini katika siku za mwisho ni sawa na Mafarisayo wa wakati huo, kwani kile wanachotilia maanani ni maarifa kuhusu Biblia na nadharia ya kitheolojia. Wanategemea fikira na mawazo yao kufafanua neno la Bwana, na kuwekea mipaka jinsi Bwana atakavyorudi. Wao hushikilia fikira na mawazo yao kwa ukaidi, na hawatafuti ukweli kabisa. Sio tu kwamba hawachunguzi kazi ya Mungu katika siku za mwisho, lakini wanampinga na kumshutumu bila kufikiria, na hivyo kufunua asili yao ya kishetani ya ukaidi, majivuno, na uhasama kwa ukweli. Wao husomea theolojia, wakijizatiti kwa maarifa ya Biblia, lakini hiyo haimaanishi kuwa wana upendo wowote kwa ukweli, na hiyo haimaanishi kwamba wanaweza kukubali na kutii ukweli. Wao hufasili maarifa ya Biblia na nadharia ya theolojia, lengo lao la pekee likiwa kuzidisha umashuhuri wao na sifa zao. Wao hufanya hivyo ili kulinda hadhi zao wenyewe, na kuwafanya waumini wawastahi kwa heshima, wawaabudu, na kuwafuata. Wanaona kwamba maneno ambayo Mwenyezi Mungu huonyesha ni ukweli, na kwamba yanaweza kuwashinda na kuwaokoa watu, na kwamba watu wengi ambao wanapenda ukweli na wanaotamani kuonekana kwa Mungu wamesoma neno la Mwenyezi Mungu na wamemgeukia Mwenyezi Mungu. Wanaamini kuwa kazi ya Mwenyezi Mungu ni tishio kwa hadhi zao na riziki yao, na kwa hivyo wanapinga kwa hasira na kufanya kila wawezalo kumshutumu na kumpinga Mwenyezi Mungu. Wao hutumia mbinu zozote za lazima kuzuia na kuwakatiza waumini kumgeukia Mwenyezi Mungu kwa jaribio la kuwatawala wateule wa Mungu wakati wote. Hii ndiyo sababu wazee wa kanisa na wahubiri hawatafuti au kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu na ndiyo sababu ya wao kumpinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu kwa hasira. Inaweza kuonekana katika matendo maovu ya wahubiri na wazee wa kanisa ambao wanampinga Mungu kwamba wao ni Mafarisayo wa wakati wetu, na kwamba wao ni vizuizi na vikwazo vinavyowazuia waumini kukubali njia ya kweli na kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Ni wapinga Kristo, ambao wanampinga Mungu na kumfanya Mungu kuwa adui wao, na ambao wamefichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho.”

Baada ya kusikia neno la Mwenyezi Mungu na yale ambayo kina dada walishiriki, niliyalinganisha na yale ambayo mchungaji na mzee wa kanisa walikuwa wamesema na kutenda. Niliona kuwa neno la Mwenyezi Mungu lilizungumzwa kwa njia ya vitendo na kwamba, ingawa mchungaji na mzee wa kanisa walikuwa wenye kutopea sana katika Biblia na waliweza kufasili Biblia, bado haikumaanisha kuwa walikuwa na maarifa yoyote kumhusu Mungu. Walitegemea talanta na maarifa ya kawaida katika kazi zao ili kujiinua ili wengine wawaabudu na kuwafuata. Kwa juu juu, walionekana kumtumikia Mungu, lakini katika hali halisi, waliyokuwa wakihudumia ni fikira na mawazo yao wenyewe, hadhi na riziki yao wenyewe. Kupitia mchungaji na mzee wa kanisa kunishambulia mara kwa mara na kunizuia, niliweza kubaini walikuwa nani kwa kweli. Walikuwa wapinga Kristo ambao walimwamini Mungu lakini hawakutafuta ukweli, na ambao walimtumikia Mungu lakini walimpinga. Hata ingawa mchungaji na mzee wa kanisa bado hawajaacha kunisumbua hadi leo, tayari nimeona waziwazi asili yao ya kweli ya mpinga Kristo ya uadui wa ukweli na upinzani kwa Mungu. Sitakubali tena kusumbuliwa nao au kudhibitiwa nao, na nina hakika kabisa kuwa kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni ya kweli. Natamani kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho kabisa, na kamwe kutokata tamaa! Amina!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mwamko wa Roho Aliyedanganywa

Na Yuanzhi, BraziliNilizaliwa katika mji mdogo huko Kaskazini mwa China na mnamo 2010, nikafuata jamaa kwenda Brazili. Hapa nchini Brazili,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp