Kurejea kwa Mwana Mpotevu

24/12/2019

Na Ruth, Marekani

Nilizaliwa katika mji mdogo kusini mwa China, katika familia ya uumini ambao ulianzia na kizazi cha bibi ya baba yangu. Hadithi za Biblia, nyimbo za kusifu na muziki takatifu uliochezwa kanisani vilikuwa marafiki wangu wa siku zote katika siku za furaha za utoto wangu. Nilipoanza kuzeeka na shinikizo la masomo likazidi, moyo wangu ulianza kuwa mbali na Bwana. Hata hivyo, Bwana hakuniacha kamwe; kila nilipomwita, Yeye angenisaidia. Neema na jina takatifu la Bwana Yesu vilikuwa vimekita mizizi ndani ya moyo wangu. Nakumbuka mwaka ambao nilifanya mitihani wa kuingia katika chuo kikuu, hakuna mtu aliyefikiria kuwa ningeweza kutahiniwa kwenye chuo kizuri, ikiwa ni pamoja na walimu wangu. Nikikabiliwa na pigo baada ya pigo, nilikuwa karibu nikate tamaa kabisa, na mimi pia nilifikiria kuwa singeweza kutahini kuingia kwenye chuo nilichotaka kuingia. Lakini kitu kiliingia akilini mwangu—kifungu nilichosikia kanisani nilipokuwa mdogo: “Mahali mwanadamu huishia, Mungu anaanza,” na kwa ghafla nilihisi kama niliyeangaziwa. Nilijua ilikuwa sahihi: Pale ninapofikia mwisho wangu ni pale ambapo Mungu anaanzia. Uwezo wa Bwana ni mkubwa zaidi, na niliamini kwamba mradi tu ninamtegemea Bwana kwa kweli basi Yeye angenisaidia. Na kwa hivyo, nilianza kumwomba Bwana Yesu mara nyingi: “Ee Bwana, tafadhali nisaidie. Ikiwa naweza kutahiniwa kuingia katika chuo kikuu cha ndoto yangu bila hitilafu basi kuanzia sasa ninaahidi kuwa sitajitenga mbali na Wewe, na nitakukubali kama mwokozi wangu wa pekee katika maisha haya.” Wakati nikifanya hivyo, nilikuwa pia nalipa gharama isiyowazika kwa watu wengi; wakati wa mwaka wangu wa mwisho katika shule ya upili nilikuwa nikifanya mazoezi ya kucheza piano wakati wowote ambapo sikuwa nakula au kulala. Nilikuwa nikifanya mazoezi kwa masaa 10 hadi 12 kwa siku. Sikujua nguvu iliyokuwa ikinishikilia ilikuwa inatoka wapi, lakini nilifikiria kuwa ilikuwa ni lazima iwe ni Bwana aliyekuwa akisikiliza maombi yangu na kunisaidia kimya kimya. Shukrani kwa Bwana ndani ya moyo wangu ilizidi kua. Mwishowe, tamanio langu la dhati la zamani lilitimizwa; nilitahiniwa kuingia katika mojawapo ya shule za juu zaidi za muziki nchini, na kwa sababu hiyo niliamini kabisa kuwa Bwana Yesu ndiye mwokozi wangu wa pekee. Katika mwaka wangu wa mwisho wa chuo kikuu sikujua ni njia gani nilipaswa kuchukua baada ya kuhitimu, kwa hivyo nilimwita Bwana Yesu na nikamwomba anionyeshe njia, anifungulie njia. Mnamo 2004, muda mfupi baada ya shambulio la kigaidi la 9/11 huko Marekani, vyeti vyote vya viza vilikuwa vimesitishwa, lakini la kushangaza nilipokea udhamini kamili wa kwenda katika chuo kikuu huko Marekani kwa sababu ya CD yangu iliyorekodiwa kitaalamu. Nilipata viza ya mwanafunzi bila kizuizi hata kimoja na nilienda Marekani kuendeleza masomo yangu. Matukio haya mawili—kutahiniwa kuingia katika chuo kikuu na kwenda ughaibuni—yalinionyesha kuwa Bwana alinisaidia kutambua ndoto ambazo singeweza kufanikisha peke yangu. Nilisadiki hata zaidi kuwa Bwana Yesu ndiye Mungu wa kweli na kwamba Yeye ndiye Mwokozi wangu, na kwamba nahitaji kutenda vizuri imani yangu kwa Bwana na kumfuata.

Siku moja mnamo 2007 nilimpigia mama yangu simu akiwa China, kama nilivyofanya kawaida kupiga gumzo. Katika mazungumzo yetu ya simu alisema: “Je, wajua ya kuwa Bwana Yesu Kristo tayari amerudi?” Kusikia akisema hivi, nilishangaa ghafla kwa furaha, lakini wakati huohuo nikafikiria jinsi katika Biblia inasema kwamba katika Siku za mwisho Makristo wa uwongo watatokea, kwa hivyo sikujua kama jambo hili kuhusu Bwana kurudi lilikuwa la kweli au la uwongo. Nilijua ni lazima niliendee kwa tahadhari. Siku hizi mtandao ni wa haraka sana na unaofaa, kwa hivyo nilifikiria ni lazima niende mtandaoni ili nichunguze hili. Baada ya kukata simu nilienda mtandaoni, nikihisi kama niliyekuwa natembea hewani, kujaribu kupata chanzo cha habari cha kuaminika. Nilishangaa kwamba, yote niliyopata yalikuwa sauti za kupinga zikikufuru na kushutumu kurudi kwa Bwana Yesu—Mwenyezi Mungu. Sikuweza kuelewa ikiwa haya yalikuwa kweli au uwongo, yakiniacha nikiogopa na mwenye wasiwasi, nikihofu kuwa mama yangu hangekuwa na utambuzi juu ya mema na mabaya na kwamba angeenda kwenye njia mbaya. Nilimpigia simu mara moja kumwambia juu ya yale mambo yote mabaya ambayo nilikuwa nimeyasoma mtandaoni, lakini mama alikuwa mtulivu sana, na akanifariji kwa kusema: “Mwanangu, hujasoma maneno ya Mwenyezi Mungu kwa hivyo huelewi, na ingechukua muda mrefu kukuelezea, lakini usijali, mimi siendi kwenye njia mbaya. Kwa kweli, ninafuata nyayo za Mwanakondoo. Tusizungumze tena juu ya hili kwenye simu tena.” Nilijua kuwa China inatawaliwa na udikteta unaomkana Mungu, na kwamba serikali ya CCP daima inawatesa na kuwakamata Wakristo, kwa hivyo haikuwa vizuri kwa mama yangu kujadili chochote kuhusu imani kwenye simu. Sikuthubutu kusema mengi sana kulihusu yeye, kwa hivyo nilimpigia simu mchungaji mmoja nchini China ambaye nilikuwa najuana na yeye vizuri kumwomba msaada, nikimsihi aende “amwokoe” mama yangu. Wakati mchungaji baadaye aliniambia habari kwamba alikuwa ameshindwa kumrudisha kwenye zizi, nilikasirika sana kwamba nilipoteza akili. Baada ya hapo, katika jitihada ya kukinga imani ya mama yangu katika Mwenyezi Mungu, hata nilimwambia lazima afanye uchaguzi kati yangu na imani yake katika Mwenyezi Mungu. Baada ya kumwambia hivyo, nilikuwa na ndoto ile ile kwa usiku tatu mfululizo, kwamba ilikuwa usiku wa giza totoro, kulikuwa kunanyesha sana, na nilikuwa nimebeba mwavuli mweusi, nikitembea kando ya bahari niliyokuwa naifahamu wakati mmoja. Hakukuwa na mtu hata mmoja karibu, na ghafla umeme ung’aao kama nuru uliupiga mwavuli wangu…. Kila nilipokuwa na ndoto hii niliamka nikiwa na hofu na nikiwa kijasho baridi, lakini nikiwa bila hisia, mjinga na mkaidi, nilishindwa kufanya juhudi hata kidogo kutafuta na kusali, kubaini ni kwa nini niliendelea kuwa na ndoto hiyo: Je, Bwana alikuwa ananionya na kuniambia nigeuke kutoka kwenye njia ya kumpinga Mungu, na badala yake nimrudie Yeye? Baadaye niliona kwamba haijalishi nilijaribu kumshawishi mama yangu kwa kiasi gani, yote yalikuwa ya bure. Juu ya hiyo nilikuwa katika nchi geni ya mbali na nilikuwa na shughuli nyingi, kwa hivyo niliacha kujaribu kumlazimisha.

Mnamo 2010 niliporudi China mama yangu aliijadili imani yake katika Mwenyezi Mungu na mimi. Alionekana kujua kile nilichokuwa nikifikiria hasa, na akaniuliza waziwazi: “Unajua kuwa nimeamini katika Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa, kwa hivyo unafikiri kuna kitu chochote kigeni kunihusu kama vitu vyote wanavyosema kwenye mtandao?” Nilishindwa na swali lake na sikuweza kujibu mara moja. Kwa kulifikiria kwa makini, niligundua kuwa vile vitu ambavyo walisema mtandaoni ambavyo vilinifanya nitetemeke kwa hofu havikuwa vimemfanyikia mama yangu; alikuwa wa kawaida kabisa, na alisimama mbele yangu mzima mzima. Kwa kweli, niliona kuwa alikuwa amebadilika zaidi tangu kupata imani katika Mwenyezi Mungu kuliko alivyokuwa baada ya kuanza kuamini katika Bwana Yesu. Sio tu kwamba alikuwa amekuwa mwenye busara katika maneno na vitendo vyake, lakini pia alikuwa amepata ufahamu mkubwa zaidi katika kuyachukulia masuala. Kuona haya yote, niliwaza: Inaonekana kama uvumi wa mtandaoni sio wa kweli, kwa sababu ukweli huzungumza zaidi kuliko maneno. Mama yangu kisha akasema, “Kwa nini humwamini mama yako, na kwa nini huangalii ukweli, lakini badala yake unaamini uvumi kwenye mtandao? Je, umechunguza na kukusanya ushahidi juu ya mambo hayo?” Nikiabika, nilimjibu “La, sijafanya hivyo.” Aliendelea: “Hukufanya utafiti wako kujua kuwa yote ni uvumi tu, lakini ukaamini uvumi ambao ulisikia mtandaoni na kufanya hitimisho la ghafla. Aibu kwako kwa kuwa na elimu ya juu sana lakini mwenye kukosa mantiki sana. Unapaswa kuangalia kwa uangalifu Injili Nne, na utaona kwamba wakati Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi Yake makuhani wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo walibuni uvumi na ushuhuda wa uwongo wa kila aina. Walisema kwamba Bwana Yesu alikuwa rafiki wa watenda dhambi, kwamba Alikuwa mtu ambaye hujiendekeza na chakula na pombe, na wakamshutumu kwa uwongo kwamba Anawachochea watu waache kulipa ushuru kwa Kaisari. Hata waliwapa askari rushwa watoe ushahidi wa uwongo, wakawafanya waseme kwamba mwili wa Bwana Yesu uliibwa na wanafunzi Wake na kwamba hakufufuliwa. Kweli unajua kuhusu mambo haya? Kile ambacho Injili Nne zinarekodi ni sehemu ndogo tu ya kazi iliyofanywa na Bwana Yesu, na zina kumbukumbu zilizoandikwa za uvumi mwingi ambao viongozi wa Kiyahudi walieneza kumhusu Bwana Yesu. Je, umefikiria juu ya haya hapo awali? Mtandao ungalikuwepo wakati huo basi makuhani wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo bila shaka wangalieneza uvumi na ushuhuda wao wa uwongo mtandaoni, na maneno yao wakimkashifu, kumkufuru, kumsingizia na kumlaani Bwana Yesu yangekuwa kote mtandaoni kama tu ilivyo na ulimwengu wa kidini leo unavyomlaani Mwenyezi Mungu. Je, unajua hili linamaanisha nini? Bwana Yesu alisema: ‘Hiki ni kizazi kibaya(Luka 11:29). ‘Na hii ndiyo shutuma, ya kwamba mwanga umekuja duniani, na wanadamu walipenda kiza badala ya mwanga, kwa kuwa vitendo vyao vilikuwa viovu. Kwa kuwa kila mtu afanyaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwa mwanga, vitendo vyake visije vikashutumiwa(Yohana 3:19-20). Mwenyezi Mungu alisema: ‘Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja). ‘Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu unaanzia mbali maelfu ya miaka huko nyuma, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunjavunja moyo wa Mungu tangu zamani sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)). Neno la Mungu linafichua wazi asili na kiini cha upinzani wa wanadamu potovu kwa Mungu na jinsi wnavyomchukua Mungu kama adui. Wanadamu wamepotoshwa sana na Shetani, na wanadamu wote wamekuwa maadui wa Mungu, hakuna mtu anayependa ukweli, na hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwa Mungu. Bwana Yesu alipokuwa Yudea akifanya kazi na kuonyesha ukweli, Alitenda miujiza mingi, watu wengi wa kawaida walivutiwa kumfuata, na kwa hivyo viongozi wa Kiyahudi walihofu kuwa watu wote wa kawaida wangemfuata Bwana Yesu na kuwaacha wao. Kwa hivyo, walibuni uvumi na kutoa ushuhuda wa uwongo kumhusu Bwana Yesu, wakampinga na kumshutumu kwa nguvu, na mwishowe wakamsulibisha msalabani. Huu ni uthibitisho thabiti wa wanadamu potovu kuchukia ukweli na kumwona Mungu kama adui. Leo hii Mungu amekuwa mwili tena, na kwa mara nyingine tena anakutana na upinzani na shutuma kali ya wanadamu potovu. Serikali ya CCP inahofu kwamba watu wote watamfuata Mwenyezi Mungu na kupata utambuzi juu ya kiini chake kiovu, kwamba kisha wataikataa, halafu itapoteza nafasi yake ya madaraka. Viongozi katika ulimwengu wa kidini pia wanahofu kwamba waumini watamfuata Mwenyezi Mungu, na kisha watapoteza hadhi na riziki zao. Kwa hivyo, kama tu vile serikali ya Warumi na viongozi wa Kiyahudi wa wakati huo, wanatumia mbinu za kudharaulika na za uovu, wakibuni uvumi wa kila aina na kutoa ushuhuda mwingi wa uwongo juu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hivyo kumkashifu na kumlaani Mwenyezi Mungu na kuliaibisha Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kusudi lao ni kuwafanya watu wasimame na kulaani na kukataa maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu, na kusimama katika njia ya watu kupokea wokovu wa Mungu. Lazima tuwe na utambuzi kuhusu ujanja wa Shetani! Serikali ya CCP ni serikali inayomkana Mungu na ya kishetani ambayo daima imekuwa adui wa Mungu. Ilipoingia katika utawala mara ya kwanza iliharibu nakala za Biblia Takatifu, ikabomoa makanisa, ikawaua Wakristo na hata ikaichukua Biblia Takatifu, kazi inayotambuliwa kote ulimwenguni, kama fasihi ya ibada mbaya na Wakristo na Wakatoliki kama washiriki wa ibada mbaya ili kuwakandamiza na kuwatesa. Hufanya kila uovu unaoweza kuwazika, kwa hivyo ni uvumi gani ambao hawangethubutu kubuni? Ukweli unaonyesha kuwa serikali ya CCP na viongozi katika ulimwengu wa kidini ni ibilisi wa kishetani wanaochukia ukweli na ni maadui wa Mungu. Hili ni jambo ambalo lazima tuone wazi. Sisi ni watu wa imani—lazima tuamini neno la Mungu na lazima tuamini ukweli. Hatuwezi kabisa kuamini uvumi na uwongo wa serikali ya CCP na viongozi katika ulimwengu wa kidini. Tukikosa utambuzi juu ya uvumi ulioenezwa na serikali ya CCP na ulimwengu wa kidini, tusipotafuta na kuchunguza neno na kazi ya Mwenyezi Mungu, basi mwishowe tutakuwa tu kama watu wa kawaida wa Kiyahudi, kumwacha Kristo na kukataa njia ya kweli kwa sababu tunadanganywa na uvumi tunaosikia. Kwa njia hiyo, sio tu kwamba tutapoteza wokovu wa Mungu, lakini mwishowe pia tutapatwa na adhabu ya haki ya Mungu kwa kumpinga Yeye!”

Niliposikiliza kile ambacho mama yangu alisema, nilihisi kana kwamba nilikuwa nikiamka kutoka kwenye ndoto na ikabidi nifikirie juu yake: “Anasema kweli. Kwa nini niliamini kwa upofu hivyo vitu hasi mtandaoni bila kusoma neno la Mwenyezi Mungu au kufanya uchunguzi wowote? Ulimwengu huu umepotoshwa sana na Shetani hadi umejawa na uwongo na udanganyifu; kuna udanganyifu mwingi kila mahali kwamba hatuwezi kweli kujilinda dhidi yake. Sikufanya utafiti wa aina yoyote katika habari hiyo mtandaoni lakini niliamini tu bila kufikiria. Nilikariri kile ambacho kila mtu alisema na nikafanya hitimisho la kiholela. Huo haukuwa uzembe mkubwa na ujinga kwa upande wangu? Hiyo haikuwa kufuata uovu na kutoa hukumu ya kiholela?” Kuona kwamba sikuwa nikisema neno lolote, mama yangu alinipa nakala ya Neno Laonekana katika Mwili na kwa utulivu akasema: “Kitabu hiki kina maneno yaliyonenwa na Mungu katika siku za mwisho. Natumai kuwa utaweza kuweka kando fikira zako na uyaangalie kwa makini. Leta maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo ili tuweze kushirikiana juu yake pamoja.” Nilichukua kitabu hicho na kuanza kukisoma bila kusema neno. Lakini sikuwa nakisoma kwa mtazamo wa kutafuta ukweli. Badala yake, nilikuwa na mawazo ya mtafiti, nikitaka kupima na kuthibitisha maneno ya Mungu dhidi ya maarifa yangu mwenyewe, na hata nilitaka kuyakanusha. Ilikuwa ni kwa sababu ya tabia yangu isiyoheshimu vitu vitakatifu na ya kinyume na maneno ya Mungu kwamba sikuweza kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, sana kiasi kwamba wakati wote sikuwa ninaifahamu kazi ya Mwenyezi Mungu. Lakini hata hivyo, niliendelea kushikilia fikira zangu zenye makosa na sikutaka kukubali kazi mpya ya Mungu. Nilijadili hili na mama yangu: “Mama, hapo awali, niliamini uvumi wote ambao nilisikia kwenye mtandao, na nikajaribu kukuzuia usimwamini Mwenyezi Mungu, lakini kwa kweli ni mimi niliyekuwa kipofu na mjinga. Kuanzia sasa, sitaipinga imani yako katika Mwenyezi Mungu, lakini siwezi kuomba na wewe katika jina la Mwenyezi Mungu, kwa sababu nililiita jina la Bwana Yesu nilipotahini kuingia katika shule ya ndoto zangu na kupokea udhamini kamili wa kuendeleza masomo yangu ughaibuni. Nimepokea neema kubwa mno, kwa hivyo ninawezaje kumwacha Bwana Yesu? Hili halitakuwa ukosefu wa shukrani na udanganyifu?” Alinipa kifungu kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu kusoma ambacho kilielekezwa kwa hii fikira yangu: “Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu. Sasa, lazima uelewe kwamba kazi yote kutoka awamu ya kwanza hadi leo ni kazi ya Mungu mmoja, ni kazi ya Roho mmoja, ambapo hakuna shaka(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). Kisha alishiriki nami ushirika huu: “Unadhani kwamba kukubali jina la Mwenyezi Mungu ni kumsaliti Bwana Yesu, lakini hii ni fikira na mawazo yako mwenyewe. Kwa kweli, Yehova Mungu, Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni wote Mungu mmoja. Katika Enzi ya Sheria, Mungu aliitwa kwa jina la Yehova; Alitoa sheria za kuongoza maisha ya wanadamu duniani na Alimfanya mwanadamu afuate sheria na maagizo Yake ili Awatawale na kuwaongoza binadamu. Kuelekea mwisho wa Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wamepotoshwa na Shetani kwamba hawangeweza kuendelea kufuata sheria, na wanadamu wote walikuwa wakiishi chini ya shutuma na laana ya sheria. Mungu alikuwa mwili Akitumia jina la Yesu ili kutekeleza kazi ya Enzi ya Neema, na ili kumkomboa mwanadamu Alisulubiwa msalabani kama sadaka ya dhambi ya milele kwa mwanadamu. Tangu wakati huo, mradi tu tunakuja mbele za Mungu kukiri dhambi zetu na kutubu, basi dhambi zetu zitasamehewa na hatutashutumiwa tena au kulaaniwa na sheria. Juu ya hayo, tunapokea pia baraka na huruma nyingi za Bwana. Hata hivyo, hata ingawa dhambi zetu zinaweza kusamehewa na tunaweza kufurahia neema nyingi za Bwana Yesu, asili yetu ya dhambi na tabia zetu potovu hazijaondolewa. Bado tunaishi katika mzunguko mbaya wa kutenda dhambi na kisha kuziungama, tuziweze kujinasua. Katika siku za mwisho, Mungu amekuwa mwili tena kama Mwenyezi Mungu kuonyesha ukweli ambao utamhukumu na kumtakasa mwanadamu; hili linamruhusu mwanadamu kufahamu ukweli na kupata ukweli kupitia hukumu ya Mungu, tutupilie mbali tabia zetu potovu za kishetani, tutakaswe kabisa na Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha mfano halisi wa binadamu. Kwa njia hii, mwishowe mwanadamu anaweza kustahili kurithi ahadi za Mungu na kuletwa ndani ya ufalme Wake. Kwa hivyo, Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu wote ni kupata mwili kwa Mungu katika enzi tofauti, na Wao ni Mungu mmoja.”

Ushirika wake ulikuwa wa maana na hakuna kitu ambacho ningepinga, lakini fikira zangu zilikuwa rudufu, kwa hivyo nilijibu mara moja: “Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerejea, basi nikimwita kwa jina Yesu au jina Mwenyezi Mungu ni yote sawa. Kwa njia yoyote ile, Yeye ndiye Mungu anayetoa neema.” “Yehova Mungu, Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja,” mama yangu akajibu, “hili bila shaka ni kweli, lakini Mungu huchukua jina tofauti katika kila enzi. Kwa hiyo, tunaweza tu kupokea wokovu wa Mungu kwa kukubali jina jipya la Mungu. Ni kama ambavyo katika Enzi ya Sheria Mungu alitumia jina Yehova kutekeleza kazi, na watu waliomba katika jina la Yehova, na Mungu alimsikiliza na kumbariki mwanadamu. Kisha, katika Enzi ya Neema Mungu alitumia jina la Bwana Yesu kutekeleza kazi, na kisha watu walihitaji kuomba katika jina la Yesu, la sivyo dhambi zao hazingesamehewa, wala hawangepokea neema na baraka za Bwana. Ni kama tu ambavyo Waisraeli waliomlilia Yehova Mungu kwenye hekalu hawakuwa na uwepo wa Mungu na hawakupokea wokovu wa Bwana Yesu kwa sababu hawakulikubali jina la Bwana Yesu. Sasa ni Enzi ya Ufalme na Mungu anatumia jina Mwenyezi Mungu kutekeleza kazi mpya. Ni kwa kuomba tu katika jina la Mwenyezi Mungu ndipo unaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kupokea wokovu wa Mungu. Ukishikilia jina Yesu na usikubali jina Mwenyezi Mungu, basi kwa kweli unaamini kazi ya zamani ya Mungu na unaipinga kazi ya sasa ya Mungu, ambayo kiasili ni kumpinga na kumsaliti Mungu. Biblia Takatifu inasema: ‘Unalo jina unaloishi, nawe ni mfu(Ufunuo 3:1). Ni kwa kukubali jina mpya la Mungu tu na kutii neno na kazi Yake ya sasa ndipo tutakapokuwa na uhalisi wa imani katika Mungu. Je, unaelewa ninachosema?”

Nilihisi kuwa kila kitu ambacho mama yangu alikuwa akisema kilikuwa cha busara na pia cha vitendo, lakini moyoni mwangu bado singeweza kuliachilia jina Yesu, kwa sababu Bwana alikuwa amenipa neema kubwa mno. Kila kitu nilicho nacho leo nimepewa na Bwana Yesu, na singekosa kufuata ahadi yangu ya asili: kutenda vizuri imani yangu katika Bwana na kumfuata Bwana. Na matokeo yake, niliendelea kuikataa injili ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya likizo yangu ya msimu wa joto kumalizika na nikarudi Marekani, masomo yangu mengi na maisha ya kasi sana yalinirudisha katika ulimwengu “halisi” kwa haraka. Kila niliporudi kwenye huduma za kanisa, niligundua kuwa hakuna mahubiri yoyote yaliyokuwa na kitu chochote kipya, bila kujali ilikuwa ni mchungaji katika kanisa la Kichina au kanisa linalozungumza Kiingereza. Vyote vilikuwa tu ni wimbo na densi zile zile za zamani kila wakati. Maisha ya kanisa yalikuwa ya kuchosha na haikuhisi kama kwamba nilikuwa nikipata riziki yoyote maishani mwangu. Katika jitihada za kushikilia kundi lao, wafanyakazi wenza wa kanisa mara nyingi wangepanga safari, matembezi, sherehe na shughuli zingine za sisi kuhudhuria. Kulikuwa na watu wa kila aina kanisani, ikiwemo watu wengi ambao hawakuwa watafutaji wa kujitolea sana, lakini badala yake ni watu tu wanaotafuta mchumba wa kiume au wa kike, mtu wa kuishi naye chumbani, mtu wa kusafiri naye, mtu wa kula naye, nk, na nikagundua kuwa kanisa halikuwa tena mahali ambapo ningeweza kupata amani ya mawazo. Hili lilinijaza uchungu na huzuni. Baadaye niliacha kushiriki katika ibnada kabisa, lakini nilikuwa katika hali ya wasiwasi kila wakati. Nilihisi kama mtoto mpotevu aliyepotea na nilikuwa nikipita maishani kwa bumbuwazi tu.

Baada ya kujifungua mtoto wa kiume mnamo mwaka wa 2014, ugomvi kati yangu na mume wangu ulizidi kuongezeka kwa sababu sikuwa na maziwa yoyote ya matiti ya kumnyonyesha mtoto wetu. Alipofika nyumbani kutoka kazini kila siku, jambo la kwanza kutoka kinywani mwake lilikuwa: “Inawezekenaje kuwa bado hakuna kitu hapo? Bila maziwa ya matiti kinga ya mwili ya mwanangu ingekuwa hatarini.” Hii ilikuwa mara ya kwanza kuwa na hisia kama hii ya kutokuwa na uwezo—nilihisi kana kwamba sikustahili kabisa kuwa mama. Niliwatembelea madaktari wa Magharibi na wa Kichina, na hata nikatafuta tiba za kinyumbani mtandaoni, lakini hakuna kitu kilichonisaidia kutoa maziwa. Nilihisi uchungu, mwenye huzuni, na hasira, kana kwamba nilikuwa karibu kuchanganyikiwa, na nilihisi kwamba kama hilo lingeendelea kweli ningepoteza akili yangu hivi karibuni. Katika muda wangu wote wa kupata ahueni baada ya kujifungua uso wangu ulikuwa na machozi kila wakati, na bila kujali nilichofanya, sikuweza kuelewa kwa nini hili lilikuwa likinitendekea. Mara nyingi nilihisi woga usioelezeka ukinijia, na ningesikia tu maneno kama “maziwa ya mama” au “kulisha,” na mara moja ningeangua kilio, nikishindwa kabisa kujidhibiti.

Baada ya mama yangu kujua kuhusu hali ngumu niliyokuwamo, alikuja ughaibuni ili kunitunza. Alipoona nilivyokuwa nateseka aliniambia: “Umewahi kufikiria kuhusu ni kwa nini kuna giza zaidi na zaidi katika maisha yako, kwa nini yamejaa mateso zaidi na zaidi? Ni kwa sababu unaamini katika Mungu lakini hutafuti ukweli. Bwana amerudi, lakini hutafuti au kuchunguza. Badala yake, unashikilia fikira na mawazo yako mwenyewe, ukifuata tu yale ambayo kila mtu mwingine anasema na kuihukumu kazi mpya ya Mungu kiholela. Huku ni kumpinga Mungu! Huikubali kazi mpya ya Mungu, kwa hivyo umepoteza utunzaji na ulinzi wa Mungu. Unaishi chini ya umiliki wa Shetani, na hili litakuacha tu ukiwa umeteswa na kuchezewa na Shetani, akijaza maisha yako kwa mateso mengi zaidi na zaidi.” Kumsikia mamangu akisema maneno haya, nilinyamaza kimya. Katika siku zilizofuata, kila wakati mama alipomlaza mtoto wangu, angeniwekea nyimbo za maneno ya Mungu ili nisikilize. Kitu cha ajabu kilitendeka—mawazo yalianza kupata amani pole pole pamoja na muziki wa nyimbo hizi. Wakati mmoja, nilisikiza wimbo huu: “moyo wa mwanadamu na roho yake viko mbali sana na Mungu. Hivyo, wakati mwanadamu anamfuata Mungu, Anachukua mfano wa mtumishi wa Shetani. Kamwe haoni hili. Hakuna aliye na ari ya kutafuta nyayo za Mungu ama kuonekana kwa Mungu. Hakuna anayetaka kuwepo na kuishi katika ulinzi na utunzaji wa Mungu. Lakini wanchagua kuharibiwa na Shetani na yule muovu kubadilika na kuzoea ulimwengu huu na kujibadili wenyewe kwa masharti ya maisha yanayofuatwa na binadamu mwovu. Katika hatua hii, moyo na roho ya mwanadamu vinageuka kuwa zawadi ambayo mwadamu anampa Shetani. Moyo na roho ya mwanadamu vinageuka kuwa chakula cha Shetani, hata mahali ambapo anaishi, na uwanja wa kuchezea. Kwa njia hii, mwanadamu bila kujua anapoteza kanuni zake za jinsi ya kuwa binadamu. Na hajui tena thamani na kusudi la kuwepo kwake. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu inapotea polepole katika moyo wa mwanadamu. Mwanadamu hatafuti tena wala kumsikiliza Mungu, hatafuti tena wala kumsikiliza Mungu. Muda unavyopita, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, wala haelewi maneno kutoka kwa Mungu ama kuelewa yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu anaanza kupinga sheria za Mungu na amri kutoka kwa Mungu; moyo wa mwanadamu na roho ya mwanadamu, moyo na roho ya mwanadamu inakufa ganzi. … Mungu anampoteza mwanadamu asili Aliyemuumba, na mwanadamu anapoteza asili ya mwanzo wake. Hii ndiyo huzuni ya binadamu huyu(“Huzuni ya Binadamu Aliyepotoka” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila mojawapo ya mstari wa mwisho wa maneno ya Mwenyezi Mungu uliushika moyo wangu. Niliweza kuona kuwa nilikuwa hasa katika hali iliyoelezwa na maneno ya Mungu, kwamba nilikuwa nimemtambua Mungu kwa maneno yangu, lakini kwa kweli moyo wangu ulikuwa umepagawa na Shetani kabisa. Mawazo na hisia zangu zote zilikuwa kuhusu masuala ya mwili, kile nilichokuwa nikifuatilia pia ulikuwa mwili, na niliyokuwa nikiifuata ilikuwa njia ya kidunia. Katika Biblia Takatifu inasema: “Kwani kujali mwili ni kifo; lakini kujali roho ni uhai na amani” (Warumi 8:6). “Hamjui kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? basi yeyote atakayekuwa rafiki wa dunia ni adui wa Mungu” (Yakobo 4:4). Nilifikiria juu ya jinsi ambavyo hakukuwa na chochote kuhusu vitendo vyangu vyovyote ambavyo vililingana na mapenzi ya Mungu, lakini yote yalienda kinyume kabisa na Mungu. Nilikuja mbele za Mungu na kuomba: “Ee Mungu, niko katika hali hii leo kwa sababu ninathamini shahada yangu, utambulisho, ndoa na mambo mengine ya ulimwengu huu, nikifikiria kwamba kuwa na vitu hivi kunapaswa kutosha. Sijatafuta ukweli tu, wala sijafuatilia maarifa ya Mungu, hadi kiwango kwamba kila wakati ambapo Umeubisha mlango wa moyo wangu na kuliweka neno la Mungu na ukweli mbele ya macho yangu, nimekosa kuthamini hili. Niliposikia kwamba Umekuja kutekeleza kazi mpya, nilikuwa mgumu na mwenye maoni mengi, na nikatoa maamuzi yasiyo na msingi. Nilikuwa najua kabisa kuwa kulikuwa na sababu katika ushirika wa mama yangu, lakini niliendelea kushikilia mawazo yangu mwenyewe bila kuchunguza njia ya kweli. Ee Mungu, nilichothamini ni neema Yako huku nikataa ukweli—kwa kweli nilikuwa mkaidi na mwasi! Ikiwa bado Utanipa nafasi, hakika nitaichunguza kazi Yako kadri ya uwezo wangu.” Wakati huo sikujua kama maombi ya aina hiyo yangesikika na Mungu, lakini bado niliendelea kumlilia Mungu kwa njia hii.

Mnamo Aprili 2015 nilirudi China pamoja na mama yangu kwa sababu ya shida ya kiafya, jambo ambalo lilinipa nafasi ya kuwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilifikiria kuhusu jinsi nilivyojitahidi na kupambana katika ulimwengu huu bila kupata furaha, na jinsi katika dini vile vile nilikuwa nimeshindwa kupata ukweli ambao ungeweza kutoa giza na utupu ndani ya moyo wangu. Nilikuwa na hisia hii kali moyoni mwangu kwamba labda ni kwa sababu Mwenyezi Mungu, ambaye nilikuwa nimeendelea kabisa kutomkubali, alikuwa Mwokozi Yesu ambaye alinisaidia kutahiniwa kuingia chuoni na kunipeleka Marekani. Hili liliponitokea, nilimwambia mama yangu kuwa nilitaka kushiriki katika shughuli za kanisa katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Muda si muda, ndugu kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuja kukutana nami, na niliona kwamba walipokutana, kile walichosoma kilikuwa neno la Mungu, kile walichoshirikiana kuhusu kilikuwa ukweli, na kile walichotenda kilikuwa ukweli. Haijalishi kile walichofanya, maneno ya Mungu yalitumika kama kiwango chao na ukweli ulitumika kama kanuni yao. Hawakutenda kulingana na mwili, wala hawakuwa na shughuli za kidunia wao kwa wao. Niliona kuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu ndilo nchi nzuri ya Kanaani ambako ukweli unatawala. Roho yangu ilijaa mahali hapo, niliruzukiwa, na moyo wangu haukuwa mtupu tena—nilipata hisia ya ukamilifu.

Siku moja katika mkutano mwingine na ndugu fulani, Dada Wang alisoma kifungu hiki kutoka katika maneno ya Mungu: “Mwenye uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana. Wakati uo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na fahamu, maana imembidi Asubiri sana kupata jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako, kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo utarudisha ghafla kumbukumbu yako: ukitambua ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, lakini wakati fulani usiojulikana ukapoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ukaanguka barabarani ukiwa hujitambui na tena wakati fulani usiojulikana ukampata ‘baba.’ Isitoshe, unagundua kuwa Mwenye uweza amekuwa hapo muda huo wote, akiangalia, akisubiri kurejea kwako, kwa muda mrefu sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza). Kifungu hiki cha maneno ya Mungu kilinigusa sana. Nilihisi kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa tu kama mama mwenye upendo anayemwita mtoto aliyepotea, Akingoja kwa hamu mtoto Wake siku moja arudi upande Wake. Niliweza kusikia kuwa hii ilikuwa sauti ya Bwana. Niligundua kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyenisaidia tena na tena kuishinda shida moja baada ya nyingine, na kwamba hakuwahi kuniacha kamwe hata kwa hatua moja njiani, lakini Alingojea kwa kunishughulikia ili nigeuke. Nilifikiria kuhusu jinsi nilivyomwamini Mungu lakini bado sikutafuta ukweli au kuamini maneno ya Mungu, lakini badala yake niliamini uvumi wa mtandaoni na maneno ya wachungaji. Nilikuwa nimempa adui utii wangu, nikijiunga na serikali ya CCP na wachungaji katika jamii za kidini katika kumshushia hadhi na kumshambulia Mungu, ambaye alikuwa akinijali usiku na mchana. Nilikuwa nimeukataa wokovu wa Mungu. Kwa kweli nilikuwa kipofu na mjinga. Imani yangu katika Mungu bado ilikuwa inategemezwa katika fikira na mawazo yangu mwenyewe; niliamini kuwa Bwana Yesu alikuwa amenisaidia kutahiniwa kuingia katika chuo kikuu na kunielekeza kwenda ughaibuni bila hitilafu kuendeleza masomo yangu, kwa hivyo ilibidi kila wakati niwe mwaminifu kwa jina la Bwana Yesu, na kwamba huku pekee ndiko kulikuwa kujitolea kwa Bwana. Nilitegemea fikira na mawazo yangu katika mtazamo wangu wa mambo. Wakati Mungu alianzisha enzi mpya na kuchukua jina jipya sikuitambua kazi ya Mungu, na mara kwa mara nilikataa wokovu wa Mungu kwangu. Huko kulikuwaje kuwa na imani kwa Mungu? Hakukuwa tu kuwa na imani ndani yangu? Kila ambacho Mungu alikuwa amenipa kilikuwa upendo, lakini muda baada ya muda nilimwumiza Mungu. Nilijua nilimwia Mungu sana….

Ilinibidi nipige magoti chini kabisa, na nililia machozi machungu huku nikimwomba Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu! Nimekuwa kipofu na mjinga. Niliamini uvumi wa serikali ya CCP na ulimwengu wa kidini; nilikutelekeza na kukulaani, na nilitegemea fikira na mawazo yangu mwenyewe ili kukuwekea mipaka. Niliikataa injili Yako ya siku za mwisho—mimi ni Mfarisayo wa wakati wa sasa. Kwa msingi wa tabia na matendo yangu tu napaswa kuangamizwa pamoja na Shetani, lakini, kwa sababu ya upendo Wako kwangu, muda baada ya mwingine Umenipa nafasi za kutubu. Ee Mungu, niko tayari, kama tu vile watu wa Ninawi, kuja mbele Yako ‘katika nguo za magunia na majivu,’ kukiri dhambi zangu Kwako na kutubu, na kukuomba Unionee huruma. Natamani kushirikiana na Wewe, na kutakaswa na kuokolewa na neno Lako.”

Baada ya hayo, ndugu kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu wangekuja kukutana nami mara tatu kwa wiki; hili liliendelea bila kukatizwa kwa zaidi ya miezi minne. Wakati huu nilisoma vifungu kadhaa kutoka katika neno la Mungu karibu kila siku, na kadiri nilivyoelewa ukweli zaidi na zaidi, uhusiano wangu na Mungu ulizidi kuwa unaofaa na imani yangu ya asili ilirejeshwa. Nilihisi amani moyoni mwangu, na sikuhisi wasiwasi au ukiwa tena. Kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kukutana kufanya ushirika juu ya ukweli, nilikuja kuwa na hakika kabisa kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu ambaye nilikuwa nimetamani sana kurudi Kwake. Nilifanya azimio kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho wa njia, na kulipa upendo wa Mungu kwa kuwa mtu anayefuatilia ukweli.

Nilirudi Marekani mnamo mwaka wa 2016, ambako niliwasiliana na ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu kupitia tovuti yao na nikaanza kushiriki katika shughuli kanisani kwao. Shukrani ziwe kwa Mungu! Ni Mungu aliyeniongoza kila hatua ya njia kufikia pale nilipo sasa. Ili kumlipa Mungu kwa ajili upendo Wake, nataka kutoa nguvu zangu zote kutekeleza kazi ya kueneza injili ya Mungu, ili watu wengi zaidi ambao wana kiu ya ukweli na waotafuta ukweli waweze kujua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerejea. Pia nitawaambia kwamba wakifuata nyayo zangu—wakiamini uvumi wa Shetani bila kufikiria, wakimpinga Mungu pamoja na Shetani—mwishowe, wao tu ndio watakaopoteza.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nimekaribisha Kurudi Kwa Bwana

Na Chuanyang, Vereinigte StaatenMajira ya baridi kali ya mwaka wa 2010 huko Amerika yaliniacha nikihisi baridi sana. Kando na baridi kali...

Sikiliza! Ni Nani Huyu Anenaye?

Na Zhou Li, ChinaKama mhubiri wa kanisa, hakuna jambo linaloumiza zaidi kama udhaifu wa kiroho na kutokuwa na lolote la kuhubiri. Nilihisi...

Upendo wa Aina Tofauti

Na Chengxin, BrazilNafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp