Njia ya Utakaso

24/12/2019

Na Christopher, Ufilipino

Jina langu ni Christopher, na mimi ni mchungaji wa kanisa la nyumbani huko Ufilipino. Mnamo mwaka wa 1987, nilibatizwa na nikamgeukia Bwana Yesu na kisha kwa neema ya Bwana, mnamo mwaka wa 1996 nikawa mchungaji katika kanisa la mtaa. Wakati huo, sikuwa nikifanya kazi tu na kuhubiri katika maeneo mengi karibu na Ufilipino, lakini pia nilikuwa nikihubiri katika sehemu kama vile Hong Kong na Malaysia. Kupitia kazi ya Roho Mtakatifu na mwongozo Wake, nilihisi kuwa nilikuwa na nguvu isiyoisha katika kazi yangu kwa Bwana na msukumo usiokuwa na mwisho katika mahubiri yangu. Mara nyingi, niliwapa msaada ndugu ambao walikuwa wakihisi hasi na dhaifu. Wakati mwingine wakati wanafamilia wao makafiri walipokuwa wakali kwangu, bado nilikuwa na uwezo wa kuwa mvumilivu na mwenye subira; sikupoteza imani katika Bwana na niliamini kuwa Bwana angeweza kuwabadilisha. Kwa hivyo, nilihisi kama kwamba nilikuwa nimebadilika sana tangu nilipoanza kuwa muumini. Hata hivyo, kuanzia mwaka wa 2011, sikuwa tena na uwezo wa kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu kwa uzito kama hapo awali. Nilipoteza nuru mpya katika mahubiri yangu polepole na nikakosa nguvu ya kuacha kuishi dhambini. Sikuweza kujizuia kukasirishwa na mke wangu na binti yangu nilipowaona wakifanya mambo ambayo sikuyapenda na nikawakemea kutokana na hasira. Nilijua kuwa jambo hili halikupatana na mapenzi ya Bwana, lakini mara nyingi sikuweza kujizuia. Jambo hili lilinisikitisha sana. Ili kujikomboa kutoka kwa maisha ya kutenda dhambi na kisha kukiri, nilijitahidi zaidi kusoma Biblia, kufunga na kusali, na nikawatafuta wachungaji wa kiroho kila mahali ili tuweze kutafuta na kuchunguza jambo hili pamoja. Lakini juhudi zangu zote ziliambulia patupu; hakukuwa na mabadiliko katika maisha yangu ya dhambi na giza iliyokuwa ndani ya roho yangu.

Njia ya Utakaso

Kisha jioni moja mnamo majira ya kuchipua mwaka wa 2016, mke wangu aliniuliza, “Christopher, nimegundua kwamba umekuwa ukitaabika sana hivi karibuni. Unafikiria nini?” Nilimwambia kilichokuwa kikinisumbua, “Nimekuwa nikjiuliza miaka michache iliyopita kwa nini siwezi kuacha kuishi katika dhambi licha ya kuwa mchungaji na kumwamini Bwana kwa miaka mingi. Siwezi tena kumhisi Bwana—ni kama kwamba Ameniacha. Hata ingawa mimi huenda kila mahali kuhubiri, mara tu ninapokuwa na wakati wangu mwenyewe, haswa usiku wa manane, kila wakati ninahisi utupu na wasiwasi, na hisia hii inakua tu. Nafikiri juu ya jinsi nilivyomwamini Bwana miaka hii yote, nimesoma sana Biblia, nimesikiza mahubiri mengi ya Bwana, na mara nyingi nimeamua kuubeba msalaba na kujishinda, lakini mimi hufungwa na dhambi siku zote. Ninaweza kusema uwongo ili kulinda maslahi yangu na heshima yangu, na nashindwa kufuata ‘Na vinywani mwao hakukuwa na hila(Ufunuo 14:5). Ninapokumbana na dhiki na usafishaji, ingawa najua haya yanatokea kwa idhini ya Bwana, bado siwezi kujizuia kulalamika juu ya Bwana na kumwelewa visivyo. Nashindwa kabisa kujihini kwa hiari. Ninahofu kwamba, kuishi katika dhambi kwa njia hii, Bwana atakapokuja, sitaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni!”

Aliposikia haya, mke wangu alisema, “Christopher, unawezaje kufikiria hivi? Lazima uwe na imani; wewe ni mchungaji! Ingawa tunaishi katika dhambi na hatujaachana na dhambi, Biblia inasema, ‘Kwamba ikiwa utamkubali Bwana Yesu kwa mdomo wako, na utasadiki ndani ya moyo wako kwamba Mungu amemfufua kutoka kwa wafu, wewe utaokoka’ (Warumi 10:9). ‘Kwani yeyote ambaye ataliita jina la Bwana ataokolewa’ (Warumi 10:13). Mradi tuendelee kusoma Biblia, kuhudhuria mikutano, kumwomba Bwana, na kuubeba msalaba, tukimfuata bila kukosea mpaka kuja kwa pili kwa Bwana, tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupokea baraka za Bwana.”

Kisha nilimwambia mke wangu, “Nilifikiri hivyo hapo awali, lakini katika 1 Petro 1:16 inasema: ‘Kwa kuwa imeandikwa, Kuweni watakatifu; kwani mimi ni mtakatifu.’ Nimemwamini Bwana kwa miaka thelathini, lakini siwezi kufuata njia ya Bwana na, kuishi katika dhambi, bado ninaweza kumpinga Bwana. Sitoshelezi matakwa ya Bwana hata kidogo. Ah! Nimeamua mara ngapi kutii mafundisho ya Bwana, lakini sijaweza kutia maneno Yake katika vitendo. Ninawezaje kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni hivi? Bwana Yesu alisema: ‘Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Kulingana na maneno ya Bwana, kuingia katika ufalme wa mbinguni si rahisi kama tunavyofikiria. Bwana ni mtakatifu, kwa hivyo watu ambao hawawezi kutia neno Lake katika vitendo na ambao wanampinga mara kwa mara wanawezaje kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni? Ni wale tu ambao wamebadilika na hufanya mapenzi ya Mungu ndio wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni!”

Mke wangu alifikiria kwa muda na akasema, “Unachosema kinaleta maana. Bwana ni mtakatifu na sisi bado ni wenye dhambi. Hatustahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Ni kwamba tu … nimekumbuka ghafla … si Mchungaji Liu alimwalika Mchungaji Kim wa Korea kanisani? Unaonaje tukichunguza suala hili?” Nilisema: “Naam, hilo ni wazo zuri. Bwana Yesu alisema: ‘Ombeni, na mtapatiwa; tafuteni, na mtapata; pigeni hodi, na mtafunguliwa(Mathayo 7:7). Alimradi tutafute, naamini kuwa Bwana atatuongoza. Kama mchungaji, lazima nizingatie maisha ya ndugu zetu. Nikiwa mwenye kiburi katika imani yangu, nitakuwa nikijifanyia mimi mwenyewe na wao pia tendo linalodhuru. Hebu tusubiri hadi Mchungaji Kim atakapokuja kisha tutafute kutoka kwake kuhusu suala hili.”

Kwa kuwa nilikuwa nikipanga kumtafuta Mchungaji Kim, nilitaka kujua machache kuhusu malezi yake. Nilikwenda mtandaoni kutafuta kanisa la Kikorea alilokuwa akishiriki. Kwenye kurasa zilizoibuka, niliona wavuti https://www.holyspiritspeaks.org. Nilipofungua, maneno haya yalinivutia: “Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Haya yaliandikwa vizuri sana kiasi kwamba ilibidi niendelee kusoma: “Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Kusoma maneno haya kulinisisimua sana. Ingawa sikuweza kuyaelewa kabisa na mengine hata yalikuwa fumbo kwangu, maneno haya yaliniruhusu nione matumaini kiasi. Nilihisi kuwa ndani ya hili ningepata njia ya kujitakasa na kujibadilisha. Nilimshukuru Mungu kwa dhati kwa kusikia ombi langu. Nilipokuwa nikiendelea kusoma, nilihisi kuwa kweli haya yalikuwa maneno mazuri ambayo yalinyunyizia na kuchunga roho yangu iliyokuwa na kiu. Niliona hili kwenye wavuti: “Ikiwa huwezi kupata simu ya moja kwa moja ya nchi au eneo lako, tafadhali tuachie ujumbe na tutawasiliana nawe haraka iwezekanavyo.” Nilitazama haraka na sikuona simu ya moja kwa moja ya Ufilipino, kwa hivyo niliandika ujumbe mara moja, na kuandika nambari yangu ya mawasiliano na anwani ya barua pepe bila kusita.

Baada ya kufika nyumbani jioni hiyo, nilimweleza mke wangu kuhusu tukio hilo na baada ya kusikia kile nilichosema, alikuwa tayari kutafuta pia. Namshukuru sana Bwana kwamba walijibu ujumbe wangu siku iliyofuata na wakapanga kuungana na sisi alasiri hiyo hiyo. Alasiri hiyo, tulizungumza na Dada Liu na Dada Su. Kutoka kwa mazungumzo hayo, nilihisi kuwa walizungumza kwa urahisi, kwa ustadi na kwa utambuzi. Mke wangu alikuwa na wasiwasi hata zaidi kuniliko na akasema, “Naweza kuuliza swali?” Walisema kwa shauku, “Bila shaka.” Mke wangu alijibu, “Kwenye wavuti yenu ya kanisa inasema kuwa, ‘Mungu wa siku za mwisho amefanya hatua ya kazi ya hukumu na kuadibu.’ Mimi na mume wangu tunajua kuwa hakuna mtu asiye mwenye haki atakayemwona Bwana kwa sababu Yeye ni mtakatifu, lakini katika Warumi inasema kwamba, ‘Kwamba ikiwa utamkubali Bwana Yesu kwa mdomo wako, na utasadiki ndani ya moyo wako kwamba Mungu amemfufua kutoka kwa wafu, wewe utaokoka’ (Warumi 10:9). ‘Kwani yeyote ambaye ataliita jina la Bwana ataokolewa’ (Warumi 10:13). Tukimwamini Bwana Yesu basi tumeokolewa tayari na tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni, kwa hivyo kwa nini Mungu wa siku za mwisho anafanya hatua ya kazi ya hukumu na kuadibu? Sina hakika juu ya suala hili na ninatumai kusikia maoni yenu.”

Dada Liu alijibu, “Shukrani kwa Mungu! Acha tufanye ushirika na hebu Mungu atuongoze. Kwanza hebu tuangalie ‘kuokolewa’ kunamaanisha nini hapa. Katika kipindi cha mwisho cha Enzi ya Sheria, watu wote walikuwa wamejitenga na Mungu na hawakuwa na mioyo inayomcha Mungu. Walikuwa wamezidi kuwa wenye dhambi na wakavuka mipaka hadi wakatoa mifugo na ndege vipofu, viwete na wagonjwa kama dhabihu. Watu wa wakati huo hawakutetea tena sheria na wote walikuwa katika hatari ya kuhukumiwa kifo kwa kukiuka sheria. Kwa kuzingatia hali hiyo, ili kuwaokoa wale walioishi chini ya sheria toka kwa kifo cha hakika, Mungu Mwenyewe alikua mwili na akaanza kazi ya ukombozi, na mwishowe Alisulibiwa ili kuwakomboa wanadamu wote kutoka dhambini. Watu waliweza kusamehewa dhambi zao kwa kumwamini Bwana Yesu, na hivyo wakastahili kuja mbele za Mungu katika sala na kufurahia neema na baraka za Mungu. Hii ndio maana ya kweli ya ‘kuokolewa’ katika Enzi ya Neema. Kwa maneno mengine, ‘kuokolewa’ ni dhambi za mtu kusamehewa tu. Yaani, Mungu hawaoni watu kama waliotiwa waa na dhambi tena, lakini hiyo haimaanishi kuwa wao sio wenye dhambi kiasili. Kwa hivyo, kuokolewa hakumaanishi kuwa tumetakaswa kabisa na tumepata wokovu kamili. Ikiwa tunataka kutakaswa, lazima tukubali kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.”

Ni baada tu ya kusikia ushirika wao ndio mimi na mke wangu tulielewa kuwa “kuokolewa,” kama inavyozungumziwa katika Waraka wa Warumi, kulimaanisha kukubali wokovu wa Bwana Yesu na kutohukumiwa tena kifo kwa kukiuka sheria. Hakukuwa “kuokolewa” ambako tulifikiria, kwa kutakaswa kabisa. Walichosema kilileta maana. Maelezo hayo ya “kuokolewa” yanapatana na hali yetu ya kuishi katika hali ya kutenda dhambi na kisha kuungama dhambi hizo. Kwa hivyo, aliyofanya Bwana Yesu ilikuwa kazi ya ukombozi tu, sio kazi ya kumtakasa kabisa na kumokoa mwanadamu. Ingawa mara tu watu wanapomwamini Bwana wameokolewa, hii haimaanishi kuwa wametakaswa kabisa. Niliposikiliza ushirika wao, nilihisi kwamba kulikuwa na ukweli wa kutafutwa ndani ya ushirika huo, kwa hivyo nilieleza dhamira yangu ya kuendelea. Nilisema, “Shukrani kwa Bwana! Unachosema ni cha ajabu. Kutoka kwa ushirika huu na ninyi sasa tunaelewa maana ya kweli ya ‘kuokolewa.’ Tafadhali endelea na ushirika wako, na Bwana atuongoze.” Dada Su aliendelea kusema, “Safi sana, acha tusome vifungu vichache vya neno la Mwenyezi Mungu na yote yatakuwa wazi. Mwenyezi Mungu alisema: ‘Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (2)). ‘Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). ‘Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Tunaweza kuona kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu kuwa tukifuata kazi ya Mungu ya ukombozi kuanzia Enzi ya Neema na tusikubali kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, basi kiini cha kuwa na dhambi kwetu hakuwezi kutatuliwa. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho amewadia na anatekeleza hatua ya kazi kwa msingi wa kazi ya ukombozi, Akihukumu na kumtakasa mwanadamu. Ananena ukweli ili kufichua ukweli wa upotovu wa mwanadamu, Akihukumu asili ya kihetani. Amekuja kubadilisha tabia ya kishetani, ili kuwaokoa kabisa kutokana na ushawishi wa Shetani ili waweze kupata wokovu kamili. Ni dhahiri kwamba kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ni kazi muhimu na ya msingi ya kuwasafisha, kuwaokoa na kuwakamilisha watu. Kwa hivyo, ni kwa kukubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho tu ndiyo tunaweza kupata ufahamu wa kweli kuhusu asili yetu potovu na tabia ya Mungu yenye haki, kuachana kabisa na ushawishi wa Shetani, kuokolewa kabisa na Mungu na kuwa watu wanaotii, wanaoabudu na wanaolingana na Mungu.”

Njia ya Utakaso

Moyo wangu ulichangamka kutokana na kusikia ushirika huu wote, na nilihisi kama kwamba utata wangu wa muda mrefu ulikuwa umetatuliwa. Imetokea kuwa Mungu alitekeleza tu kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, sio kazi ya kuwaondolea watu tabia yao potovu ya kishetani. Kazi ya Mungu ya hukumu ya kufichua ukweli kupitia kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ni kazi ya utakaso na wokovu mkamilifu wa wanadamu. Kwa hivyo Mungu huwatakasaje, kuwabadilisha na kuwaokoa watu kabisa kwa kweli? Nilikuwa na hamu ya kujua jibu la swali hili, kwa hivyo bila kupoteza muda niliuliza, “Ninaelewa kile ulichosema hivi sasa, na sasa najua kuwa tunaweza tu kupata utakaso kupitia Bwana aliyerejea kutekeleza hatua ya kazi ya hukumu. Nimekuwa nikitamani sana jambo hili kwa muda mrefu sana. Ninachotaka sana kujua sasa ni Mwenyezi Mungu hufanyaje kazi Yake ya hukumu ili kuwasafisha na kuwaokoa watu? Tafadhali shiriki ushirika wako.”

Dada Su aliendelea, “Swali la jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu ili kuwasafisha na kuwaokoa watu ni muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kufikia mabadiliko na utakaso. Maneno ya Mwenyezi Mungu yanatoa ufafanuzi mahsusi juu ya kipengele hiki cha ukweli. Nitawatumia. Ndugu, tafadhali yasome!”

Huku nikisisimka, nilisoma maneno ya Mwenyezi Mungu: “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Baada ya kumaliza kusoma maneno ya Mungu, Dada Su aliendelea na ushirika wake, “Maneno ya Mwenyezi Mungu yanaeleza waziwazi jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwatakasa watu. Katika siku za mwisho, Mungu kimsingi anatamka ukweli ili kulenga tabia potovu ya mwanadamu na asili ya kishetani ya kumpinga Mungu ili kuwahukumu, kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu. Mwenyezi Mungu ametamka vipengele vingi sana vya ukweli—jinsi Shetani anavyowapotosha watu, jinsi Mungu anavyowaokoa watu, kumfuata tu mwanadamu ni nini na kumtii Mungu ni nini, mitazamo tunayopaswa kuwa nayo katika imani yetu, badiliko la kitabia ni nini, kumuogopa Mungu na kuepuka maovu ni nini, kukosea tabia ya Mungu ni nini, jinsi ya kuwa mtu mwaminifu, nk. Ukweli huu wote una mamlaka na nguvu, na unaweza kuwapa watu riziki ya maisha yao. Ni njia ya uzima wa milele ambayo Mungu amewapa wanadamu. Mradi watu wakubali na kutenda neno la Mungu, wanaweza kupata utakaso na wokovu. Baada ya kupitia miaka kadhaa ya kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu tumepitia haya yote sisi wenyewe. Tunaposoma maneno ya Mwenyezi Mungu ya kumhukumu, kumwadibu, na kumfichua mwanadamu, tunahisi kuwa ni kama upanga wenye kuwili, yakifichua uasi, upotovu, upinzani, nia mbaya, fikira na mawazo yetu na hata sumu za Shetani zilizofichwa ndani kabisa ya mioyo yetu. Yanatufanya tuone kuwa kweli tumepotoshwa sana na Shetani na tumejawa na tabia za kishetani kama vile kuwa na kiburi na kujidai, kuwa wapotovu na wajanja, wabinafsi, katili na wasiotambua mengine ila masilahi yetu wenyewe, bila kumcha Mungu hata kidogo. Tunaona kwamba tumejaa uchafu na upotovu katika matendo, mioyo na akili zetu, bila ufanani wowote wa kibinadamu. Tunahisi aibu sana kuonyesha sura zetu na tunagundua kuwa tukiendelea kuishi kulingana na tabia zetu za kishetani, tutakuwa watu wanaomchukiza Mungu kila wakati, hatutaweza kamwe kupata sifa za Mungu na tutatakiwa kuondolewa na kuadhibiwa. Hukumu na ufunuo wa maneno ya Mwenyezi Mungu hutufanya tugundue tabia ya Mungu adhimu, yenye ghadhabu, yenye haki na kukuza moyo wa kumwogopa Mungu polepole na toba ya kweli na mabadiliko. Sasa tunahisi kuwa tunaishi kwa kudhihirisha mfano kidogo wa kibinadamu na tunaona kuwa kweli tumepata wokovu mkubwa wa Mungu. Hukumu ya Mungu isingetujia, tusingepata nafasi ya kujua tabia ya Mungu yenye haki ambayo haivumilii makosa ya mwanadamu na asili Yake takatifu na karimu. Hatungeweza kuja kuchukia uasi na upotovu wetu, wala hatungeweza kuacha upotovu wetu na kutakaswa. Kwa hivyo, kadiri tunavyozidi kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, ndivyo tunavyozidi kuona kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu ni utunzaji bora kwetu, baraka zetu kuu zaidi na wokovu wa kweli zaidi!”

Dada Liu pia alishiriki hili katika ushirika, “Hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu kwa siku za mwisho ni kazi ya kuwasafisha, kuwaokoa na kuwakamilisha watu kabisa. Tusipokubali hukumu mbele ya kiti cha Kristo wa siku za mwisho, basi hatutaweza kupata utakaso na mabadiliko ya tabia yetu ya maisha. Matokeo yetu bila shaka yatakuwa kukataliwa na kuondolewa na Mungu; tutapata kuteseka milele na tutaangamia. Hatutawahi kuwa na nafasi ya wokovu na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Jambo hili halina shaka.”

Nilisema kwa furaha, “Shukrani kwa Mungu! Moyo wangu umechangamshwa sana na ushirika wako. Nimemwamini Bwana kwa miaka mingi sana lakini kwa kweli nimekuwa nikiishi katika dhambi na sijakuwa na uwezo wa kuacha dhambi. Sasa ninaelewa kuwa nisipopitia hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho, sitaweza kuachana na utumwa na vizuizi vya dhambi. Sasa nimepata njia ya utakaso na wokovu kamili.” Baada ya ushirika wa siku kadhaa, mimi na mke wangu tulielewa ukweli kiasi na tukakubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo na wokovu Wake kwangu! Mimi kama mchungaji, nina jukumu na wajibu wa kuwaleta wachungaji na ndugu wengine wote ambao ninawajua mbele za Mungu. Baada ya kufanya kazi na ndugu hawa kwa muda, sio tu kuwa idaid kubwa ya ndugu katika kanisa ambao mara nyingi huhudhuria mikusanyiko wote walimkubali Mwenyezi Mungu, lakini pia nilimleta mchungaji wa kanisa lingine la nyumbani katika familia ya Mungu, na ndugu wengi kutoka kanisa lake pia walimgeukia Mungu. Nilifurahi kuona wale ndugu wakikubali wokovu wa Mungu wa siku za mwisho na kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Haya yote ni matokeo ya kazi ya Mwenyezi Mungu: Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!

Iliyotangulia: Kufichua Fumbo la Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wokovu wa Aina Tofauti

Na Huang Lin, ChinaNilikuwa mwumini wa kawaida katika Ukristo wa Kipaji, na tangu nianze kuamini katika Bwana sikuwahi kukosa ibada....

Niliupata Mwanga wa Kweli

Qiuhe, Japani Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp