Kuzinduka Katikati ya Mateso na Dhiki

26/01/2021

—Matukio Halisi ya Mateso ya Mkristo Mwenye Umri wa Miaka 17

Na Wang Tao, Mkoa wa Shangdong

Mimi ni Mkristo katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilibahatika zaidi miongoni mwa watoto wa rika moja, kwa sababu niliwafuata wazazi wangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho nikiwa na umri wa miaka nane. Ingawa nilikuwa mchanga wakati huo, nilifurahia sana kumwamini Mungu na kusoma neno la Mungu. Kwa kuendelea kusoma neno la Mungu na kushiriki na washiriki wenye umri mkubwa kuniliko wa kanisa hilo, baada ya miaka kadhaa, nilikuja kufahamu ukweli kiasi. Hasa nilipowaona ndugu zangu wote wakifuatilia ukweli na kufanya juhudi kuwa waaminifu, na kumwona kila mtu akielewana na mwingine kwa amani, nilihisi kuwa hizi ndizo nyakati za furaha zaidi na za shangwe zaidi. Baadaye nilisikia katika mahubiri, “Katika Bara la China, kumwamini Mungu, kufuatilia ukweli, na kumfuata Mungu kwa kweli ni kuweka maisha yako hatarini. Huku si kutia chumvi” (“Maswali na Majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III). Wakati huo sikuelewa hili lilimaanisha nini, lakini kupitia ushirika wa ndugu zangu, nilijifunza kuwa waumini katika Mungu hukamatwa na polisi, na kwamba kwa sababu China ni nchi inayomkana Mungu, hakuna uhuru wa itikadi za kidini. Hata hivyo, wakati huo sikuyaamini maneno haya. Nilidhani kwamba kwa sababu nilikuwa mtoto, hata kama ningekamatwa, polisi hawangenitendea chochote. Hilo lilibadilika siku ambayo mimi binafsi nilipata kukamatwa na kutendewa ukatili mikononi mwa polisi; hatimaye niliona waziwazi kuwa polisi, ambao nilikuwa nikiwaheshimu kana kwamba ni wajomba, kweli walikuwa kikundi cha ibilisi wakali!

Nilipokuwa na umri wa miaka 17, jioni ya Machi 5, mwaka wa 2009, mimi na kaka yangu mkubwa tulikuwa njiani kuelekea nyumbani kutoka kuhubiri injili wakati ghafla njia yetu ilizuiwa na gari la polisi. Maafisa watano wa polisi walishuka kutoka kwenye gari na bila onyo, walichopoa skuta yetu ya umeme kama majambazi, wakatusukuma hadi chini, na kututia pingu mikononi kwa nguvu. Nilitunduwazwa na ughafula wa yale ambayo yalikuwa yamejiri. Nilikuwa nimesikia mara nyingi ndugu zangu wakizungumza kuhusu jinsi waumini wa Mungu walivyokamatwa, lakini sikuwahi kufikiri kama kweli ingenitendekea siku hiyo. Nilishikwa na hofu; moyo wangu ulikuwa ukipiga kwa nguvu sana na ulihisi kama ungeruka kutoka kifuani mwangu. Nilimwomba Mungu moyoni mwangu bila kukoma, “Mwenyezi Mungu! Polisi wamenikamata, na naogopa sana. Sijui ninachopaswa kufanya au wanapanga kunitendea nini, kwa hivyo nakuhisi Uulinde moyo wangu.” Nilihisi mtulivu zaidi baada ya kusali. Nilidhani kwamba polisi hawangetenda chochote kwa mtoto kama mimi, kwa hivyo sikuwa na wasiwasi sana. Lakini hali hiyo haikuwa rahisi kama nilivyotarajia. Polisi walipotupata na vitabu kuhusu imani yetu katika Mungu, walitumia hili kama ushahidi wa kuhalalisha kutupeleka kwenye kituo cha polisi.

Ilikuwa mwanzoni wa majira ya kuchipua kaskazini mwa China, na hali ya hewa bado ilikuwa baridi sana, ikifika chini ya selisiasi hasi 3-4 wakati wa usiku. Mkuu wa kituo cha polisi alizichukua koti na viatu vyetu kwa nguvu na hata mikanda yetu, na wakatia mikono yetu pingu kwa kukaza migongoni mwetu. Ilikuwa chungu sana. Aliwaagiza maafisa kadhaa watushikilie sakafuni, kisha nyuso na vichwa vyetu vilichapwa kikatili kwa ukanda wa ngozi, ambayo mara moja yalisababisha maumivu makali kichwani mwangu—nilihisi kama kilikuwa karibu kilipuke na machozi yalianza kutiririka usoni mwangu kwa hiari. Nilikasirika wakati huo, kwa sababu kauli mbiu “Staarabika katika Kushughulikia Kesi” iliandikwa waziwazi kwenye ukuta, lakini walikuwa wakitutendea kama majambazi au wauaji wakatili wa barabara kuu! Haukuwa ustaarabu hata kidogo! Kwa hasira, nilidai, “Tumefanya kosa gani? Je, mbona mnatukamata na kutupiga?” Alipokuwa akiendelea kunichapa, mmoja wa hawa polisi wabaya alisema kwa ukali, “Ewe mshenzi mchanga, usinizungumzie kwa namna hiyo! Tuko hapa kuwakamata waumini katika Mwenyezi Mungu! Wewe ni kijana ambaye angefanya kitu kingine chochote, kwa nini hiki? Kiongozi wenu ni nani? Ulivipata wapi vitabu hivi? Nijibu! Ukikosa kujibu, nitakupiga hadi ufe!” Kisha nikagundua kwamba kaka yangu mkubwa alikuwa akikaza meno sana na kukataa kutamka hata neno moja, kwa hivyo niliapa kiapo mwenyewe: “Nakataa pia kuwa Yuda! Hata wakinipiga hadi nife, sitazungumza! Maisha yangu yamo mikononi mwa Mungu, na Shetani na ibilisi wake hawana nguvu juu yangu.” Alipoona kwamba hakuna mmoja wetu aliyezungumza, mkuu wa kituo aligadhibika ghafla, akasema kwa sauti kubwa, akituelekezea kidole, “Basi! Mnataka kuwa wenye kiburi? Hamzungumzi? Wapige vibaya! Waonyeshe kweli nini kinaendelea na waonyeshe nini kilicho kigumu!” Polisi hawa wabaya walitushambulia ghafla, wakitunyakua kwa videvu huku wakitupiga makonde usoni kwa nguvu sana hivi kwamba niliona vimulimuli na uso wangu uliuma kwa maumivu makali. Nilikuwa nimedekezwa na kutunzwa na wazazi wangu tangu utotoni; Sikuwahi kupitia vurugu kama hio. Nilifedheheshwa sana kwamba sikuweza kujizuia kulia, na niliwaza, “Polisi hawa ni wakatili sana, na wenye kuzidi! Shuleni, waalimu wetu walitwambia kila mara twende kwa polisi ikiwa tutapata shida. Walisema kwamba polisi ‘waliwatumikia watu’ na walikuwa ‘mashujaa ambao huwalinda watu wema dhidi ya dhuluma,’ lakini sasa, kwa sababu tu tunamwamini Mwenyezi Mungu na kutembea kwenye njia sahihi maishani, wanatukamata kwa udhalimu na kutupiga bila huruma. Je, watu hawa wanawezaje kuwa ni ‘Polisi wa watu’? Wao ni kikundi cha ibilisi tu! Si ajabu katika mahubiri ilisemwa, ‘Wengine wanasema kuwa joka kubwa jekundu ni pepo mbaya, wengine wanasema ni kikundi cha watenda maovu, lakini tabia na asili ya joka hili kubwa jekundu ni gani? Ni ile ya pepo mbaya. Wao ni kundi la pepo wabaya ambao wanampinga na kumshambulia Mungu! Watu hawa ni udhihirisho wa Shetani, Shetani aliyepata mwili, kupata mwili kwa pepo wabaya! Watu hawa si wengine ila Shetani na pepo wabaya’ (“Umuhimu wa Kweli wa Kuachana na Joka Kubwa Jekundu ili Kupokea Wokovu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III). Hapo zamani, nilidanganywa na uwongo wao, nikiamini kwamba polisi ni ‘watu wazuri’ wanaofanya kazi kwa niaba ya watu wa kawaida. Sikugundua kuwa hiyo ilikuwa taswira danganyifu, lakini leo hatimaye naona kuwa wao ni kundi la ibilisi wabaya wanaompinga Mungu!” Sikuweza kujizuia kuanza kuwachukia kwa moyo wangu wote. Mkuu wa kituo alipoona kuwa bado hatuzungumzi, alisema kwa sauti kubwa, “Wape kichapo kingine kibaya!” Vibaraka wake wawili walituvumania. Walituamuru tuketi sakafuni miguu yetu ikiwa imenyooka, kisha wakatupiga mateke kwa nguvu miguuni mwetu kwa sehemu ya mbele ya viatu vyao, na vile vile kusimama kwenye miguu yetu na kukanyaga wawezavyo kwa nguvu. Miguu yangu ilikuwa na maumivu makali nilihisi kana kwamba ilikuwa karibu ivunjike, na sikuweza kujizuia kupiga mayowe, lakini nilipozidi kupiga mayowe, ndivyo walivyonipiga kwa nguvu zaidi. Sikuwa na la kufanya ila kuvumilia uchungu huku nikimwomba Mwenyezi Mungu moyoni mwangu, “Mungu! Ibilisi hawa ni wakatili sana! Kwa kweli siwezi kuyavumilia haya. Tafadhali, nipe imani na unilinde ili nisikusaliti.” Mara tu, kifungu hiki cha maneno ya Mungu kilinijia ghafla akilini mwangu “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). Maneno ya Mungu yalikuwa chemichemi ya imani na nguvu kuu kwangu. Nilielewa kuwa hali niliyokuwa nikipitia iilikuwa ikijiri kwa idhini kutoka kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwamba huu ndio wakati niliotakiwa kusimama kidete na kuwa shahidi kwa Mungu. Ingawa nilikuwa mchanga, nilikuwa na Mungu kama msaada wangu dhabiti, kwa hivyo sikuwa na chochote cha kuogopa! Niliazimia kusimama kidete na kumshuhudia Mungu, kutokuwa mwoga kabisa, na kutomtii Shetani! Kupitia mafundisho na mwongozo katika neno la Mungu, nilipata ujasiri na azimio la kuvumilia mateso na kusimama kidete na kumshuhudia Mungu.

Jioni hiyo baada ya saa 1 jioni, mkuu wa kituo alikuja kunihoji tena. Aliniamuru niketi kwenye sakafu ya saruji iliyokuwa baridi sana kwa jaribio la kimakusudi la kunigandisha. Ni wakati tu nilipokuwa na baridi nyingi hadi miguu yangu yote ilikuwa imekufa ganzi na nilikuwa nikitetemeka kote ndipo aliwaamuru vibaraka wake waninyanyue na kuniegemeza ukutani, ambapo baadaye alinitia bila huruma mshtuo kwenye mikono yangu kwa kutumia kirungu cha umeme. Mishtuo ilijaza mikono yangu malengelenge na kufanya meno yangu yote kufa ganzi kwa sababu ya uchungu (hata leo bado meno yangu yanauma ninapotafuna). Lakini hata wakati huo, ibilisi huyu, bado akiwa mwenye wayowayo kwa ajili ya ghadhabu, hakuwa amechoshwa; alianza tu kutumia kirungu chake cha umeme kwenye nusu ya sehemu ya chini ya mwili wangu. Mateso hayo yaliniacha nikiwa na maumivu mabaya sana, lakini aliinamisha kichwa chake nyuma na kucheka. Wakati huo, nilimchukia pepo huyu, aliyekosa utu kabisa, kwa moyo wangu wote. Lakini bila kujali ni jinsi gani polisi hawa wabaya walinihoji au kunitesa, niliyakaza meno yangu na nikakataa kusema lolote. Mateso yaliendelea hadi saa mbili au saa tatu asubuhi, ambapo mwili wangu wote ulikuwa umekufa ganzi—sikuwa na hisia yoyote mahali popote. Mwishowe, baada ya kuchoswa kwa ajili ya kunipiga, walinirudisha kwenye chumba kidogo na kunitia pingu kwa yule ndugu mkubwa ambaye alikuwa amekamatwa pamoja nami. Walituamuru tuketi kwenye sakafu baridi, kisha wawili wao walipewa kazi ya kutuchunga ili kuhakikisha kwamba hatulali. Wakati mmoja wetu alifunga macho yake wangetupiga makonde na mateke. Baadaye usiku huo nilitaka kwenda msalani, lakini polisi hawa wabaya walinikaripia, “Ewe bwege mchanga, hadi utakapotuambia kile tunachotaka kujua, huendi popote! Utakwenda haja ndogo kwenye suruali yako!” Mwishowe, kwa kweli sikuweza kujizuia tena, na ilinibidi nijisaidie katika suruali yangu. Katika hali hiyo ya hewa yenye kibaridi kikali, suruali yangu yenye pedi illikuwa imejaa mkojo, ikiniacha na baridi tele kwamba sikuweza kukoma kutetemeka.

Baada ya kuvumilia mateso ya kikatili kama haya ya ibilisi hawa, nilikuwa na maumivu yasiyovumilika kote, na singeepuka kuhisi dhaifu na hasi, “Sijui hasa ni mateso gani watakayotekeleza kwangu kesho. Je, nitaweza kustahimili?” Lakini wakati huo, ndugu huyo mkubwa, akihangaika kwamba singeweza kuhimili mateso hayo na kuhisi hasi, alininong'onezea kwa wasiwasi, “Tao, unaonaje kuhusu ibilisi hao wabaya wanaotutesa namna hii leo? Unajuta kumwamini Mwenyezi Mungu na kufanya wajibu wako?” Nikasema, “La, nahisi tu nimedhalilishwa kwa kupigwa na pepo hawa. Nilidhani kuwa hawatanifanyia chochote kwa sababu mimi ni mtoto tu. Sikujua kuwa wangekuwa tayari kuniua.” Ndugu yangu mkubwa alifanya ushirika kwa dhati, “Tumechukua mwelekeo wa kumwamini Mungu, na tunatembea kwenye njia sahihi maishani kwa ajili ya mwongozo wa Mungu, lakini Shetani hataki tumfuate Mungu au kuokolewa kikamilifu. Bila kujali kitakachotokea, tunahitaji kusimama kidete katika imani yetu. Hatupaswi kamwe kujitiisha kwa Shetani; hatuwezi kuvunja moyo wa Mungu.” Maneno ya huyu ndugu yalikuwa yenye kutia moyo sana. Nilijisikia kuwa nimefarijiwa, na sikuepuka kufikiria maneno ya Mungu, “Mshindi ni nini? Wanajeshi wazuri wa Kristo lazima wawe jasiri na kunitegemea kuwa wenye nguvu kiroho; lazima wapigane kuwa wapiganaji na wapambane na Shetani hadi kufa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 12). Wakati huo, nilifahamu mapenzi ya Mungu na kuhisi nguvu moyoni mwangu. Sikuhisi nimedhalilishwa tena au kuwa na taabu, lakini nikawa tayari kukabiliana na jaribio hili kwa ushupavu. Bila kujali ni jinsi gani Shetani alinitesa, ningemtegemea Mungu kumshinda Shetani; Nilimwonyesha Shetani kuwa waumini wote katika Mwenyezi Mungu ni wanajeshi Wake bora zaidi, wote wakiwa wapiganaji shupavu.

Asubuhi iliyofuata, polisi hao wabaya walinirudisha kwenye chumba cha mahojiano na yule mkuu mwovu wa kituo tena alijaribu kunilazimisha nikiri. Aliponda kwenye meza huku akinielekezea kidole moja kwa moja kwenye pua langu na kunitukana, akisema, “Kijana, jana usiku ulibadili maoni? Umemwamini Mwenyezi Mungu kwa muda gani? Umewahubiria watu wangapi? Jibu maswali yetu, au utahisi uchungu zaidi!” Niliwaza, “Siwezi kumwogopa Shetani tena. Nahitaji kuwa shupavu na kuwa na ujasiri!” Kwa hivyo, nilisema kwa udhabiti, “Sijui chochote!” Mkuu mweovu wa kituo aligadhibika ghafla na kusema kwa sauti kubwa, “Kijana, unataka kufa? Kwa sababu nitakuua kabla hatujamaliza, na kisha utaaacha kuongea hakika!” Alipokuwa akisema kwa sauti kubwa alinirukia, kisha akashika nywele zangu kwa nguvu na kukigongesha kichwa changu ukutani. Masikio yangu mara moja yalianza kuwangwa, na maumivu yalikuwa makali sana kwamba sikujizuia kulia na machozi yalitiririka usoni mwangu. Mwishowe, baada ya ibilisi hao kugundua kuwa hawatapata walichotaka kutoka kwangu, hawakuwa na lingine la kufanya ila kunirudisha kwenye chumba kidogo. Kisha walimchukua ndugu huyo mkubwa kumhoji. Muda si muda, nilimsikia akipiga mayowe kwa uchungu, na nilijua kuwa walikuwa wamemtendea kitu kibaya. Nilikunjamana ndani ya chumba kidogo kama kondoo aliyezungukwa na mbwa mwitu wakali nikihisi uzuni mwingi na asiyejiweza, na machozi yalipokuwa yanatiririka usoni mwangu, nilimwomba Mungu amlinde ndugu huyu dhidi ya wale ibilisi wabaya walipokuwa wakijaribu kumlazimisha akiri kwa kutumia mateso. Walituhoji kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, na hawakutupa hata chakula chochote wala tone la maji. Nilikuwa nahisi baridi na njaa, nilichanganyikiwa, na kichwa changu kilikuwa kimevimba na kuuma sana. Wakiogopa kuwa wangetuua, hawakuwa na lingine la kufanya ila kukomesha mateso yao.

Baada ya mateso ya kikatili na ya kinyama ya serikali ya CCP, nilipata kupitia kwa kweli kile nilichokuwa nikisikia kuhusu katika mahubiri: “Katika magereza ya joka kubwa jekundu, bila kujali ikiwa wewe ni mwanamume au mwanamke, wanaweza kukudhulumu kwa njia yoyote waipendayo. Wao ni waovu na wanyama. Wanawadhulumu watu visivyotarajiwa kwa kutumia virungu vya umeme, na kukutendea chochote kile unachoogopa zaidi. Chini ya utawala wa joka kubwa jekundu, watu hukoma kuwa binadamu na hata ni wakatili zaidi kuliko wanyama. Joka kubwa jekundu haswa ni katili na la kinyama namna hii. Ni wanyama, ibilisi, wasio na haki hata kidogo. Hakuna njia ya kujadiliana nao, kwa sababu hawana haki” (“Umuhimu wa Kweli wa Kuachana na Joka Kubwa Jekundu ili Kupokea Wokovu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III). Wakati huo, hatimaye niliona waziwazi asili ya serikali ya CCP inayopinga maendeleo kama adui wa Mungu. Kwa kweli ni dhihirisho la Shetani, pepo ambaye huua bila kuonyesha hisia! Hawana maadili au haya, hata kutonihurumia, mtoto wa umri pungufu. Wote wako tayari kuniua kwa sababu tu namwamini Mungu na hutembea katika njia sahihi maishani. Wao ni wanyama watu wakali wasio na msimamo, maadili, au ubinadamu. Sikuyakaribisha tena matumaini yoyote danganyifu kwamba polisi wangenitendea kwa huruma kwa sababu ya umri wangu; niliomba tu kwamba Mwenyezi Mungu anilinde na kuniongoza kushinda mateso mabaya ya Shetani na ya wale pepo, kwamba niweze kuvumilia mateso yote, na kwamba niweze kuwa shahidi mkubwa kwa Mungu.

Alasiri ya Machi 9, polisi waovu walipoona kwamba hawangeweza hasa kupata chochote kutoka kwetu, walitushika mikono na kutulazimisha kutia saini kukiri ghushi na kutushtaki kwa makosa ya “kuvunja sheria ya kitaifa, kuvuruga amani ya jamii, na kupindua mamlaka ya serikali,” kisha wakatupeleka kwa nyumba ya kizuizini. Mara tu tulipofika walinyoa nywele zetu kabisa, wakavua nguo zetu, na kisha wakaturudishia baada ya kuzikatakata hadi karibu ziwe utepe. Sikuwa na ukanda wangu tena, kwa hivyo ilinibidi nifunge mifuko ya plastiki kuwa kamba ili ishikilie suruali yangu. Hata katika hali ya hewa yenye kibaridi kingi, polisi waliamuru wafungwa wengine watuogeshe kwa kumwaga beseni baada ya beseni ya maji baridi kwenye vichwa vyetu. Nilihisi nimekufa ganzi hadi kiwango ambacho nilikuwa nikitetemeka kutoka utosini hadi kidoleni, na damu yangu ilihisi kama imeganda ndani ya mishipa yangu. Sikuweza hata kusimama baada ya hapo. Wafungwa wote waliozuiliwa katika gereza hilo walikuwa wabakaji, wezi, wanyang'anyi, na wauaji…. Kila mmoja alionekana kuwa mwovu zaidi kuliko mwingine, na wazo la kuzuiliwa mahali hapo paovu pamoja nao lilinifanya nitetemeke kwa ajili ya hofu. Usiku, zaidi ya watu 30 miongoni mwetu walilala pamoja kwenye mwamba wa saruji ngumu, na blanketi zilinuka kwa uvundo ambao ulifanya kulala kuwe karibu kusiwezekane. Milo tuliyopewa na polisi hao wabaya ilikuwa tu mkate mdogo uliopikwa na mvuke na kiasi kidogo cha uji wa majimaji wa mahindi, usio wa kutosha hata kidogo kutulisha vya kutosha, na wakati wa mchana tulipewa kazi za sulubu za kupita kiasi. Ikiwa hatungemaliza kazi zetu za siku hiyo, walituadhibu kwa kutulazimsiha tuwe walinzi wa seli usiku kucha katika zamu ya usiku, kumaanisha kwamba tulihitajika tusimame kwa saa nne na tulipata saa mbili tu za kulala. Wakati mwingine nilikuwa nimechoka sana hadi nilisinzia nikiwa nimesimama. Polisi hao wabaya pia walimwambia mfungwa mkuu wa seli atafute njia za kunitesa, kama vile kunipa kazi nyingi kuongeza kwenye sehemu yangu ya kazi au kunilazimisha nisimame usiku kucha. Nilihisi kana kwamba nilikuwa karibu kuzimia. Mara nyingi sana nilikuwa nikiteswa na kudhulumiwa na pepo hao, ilionekana kana kwamba nilikuwa na uhuru mdogo kuliko mbwa anayezurura mitaani, na sikuwa hata nikila kama nguruwe au mbwa. Nilipowaza mambo haya, nilikumbuka nyumbani kwangu na wazazi sana na nilihisi nyumba ya uzuiliaji si mahali pa watu pa kuishi. Sikutaka kukaa hapo kwa muda mwingine zaidi. Hakuna kitu nilichotamani zaidi ya kuondoka mara moja mahali hapo pa kutisha. Katika upeo wa huzuni na udhaifu wangu, niliweza tu kumwomba Mungu kwa dhati, na hapo ndipo maneno ya Mwenyezi Mungu yalinipa nuru na kunipa mwongozo: “Usivunjike moyo, usiwe dhaifu, Nitakufichulia. Njia ya kwenda kwa ufalme sio laini hivyo, hakuna kitu kilicho rahisi hivyo! Unataka baraka zije kwa urahisi rahisi, sivyo? Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi…. Wale wanaoshiriki katika uchungu Wangu bila shaka watashiriki utamu Wangu. Hiyo ni ahadi Yangu na baraka Zangu kwenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 41). Maneno ya Mungu yalikuwa chemichemi nzuri ya faraja na ya kutia moyo. Yalinisaidia kufahamu kuwa mateso na shida ambazo nilikuwa nikivumilia zilikuwa baraka kutoka kwa Mungu. Mungu alikuwa akitumia hali hizi ngumu kunisafisha na kunikamilisha, na kunifanya niwe mtu ambaye upendo na uaminifu wake kwa Mungu unastahili ahadi ya Mungu. Nilipofikiria jinsi nilivyodekezwa tangu utotoni na sijapata kuvumilia mateso au hata matusi madogo, niliona kwamba ikiwa nilitaka kupata ukweli na uzima, nilihitaji kuwa na azimio la kuvumilia mateso na nilihitaji imani thabiti. Bila kupitia mateso haya, upotovu ndani yangu haungeweza kutakaswa. Kwa kweli mateso yangu yalikuwa baraka kutoka kwa Mungu, na kwa hivyo nilifaa kuwa na imani, kushirikiana na Mungu, na kumruhusu Mungu afanye kazi Yake ya kweli ndani yangu. Mara nilipofahamu mapenzi ya Mungu, sala kwa Mungu liliibuka ndani yangu kwa hiari, “Mungu! Sijisikii tena dhaifu na hasi. Nitasimama kwa nguvu, Nitakutegemea bila kuyumbayumba, nitapigana na Shetani hadi mwisho, na nitajitahidi kukupenda na kukuridhisha. Naomba unipe imani na uvumilivu.” Katika siku ambazo nilipitia dhuluma na fedheha katika nyumba ya kizuizini, nilimwomba na kumtegemea Mungu zaidi kuliko wakati wowote tangu nilipopata imani yangu katika Mwenyezi Mungu, na ndipo nilipomkaribia Mungu sana zaidi. Wakati huo, moyo wangu haukuwahi kumwacha Mungu hata kwa muda mfupi, na nilikuwa nikihisi akiwa pamoja nami daima. Bila kujali niliteseka kiasi gani, haikuonekana kama kuteseka hata kidogo, na nilielewa waziwazi kuwa yote haya ni Mungu alikuwa akinijali na kunilinda.

Asubuhi moja mwezi mmoja baadaye, walinzi wa gereza waliniita pamoja na huyo ndugu mkubwa. Nilihisi msisimko mwingi niliposikia wito, nikidhani kuwa wanaweza kutuachilia huru na kwamba sitaweza kuteseka tena mahali hapo pa mateso. Ukweli haukuwepo kabisa katika tumaini langu. Mkuu wa kituo cha polisi alitusalimu kwa tabasamu lenye uovu na hukumu zilizoandikwa, akisema, “Ninyi wawili mmehukumiwa mwaka mmoja wa kupata upya elimu kwa kufanya kazi kwa ajili ya kumwamini Mwenyezi Mungu. Hata ingawa hamkuzungumza, tunaweza kuwahukumu hata hivyo. Chama cha Kikomunisti kinatawala taifa hili, na hata kesi haitawafaidi vyovyote vile!” Nilipoona jinsi alivyokuwa na furaha kwa ajili ya taabu zetu nilikasirisha sana: Serikali ya CCP haifuati sheria au maadili yoyote, na zaidi tu ya kumtesa mtoto mwenye umri mdogo kama mimi, ilikuwa ikinipa hukumu bila ya kuwa na kosa hata kidogo! Mimi na ndugu huyo mwingine tulipelekwa kwenye kambi ya kazi ya mkoa siku hiyo. Wakati wa uchunguzi wetu wa kiafya, daktari aligundua kwamba ndugu huyo alikuwa na shinikizo la damu, tatizo la moyo, na shida nyingine za kiafya. Walinzi wa kambi ya kazi waliogopa kuwajibika ikiwa angekufa katika kituo chao, kwa hivyo walikataa kumkubali; polisi hawakuwa na lingine la kufanya ila kumrudisha, kumaanisha kwamba nilibaki peke yangu. Nilianza kulia wakati huo—nililia kwa uchungu. Nilikumbuka nyumbani kwangu na kuwakumbuka wazazi wangu, na ukizingatia kwamba niliachwa bila ndugu yangu wa kushiriki pamoja, je, ningewezaje kustahimili mwaka mrefu kama huo? Katika mwezi uliopita wa kuteswa na kudhulumiwa na ibilisi hao, kila nilipohisi hasi na dhaifu kwa sababu sikuweza kuvumilia ukatili wao, alishiriki nami kuhusu neno la Mungu ili anitie moyo na kunifariji, akinisaidia kupata nguvu kupitia kufahamu mapenzi ya Mungu. Pia, kuona azimio lake kulinipa imani na nguvu ya kupigana na kuwashinda hao pepo pamoja naye. Lakini wakati huo, niliachwa kupigana vita hivyo peke yangu. Je, nitaweza kusimama kidete? … Nilipowaza zaidi, ndivyo nilihisi masikitiko zaidi, na uhasi, upweke, uchungu, na udhalilishaji mwingi zaidi ulikita mizizi moyoni mwangu. Taabu yangu iliponikandamiza hadi nikawa karibu kukata tamaa, nilimwomba Mungu kwa haraka, “Mungu! Kimo changu ni kidogo sana. Nitawezaje kuhimili jaribio kubwa hivi? Ninapaswaje kustahimili mwaka huu mrefu wa masomo ya upya kupitia kazi? Mungu! Nakusihi uniongoze na unisaidie, unipe imani na nguvu….” Machozi yalitiririka usoni mwangu huku nikilia bila sauti. Nilipokuwa nikiomba, ghafla nilikumbuka tukio la Yusufu la kuuzwa kwenda Misri akiwa na umri wa miaka kumi na saba. Ingawa alikuwa peke yake huko Misri na alivumilia fedheha na mateso, kamwe hakumwacha Mungu wa kweli au kujisalimisha kwa Shetani. Ingawa wakati huo nilikuwa nikiteswa na pepo gerezani, ilikuwa ikitokea kwa idhini ya Mungu, na ilimradi ningemtegemea Mungu na kukataa kujisalimisha kwa Shetani, Mungu pia angeniongoza katika kumshinda Shetani na kuondoka mafichoni mwa pepo. Wakati huo, nilikumbuka tena maneno ya Mungu, “Usijidunishe kwa sababu wewe ni mdogo; unapaswa kujitoa Kwangu. Sioni watu wako vipi juu juu au ni wa umri upi. Naona tu iwapo wananipenda kwa kweli au la, na iwapo wanafuata njia Yangu na kutenda ukweli wakipuuza mambo mengine yote. Usijali kuhusu jinsi kesho itakuwa au jinsi siku za baadaye zitakuwa. Alimradi unitegemee kuishi kila siku, basi hakika Nitakuongoza(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 28). Maneno ya Mungu yalichangamsha moyo wangu kama jua la majira ya joto. Yaliniwezesha nione kwamba Mungu hampendelei mtu yeyote, na hata ingawa nilikuwa mchanga, ilimradi nilikuwa na moyo wenye upendo wa kweli kwa Mungu na kuishi kulingana na neno la Mungu, daima ningepokea mwongozo wa Mungu. Niliwaza jinsi, tangu wakati wa kukamatwa kwangu, Mungu alikuwa nami kila wakati, akinisaidia kustahimili kila shida na kuniwezesha kusimama kidete. Bila uwepo wa Mungu na mwongozo wake, ningewezaje kuvumilia adhabu kali na mateso ya kikatili ya pepo hao? Nilikuwa nimeponea chupuchupu shida kubwa namna hiyo kwa kumtegemea Mungu, na nilikuwa nikikabiliana na mwaka mmoja wa masomo upya ya kupitia kazi, hivyo kwa nini nilikosa imani? Je, si ni Mungu pekee ndiye niliyehitaji kumtegemea? Mungu alikuwa nami, na angenipa mwongozo kila wakati, hivyo kwa nini nihisi upweke au kuogopa? Hali hizo zilikuwa nafasi yangu ya kujifunza kuishi kwa kujitegemea na kukomaa maishani. Sikujiona tena kama mtoto, wala sikukuwategemea watu wengine ilhali simtegemei Mungu. Nilipaswa kupevuka, kumtegemea Mungu kuitembea njia yangu mwenyewe, na kuamini kwamba hakika nitaweza kuendelea katika njia hiyo, nikimtegemea Mungu. Shetani kamwe hana uwezo wa kuwashinda watu ambao wana azimio la kumtegemea na kumpenda Mungu! Ulikuwa wakati wangu wa kuwa na ujasiri, na kumruhusu Mungu kupata utukufu kupitia matendo yangu. Mara tu nilipofahamu mapenzi ya Mungu nilihisi kana kwamba kuna nguvu yenye uwezo iliyokuwa ikiniegemeza, na moyoni mwangu nilikuwa na azimio la kukabili maisha yangu gerezani.

Walinzi katika kambi ya kazi walipogundua kwamba namwamini Mwenyezi Mungu walianza kunitesa kwa makusudi. Walinipa kazi nzito za sulubu, kubeba mifuko mizito sana yenye uzito wa zaidi ya kilo 50 kutoka kwenye ghorofa la tatu hadi la kwanza kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, na ikiwa singemaliza sehemu yangu ya kazi, ningelazimika kufanya kazi kwa masaa zaidi hadi usiku wa manane. Sikuwahi kufanya kazi ya sulubu kabla, na sikupata chakula cha kutosha katika nyumba ya kizuizini, kwa hivyo nilikuwa nimechoka sana kila wakati. Hapo mwanzo, sikuweza kuinua mifuko hiyo hata kidogo, lakini baadaye, kupitia kumtegemea Mungu kwa dhati, polepole niliweza kuinyanyua. Kazi nzito ilisababisha niwe mchovu kabisa kila siku, na kusababisha kiuno na miguu yangu kuuma. Walinzi mara nyingi waliamuru wafungwa wengine wanipige kikatili, mara nyingi wakiniacha nimejawa na majeraha na vilio vya damu. Wakati fulani walinzi waliagiza mfungwa mkuu anipigie kwa sababu nilirudi kutoka kuchota maji nikiwa nimechelewa. Wakati wa adhabu kiwambo cha sikio langu kilitoboka na kupasuka, karibu inipelekee kuwa kiziwi. Nilikaza meno yangu kwa ajili ya chuki ya kulazimika kuvumilia unyanyasaji na dhuluma ya aina hii, lakini sikuweza kupinga. Nilikuwa mwenye huzuni na malalamiko, lakini sikuwa na mahali pa kutafuta haki. Ningeweza tu kuja mbele za Mungu na kushiriki dhiki yangu pamoja na Yeye katika maombi. Katika gereza hilo lenye uovu, nilijifunza kumkaribia Mungu, kumtumainia na kumtegemea Mungu katika mambo yote—kile kilichoniletea furaha kubwa zaidi maishani ni kumwomba Mungu ili nishiriki mawazo yangu ya chokomeani. Kila wakati nilipohisi huzuni au kuwa dhaifu, wimbo ambao nilipenda zaidi kuimba ulikuwa “Nimedhamiria Kumpenda Mungu Kwa Moyo Wangu”: “Ee Mungu! Moyo wangu hauwezi kukupenda kweli, nataka kukupenda lakini sina nguvu. Napaswa kufanya nini? Napenda Ufungue macho ya roho yangu, napenda Roho Wako auguse moyo wangu, ili mbele Yako nivuliwe hali zote za kutoonyesha hisia, na nisishurutishwe na mtu yeyote, jambo, au kitu; nauweka moyo wangu wazi kabisa mbele Yako, ili nafsi Yangu yote ijitoe mbele Yako, na Uweze kunijaribu vile Utakavyo. Sasa, siwazii matarajio yangu, wala sifungwi na kifo. Kwa kuutumia moyo wangu ambao unakupenda, napenda kutafuta njia ya uzima. Vitu vyote na matukio viko mikononi Mwako, majaliwa yangu yako mikononi Mwako, na, zaidi ya hayo, maisha yangu yanadhibitiwa na mikono Yako. Sasa, nafuatilia kukupenda Wewe, na bila kujali kama Wewe unaniruhusu kukupenda, haijalishi jinsi Shetani anavyoingilia, nimeamua kukupenda Wewe(Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipoimba na kuimba, ningeguswa hadi kulia, na yangeleta faraja kubwa na msukumo moyoni mwangu. Mwenyezi Mungu alikuwa Amenisaidia mara kwa mara na kuniegemeza, Akiniwezesha kupata kwa kweli mapenzi ya kweli ya Mungu kwangu. Kama mama mwenye huruma, Mungu alisimama karibu nami akinilinda, akinifariji na kuniegemeza wakati wote, akinipa imani na nguvu, na kuniongoza kupitia mwaka huo ambao kamwe sitaweza kusahau.

Baada ya kupitia uovu wa wakati wangu gerezani, nilikomaa zaidi maishani, na pia nilipata maarifa mengi kuhusu ukweli. Sikuwa tena mtoto mjinga, asiye na hatia. Ilikuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyoniongoza kushinda mateso na adhabu ya polisi waovu mara kwa mara, na pia yaliniwezesha kuibuka kutoka katika udhaifu na uhasi, kuinuka, na kusimama kidete. Yaliniwezesha kuelewa jinsi ya kuzingatia na kuufariji moyo wa Mungu, na pia jinsi ya kumtegemea Mungu na kusimama kidete, na jinsi ya kumshuhudia Mungu na kulipiza upendo wa Mungu. Pia yaliniwezesha kuona waziwazi ukatili na ubaya wa Shetani na pepo wake na asili yao mbaya ya kupinga maendeleo kama maadui wa Mungu. Yalinipa utambuzi juu ya taswira danganyifu ya “Polisi wa watu ambao wanawapenda watu.” Sijawahi kudanganywa tena na uwongo wa Shetani. Mateso na taabu nilizovumilia hazikukosa kuniangamiza tu, lakini pia zikawa msingi ambao kwao natembea kwenye njia ya imani. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza katika njia hii yenye muinuko mkali na yenye miamba na kuniwezesha kujifunza kuvumilia mateso ya ukatili katika umri mdogo kama huu. Kupitia haya, niliona uweza na mamlaka ya Mungu, na kwamba huu ulikuwa wokovu maalum wa Mungu kwangu! Nilihisi kwa uzito kuwa katika ulimwengu mwovu unaotawaliwa na pepo, ni Mungu tu anayeweza kuwaokoa watu, ni Mungu tu anayeweza kuwa tegemeo letu na kutusaidia wakati wowote tunapomhitaji, na ni Mungu tu anayewapenda watu kwa kweli. Mateso na magumu niliyoyavumilia yakawa hazina ya thamani ya ukuaji wa maisha kwa ajili yangu, na yalikuwa ya faida sana kwa kupata kwangu kwa wokovu kamili. Ingawa niliteseka wakati huo, mateso hayo yalikuwa ya thamani sana na yenye maana. Ni kama tu neno la Mungu lisemavyo, “Ikiwa uko tayari kuwa kwenye mkondo huu na kufurahia hukumu hii na wokovu huu wa ajabu, na kufurahia baraka hizi ambazo haziwezi kupatikana kokote katika ulimwengu wa wanadamu, na kufurahia upendo huu, basi kuwa mzuri: Salia kwenye mkondo huu ili kukubali kazi ya ushindi ili uweze kufanywa mkamilifu. Leo, unaweza kupitia mateso na usafishaji kidogo kwa sababu ya hukumu ya Mungu, mateso haya ni ya thamani na ya maana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)).

Iliyotangulia: Imani Isiyoweza Kuvujika

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Imani Isiyoweza Kuvujika

Meng Yong, China Mimi kwa asili ni mtu mwaminifu, ikiwa ndiyo maana nimekuwa nikidhulumiwa daima na watu wengine. Kwa sababu hiyo, nimeonja...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp