Uzoefu wa Kina Zaidi wa Upendo wa Mungu Kupitia Kuingia Katika Pango la Pepo
Licha ya kulelewa chini ya utunzaji wenye upendo wa wazazi wangu tangu nilipokuwa mtoto, moyoni mwangu, mara nyingi nilihisi mpweke na kwamba sikuwa na mtu wa kutegemea. Siku zote nilionekana kushikwa na shida fulani zisizofumbulika ambazo sikuweza kushinda. Mara nyingi nilijiuliza: Kwa nini watu wako hai? Tunapaswa kuishije? Lakini sikuweza kupata jibu kamwe. Mnamo mwaka wa 1999, hatimaye nilikuwa na bahati nzuri ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Lishe na riziki ya neno la Mungu viliufariji moyo wangu mpweke, na nilihisi kwamba hatimaye nilikuwa nimekuja nyumbani. Nilihisi hasa kuwa salama salamini. Ni hapo tu ndipo mwishowe nilijua maana ya kuwa na furaha. Baadaye, nilisoma katika neno la Mungu kwamba: “Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. … Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Hapa, mwishowe niligundua kuwa kula vizuri, kuvaa nguo za kupendeza, na kufurahia si kile ambacho watu wanahitaji kuishi. Kile ambacho watu wanahitaji ni wokovu wa Mungu na ugavi wa maisha Wake Mungu. Ni kwa vitu hivi tu ndipo utupu katika roho za watu unaweza kutatuliwa. Maswali ambayo yalinisumbua kwa muda mrefu sana hatimaye yakajibiwa: Mungu anajali kila kiumbe aliyeumbwa—watu wanapaswa kuishi kwa kumtegemea Mungu na wanapaswa kuishi kwa ajili ya Mungu, kwani ni kwa kuishi kwa njia hii tu ndiyo maisha ya watu yanaweza kuwa ya maana. Niliposoma zaidi neno la Mungu, polepole nilipata kuelewa ukweli kiasi, na baadaye nikachukua wajibu kanisani. Mara nyingi nilienda kwenye mikutano na kushirikiana na ndugu zangu, na niliishi siku zangu nikihisi kana kwamba nilikuwa naishi maisha kamili, yenye kuridhisha. Lakini, kukamatwa kwa ghafla kuliyaharibu kabisa maisha yangu ya kimya na kunitupa kwenye pango la mapepo …
Ilikuwa ni siku ya kiangazi yenye mvua mnamo Julai 17, 2009, wakati mimi na dada zangu watatu tuliamka kutoka katika usingizi mfupi wa mchana na kumsikia mbwa kwenye uga akianza kubweka ghafla bila kukoma. Nilitazama nje kuona kilichokuwa kikiendelea, na nikaona zaidi ya polisi 20 wasio na sare rasmi wakipanda juu ya ukuta na kuingia ugani. Kabla sijapata wakati wa kufanya chochote, walikimbia ndani ya nyumba na kutuvuta tuingie sebuleni. Mabadiliko ya ghafla ya hali yaliniacha mwenye hofu kubwa huku nikiwaza jinsi nitakavyojibu maswali ya polisi. Lakini wakati huo, wazo lilinijia: Mungu alikuwa ameruhusu hali hizi zitokee, kwa hivyo ni lazima nitii. Baada ya hapo, polisi walituamuru tuchuchumae chini na wawili kati yao walinipindua mikono yangu nyuma ya mgongo, na kushinikiza kirungu cha umeme shingoni mwangu, na kuweka koti juu ya kichwa changu. Waliendelea kunisukuma chini na miguu yangu ikafa ganzi. Kusonga kidogo kulileta wimbi la matusi na kukemea. Polisi hawa waovu walipekua nyumba kama majambazi, na nilimwomba Mungu moyoni mwangu bila kusita nikisema, “Mungu! Najua kila kitu kiko mikononi Mwako na ni kupitia nia Zako nzuri kwamba nimekabiliwa na hali hii. Hata ingawa sielewi kwa sasa, niko tayari kutii. Mungu! Nahisi mwenye hofu sana sasa, ninaogopa sana, na sijui nitazikabili hali za aina gani kufuatia. Najua kimo change ni kidogo sana, na kwamba naelewa ukweli kiogo sana, kwa hivyo naomba ulinzi na mwongozo Wako. Nipe imani na nguvu, ili niweze kusimama imara, na nisiwe Yuda na kukusaliti.” Nilisali tena na tena, bila kuthubutu kumwacha Mungu hata kwa muda mfupi. Katika utafutaji wao, polisi walipata kompyuta nne ndogo za kupakata, simu kadhaa za rununu, vidude kadhaa vya kuhifadhi data na vicheza rekodi vya MP3, na zaidi ya RMB 1,000 pesa taslimu. Baada ya kumaliza kuipekua nyumba, walichukua kila kitu walichopata, wakampiga kila mmoja wetu picha, na kisha wakatulazimisha kuingia kwenye gari lao. Nilipokuwa nikitoka nje, niliona magari ya polisi na polisi wengi ambao singewza kuhesabu.
Polisi walitupeleka kwenye bweni katika eneno dogo la jeshi, ambapo walitutenganisha ili kutuhoji mmoja mmoja. Kulikuwa na polisi wawili waliolinda mlango. Mara tu waliponisukuma ndani ya chumba, maafisa watatu wa kiume na afisa mmoja wa kike walianza kunihoji. Aafisa mmoja wa kiume alianza kwa kuuliza, “Unatoka wapi? Jina lako ni nani? Unafanya nini katika eneo hili? Fedha za kanisa ziko wapi?” Nilimwomba Mungu moyoni mwangu bila kukoma, na bila kujali walichoniuliza, nilikataa kutoa sauti. Baada ya kuona hili, wote walikasirika. Waliniamuru nisimame kama mlingoti na hawakuniruhusu niegemee ukutani. Kwa njia hii, waliendelea kubadilishana kunihoji kwa siku tatu na usiku tatu na, wakati huo, hawakuniruhusu nile au kulala. Mwili wangu uliokuwa mwembamba na dhaifu tayari haukuweza kuhimili unyanyasaji kama huo. Kichwa changu kilihisi tayari kulipuka, nilihisi kana kwamba moyo wangu ulikuwa umefukuliwa, nilikuwa na uchovu na mwenye njaa, na sikuweza kusimama imara. Lakini kila nilipofunga macho yangu, walinisukuma na kuniambia, “Hulali kabla hujajibu maswali yetu! La hasha! Tuna wakati wote duniani. Acha tuone unaweza kudumu kwa muda gani!” Mara nyingi waliniuliza maswali juu ya kanisa. Nilikuwa na wasiwasi sana wakati huo wote wa mateso, na niliogopa kwamba ningeweza kusema kitu kimakosa katika wakati wa uzembe. Nilihisi kuteswa kimwili na kiroho, lakini nilipofikiria kuwa nilikuwa nimestahimili yote ambayo ningeweza kustahimili na singeweza kuvumilia, Mungu alinipa nuru kwa kunifanya nikumbuke kifungu hiki cha neno Lake, “Unapokabiliwa na mateso ni lazima uweze kuweka kando masilahi ya mwili na usifanye malalamiko dhidi ya Mungu. Wakati Mungu anajificha kutoka kwako, ni lazima uweze kuwa na imani ya kumfuata Yeye, kudumisha upendo wako wa awali bila kuuruhusu ufifie au kutoweka. Haijalishi anachofanya Mungu, ni lazima utii mpango Wake na uwe tayari kuulaani mwili wako mwenyewe badala ya kulalamika dhidi Yake. Wakati unakabiliwa na majaribu, lazima umridhishe Mungu, ingawa unaweza kulia kwa uchungu au uhisi kusita kuhusu kuacha kitu unachopenda. Huu tu ndio upendo wa kweli na imani. Haijalishi kimo chako halisi ni kipi, ni lazima kwanza umiliki nia ya kupitia ugumu na imani ya kweli, na ni pia lazima uwe na nia ya kuutelekeza mwili” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji). Kila mstari wa maneno ya Mungu ulinitia moyo. Hiyo ni kweli, Shetani alikuwa akitumia udhaifu wangu wa mwili kunishambulia. Alitarajia kutumia hamu yangu ya kuulinda mwili wangu na kuishi katika raha na urahisi kunifanya nimtii. Singemruhusu anidanganye na kunifanya niishi kama Yuda mwoga, aliyeshuka hadhi. Nilikuwa tayari kuishi kwa kufuata neno la Mungu, kuunyima mwili, na kumpenda Mungu. Ni afadhali niulaani mwili wangu kuliko kulalamika dhidi ya Mungu au kumsaliti. Maneno ya Mungu yalikuwa chanzo cha nguvu isiyo na mwisho, na yalinipa azimio la kuvumilia mateso yangu. Usiku wa manane siku ya tatu, mtu mwenye umri wa makamu alikuja, dhahiri kuwa alikuwa mkubwa wao, na alipoona kuwa hawakuwa wameweza kupata neno kutoka kwangu, alikuja kusimama moja kwa moja mbele yangu na kusema, “Wewe ni mwanamke mchanga, na asiye na sura mbaya. Unaweza kufanya chochote unachotaka. Kwa nini unasisitiza kumwamini Mungu? Kwa nini usituambie tu kile unachojua? Kuchelewesha vitu hakutakufaidi. Kadiri unavyochelewa zaidi, ndivyo utakavyoteseka zaidi.” Wakati huo, mwili wangu ulikuwa dhaifu sana, na azimio langu likaanza kutikisika. Nilifikiria, “Labda niwaambie tu jambo lisilo muhimu. Nikiendelea kuahirisha mambo namna hii, ni nani ajuaye njia zingine wanazoweza kutumia kunitesa?” Lakini mara moja nikawaza, “Hapana! Siwezi kusema chochote! Nikisema kitu kimakosa watauliza zaidi na zaidi. Sitaweza kukoma mara nitapoanza, na kisha kwa kweli nitakuwa Yuda.” Nilipogundua hili, nilielewa kuwa nilikuwa karibu kuanguka katika hila ya Shetani. Hii ilikuwa hatari! Mashetani waovu, wanaostahili dharau kweli! Walikuwa wakitumia unyonge wangu, wakitumia mbinu ngumu na rahisi kunifanya nilisaliti kanisa. Singeweza kujiruhusu nidanganywe na Shetani. Ningekufa kabla sijafanya chochote kumsaliti Mungu.
Siku ya nne, polisi hawa waovu walipoona kuwa bado sikuwa nimewaambia chochote, walijaribu mbinu nyingine. Walinipeleka ndani ya chumba kingine na kufunga mlango. Kisha, nilikumbuka kuwa nilishawahi kumsikia mtu akielezea jinsi polisi walivyomleta dada mmoja kwenye chumba cha jela kilichojaa wanaume na kuwaruhusu wafungwa wa kiume wamdhalilishe. Nilihisi hofu sana, kana kwamba nilikuwa mwanakondoo katika kinywa cha chui bila tumaini la kutoroka, na nikawaza,“Sasa watanitesaje? Je, nitakufa katika chumba hiki? … Mungu, naomba unilinde na unipe nguvu!” Mara kwa mara niliomba na kumwita Mungu, nisithubutu kumwacha hata kwa muda mfupi. Polisi waovu walikaa kitandani. Waliniambia nisimame mbele yao na wakaniuliza maswali yaleyale, na walipoona bado sikuwa nazungumza, mmoja wao alikasirika. Alishika mikono yangu kwa nguvu, na kuipindua nyuma ya mgongo wangu, akanitia pingu, na kuniamuru nisimame kama anayeendesha farasi. Miguu yangu tayari ilikuwa haina nguvu wakati huu. Ilikuwa dhaifu sana hata haingeweza kusimama, sembuse kunitegemeza katika kusimama kama anayeendesha farasi. Sikuweza kudumisha mkao huo hata kwa dakika moja. Wakati mkao wangu haukukidhi mahitaji yao, mmoja wao alinipiga teke kwa ukali kwenye muundi wangu, akaniangusha chini. Afisa mwingine mkubwa wa kiume alisogea mbele na kuniinua kwa kuvuta pingu nilizofungwa, kisha akainua mikono yangu nyuma juu hewani, akanikaripia huku akifanya hivyo, “Utaongea sasa? Usiujaribu uvumilivu wangu!” Kadiri alivyoniinua zaidi, ndivyo pingu zilivyozidi kukazika, na nikalia kwa uchungu. Kadiri nilivyopiga unyende, ndivyo alivyoniinua zaidi na ndivyo alivyonikaripia kwa ukali zaidi, lakini sikuweza kuhisi chochote isipokuwa kwamba mikono na vifundo vya mikono yangu vilikuwa karibu kuvunjika. Katika maumivu yangu, kifungu cha neno la Mungu kilitokea akilini mwangu. “Katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Katika wakati huo, nilihisi kwa dhati faraja na kutiwa moyo na Mungu. Nilihisi kwamba Mungu alikuwa kando yangu, kwamba Alikuwa pamoja nami, Akinihimiza nisimame imara bila kujali mateso yalivyokuwa makubwa, na kuwa mwaminifu Kwake mpaka mwisho, kwa sababu huu tu ndio ushuhuda mkuu wenye nguvu. Nilimwomba Mungu kimya kimya, “Mungu, sasa Unanihitaji nisimame imara na kushuhudia kwa ajili Yako. Haijalishi ninateseka kiasi gani, nitashuhudia kwa ajili Yako mbele ya Shetani, na hata nikifa sitakusaliti! Sitamtii Shetani!” Baada ya duru nyingine ya kuteswa, yule polisi aliona kuwa bad0 sikuwa nazungumza, kwa hivyo alinirusha chini sakafuni kwa ukali. Baadaye, niliona kuwa pingu zilikuwa zimekata majeraha mawili katika vifundo vya mikono yangu, na maumivu yalionekana kuupitia mwili wangu mzima. Hata leo, siwezi kuinua vitu vizito kwa kifundo cha mkono wanguwa kulia.
Polisi walinitesa kwa kurudia kwa zaidi ya siku kumi ili kupata habari juu ya kanisa. Walipoona kwamba mbinu zao za uchokozi hazikuwa zinafanya kazi, walijaribu mkakati tofauti. Siku moja, walimtuma afisa wa kike aje awe mwandani wangu. Aliniletea bidhaa za matumizi ya kila siku, na kisha akajaribu kujipendekeza kwangu, akisema, “Jitazame mwenyewe—mwanamke mchanga, mrembo, ambaye lazima awe na diploma nzuri. Kama hungekuwa unamwamini Mungu, tungeweza kuwa marafiki. Kama huna mahali pa kwenda, unaweza kukaa nyumbani kwangu. Naweza kukusaidia kupata kazi nzuri hapa, na nikujulishe kwa kipenzi mzuri wa kiume. Unaweza kuwa na nyumba yako mwenyewe, mumeo, mtoto, na ufurahie siku zako na familia yako. Je, hilo halingekuwa jambo zuri? Mambo yalivyo sasa, huwezi kurudi nyumbani. Huikosi nyumba yako na wazazi wako?” Afisa wa kiume aliyekuwa karibu nao akajiunga ndani, akisema, “Hiyo ni kweli. Kwa nini unashinda siku zako kujificha, ukihama kutoka mahali pamoja hadi pengine? Kwa nini ujiweke katika hali hiyo? Alimradi ushirikiane na sisi, nakuahidi kuna suluhisho kutoka kwa haya yote kwako.” Niliwasikia wakinijaribu, na moyo wangu haukuwa na budi ila kuwa dhaifu, “Wanasema kweli. Nimeshinda miaka iliyopita karibuni mafichoni, nikiogopa kukamatwa na polisi. Sijakuwa na anwani maalum, na nimekuwa mwoga kila wakati. Je, siku hizi za mateso zitaisha lini? Kuishi namna hii ni kwa kusikitisha kweli!” Lakini wazo hilo lilileta giza moyoni mwangu ghafla, kwa hivyo nilimlilia Mungu, “Mungu! Najua hali yangu siyo sahihi. Natoa madai Kwako na kulalamika juu Yako. Huu ni uasi na upinzani wangu. Mungu! Nakuomba Unipe nuru ili nigeuke kutoka katika hali hii isiyo sahihi, niikomeshe njama ya Shetani isifaulu, na nijizuie kuanguka katika mtego wa Shetani.” Baada ya kuomba, nilikumbuka kifungu cha neno la Mungu, “Pengine utayakumbuka maneno haya: ‘Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.’ Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?). Nuru katika maneno ya Mungu iliuangaza moyo wangu. Nilikuja kuelewa umuhimu wa kupitia mateso na dhiki. Mungu hutumia mateso ya mapepo hawa kutupa azimio la kuvumilia mateso na kukamilisha uaminifu na imani yetu katika kumfuata, ili uzoefu na ushuhuda wetu uweze kuwa dhibitisho la nguvu la Mungu kumshinda Shetani, na ili watu wote waweze kuona ushuhuda kama huo kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho siyo kazi ya mwanadamu, lakini ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Bila kazi ya Mungu na mwongozo na ruzuku ya maneno ya Mungu, hakuna mtu anayeweza kuvumilia ukatili na mateso ya kuvunja binadamu ya muda mrefu ya mapepo hawa. Kuweza kumwamini Mungu na kumfuata Mungu hata kwa gharama ya maisha ya mtu ni athari inayopatikana na kazi ya Mwenyezi Mungu kwa watu. Ni ushuhuda wa utukufu uliopatikana na Mungu, na nguvu ya uweza ya Mungu. Katika hatua hii ya mwisho ya kazi Yake, Mungu anataka kupata kikundi cha washindi ambao wanaweza kustahimili mateso na dhuluma mbaya ya Shetani na kugeukia haki kwa ujasiri. Hawa ndio washindi ambao Mungu anatamani kuwapata hatimaye! Neno la Mungu linasema, “Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?). Katika mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita, Mungu amefanya hatua tatu za kazi na Amepata mwili mara mbili. Katika kupata mwili Kwake kwa mwisho, Amekuja kufanya kazi nchini China, nchi inayomkana Mungu ambayo humsumbua Mungu kwa nguvu sana, na Anatimiza sehemu ya utukufu Anaopata katika siku za mwisho juu ya wale kati yetu ambao tumeumizwa vibaya na kwa kina na Shetani, hivyo kumshinda Shetani, na wakati huo huo kufanyiza ukweli na uzima ndani yetu. Hakika tunapata mengi sana kutoka kwa Mungu, na hivyo tunapaswa kushuhudia kwa ajili ya Mungu. Hili ni agizo la Mungu, na vile vile neema na uinuaji Wake, na ni heshima yetu. Kwa hivyo, mateso tunayostahimili leo yana maana na ni ya thamani, na yanawakilisha fadhili ya Mungu kwetu. Kupitia nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu, nilielewa mapenzi ya Mungu, nikabaini hila za Shetani, na nikapata azimio la kustahimili mateso yoyote kusimama imara na kushuhudia kwa ajili ya Mungu. Baada ya hapo, polisi waliendelea kunihoji kwa majuma mengine mawili, lakini sikuwahi kuwaambia habari yoyote kuhusu kanisa.
Baadaye, nilihamishiwa kwa nyumba ya kuzuilia ya mahali hapo. Mara tu nilipofika, afisa wa kike aliniamuru nivue nguo zote nichunguzwe, naye akachukua pesa nilizokuwa nimebeba pia. Nilipoingia katika seli, harufu ilikuwa mbaya sana. Zaidi ya watu ishirini walifinyiliwa kwenye jukwaa moja la kulala. Sote tulikula, kunywa, kukojoa na kunya katika chumba kimoja. Katika mwezi uliofuata, niliamuriwa na polisi hawa waovu kufanya kazi ya ziada na kuchukua wajibu wa ziada kila siku. Walikuwa wamechukua miwani yangu, kwa hivyo sikuweza kuona vyema, na ilinibidi nivute vitu karibu na macho yangu nilipofanya kazi ili nione vizuri. Zaidi ya hayo, taa za nyumba ya kizuizini zilikuwa ndogo na zenye mwangaza mdogo. Wakati wengine walilala, ilinibidi niendelee kufanya kazi hadi usiku kwa sababu ilinichukua muda mrefu sana kumaliza kazi zangu. Macho yangu yalikuwa yamechoka sana, na nilihofu kazi hiyo ingenifanya niwe kipofu. Sikuweza kulala vizuri usiku, na kila usiku nililazimika kufanya saa moja ya kazi ya zamu katika seli. Zaidi ya kazi nzito kila siku, pia nilihojiwa mara mbili kwa wiki, na kila wakati, polisi hawa waovu walinitia pingu na silisili, na pia sare ya mfungwa ya “manjano ya kibeberu”. Nakumbuka, siku moja kama hiyo, kulikuwa kunanyesha. Nilitembea kando ya afisa wa polisi wa kiume, ambaye alikuwa ameshikilia mwavuli juu yake. Nilitembea kwa ugumu mkubwa, nikiwa nimefungwa pingu na silisili na nimevalia sare yangu nyembamba ya gereza, nikitetemeka huku mvua baridi ikininyea. Silisili hizo zilikuwa nzito sana, na zilikwaruza vifundo vya miguu yangu na kutoa sauti kwa kila hatua. Hapo zamani nilikuwa nimeona vitu kama hivyo kwenye runinga tu, lakini sasa nilikuwa nikivipitia mwenyewe. Sikuwa na budi ila kuidharau hali yangu, na nikalia moyoni mwangu, “Hivi ndivyo wauaji na wabakaji huhojiwa! Nilifanya nini kustahili hili?” Ilikwa ni wakati huo ndipo Mungu alinipa nuru na nikakumbuka maneno ya Mungu, “Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! … Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)). Nilipolinganisha maneno ya Mungu na uhalisi nilioukabili, hatimaye niliona kwamba ingawa CCP inatangaza kwa kila njia kwa ulimwengu wa nje kwamba watu wote wanastahili uhuru wa kidini, wakati mtu yeyote anamwamini Mungu kweli, inajibu na kila aina ya mateso, ukamataji, dhuluma, matusi, shutuma, na kufunga jela. Haiwatendei watu kwa njia yenye huruma. Maadili ya “uhuru wa imani ya kidini” na “demokrasia na haki za binadamu” ni hila zilizokusudiwa kudanganya, kupofusha, na kucheza na wengine tu! Chama hiki kiovu hujipamba na ufasaha wa kila aina, lakini kwa kweli ni dhalimu na kikatili kama mnyama mwenye pepo, kweli ni kibaya na kiovu kabisa! CCP inapuuza kwa makusudi na haiwaangalii waovu na watendaji maovu ulimwenguni ambao hudanganya, hulaghai, huua, na kuiba, na nyakati nyingine hata inawalinda, lakini inawatesa kikatili na kuwaua watu wanaomwamini Mungu na kufuata njia sahihi. CCP kweli ni pepo anayejifanya adui wa Mungu! Nilipofikiria juu ya vitu hivi, sikuwa na budi ila kudharau pepo huyu mwovu. Niliapa kumwasi hata kama ingenigharimu maisha yangu, na nilijitoa kwa Mungu! Baada ya mwezi, licha ya kukosa ushahidi wowote, polisi walinihukumu mwaka mmoja wa kufunzwa upya kupitia kazi kwa mashtaka ya “kuvuruga utaratibu wa umma.”
Nilipofika katika kambi ya kazi, niligundua kuwa hapa palikuwa ni mahali pa giza zaidi. Hapa, hapakuwa na uhuru hata kidogo. Wazuiliwa wangeweza tu kula, kunywa, au kwenda chooni kwa maagizo ya walinzi wa kitengo chao, na tulilazimika kuwatii walinzi katika kila kitu au tungeadhibiwa. Tulipoingia na kutoka chumbani humo, tulilazimika kusema nambari zetu, na mtu yeyote angesema nambari isiyo sahihi, kitengo kizima kingeadhibiwa kwa kushinda saa mbwili chini ya jua kali au kuloweka katika mvua. Tulipoenda kula katika kafeteria, mtu yeyote angeripoti nambari isiyo sahihi, kitengo chote kingeadhibiwa kwa kulazimishwa kungoja nje na kutoruhusiwa kula. Tungetazama tu bila msaada wafungwa wengine walipokula milo yao. Tulilazimika pia kuimba wimbo wa kijeshi kabla ya kila mlo, kwa nguvu zetu zote, na ikiwa mtu angeimba bila kufuata mfumo wa sauti au kwa sauti ya chini, tungelazimika kuanza wimbo tena, mara moja, mara mbili…. Tuliruhusiwa tu kula mara walinzi wa kitengo chetu waliporidhika. Mfumo huu unadaiwa “mfumo wa usimamizi” upo tu kutosheleza matamanio ya walinzi hao waovu ya kuwa mabwana wa wengine, kuwaamuru wengine huku na kule, na kufurahia hadhi. Wao kila siku huwaweka wengine ukingoni. Hapa, zaidi ya kuwasafishia walinzi na kukunja mifarishi yao, wafungwa walilazimika kuchot maji ya kuosha miguu yao na kukanda migongo yao. Walinzi walitenda kama watawala na malkia, wakikutabasamia ikiwa umewahudumia vizuri, lakini wakikukaripia vibaya au kukupiga ikiwa umewahudumia vibaya. Haijalishi tulikuwa tunafanya nini, hata kama tungekuwa bafuni, punde tulipowasikia walinzi wakipaza sauti, tulilazimika kujibu kwa sauti “nipo” na kukimbia haraka kusikiliza maagizo yao. Hivi ndivyo kambi za kazi chini ya serikali ya CCP zinaendeshwa. Ni zenye giza, za kukandamiza, katili, na za kudhihaki. Nikiwa nimekabiliwa na haya yote, sikuhisi chochote isipokuwa chuki na kukosa msaada. Na zaidi ya hayo, polisi hawa waovu waliwachukulia wafungwa wa kambi ya kazi kama wanyama wavutao mizigo na watumwa, kama tu zana za kuchuma pesa. Walituzidishia kazi kila siku, hadi kufikia kiwango ambapo kando na kula na kulala, tulitumia wakati wetu mwingine kufanya kazi ili kuwatengenezea mali. Kila siku, zaidi ya kanuni kadhaa tulizolazimika kufuata, ilitubidi pia kushughulika na kazi nyingi, na hatungejua ni lini tungeadhibiwa na kutukanwa, kwa kweli singeweza kustahimili kuishi kwa namna hiyo, na sijui ni mara ngapi niliwaza moyoni mwangu, “Je, nitakufa katika kambi hii ya kazi? Kila siku wanatusukuma hadi kuchoka. Nitaishi vipi mwaka mgumu kama huu? Hili litaisha lini? Siwezi kustahimili dakika nyingine, sekunde nyingine, mahali hapa pabaya mno….” Juu ya hilo, hakukuwa na mtu ambaye ningeweza kushiriki naye wazi kuhusu hisia zangu. Kila siku, ilinibidi nistahimili kila kitu kwa kimya na kufanya kazi bila kukoma, na nilihisi mnyonge. Usiku, wakati kila mtu alikuwa amelala, nilipoangalia nje kuona nyota kupitia dirisha lililowekwa vyuma, nilizidiwa na huzuni. Nilihisi nikiwa nimetengwa na mpweke, na sikuwa na budi ila kulia kwenye mto wangu. Lakini wakati nilipohisi dhaifu zaidi, nilikumbuka neno la Mungu ghafla, “Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe ‘jahanamu’ na ‘kuzimu,’ katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (9)). Kila mstari wa neno la Mungu ulifariji moyo wangu ulioteseka. Ndiyo! Nilihisi mpweke na niliyetengwa sana katika gereza hili la mapepo kwa sababu sikuwa na mtu wa kumwamini, lakini Mungu alishuka duniani kutoka mbinguni na akavumilia matusi na mateso mabaya ili kutuokoa, wanadamu, tuliomwasi na kumpinga, na hakuna mtu hata mmoja angeweza kumwelewa au kujali mapenzi Yake. Badala yake, alikabiliwa na kuelewa vibaya kwa watu, malalamiko, kupuuzwa, mashambulizi, udanganyifu, na usaliti wa watu. Je, Mungu hakuhisi kutengwa na upweke kama huo? Je, Mungu pia hakuteswa na kuumizwa? Lakini licha ya hili, sikuyafikiria mapenzi ya Mungu hata kidogo, na nikawa hasi na dhaifu baada ya mateso kidogo tu. Nilitaka tu kujiondoa na kutoroka. Kwa kweli nilikuwa mwasi! Mungu aliruhusu mateso ya mashetani hawa yanifikie siyo kwa sababu Alitaka kunifanya niteseke kwa makusudi, lakini kwa sababu Alitaka nione wazi uso mbaya wa CCP kupitia katika mateso yake mabaya, niweze kuiacha kwa kweli, na mwishowe nimgeukie Mungu kabisa. Haya yote yalifanywa na nia njema na wokovu wa Mungu. Kwa vyovyote vile, Kristo alikuwa Akiteseka pamoja nami sasa, kwa hivyo sikuwa peke yangu tena. Ilikuwa tu wakati huo ndipo nilihisi kuwa katika yote ambayo Mungu hufanya kwa mwanadamu, kuna wokovu na upendo tu. Ingawa niliteseka katika mwili, lilikuwa jambo la manufaa sana katika kuingia kwangu katika maisha! Mara nilipoelewa mambo haya, polepole nilianza kutoka katika hali yangu hasi, dhaifu, na nikapata azimio la kuridhika na mateso ili kutoa ushahidi kwa Mungu.
Mwishoni wa Juni 2010, niliachiliwa mwezi mmoja kabla ya wakati. Kwa kupitia mateso na ugumu huu, nilihisi kweli kuwa wokovu wa Mungu kwa watu ni wa kweli na wa vitendo, na kwamba upendo wa Mungu kwa watu ni wa kina na ni wa kweli! Nisingepitia mateso na kukamatwa na pepo hawa, imani, ujasiri, na azimio langu la kuteseka havingekamilishwa, na kamwe singeweza kuona wazi uso halisi na mbaya wa pepo. Singemdharau kwa dhati kamwe, na kamwe singeweza kuugeuza moyo wangu kwa Mungu na kujitolea kabisa kwa Mungu. Bila uzoefu halisi wa uchungu wa mateso na ugumu, singeweza kamwe kuelewa au kufahamu huzuni ambayo Mungu anasikia au gharama Anayolipa kwa kuja katika mwili mahali hapa pachafu kutuokoa. Hili liliniruhusu nihisi upendo wa Mungu kwa kina zaidi na liliuleta moyo wangu karibu na Yeye zaidi. Ninashukuru kwa maneno ya Mungu kwa mwongozo ambao yalinipa kila wakati, na kwa kuandamana nami kwa mwaka mzima wa kuishi gizani katika gereza. Leo, nimerudi kanisani, nasoma neno la Mungu na kushiriki juu ya ukweli na ndugu zangu, nimechukua wajibu wangu tena, na moyo wangu umejawa na furaha na raha isiyo na mwisho. Namshukuru Mungu kwa dhati sana, na nimekula kiapo mwenyewe: Haijalishi ni hali au majaribu gani ambayo yatanipata katika siku zijazo, natamani tu kufuatilia ukweli kwa nguvu yangu yote na kumfuata Mungu hadi mwisho!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?