Moyo Unaorandaranda Wakuja Nyumbani

14/01/2020

Na Novo, Ufilipino

Jina langu ni Novo, na mimi natoka Ufilipino. Nimemfuata mama yangu katika imani yake katika Mungu tangu nilipokuwa mdogo, na ningeenda kusikiliza mahubiri kanisani na ndugu zangu. Ingawa nilikuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, nilihisi kuwa sikuwa nimepitia mabadiliko yoyote na kwamba nilikuwa sawa na mtu asiyeamini. Ndani ya moyo wangu nilikuwa nikifikiria kila wakati juu ya jinsi ya kuchuma pesa zaidi, na juu ya jinsi ya kushinda siku zangu katika raha na kufurahia maisha mazuri. Juu ya hiyo, pia ningeenda nje kunywa na marafiki wangu wakati wote, na punde nilipokuwa na pesa zozote zaidi ningeenda kucheza kamari. Nilijua kuwa kufanya mambo haya kulikinzana na mapenzi ya Bwana—mara nyingi ningemwomba Bwana na kukiri dhambi zangu, na ningeamua kwa dhati Kwake kwamba nitaacha tabia hizi mbaya na sitafanya dhambi tena kutoka siku hiyo kuendelea. Lakini kwa kubembeleza na kushawishi kwa marafiki wangu, singeweza kujidhibiti mwenyewe kasbisa. Na kwa hivyo ilikuwa kwamba nilizidi kuwa mpotovu, moyo wangu ulizidi kuwa mbali zaidi na Mungu, hakukuwa na ukweli wowote katika maombi yangu. Kila wiki ningesema sala chache rahisi ili nimalize tu. Wakati mwingine nilihisi kukata tamaa kwa kweli kwani nilijua kuwa Bwana atakaporudi Atamhukumu kila mtu kulingana na vitendo na tabia zake, na kisha kuamua iwapo angeenda mbinguni au chini kuzimu. Nilihisi kuwa nilikuwa mpotovu sana hata Mungu asingenisamehe tena. Baadaye nilifunga ndoa na nikapata watoto, na yote niliyofikiria ilikuwa ni mke wangu na watoto wangu. Nilikuwa nimesahau kabisa kuhusu imani yangu zamani. Ili kuwapa wanangu maisha bora na kutimiza hamu yangu ya kuwa tajiri, niliamua kwenda kufanya kazi ughabuni, ambayo ndiyo iliyonileta Taiwani. Baada ya kupata kazi bado sikufanya mabadiliko yoyote katika mtindo wa maisha. Katika wakati wangu wa burudani ningeenda na wafanyakazi wenzangu kunywa na kuimba karaoke, nikiishi maisha ya raha; kwa muda mrefu nilikuwa nimeisukuma imani yangu katika Mungu nyuma ya akili yangu.

Mnamo mwaka wa 2011, nilifanya kazi ya kutia weko vifaa katika kiwanda huko Taiwan. Siku moja mnamo 2012, mfanyakazi mwenzangu huko Taiwan aligundua kuwa nilikuwa Mkatoliki, kwa hivyo alinialika kwenda Misa katika kanisa lake. Jumapili moja asubuhi, alikuja kunichukua kutoka kiwandani na akanipeleka nyumbani kwa rafiki yake. Ilikuwa huko ndiko nilikokutana na Ndugu Yusufu. Aliniuliza, “Ndugu, je, unaamini katika kuja kwa pili kwa Bwana Yesu?” Nilisema kwamba niliamini. Kisha akaniuliza, “Je, unajua ni kazi gani ambayo Bwana Yesu atafanya Atakaporudi?” Nilimjibu, “Ninaamini kuwa Bwana Yesu atakaporudi, Ataketi kwenye kiti cheupe cha enzi na kuwahukumu wanadamu. Kila mtu atatoa hesabu ya dhambi zake akipiga magoti mbele ya kiti cha hukumu, na kisha Bwana ataamua ikiwa atakwenda mbinguni au chini kuzimu kutegemea na vitendo na matendo yake.” Ndugu Yusufu aliendelea kuniuliza, “Tukikwambia kwamba Bwana Yesu tayari amerejea na kwa sasa Anafanya kazi Yake ya kuhukumu ya siku za mwisho, na hivyo kutimiza unabii kwamba ‘lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu,’ je, utaamini hii?” Nilishangaa sana nilipomsikia akisema hili. Niliwaza: “Je, Bwana Yesu tayari amerudi? Hili linawezekanaje? Sijaona kiti cheupe cha enzi kikitokea angani, na sijamwona Bwana akishuka juu ya wingu jeupe. Ilhali anasema kwamba Bwana amerudi kufanya kazi Yake ya hukumu, na hivyo kutimiza unabii kwamba ‘lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu.’ Inaleta maana. Hekima ya Mungu ni isiyoeleweka kwa mwanadamu, kwa hivyo ni afadhali niendelee kutafuta.” Kisha nikamjibu, “Ndugu, siwezi kuthubutu kusema kama Bwana Yesu amerudi au hajarudi, kwa hivyo tafadhali shiriki nami kuhusu hili.” Kisha alipata vifungu kadhaa ndani ya Biblia kuhusu unabii wa kurudi kwa Bwana na kufanya Kwake kazi ya hukumu ambavyo alnisomea. Kwa mfano, kulikuwa na sura ya 4, aya ya 17 kwenye Waraka wa Kwanza wa Petro ambao unasema: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu.” Na pia sura ya 16, aya 12-13 katika Injili ya Yohana: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo.” Ndugu Yusufu alisema hii “Roho wa ukweli” inarejelea kurudi kwa Bwana na kuonyesha Kwake ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu. Mungu wa siku za mwisho amerejea katika mwili kama Mwana wa Adamu. Kwa msingi wa kazi Yake ya ukombozi katika Enzi ya Neema, Anaonyesha ukweli na kufanya hatua ya kazi Yake ya hukumu ikianza na nyumba ya Mungu. Kwa ukweli, kazi hii ya hukumu ni kazi ya kutakasa kabisa na kumwokoa mwanadamu. Hii inatimiza hasa unabii wa Bwana Yesu: “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana…. Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:22-27). Nilisikiliza kwa makini ushirika wa ndugu huyo, na niliamini kwamba ujumbe huu wote ambao alikuwa akishiriki nami ulikuwa wa kweli kwa sababu ninaamini kwamba unabii wote wa Bwana lazima ukamilike, lazima utimie.

Baadaye, Ndugu Yusufu alinisomea vifungu viwili vya Maneno ya Mwenyezi Mungu katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli”: “Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.” “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya kusoma maneno haya, Ndugu Yusufu alishiriki nami ukweli mwingi juu ya kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho. Nilikuja kuelewa kuwa kazi ya Mungu ni ya vitendo sana na ni ya kawaida kabisa, kwamba kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho sio kabisa kama nilivyokuwa nimefikiria. Nilikuwa nimewaza Mungu akiiweka meza kubwa katikati ya hewa, Mungu akiwa ameketi kwenye kiti kikuu cheupe cha enzi na wanadamu wote wakipiga magoti mbele Yake. Kisha Mungu angeorodhesha dhambi zetu moja baada ya nyingine ili kuamua ikiwa sisi ni wema au mbaya, na Angeamua ikiwa tungepanda kwenda mbinguni au kushuka chini kuzimu. Badala yake, Mungu amekuwa mwili na Amekuja ulimwenguni kuonyesha ukweli kwa njia ya vitendo, kuhukumu dhambi za mwanadamu, na kufunua ukweli wa upotovu wa mwanadamu na vile vile asili na kiini chake. Ndugu Yusufu aliendelea katika ushirika kutuambia kwamba tabia zetu za kishetani, kama vile kiburi chetu na kujithamini, ukora na ujanja wetu, na ubinafsi na na hali zetu za chini, lazima vyote vipitie hukumu ya Mungu kabla hatujatakaswa. Matokeo ya mwisho ya kazi ya Mungu ya hukumu ni ili tuweze kuona uchafu na upotovu wetu wenyewe, ubaya na uovu wetu, na tuone kiini chetu kinachompinga na kumsaliti Mungu, ili tujue ya kuwa tumepotoshwa sana na Shetani, kwamba tumejawa na tabia za kishetani, ya kwamba sisi ni mfano kamili wa Shetani, na kwamba tunapaswa kuangamia. Ni kwa njia hii tu ndiyo tunaweza kuja kujichukia na kujilaani, na kumwacha Shetani mara moja. Aidha, ni kwamba, ndani ya hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tunaweza kuja kuijua tabia ya Mungu yenye haki, takatifu na isiyoweza kukosewa. Tunaweza basi kukuza moyo wa kumcha Mungu bila kujua, kamwe tusithubutu tena kutomtii na kumpinga Mungu kiholela, na kuweza kuitelekeza miili yetu, na tutende ukweli. Mara tu tabia zetu za maisha zinapopitia mabadiliko basi tutaweza kumtii na kumwabudu Mungu kweli. Na mara tu tutakapopata vipengele mbali mbali vya ukweli ulioonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho, basi tutatakaswa kabisa na kuokolewa na Mungu, na kustahili kuletwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokataa kukubali kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho hawawezi kupata utakaso wa Mungu—mwishowe wanaweza tu kuondolewa na kazi ya Mungu, na watakuwa wamepoteza fursa ya kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kusikia ushirika wa Ndugu Yusufu, nilihisi kuwa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu ni ya kweli sana na ni ya vitendo!

Nilifikiria kuhusu jinsi nilivyokuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi na ingawa mara nyingi nilikiri dhambi zangu kwa Bwana na kutubu, ningeendelea kutenda dhambi, kusema uwongo, kudanganya, kuwa mkora na mjanja, na mara nyingi hata ningefichua tabia yangu ya kishetani yenye kujitakia makuu, kiburi na yenye kujidai. Nilikuwa daima naishi katika mzunguko wa dhambi na kukiri, kukiri na kutenda dhambi—nilikuwa nikiishi katika uchungu sana. Mungu sasa amekuja kufanya kazi Yake ya hukumu na utakaso ya siku za mwisho, na hii inahitajika sana na wanadamu potovu. Wale wanaomwamini Bwana na wamesamehewa dhambi zao bado wanahitaji utakaso wa kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Biblia inasema, “Utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14). Bwana ni mtakatifu. Ikiwa tutasamehewa tu dhambi zetu, lakini asili yetu ya dhambi na tabia za kishetani havijatakaswa, basi wakati wowote bado tuna uwezo wa kutenda dhambi na kumpinga Mungu, wa kulalamika mara kwa mara au hata kumsaliti Mungu. Tunawezaje, sisi tuliojawa na unajisi na upotovu, kuwa wenye sifa za kutazama uso wa Bwana? Ni hapo tu ndipo nilihisi moyoni mwangu jinsi kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ni muhimu sana! Lingekuwa jambo lisilo la busara, lisilowezekana kama Bwana angekuja na kumchukua kila mtu angani kukutana naye kulingana na fikira na mawazo ya watu! Ndugu Yusufu kisha alishiriki nami uzoefu na ushuhuda wake wa jinsi alivyokubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa kweli nilihisi kwamba ushirika wake ulikuwa na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Kuusikiliza kulikuwa kwa kujenga maadili sana, na niliamini kwamba Bwana Yesu lazima kweli awe amerudi. Kwa hivyo niliamua kutafuta na kuichunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho ili nisikose nafasi yangu ya kukaribisha kuja kwa Bwana.

Baada ya hapo, Ndugu Yusufu alinipa nakala ya Neno Laonekana katika Mwili, na nilifurahia sana. Niliporudi kwenye bweni langu jioni hiyo, nilianza kusoma maneno ya Mungu na niliyasoma usiku kucha. Nilisoma maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjawahi kunena maneno ya ukweli Kwangu, wala maneno matakatifu, wala maneno ya kunitii baada ya kulipitia neno Langu. Hatimaye, hii imani yenu ni ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali, mawazo yenu yamejaa mali ya kilimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na vyema zaidi, vitu zaidi vya raha. Vile vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi, wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), mwanao, bintiyo au mlacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata wakati ambapo, kwa nje, mnavalia mavazi ya kupendeza sana, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri kila mara, mnafanya kazi na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna yeyote anayeshughulika wala kufikiria kuhusu mapenzi Yangu. Ni nini ambacho bado mnatarajia kufaidi kutoka Kwangu?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa).

Kile ambacho maneno haya yalifunua kilikuwa hasa hali katika maisha yangu, na kilikuwa jinsi nilivyohisi kweli moyoni mwangu. Maneno hayo yalikuwa kama upanga wenye makali kuwili ambao ulikata moyo wangu uliokufa ganzi. Nilijua kuwa ni Mungu pekee anayeweza kuchunguza kina cha moyo wa mwanadamu, na ni Mungu pekee anayeweza kufunua ukweli wa upotovu wa wanadamu na kile kilichofichika ndani kabisa ya mwanadamu. Nilihisi kuwa maneno haya yalikuwa matamko ya Roho Mtakatifu, na yalikuwa sauti ya Mungu. Kutoka katika maneno ya Mungu, nilijua kuwa ingawa nilikuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi na mara nyingi nilikiri na kutubu kwa Bwana, asili yangu ya dhambi na tabia ya kishetani ilikuwa haijatakaswa na haijabadilishwa kabisa. Nilikuwa nikitambua tu jina la Bwana, lakini hakukuwa na nafasi ya Bwana moyoni mwangu, wala sikujitumia au kumfanyia Bwana kazi Siku zote nilikuwa nimeshikwa katika jinsi ya kuchuma pesa zaidi, jinsi ya kuongeza raha zangu za mwili, na jinsi ningeweza kuifanya familia yangu ipate kuishi kwa ufanisi zaidi, kamwe sikujishughulisha na mapenzi ya Mungu. Hata nilijua kuwa nilisema uwongo na nilitenda dhambi mara nyingi lakini sikufikiria chochote kuhusu hili. Siku zote nilikuwa nimeamini kuwa Mungu ndiye Mungu mwenye upendo milele, mwenye huruma milele, na hata nikitenda dhambi, Angenisamehe dhambi zangu, Anirehemu na Anibariki. Ni baada tu ya kusoma matamko haya yaliyoonyeshwa na Mungu katika siku za mwisho ndipo niliona tabia ya Mungu yenye haki na takatifu, na nilijua kwamba tabia ya Mungu ni jambo ambalo hakuna mtu anayeweza kuikosea. Hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu viliibua uchaji Kwake ndani yangu na niliomboleza mambo yangu ya zamani. Nilianguka kifudifudi mbele ya Mungu na nikalia sana: “Ee Mungu, nimekuasi, nimekudanganya na kukudharau kwa mambo mengi, na sistahili kuja mbele Yako. Yote ambayo nimefanya yanastahili adhabu tu. Ee Mungu, asante kwa kunipa nafasi ya kutubu na kuokolewa. Kuanzia sasa, nitafanya yote katika uwezo wangu kufuatilia ukweli, kutekeleza waibu wangu vizuri na kulipa mapenzi Yako.” Baada ya kuomba, nilifanya azimio langu kuwa thabiti: Lazima nikubali hukumu ya Mungu na nibadilishe maisha yangu ya kutenda dhambi na kukiri; lazima nisome maneno ya Mungu zaidi na kuyatafakari zaidi ili niweze kuelewa ukweli zaidi na kuwa na nguvu ya kuuacha mwili wangu, kutenda ukweli na kutimiza mapenzi ya Mungu.

Kuanzia wakati huo kuendelea, nilikichukua Neno Laonekana katika Mwili kazini ili niweze kusoma na kutafakari maneno ya Mungu wakati wa mapumziko yangu ya kazi. Kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu, niliona jinsi tabia na mawazo yangu yalikuwa potovu na ya uasi. Baadaye, nilisoma maneno haya ya Mungu ambayo yanasema: “Unapaswa kuomba, hatua kwa hatua, kwa mujibu wa hali yako ya kweli na kile kinachotakiwa kufanywa na Roho Mtakatifu, na unapaswa kuwasiliana kwa karibu na Mungu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa mwanadamu. Unapoanza kufanya mazoezi ya maombi yako, kwanza peana moyo wako kwa Mungu. Usijaribu kufahamu mapenzi ya Mungu; jaribu tu kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu. Unapokuja mbele za Mungu, sema hivi: ‘Ee Mungu! Leo tu ndio natambua kuwa nilikuwa nikikuasi. Mimi kweli ni mpotovu na mwenye kustahili dharau. Awali, nilikuwa nikipoteza muda wangu; kuanzia leo nitaishi kwa ajili Yako, nitaishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na kuridhisha mapenzi Yako. Ningependa Roho Wako afanye kazi ndani yangu daima, na daima aniangaze na kunipa nuru, ili nipate kuwa na ushuhuda wenye nguvu na unaosikika mbele Zako, unaomruhusu Shetani kuuona utukufu Wako, ushuhuda Wako, na thibitisho la ushindi Wako ndani yetu.’ Wakati unapoomba kwa njia hii, moyo wako utawekwa huru kabisa, baada ya kuomba kwa njia hii, moyo wako utakuwa karibu na Mungu, na kwa kuomba hivi mara kwa mara, Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila shaka(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Desturi ya Sala). Katika maneno ya Mungu, nilipata njia ya kutenda kutatua tabia yangu potovu, na nilianza kumwomba Mungu kwa dhati kwa moyo mkunjufu, nikimwambia Mungu juu ya tabia yangu potovu na kumwambia Mungu juu ya yale niliyotumainia kupata ndani ya moyo wangu. Nilimwomba aniongoze niweze kuishi kwa kufuata maneno Yake. Kupitia maombi ya aina hii, mara nyingi nilihisi kuwa Mungu alikuwa akiniongoza na kunipa nuru, na moyo wangu ulijawa na imani na nguvu. Sikuishi tena namna nilivyokuwa nimeishi hapo awali, wala sikutenda tena kulingana na fikira na mawazo potovu niliyokuwa nayo moyoni mwangu. Maisha yangu yalikuwa yamebadilika; hayakuwa tena maisha potovu ambayo nilikuwa nimeishi hapo awali ya kutenda dhambi na kukiri, lakini badala yake nilikuwa kweli naishi mbele za Mungu, na nilikuwa nimepata utunzaji na ulinzi wa Mungu.

Mnamo Julai 2014, nilirudi Ufilipino, na ni hapo tu ndipo nilipogundua kuwa Mungu alikuwa amewachagua ndugu wengi huko Ufilipino. Nilifurahia sana. Sasa ninashiriki maneno ya Mungu na ndugu kanisani, tunaishi maisha ya kanisa, na tunasaidiana na kuungana mkono. Sote tunafuatilia ukweli; tunatafuta kubadilisha tabia zetu na kuokolewa na Mungu. Pia tunakuwa na ushuhuda kwa kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa watu wa nchi yetu na vile vile kwa wale wa nchi zingine ili wajue kuwa Bwana Yesu tayari amerudi na wanaweza kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho kama sisi. Mshukuru Mwenyezi Mungu! Sasa ninaishi maisha yaliyojazwa na yenye furaha sana. Nimeondokana kabisa na aina ya maisha ambayo ni potovu, yaliyoharibika ambayo nilikuwa naishi hapo awali. Ni Mwenyezi Mungu ambaye ameniongoza kupata lengo na mwelekeo wa maisha yangu. Nahisi kuwa hii ndiyo njia pekee ya kuishi maisha yenye maana!

Iliyotangulia: Sauti Hii Yatoka Wapi?
Inayofuata: Kuja Nyumbani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Upendo wa Aina Tofauti

Na Chengxin, BrazilNafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na...

Niliupata Mwanga wa Kweli

Qiuhe, Japani Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana...

Kufuata Nyayo za Mwanakondoo

“Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa ‘kumfuata Mwanakondoo popote...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp