Ni Nini Husababisha Uongo

13/01/2018

Xiaojing Jijini Heze, Mkoani Shandong

Kila mara nilipoona neno la Mungu likituomba kuwa watu waaminifu na kuzungumza kwa usahihi, niliwaza, “Sina tatizo na kuzungumza kwa usahihi. Si ni kusema tu kitu jinsi kilivyo na kusema mambo jinsi yalivyo? Je, hiyo si rahisi? Kilichokuwa kimenikera zaidi daima katika dunia hii walikuwa watu waliotia chumvi walipozungumza.” Kwa sababu ya hili, nilihisi imani kuu, nikifikiri kwamba sikuwa na shida katika hali hii. Lakini kupitia tu kwa ufunuo wa Mungu ndio niligundua kwamba, bila kuingia katika ukweli au kubadili tabia ya mtu, mtu hawezi kwa vyovyote kuzungumza kwa usahihi.

Wakati mmoja, niliona kwamba XX hakuwa na utunzaji na kujali kuelekea kwa hali ya kimwili ya wengine, kwa hivyo nilisema kwamba hakuwa na huruma. Baadaye, ni kupitia tu katika ushirika ndiyo nilielewa kwamba upendo wetu wa kweli kwa kila mmoja unajumuishwa kimsingi katika ushirikiano wa pamoja na usaidizi tunaoleta katika kuingia kwetu katika maisha. Wakati mwingine, nilipoona XX akitumia zaidi dola kadhaa wakati wa wajibu wake, nilisema kwamba mtu huyu alikuwa na asili ambayo ni yenye uroho sana. Ni baadaye tu ndiyo niligundua kwamba kuna tofauti kati ya watu wanaoonyesha tabia ya upotovu kidogo na kuwa na asili ya aina hiyo. Kisha kulikuwa na wakati mwingine ambapo kiongozi wangu aliniuliza kuhusu hali ya dada fulani. Kwa sababu nilikuwa na mawazo ya awali kumhusu dada huyu, hata ingawa nilijua wakati huo kwamba nilipaswa kutoa ripoti isiyoegemea upande wowote, bado sikuwa na budi bali kusema kwa ukali kuhusu upotovu ambao alikuwa amedhihirisha, na kukosa kusema hata neno moja kuhusu sifa zake nzuri. Wakati kulitokea mkengeuko au dosari katika kazi yangu mwenyewe, kila wakati ningeripoti hali hiyo kwa viongozi kisirisiri, nikificha ukweli wa mambo ya hakika ili kulinda sura na hadhi yangu. ...

Nikikumbwa na hali kama hizo, nilihisi kupigwa na bumbuwazi kabisa: Ni kwa nini moyo wangu ulikuwa tayari kuzungumza ukweli, kuzungumza kisahihi, lakini nilipofungua mdomo wangu singeweza kamwe kuzungumza bila upendeleo au kisahihi? Na swali hili, nilienda mbele ya Mungu kuomba na kutafuta uongozi. Baadaye, nilisoma hili katika mahubiri: “Kwa nini kamwe watu hawawezi kuzungumza sawasawa? Kuna sababu tatu za kimsingi: Sababu moja ni kwa sababu ya kiburi potovu cha watu. Jinsi wanavyoangalia vitu si sahihi, kwa hivyo pia wanazungumza kwa namna isiyo sahihi. Sababu ya pili ni kwamba ubora wa tabia yao una upungufu sana. Wanafanya mambo kiholela bila uchunguzi wowote wa utendaji na wanapenda kusikiliza uvumi, na matokeo kwamba wanaishia kuongeza kutia chumvi nyingi. Kuna sababu nyingine, ambayo ni kwamba watu wana tabia mbaya. Wanatumia mchanganyiko wa nia za binafsi wanapozungumza na, ili kutimiza malengo yao wenyewe, wanaunda uongo kuwadanganya wengine na kwa kupenda wanaubadilisha ukweli ili kuwadanganya watu. Hali hii imeundwa na mwanadamu, na lazima itatuliwe na ufuatiliaji wa ukweli na kwa kuijua hali kamili ya mtu mwenyewe” (Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu). Mara nilipoona maneno haya kwa ghafla niliona mwanga. Sasa niliona kwamba kuzungumza kwa usahihi hakukuwa rahisi nilivyokuwa nimefikiri. Kuna mambo mengi yanayoweza kuwafanya watu wazungumze visivyo sahihi, kama vile mitazamo ya watu kuwa yenye kiburi kimakosa, kutokuwa na ukweli, kukosa uhalisi au kuwa na tabia potovu. Kuhusu mimi mwenyewe, nilipowaona wengine wakionekana kufanya mambo kwa njia isiyoambatana na fikira zangu, nilikuwa mwepesi sana wa kuwaona kama wasio na huruma. Nilipowaona wengine wakionyesha tabia potovu kidogo, nilifafanua kama watu wa aina fulani. Nilipokuwa na maoni kumhusu mtu mwingine na kuripoti hali yake, niliupiga ukweli chuku na kutia chumvi. Katika kutenda wajibu wangu, kwa ajili ya maslahi yangu mwenyewe ningewadanganya wengine na kumhadaa Mungu. ... Je, hali hizi zote na maonyesho havikuletwa kwa sababu sikuwa nimeingia katika ukweli, kwa sababu mtazamo wangu ulikuwa wenye kiburi kimakosa, kwa sababu hakukuwa na mabadiliko katika tabia yangu? Ni sasa tu ndiyo ninaelewa: Mtu anapoelewa ukweli, aingie katika ukweli na kubadilisha tabia yake tu ndiyo anaweza kuakisi ukweli usioegemea upande wowote bila kukosea na kwa haki na ukweli kuangalia kila kitu kinachofanyika kwake. Bila kumiliki ukweli, mtu hawezi kubaini kiini cha suala na hivyo hawezi kuzungumza kwa usahihi. Akiishi ndani miili potovu, na tabia isiyobadilika na kufanya mambo kwa ajili ya nia binafsi na malengo ya mtu, ni vigumu hata zaidi kwa mtu kuweza kuzungumza kwa usahihi.

Ee Mungu! Natoa shukrani kwa ajili ya kutoa nuru Kwako na uongozi ulionifanya nigundue kwamba nilikuwa ujinga na mpuuzi kuwa na wazo kwamba ningeweza kuzungumza kwa usahihi kwa kutegemea uasili wangu mwenyewe na kutegemea ustahimilivu wangu mwenyewe! Kwamba ningeweza kujigamba kwa njia ya kiburi na upumbavu hivyo kunafichua zaidi kabisa jinsi sikutambua ni kwa kina kipi Shetani alikuwa amenipotosha. Kuanzia leo, ningependa kuweka juhudi zaidi katika kutafuta ukweli, kutoacha juhudi yoyote katika kufuatilia mabadiliko katika tabia yangu, kufanya mazoezi ya kuona watu na mambo kulingana na maneno ya Mungu, na kujitahidi hivi karibuni kuwa mtu mwaminifu ambaye anazungumza kwa usahihi na kufanya kazi kwa bidii.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Utajiri wa Maisha

Wang Jun Mkoa wa Shandong Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp