Historia ya Kweli ya Kazi ya Enzi ya Ukombozi

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, unajumuisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria ikiwa ya kwanza; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na Enzi ya Ufalme ya siku za mwisho. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu inatofautiana katika maudhui kulingana na kila enzi, lakini katika kila hatua kazi hii inafanywa kulingana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na hila ambazo Shetani anatumia katika vita Ninavyopigana dhidi yake. Kusudi ni kumshinda Shetani, kufunua hekima Yangu na uweza Wangu, kufichua hila zote za Shetani, na hivyo kuokoa jamii nzima ya wanadamu, ambayo inaishi chini ya nguvu za Shetani. Ni ili kufunua hekima Yangu na uweza Wangu, na kuweka wazi ubaya usiovumilika wa Shetani; hata zaidi ya hayo, ni ili kuruhusu viumbe walioumbwa kubainisha kati ya mema na mabaya, kujua kwamba Mimi ndimi Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, mpotovu, yule mwovu, na kuwawezesha kutofautisha, kwa uwazi kabisa, kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, na kile kilicho kikuu na kile kilicho duni. Ni ili kuwawezesha wanadamu wasio na ufahamu kunishuhudia kwamba si Mimi ninayewapotosha binadamu, na kwamba ni Mimi tu—Muumba—Ninayewaokoa binadamu, na kuwapa watu vitu ambavyo wanaweza kufurahia; ni ili kuwaruhusu wajue kwamba Mimi ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni kiumbe tu Niliyemuumba na ambaye baadaye alinisaliti. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu, na Ninafanya kazi hivi ili kufikia matokeo ya kuwawezesha viumbe walioumbwa wanishuhudie, waelewe nia Zangu, na wajue kwamba Mimi ndimi ukweli. Hivyo, wakati wa kazi ya awali ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, Nilitekeleza kazi ya sheria, ambayo ilikuwa kazi ya Yehova ya kuwaongoza watu. Katika hatua ya pili, Nilianzisha katika vijiji vya Yudea kazi ya awali ya Enzi ya Neema. Yesu anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alipata mwili, na kupigiliwa misumari msalabani, na Yeye pia Alianzisha Enzi ya Neema. Alikuja kusulubiwa na kukamilisha kazi ya ukombozi, na Alikuja kutamatisha Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Aliitwa “Jemadari Mkuu,” “Sadaka ya Dhambi,” na “Mkombozi.” Kutokana na hayo, kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova alianzisha Enzi ya Sheria, akiweka msingi—kituo cha mwanzo—kwa ajili ya kazi ya Mungu duniani, na kutoa sheria na amri. Hizi ni sehemu mbili za kazi Alizozitekeleza, na zinawakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ambayo Yesu alifanya katika Enzi ya Neema haikuwa kutoa sheria, bali kuzitimiza, na hivyo kuanzisha Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilikuwa imedumu kwa miaka elfu mbili. Yeye alikuwa mfungua njia, ambaye Alikuja ili kuanzisha Enzi ya Neema, lakini sehemu kuu ya kazi Yake ilikuwa katika ukombozi. Na hivyo kazi Yake pia ilikuwa ya sehemu mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake, na baada ya hapo Aliondoka. Na kuanzia hapo kuendelea Enzi ya Sheria ilifika mwisho na Enzi ya Neema ikaanza.

Kazi ambayo Yesu alifanya ilikuwa kulingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Jukumu Lake lilikuwa kuwakomboa binadamu, kuwasamehe dhambi zao, na hivyo tabia Yake kikamilifu ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, uchaji Mungu, ustahimilivu, rehema, na wema. Aliwaletea binadamu neema na baraka tele, na vitu vyote ambavyo watu wangeweza kufurahia. Aliwapa kwa ajili ya kufurahia kwao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo Wake, rehema Yake na wema Wake. Wakati huo, vitu vingi vya kufurahia ambavyo watu walikumbana navyo—hisia ya amani na usalama ndani ya mioyo yao, hisia ya faraja ndani ya roho zao, na wao kumtegemea Yesu Mwokozi—vilitokana na enzi walimoishi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alikuwa tayari amepotoshwa na Shetani, na hivyo kutekeleza kazi ya kuwakomboa binadamu wote kulihitaji neema tele, ustahimilivu na uvumilivu usio na kikomo, na hata zaidi ya hayo, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za binadamu, ili kuwa na matokeo. Kile ambacho binadamu waliona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi za binadamu: Yesu. Walichojua tu ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye rehema na ustahimilivu, na walichoona tu kilikuwa rehema na wema wa Yesu. Hili kikamilifu lilikuwa kwa sababu walizaliwa katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya wao kukombolewa, walipaswa kufurahia neema tele ambayo Yesu aliwapa. Ni kwa njia hiyo tu ndiyo wangeweza kufaidika, kuwawezesha kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na kuwapa fursa ya dhambi zao kulipiwa kupitia kufurahia kwao ustahimilivu na uvumilivu wa Yesu. Ni kupitia tu ustahimilivu na uvumilivu wa Yesu ndiyo walistahili kupokea msamaha na kufurahia wingi wa neema iliyotolewa na Yesu. Kama vile Yesu alivyosema: Sijakuja kuwakomboa wenye haki bali wenye dhambi, ili kuwaruhusu wenye dhambi wasamehewe dhambi zao. Kama, wakati Alipopata mwili, Yesu angeleta tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu hangewahi kupata fursa ya kukombolewa, na angesalia mwenye dhambi milele. Kama ingekuwa hivi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekomea katika Enzi ya Sheria, na Enzi ya Sheria ingerefushwa kwa miaka elfu sita. Dhambi za mwanadamu zingekuwa tu nyingi zaidi na nzito zaidi, na uumbaji wa binadamu ungekuwa bure. Watu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya sheria, lakini dhambi zao zingezidi zile za wanadamu wa kwanza walioumbwa. Kadiri Yesu alivyozidi kuwapenda wanadamu, Akiwasamehe dhambi zao na kuwaletea rehema na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walivyozidi kustahili kuokolewa na Yesu, na hivyo waliitwa kondoo waliopotea ambao Yesu aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hangeweza kuingilia kazi hii, kwa maana Yesu aliwatendea wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyomtendea mtoto mchanga kifuani pake. Hakuwakasirikia au kuwachukia, bali Alijawa faraja; Hakuwahi kuonyesha ghadhabu kuu miongoni mwao, bali Alivumilia dhambi zao na kufumbia macho upumbavu na ujinga wao, hadi kufikia kusema, “Wasamehe wengine saba mara sabini.” Hivyo ndivyo mioyo ya wengine ilivyoguswa na kurekebishwa na moyo Wake, na ni kwa njia hii tu ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi zao kupitia ustahimilivu Wake.

Ingawa Yesu katika kupata mwili Kwake hakuwa na hisia za kimwili hata kidogo, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, aliwaruzuku, aliwasaidia, na aliwategemeza. Alifanya kazi nyingi sana, Alivumilia mateso mengi sana, na Hakuwahi kutoa madai ya kupita kiasi kwa watu, lakini daima Alikuwa mvumilivu na mstahimilivu wa dhambi zao, kiasi kwamba watu wa Enzi ya Neema walimwita kwa upendo “Mwokozi Yesu anayependeka.” Kwa watu wa wakati huo—kwa watu wote—kile Yesu Alichokuwa nacho na alichokuwa, kilikuwa rehema na wema. Hakuwahi kukumbuka makosa ya watu, na jinsi Alivyowatendea haikuwahi kutegemea makosa yao. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, Yeye mara nyingi Aliwapa watu chakula tele ili waweze kula na kushiba. Aliwatendea watu wote waliomfuata kwa neema, Akiwaponya wagonjwa, akifukuza mapepo, na akiwafufua wafu. Ili watu wapate kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanywa kwa dhati na kwa ukweli, Alifikia hatua ya kufufua maiti inayooza, akiwaonyesha kwamba katika mikono Yake hata wafu wangeweza kurudi katika uzima. Yeye daima Alivumilia kimya kimya na akatekeleza kazi Yake ya ukombozi miongoni mwao kwa njia hii. Yaani, kabla Hajapigiliwa misumari msalabani, Yesu alikuwa tayari Amejitwika dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu. Kabla ya kusulubiwa, Alikuwa amefungua njia ya msalaba ili kuwakomboa wanadamu. Hatimaye, Alipigiliwa misumari msalabani, Akijitoa kama dhabihu kwa ajili ya msalaba, na Aliwapa wanadamu rehema Yake yote, wema Wake wote, na utakatifu Wake wote. Kwa binadamu, Yeye daima Alikuwa mvumilivu, Hakuwahi kuwa na kisasi, akiwasamehe dhambi zao, akiwahimiza kutubu, na Akiwafundisha kuwa na subira, ustahimilivu, na upendo, kufuata hatua Zake na kujitoa dhabihu kwa ajili ya msalaba. Upendo Wake kwa akina ndugu ulizidi upendo Wake kwa Mariamu. Kazi Aliyofanya ilikuwa na kanuni ya kuwaponya wagonjwa na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alienda wapi, Aliwatendea wote waliomfuata Yeye kwa neema. Aliwafanya maskini kuwa matajiri, vilema kutembea, vipofu kuona, na viziwi kusikia. Hata Aliwaalika wale wa hali ya chini kabisa, masikini wasio na kitu, wenye dhambi, kuketi kwenye meza moja pamoja na Yeye, Hakuwahi kuwadharau bali daima Alikuwa mvumilivu, hata Akisema: Mchungaji anapopoteza kondoo mmoja kati ya mia moja, atawaacha wale tisini na tisa ili amtafute yule kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata atafurahi sana. Aliwapenda wafuasi Wake kama vile kondoo jike anavyowapenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wapumbavu na wasio na ufahamu, na walikuwa wenye dhambi machoni Pake, na zaidi ya hayo walikuwa washiriki wa hali ya chini kabisa katika jamii, Yeye aliwachukulia wenye dhambi hawa—watu ambao wengine waliwadharau—kama mboni ya jicho Lake. Kwa kuwa Aliwatazama kwa upendeleo, Aliyatoa maisha Yake kwa ajili yao, kama vile mwanakondoo alivyotolewa kwenye madhabahu. Alitembea katikati yao kana kwamba Alikuwa mtumishi wao, akiwaruhusu wamtumie na kumchinja, Akiwatii bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mwokozi Yesu anayependeka, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwafundisha watu kutoka kwenye mimbari ya juu, Hakuonyesha rehema na wema, bali chuki na karaha. Hakufanya kazi nyingi miongoni mwa Mafarisayo, mara kwa mara tu Akiwafundisha na kuwakemea; katikati yao Hakufanya kazi ya ukombozi, wala Hakufanya ishara na maajabu. Aliwapa wafuasi Wake rehema Yake yote na wema Wake wote, Akivumilia kwa ajili ya wenye dhambi hawa hadi mwisho kabisa, Alipopigiliwa misumari msalabani, na Akiteseka kila udhalilishaji, hadi Alipokuwa amewakomboa binadamu wote kikamilifu. Hii ilikuwa jumla ya kazi Yake.

Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi katika dhambi milele na kuwa uzao wa dhambi, wazao wa mapepo. Hali ingeendelea hivi, ulimwengu mzima ungekuwa nchi ambamo Shetani anakaa, mahali pake pa makazi. Kazi ya ukombozi, hata hivyo, ilihitaji kuonyesha rehema na wema kwa wanadamu; ni kwa njia kama hizo tu ndiyo wanadamu wangeweza kupokea msamaha na hatimaye kustahili kufanywa kuwa kamili na kupatwa na Mungu kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea. Yesu asingalisulubiwa, kama Angaliponya tu wagonjwa na kutoa mapepo, basi watu wasingeweza kusamehewa dhambi zao kikamilifu. Katika miaka mitatu na nusu ambayo Yesu alitumia Akifanya kazi Yake duniani, Alikamilisha nusu tu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha, kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa mfano wa mwili wenye dhambi, kwa kukabidhiwa kwa yule mwovu, Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na kutawala hatima ya wanadamu. Ni baada tu ya Yeye kukabidhiwa mikononi mwa Shetani ndipo Alipowakomboa wanadamu. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, akidhihakiwa, akisingiziwa, na akitelekezwa, hata kufikia hatua ambapo Hakuwa na mahali pa kulaza kichwa Chake, bila mahali pa kupumzika, na baadaye Alisulubiwa, huku nafsi Yake yote—mwili mtakatifu na usio na hatia—ikipigiliwa misumari msalabani. Alivumilia kila aina ya mateso. Wale walio madarakani walimdhihaki na kumpiga mijeledi, na hata askari walimtemea mate usoni Mwake; lakini Alibaki kimya na akavumilia hadi mwisho, akatii bila masharti hadi kufa, ambapo Alikomboa binadamu wote. Hapo tu ndipo Alipokuja kufurahia mapumziko. Kazi aliyofanya Yesu inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria, wala si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo wanadamu wamepitia—Enzi ya Ukombozi.

Iliyotangulia: Kazi katika Enzi ya Sheria

Inayofuata: Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp