Wewe U Mwaminifu kwa Nani?

Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho na kila dakika inayopita. Mnapaswa kutumia muda wenu vizuri ili muweze kujinufaisha, ili msije kuishi maisha haya bure. Pengine mnajihisi kukanganyikiwa mnaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yenu si vile tu mlivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyenu vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho. Hivi ndivyo mtakavyonifidia mwishowe, ambacho ni kitu ambacho Sijawahi kutarajia. Sitamani kuzungumza kinyume cha ukweli, kwa maana mmenivunja moyo sana. Pengine hampendi kuiachia mada hapo na hutaki kuukabili ukweli, lakini ni lazima niwaulize swali hili: Kwa miaka hii yote, mioyo yenu imejawa na nini? Mioyo yenu inamwamini nani? Usiseme kwamba swali Langu limekuja ghafla sana, na usiniulize kwa nini Nauliza swali kama hilo. Mnapaswa kujua hili: Ni kwa sababu Ninawafahamu vizuri, ninawajali sana, na Ninajitolea moyo Wangu sana kwa kile mnachofanya, ndio maana Ninawauliza kwa kurudiarudia na kubeba taabu isiyoelezeka. Hata hivyo, malipo Yangu yamekuwa ni kupuuzwa na kukataliwa kusikostahimilika. Hivyo mmekuwa na ajizi sana juu Yangu; Ninawezaje kutojua kitu kuhusu hilo? Kama mnaamini kwamba hili linawezekana, inathibitisha ukweli zaidi kwamba hamnitendei wema kabisa. Kisha Ninawaambia kwamba mnajidanganya nyinyi wenyewe. Nyinyi nyote ni werevu sana kiasi kwamba hamjui kile mnachofanya; sasa mtatumia nini ili kunipatia ufafanuzi?

Swali muhimu sana kwangu ni mioyo yenu inamwamini nani. Pia Ningependa kila mmoja wenu afikiri vizuri na kisha ajiulize uaminifu wake uko kwa nani na anaishi kwa ajili ya nani? Pengine hamjawahi kuliangalia swali hili kwa makini, hivyo nitawapatia jibu lake.

Wale wenye kumbukumbu nzuri wataukubali ukweli huu: Mwanadamu anaishi kwa ajili yake mwenyewe na ni mwaminifu kwake mwenyewe. Siamini kwamba jibu lenu ni sahihi kabisa, kwa maana kila mmoja wenu anaishi maisha yake, kila mmoja wenu anapambana katika dhiki yake. Kwa hivyo, kile mnachokuwa waaminifu kwacho ni watu mnaowapenda, na vitu vinavyowapendeza, na wala nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu wenyewe. Kwa sababu kila mmoja wenu anaathiriwa na watu, matukio, na vitu vinavyowazunguka, kimsingi nyinyi si waaminifu kwa nafsi zenu. Nasema maneno haya siyo kwa sababu ya kuunga mkono ninyi kuwa waaminifu kwa nafsi zenu, bali kufichua uaminifu wenu kwa kitu chochote kile. Maana kwa miaka yote hii Sijawahi kupokea uaminifu kutoka kwa mtu yeyote kati yenu. Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. Mnapokuwa na hamu ama shauku na kitu chochote kile Mnachokipenda, siku zote mnakuwa ni wakati ambapo mnanifuata, au hata wakati mnaposikiliza maneno Yangu. Hivyo nasema, mnatumia uaminifu ninaowataka muonyeshe, kuwa badala yake waaminifu na kufurahia “vipenzi” wenu. Ingawa mnaweza kutoa sadaka ya kitu kimoja au vitu viwili kwa ajili Yangu, hakuwakilishi vitu vyenu vyote, na haionyeshi kwamba ni Kwangu ambako uaminifu wako uko kwa kweli. Mnajiweka wenyewe katika shughuli ambazo mnazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake. Kwa maana kile ambacho mnakuwa waaminifu kwacho, hujawahi kuhisi kuchoshwa au kukerwa nacho, badala yake, mnatamani kuwa na kiasi kikubwa zaidi na ubora wa vitu ambavyo ninyi mu waaminifu kwavyo na hamjawahi kukata tamaa. Mimi mwenyewe na maneno Yangu daima hutupwa pembeni katika masuala ya vitu mnavyovipenda. Na hamna namna isipokuwa kuyaweka mwisho; wengi hata wanaondoka sehemu ya mwisho kwa ajili ya kuwa waaminifu kwa kitu ambacho hawajakigundua bado. Hawajawahi kuniweka mioyoni mwao kwa kiwango chochote kile. Pengine mtafikiri kwamba ninahitaji mambo mengi sana kutoka kwenu au Ninawahukumu kimakosa, lakini je, mmeshawahi kufikiri kuhusu ukweli huu kwamba mnapotumia muda kwa furaha pamoja na familia yenu, hujawahi kuwa mwaminifu kwangu hata mara moja? Wakati kama huu, hii haiwaumizi? Mioyo yenu inapojawa na furaha kwa kupokea malipo kwa kazi zenu, haiwavunji moyo kwamba hamjajitweka kwa ukweli wa kutosha? Ni lini mmewahi kulia kwa kukosa idhinisho langu? Mnaitesa akili yenu na kupata maumivu makubwa kwa ajili ya watoto wenu, lakini bado hamjaridhika, bado mnaamini kwamba hamjaweka jitihada za kutosha kwao, kwamba hamjatumia nguvu zenu zote. Lakini Kwangu, mmekuwa ajizi na wa kutojali, mkiniweka tu katika kumbukumbu zenu na wala Sidumu ndani ya mioyo yenu. Kujitolea Kwangu na jitihada zangu daima hupita bila nyinyi kuzihisi, na wala hamjawahi kuweka jitihada ili muweze kuelewa. Nyinyi hutafakari kidogo tu na kuamini kwamba hiyo itatosha. “Uaminifu” wa aina hii sio ule ambao Nimekuwa nikiutazamia, bali ni ule ambao umekuwa machukizo Kwangu kwa muda mrefu. Hata hivyo, licha ya kile Ninachokisema, mtaendelea kukubali kitu kimoja tu au vitu viwili na kushindwa kukikubali kwa ukamilifu, kwa maana nyote “mnajiamini” sana, na siku zote mnachagua kipi mtakachokikubali kutoka katika maneno Niliyoyasema. Kama bado mko hivi, Nina njia katika akiba za kukabiliana na kujiamini kwenu, na Nitazitumia ili muweze kuyatambua maneno Yangu yote kuwa ni kweli na sio upotoshaji wa ukweli.

Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba[a] sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Si ndivyo ilivyo? Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika. Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni[b] kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa. Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu? Kwa wakati wa sasa, chaguo lenu ni nini? Mtayakubali maneno Yangu, au yatawachosha? Siku Yangu imewekwa wazi kabisa mbele ya macho yenu, na kile mnachokiona ni maisha mapya na mwanzo mpya. Hata hivyo, ni lazima niwaambie kwamba huu mwanzo mpya si mwanzo wa kazi mpya iliyopita, bali ni mwisho wa ya kale. Yaani, hili ni tendo la mwisho. Ninaamini nyote mtaelewa kitu ambacho si cha kawaida kuhusu mwanzo huu mpya. Lakini siku moja hivi karibuni, mtaelewa maana halisi ya huu mwanzo mpya, kwa hivyo hebu sote tuipite na kuikaribisha tamati inayofuata! Hata hivyo, kitu ambacho Ninaendelea kutofurahishwa nacho ni kwamba pale mnapokabiliwa na mambo ambayo si ya haki na mambo ya haki, daima mmekuwa mkichagua chaguo la kwanza. Lakini hayo yote yako katika maisha yenu ya zamani. Pia Ninatumai kuyasahau yale yote yaliyotokea katika maisha yenu ya zamani, kitu kimoja baada ya kingine, ingawa hili ni gumu sana kufanya. Lakini bado nina njia nzuri sana ya kulitimiza. Acha maisha ya baadaye yachukue nafasi ya maisha ya zamani na kuacha kivuli cha maisha yenu ya zamani kiondolewe badala ya utu wenu halisi wa leo. Hii ina maana kwamba nitawasumbua tena ili uweze kufanya maamuzi kwa mara nyingine tena na tutaona kabisa nyinyi ni waaminifu kwa nani.

Tanbihi:

a. Matini ya asili haina kauli “kuelewa kwamba.”

b. Kurudi ufuoni: nahau ya Kichina, ikiwa na maana kwamba “mtu kuacha njia zake za uovu.”

Iliyotangulia: Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Inayofuata: Juu ya Hatima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp