29. Mwanga ni wa Vuguvugu Wakati wa Kupenya Shimo
Kama tu ndugu wengine ambao wana kiu ya kurudi kwa Bwana Yesu, mimi pia naendelea kutamani sana Bwana wetu kwa hamu arudi kutupokea katika ufalme wa mbinguni karibuni ili kwamba tuweze kufurahia baraka zake. Siku moja katika mwezi wa Novemba mwaka 2006 nilisikia hatimaye habari ya kurudi kwa Bwana. Kupitia kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu na kupitia kushiriki kwenye subira kuhusu na kushuhudia kazi ya Mungu katika siku za mwisho kutoka kwa ndugu, niligundua hatimaye kwamba Mwenyezi Mungu mwenye mwili ni kurudi kwa Bwana Yesu. Kwa hiyo, kwa hiari nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.
Katika mkutano, Dada Yang aliniambia kwa sauti nzito: “Sasa hivi kuna ndugu wengi ambao, baada ya kukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, wanakumbana na baadhi ya usumbufu na majaribu ya Shetani. Wengine wanadanganywa na uongo wa CCP, wengine wanakumbana na usumbufu na vitisho vya wahubiri na wazee wa kanisa, wengine wanalazimishwa ama kuzuiwa na familia zao, na washirika wa familia wa wengine wanapitia ugonjwa au misiba. Hizi ni hila za Shetani kujaribu kutuzuia dhidi ya kurudi kwa Mungu. Sote tayari tunaelewa kwamba kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu huanza kwa nyumba ya Mungu, na hii ni hatua ya mwisho ya Mungu katika kuwaokoa wanadamu. Anafanya kila kitu Anachoweza kufanya kumwokoa mwanadamu, na Shetani daima anatenda hila na usumbufu wake kwetu ili kutuzuia dhidi ya kuja mbele ya Mungu na kupokea wokovu Wake. Sasa hivi mapigano ambayo yanafanyika katika dunia ya kiroho yanakuwa makali zaidi na zaidi, kwa hivyo tunahitaji kwa dharura kujiandaa na ukweli na kuwa na ujuzi wa utambuzi ili kutodanganywa wakati wowote hila za Shetani zinatupata na kumshuhudia Mungu. Sasa, hebu tusome fungu kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu.” Hivyo, nilichukua kitabu cha neno la Mungu na kusoma kwa makini fungu lifuatalo: “Huku Mungu akifanya kazi, Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake; vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na mipaka. Shetani amempotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa; siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema, Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya ushawishi wote wa giza. … Mungu ni mwenye busara kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani kwa mbali. Hivyo basi, Niliwahi kutaja awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa Shetani. Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama zozote zingine za kutumia!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo). Dada Yang aliniambia kwa upole: “Kupitia neno la Mungu tunaweza kuona kwamba katika kazi ya usimamizi ya Mungu Shetani anafuata nyuma kwa karibu kila hatua ya kazi ya Mungu. Mungu yuko mbele akitekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu, na Shetani yuko nyuma, akisumbua na kuiharibu. Daima anapigania mwanadamu na Mungu, na hii ni kweli hasa wakati wa hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu katika kumwokoa mwanadamu kikamilifu. Wakati huu Shetani anafanya hata zaidi kula kitu anachoweza, akinyonya watu na vitu vya kila aina kutusumbua na kutuzuia dhidi ya kukubali na kutii kazi ya Mungu. Ni lengo lenye kustahili dharau la Shetani kuweka mwanadamu mbali na Mungu na kumfanya mwanadamu amkane Mungu na kumsaliti Mungu, hivyo kupoteza wokovu wa Mungu. Lakini hekima ya Mungu inatekelezwa kwa kujibu ulaghai wa Shetani. Anaweza kutumia usumbufu wa Shetani kutuleta kwa ufahamu wa kazi Yake na hekima Yake na uweza, na pia kuturuhusu kuona wazi uovu na ubaya wa Shetani. Kwa hivyo, bila kujali kile kinachofanyika katika siku za baadaye, sote lazima tuombe kwa Mungu na kumtegemea Mungu na kutafuta ukweli, na ni lazima tubaini ulaghai wa Shetani ili kwamba tuweze kumshuhudia Mungu. Ni kama tu majaribu ambayo Ayubu alipitia. Alimshuhudia Mungu, kumsababisha Shetani kukimbia kwa fedheha….” Baada ya kusikia Dada Yang akiniambia hili, nilijibu kwa imani kamili: “Ndiyo, tunamwamini Mungu wa kweli. Tukimtegemea Mungu basi hatuna chochote cha kuogopa: nikikabiliwa na majaribu ya Shetani, bila shaka nitasimama kwa upande wa Mungu.”
Siku moja si muda mrefu baada ya hili wakati nilikuwa nimemaliza kueneza injili nilikuwa tena kwa mlango wangu wa mbele wakati jirani yangu alikuja kwangu kwa kasi akipunga mikono yake, akisema: “Umekuwa wapi? Kitu kikubwa kimefanyika! Leo marafiki wa mtoto wako wa kiume Liu na Hu walikuja kuazima lori lako, na Hu aliliweka moja kwa moja katika gia ya tano na ghafla lilianza kusonga na kamba ya chuma ilitoa sauti kubwa ya kuvunjika na kukatika na kumgonga Hu panjani mwake, na damu mara moja ilianza kufoka nje. Tayari amekimbizwa hospitalini….” Ghafla akili yangu ikawa tupu, na nikakimbia nyumbani mwangu kumwomba Mungu: “Ee Mungu! Sielewi mapenzi Yako. Mbona hili limenifanyikia ghafla? Tafadhali nipe nuru….” Baada ya kuomba nilifikiria ushirika wa Dada Yang kuhusu ukweli wa mapigano ya kiroho. Kisha nikaelewa. Shetani alitaka tu kutumia mambo haya yasiyofaa kunishambulia ili kwamba ningemshuku Mungu, kumlaumu Mungu na kumkana Mungu. Haya kwa kweli ni mapigano ya kiroho! Ilikuwa wakati huu ambapo nilifikiri kuhusu kitu kingine ambacho Mungu alikuwa amesema: “Ikiwa unaweza kusimama upande wa Mungu anapopigana na Shetani, na usimgeukie Shetani, basi utakuwa umefanikisha mapenzi ya Mungu, na utakuwa umesimama imara katika ushuhuda wako” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Maneno haya ya Mungu yalinijaza na imani, na niliwaza mwenyewe: Shetani, bila kujali jinsi unavyonisumbua sitadanganywa na hila zako, sitamlaumu Mungu ama kumshuku Mungu, nitasimama kwa upande wa Mungu, nitamfuata Mwenyezi Mungu vizuri. Punde nilipoelewa mapenzi ya Mungu nilihisi thabiti zaidi katika moyo wangu.
Lakini Shetani hakuwa tayari kukubali kushindwa, na bado hunisumbua siku zote kupitia watu na vitu. Wakati Hu alilazwa hospitalini familia yake iliweka majukumu yote kwa familia yangu. Walinitaka kulipia gharama zote za tiba. Niliendelea kujaribu kujadiliana na wao, nikiwaambia kwamba nilikuwa tayari kulipa nusu, lakini wakati huo wote hawangekubaliana na mimi. Baada ya wiki tatu Hu tayari alikuwa amepona, lakini bado hakuwa ameondoka hospitalini. Hili lilifanywa kwa makusudi ili kupokonya pesa kutoka kwa familia yangu. Kisha siku moja Hu alisema: “Lori ni lako, kwa hivyo gharama zote zinapaswa kulipwa na wewe.” Mke wa Hu pia alisimama na kusema kwa sauti kubwa: “Hiyo ni sahihi! Kwa kuwa ni lori lako ambalo lilihusika katika ajali hiyo basi unapaswa kulipa gharama zote….” Nikiwa nimesimama hapo na wao wakinisumbua bila mwisho nilianza kua na hasira sana. Nilikuwa nimepatwa katika suala hili pasipo kutaka. Nilihisi uchungu fulani, nilikuwa mwenye kuhangaika na wasiwasi, na sikutaka kuwaongelesha tena, kwa hivyo bila furaha nilitoka kwa chumba hicho. Nilipofika chini niliwaza mwenyewe: Mimi ni mwamini wa Mungu; wakati vitu kama hivi hunifanyikia sipaswi kuwa na hasira kwa njia hii, napaswa kuaminia swala hili mikononi mwa Mungu. Nahitaji kumtegemea Mungu. Niliporudi nyumbani nilifungua kitabu cha maneno ya Mungu na kuona maneno yafuatayo ya Mungu: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. …Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli). Nilipokuwa nikisoma maneno haya nilifikiri nyuma kwa ile siku ambapo nilijigamba mbele ya Dada Yang kwamba kwa hakika ningesimama kando ya Mungu wakati wowote majaribu yatanifikia. Sikuwa nimefikiri kwamba wakati Shetani aling’ang’ana kunisumbua, singeweza kumshuhudia Mungu, akili yangu daima ilishughulika, kwa hivyo singetafuta mapenzi ya Mungu mbele Yake kwa utulivu. Badala yake, nilikuwa nikifikiri nini kilikuwa sahihi na nini hakikuwa sahihi. Nilikuwa nimedanganywa na hila za Shetani. Nilikuwa nimetumbukia gizani. Haikuwa hadi nilipomaliza kufikiri kuhusu vitu hivi ambapo ningeweza kuona hatimaye jinsi kwa kweli Shetani ni mbaya na mwovu. Alikuwa ametumia jambo hili kunisumbua, alikuwa amefikiri kila kitu angeweza kufanya kunifanya nikane ukuu wa Mungu, kunitega katika mahali ambapo nilipata hasira nikifikiri kuhusu kile kilikuwa sahihi na kile hakikuwa sahihi nikifikiri kile ambacho kingeleta manufaa kiasi kwa mwili wangu, na hata zaidi alitaka kutumia vitu hivi kunifanya nimkane Mungu Mwenyezi na kumsaliti Mungu Mwenyezi. Lakini sitadanganywa na hila za Shetani. Niko tayari kumtegemea Mungu, na kuleta vitu hivi mikononi mwa Mungu. Iwapo Hu angetoka hospitalini au la, ni kiasi gani cha pesa ingenibidi kutumia mwishowe, nilikubali kwamba vitu hivi vingepangwa na mkono wa Mungu, na bila kujali matokeo, ningekuwa tayari kutii. Punde nilipokuwa nimeelewa mapenzi ya Mungu, punde nilipokuwa tayari kumshuhudia Mungu, bila kutarajia nilishuhudia mojawapo ya matendo ya ajabu ya Mungu siku iliyofuata. Mungu alikuwa ameamsha kijana mdogo kuenda kwa chumba cha hospitali cha Hu na kumkaripia: “Siwezi kuvumilia kumwangalia mtu kama wewe, mtu ambaye anadhulumu watu wazuri, na mtu ambaye anapokonya mtu mwingine pesa yake. Ingekuwa mimi singekupa hata senti moja.” Mtu mwingine katika chumba pia aliingilia mazungumzo: “Hiyo ni sahihi, ni yeye aliyeingia ndani ya lori, na sasa anataka pesa ya mtu huyu, jambo lisilo la busara vipi!” “Ndiyo! Yule aliyeomba lori anapaswa pia kulipa pesa fulani! Hapaswi kumfanya mwenye lori hilo alipie kila kitu!” Baada ya Hu kusikia hili aliinamisha kichwa chake na hakusema neno. Siku tatu baadaye Hu alitoka hospitalini. Nilijua ndani ya moyo wangu kwamba nyuma ya matukio haya yaliyokuwa yakitokea ilikuwa Mungu ambaye alikuwa amenifungulia njia hii.
Baada ya kupitia hili, niliweza kuona uovu na kustahili dharau kwa Shetani. Alikuwa amewatumia watu na vitu ambavyo nilijua kunisumbua na kunishambulia katika jaribio la kunifanya kulalamika kwa Mungu na kumlaumu na kujiweka mbali na Yeye kwa sababu ya ukweli kwamba ningepoteza pesa kiasi, na alitaka niishi katika mateso. Wakati uo huo, ningeweza kuona pia kwamba wakati niliacha kufikiria faida na hasara zangu za mwili, nilipomtegemea Mungu kupitia imani yangu Kwake, niliposimama kwa upande wa Mungu, basi Mungu alitumia maneno ya wasioamini kunifungulia njia, kumlazimisha Shetani kukimbia kwa fedheha. Hili lilinipa fursa ya kuona mamlaka ya Mungu ambayo yanahamasisha kutawala vitu vyote. Ni kama tu ilivyoandikwa katika neno la Mungu: “Mimi Nitawahamasisha wote kunitumikia Mimi, na zaidi ya hayo, Mimi Nitafichua nguvu Yangu, ili kila mtu aweze kuona kwamba katika ulimwengu dunia wote hakuna kitu hata kimoja ambacho hakimo mikononi mwetu, hakuna mtu hata mmoja ambaye hayuko katika huduma Yetu, na hakuna ufanikishaji hata mmoja ambao haujatekelezwa kwa ajili yetu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 119). Ninavyozidi kusoma neno la Mungu ndivyo ninavyoona zaidi kwamba Mungu ni mwenyezi, kwamba Mungu ni wa ajabu. Naona sasa kwamba vitu vyote vimo mikononi mwa Mungu, na niko tayari sasa kupitia kazi zaidi ya Mungu katika chochote kitakachofanika kufuatia, na nitamtegemea Mungu ili kutodanganywa tena na majaribu ya Shetani.
Baada ya mwezi majaribu ya Shetani yalinipata tena. Siku moja, binti yangu ambaye alikuwa ameolewa karibuni alirudi nyumbani ambapo alizirai ghafla kwa mlango wa mbele. Jirani yangu alimbeba na kumsaidia kuingia nyumbani. Nilipoona kwamba binti yangu alikuwa mgonjwa nilifikiri mara ya kwanza kwamba ilikuwa homa ya kawaida tu, sikuitilia maanani sana. Bila shaka sikuwa nikitarajia kwamba nusu usiku ghafla angeanza kutetemeka mwili mzima. Niliogopa na sikujua cha kufanya. Nilimchukua tu kwa haraka na kumshikilia kwa kifua changu, na baada ya muda mfupi alionekana kuwa na afueni kiasi. Asubuhi iliyofuata binti yangu aliniambia: “Mama, nenda ukatekeleze wajibu wako, Nitakuwa sawa.” Nilimwomba Mungu kwa kimya: “Ewe Mungu! Vitu vyote vimo mikononi mwako, kwa hivyo nakuaminia bini yangu….” Baada ya hili nilimgeukia binti yangu na kusema: “Jing, unahitaji kumwomba Mungu zaidi na kumtegemea Mungu, kwa kuwa Yeye ni msaada wa nguvu tunaohitaji.” Baada ya kumsihi binti yangu kuhusu hili nilienda kutekeleza wajibu wangu. Sikutarajia kwamba baada ya siku mbili niliporudi ningempata binti yangu katika kitanda cha hospitali bila fahamu. Binti mkwe alinigeukia na kuniambia kwa sauti ya huzuni: “Mama, baada ya wewe kuondoka, ugonjwa wa Jing ulianza kuwa hatari sana. Wakati daktari alimchunguza, alisema alikuwa na hemoraji ya ubongo na kwamba alihitaji upasuaji wa fuu la kichwa. Lakini kwa sababu wewe na mume wake hamjakuwa hapa siku hizi mbili zilizopita, hakukuwa na mtu wa kuidhinisha upasuaji wake kwa kuweka sahihi, na sasa tumepoteza wakati wa upasuaji. Nilisikia pia daktari akimwambia mama mkwe wa Jing kwamba hali yake haikuwa nzuri na kwamba hata kama angeamka angekuwa katika hali ya kuishi kama mmea bila kutumia akili.” Niliposikia hili ilihisi kama kwamba kisu kilikuwa kimesokotwa moyoni mwangu, na machozi yalianza kutoka machoni mwangu. Singeweza tu kukubali hili kama ukweli. Kwa hivyo nilishikilia matumaini kidogo na kuenda kuongea na mtaalamu, lakini alitikisa kichwa chake alipokuwa akiniambia: “Tumetumia dawa zote ambazo tungeweza kutumia, tumejaribu kwa bidii kiasi tungeweza, matokeo bora kabisa yanayowezekana ni kwamba aamke katika hali ya kuishi kama mboga bila kutumia akili.” Baada ya kusikia maneno ya daktari huyu nilihisi kwamba hata mbinguni ilikuwa imeanguka kwa kishindo. Ilihisi kama niliishi katika mateso yasiyoisha…. Baadaye, wakati mwana mkwe wangu aliwasili na kuona hali ambayo binti yangu alikuwa, sio tu kwamba hakushughulika kuhusu iwapo angeishi au kufa, lakini pia alinigeukia na kuonyesha ukosefu wa ubinadamu kabisa akiniambia kurudisha pesa ya uchumba ambayo alikuwa ametupa wakati wa ndoa. Siku hiyo njia nyumbani kutoka hospitali ilionekana kuwa ndefu sana, nilikuwa nafsi iliyopotea nikizurura njia hiyo. Ilihisi kama nilikuwa nikitembelea shimo ndefu la giza ambapo singeweza kuona mwanga wowote mbele yangu.
Niliporudi nyumbani nilikuwa nikihisi kuvunjika moyo na kwa unyonge nikafungua kitabu cha neno la Mungu na kusoma maneno yafuatayo: “Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, na bila kukoma wanatafuta maiti za wanadamu zinazoweza kuliwa. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya utunzaji Wangu na ulinzi. Kamwe msiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10). “Unapokabiliwa na mateso ni lazima uweze kuweka kando masilahi ya mwili na usifanye malalamiko dhidi ya Mungu. Wakati Mungu anajificha kutoka kwako, ni lazima uweze kuwa na imani ya kumfuata Yeye, kudumisha upendo wako wa awali bila kuuruhusu ufifie au kutoweka. Haijalishi anachofanya Mungu, ni lazima utii mpango Wake na uwe tayari kuulaani mwili wako mwenyewe badala ya kulalamika dhidi Yake. Wakati unakabiliwa na majaribu, lazima umridhishe Mungu, ingawa unaweza kulia kwa uchungu au uhisi kusita kuhusu kuacha kitu unachopenda. Huu tu ndio upendo wa kweli na imani” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji). Nilipokuwa nikisoma maneno haya ya Mungu nilikumbuka matukio ambayo yalikuwa yamefanyika karibuni, na kwa kweli ningeona dharau, uovu na ukatili wa Shetani. Alitaka kunitoa mikononi mwa Mungu, alitaka kuteketeza roho yangu. Alikuwa akitenda njama zake janja dhidi yangu kila mahali angeweza ili kunisumbua na kunishambulia. Kwanza, nilipokonywa na wengine, na kwa kuwa nilipoteza pesa niliishi katika mateso; wakati huu Shetani alitumia binti yangu mpendwa kunijaribu tena, alijaribu kutumia ugonjwa wa binti yangu kunifanya kulalamika kwa Mungu, kumkana Mungu na kumsaliti Mungu, ili kwamba ningepoteza wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Hizi zote zilikuwa njama janja za Shetani. Ilikuwa tu kama majaribu ambayo Ayubu alikumbana nayo wakati wake. Katika usuli kulikuwa na mapigano, na Shetani alitaka Ayubu kumwacha Mungu na kumkana Mungu kwa kumfanya apoteze utajiri wake na watoto wake, lakini Ayubu kamwe hakulalamika kwa Mungu. Badala yake, alisifu jina la Mungu, kusababisha Shetani kukimbia kwa fedheha na kutoa ushuhuda mzuri na mkubwa sana kwa Mungu. Ingawa mwili wangu ni dhaifu pia mimi lazima nibaini njama janja za Shetani na kusimama kando ya Mungu. Mungu anasema: “Na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani.” “Wakati unakabiliwa na majaribu, lazima umridhishe Mungu, ingawa unaweza kulia kwa uchungu au uhisi kusita kuhusu kuacha kitu unachopenda. Huu tu ndio upendo wa kweli na imani.” Mungu anatumia mashambulizi ya Shetani kukamilisha imani na ibada yangu kwa Mungu. Maisha na kifo cha mwanadamu yote yako mikononi mwa Mungu. Nilipofikiri hili, nilipiga magoti sakafuni huku machozi machungu yakitiririka usoni mwangu, na nikamwomba Mungu: “Mwenyezi Mungu! Majaliwa ya mwanadamu yako mikononi Mwako, niko tayari kuleta binti yangu mikononi Mwako. Lakini Usipokubali hili basi binti yangu hatakufa ilimradi pumzi moja imo mwilini mwake, na kama ni jinsi daktari alivyosema basi atakuwa akiishi kama mmea bila kutumia akili, basi sitakulaumu, bado nitakufuata.”
Usiku wa manane sana nilikuwa nikiketi kichwani mwa kitanda cha hospitali cha binti yangu hadi sikuwa na uhakika nilisinzia saa ngapi. Niliamka kama nimetunduwaa kusikia binti yangu akisema, “Mama, mama, nahitaji maji.” Moyo wangu uliruka niliposikia sauti ya binti yangu, na nikasimama kwa mruko. Nilisugua macho yangu na kumkodolea macho. Mikono ya binti yangu ilikuwa ikisonga na macho yake yalikuwa wazi. Hii mara moja ilinijaza na hisia hadi kiwango ambacho sikujua cha kusema, na yote ambayo ningeweza kufanya ilikuwa kuendelea kuropoka: “Ee! Mungu! Ee! Mungu! ...” Mtu mwingine katika wadi pia alisema kwa mshangao: “Ee! Ni miujiza! Ni vipi amepata afueni ghafla hivyo?” Nilitoa kwa haraka tabasamu isiyozuilika. Niliona kwamba hili kwa kweli ilikuwa Mungu akitawala kudura ya mwanadamu. Matendo ya Mungu kwa kweli ni ya ajabu. Ilikuwa ni Mungu ambaye alimwokoa binti yangu. Baada ya siku tatu, binti yangu alipata afya yake kwa miujiza, na alionekana kama mwanadamu wa kawaida tu tena. Baada ya kupitia mateso haya kupitia mikono ya Shetani niliweza kuona kwamba mapigano yaliyofanyika katika dunia ya kiroho yalikuwa makali sana, na ningeweza kuona wazi uovu mbaya na ukatili mwovu wa Shetani. Wakati uo huo nilikuwa na ufahamu bora zaidi wa mapenzi ya Mungu. Mungu alikuwa ameruhusu majaribu haya kunijia ili kwamba Angeweza kuniokoa na kunifanya kamili vyema zaidi, kwa kuwa hili liliniruhusu kutambua uweza na hekima ya Mungu, na pia liliniruhusu kuona mamlaka na utawala wa Mungu. Hili lilikamilisha imani, ibada, na utii wangu kwa Mungu. Aliniokoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani, akiruhusu maisha yangu kukua. Mungu kwa kweli ni wa kupendeka sana!
Baadaye nilisoma fungu lifuatalo kutoka neno la Mungu: “Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni ili kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufichua ubovu wa Shetani usiovumilika. Aidha, ni ili kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kujua, kwa uhakika kabisa tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, kilicho kikuu na kilicho cha aibu. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wataweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Bwana wa viumbe—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Ninayeweza kumpa mwanadamu vitu kwa ajili ya raha yake; na atapata kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na Shetani ni mmoja tu wa viumbe niliowaumba na ambaye baadaye alinigeuka” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi). Kupitia maneno haya ya Mungu nilipata ufahamu bora zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ningeweza kuona kwamba kila kitu ambacho Mungu hufanya ni wokovu na upendo kwa mwanadamu. Nilipokumbuka majaribu yote ambayo nilipitia, ingawa kweli nilistahimili taabu fulani, pia nilipata vitu vingi. Kupitia uzoefu huu niliona kwamba Shetani aliendelea kutumia watu na vitu kando yangu kunisumbua, lakini wakati huo wote nilikuwa na Mungu kando yangu. Alitumia maneno Yake kunipa nuru na kuniongoza, ili kwamba ningeweza kutofautisha vitu vizuri zaidi. Alinipa njia ya kufuata, akanipa imani na nguvu, ili kwamba ningeweza kuwa imara nyakati za ubaridi na udhaifu. Kila hatua ya njia niliweza kujinasua kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani na kushuhudia matendo ya Mungu ya ajabu. Katika maisha yangu nilikua sugu zaidi kupitia uzoefu huu. Baada ya kupitia uzoefu huu nilihisi kwamba sihitaji kuogopa usumbufu na mateso haya kutoka kwa Shetani tena, kwa sababu nina Mungu kando yangu. Ilimradi tumtegemee Mungu na tusiache neno la Mungu, ilimradi tuna imani kwa Mungu, basi Mungu atatulinda kwa ushindi dhidi ya njama janja na mashambulizi ya Shetani, na tutaishi tukiwa tumelindwa chini ya macho angalifu ya Mungu. Sasa mimi ni wa kusadiki sana hata kwa uthabiti zaidi kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu. Yeye ni Bwana wangu, Mungu wangu! Pia natambua kwamba sisi ni viumbe, bila kujali iwapo tunapokea baraka ama kuvumilia taabu, daima tunapaswa kumtii Mungu na kumwabudu Mungu. Nasimama hapa na uamuzi wangu thabiti: Moyo wangu umedhamiria kumfuata Mwenyezi Mungu hadi mwisho wa njia!