27 Umeme Uwakapo Kutoka Mashariki

1 Watu wote wanapotilia maanani, wakati vitu vyote vinafanywa upya na kuhuishwa, wakati kila mtu anamtii Mungu bila shaka, na yuko tayari kubeba jukumu zito la mzigo wa Mungu—hapa ndipo wakati umeme wa mashariki unatoka, ukiangaza yote kutoka Mashariki hadi Magharibi, ukiyatisha yote ya ulimwengu na ujaji wa mwanga huu; na wakati huu, Mungu tena huanza maisha Yake mapya. Ambayo ni kusema, wakati huu Mungu huanza kazi mpya duniani, akitangaza kwa watu wa ulimwengu wote kwamba “Wakati umeme unatoka Mashariki—ambao pia ni wakati hasa Naanza kutamka maneno Yangu—umeme unapotoka, mbingu yote inaangazwa, na mabadiliko yanatokea kwenye nyota zote.”

2 Kutoka wakati ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe huanza, hadi wakati Yeye huanza kufanya kazi, mpaka wakati uungu huanza kushika madaraka makuu pande zote duniani—huu ni mwale unaong’aa wa umeme wa mashariki, ambao daima umemulika kwa ulimwengu mzima. Wakati ambapo nchi duniani zinakuwa ulimwengu wa Kristo ndio wakati ambapo ulimwengu mzima unatiwa nuru. Sasa ndio wakati ambapo umeme wa mashariki unatoka: Mungu mwenye mwili Anaanza kufanya kazi, na, zaidi ya hayo, Anaongea moja kwa moja katika uungu. Inaweza kusemwa kwamba Mungu anapoanza kuongea duniani ni wakati ambapo umeme wa mashariki unatoka. Kwa usahihi zaidi, wakati ambapo maji ya uhai yanatiririka kutoka katika kiti cha enzi—wakati ambapo matamshi kutoka katika kiti cha enzi huanza—bila shaka ni wakati ambapo matamshi ya Roho saba huanza kirasmi.

3 Wakati huu, umeme wa mashariki unaanza kutoa nje, na kwa sababu ya kipindi chake, kiwango cha mwangaza pia kinabadilika, na kunao, pia, mpaka kwa mawanda ya nuru. Lakini kadri kazi ya Mungu inavyoendelea, kadri mpango Wake unavyobadilika—kadri kazi kwa wana na watu wa Mungu inavyobadilika—umeme unazidi kutekeleza kazi yake ya asili, kiasi kwamba yote kotekote duniani yanaangazwa, na hakuna mashapo ama takataka zinazobaki. Huu ndio udhihirisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6000, na tunda hasa linalofurahiwa na Mungu. Wakati ambapo mwale wa mwanga kutoka kwa Mungu unaiangaza nchi yote, vitu vyote mbinguni na duniani vitabadilika kwa viwango mbalimbali, na nyota angani pia zitabadilika, jua na mwezi vitafanywa upya, na watu duniani watafanywa upya baadaye—ambayo yote ni kazi inayofanywa na Mungu katikati ya mbingu na dunia.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 12” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 26 Matarumbeta Saba ya Mungu Yanasikika Tena

Inayofuata: 28 Kondoo wa Mungu Waisikia Sauti Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp