65 Upendo wa Mungu Unauzingira Moyo Wangu

1

Jua la haki linainuka Mashariki.

Ee Mungu! Utukufu Wako unajaza mbingu na dunia.

Mpendwa wangu, upendo Wako unauzunguka moyo wangu.

Wale wanaotafuta ukweli—wanampenda Mungu, kila mmoja.

Asubuhi na mapema, ingawa naamka peke yangu,

furaha iko moyoni mwangu ninavyoyatafakari maneno ya Mungu.

Maneno Yake ya upole, kama yale ya mama mwenye upendo;

Maneno Yake ya hukumu, makali kama kukaripia kwa baba.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Mwenyezi Mungu ni mzuri sana.

Hakuna kingine duniani ninachopenda.

Nampenda kikamilifu, nampenda Yeye pekee.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

2

Mapenzi ya Mungu yamefichuliwa

kuwakamilisha wale wanaompenda kweli.

Msio na hatia, mnaobubujikwa na uzima,

toneni sifa zenu Kwake.

Dansi ya furaha ni nzuri,

rukeni na kucheza karibu na kiti cha enzi.

Kutoka katika pembe nne za dunia, tunakuja,

tukiitwa na sauti ya Mungu.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Mwenyezi Mungu ni mzuri sana.

Hakuna kingine duniani ninachopenda.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Nampenda kwa ukamilifu, nampenda Yeye pekee.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Maneno Yake ya uzima tulipewa sisi,

tunatakaswa na hukumu Yake.

Upendo unakuwa wa nguvu zaidi kwa kusafishwa.

Ni utamu kufurahia upendo wa Mungu.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Mwenyezi Mungu ni mzuri sana.

Hakuna kingine duniani ninachopenda.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Nampenda kwa ukamilifu, nampenda Yeye pekee.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu, eh Mungu!

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Upendo Wako unauzingira moyo wangu, mpendwa Mungu!

Upendo wa Mungu unauzingira moyo wangu.

Iliyotangulia: 64 Upendo wa Kweli

Inayofuata: 66 Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp