297 Kilio kwa Dunia ya Mikasa

1

Kuelea katika wakati, kupitia maisha. Miaka inageuka kama ndoto.

Tukizunguka kwa ajili ya umaarufu na mali.

Maisha kutumika kwa vitu vya mwili. Hakuna kitu ambacho kimetolewa kwa ukweli.

Ujana umepita hivyo tu.

Hakuna fikira ya mateso ya Mungu mwenyewe ama uzuri Wake mkuu.

Kupisha tu siku kwa uzembe. Hakuna hata siku moja inayoishiwa Mungu.

Hatukufanya midomo wa Mungu kutabasamu kamwe. Kavu na bila kitu cha kipekee.

Nani ameulewa moyo wa Mungu?

Nani anaweza kushiriki na Mungu uzima na kifo?

Nani amethamini maneno Yake yote?

Nani ametoa kwa Mungu kila kitu chake?

Ni lini maua ya majirira ya kuchipua yatasita kuchanua?

Upendo wa kweli umo humu duniani.

Huzuni na furaha, vipindi vya heri na shari. Mzunguko wa majira, yakiendelea zaidi na zaidi.

Mungu ametelekezwa mwaka baada ya mwaka. Ni dunia ya dhiki iliyoje!

2

Mwanadamu ana nyumbani kwake, mahali pa kutulia. Ilhali Mungu hana mahali pa kupumzisha kichwa Chake.

Ni wangapi wanajitoa wenyewe? Yeye amejawa na baridi,

akavumilia mateso ya dunia nzima. Lakini hakuna ambaye ameonyesha huruma yake.

Akiwa na wasiwasi kwa mwanadamu, Mungu anashugulika kati yao na Anaendelea kufanya kazi bila kuchoka.

Ni nani anayemfikiria Mungu?

Ingawa majira yanakuja na kupita, Yeye anajitolea yote kwa ajili ya mwanadamu.

Nani amewahi kuulizia kuhusu starehe Yake?

Jinsi mwanadamu anavyodai kutoka kwa Mungu! Kamwe hafikirii kuhusu mapenzi Yake.

Akifurahia maisha mazuri ya familia, lakini mbona wanamfanya Yeye alie?

Ni lini maua ya majirira ya kuchipua yatasita kuchanua?

Upendo wa kweli umo humu duniani.

Huzuni na furaha, vipindi vya heri na shari. Mzunguko wa majira, yakiendelea zaidi na zaidi.

Mungu ametelekezwa mwaka baada ya mwaka. Ni dunia ya dhiki iliyoje!

Iliyotangulia: 296 Hakuna Moyo Ulio Bora Kuliko wa Mungu

Inayofuata: 299 Kusubiri Habari Njema za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp