58 Kuenda Nyumbani

Nilikuwa nikifikiria kama nisiyejua

kwamba dunia ilikuwa na ndoto zangu zote,

ningepata maisha mazuri

kupitia bidii na kujitahidi.

Lakini baada ya kushindwa kwingi,

mawazo yangu yanaonekana ya upuuzi.

Katika ulimwengu huu uliojaa maovu na njama,

nilipoteza usafi wangu, uzuri wangu.

Nilitafuta umaarufu na kutafuta utajiri,

kama mnyama niliishi.

Ukatili wa dunia

na kutojali kuliponda moyo wangu.

Watu wanapigana na kuuana,

wamejaa uwongo na vurugu.

Hakuna njia rahisi ya kuishi,

bila kuunga mkono na njama.

Hata kutembea njia sahihi

na kuwa na imani katika Mungu

kutasababisha ubaguzi

na kutasababisha kufungwa.

Naona wazi kuwa ulimwengu huu

umejaa mabaya na giza.

Sina msaada na nimeumia.

Nimejawa na uchungu moyoni mwangu.

Mwelekeo wangu hauwezi kupatikana,

ingawa nipo mpweke na natafuta sana.

Nyumbani kuzuri kuko wapi?

ninakotamani sana moyoni mwangu?

Sauti ninayoijua yaniita.

Maneno ya Mungu yenye fadhili, yaupa moyo wangu joto.

Naona ni Mwana wa Adamu

Anayenena na mlangoni kwangu Anabisha.

Kwa kuja mbele za Mungu naona

kanisa ni mbingu na dunia mpya.

Watu hapa ni safi na wazuri,

wawaonyesha wengine uaminifu.

Hapa kuna usawa, haki.

Maneno ya Mungu, ukweli, yana nguvu kuu.

Yanafichua siri za maisha,

yauamsha moyo wangu, maisha yanakuwa wazi.

Kuujua ukweli kunaniwezesha

kubainisha mema na mabaya.

Kutotafuta umaarufu au utajiri tena,

napambana kutoka katika wavu wa Shetani.

Sasa mwaminifu, Mungu anibariki.

Moyo wangu una amani; niko mtulivu.

Nawuogopa Mungu na kuepuka uovu.

Njia sahihi ya maisha naitembea.

Mungu anapendeza sana;

moyo wangu wamtamani sana.

Sasa naweza kuishi katika nuru,

nimtii, nimpende Mungu milele.

Kwa kuja mbele za Mungu naona

kanisa ni mbingu na dunia mpya.

Watu hapa ni safi na wazuri,

wawaonyesha wengine uaminifu.

Hapa kuna usawa, haki.

Nitamtii, nitampenda Mungu milele.

Iliyotangulia: 57 Umo Moyoni Mwangu

Inayofuata: 59 Kukubali Ukweli ni Kuwa Mwanamwali Mwenye Busara

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp