Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hushikilia mamlaka katika ulimwengu wa kidini na watu wengi huwatii na kuwafuata—huu ni ukweli. Unasema kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hawaukubali ukweli wa Mungu kuwa amekuwa mwili, kwamba hawaamini ukweli ulioonyeshwa na Mungu mwenye mwili na kwamba wanaitembea njia ya Mafarisayo, na tunakubaliana na jambo hili. Lakini kwa nini unasema kuwa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote ni Mafarisayo wanafiki, kuwa wote ni wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kwamba wataingia katika maangamizo mwishoni? Hatuwezi kukubali jambo hili kwa wakati huu. Tafadhali shiriki unachotegemeza dai hili, kwamba watu hawa hawawezi kuokolewa na kwamba ni lazima wote waingie katika maangamizo.

09/06/2019

Jibu:

Asili ya jinsi watu katika jamii ya kidini wanavyomkana Mungu zinaweza tu kufichuliwa na kuchanguliwa baada ya kuja kwa Kristo mwenye mwili. Hakuna wanadamu wapotovu wanaoweza kuutambua ukweli na asili ya jamii ya kidini ya kumkana Mungu, kwa sababu wanadamu wapotovu hawana ukweli. Wanaweza tu kudhibitiwa, kuchanganywa, na kuchezewa na wachungaji wa uwongo na pepo wapinga Kristo ili kujiunga nao katika kufanya uovu, na kuwa watumishi na washiriki wa Shetani katika kumkana Mungu. Hili ni jambo la kawaida. … Hebu tuone jinsi, wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alivyoufichua ukweli na asili ya jinsi pepo wabaya wapinga Kristo katika jamii ya kidini walivyomuasi Mungu daima:

Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi.

Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.

Ole wenu ninyi, viongozi mlio vipofu, mnaosema, Yeyote atakayeapa kupitia kwa hekalu, haimaanishi chochote; lakini yeyote atakayeapa kupitia kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa kwa kiapo hicho. Ninyi mlio wapumbavu na vipofu: kwa kuwa kipi kilicho kikubwa zaidi, hiyo dhahabu, au hilo hekalu linaloitakasa dhahabu? Na, Yeyote atakayeapa kupitia kwa madhabahu, haimaanishi chochote; lakini yeyote atakayeapa kupitia kwa sadaka iliyo juu ya madhabahu hiyo, amefungwa kwa kiapo hicho. Ninyi mlio wapumbavu na vipofu, kwa kuwa ni kipi kilicho kikubwa zaidi, hiyo sadaka, au hiyo madhabahu inayoitakasa sadaka? Basi yeyote anayeapa kupitia kwa madhabahu, huapa kupitia kwa madhabahu hiyo, na kila kitu kilicho juu yake. Na yeyote anayeapa kupitia kwa hekalu, huapa kupitia kwa hekalu hilo, na kupitia kwa yeye anayekaa hekaluni. Na yule anayeapa kupitia kwa mbingu, huapa kupitia kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kupitia kwa yule anayeketi juu yake.

Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, ninyi wanafiki! kwani mnatoa fungu la kumi la mnanaa na bizari na jira, na mmeacha mambo muhimu zaidi ya sheria, hukumu, fadhili, na imani: mlipaswa kuyafanya haya, na sio kutolifanya lingine. Nyinyi viongozi vipofu, mnaochunguza sana visubi, na kumeza ngamia.

Ole wenu ninyi, waandishi na Mafarisayo, wazandiki! Kwa maana mnaosha nje ya kikombe na sahani, lakini ndani yake kumejaa kutoza kwa nguvu na kupenda zaidi ya kiasi. Ewe Farisayo aliye kipofu, osha kwanza kikombe na sahani kwa ndani, ili nje viwe safi pia.

Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, nyinyi wanafiki! Kwani nyinyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, ambayo kwa nje yanaonekana mazuri sana, lakini ndani yake mna mifupa ya wafu, na yenye uchafu wote. Hata hivyo ninyi pia mnaonekana wenye haki kwa wanadamu, lakini ndani yenu mmejaa unafiki na dhambi.

Ole wenu, ninyi waandishi na Mafarisayo, wazandiki! kwa sababu mnajenga makaburi ya manabii, na kupamba makaburi ya wenye haki, Na kusema, iwapo tungelikuwa katika siku za baba zetu, hatungelishiriki na wao kuwaua manabii. Kwa nini mnakuwa mashahidi kwenu wenyewe, kuwa ninyi ni wana wa hao ambao waliwaua manabii. Basi kijazeni kiwango cha baba zenu. Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu? Hivyo, tazama, natuma kwenu manabii, na wanadamu wenye busara, na waandishi: na mtauwa na kusulubisha baadhi yao; na mtawacharaza baadhi yao katika masinagogi yenu, na kuwatesa kutoka mji mmoja hadi mji mwingine: Ili damu yote yenye haki iliyomwagika duniani iweze kuwa juu yenu, kuanzia damu ya Habili aliyekuwa mwenye haki hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia, ambaye mlimwua katikati ya hekalu na madhabahu. Kweli nawaambieni, Mambo haya yote yatakifuata kizazi hiki(Mathayo 23:13-36).

Haya ndiyo maneno maarufu zaidi ya Bwana Yesu wakati wa Enzi ya Neema ambayo yanawafichua na kuwahukumu makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa Kiyahudi wa jamii za kidini.

Kutokana na ukweli kwamba Bwana Yesu alitangaza “masikitiko saba” ambayo yaliwafichua na kuwachangua makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo kutoka kwa jamii za kidini wakati wa Enzi ya Sheria, tunaweza kuona kwamba wengi wa viongozi wa kidini ni Mafarisayo wa uongo na, tangu zamani sana, wamekuwa vikosi viovu vya shetani vinavyompinga Mungu. Huu tayari ni ukweli usiokanika.

…………

“Masikitiko saba” ya Mafarisayo yaliyofichuliwa na Bwana Yesu yalikuwa tayari yameonyesha kwamba giza na upotovu wa jamii za kidini si tofauti na yale ya ulimwengu wa kidunia. Kwa hiyo watu wanaweza kuona kabisa kwamba matendo ya makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo wa jamii za kidini hawakuwa wakimtumikia Mungu kamwe, bali walikuwa wakimkana na kumpinga Mungu. Walisimama kama makuhani na viongozi katika nafasi za kumtumikia Mungu, lakini hawakutenda ukweli na haki. Badala yake, walifanya aina zote za matendo ya kutisha, na hata walimtendea Yesu Kristo mwenye mwili kama mpinzani, wakimhukumu na kumdhulumu na kumtundika Yeye msalabani. Baada ya kutenda dhambi hizi kubwa, wangekosaje kupata ghadhabu ya Mungu? Ndio sababu Mungu aliwachukia na kuwa na hasira kwao, na ndiyo maana aliwafichua, kuwahukumu, na kuwalaani. Hili ni jambo la kawaida kabisa. Hili linatuonyesha kwamba Mungu hamruhusu mtu yeyote aikosee tabia Yake ya haki. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu alikuwa ameyadharau na kuyachukia matendo mbalimbali maovu dhidi ya ukweli na Yeye mwenyewe yaliyotendwa na makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa jamii za kidini. Ufunuo usio na huruma na hukumu Alivyovitumia dhidi yao vinaonyesha kwamba Mungu ni mwenye haki na mtakatifu. Mungu hajawahi kamwe kuwasifu wale walio katika jamii za dini ambazo humtumikia Mungu lakini bado humkana Yeye. Mungu alipata mwili kabisa kwa ajili ya kuja kwa ulimwengu wa binadamu binafsi ili kuwatafuta kondoo Wake, kuwaokoa wote wanaoupenda ukweli na wanaoweza kuisikia sauti ya Mungu. Mungu huwachukua wale wote ambao humtaka Mungu kikamilifu, na wanaoweza kuukubali ukweli. Wakati wa kuhubiri kwa Bwana Yesu, makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa jamii za kidini wote walikuwa lengo la laana na uondolewaji wa Mungu. Hili linaonyesha haki na utakatifu wa Mungu. Ni Mungu peke yake anayependeka, aliye wa thamani kubwa, mwenye heshima, na mwaminifu, na viongozi, waandishi na Mafarisayo wa jamii za kidini wote walikuwa wanafiki, waliojaa uongo, udanganyifu, ubaya, na uovu. Wote walikuwa ni wa jinsi ya nyoka ambao waliwachanganya watu na kumkana Mungu. Walikuwa ni aina ya watu ambao kabisa wanapaswa kutelekezwa. Wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alipokuwa akitekeleza kazi Yake ya ukombozi, hakuna makuhani wowote wakuu wa Kiyahudi, waandishi, au Mafarisayo waliokuja mbele ya Bwana Yesu kwa toba kamwe. Wala Mafarisayo wengi hawakutafakari na kujutia matendo yao maovu baada ya Bwana Yesu kutundikwa msalabani na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi. Kama walikuwepo, kulikuwa na watu wachache tu. Ukweli huu unatosha kuthibitisha kwamba makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo wote walikuwa pepo ambao waliuchukia ukweli na walimkana Mungu. Bila kujali ni uovu kiasi gani walioutenda, hata kumtundika Yesu msalabani, hawakuyajutia matendo yao. Suala hili kwa hakika ni la kuvutia hisia. Hapa si vigumu kuona kwamba viongozi wengi katika jamii za kidini ni wachungaji wa uongo ambao humtumikia Mungu lakini bado humkana Mungu. Wao kwa hakika ni mfano halisi wa shetani mpinga Kristo. Lakini, watu wengi wanaomwamini Mungu bado wanawaabudu na kuwafuata. Hili linatosha kuonyesha kwamba wanadamu wamepotoka kabisa, na tayari wamewadanganywa na uongo na dhambi. Shetani ameyapofusha macho yao. Ingawa wameharibiwa na pepo, bado wanakataa kwa ukaidi kubadili, kana kwamba walikuwa wamekufa tayari. Kwa hiyo, tunaweza kuona jinsi kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu waliopotoshwa ilivyo ngumu! Hili ni swali muhimu ambalo wanadamu wote wapotovu wanapaswa kutafakari na kutambua.

…………

Biblia inasimulia matukio mengi ya makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo wakimkana na kumhukumu Bwana Yesu. Hapa watu wanaweza kuona kwamba hawa makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo walizingatia tu kufanya ibada za kidini na kuwafundisha watu kufuata amri na kutii sheria. Hili linatosha kuonyesha kwamba hawa makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo hawakutenda ukweli wowote na hawakuwa na uhalisi kabisa. Walikuwa wamesoma vizuri mambo ya Biblia na kujifunza sheria, lakini hawakumjua Mungu kabisa. Jambo la karaha mno ni kwamba waliweza hata kuwaua manabii na watu wenye haki. Hawakukosa kumtii Kristo tu, ambaye alikwisha kuwa mwili na kuonyesha ukweli, waliweza hata kumhukumu, kumkamata, kumnasa, na kumuua, wakijifanya kuwa maaadui wa Mungu. Kwa hiyo chuki ya Mungu kwao ilikuwa imekita mizizi, na Yeye aliwafichua, akawachangua, na kuwahukumu. Aidha, hili linaonyesha kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki na mtakatifu. Anawapenda wale wanaofanya haki, na huwachukia wale wanaofanya maovu. Mungu kamwe hakuwasifu makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo wa jamii za kidini za Kiyahudi. Mungu aliwafichua, kuwahukumu, na kuwawalaani tu. Huu ni ukweli ambao unatambuliwa na wote wanaomwamini Bwana Yesu. Kama watu kwa kweli wanaielewa Biblia, kwa nini hawawezi kutumia maneno ya Bwana Yesu ili kuzitambua nyuso za kweli za unafiki, za wachungaji na wazee katika jamii za kidini wakataa Mungu wa kisasa? Kwa nini watu hawawezi kusimama upande wa Bwana Yesu ili kutofautisha na kuwatelekeza watu wasio na shukrani wa jinsi ya nyoka ambao humtumikia Mungu na bado humkana Yeye? Kama watu kwa kweli wanaielewa Biblia, basi wanapaswa kuona ukweli wa kuogofya hata zaidi ambao viongozi wengi na wachungaji katika jamii za kidini leo wanachukua nafasi sawa na zile za makuhani wakuu, waandishi, na Mafarisayo waliomkana Bwana wetu Yesu wakati wa Enzi ya Neema. Bado wanaendelea kumkana Mwenyezi Mungu aliyekuwa mwili katika siku za mwisho, na dhambi zao hata ni kubwa zaidi kuliko za makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo waliomkana Bwana Yesu. Wao huuchukia ukweli kabisa, na wao huogopa kabisa kwamba watatengwa wakati watu wateule wa Mungu wanapokea njia ya ukweli, kuitii kazi ya Mungu, na kupatwa na Mungu. Wao hata hugeuza ukweli, kupotosha ukweli, kubuni na kuponza, kukashifu na kushutumu, na kwa utovu wa haya, hutafsiri Biblia vibaya kwa makusudi ili kumhukumu Kristo na kuikufuru kazi ya Roho Mtakatifu na matamshi ya Mungu. Ili kuziokoa nafasi zao na riziki zao, hutumia aina zote za hila kumhukumu Mungu, kukufuru dhidi ya Mungu, na kumkana Mungu. Matendo yao ni sawa kabisa na hila mbalimbali za shetani zilizotumiwa na makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo katika kumkana Bwana Yesu. Wote wanaitembelea njia ya mpinga Kristo ya kumpinga Mungu. Kwa kufuata aina mbalimbali za kumtumikia Mungu kwa nje—lakini kwa ndani wakimpinga Yeye—jambo linalofanywa na viongozi wengi na wachungaji wa jamii za kidini, tunaweza kuona kwamba kuna matendo saba hasa yaliyo maovu ambayo tayari yamemchukiza Mungu. Bila shaka yataadhibiwa. Matendo hayo saba maovu yanayofanywa na wachungaji wengi na viongozi katika jamii za dini yameorodheshwa hapa:

1. Wao hufanya tu matambiko ya kidini ambayo hudumisha na kutamka urithi wa wanadamu na mafundisho, lakini huziacha amri za Mungu. Huwa hawawafundishi watu kumtii Mungu kamwe, kumjua Yeye, au kuyasikiliza maneno Yake. Hawazungumzii kamwe uhalisi wa kweli, na kamwe hawazungumzii maneno ya Mungu ili kulifichua giza katika jamii za kidini ili kuwaruhusu watu kujua kuhusu enzi ya uovu.

2. Hawamheshimu Mungu kamwe. Hawana nafasi kwa ajili ya Mungu mioyoni mwao, lakini wao kwa ulafi na kwa kunyemelea hula kutoka kwa sadaka kwa Mungu. Hawawezi kwa kweli kumtumikia Mungu, lakini wao hutumia sadaka kwa Mungu kama riziki zao, na mara nyingi huwasihi na kuwalazimisha watu kutoa mchango ili waweze kuishi kwa starehe zaidi, wakijifanya wanyonya damu na vimelea vya kweli.

3. Wao huzunguka ardhi na bahari wakiwashawishi watu waingie katika kanisa lao, na mara wanapofanya hivyo, watu huchanganyikiwa na kudhibitiwa hadi kuwa watumwa. Hawawapatii watu haki ya kuchagua njia ya kweli kwa uhuru, na hawawaruhusu watu kuchunguza njia ya kweli, kutafuta kuonekana kwa Mungu na kazi Yake, wakiwasababisha kushuka na kuwa watoto wa kuzimu. Ni vipofu wakiwaongoza vipofu, na wote wataanguka shimoni.

4. Katika mahubiri yao mara nyingi wao huiba utukufu wa Mungu ili kujidhihirisha wenyewe na kujishuhudia wenyewe ili watu kuiga, kupenda, na kufuata, wakiwafanya watu kuwaabudu kama mungu ili kuwanasa na kuwadhibiti. Kwa hakika na kwa uaminifu hawamshuhudii Mungu na kumheshimu Mungu kama mkuu kamwe, ili watu wamtii na kumwabudu Mungu.

5. Wao huuchukia ukweli, na wana wivu hasa kwa watu wanaofuatilia na kuuelewa ukweli: Huwazuia, kuwakataa, na kuwahukumu. Wao huwaruhusu watu kuwaabudu na kuwafuata tu, lakini wao huwakwamisha na kuwazuia watu wasimkubali Kristo, na wao huyazingia makanisa kwa sababu wanaogopa watu wanaoishuhudia kazi ya Mungu katika siku za mwisho.

6. Ili kuokoa nafasi zao na riziki zao, wao hata hubuni uvumi wa aina zote na uongo ili kumkashifu, kumhukumu, na kumkufuru Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu. Wao hujaza kila kitu na giza yao, na hata wangependelea mapambano ya maisha na kifo dhidi ya Mungu hadi mwisho. Ni dhahiri kwamba hawamtumikii Mungu lakini badala yake nafasi zao wenyewe na riziki zao.

7. Hawaukubali ukweli wa kupata mwili kwa Mungu, wala hawaamini neno na kazi ya Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho. Hili linatosha kuthibitisha kwamba wote wana asili na kiini cha wapinga Kristo wa kuuchukia ukweli. Wao huitembea njia ya mpinga Kristo ya kumtumikia Mungu lakini wakimkana na kumpinga Mungu.

Haya matendo saba maovu ya vikosi vya mpinga Kristo katika jamii za kidini ambayo humkana Mungu ni ukweli unaotambulika na waumini wote wa Mungu. Haya matendo saba maovu yanayotendwa katika jamii za kidini leo yana karibu sifa sawa na “masikitiko saba” ambayo kwayo Bwana wetu Yesu alifichulia na kuhukumia Mafarisayo. Haya yanatosha kuthibitisha kwamba viongozi wa kidini, kwa muda mrefu, daima walionekana kumtumikia Mungu lakini kwa kweli wamemkana Mungu na kuitembea njia ya mpinga Kristo. Ukweli huu pia umefichua kwamba wote wana asili ya Shetani na kiini cha kuuchukia ukweli na kumkana Mungu. Hii ndiyo maana wanaweza kuwa vikosi vilivyo na uhasama kwa Kristo wa siku za mwisho: Wao huziongoza jamii za kidini kwa giza na uovu. Hili linatimiza kabisa unabii katika Kitabu cha Ufunuo cha Biblia kwamba jamii za kidini ni “kahaba mkubwa” na “Babeli kubwa.” Sasa, watu fulani wanaompenda Mungu na wanatamani kuonekana kwa Mungu tayari wamegundua asili ya mpinga Kristo na asili ya Mafarisayo hawa wa kisasa, na wameanza kuondoka kwa jamii za kidini ili kuzitafuta nyayo za kazi ya Mungu. Ingawa hawa “Mafarisayo” wa jamii za kidini wanafahamu wazi kwamba maneno yote yaliyoonyeshwa na Kristo wa siku za mwisho ni ukweli, hukumu na adabu zilizolenga wanadamu wapotovu, wao hata hivyo walichagua kuchukua mwelekeo wa kumkana, kumhukumu, kumshutumu, na kumpinga Mungu kwa sababu ya chuki yao ya ukweli. Hasa, pia wamefanya dhambi mbaya sana ya kumkufuru Roho Mtakatifu na kazi ya Mungu. Maonyesho makuu matatu ya dhambi hii yameorodheshwa kama ifuatavyo:

1. Wao hubuni uongo ili kuukashifu mwili wa Mungu. Huku ni kukufuru dhidi ya Mungu.

2. Wao huyachukua maneno ya Mungu kama maneno ya binadamu, na wao husema kwamba kuna pepo wabaya katika maneno ya Mungu ambao huwaroga watu wanapoyaangalia. Huku ni kukufuru kuzito dhidi ya Mungu.

3. Wao huielezea kazi ya Mungu katika siku za mwisho kama kazi ya pepo wabaya, ambayo ni kama kusema kuwa kazi ya Roho Mtakatifu ni kazi ya pepo wabaya. Hii ni kufuru dhidi ya Mungu.

Watu katika jamii zote za kidini wanaeneza kufuru dhidi ya Mungu kwa njia hizi tatu. Kama kwa kweli walikuwa watu ambao walimheshimu Mungu, hawangethubutu kabisa kusema mambo kama hayo. Tukikumbuka wakati wa siku za kuhubiri za Bwana wetu, wakati huo kulikuwa na watu wa kidini ambao walisema kuwa Bwana Yesu alitumia Beelzebuli, mfalme wa pepo, kuwatoa pepo. Huku kwa kweli ni kutenda dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Bwana Yesu alisema, “Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu(Mathayo 12:31). Katika jamii za kidini za leo, viongozi wengi na wachungaji hutoka na kueneza uvumi na kashfa ambazo hukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali nia zao na malengo yao ni nini, tayari wamefanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Wale ambao kwa hakika humheshimu Mungu sana hawangethubutu kusema ovyo ovyo bila kwanza kufanya uchunguzi wa kina wa njia ya kweli, lakini wanaamua kiholela kwamba Umeme wa Mashariki ni kazi ya pepo wabaya, na kwamba watu hudanganywa wanaposikia ujumbe wake. Kwa hakika hili ni jambo la dhihaka! … Wachungaji wengi na viongozi katika jamii za dini tayari wamefichuliwa kuwa wale wanaoitembea njia ya mpinga Kristo kabisa. Ili kuweka hadhi yao na riziki yao wanajitahidi kwa kukata tamaa dhidi ya Kristo mpaka mwisho. Mioyo yao ni migumu, hawana majuto, na wanafikiri kwamba hatimaye Mungu ataafikiana nao, kwa namna ambayo Bwana Yesu alimtendea Paulo wakati wa Enzi ya Neema. Wanafikiri kwamba Mungu atajifichua Mwenyewe na kuwaita kutoka mbinguni. Kumtundika Mungu msalabani na kisha kutamani kupokea huruma ya Mungu tayari ni utovu wa haya kupita kiasi. Wao ni wapumbavu na wagumu hadi kifo, wakionyesha mitazamo ya “kishujaa, dhabiti” na “ujasiri” wa nasaba za kidini. Hili linatimiza unabii katika Kitabu cha Waebrania katika Biblia: “Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi, lakini kuitafuta kwa hofu hukumu na uchungu mkali, ambao utawala maadui(Waebrania 10:26-27).

… Sasa ni wakati muhimu wa kueneza injili ya ufalme. Watu wengi, wanapokuwa wakikagua njia ya kweli, wao hutunduwazwa na kuchanganywa na uongo na uvumi wa pepo wa wapinga Kristo katika jamii za kidini. Wao huchanganywa na uongo na uasi wa joka kubwa jekundu hivyo hawathubutu kuikubali njia ya kweli. Watu wengi, wanapokuwa wakiikagua njia ya kweli, wamezuiwa na kuchanganywa na viongozi na wachungaji katika jamii za kidini, hivyo hawawezi kuja mbele ya Mungu. Maisha yao kisha yanaharibiwa na kusongwa na viongozi wa kidini, wachungaji, na joka kubwa jekundu. Kwa wachungaji na viongozi katika jamii za kidini kupigana na Mungu juu ya wateule Wake ni upotovu kiasi cha kuwa maadui wa Mungu. Hawawapi wateule wa Mungu haki ya kuchunguza njia ya kweli au kuchagua kwa uhuru. Ukweli huu muovu unatosha kueleza kwamba wao, kama joka kubwa jekundu, ni pepo ambao huponda ponda maisha na kuzila kwa ulafi roho za binadamu. Tayari wamefanya dhambi hii mbaya sana ya kumkosea Mungu. Je, si ukweli kwamba wanaweza kuwazuia watu ovyo ovyo sana kuikubali njia ya kweli na kurudi kwa Mungu unawafichua kama washiriki na wasaidizi wa Shetani? Deni la damu wanalowiwa na wanadamu ni lazima lilipwe kikamilifu. Mungu atawalipa kwa kutegemeza matendo ya kila mmoja, na hii ni sababu ya msingi ya Mungu kutojidhihirishi Mwenyewe na kufanya kazi katika jamii za kidini katika kupata mwili Kwake katika siku za mwisho. Jinsi Bwana Yesu alivyowachukia, kuwafichua, kuwahukumu makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa jamii za kidini ndivyo jinsi Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho huwachukia, kuwafichua, kuwahukumu, na kuwalaani wachungaji na wazee wa jamii za kidini za kisasa ambao huitembea njia ya mpinga Kristo. Unaweza kuona kwamba wakati Mungu ameonekana katika mwili kufanya kazi tena, ingawa jina Lake limebadilika, tabia Yake na asili havijabadilika. Mungu daima ni Mungu, wanadamu daima ni wanadamu, na Shetani daima ni adui wa Mungu. Huu ni ukweli usiobadilika. Watu ni lazima waone wazi asili na ukweli wa jamii za kidini zikimtumikia Mungu na bado zikimuasi Mungu, ili waweze kuikubali njia ya kweli, kuitii kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kupata wokovu wa Mungu. Hili ni jambo la haraka na haliwezi kucheleweshwa, kwa maana siku ya Mungu inakuja. Mwenyezi Mungu anasema: “Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Tunaweza kuona ukweli kutoka kwa Biblia kwamba, wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu hakukosa tu kuwaita makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa jamii za kidini, lakini kinyume chake, Aliwafichua na kuwahukumu. Hasa, kila mtu aliyehusika katika kumtundika Yesu msalabani aliadhibiwa bila huruma, na wote walipata mateso ya kuogofya. Huu ni ukweli unaotambuliwa na wote. Kuna mtu yeyote anayefikiria kwamba Mwenyezi Mungu anayekuja katika Enzi ya Ufalme anaweza kuwa akivihurumia na kuvisamehe vikosi vya mpinga Kristo katika jamii za kidini? Hapana kabisa, kwa sababu Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, na Mungu hamruhusu mtu yeyote kuikosea tabia yake. Mwenyezi Mungu amekwisha kuamua miisho yao, na kudhihirisha wazi ukweli kwamba wachungaji wengi na viongozi katika jamii za kidini leo humpinga Mungu. Hebu tuone kile ambacho Mwenyezi Mungu anasema: “Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia).

Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[1] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu kuliko mfalme wa wote, kujua kidogo kwamba wao si zaidi ya nzi wenye uvundo. Na bado, wanatumia vibaya uwezo wa nguruwe na mbwa ambao ni wazaziwe ili kukashifu uwepo wa Mungu. Kama nzi wadogo, wanaamini wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi wenye meno.[2] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, ilihali wazazi wao ni nguruwe wachafu mara mamia ya mamilioni kuliko wao wenyewe kwa ukubwa? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na kwa njia hizi wanaleta ukandamizaji kwa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea yale yanayoendelea kwa nyuma katika ulimwengu wa kidini). Ni jinsi gani mwanadamu angejua kwamba, licha ya urembo mzuri wa mbawa za nzi, nzi mwenyewe ni kiumbe mdogo tu, aliye na tumbo iliyojaa uchafu na mwili uliojaa vijidudu? Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza tena mkondo mwingine wa usaliti, wakianzisha kazi yao yenye miaka maelfu kadhaa iliyopita. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize.(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)).

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Fikiria kuhusu Enzi ya Neema, wakati wanadamu waliopotoshwa kabisa walimpigilia misumari Bwana Yesu msalabani. Je, ni nini hasa asili ya matendo yao? Ili kuweza kumkabidhi Bwana Yesu, ambaye aliyehubiri njia ya ufalme wa mbinguni, kwa mfalme wa mashetani, na zaidi ya hayo kusema kwamba lazima Bwana Yesu asulubiwe msalabani, na kwamba ingekuwa ni heri kumwachilia mwizi kuliko kutomsulubisha Bwana Yesu, wanadamu kama hawa hawakuwa waliopotoshwa wenye pepo? Ni pepo pekee ambao wangeweza kumchukia Mungu sana kiasi kwamba wangejihusisha katika uhasama mkali na Mungu. Makuhani wakuu, waandishi, na wafuasi wengi sana waliopaza sauti kwa pamoja wakisema kuwa Bwana Yesu lazima asulubiwe; wangekuwa tu umati wa mapepo ambao walimchukia Mungu, si hivyo? Sasa, si wachungaji wengi na viongozi katika jamii ya kidini, pamoja na waumini wengi, pia wanamhukumu Mwenyezi Mungu kwa sauti moja? Je, hawa sio mapepo ambao wanampinga Mungu? Hasa sasa, wakati joka kubwa jekundu linapinga na kukataa kazi ya Mungu kwa hamaki, jamii ya kidini pia kuunga mkono joka kuu jekundu, na hata kushirikiana nalo ili kumpinga Mungu, kumshutumu Mungu, na kumkufuru Mungu. Kwa hivyo jamii ya wanadamu inashuhudia jamii ya kidini na joka jekundu kwa pamoja wakiunda vita vya muungano na kuungana katika kambi ya Shetani. Jamii ya kidini kwa muda sasa imekuwa mshiriki wa Shetani, ambayo inaonyesha kabisa kwamba kiini kiovu na kipotovu cha jamii ya kidini cha kumtumikia Mungu kwa kweli kinampinga Mungu. Hili linathibitisha kabisa maneno ambayo Bwana Yesu alinena yaliyofunua na kuwahukumu Mafarisayo wa Kiyahudi, yalifichua hasa kiini hichohicho kiovu na kipotovu cha jamii ya kidini leo. Upinzani dhidi ya Mungu kwa jamii ya kidini leo ni sawa na au unapita ule wa jamii ya kidini katika Enzi ya Neema. Wao ni kikundi cha mapepo wapinga Kristo ambao Mungu amewakataa na kuwashutumu, na wao wanamilikiwa kabisa na nguvu za uovu za Shetani. Kutokana na haya, ni dhahiri kwamba kupotoka kwa jamii ya binadamu kumekithiri kiasi cha kuweza kwa kweli kumsulubisha Kristo tena, ambaye katika siku za mwisho anawasilisha ukweli na kutoa hukumu. Hii inatosha kuonyesha kwamba jamii ya binadamu imepotoshwa kabisa na Shetani hadi ikageuka kuwa pepo. … Hukumu na kuadibu kwa Mungu katika siku za mwisho ni kazi ya kuitamatisha hatima ya Shetani. Je, inawezekana kwamba Mungu ataonyesha huruma kwa hawa wapinga Kristo wa kipepo wa jamii ya kidini ambayo inashiriki katika uhasama mkali na Mungu mwenye mwili halisi wa siku za mwisho? Kila mtu anaweza kusubiri na kuona kitakachokuwa wakati mataifa na watu wa dunia watashuhudia kuonekana kwa hadhara kwa Mungu. Je, kwa nini watu wataomboleza? Kisha ukweli utaletwa mchana!

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Tanbihi:

1. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

2. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Unafiki ni nini?

Maneno Husika ya Mungu: Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp