Ukungu Waondoka na Napata Njia ya Ufalme wa Mbinguni

28/12/2019

Na Che Ai, China

Niliwafuata wazazi wangu katika imani yao katika Bwana tangu nilipokuwa mdogo, na sasa uzee umenikaribia. Ingawa nimemwamini Bwana katika maisha yangu yote, tatizo la jinsi ya kujiondolea dhambi na kuingia katika ufalme wa mbinguni lilikuwa limekuwa kitendawili kisichotatuliwa ambacho kilinisababishia fadhaa ya siku zote, likiniacha nikihisi nimekanganyikiwa na kuhuzunishwa. Nilitamani sana kuweza kuelewa katika kipindi cha maisha yangu jinsi ya kujiondolea dhambi na kuingia katika ufalme wa mbinguni ili wakati wangu wa kufariki utakapofika niweze kukabili kifo nikiwa na ufahamu kuwa maisha yangu yalikuwa yamekamilika, na niweze mwishowe kukutana na Bwana nikiwa na amani moyoni mwangu.

Katika jaribio la kutatua mtanziko huu, nilitafuta maoni kwa shauku katika Biblia, nikianza kutoka Agano la Kale hadi Jipya na kutoka Agano Jipya kurudi hadi la Kale, nikisoma Biblia tena na tena. Lakini hatimaye, sikuweza kupata jibu sahihi. Kwa sababu ya kukosa chaguo, nilichoweza tu kufanya ni kutia jitihada yangu katika kuwa na mwenendo mzuri kadiri nilivyoweza kulingana na mafundisho ya Bwana, kwa kuwa Bwana alisema: “Ufalme wa mbinguni hupata mashambulizi, na wenye nguvu huuteka kwa nguvu(Mathayo 11:12). Lakini niligundua kuwa katika maisha halisi, bila kujali nilijitahidi kiasi gani, bado singeweza kuishi kulingana na kilichotakiwa na Bwana kutoka kwangu. Kama vile Bwana alivyosema: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda(Mathayo 22:37-39). Bwana anataka tumpende Mungu kwa mioyo yetu yote na akili zetu zote, na kwamba ndugu wapendane. Lakini bila kujali nilichofanya, sikuweza tu kupata upendo wa aina hii, kwa sababu upendo wangu kwa familia yangu ulikuwa mkubwa kuliko upendo wangu kwa Bwana, na sikuwa tu na uwezo wa kuwapenda kwa dhati ndugu zangu kanisani kama nilivyojipenda. Badala yake, mara nyingi nilikuwa mwenye kujishughulisha na mambo madogo madogo na mwenye hila kwa wengine masilahi yangu mwenyewe yalipohusika, sana kiasi kwamba chuki ingeamshwa ndani yangu. Je, mtu kama mimi angewezaje kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni? Bwana Yesu pia alisema mambo mengi kuhusu kuingia katika ufalme wa mbinguni, kama vile: “Kweli nawaambia, Ila msipobadilishwa, na kugeuka kama wana wadogo, hamtaingia ndani ya ufalme wa mbinguni(Mathayo 18:3). “Kwa kuwa nawaambieni, Kuwa isipokuwa haki yenu izidi haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia ufalme wa Mbinguni hata kidogo(Mathayo 5:20). Sikuweza kuweka katika vitendo mahitaji yoyote kati ya mahitaji haya ya Bwana. Mara nyingi ningesema uwongo, na ningemlaumu Bwana kila nilipokabiliwa na kitu ambacho sikukipenda. Mawazo yangu yalikuwa na ulaghai na udanganyifu, na nilikuwa nikiteseka daima katika dhambi, nikitenda dhambi na kutubu, nikitubu na kutenda dhambi tena na tena. Bwana ni mtakatifu, na katika Biblia inasema: “Utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14). Je, mtu najisi sana kama mimi angewezaje kuwa mwenye kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni? Hili lilikuwa likinichukiza sana. Lakini kila niliposoma kuhusu njia ya kuhesabiwa haki kwa imani kama ilivyoungwa mkono na Paulo katika Warumi, Wagalatia, na Waefeso—kwamba kuwa na imani na kubatizwa kunamaanisha kuwa mtu bila shaka ameokolewa, kwamba ikiwa tunamwamini Bwana mioyoni mwetu na kumkiri kwa vinywa vyetu, basi tumehesabiwa haki kwa imani, tumeokolewa milele, na kwamba Bwana atakapokuja tena bila shaka Atatunyakua hadi katika ufalme wa mbinguni—ningehisi kujawa na furaha. Ningehisi kwamba sikuhitaji kuwa na wasiwasi kuhusu kuingia katika ufalme wa mbinguni. Lakini baadaye ningekumbuka kile alichokisema Bwana kuhusu watu kuweza tu kuingia katika ufalme wa mbinguni kupitia juhudi zao wenyewe, na ningehisi wasiwasi. Kuhesabiwa haki kwa imani na kisha kuingia katika ufalme wa mbinguni—je, kunaweza kuwa rahisi hivyo? Hasa nilipowaona waumini wakongwe wacha Mungu wakikaribia mwisho wa maisha yao na wakionekana wasiotulia na wenye wasiwasi, sana kiasi kwamba hata wangelia sana na hakuna hata mmoja kati yao aliyeonekana kufurahi kuaga dunia, sikuweza kujizuia kujiuliza: Ikiwa wanasema kwamba wanaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni kupitia kuhesabiwa haki kwa imani peke yake, kwa nini basi wanaonekana wenye hofu nyingi sana wanapokaribia kufa? Ilionekana kana kwamba wao wenyewe hawakuwa na habari iwapo walikuwa wameokolewa au la, wala wangekuwa wakienda wapi baada ya kifo. Nilitafakari maneno ya Bwana Yesu tena na tena, na nilitafakari maneno ya Paulo, pia, na nikagundua kuwa maneno ya Yesu na maneno ya Paulo yalitofautiana sana kuhusu suala la ni nani angeweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kulingana na Paulo, mtu anahesabiwa haki kwa imani kwa kumwamini Bwana tu—kama ingalikuwa hivyo, basi kila mtu angeokolewa. Hivyo basi ni kwa nini Bwana Yesu alisema, “Tena ufalme wa mbinguni ni kama wavu, uliotupwa baharini, na ukakusanya kila aina: Ambao, ulipojaa, waliuvuta ufukoni, na wakaketi chini, na kukusanya walio wazuri ndani ya vyombo, lakini wakawatupa walio wabaya(Mathayo 13:47-48)? Kwa nini, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho, Anahitaji kutenganisha ngano na magugu, kondoo na mbuzi, na watumishi wazuri na watumishi waovu? Kutoka kwa maneno haya yaliyosemwa na Bwana Yesu, ni wazi kuwa sio kila mtu anayemwamini anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo nilijiuliza: Je, nimeokolewa? Na, je, nitaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni nitakapokufa? Maswali haya bado yalikawia akilini mwangu kama vitendawili, na sikujua kuyajibu.

Katika juhudi ya kutatua tatizo hili, nilitafuta maoni katika kazi za sanaa zilizoandikwa na watu mashuhuri wa kiroho wanaojulikana katika enzi zote, lakini nyingi nilizosoma zilikuwa tafsiri za kuhesabiwa haki kwa imani kama inavyoonekana katika Warumi, Wagalatia na Waefeso, na hakuna kimoja kati ya vitabu hivyo kiliweza kuondoa mkanganyiko wangu. Kisha niliwatembelea wazee wote mashuhuri katika Bwana na kuhudhuria mikusanyiko ya madhehebu mengi tofauti, lakini niligundua kwamba wote walisema mambo sawa kabisa, na hakuna mtu aliyeweza kunieleza waziwazi siri ya jinsi ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Baadaye, nilipata dhehebu mpya la kigeni linalochipuka, na nilijiwazia kuwa kanisa la aina hii pengine lingeweza kufafanua zaidi. Na kwa hivyo, nikiwa mwenye furaha, nilienda kuhudhuria moja ya mikutano yao. Mwanzoni mwa mahubiri yao nilikuta kuwa yenye kuangazia kwa kiasi fulani, lakini kufikia mwisho, niligundua kuwa wao pia walikuwa wakihubiri njia ya kuhesabiwa haki kwa imani, na nilihisi nimevunjwa matumaini sana. Baada ya mkusanyiko, nilimtafuta mchungaji mkuu, na kumuuliza, “Mchungaji, nasikitika sikuelewa uliposema, ‘Ukiokolewa mara moja, umeokolewa daima.’ Je, unaweza kushiriki ushirika zaidi pamoja nami kuhusu hili?” Mchungaji akasema, “Jambo hili ni rahisi sana kuelewa. Inasema katika Warumi, ‘Ni nani atawalaumu wateule wa Mungu kuhusu chochote? Ni Mungu ambaye huhalalisha. Ni nani anayeshutumu?’ (Warumi 8:33-34). Bwana Yesu Kristo tayari ametusamehe dhambi zetu zote kwa kusulubiwa msalabani. Yaani dhambi zetu zote, iwe ni dhambi tulizotenda hapo zamani, dhambi tunazotenda leo, au dhambi ambazo bado tutazitenda katika siku zijazo, zote zimesamehewa. Tunahesabiwa milele kuwa wenye haki kwa imani katika Kristo, na ikiwa Bwana hatatuhukumu kwa ajili ya dhambi zetu, je, ni nani anayeweza kutushutumu? Kwa hivyo, hatupaswi kupoteza imani ya kuingia katika ufalme wa mbinguni.” Jibu la mchungaji lilinikanganya hata zaidi, kwa hivyo nilifuatilia kwa kuuliza, “Je, unaelezaje yaliyoandikwa katika Waebrania, ‘Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi’ (Waebrania 10:26)?” Uso wa mchungaji uliiva na hakusema lolote tena, na swali langu lilisalia bila majibu. Sio tu kwamba mkusanyiko huu haukufanikiwa kutatua mkanganyiko wangu, bali badala yake, ulikuwa umeongeza chukizo langu. Nilijiwazia: “Nimemwamini Bwana kwa muda wa miongo mingi, lakini kama hata sina uhakika iwapo nafsi yangu itakwenda kwa Bwana nitakapokufa au la, je, hilo halimaanishi kuwa nimekuwa na aina ya imani tatanishi maishani mwangu mwote?” Kisha nilianza kwenye njia ya kutafuta jibu la tatizo langu mahali kote kabisa.

Mnamo mwezi Machi mwaka wa 2000, nilikwenda kusoma katika seminari iliyoendeshwa na raia wa kigeni, nikiwa mwenye imani kuwa mahubiri yaliyohubiriwa na raia wa kigeni yangekuwa bora zaidi na kwamba bila shaka yangetatua mkanganyiko wangu. Kwa mshangao wangu, hata hivyo, baada ya kusoma huko kwa muda wa miezi miwili, wakati ambao nilikuwa nimejawa na imani, niligundua kuwa wachungaji wote walihubiri mambo yale yale ya kale, na hakukuwa na nuru mpya katika mahubiri yao hata kidogo. Nikiwa huko, sikusikia kuhusu mahubiri yoyote ya kuhuisha, wala sikusoma hata insha moja ya kiroho. Sio tu kwamba mkanganyiko wangu haukuwa umeondolewa, lakini badala yake wakati wangu huko uliniacha tu nikihisi mwenye kuhangaikahangaika zaidi. Sikuweza kujizuia kuchanganyikiwa, na niliwaza: “Nimekuwa hapa kwa muda wa zaidi ya miezi miwili, lakini nimepata nini? Ikiwa sitaweza kupata riziki hapa, basi umuhimu wa kuendelea na masomo haya ni upi?”

Jioni moja baada ya dhifa, nilimuuliza mchungaji, “Mchungaji, kama wanafunzi wa theolojia, je, haya ndiyo yote tunayosoma? Je, hatuwezi kuzungumza kuhusu njia ya uzima?” Mchungaji alijibu kwa makini sana, “Iwapo hatutajadili mambo haya katika masomo yetu ya theolojia, basi tunapaswa kuzungumzia nini? Tulia tu na uendelee kusoma! Sisi ndio shirika kubwa zaidi la kidini duniani na tunatambuliwa kimataifa. Tutakufundisha hapa kwa muda wa miaka mitatu na kisha utathibitishwa kimataifa kama mchungaji. Wakati huo utakapofika, utaweza kupeleka cheti hicho mahali popote ulimwenguni ili kuhubiri injili na kuanzisha makanisa.” Jibu la mchungaji lilikuwa la kuvunja moyo sana kwangu. Sikutaka kuwa mchungaji, nilitaka tu kujua jinsi ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Na kwa hivyo nilimuuliza, “Mchungaji, kwa sababu kuwa na cheti cha mchungaji kunafungua milango mingi, je, nitaweza kukitumia kuingia katika ufalme wa mbinguni?” Aliposikia hayo, mchungaji alinyamaza. Niliendelea. “Mchungaji, nilisikia kuwa umemwamini Bwana tangu ulipokuwa mvulana. Sasa miongo mingi imepita, kwa hivyo najiuliza, je, umeokolewa?” Alijibu, “Ndiyo, nimeokolewa.” Niliuliza, “Kwa hivyo utaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni?” Kwa kujiamini, alisema, “Hakika, nitaingia!” Kisha niliuliza, “Naomba nikuulize basi, msingi wako wa kusema kuwa utaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni ni upi? Je, wewe ni mtu mwenye haki zaidi kuliko jinsi waandishi na Mafarisayo walivyokuwa? Je, unawapenda majirani zako kama unavyojipenda? Je, wewe ni mtakatifu? Tafakari hili: Bado hatuwezi kujizuia kutenda dhambi wakati wote na kwenda kinyume na mafundisho ya Bwana, na kila siku tunaishi katika hali ya kutenda dhambi mchana na kukiri usiku. Mungu ni mtakatifu, kwa hivyo, je, unafikiri kweli tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni tukiwa tumejawa na dhambi?” Mchungaji aliduwaa na uso wake uliiva kuwa wa rangi ya kiazisukari chekundu, na hakutamka neno lingine kwa muda mrefu. Nilikuta onyesho lake la hisia likiwa la kuvunja moyo sana, na nilihisi kwamba ikiwa ningeendelea na masomo yangu huko singeweza kufahamu siri ya jinsi ya kupata uzima na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Na kwa hivyo, niliacha masomo yangu kwenye seminari na kurudi katika mji wa nyumbani kwangu.

Katika safari yangu ya kuelekea nyumbani, nilikuwa mwenye huzuni zaidi kuliko wakati wowote ule; nilihisi kana kwamba tumaini langu la mwisho lilikuwa limevunjwa. Nilijiwazia: “Hata katika seminari iliyoendeshwa na wachungaji wa kigeni kutafuta kwangu hakukutoa njia ya kujiondolea dhambi na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Je, ninaweza kwenda wapi kwingine kutafuta njia hii?” Nilihisi kama nimefika kikomo. Wakati huo huo, picha ya baba yangu mkongwe na mchungaji mkongwe wakilia walipokuwa wakikaribia kifo ilinijia ghafla machoni pangu tena. Nilifikiria kuhusu jinsi walivyokuwa wametumia maisha yao yote wakihubiri njia ya kuhesabiwa haki kwa imani, kwamba watu wangeweza kuingia katika ufalme wa mbinguni baada ya kifo, lakini hatimaye walifariki wakiwa wamejawa na majuto. Nilikuwa nimemwamini Bwana maisha yangu yote na nilikuwa nimewaambia watu kila siku kuwa wangeingia katika ufalme wa mbinguni watakapokufa, na bado sikuwa nimewahi kuwa na uwazi halisi kuhusu jinsi ya kuingia katika ufalme wa mbinguni kwa kweli—je, ningeaga dunia nikiwa nimejawa na majuto kama tu baba yangu na mchungaji walivyofanya? Katikati ya huzuni yangu, maneno haya ya Bwana yalinijia akilini ghafla: “Ombeni, na mtapatiwa; tafuteni, na mtapata; pigeni hodi, na mtafunguliwa(Mathayo 7:7). “Hayo ni kweli, niliwaza. Bwana ni mwaminifu, ilimradi nitafute kwa moyo wa kweli basi Bwana bila shaka. Siwezi kufa moyo. Ilimradi kuna pumzi moja iliyosalia mwilini mwangu, nitaendelea kutafuta njia ya ufalme wa mbinguni!” Kisha nikaenda mbele za Bwana kuomba: “Bwana mpendwa, nimetafuta kila mahali njia ya kujiondolea dhambi na kuingia katika ufalme wa mbinguni, lakini hakuna mtu yeyote ambaye ameweza kusuluhisha tatizo langu. Bwana mpendwa, je, ninapaswa kufanya nini? Kama mhubiri, mimi huwaambia ndugu kila siku kwamba wanapaswa kuwa watafutaji wenye bidii na kuwa na subira hadi mwisho, na kwamba Utakuja kutuchukua tuingie katika ufalme wa mbinguni baada ya sisi kufa. Lakini kwa wakati huu, kwa kweli sijui jinsi ya kujiondolea dhambi na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Je, mimi si kipofu anayeongoza kipofu, nikiwaongoza kina ndugu zangu kuingia katika shimo? Bwana mpendwa, ninapaswa kwenda wapi kutafuta njia ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Tafadhali niongoze!”

Baada ya kurudi mji wa nyumbani kwangu, nilisikia kwamba kondoo wengi wazuri na kondoo viongozi katika kanisa letu walikuwa wameibwa na kanisa la Umeme wa Mashariki. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa njia ya kanisa la Umeme wa Mashariki ilitoa ufahamu mpya na nuru mpya, na hata wachungaji wenye uzoefu walivutiwa na mahubiri yao. Kila niliposikia mambo haya, ningewaza: “Inaonekana kana kwamba mahubiri yanayotolewa na kanisa la Umeme wa Mashariki ni ya fahari kweli. Ni aibu sijakutana na mtu yeyote kutoka katika kanisa la Umeme wa Mashariki. Lingekuwa jambo zuri sana ikiwa ningekutana nao siku moja! Kama siku hiyo itawadia, bila shaka nitasikiliza na kutafuta kwa dhati kufahamu ni kwa nini hasa mahubiri yao ni mazuri sana, na iwapo wanaweza au hawawezi kuondoa mkanganyiko huu ambao nimekuwa nao kwa miaka mingi.”

Siku moja, kiongozi wa kanisa aliniambia, “Kanisa fulani limeibiwa kondoo wake wazuri na kanisa la Umeme wa Mashariki. Madhehebu yote sasa yanafunga makanisa yao, na ni sharti tuwasihi ndugu zetu wasijihusishe na mtu yeyote kutoka kwa kanisa la Umeme wa Mashariki, na hasa wasisikilize mahubiri yao. Waumini wetu wote wakianza kuamini katika Kanisa la Umeme wa Mashariki, je, ni nani atakayebaki kwetu wa kumhubiria?” Nilichukizwa kusikia kiongozi wa kanisa akiyasema haya, na nilijiwazia: “Kanisa letu liko wazi kwa kila mtu, hivyo kwa nini tulazimike kulifunga? Mbona usimkaribishe mgeni anayetoka sehemu ya mbali? Inasema katika Biblia: ‘Msisahau kuwakaribisha wageni, kwani kwa jinsi hiyo baadhi wamewakaribisha malaika bila kujua’ (Waebrania 13:2). Abrahamu aliwapokea wageni na kwa hivyo alibarikiwa na Mungu, na alipata mtoto wa kiume akiwa na umri wa miaka mia moja; Lutu aliwapokea malaika wawili na kwa hivyo aliokolewa kutokana na maangamizo ya Sodoma; Rahabu yule kahaba aliwapokea majasusi kutoka Israeli na familia yake yote iliokolewa; na mjane masikini alimpokea nabii Eliya na kwa hivyo aliepuka kushinda njaa kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Kati ya watu wengi sana, hakuna hata mmoja aliyedhuriwa kwa sababu aliwapokea wageni kutoka sehemu ya mbali lakini, badala yake, wote walibarikiwa na Mungu. Kwa hivyo ni dhahiri kuwa kuwapokea wageni kunakubaliana na mapenzi ya Bwana. Kwa hivyo basi mbona uende kinyume na mapenzi ya Mungu, ukifunga kanisa kwa utukutu na kutowaruhusu wageni wowote waingie?” Nilipokuwa nikifikiria hili, nilitikisa kichwa changu, na kumwambia, “Kufanya hili kunapingana na mapenzi ya Bwana. Kanisa letu ni la Mungu na liko wazi kwa wote. Mradi tu ushirika wao unahusu imani katika Bwana, tunapaswa kumpokea yeyote, bila kujali yeye ni nani, na tunapaswa kutafuta tukiwa na akili za kuzingatia mawazo mapya na kutafiti mawazo pamoja. Ni kwa kufanya hivi tu ndipo tutapatana na mafundisho ya Bwana.”

Siku moja mnamo Julai mwaka wa 2000, nilikutana na dada wawili ambao walikuwa wakihubiri kanisa la Umeme wa Mashariki nilipokuwa katika nyumba ya Ndugu Wang. Baada ya kusalimiana, niliwauliza, “Nimekuwa daima nikitatanishwa kuhusu iwapo ninaweza au siwezi kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ulimwengu mzima wa kidini sasa unafuata maneno ya Paulo kwa imani kwamba tutaokolewa kwa kuamini na kubatizwa tu, na kwamba kwa kumwamini Bwana moyoni mwako na kumkiri Bwana kwa kinywa chako, umehesabiwa haki kwa imani, umeokoka milele, na kwa hakika utanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Lakini binafsi, sidhani kuingia katika ufalme wa mbinguni kunaweza kuwa rahisi hivyo. Kama inavyosema katika Biblia: ‘Utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana’ (Waebrania 12:14). Iwapo ni mimi au ndugu karibu nami anatumia siku nzima kila siku kuteseka katika dhambi, sidhani kwamba watu kama sisi ambao tunaishi kila siku katika dhambi tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ningependa tu kujua jinsi hasa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Je, unaweza kushiriki ushirika pamoja nami kuhusu jambo hili?”

Dada Zhou alitabasamu na kusema, “Ndugu, swali hili unalouliza ni muhimu. Jinsi ya kuingia katika ufalme wa mbinguni ni jambo kuu kwa kila muumini. Kupata uwazi kuhusu swala hili kunamaanisha kwanza kujua kwamba waumini katika Bwana wanapaswa daima kutenda kulingana na maneno ya Yesu Kristo, na sio kulingana na yale ambayo wanadamu wamesema. Bwana Yesu ametuambia kwa uwazi: ‘Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Bwana hakuwahi kusema kwamba tunaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni kwa kutegemea neema ya kuokolewa tu, au kwa kuhesabiwa haki kwa imani. Kuhesabiwa haki kwa imani, kuokolewa milele kwa sababu ya imani, na kisha kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni—hayo yalikuwa maneno ya Paulo. Paulo alikuwa mtume tu, mmoja wa wanadamu potovu, na alihitaji wokovu wa Bwana yesu pia. Je, angewezaje kuamua iwapo watu wengine wangeweza kuingia katika ufalme wa mbinguni au la? Bwana Yesu tu ndiye Bwana wa ufalme wa mbinguni, Mfalme wa ufalme wa mbinguni; maneno ya Bwana tu ndiyo ukweli, na ndiyo tu yenye mamlaka. Kwa hivyo, inapofikia jinsi tunavyoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni, tunapaswa kusikiliza maneno ya Bwana tu—hili ni hakika kabisa!

“Alafu kuna maswali ‘Je, kuhesabiwa haki kwa imani na kuokolewa kwa sababu ya imani vinanahusu nini?’ na ‘Je, unaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni mara baada ya kuokolewa?’ Haya yameelezwa dhahiri shairi katika maneno ya Mwenyezi Mungu, hivyo hebu sasa tusome vifungu kadhaa vya maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: ‘Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho). ‘Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).”

Dada Wang aliendelea na ushirika wake, akisema, “Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi wa mwanadamu, Akawa sadaka ya dhambi kwa binadamu kwa njia ya kusulubiwa, na kutukomboa kutoka katika mifumbato ya Shetani. Mradi tu tupokee wokovu wa Bwana na kukiri na kutubu dhambi zetu kwa Bwana, basi dhambi zetu zimesamehewa, na kisha tutakuwa wenye kustahili kufurahia neema na baraka za Bwana. Ninachomaanisha kwa kusema ‘dhambi zetu zimesamehewa’ ni kwamba hatulaaniwi tena au kuhukumiwa kifo chini ya sheria kwa ajili ya kukiuka sheria, na hii ndiyo maana halisi ya kuhesabiwa haki kwa imani na kuokolewa kwa sababu ya imani. Lakini hili halimaanishi kwamba basi hatuna dhambi au hatuna najisi, wala halimaanishi kwamba tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Hii ni kwa sababu, ingawa dhambi zetu zinaweza kuwa zimesamehewa, asili zetu zenye dhambi zinabaki zikikita mizizi ndani yetu, na tunapokabiliwa na matatizo bado mara nyingi sisi husema uongo na kuwadanganya wengine ili kulinda nafasi zetu na maslahi yetu wenyewe. Tunapofurahia neema ya Bwana, tunamshukuru na kumsifu, na tunajitumia kwa bidii kwa ajili ya Bwana. Lakini janga linapotokea, au kitu kibaya kinapozifanyikia familia zetu, tunamwelewa Bwana visivyo na kumlaumu, kiasi kwamba hata tunaweza kumkana na kumsaliti Bwana. Na kwa hivyo kama sisi, ambao wamekombolewa lakini ambao mara nyingi hutenda dhambi na kumpinga Mungu, watawezaje kupata sifa za kuingia katika ufalme wa mbinguni? Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, na kamwe hawezi kuruhusu watu najisi na potovu waingie katika ufalme Wake. Ili kutuokoa sasa na kwa mara ya mwisho kutokana na ushawishi wa Shetani, Anafanya kazi kulingana na mpango Wake wa usimamizi na mahitaji yetu kama wanadamu potovu, Akitekeleza kazi Yake ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu katika siku za mwisho. Mungu mwenye mwili ameonyesha mamilioni ya maneno ili kuhukumu upotovu wetu, uchafu, uovu na upinzani wetu, na ili kutuonyesha njia ya kuacha tabia zetu potovu. Wakati ambapo, kwa sababu ya kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tunaacha tabia zetu potovu na za kishetani, tunaweza kuweka maneno ya Mungu katika vitendo, na tumekuwa watu ambao kwa kweli wanamtii Mungu na kumwabudu, ni wakati huo tu ndipo tutakuwa wenye kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa kweli, Bwana Yesu alitabiri hapo zamani kwamba angerudi katika siku za mwisho kutekeleza kazi ya hukumu. Kama Alivyosema: ‘Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48). ‘Na wakati atakuja, ataushutumu ulimwengu kuhusu dhambi, na kuhusu haki, na kuhusu hukumu(Yohana 16:8). Kwa hivyo ni dhahiri kwamba ni kwa kupokea kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, kuacha tabia zetu potovu na kupata utakaso ndipo tu tutaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.”

Baada ya kusikiliza ushirika wa kina dada, kila kitu kwa ghafla kilianza kuwa dhahiri na papo hapo nuru ilijaa moyoni mwangu. “Aa, kwa hivyo hiyo ndiyo jinsi ya kuingia katika ufalme wa mbinguni!” Niliwaza. “Ni sasa tu ndipo hatimaye ninafahamu kwamba Bwana Yesu alitekeleza kazi ya kuwakomboa wanadamu, sio kazi ya kutuondolea dhambi. Bwana kweli alitusamehe dhambi zetu, lakini asili zetu za dhambi zinasalia zikikita mizizi ndani yetu, na bado mara nyingi tunafanya dhambi na kumpinga Bwana bila kujua. Si ajabu kuwa sijawahi kuweza kujikomboa kutoka kwa minyororo na vizuizi vya dhambi—inatokea kuwa ni kwa sababu sijakubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho!” Na kwa hivyo, niliwaambia dada hao wawili, “Shukrani kwa Bwana! Kwa kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wenu, mwishowe ninafahamu kwamba imani ambayo tumeshikilia—kwamba kila mtu ambaye anaamini katika Bwana moyoni mwake na anamkiri Bwana kwa kinywa chake anaweza kunyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni—ni wazo letu tu na kukisia! Sasa ninaelewa kwamba kazi ambayo Bwana Yesu alitekeleza ilikuwa kazi ya ukombozi, na kwamba Bwana aliyerejea atatekeleza kazi ya hukumu. Yaani, Atatakasa kabisa na kugeuza tabia zetu potovu, na ni wakati huo tu ndipo tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Si ajabu kwamba nimesoma vitabu vingi vya kiroho lakini sijawahi kupata suluhisho la tatizo la utendaji dhambi wa mwanadamu! Kina dada, basi Mungu hutekelezaje kazi ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho? Je, mnaweza kushiriki ushirika zaidi pamoja nami?”

Dada Wang kisha akasema, “Jibu la swali hili limesemwa dhahiri katika maneno ya Mungu, kwa hivyo hebu tusome kifungu cha maneno hayo. Mwenyezi Mungu anasema: ‘Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

“Maneno ya Mungu yanatuambia dhahiri kwamba, katika siku za mwisho, Mungu anaonyesha ukweli wote tunaohitaji ili kupata wokovu kamili, Akihukumu na kuweka wazi asili zetu za kishetani zenye kumpinga Mungu na nafsi zetu potovu. Maneno haya yote ni ukweli, yana mamlaka na uwezo wa Mungu, na yanatufichulia kile Mungu anacho na kile Alicho na pia tabia Yake yenye haki ambayo haistahimili dhambi. Kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kwa ufunuo wa ukweli, tunakuja kuwa na ufahamu fulani wa asili zetu za Shetani na ukweli wa kupotoshwa kwetu na Shetani; tunaona kwamba tumepotoshwa sana na Shetani, kwamba sisi kwa kawaida ni wenye kiburi, wenye majivuno, wasio waaminifu, wachoyo, wenye ubinafsi, walafi, waovu, wenye hamu ya kushinda wengine, na kwamba yote tunayofichua ndani ya nafsi zetu kabisa ni tabia zetu za kishetani. Tukitawaliwa na tabia hizi potovu, sisi humpinga na kumwasi Mungu siku zote ingawa hatukutaka kufanya hivyo. Kwa mfano, tunapofanya kazi na kutoa mahubiri katika makanisa yetu, sisi hurindima kwa hotuba za sauti za juu, na tunaringa na kujiinua ili wengine watustahi na kutuheshimu sana; mara nyingi sisi husema uongo na kuwadanganya wengine ili kulinda maslahi yetu wenyewe, hata tunavuka mipaka kwa kushiriki katika kula njama na kushindana sisi kwa sisi; tunapokabiliana na watu, hafla, vitu au hali ambazo zinatofautiana na dhana zetu wenyewe, sisi daima hutoa madai kwa Mungu yenye kuzidi au kuwa na matamanio ya kupita kiasi, na hatuwezi kujisalimisha kwa mipango na utaratibu wa Mungu. Kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, sisi polepole huja kufahamu ukweli kiasi, tunapata ufahamu kiasi wa kweli kuhusu asili zetu za kishetani na kuhisi chuki ya kweli kwake, na pia tunakuja kuwa na ufahamu kiasi wa kweli kuhusu tabia ya Mungu yenye haki. Tunajua ni watu wa aina gani ambao Mungu anapenda na ni watu wa aina gani Anaowachukia na pia ni aina gani ya ufuatiliaji unapatana na mapenzi Yake. Tunajifunza utambuzi fulani kati ya mambo chanya na hasi. Mara tunapoelewa mambo haya, tunakuwa tayari kuiacha miili yetu kwa dhati na kutenda kulingana na maneno ya Mungu. Polepole, baada ya muda, shauku ya kumcha na kumpenda Mungu huibuka ndani yetu, tunakombolewa kutoka kwa minyororo na vizuizi vya tabia zetu potovu na za kishetani, na tunatoa madai machache kwa Mungu yenye kuzidi. Tunaanza kuwa na uwezo wa kuchukua nafasi yetu kama viumbe walioumbwa na kutekeleza wajibu wetu, tunajisalimisha kwa mipango na utaratibu wa Mungu, na tunaanza kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu wa kweli. Tunapopitia kazi ya Mungu, tunakuja kuwa na utambuzi mkubwa wa ukweli kwamba njia pekee ya sisi kuingia katika ufalme wa mbunguni ni kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya kuhukumu na kuadibu katika siku za mwisho, kufuatilia ukweli, kupata ufahamu wa Mungu na ufahamu wetu, na tabia zetu kubadilishwa.”

Kusikia maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ushirika wa dada kuliniletea hata uwazi mkuu zaidi wa ndani. Ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni wa vitendo mno na kweli ni kile tunachohitaji sisi wanadamu potovu. Ni kwa kukubali na kupitia kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ndio tu tutaweza kutupa minyororo na vizuizi vya tabia zetu potovu sasa na kwa mara ya mwisho! Sikuweza kujizuia kushusha pumzi, na kusema, “Nimeamini katika Bwana kwa muda wa miaka mingi na bado, mimi daima hufanya dhambi mchana na kisha kukiri dhambi hizo usiku, nikiishi maisha ya kuteseka katika dhambi tu. Mungu asingekuwa ameonyesha ukweli wote ili kumtakasa mwanadamu, Asingekuwa ametuonyesha njia ya kujiondolea tabia zetu potovu, bila shaka ningekuwa nimefungwa kwa kubanwa sana na dhambi kiasi kwamba kamwe singeweza kuwa nimeipata njia ya kuwa na uhuru. Si ajabu Bwana alisema, ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Bwana Yesu alituambia hapo zamani kuwa alikuwa na maneno mengi ya kuonyesha katika siku za mwisho na kwamba angetuongoza kuingia katika ukweli wote. Maneno ya Mwenyezi Mungu yana mamlaka na uwezo, yamefichua ukweli wote na siri zote ambazo nilikuwa nimetaka kufahamu lakini kamwe sikuweza, na yameniaminisha kabisa. Hatimaye, nimepata njia ya kuingia katika ufalme wa mbinguni!” Dada hao wawili waliamkia kwa vichwa kwa furaha.

Kisha nilisema kwa msisimko, “Hii ni sauti ya Bwana. Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi! Kitu ambacho nimekitamani kwa muda mrefu hatimaye kimefanyika, na nina bahati sana, nimebarikiwa sana! Hapo nyuma Bwana Yesu alipozaliwa, Simioni alihisi furaha kubwa alipomwona mtoto Yesu aliyekuwa na umri wa siku nane tu. Kuwa na uwezo wa kupokea kurudi kwa Bwana na kusikia maneno ya Mungu Mwenyewe katika maisha yangu, nimebahatika zaidi hata kuliko Simioni alivyokuwa, na ninamshukuru Bwana sana!” Nilipokuwa nikizungumza, nilizidiwa na hisia na nilitoa machozi ya msisimko. Nilipiga magoti sakafuni kumwomba Mungu lakini nilikuwa nikilia sana kiasi kwamba sikuweza kuzungumza; kina dada waliguswa hadi wakalia pia.

Chukizo ambalo lilikuwa limenitaabisha kwa muda wa miaka mingi sana hatimaye lilikuwa limepata suluhisho lake katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Niliwaza kuhusu jinsi nilivyokuwa nimetafuta kila mahali lakini kamwe sikuweza kupata njia ya utakaso ambayo ingeniongoza hadi katika ufalme wa mbinguni, lakini sasa hatimaye nimeipata. Najua kwamba hii ni neema na wokovu wa Mungu kwangu! Baadaye, kupitia kuhudhuria mikusanyiko na kushirikiana pamoja na kina ndugu kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu, nilikuja kufahamu ukweli zaidi, na nilipata ufahamu fulani wa mapenzi ya Mungu ya kutuokoa. Sasa ningependa kupokea hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu zaidi, kupitia kazi Yake, kujiondolea tabia potovu na kutakaswa pole pole. Shukrani ziwe kwa Mungu!

Iliyotangulia: Bwana Ameonekana Mashariki
Inayofuata: Upendo wa Aina Tofauti

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Neno La Mungu Ni Nguvu Yangu

Na Jingnian, KanadaNimefuata imani ya familia yangu katika Bwana tangu nilipokuwa mtoto, nikisoma Bibilia mara nyingi na kuhudhuria ibada....

Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Na Jingmo, MalaysiaNilikuwa na bahati katika mwaka wa 1997 kukubali injili ya Bwana Yesu na nilipobatizwa, mchungaji aliomba na kunibatiza...

Nimeunganishwa Tena na Bwana

Mwenyezi Mungu anasema, “Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp