Kwa Nini Mungu Anapata Mwili ili Kufanya Kazi Yake ya Hukumu ya Siku za Mwisho?

23/04/2023

Tayari tumezungumza mara chache kuhusu kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Leo tungependa kuangalia ni nani anayefanya kazi hii ya hukumu. Waumini wote wanajua kwamba Mungu atatekeleza hukumu Yake miongoni mwa binadamu katika siku za mwisho, kwamba Muumba atawaonekania binadamu na kuonyesha matamshi Yake yeye binafsi. Hivyo, Mungu anaitekelezaje hukumu hii? Je, ni Roho Wake anayeonekana angani na kunena nasi? Hilo haliwezekani. Bwana Yesu mwenyewe alituambia: “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana(Yohana 5:22). “Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu(Yohana 5:27). Tunaweza kuona kutoka katika hili kwamba kazi ya hukumu inafanywa na “Mwana.” Kwa kutajwa kwa “Mwana wa Adamu,” tunapaswa kujua kuwa huyu ni Mungu mwenye mwili, kwa hivyo hii inamaanisha Anakuja katika mwili katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu. Hili ni jambo muhimu sana! Kwa hivyo mnajua kazi ya hukumu ya siku za mwisho inahusu nini? Kwa nini Mungu awe mwili ili kuitekeleza? Kwa maelezo rahisi, huyu ndiye Mwokozi anayekuja kuwaokoa binadamu. Mungu anapofanyika mwili na kuja duniani, huyu ndiye Mwokozi anayeshuka. Yeye binafsi aniatekeleza kazi ya hukumu kuwaokoa binadamu kutoka dhambini mara moja Kwa kukubali hukumu Yake, unaweza kuwekwa huru kutoka dhambini, utakaswe, na kuokolewa. Kisha utahifadhiwa kupitia katika majanga na hatimaye uingie katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, kukubali kazi ya hukumu ya Mwokozi kunahusiana na matokeo na hatima ya mtu—je, hamwezi kusema kwamba hilo ni jambo muhimu? Waumini wengi wanaweza kuuliza kwa nini Mungu lazima kabisa Awe mwili kwa ajili ya hukumu Yake katika siku za mwisho. Wanafikiri kwamba Bwana Yesu anakuja juu ya wingu katika umbo la roho, kwamba Mungu atanyosha mkono na Atuchukue sote, moja kwa moja hadi katika ufalme—si hilo litakuwa jambo la ajabu? Mawazo ya aina hii si kwamba ni rahisi tu, lakini pia ni yasiyowezekana. Mnapaswa kujua kwamba Mungu ana tabia takatifu na yenye haki. Je, anaweza kuwachukua wenye dhambi katika ufalme Wake? Sote tunaufahamu mstari huu wa Biblia, “Bila utakatifu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana(Waebrania 12:14). Kila mtu ni mwenye dhambi, na anatenda dhambi kila mara. Mungu hawezi kumchukua mwanadamu moja kwa moja hadi katika ufalme—hivyo sivyo Anavyotuokoa. Mungu anawachukia wenye dhambi, na hawana sifa za kumwona Mungu. Hakuna shaka kuhusu hili. Kwa hivyo basi Mwokozi anakujaje kuwaokoa binadamu katika siku za mwisho? Kwanza, Anafanya hukumu Yake ili kututakasa kutokana na upotovu, Akituokoa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani, na kisha kutupeleka katika ufalme. Mungu hawezi kukuokoa wewe kutokana na majanga, sembuse kukupeleka katika ufalme ikiwa dhambi yako haijatatuliwa. Majanga tayari yameanza na kila mtu anahisi kwamba dunia inaisha, kana kwamba kifo kinakaribia. Kila mtu anasubiri Mwokozi aje kuwaokoa binadamu, hivyo kumkubali Yeye na kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho ni jambo muhimu sana! Hapa kuna jambo muhimu kuhusu ikiwa waumini wataokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Lakini kwanza hebu tuzungumze kuhusu kazi ya hukumu ya siku za mwisho ni nini. Watu wa kidini hufikiria hukumu ya siku za mwisho kuwa kitu rahisi sana, na kwa kutajwa kwa “hukumu,” wanahisi hakika kwamba itafanywa na Bwana Yesu katika umbo la roho, kwamba Bwana atakuja na kukutana nasi na kutuchukua tuingie katika ufalme, kisha wasioamini watahukumiwa na kuangamizwa. Kwa kweli, hapo wamekosea pakubwa. Kosa lao liko wapi? Kila wakati Mungu anapokuja kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu, kwa kweli ni ya vitendo sana, ya kweli sana, si ya kimuujiza. Zaidi ya hayo, wanapuuza unabii muhimu zaidi wa kibiblia kuhusu ujio wa Bwana—unabii kuhusu Mungu kuwa mwili kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu. Bwana Yesu alisema dhahiri shahiri: “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana(Yohana 5:22). “Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). Na kuna 1 Petro 4:17: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu.” Je, unabii huu hauko dhahiri kabisa? Bwana anakuwa mwili katika siku za mwisho kama Mwana wa Adamu, akionyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu. Hakuna shaka juu ya hili. Kazi ya hukumu si jinsi watu wanavyofikiri, Mungu akiwachukua waumini moja kwa moja hadi mbinguni, kisha kuwahukumu na kuwaangamiza wasioamini, na iishie hapo. Si rahisi hivyo. Hukumu ya siku za mwisho huanza na nyumba ya Mungu na inatekelezwa kwanza kati ya wale wanaokubali hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Yaani, Mwana wa Adamu katika mwili anakuja duniani, Akionyesha ukweli mwingi ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, Akiwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika ukweli wote. Hii ni kazi ya Mwokozi katika siku za mwisho, na Mungu alishapanga hili zamani sana. Na wasioamini watahukumiwa moja kwa moja na kuangamizwa kupitia majanga. Sasa, Mwokozi tayari amekuja kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, akionyesha ukweli wote unaohitajika kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, Akifanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Ukweli huu ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu umeutikisa ulimwengu mzima, na karibu kila mtu kutoka kila taifa amesikia kuuhusu. Tunaweza kuona kwamba unabii wa Biblia kuhusu kurudi kwa Bwana umetimizwa kikamilifu. Kwa bahati mbaya, bado kuna watu wengi ambao hawaelewi kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho na wanaendelea tu kutumaini kuona kitu kisicho cha kawaida: Mungu akionekana na kuzungumza akiwa angani. Hili ni jambo lisiloshikika. Hebu tuangalie kile ambacho Mwenyezi Mungu anasema ili tuelewe vyema jinsi ambavyo Mungu hutekeleza hukumu Yake.

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya Mungu ya hukumu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Sasa tunapaswa kuelewa jinsi ambavyo Mungu anafanya hukumu Yake ya siku za mwisho. Kimsingi ni kupitia katika kuonyesha ukweli, na kuutumia kuwahukumu, kuwatakasa, na kuwaokoa binadamu. Yaani, katika siku za mwisho Mungu hutumia kazi hii ya hukumu kuutakasa upotovu wa mwanadamu, kuliokoa na kulikamilisha kundi la watu, kulikamilisha kundi la watu wenye moyo mmoja na akili moja na Mungu. Haya ni matunda ya mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000, na hiki ndicho kiini cha kazi ya hukumu ya siku za mwisho. Ndiyo maana Mwokozi, Mwenyezi Mungu, anaonyesha ukweli mwingi sana, Akifichua na kuhukumu tabia zote potovu za mwanadamu, Akiwasafisha na kuwabadilisha watu kupitia katika ushughulikiaji, upogoaji, majaribio, na usafishaji, Akitatua chanzo cha dhambi ya mwanadamu, na kuturuhusu kuepuka dhambi kikamilifu na kuepuka nguvu ya Shetani, kukuza utii na uchaji kwa Mungu. Hili linaweza kuwa na utata kidogo kwa baadhi ya watu. Bwana Yesu aliwakomboa wanadamu, kwa hivyo kwa nini Mungu anahitaji kuonyesha ukweli ili kuwahukumu wanadamu katika siku za mwisho? Hawawezi kuona jinsi ambavyo mwanadamu amepotoshwa kwa kina na Shetani. Mungu anamwokoa mwanadamu katika siku za mwisho kwa kutatua tabia zetu potovu. Hili si jambo rahisi. Si tu kuhusu kukiri dhambi zetu, kuungama na kutubu kwa Bwana, na liishie hapo. Tabia potovu ni tofauti na dhambi. Hazihusu tabia ambazo ni za dhambi, lakini ni kitu kinachoishi ndani ya akili zetu, ndani ya nafsi zetu. Ni tabia ambazo zimekita mizizi ndani yetu, kama vile kiburi, ujanja, uovu, na kuchukia ukweli. Tabia hizi potovu zimefichika ndani kabisa ya mioyo ya watu na ni vigumu sana kwetu kuzipata. Wakati mwingine hakuna aina yoyote ya dhambi ya waziwazi na mtu anaweza kusema mambo ya kupendeza, lakini ana nia za hila na za kudharauliwa moyoni mwake, akiwadanganya na kuwapotosha wengine. Hili ni tatizo katika tabia yake. Bila hukumu na ufunuo wa muda mrefu wa Mungu, pamoja na ushughulikiaji, upogoaji na majaribio, watu hawataona hili, sembuse kubadilika. Ni nani kati ya waumini wa Bwana ambaye ameepuka dhambi baada ya kuungama dhambi zake maishani mwake mwote? Hakuna hata mmoja. Na kwa hivyo, kupata tu ukombozi wa Bwana bila hukumu ya siku za mwisho humruhusu tu mtu atambue tabia yake ya dhambi, lakini asili yake ya dhambi, kiini cha dhambi zake—yaani, tabia potovu iliyokita mizizi ndani yake—siyo kitu ambacho watu wanakiona, sembuse kukirekebisha. Hakuna anayeweza kukana hili! Kwa hivyo, ni kupitia tu kwa Mungu mwenyewe kupata mwili na kutekeleza hukumu katika siku za mwisho, Akionyesha ukweli mwingi, na kupitia katika ufunuo Wake wa muda mrefu na hukumu, ndiyo watu wanaweza kuona kwa uwazi ukweli wa upotovu wao na kujua kiini chao wenyewe, na ni kupitia katika hukumu hii ndiyo wanakuja kujua haki na utakatifu wa Mungu, na kukuza mioyo ya uchaji kwa Mungu. Hii ndiyo njia pekee ya kutupilia mbali upotovu na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu. Kwa hivyo, ni kwa Mungu kupata mwili tu na kuonyesha ukweli ili kufanya hukumu katika siku za mwisho ndiyo matunda haya yanaweza kupatikana. Wengine wanaweza kuuliza: Kwa nini Mungu Mwenyewe lazima afanye hili katika mwili? Kwa nini hawezi kufanya hivyo katika umbo la roho? Hebu tutazame video ya usomaji wa maneno ya Mungu ili kila mtu apate ufahamu bora wa jambo hili.

Mwenyezi Mungu anasema, “Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili. Kama Mungu hangegeuka na kupata mwili, hakuna mtu mwenye mwili ambaye angepokea wokovu huo mkuu, wala hakuna mtu hata mmoja ambaye angeokolewa. Kama Roho wa Mungu angefanya kazi moja kwa moja kati ya mwanadamu, mwanadamu angepigwa ama kubebwa kabisa kama mfungwa na Shetani kwani mwanadamu hawezi kushirikiana na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. Ikiwa hukumu ingefanywa moja kwa moja na Roho wa Mungu, basi isingekuwa inajumuisha wote. Aidha, kazi kama hiyo itakuwa vigumu kwa mwanadamu kuikubali, maana Roho hawezi kukutana uso kwa uso na mwanadamu, na kwa sababu hii, matokeo hayawezi kuwa ya haraka, sembuse mwanadamu hataweza kuona kwa uwazi kabisa tabia ya Mungu isiyokosewa. Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine. Ikiwa kazi hii ingefanywa na Roho wa Mungu, basi usingekuwa ushindi dhidi ya Shetani. Roho kiasili huwa ameinuliwa sana kuliko viumbe wenye mwili wa kufa, na Roho wa Mungu ni mtakatifu kwa asili, na anaushinda mwili. Ikiwa Roho angefanya kazi hii moja kwa moja, Asingeweza kuhukumu kutotii kote kwa mwanadamu, na asingeweza kufichua hali nzima ya mwanadamu ya kutokuwa na haki. Kwa maana kazi ya hukumu pia inafanywa kwa mitazamo ya mwanadamu juu ya Mungu, na mwanadamu hajawahi kuwa na dhana yoyote juu ya Roho, na hivyo Roho hana uwezo wa kufunua hali ya mwanadamu ya kutokuwa na haki, wala kuweza kuweka wazi kabisa hali hiyo ya kutokuwa na haki. Mungu mwenye mwili ni adui wa wale wote wasiomjua. Kupitia kuhukumu dhana za mwanadamu na kumpinga, Anafunua hali yote ya kutotii ya mwanadamu. Matokeo ya kazi Yake katika mwili yapo dhahiri zaidi kuliko yale ya kazi ya Roho. Na hivyo, hukumu ya wanadamu wote haifanywi moja kwa moja na Roho, bali ni kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu mwenye mwili anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu, na Mungu mwenye mwili anaweza kumshinda kabisa mwanadamu. Katika uhusiano wake na Mungu mwenye mwili, mwanadamu huwa anapiga hatua kutoka katika upinzani na kuwa mtii, kutoka katika mateso na kukubaliwa, kutoka katika mitazamo na kuwa na maarifa, na kutoka kukataliwa hadi upendo. Haya ni matokeo ya kazi ya Mungu mwenye mwili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Sasa nadhani sote tunaelewa vyema zaidi kwa nini Mungu mwenyewe aifanye kazi ya hukumu katika mwili. Ni kwa sababu Mungu kufanyika mwili ndiyo njia pekee ya Yeye kuingiliana na watu kivitendo, kuzungumza na kushiriki juu ya ukweli nasi popote na wakati wowote, kutufichua na kutuhukumu kulingana na upotovu tunaofichua, na kutunyunyizia, kutuchunga, na kututegemeza kulingana na mahitaji yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo Anaweza kuwasilisha waziwazi mapenzi na mahitaji ya Mungu. Je, kusikia kuhusu njia ya Mungu na kuelewa ukweli Anaoonyesha moja kwa moja kwa manufaa zaidi kwa kupata kwetu ukweli na wokovu? Zaidi ya hayo, Mungu anapofanyika mwili kama mtu wa kawaida, wa kila siku, je, unaweza kusema watu wanaweza kuwa na mawazo, kwamba wanaweza kuwa waasi? Bila shaka. Wakati watu wanaona sura ya nje ya kawaida ya Kristo, mawazo, uasi, na upinzani wao hutokea, na hata kama hawasemi chochote au kuruhusu mambo haya yaonekane, bila kujali jinsi wanavyojifanya, Mungu anatazama, na hakuna majaribio ya kuficha hili yanayoweza kufanikiwa. Mungu hufichua chochote kilichofichwa ndani ya watu, akigonga ndipo. Kwa hivyo, ni Mungu katika mwili pekee anayeweza kuwafichua watu vyema zaidi, Akifichua uasi na upinzani wao. Hili ni la manufaa zaidi kwa kazi ya hukumu. Na kama Mungu angetamka maneno moja kwa moja kupitia kwa Roho, je? Watu hawangeweza kuona, kugusa, au kusogea karibu na Roho Wake, na Roho Wake kuzungumza kungetisha. Basi wanawezaje kuiweka wazi mioyo yao kwa Mungu, au kujifunza ukweli? Na ni nani angethubutu kuwa na mawazo anapokabiliwa na Roho? Nani angethubutu kufichua upotovu, au kuwa muasi au mpinzani? Hakuna mtu angeweza. Kila mtu angekuwa akitetemeka kwa woga, akisujudu, nyuso zikiwa na woga. Watu wakiwa katika hali hiyo ya hofu, ukweli kuwahusu ungewezaje kufichuliwa? Hakuna hata moja kati ya mawazo au uasi wao ambao ungeonyesha, kwa hivyo hukumu ingefanywaje? Kungekuwa na ushahidi gani? Hii ndiyo sababu kazi ya Roho wa Mungu haikuweza kuibua tabia halisi zaidi za watu, kuwafunua, na kazi ya Mungu ya hukumu haingeweza kukamilika. Na kupata mwili kwa Mungu kunafaa zaidi kwa kazi ya hukumu kuliko Roho Wake. Tunaweza kumwona Mwenyezi Mungu akiishi miongoni mwa wanadamu, pamoja nasi kuanzia asubuhi hadi usiku. Kila hatua yetu, kila wazo letu, kila aina ya upotovu tunaofichua, yote yanaonekana na kushikwa kikamilifu na Mungu. Anaweza kuonyesha ukweli ili kutufunua na kutuhukumu wakati wowote na mahali popote, na kuweka wazi upotovu, mawazo na fikira zetu kuhusu Mungu, pamoja na asili yetu ya kumpinga na kumsaliti Mungu. Tunaposoma maneno ya Mungu, ni kana kwamba tuko ana kwa ana na Yeye tukihukumiwa. Inahuzunisha na kufedhehesha sana, na tunaona ukweli wa upotovu wetu kwa uwazi sana ndani ya maneno Yake. Tunajichukia na kujuta kutoka moyoni na kuhisi hatustahili kuishi mbele za Mungu. Kupitia hukumu ya Mungu, tunaona pia jinsi alivyo mwenye haki na mtakatifu wa ajabu, na kwamba Yeye kwa kweli huona ndani ya mioyo na akili zetu. Fikira na mawazo potovu yaliyo katika vina vya mioyo yetu, mengine ambayo hata hatujayatambua, yanafunuliwa na kuhukumiwa na Mungu, moja baada ya nyingine. Wakati mwingine ni kupitia shutuma kali na laana, ikituruhusu tuione tabia ya Mungu isiyokosewa, na kisha hatimaye, tutakuja kumcha Mungu. Bila kupitia hukumu ya Mungu, hakuna hata mmoja wetu ambaye angejua haki au utakatifu wa Mungu, na hakuna ambaye angeweza kuona kwamba watu wanapoishi kulingana na asili zao za kishetani, wao ni wa aina inayompinga Mungu, kwamba wanastahili laana na adhabu ya Mungu. Ni kwa msaada wa hukumu, kuadibu, na majaribio ya Mungu kwamba tunaweza kutubu kwa kweli, hatimaye kutupilia mbali upotovu, na kutakaswa na kubadilishwa. Na kwa kumfuata Kristo hadi siku ya leo, tunaweza kuona kwamba Mungu mwenye mwili anaishi miongoni mwetu, mnyenyekevu na aliyefichwa, Akionyesha ukweli mwingi sana kwa bidi na uvumilivu kabisa kwa ajili ya kutuokoa kikamilifu sisi wanadamu potovu. Kama si Mungu mwenye mwili kuja binafsi kutuhukumu na kututakasa, Akitupa ukweli wote, watu waasi na wapotovu kama sisi bila shaka tungeondolewa na kuadhibiwa. Basi tungewezaje kuokolewa? Upendo wa Mungu kwa wanadamu ni mkuu sana, na Mungu ni mzuri sana. Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli miongoni mwetu, akituongoza, kututegemeza, Akiandamana na wanadamu kwa njia za vitendo. Hii ndiyo nafasi yetu pekee ya kusikia sauti ya Mungu na kuuona uso Wake, kuhukumiwa na kutakaswa na Mungu, kujifunza na kupata ukweli mwingi na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu. Wale wanaofaidika zaidi kutokana na kazi ya Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho ni kundi hili letu linalomfuata Kristo. Kile tunachopata kutoka kwa Mungu hakika hakina kipimo. Kama tu maneno ya Mwenyezi Mungu yanavyosema, “Kitu kizuri zaidi kuhusu kazi Yake katika mwili ni kwamba anaweza kuacha maneno sahihi na ushawishi, na mapenzi Yake mahususi kwa mwanadamu kwa wale wanaomfuata, ili kwamba hapo baadaye wafuasi Wake waweze kueneza kazi Yake yote katika mwili kwa usahihi zaidi na kwa udhabiti na mapenzi Yake kwa wanadamu wote kwa wanaoikubali njia hii. Ni kazi ya Mungu mwenye mwili pekee miongoni mwa wanadamu ndiyo inayokamilisha ukweli wa Mungu kuwepo na kuishi pamoja na mwanadamu. Ni kazi hii pekee ndiyo inayotimiza shauku ya mwanadamu kuutazama uso wa Mungu, kushuhudia kazi ya Mungu, na kusikia neno la Mungu. Mungu mwenye mwili anahitimisha enzi ambapo Yehova alionekana mgongo tu, na pia anahitimisha enzi ya mwanadamu kuamini katika Mungu asiye dhahiri. Kwa umahususi, kazi ya Mungu mwenye mwili wa mwisho inawaleta wanadamu wote katika enzi ambayo ni halisi zaidi, ya utendaji zaidi na nzuri zaidi. Hahitimishi tu enzi ya sheria na mafundisho ya kidini; la umuhimu zaidi, Anamfunulia mwanadamu Mungu ambaye ni halisi na wa kawaida ambaye ni mwenye haki na mtakatifu, ambaye anafungua kazi ya mpango wa usimamizi na kuonyesha siri za hatma ya mwanadamu, ambaye alimuumba mwanadamu na kuhitimisha kazi ya usimamizi, na ambaye amebakia sirini kwa maelfu ya miaka. Anaihitimisha enzi ya Mungu asiye yakini, Anaihitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanatamani kuutafuta uso wa Mungu lakini wanashindwa, Anahitimisha enzi ambayo kwayo wanadamu wote wanamtumikia Shetani, na Anawaongoza wanadamu wote katika enzi mpya kabisa. Haya yote ni matokeo ya Mungu mwenye mwili kwa niaba ya Roho wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).

Mwenyezi Mungu amekuwa akionyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho kwa miongo mitatu kamili sasa. Watu wateule wa Mungu wametakaswa tabia zao potovu kupitia hukumu ya maneno Yake, na Mungu amekamilisha kundi la washindi kabla ya majanga—wao ni malimbuko. Wamedumu katika kufuata na kutoa ushuhuda kwa Kristo hata kupitia ukandamizaji mkali wa joka kubwa jekundu. Wamemshinda Shetani na kutoa ushahidi wa ajabu kwa Mungu. Hii inatimiza unabii wa Ufunuo: “Hawa ndio waliotoka katika taabu kubwa, na wameosha mavazi yao, na kuyageuza kuwa meupe katika damu ya Mwanakondoo(Ufunuo 7:14). Wakati Mungu mwenye mwili amekuwa Akionyesha ukweli, viongozi na wapinga Kristo, wakubwa kwa wadogo, kutoka kila madhehebu, wamefunuliwa kabisa. Wanaona kwamba Mwenyezi Mungu anaonekana kuwa mtu wa kawaida, kwamba Yeye si Roho, na hivyo wanampinga na kumshutumu kwa makusudi. Ili kuhifadhi hadhi na maisha yao wenyewe, wanakuwa wazimu wakiwazuia waumini wasiisikie sauti ya Mungu na kuchunguza njia ya kweli. Nyuso za kweli za watu hawa za kuchukia ukweli zimefunuliwa, na wamelaaniwa na kuondolewa. Bila Mungu kufanyika mwili, wangebaki wamefichika makanisani, wakiendelea kunyonya damu ya waumini, wakila matoleo ya Mungu, wakiwapotosha na kuwaharibu watu wengi sana. Kwa sababu Mungu anafanya hukumu Yake katika mwili, wapinga Kristo na wasioamini, wale wanaopenda au wasiopenda ukweli, wale wanaochukia au kudharau ukweli, wote wamefichuliwa. Na wale wanaopenda na kuelewa ukweli wameona waziwazi sura mbaya ya Shetani na jinsi Shetani anavyofanya kazi dhidi ya Mungu na kuwapotosha wanadamu. Wamemkataa kabisa na kumtelekeza Shetani, na kumgeukia Mungu kikamilifu. Hatimaye Mungu anawatuza wema na kuadhibu waovu, Akitumia maafa makubwa kumaliza nguvu zote za uovu zinazofanya kazi dhidi ya Mungu, hatimaye kuitamatisha enzi hii nzee ya Shetani kushikilia mamlaka, na kisha kuwaleta wale ambao wametakaswa kupitia hukumu Yake kwenye hatima nzuri. Hili linatimiza unabii wa Ufunuo: “Yule aliye dhalimu, basi aendelee kuwa dhalimu; na yeye aliye mtakatifu, na awe mtakatifu bado; na yeye aliye mwenye haki, awe mwenye haki bado: na yeye aliye mtakatifu, awe mtakatifu bado(Ufunuo 22:11). “Tazama, Naja upesi; na Nina thawabu Yangu, kumpa kila mwanadamu kulingana na vile matendo yake yatakuwa(Ufunuo 22:12).

Hebu tutamatishe kwa kifungu kingine kutoka kwa Mwenyezi Mungu. “Wengi wana hisia mbaya kuhusu kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu angefanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Hata hivyo, lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi sana matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu tu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni utoneshaji wa hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu, ambalo kwalo Nasema ni wazi nani atapata hasara mwishowe. Nawasihi nyote msijichukulie kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Ni vipi ambavyo ninyi ni bora zaidi kuliko wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu tu ya ‘mchango’ ambao umetoa, na utajawa na majuto mengi kwa kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje tu kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani kipitishe hukumu juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambazwa kote ulimwenguni hadi miisho ya dunia. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu aje kukupeleka mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni kipande sugu cha mti mkavu. Yesu hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Hasha, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kunyakuliwa ni Nini Hasa?

Miaka 2,000 iliyopita, baada ya Bwana Yesu kusulubishwa na kukamilisha kazi Yake ya ukombozi, Aliahidi kwamba Atarudi. Tangu wakati huo,...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp