106 Nina Furaha Kuu Kupata Upendo wa Mungu

1 Kristo wa siku za mwisho huonekana duniani na kuleta njia ya uzima wa milele. Kwa kuelewa ukweli katika neno la Mungu, nina mwelekeo maishani. Sikuweza kujiondolea vifungo vya uovu nilipomwamini Bwana. Sasa baada ya kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, nakuja kujijua. Natii majaribu na usafishaji wa Mungu, na tabia yangu ya maisha imebadilishwa. Kwa kutakaswa na hukumu ya Mungu, naona upendo Wake wa kweli. Sasa naishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu, hatimaye kupata wokovu wa Mungu. Ee Mungu, Upendo Wako ni wa kweli na unapendeza sana. Umeushinda moyo wangu. Nakupenda kwa dhati sana.

2 Moyo wangu ni mwepesi na roho yangu ina furaha, neno la Mungu linanitia moyo. Kwa kusoma neno la Mungu, kushiriki kuhusu ukweli, moyo wangu unafurahi. Kwa kuelewa ukweli na kutenda maneno ya Mungu, nina njia ya kufuata katika kila jambo. Nimeepuka kabisa ushawishi wa Shetani, na moyo wangu umewekwa huru. Ninafurahi sana kupata upendo wa Mungu, ni raha sana kufurahia upendo Wake. Upendo wa Mungu unaujaza moyo wangu, mimi ni mtu mwenye furaha zaidi. Nimetekeleza wajibu wa mwanadamu kwa uaminifu, ili Mungu apate kufarijiwa karibuni. Ukweli huniweka huru, ili niweze kuishi mbele ya Mungu maisha yangu yote. Wale wanaompenda Mungu ni watu wenye furaha zaidi.

3 Mwenyezi Mungu! Ulinipa maisha ya furaha. Nilitoroka maisha ya zamani ya upotovu, uharibifu, na matupu. Nina furaha sana kupata ukweli na kuongozwa na maneno ya Mungu. Nampenda na kumcha Mungu moyoni mwangu, na daima naishi katika nuru. Wokovu Wako ni mkubwa mno, siwezi kamwe kusema ya kutosha. Mpendwa Mwenyezi Mungu! Nitakupenda siku zote. Upendo Wako umeushinda moyo wangu, nataka tu kukupenda kwa uaminifu. Upendo Wako hubaki moyoni mwangu daima, na moyo wangu wote ni Wako. Nitakupenda Wewe na kukusifu milele.

Iliyotangulia: 105 Nina Furaha Sana Kuishi Mbele za Mungu

Inayofuata: 108 Imani Katika Mungu ni ya Furaha Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

901 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki