206 Hukumu ya Mungu ni Baraka

1

Ee Mungu, Unaonyesha ukweli kuhukumu na kuwatakasa wanadamu, ukifunua upendo Wako.

Ulipofunua asili ya binadamu kwa maneno makali, nilishindwa kuuelewa moyo Wako.

Sikukuelewa, nikakushuku na kujikinga dhidi Yako, ambalo liliuvunja moyo Wako.

Nilikuwa mjinga na mpumbavu sana kutojua kwamba maisha ndani ya maneno Yako ni ya thamani.

Mara nyingi nilipokuwa najisikia dhaifu na hasi, maneno Yako yalinipa imani na nguvu.

Mara nyingi niliposhindwa na kujikwaa, maneno Yako yaliniinua juu tena.

Mara nyingi nilipokuwa na kiburi na asiyetii, maneno Yako yalinihukumu na kuuamsha moyo wangu.

Ni sasa tu ndiyo naona kwamba maneno Yako ni ya thamani sana na kwamba ni ruzuku ya maisha yangu.

2

Unanena maneno, ukiwatolea wanadamu ukweli, njia na uzima.

Unahukumu na kuwatakasa binadamu, ukiwaruhusu watu wapate uzima, hii yote ni baraka Yako.

Kuelewa ukweli na kutupilia mbali upotovu wetu, tunaweza kuishi kwenye nuru.

Kwa kuyategemea maneno Yako, tunasimama imara katika mateso, taabu, majaribu na usafishaji..

Tunalia tunaposhindwa na kujikwaa, lakini maneno Yako yatufariji na kutuongoza.

Kukufuata Wewe, tunapopitia dhiki na majaribio, ingawa tumeteseka tumepata ukweli.

Tabia yetu imebadilika kidogo, tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu yote kwa ajili ya neema Yako.

Neno Lako la uzima daima litakuwa msingi wa kuwepo kwetu.

3

Wewe ni ukweli, njia na uzima, Unazunguka vitu vyote, Unatoa kila kitu.

Maneno Yako yote ni ukweli, yote ni ya muhimu katika maisha yetu.

Unalipa gharama yoyote kututakasa na kutukamilisha.

Kwa unyenyekevu na kujificha, Unafanya kazi kati ya wanadamu, upendo Wako wa mwanadamu ni wa kina sana.

Hukumu Yako ni baraka, tumeonja hili kwa kina.

Tumefurahia sana upendo Wako mwingi kiasi kwamba hatutaweza kamwe kulipa.

Ingawa kuna mateso katika kukufuata, tumepata mengi sana.

Tumepata ukweli na uzima kutoka Kwako, tutakupenda na kuwa na ushuhuda Kwako milele.

Iliyotangulia: 205 Sitaacha Majuto Moyoni Mwangu

Inayofuata: 207 Sitawahi Tena Kujitenga na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki