207 Sitaacha Majuto Moyoni Mwangu

1

Kwa miaka mingi nilimwamini Bwana, lakini sikujua kufuatilia ukweli.

Nilishikilia taratibu za dini, imani yangu katika Mungu ilikuwa ya wasiwasi na ya dhahania.

Nilielewa kidogo kuhusu Biblia, na kwa hivyo nilidhani nilimjua Mungu.

Nilitumia rasilmali na kuteseka kwa ajili ya Bwana ili kupewa thawabu, ili kuvikwa taji.

Moyo wangu ulijaa dhana na mawazo kuhusu Mungu.

Moyo wangu ulitamani raha ya neema na baraka za Mungu.

Nilipoona matamshi ya Mwana wa Adamu mwenye mwili,

nilitumia maneno ya Biblia kupima kazi ya Mungu

Nilishikilia dhana za dini, na nikadhani huu ulikuwa uaminifu kwa Bwana.

Matendo yangu yalitofautianaje na ya Mafarisayo?

2

Nilipopitia hukumu ya maneno ya Mungu, ilikuwa kama kuamka kutoka ndotoni.

Niliona jinsi mtazamo wangu kuhusiana na Mungu ulivyokuwa bila busara na mantiki.

Bila ukweli, nilitumia dhana na mawazo mara nyingi kumpima Mungu.

Pia nilimhukumu Kristo na nikamkana, kana kwamba ni mtu wa kawaida.

Niliposhindwa na maneno ya Mungu tu ndipo nilipoona kuonekana kwa Mungu.

Nilijidharau kwa kuwa mwenye kiburi sana na kutoweza kumjua Mungu.

Nilipofikiri juu ya uasi na upinzani wangu wa zamani, nilijawa na majuto.

Nilipoinama mbele za Mungu, nilihisi majuto mengi mno.

Niliamua kufuatilia ukweli na kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu.

Nilidhamiria moyo wangu kumfuata Mungu, na sitapumzika hadi nitakapopata ukweli.

Iliyotangulia: 206 Sitawahi Tena Kujitenga na Mungu

Inayofuata: 208 Hukumu ya Mungu ni Baraka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp