36 Mtukuze Mwenyezi Mungu Kwa Sauti Kubwa

1

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho,

anaonekana Mashariki mwa ulimwengu.

Yeye ananena ukweli ili kuwaokoa wanadamu,

Yeye ni muonekano wa Mwokozi.

Watu wa Mungu wanaisikia sauti Yake, wanainuliwa hadi kiti Chake cha enzi.

Tunakula na kunywa maneno ya Mungu,

tunajua ukweli na siri,

tumeshindwa kabisa na maneno ya Mungu.

Kupitia kwa majaribio na usafishaji,

tunateseka maumivu makali, upotovu wetu unatakaswa.

Kwa kukubali mafundisho ya ufalme,

tunapata ukweli na tunapata uzima.

Tunamtukuza Mwenyezi Mungu kwa sauti kubwa,

kwa maana Yeye hutakasa na kuokoa maisha yetu.

2

Kupitia mateso na majaribio,

tunaona sura mbaya ya Ibilisi.

Shetani anatumika kumkamilisha mwanadamu,

hivyo mwanadamu hufahamu ukweli na humjua Mungu.

Tunamchukia Shetani kikamilifu, tutamfuata Mungu mpaka hatima.

Mungu hunena ukweli na huwashinda wanadamu,

ingawa upotovu una kina kirefu.

Maneno ya Mungu huhukumu na hutakasa

kizazi cha Joka kubwa jekundu.

Katika nchi ya Joka, washindi hufanywa.

Kwa kukubali mafundisho ya ufalme,

tunapata ukweli na tunapata uzima.

Tunamtukuza Mwenyezi Mungu kwa sauti kubwa,

kwa maana Yeye hutakasa na kuokoa maisha yetu.

3

Mungu alishinda Shetani kikamilifu,

na utukufu wote Mungu ameupata.

Haipingwi kwamba neno la Kristo

ni ukweli, uzima na njia.

Mwanadamu hana budi kupenda na kuheshimu sana unyenyekevu wa Mungu kwa hakika.

Tabia ya Mungu ni ya haki,

kwa uchaji tunamtazamia Yeye.

Matendo yake yashangaza, magumu kuelewa,

bila hatima tunamsifu Yeye kikamilifu.

Nguvu za Mungu zinafanya nchi zote kutii na kumtukuza Yeye.

Kwa kukubali mafundisho ya ufalme,

tunapata ukweli na tunapata uzima.

Tunamtukuza Mwenyezi Mungu kwa sauti kubwa,

kwa maana Yeye hutakasa na kuokoa maisha yetu.

4

Tunapata njia ya uzima wa milele

na kumsifu Mungu kwa sauti za juu.

Kwa kukubali mafundisho ya ufalme,

tunapata ukweli na tunapata uzima.

Tunamtukuza Mwenyezi Mungu kwa sauti kubwa,

kwa maana Yeye hutakasa na kuokoa maisha yetu.

Iliyotangulia: 35 Amkeni na Kumchezea Mungu

Inayofuata: 37 Kazi Kuu ya Mungu Imekamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp