62 Kujituliza Mbele za Mungu

1

Najituliza mbele za Mungu,

naomba na kumfunulia moyo wangu.

Kwa uaminifu najifunua kabisa,

nazungumza kwa dhati.

Namkabidhi Mungu ugumu na upungufu wangu

na kumtegemea Yeye.

Naomba Mungu anipe nuru na kuniangaza

nielewe mapenzi Yake.

Kupitia kutafuta kwa dhati

napata nuru ya Roho Mtakatifu ndani yangu.

Ninapoelewa ukweli,

napata utambuzi

na kuwa na njia ya kutenda.

Kwa mwongozo wa Mungu naishi katika nuru,

moyo wangu umejaa furaha na utamu.

Najituliza mbele za Mungu.

2

Kimya mbele ya Mungu,

natafakari maneno Yake.

Naona upotovu wa binadamu,

jinsi tumepoteza mfanano wote wa kibinadamu.

Na ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu

najitafakari:

Nia ziko ndani ya maneno yangu,

nasema uwongo sana.

3

Katika wajibu wangu,

sina kanuni za ukweli,

nafuata sheria katika vitendo vyangu.

Sina upendo kwa ndugu,

nina kiburi na ubinafsi.

Bado nahitaji kukubali Zaidi

hukumu ya Mungu, majaribio, na utakaso.

Najituliza mbele za Mungu.

4

Kujituliza mbele ya Mungu

na kutafuta ukweli,

Polepole nakua katika maisha yangu.

Kujituliza mbele ya Mungu

na kujitafakari,

napata toba ya kweli.

Mimi mara nyingi hujituliza mbele ya Mungu

na kuwasiliana na Yeye kweli.

5

Inaniruhusu kumcha Mungu na kuepuka maovu,

na kuishi mbele Zake.

Katika kila kitu nakubali

ukaguzi wa Mungu;

naishi katika nuru.

Utakaso wafanyika ndani yangu,

na naishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli.

Najituliza mbele za Mungu.

6

Mara nyingi nifikiriapo maneno ya Mungu,

nimevuna mavuno mengi.

Roho Mtakatifu amenipa nuru

kuelewa hata ukweli zaidi.

Kutimiza wajibu wangu,

niko mtulivu na napata raha.

Kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, napokea

baraka na upendo Wake.

Kupitia kutafuta kwa dhati

napata nuru ya Roho Mtakatifu ndani yangu.

Ninapoelewa ukweli,

napata utambuzi

na kuwa na njia ya kutenda.

Kwa mwongozo wa Mungu naishi katika nuru,

moyo wangu umejaa furaha na utamu.

Najituliza mbele za Mungu.

Moyo wangu umejaa furaha na utamu.

Najituliza mbele za Mungu.

Iliyotangulia: 61 Kutiwa Moyo na Upendo wa Mungu

Inayofuata: 63 Tunapaswa Kukimya Mbele za Mungu Daima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp