110 Kutembea kwenye Njia Sahihi ya Maisha ya Binadamu

1

Maneno ya Mungu ni ukweli, kadiri niyasomavyo zaidi, ndivyo moyo wangu ung’aavyo zaidi.

Maneno ya Mungu yanafichua siri ya maisha. Ghafla nauona mwanga.

Yote niliyo nayo yanatoka kwa Mungu. Yote ni kwa neema ya Mungu.

Kiitiko

Namfuata Kristo, nafuatilia ukweli na uzima; natembea kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Namfuata Kristo, naipitia kazi ya Mungu Njia inang’aa zaidi kadiri ninavyosonga. Njia inang’aa zaidi kadiri ninavyosonga.

Hukumu na kufunuliwa kwa maneno ya Mungu vyaniruhusu nione upotovu wa mwanadamu.

Zamani niliishi kwa ajili ya mwili katika njia za Shetani, nikipenda raha za dhambi, kama mnyama.

Na nilitamani sana umaarufu na hadhi, nikionja uchungu wa upotovu.

Maneno ya Mungu yaliniamsha, na kutoka gizani nikaona mwanga.

Kiitiko

Namfuata Kristo, nafuatilia ukweli na uzima; Natembea kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Namfuata Kristo, naipitia kazi ya Mungu. Njia inang’aa zaidi kadiri ninavyosonga. Njia inang’aa zaidi kadiri ninavyosonga.

2

Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, Naona upotovu wangu. Kwa kujua ukweli unasafishwa. Ukweli ni wa thamani namna gani!

Kwa kutenda ukweli, kutekeleza wajibu wangu, moyo wangu ni mtulivu na wenye amani.

Nakuwa shahidi katika majaribu na usafishaji. Kwa sababu ya utunzaji na ulinzi wa Mungu.

Kuonja kupendeza Kwake, kupitia dhiki, moyo wangu utampenda Mungu milele.

Sitachanganyikiwa, Maneno ya Mungu yataniongoza. Hukumu Yake imeniokoa; Moyo wangu unamsifu milele.

Kiitiko

Namfuata Kristo, nafuatilia ukweli na uzima; Natembea kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Namfuata Kristo, naipitia kazi ya Mungu. Njia inang’aa zaidi kadiri ninavyosonga. Njia inang’aa zaidi kadiri ninavyosonga.

Iliyotangulia: 109 Maisha ya Mwanadamu Mpya

Inayofuata: 111 Natembea Katika Njia ya Kwenda kwa Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp