157 Kuna Kundi Kama Hili la Watu

1

Tumepitia hukumu na utakaso mbele ya kiti cha Kristo, tumeelewa ukweli na tumewekwa huru.

Ndugu wanapendana, maisha ya kanisa yanaleta furaha isiyo na kifani.

Tabia zetu potovu zimetakaswa, tunaimba na kucheza, na kumsifu Mungu kikamilifu.

Mji mtakatifu ulio mbinguni umekuja ulimwenguni, tunaishi katika kitanda cha furaha.

2

King’ora cha polisi kinasikika kwa mbali, askari wa joka kubwa jekundu wanaingia kwa ghafla mlangoni.

Mlio wa bunduki unasikika, wanamwambia kila mtu asisonge, lakini sote tunakimbia kila upande bila tumaini.

Baadaye tunakusanyika kama kawaida na kula na kunywa maneno ya Mungu, waoga wanatishwa sana.

Wale wanaomtamani Mungu kwa kweli wanasonga mbele licha ya hatari, kuna wale wanaothubutu kuitembea njia hii nyembamba.

3

Jaribio la watendaji huduma linavunja mioyo yetu, kupitia usafishaji machozi yetu yanatiririka hadi mitoni.

Tunakula viapo vya uaminifu kuhudumu hadi mwisho, kupitia kutokuwa na tumaini kwetu tunaona mkono wa Mungu.

Tunapokuwa tayari kuhudumu, Mungu anatugeuza kuwa watu Wake; niko tayari kumfanyia chochote, hata nikiambiwa nife.

Katika mtiririko mkunjufu wa upendo kwa Mungu, kila mteule wa Mungu anampenda.

4

Kifungu baada ya kifugu cha maneno ya Mungu kinaja kutuhukumu kama mvua kubwa, yanachoma mioyo yetu kama upanga mkali.

Sote tumeshindwa na tunasujudu ardhini, tukihisi maumivu yasiyoelezeka kana kwamba tunateswa na moto.

Tuna nyuso zilizo kwajuka na wenye aibu, ukweli kuhusu upotovu wetu umefunuliwa kabisa.

Tumeelewa ukweli na kujijua sisi wenyewe, tunakubali mipango yote ya Mungu bila malalamiko.

5

Tumepitia majaribio na dhiki na tumepata wokovu, tumeshindwa na maneno ya Mungu na kuwa watu Wake.

Imani yetu inazidi kuwa ya vitendo, tuna imani ya kweli, na tunasifu uweza na hekima ya Mungu.

Maneno yote ya Mwenyezi Mungu ni ukweli, Yeye ndiye Mungu wa vitendo mwenye mwili.

Siwezi kulazimishwa kuondoka, kuwa mtendaji huduma kumekuwa rafiki yangu mzuri.

6

Nimeazimia kuwa mtu mpya, dhamiri na mantiki ni alama za ubinadamu.

Watendaji maovu hutenda uovu na hufunuliwa na kuondolewa, wale wanaotenda ukweli wanakubaliwa na Mungu.

Majaribio na taabu vimefanyiza kundi la washindi, tumeazimia kabisa kumfuata Mungu hadi mwisho.

Tunafuatilia ukweli na sote tuna ushuhuda mzuri, watu waaminifu hupata baraka za Mungu.

Iliyotangulia: 156 Upendo Wangu kwa Mungu Hautabadilika Kamwe

Inayofuata: 158 Ni Nani Anayeufikiria Moyo wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp