Nabaini Uwongo wa Serikali ya CCP na Upendo wa Mungu Unanirudisha Kwake

02/12/2019

Na Kemu, Korea ya Kusini

“Nakuambia kwa mara nyingine tena—usiendelee kuzungumza nami juu ya mambo hayo ya Mungu, na huruhusiwi kujihusisha tena na waumini hao wa Mungu. Nikiona kuwa umekuwa ukiwasiliana nao tena, nitavunja simu yako iwe vipande vipande!”

“Kwa nini? Kwa nini unazuia imani yangu?” mke wangu aliuliza, uso wake ukiwa umejaa wasiwasi.

“Kwa nini? Ni kwa manufaa yako mwenyewe na kwa manufaa ya familia yetu. Hujui kuwa serikali ya CCP inalichukulia hatua kali sana na kulikomesha Kanisa la Mwenyezi Mungu? Hujui kuhusu kesi ya Zhaoyuan ya mnamo Mei 28 mwaka wa 2014? Inasemekena mtandaoni kwamba Zhang Lidong, mhalifu mkuu katika kesi hiyo, alikuwa mshiriki wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Ukikutana na watu hao, utakuwa tu unajiweka kwenye hatari kubwa!”

Alijibu kwa ushupavu, “Zhang Lidong na wale wengine hawakuwa pamoja wa Kanisa la Mwenyezi Mungu—huwezi kuamini mambo yasemwayo mtandaoni. Nimekuwa nikiwasiliana na ndugu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa miezi miwili au mitatu na kile ambacho nimeona ni kwamba wote ni watu waadilifu ambao ni wema na waaminifu kwa wengine. Wanasaidiana wakati wowote mtu yeyote anapokuwa na shida, na si kama wanavyosema mtandaoni.”

Nilikasirika na nikasalia kutoshawishika. “Nenda mtandaoni ujionee mwenyewe, kisha utajua ikiwa ni sahihi au la.”

Mke wangu kisha alinielekeza kwenye kiti na akasema, “Wewe ni aina ya mtu anayefikiria mambo kabisa. Lazima ulikabili jambo hili kwa mantiki na kuongea kulingana na ukweli—huwezi tu kusikiliza upande mmoja wa hadithi! Kila chombo kikuu cha habari nchini China ni msemaji tu wa serikali ya CCP; ni vifaa tu vya serikali vya kuwadanganya watu. Je, ripoti zao zina uaminifu wa aina gani? Hukumbuki maandamano ya Tiananmen Square ya mnamo mwaka wa 1989? Wanafunzi wa Tiananmen Square walikuwa wakilalamikia ufisadi na kutetea uhuru wa kidemokrasia, lakini serikali ya CCP ilitafuta watu wengine wasiojulikana na wakawafanya wajifanye kuwa wanafunzi na kupenya kwenye safu ya wanafunzi, kisha wakawafanya waanze kupiga, kuponda, kupora, kuchoma, na kupindua magari ya kijeshi. Watu hao walifanya fujo sana, na kisha serikali ya CCP ikawasingizia wanafunzi kwa makosa yao. Baada ya hayo, serikali ya CCP ilitumia vyombo vya habari kama televisheni na redio kupeperusha ripoti zao, ikikashifu tapo la wanafunzi kama ghasia za ubishani, na kisha ikaanza kulichukulia hatua kali ya umwagaji damu, jambo ambalo lilisababisha wanafunzi wasiopungua elfu kadhaa kuuawa kwa kupigwa risasi au kupondwa na vifaru. Yeyote anayejua kuhusu historia ya serikali ya CCP anajua kuwa kila wakati imekuwa ikipinga vikali haki, na kwamba haivumilii kabisa kuwepo kwa vikundi au watu wowote ambao wana maoni na mawazo tofauti ya kisiasa. Ili kufanikisha udikteta, serikali ya CCP imekuwa ikishambulia na kushutumu vikundi au watu hao kila mara, mpaka kuwakomesha au kuwapiga marufuku kabisa. Kila wakati serikali ya CCP inapokomesha vikali imani ya kidini, harakati za haki za kidemokrasia, au maandamano ya kabila ya walio wachache, kwanza huanza kwa kubuni kesi za uwongo, kasha huvumbua makele makuu ya umma ili kuwachochea watu, kisha huwakomesha vikali. Huo ni ukweli. Kesi ya Zhaoyuan ya mnamo Mei 28 ilikuwa serikali ya CCP kulisingizia Kanisa la Mwenyezi Mungu—ilibuni kwa makini kesi nyingine ya uwongo.”

Sikuweza kukanusha kile alichokuwa amesema hata kidogo, na nikajiwazia, “Amewajua wanafamilia wengine wa waathiriwa wa maandamano ya Tiananmen Square na anajua hadithi ya kweli. Kila kitu alichosema ni kweli. Lakini bado, hata ikiwa tukio hilo la Zhaoyuan halihusiani na Kanisa la Mwenyezi Mungu, sijawahi kuwasiliana na washiriki wao na sijui ni kanisa la aina gani. Tunaishi katika ulimwengu wenye shida nyingi sasa—itakuwa vipi akidanganywa?” Kwa hivyo, nilimwambia tena kwamba haruhusiwi kuwasiliana na mtu yeyote kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilipokuwa nikiondoka, nilibamiza mlango, na kumwacha akitokwa na machozi.

Ilikuwa usiku wa giza kabisa ambao haukuwa na mwanga wa mwezi na hakukuwa na nyota. Nilihisi vibaya sana nilipokuwa nikitembea njiani. Nilifikiri juu ya miaka kumi ya ndoa yetu—kuanzia mkutano wetu wa kwanza, hadi kupendana, kufunga ndoa, tulikuwa tumepitia mengi, lakini bila kujali tulichokabili tulikuwa tukijadiliana kila mara na kusaidiana. Hatukuwa tumewahi kuwa na ugomvi mkubwa. Hata hivyo, nilikuwa tu nimesuta imani yake—nilihisi sikustahili kumtendea hivyo. Lakini aidha, ilisemekana mtandaoni kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu halikuwa zuri, kwa hivyo kwa kumruhusu atekeleze imani yake nilikuwa nikimfanyia upendeleo. Ni kwa nini hakuweza kunielewa? Wakati huo nilihisi mchovu na mwenye hasira sana. Nilitoa simu yangu na picha nzuri ya familia yetu yenye furaha ilinijia machoni pangu—tabasamu tamu ya binti yetu iliondoa uchovu wangu kwa muda mfupi. Nilifikiria jinsi nilivyokuwa tegemeo la familia na kwamba kuzuia mke wangu kutekeleza imani yake kulikuwa kwa ajili ya usalama wake mwenyewe na kulikuwa kwa faida ya familia yetu, kwa hivyo niliamua kwamba nililazimika kushikilia msimamo wangu.

Katika muda uliofuata, niliogopa kudhuru hisia za mke wangu kwangu na kwa hivyo sikuthubutu kuanza ugomvi wowote mkubwa, kwa hivyo nilimwambia tu asizungumze nami kuhusu chochote kilichohusiana na Mungu. Hata ingawa tulionekana kuelewana kwa kawaida kijuujuu, tayari kulikuwa na tofauti iliyokuwa ikitokea baina ya hisia zetu.

Siku moja, nilipokuwa tu nimeimeingia mlangoni baada ya kutoka zamu yangu ya kazi ya asubuhi, nilisikia sauti ya shangwe ya muziki ikitoka chumbani pamoja na kicheko cha furaha kutoka kwa mke na binti yangu. Kwa kutaka kujua, nilidhani, “Mh? Sijasikia sauti ya furaha kama hii nyumbani kwa muda mrefu sana. Tangu mke wangu aje kutoka Korea Kusini, hajawahi kwa kweli kuzoea mazingira ya hapa kwa sababu ya mtindo wa maisha, lugha na utamaduni tofauti. Hususan, alimwacha mama yake mkongwe na kazi ambayo aliyokuwa akipenda, na hana jamaa na marafiki wowote kando yake—yeye hukaa peke yake na kulia mara nyingi. Nimemwona akionekana kuumizwa na kufadhaika lakini sijawahi kujua jinsi ya kumfariji, kwa hivyo ni aina gani ya wimbo ambao unaweza kumletea furaha nyingi sasa?” Nilinyamaza kimya kwa utulivu na nikaona video ya densi na wimbo uliotolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu “Upendo wa Kweli wa Mungu” ukionyeshwa kwenye skrini ya kompyuta. Wanawake sita walikuwa wakicheza kwa furaha na kuimba kwa hisia kuu, lakini ni nyuso zao zilizokuwa zimejaa tabasamu za furaha kuu ambazo ziliuvuta moyo wangu mara moja. Nilitaka kujua sana, nikifikiri, “Hili ni kanisa la aina gani, na hiki ni kikundi cha aina gani? Kwa nini nyimbo na densi zao ni za kuathiri na kutuliza sana? Kama kwa kweli wangekuwa watu wabaya, wangewezaje kuwa na tabasamu njema na za kweli?”

Binti yangu aliponiona, alisema kwa furaha, “Baba, si huu ni wimbo mzuri? Mimi na mama tunaupenda sana. Imba na ucheze nasi!” Nilimchukua kwa kumkumbatia na kubusu uso wake mdogo, kisha nikasema kwa moyo mkunjufu, “Mpenzi, napenda nyimbo na densi zenye nguvu.” Alitikisa kichwa chake na kufikiria kwa muda. “Baba, unapenda kucheza densi ya kugongagonga mguu chini, siyo? Mama, mchezee video hiyo yenye densi nzuri sana.” Sikuweza kumkatisha na nikadhani kuwa ningeitazama kwa muda kidogo tu hata ikiwa ilitoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu—siku hizi mazingira mapatanifu kama haya yalipatikana kwa nadra nyumbani kwetu. Huku nikimshika binti yangu, nilikaa karibu na mke wangu na kuanza kutazama. Video ya densi na wimbo “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki” ilikuwa yenye nguvu na yenye wimbo wa kupendeza. Kwa mtindo wa densi ya kugongagonga mguu chini, walicheza na nguvu kama ya kishujaa; nilipenda kuimba na kucheza siku zote, kwa hivyo nilivutiwa sana. Mke wangu alipoona nilivyojihusisha, alisema kwa raha, “Nyimbo na densi hizi zote zimepangwa na kurekodiwa na ndugu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hakuna hata mmoja wao ambaye ni mtaalamu.” Sikuwa na budi kutafakari sana juu ya hili. “Watu wasio na mafunzo ya kitaaluma wanawezaje kucheza vizuri sana?” Nilifikiri. Alisema huku akitabasamu, “Ni jambo la kushangaza, siyo! Bila kazi na mwongozo wa Mungu Mwenyewe, watu wasio wataalamu wangewezaje kucheza hivyo? Utashangaa zaidi ukiona filamu ambazo wametunga. Kanisa la Mwenyezi Mungu lina kazi ya Roho Mtakatifu—lina baraka ya Mungu. Ndio sababu nyimbo, densi na filamu zao zimetungwa vizuri, na zaidi ya hayo, ukweli wote uliotolewa kwenye filamu zao huwanufaisha watu sana. Hizo propaganda zote mbaya zilizomo kwenye mtandao ni serikali ya CCP tu inayoeneza uwongo juu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu. Zote si kweli. Sababu ya serikali ya CCP kueneza uwongo huu ni kwamba kila mtu atakuwa adui wa Kanisa la Mwenyezi Mungu na hatathubutu kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kwa hivyo atapoteza wokovu wa Mungu.”

Niliposikia kile alichosema na kuona sura yake iliyong’aa, nilitaka kujua hata zaidi. Nilifikiri juu ya jinsi ambavyo, tangu alipoanza kumwamini Mwenyezi Mungu, alikuwa amepata ahueni kuotokana na mfadhaiko wake wa kuhisi huzuni na kumkumbuka mama yake. Niliona pia kwamba alikuwa amemvumilia zaidi binti yetu na hakuwa na hasira tena; alikuwa pia ameanza kunitunza vyema sana. Yaweza kwa kweli ikawa kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amembadilisha mke wangu? Je, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuwa zuri kama alivyosema? Nilipokuwa nikifikiri kuhusu haya yote, moyo wangu ulihisi kuchanganyikiwa—sikujua ikiwa nilifaa kumruhusu aendelee kutekeleza imani yake. Baada ya kushikwa ghafla na mapambano ya ndani, niliamua kwenda kwa Kanisa La Mwenyezi Mungu na kulipeleleza mimi mwenyewe. Ikiwa haikuwa kama vile ilivyosemekana mtandaoni, basi singemzuia tena.

Mwishoni mwa juma wakati ambapo sikuwa na kazi, nilimwendea mke wangu na kumwambia kwamba ninlitaka kwenda kuliangalia Kanisa la Mwenyezi Mungu—alishangaa na kufurahia. Mara tu tulipofika huko ndugu walitupokea ukunjufu, na nilihisi kutoka kwa matamshi yao, matendo yao, na jinsi walivyoingiliana na wengine kuwa walikuwa wema na waaminifu. Woga na uhadhari wangu ulipungua polepole. Kisha, dada alimwambia kila mtu kwa furaha, “Ndugu, Hadithi ya Xiaozhen ya muziki ilishinda tuzo ya kimataifa!” Niliuliza kwa kutaka kujua, “Naweza kuitazama?” Wote walitoa makubaliano yao kwa pamoja na kuanza kucheza muziki. Mema na mabaya ya Xiaozhen katika hadithi yaligusa moyo wangu sana na nilifikiria jinsi mimi mwenyewe nilivyokuwa Xiaozhen mwingine. Nilizurura kwenye jamii nilipokuwa mchanga kwa sababu ya bahati mbaya ya kifamilia, nikipitia kila aina ya uonevu na fedheha ili tu kukubalika na kudharauliwa. Na sasa nilikuwa nikijitahidi na kutia bidii ili kupata riziki na nilikuwa nimepitia vitu vya kila aina, vitamu na vichungu. Nilipitia mema na mabaya sana kwa miaka mingi, na nilihisi mchovu na mwenye huzuni, lakini nilijifanya kuwa imara mbele ya mke na marafiki zangu kila mara. Ni nani ambaye angeweza kujua uchungu uliokuwa moyoni mwangu? Karibu ya mwisho wa muziki wimbo huu uliimbwa: “Mwenye uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana. Wakati uo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na fahamu, maana imembidi Asubiri sana kupata jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako, kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote(“Mungu Anautafuta Moyo Wako na Roho Yako” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila mstari wa wimbo huo ulitia ukunjufu roho yangu iliyopotea na iliyoteseka, na kila maneno niliyoimba yalihisi kama mama aliyemnyooshea mtoto wake aliyepotea mikono yake. Kile ambacho nilihisi ni wito wa upendo—niliguswa sana. Sikuweza kuzuia machozi kutiririka usoni mwangu muziki ulipokuwa ukifika kikomo. Ilikuwa mara ya kwanza kuwahi kulia mbele ya watu wengi na nilihisi aibu kidogo, kwa hivyo kwa haraka na kwa kimya nikageuza kichwa changu ili kufuta machozi. Nilitamka ghafla kwa mshangao, “Huo ni muziki mzuri sana!” Kisha nikapigia makofi Hadithi ya Xiaozhen.

Mke wangu alinitazama na kuniambia kwa furaha na kwa hisia kuu, “Kwamba moyo wako umevutiwa na Hadithi ya Xiaozhen ni kwa sababu Mungu amekugusa! Najua kuwa Kesi ya Zhaoyuan ya mnamo Mei 28 ilikuwa na athari kwako na kwamba umekuwa na kutoelewa kwingi kuhusu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Najua pia kuwa unahangaikia usalama wangu na usalama wa binti yetu, kwa hivyo leo tuangalie kabisa na tuone ni nini kilichotokea katika kesi hiyo.”

Ndugu kisha walinichezea video, Ukweli Wafichuliwa Kuhusu Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28. Ilifunua sehemu kuu kadhaa za kuleta shaka za kesi hiyo na kisha kuzichambua safu kwa safu. Niliizamia kabisa na nikafanya uchanganuzi wangu mwenyewe wa kesi hiyo pamoja na video ili kujua ukweli. Kunjo lililokuwa katika uso wangu lililegea polepole video ilipokuwa ikiendelea kucheza na, nilipoona safu baada ya safu ya uwongo ikifunuliwa, nilishusha pumzi ndefu. Niligundua kuwa Kesi ya Zhaoyuan ya mnamo Mei 28 ilikuwa imebuniwa na serikali ya CCP ili kuzuia imani ya dini na kukomesha Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahalifu katika kesi hiyo, Zhang Lidong, Zhang Fan na wengine, walikanusha kwa midomo yao wenyewe kuwa walikuwa washiriki wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na wakasema kwamba hawakuhusika kabisa na kanisa hilo. Lakini serikali ya CCP ilipuuza kabisa ushuhuda wa watuhumiwa na ilikwenda kinyume na ukweli bila haya, ikisisitiza kwamba uhalifu huo umetekelezwa na watu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kilichokuwa cha ajabu hata zaidi ni kwamba hata bila kesi au uamuzi wa mahakama, serikali ya CCP ilikurupuka hadharani na kwa hakika bila kufikiri kuisakazia Kanisa la Mwenyezi Mungu kesi hiyo kupitia vyombo vya habari vya televisheni na mtandao, ili tu kubuni ghasia za umma ili kukandamiza kanisa na kuliondoa. Serikali ya CCP ilisingizia kanisa na kutunga kesi ya uwongo ili iweze kuanza kuwakomesha na kuwakamata kwa hasira Wakristo kanisani bila kikwazo. Ni kama tu jinsi walivyokomesha tapo la wanafunzi mnamo Juni 4 mwaka wa 1989—kwanza walibuni uvumi ili kufafanua tapo la uzalendo la wanafunzi kama fujo ya kupinga maendeleo, na kisha wakaanza kutekeleza ukamataji na mauaji ya watu. Nilipokabiliwa na ukweli huo, niliona mwishowe waziwazi kabisa kuwa mbinu ya serikali ya CCP ya kukomesha wapinzani wowote imekuwa kwanza kubuni uvumi na kupotosha ukweli, kisha kuwasingizia, na kisha kuwakomesha vikali sana. Kwa kugeuza ukweli kuwa uwongo, kupotosha ukweli na kusingizia Kanisa la Mwenyezi Mungu, serikali ya CCP huwafanya watu ambao hawajui ukweli wadanganywe na uwongo wake na wataielewa vibaya kanisa—serikali ya CCP ni ya kuleta hizaya kabisa! Lakini kitu ambacho bado sikuelewa ni kwamba ndugu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ni watu waadilifu ambao si kama inavyosemekana mtandaoni, kwa hivyo kwa nini serikali ya CCP ilitese kanisa kwa hasira na kufanya kila liwezekanalo kulisakazia Kanisa la Mwenyezi Mungu kesi ya mauaji na kuwakamata washiriki wake? Ni nini kilichokuwa kikiendelea kwa kweli?

Nilizungumza juu ya wasiwasi wangu na dada akajibu, akisema, “Hebu kwanza tusome vifungu viwili kutoka kwa maneno ya Mungu. ‘Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II). ‘Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II).”

Baada ya kusoma maneno ya Mungu, alitoa ushirika, akisema, “Maneno ya Mungu yanafunua sababu ya Shetani kumpinga Mungu na kuwadhuru wanadamu. Kwa hivyo tukitumia maneno ya Mungu kuangalia vitendo vya serikali ya CCP vinavyompinga Mungu na mateso yake kwa Wakristo, tunaweza kuona waziwazi kuwa ni mfano halisi wa Shetani, Ibilisi, na ni mfumo wa utawala wa Shetani unaochukia ukweli na kumpinga Mungu. Haitakubali kabisa watu wamwamini Mungu au kuchukua njia sahihi ili kuimrisha nchi ya China kama eneo la ukanaji Mungu—inataka kuondoa imani zote za kidini. Hii ni kweli kabisa katika siku za mwisho—Mwenyezi Mungu mwenye mwili ameonekana na kufanya kazi nchini China, Akionyesha ukweli ili kuwaletea wanadamu mwanga. Watu kutoka katika dini na madhehebu yote ambao wanamwamini Mungu kwa kweli na wanaopenda ukweli, baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, wanakuwa na uhakika kuwa maneno hayo ni ukweli, na, moja kwa moja, wanakubali kazi Yake ya siku za mwisho. Watu wengi wameelewa ukweli kwa kusoma maneno ya Mungu na wamejifunza jinsi ya kutambua kati ya mema na mabaya. Kwa hivyo wanakuja kuona waziwazi asili mbovu ya serikali ya CCP na kuwa tayari kuikataa, na wanaanza kufuatilia ukweli na kuchukua njia sahihi maishani. Inapowaona watu zaidi na zaidi wakipata imani katika Mungu na kumfuata, macho yake yanawaka kwa ghadhabu. Inatarajia bila kufaulu kuwavuta watu na kuwarudisha kambini mwake ili waweze kuendelea kuwa watumwa wake na kusalia kuwa wa kudhalilishwa. Kwa sababu hiyo, serikali ya CCP hutesa na kukomesha Kanisa la Mwenyezi Mungu sio tu kwa kubuni kila aina ya uwongo ili kulisingizia na kulikashfa, bali pia kwa kutumia kila aina ya mbinu zenye kuleta hizaya. Wametoa nyaraka za siri mara nyingi ili kuhamasisha idadi kubwa ya polisi wenye silaha na wanajeshi wawakamate na kuwatesa kwa hasira Wakristo kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha kitaifa katika jaribio la udanganyifu la kuzuia kuenea kwa kazi ya injili ya Mungu na kuondosha kabisa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hasa katika miaka michache iliyopita, kila aina ya filamu na video za injili zilizotolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu zimewekwa kwenye mtandao moja baada ya nyingine na injili ya ufalme wa Mungu imeenea kote ulimwenguni haraka sana. Serikali ya CCP inajua hatia yake, inajua kwamba tangu iingie madarakani, imefanya mauaji mengi sana na imefanya kila aina ya uovu; deni lake la damu iliyotokana na kuwatesa Wakristo ni zito. Inahofu kuwa watu ulimwenguni kote watakubali kazi ya Mungu, wataelewa ukweli, wataona waziwazi sura yake mbaya kisha wataikataa, jambo ambalo litaiacha bila nafasi ulimwenguni. Kwa hivyo hamu yake kuu ya kudhibiti binadamu wote na kuwa mungu itaharibika. Hii ndio sababu mateso ya serikali ya CCP kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu yameongezeka. Ilibuni kesi ya mnamo Mei 28 ya Zhaoyuan kwa uangalifu sana ili kulisingizia kanisa, katika jaribio la kuwakera na kuwakanganya wale ambao hawajui ukweli ili wamchukie Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kufanya uovu pamoja nayo. Tunaweza kuona kutoka kwa hili kwamba serikali ya CCP ni potovu na huenda kinyume na Mbingu, na kwamba inamchukia Mungu na kuchukia ukweli. Ni adui wa Mungu—pepo anayepinga Mungu. Hata hivyo, Mungu mwenye uweza na hekima Yake hutekelezwa kulingana na hila za Shetani. Uso mbaya wa serikali ya CCP umebainishwa na upinzani na udhalimu wake mwenyewe, na wateule wa Mungu wanaweza kuona asili yake mbovu na ya kupinga maendeleo waziwazi hata zaidi. Wanakuza utambuzi wa asili yake ya kudharaulika na mbaya, ridhaa yao ya kumfuata Mungu yanakuwa madhubuti hata zaidi, na badala yake wanatoa maisha yao kuliko kuacha kumfuata Mungu. Hii inaonyesha kuwa bila kujali serikali ya CCP ni katili kiasi gani, haiwezi kuwazuia waumini wa kweli kumfuata Mungu, sembuze kuweza kusimamisha kazi ya Mungu.”

Baada ya kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu na ushirika wa dada huyu, nilielewa kuwa serikali ya CCP hulitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa sababu asili yake ni ile ambayo inachukia ukweli na ni adui wa Mungu. Inataka kuwadhibiti watu, kuwashika watu kwa uthabiti katika, lakini ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu hukita mizizi katika mioyo ya watu. Serikali ya CCP bila shaka haitaki watu watembee na Mungu, kwa hivyo inafanya kila iwezalo kubuni uvumi ili kudanganya umma na kutunga kesi za uwongo, ikiendeleza hasira ya umma ili kutesa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo kesi ya mnamo Mei 28 ya Zhaoyuan ilivyotokea. Wasiwasi wangu juu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu uliondolewa mara tu nilipoelewa ukweli. Hata hivyo, bado nilikuwa na shaka: Kwa kuwa serikali ya CCP hulidhalimu kanisa sana, itakuwa salama kwa mke wangu kumwamini Mungu?

Ndugu kisha walinichezea sinema, Manifesto ya Ukomunisti. Kulikuwa na kifungu cha maneno ya Mungu ndani yake ambayo yaliugusa moyo wangu kweli. “Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Niliweza kuhisi mamlaka na uadhama wa Mungu kutoka kwa maneno Yake. Hakuna nguvu mbaya ya Shetani au mwanadamu yeyote anayeweza kuzuia kazi ya Mungu. Ijapokuwa wale walio kwenye serikali ya CCP wanapiga bongo zao ili kuliaibisha na kulishutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu, hata wakiwakamata na kuwatesa ndugu wa kanisa hilo kikatili, ndugu bado wanaendelea kumwamini na kumfuata Mungu, na filamu za injili, kazi za uimbaji, na video za densi na nyimbo ambazo wao hutoa zinawekwa mtandaoni kila mara, pasipo kuzuiwa kabisa na serikali ya CCP. Mwishowe niliona jinsi ambavyo Mungu alivyo Mwenye uweza na kwamba hakuna nguvu inayoweza kusimamisha kazi Yake. Katika kumwamini kwake Mungu, mke wangu ana Mungu kama tegemeo lake la nguvu, kwa hivyo hakuna chochote cha kuonea wasiwasi. Baada ya kuelewa yote hayo, wasiwasi na mashaka yaliyokuwa moyoni mwangu yalipotea yote. Huku nikitabasamu, nilimwambia mke wangu, “Ni sawa kwako kumwamini Mwenyezi Mungu. Nilikuwa kipofu hapo zamani—niliamini kimakosa kile nilichosikia na kukufanya uteseke sana. Nilinikosea sana. Kuanzia sasa na kuendelea, nitakuunga mkono kabisa katika imani yako.” Machozi yaliongezeka machoni pake na akasema huku akiwa na hisia, “Namshukuru Mungu kwamba umeweza kubaini uwongo wa serikali ya CCP na kuibuka kutoka kwa ukungu wa utatanishi. Huu ni mwongozo na uongozi wa Mungu!”

Kuanzia hapo nilianza kutazama video zilizotengenezwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu mara chache na mke wangu, na nikamsikiliza akizungumza juu ya imani yake. Hata hivyo, bado nilihisi kwamba imani katika Mungu ilikuwa aina ya imani rahisi. Kweli, niliweza kuamini Mungu moyoni mwangu. Lakini bado nilihitaji kupata riziki na kuilea familia yangu, na kutoa mahitaji ya kutosha ili tuweze kuishi maisha mazuri. Ni baadaye tu, baada ya kupata ugonjwa wa kiafya, ndipo nilipopata ufahamu mpya kabisa juu ya imani katika Mungu.

Manamo jioni moja familia yetu ilipokuwa ikila chakula cha jioni, nilianza kupata maumivu makali ya tumbo na matone makubwa ya jasho baridi yakaanza kuteleza usoni pangu. Mke wangu alinipeleka hospitalini haraka ambapo nilibainishwa kuwa na kibole kilichopasuka. Nilikuwa hali mahututi ambayo ilihitaji upasuaji wa haraka. Nilihisi hali ya kutojiweza na hofu ambayo sikuwahi kuhisi hapo awali—ikiwa singeendelea kuishi, mke na binti yangu mdogo wangewezaje kwenda katika nchi ya kigeni? Nani angewasaidia? Mke wangu alipoona nilichokuwa nikifikiri, alinishika mkono na kusema, “Najua unachoonea wasiwasi. Mungu ni mwenye uweza, na vitu vyote vimo mikononi Mwake. Yeye ndiye mwenye kauli ya mwisho kuhusu iwapo upasuaji huu utafaulu, pia. Lazima tumtegemee Mungu na, bila kujali upasuaji huu utakavyokuwa mwishoni, hatuwezi kumlaumu Mungu, lakini lazima tutii sheria na mipango Yake.” Nilitikisa kichwa baada ya kusikia kile alichosema. Mara mlango wa chumba cha upasuaji ulipofungwa, niliyafumba macho yangu na kumwomba Mungu. “Ee Mwenyezi Mungu! Naogopa. Tafadhali nipe imani ili nisiogope tena. Niko tayari kukutegemea.” Nilihisi hofu kidogo baada ya kusali, na dondoo ya maneno ya Mungu kutoka kwenye video ikanirudia: “Kila kitu ambacho mwanadamu anacho—amani na furaha, baraka na usalama wa kibinafsi—yote hakika yanadhibitiwa na Mungu, na Anaongoza na kuamua hatima ya kila mtu(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI). “Ni kweli,” nilifikiri. “Mungu ni mwenye uweza na maisha yangu yamo mikononi Mwake. Mafanikio ya upasuaji wangu hivi leo yanategemea utawala na mipango ya Mungu, kwa hivyo kwa kumkabidhi Mungu kila kitu, hakuna chochote cha kuonea wasiwasi.” Maneno ya Mungu yalinipa imani; moyo wangu uliokuwa na wasiwasi ulitulia, na sikuwa na wasiwasi tena juu ya kutofaulu kwa upasuaji ambako kuliwezekana. Nilipoteza fahamu polepole kwa ajili ya athari ya nusukaputi. Nilipopata fahamu, daktari aliniambia kwamba upasuaji huo ulifanikiwa, na nilijua kuwa Mungu alikuwa amenilinda. Nilitoa sifa na shukurani kwa Mungu tena na tena.

Baadaye, niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kitu cha kwanza ambacho mtu lazima aelewe, anapokanyaga guu lake hapa duniani, ni wapi binadamu hutoka, kwa nini watu wako hai, nani anayeamuru hatima ya binadamu, ni nani anayekidhi mahitaji ya binadamu, na Aliye na ukuu juu ya uwepo wa binadamu. Maarifa haya ndiyo njia ya kweli ambayo kwayo mtu huishi, msingi muhimu kwa kuwepo kwa binadamu—kutojifunza namna ya kutosheleza familia ya mtu au namna ya kutimiza umaarufu na utajiri, kutojifunza namna ya kujitokeza katika umati wala namna ya kuishi maisha mazuri zaidi, bila kutaja namna ya kutia fora na kushindana kwa ufanisi dhidi ya wengine. Ingawaje mbinu mbalimbali za kuishi ambazo watu huishi wakijaribu kumiliki zinaweza kumpa wingi wa tulizo la mali, hazijawahi kuleta amani na tulizo la kweli moyoni, lakini badala yake hufanya watu kila wakati kupoteza mwelekeo wao, kuwa na wakati mgumu kujidhibiti, na kukosa kila fursa ya kujifunza maana ya maisha; mbinu hizi za kuishi huleta mawimbi fiche ya wasiwasi kuhusu namna ya kukabiliana na kifo vizuri. Maisha ya watu huharibika kwa njia hii. Muumba hushughulikia kila mmoja bila mapendeleo, huku akipatia kila mmoja wetu fursa ya kutosha maisha yote ili kuweza kupitia na kujua ukuu Wake, ilhali ni mpaka tu kifo kinapokaribia, wakati kivuli cha kifo kinaponing’inia karibu na mtu, ndipo mtu huyu huanza kuona nuru—na kisha muda huwa umeyoyoma mno(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III).

Moyo wangu ulichangamka baada ya kusoma maneno ya Mungu na nilielewa kuwa hatuishi tu hapa duniani ili tuishi maisha duni ya kulisha familia zetu na kufanikiwa, au kuonewa kijicho na wengine na kuheshimiwa na wengine, tukitafuta umaarufu na faida. Sisi wanadamu ni viumbe wa Mungu na kwa kumwamini na kumwabudu Mungu, kufuatilia na kuelewa ukweli, kupata maarifa juu ya Mungu, na kuelewa waziwazi kuwa Mungu ndiye anayetawala vitu vyote katika maisha yetu na kwamba kudura zetu ziko mikononi Mwake pekee ndiyo tunaweza kutii utawala na mipangilio Yake kwa kweli na kutenda kulingana na maneno Yake. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuishi kuliko maana na thamani; ndiyo njia pekee ya kutoishi maisha haya bure. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nimehisi hapo awali, kwamba imani katika Mungu ilikuwa aina rahisi ya imani, na kwamba kupata pesa kwa ajili familia yangu ndiko nilipaswa kufanya katika maisha yangu. Ni wakati tu nilipokuwa na ugonjwa huo unaotishia uhai ndipo mwishowe niliamka. Bila kujali tunapata pesa ngapi au hadhi yetu ni ya juu kiasi gani, tunapougua, mambo hayo hayawezi kupunguza mateso au woga wetu na kutojiweza ndani ya mioyo yetu. Unapochungulia kaburi, pesa, umaarufu na mali haviwezi kabisa kuturudishia maisha yetu au kurefusha maisha yetu. Namshukuru Mungu—ni Yeye aliyenipa imani na nguvu kupitia maneno Yake nilipokabiliwa na ugonjwa na nilipohisi mwoga na dhaifu sana. Alinipa kitu cha kujitegemeza ili niweze kukabili kwa utulivu kila kitu ambacho kingetokea. Hasa, ni utunzaji na ulinzi tu wa Mungu ambao uliniruhusu kupitia upasuaji wangu bila kikwazo. Kupitia uzoefu huo nilipata hisia kuwa Mungu ni halisi na Aliye hai, kwamba Anaweza kuwa muawana na msaada wetu wakati wowote, na kwamba Yeye pia ni tegemeo letu dhabiti. Kile ambacho sisi kama wanadamu tunapaswa kufuatilia zaidi katika maisha yetu yote ni kumwamini Mungu, kumwabudu Mungu, na tunapaswa kuelewa na kutii utawala wa Mungu. Roho zetu zinahitaji hayo zaidi, na hayo ndiyo maisha yenye maana zaidi ambayo tunapaswa kufuatilia. Uzoefu huo pia ulibadilisha maoni yangu mabaya kuwa imani katika Mungu ni aina rahisi ya imani na niliamua kutekeleza imani yangu pamoja na mke wangu, kusoma maneno ya Mungu, na kuchukua njia ya kufuatilia ukweli na kumjua Mungu.

Ndugu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu walisikia kwamba nilikuwa nimeugua, kwa hivyo wakaja kunitembelea hospitalini. Walipopata habari kuwa singeweza kufanya kazi kwa muda na familia yetu isingekuwa na chanzo chochote cha mapato, walinisaidia kuomba malipo ya wasiojiweza na kuomba kurudishiwa sehemu kubwa ya gharama yangu ya matibabu. Katika jamii baridi na isiyojali kama hiyo, msaada wa kweli wa ndugu ulinipa hisia za ukunjufu, kama kwamba sote tulikuwa sehemu ya familia moja. Baada ya kuwasiliana nao kwa muda, niliona kuwa wote walikuwa watu wenye huruma sana ambao walitegemea maneno ya Mungu katika mwingiliano wao na wengine, kwamba waliwatendea watu wengine kwa moyo safi, walikuwa wadilifu na wenye heshima katika maneno na matendo yao, na kwamba ubinadamu wao na jinsi walivyoishi maisha yao yalikuwa sawasawa kabisa na jinsi ambavyo ilipaswa kuwa kwa Wakristo. Walikuwa tofauti kabisa na watu ambao nilifanya nao kazi—hakukuwa na watu wowote kama wao waliobaki ulimwenguni. Nilihisi kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yangewabadilisha watu na kutuongoza kwenye njia sahihi, na nilihisi kwamba kanisa hili limejaa upendo na kwamba linawapa watu hisia kuu ya ukunjufu.

Nafikiri juu ya mambo ya zamani nilipokuwa nimepofushwa na uwongo wa serikali ya CCP na nikataa tena na tena kutafuta au kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na hata nikasimama katika njia ya imani ya mke wangu, lakini Mungu hakuacha kujaribu kuniokoa. Kwa kutumia maneno Yake ambayo ndugu walinisomea na video walizonichezea, Mungu aliniruhusu nibaini uwongo wa serikali ya CCP na kuona waziwazi ukweli mbaya ulioyasababisha. Nilipokuwa na wasiwasi juu ya matokeo ya upasuaji wangu na nilipokuwa nikiishi kwa hofu, maneno ya Mungu yalinipa nuru na kunielekeza, yalinipa imani na nguvu, na yakarekebisha mitazamo yangu mibaya. Wakati ambapo sikuweza kufanya kazi baada ya upasuaji, Mungu alinisaidia na kuniauni kupitia kina ndugu. Nilipata upendo na huruma ya Mungu kwangu na mamlaka na maneno Yake, na nilikubali kwa furaha kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Sasa, mimi huhudhuria mikutano na mke wangu na husoma maneno ya Mungu, na moyo wangu umekamilika na umejaa furaha! Namshukuru Mungu kwa kuniokoa!

Iliyotangulia: Wokovu wa Aina Tofauti

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Niliupata Mwanga wa Kweli

Qiuhe, Japani Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp