Kuingiza kwenye Njia ya Imani katika Mungu

16/01/2018

Rongguang Mji wa Harbin, Mkoa wa Heilongjiang

Mnamo mwaka wa 1991, kwa neema ya Mungu, nilianza kumfuata Mwenyezi Mungu kwa sababu ya ugonjwa. Wakati huo sikujua kitu chochote kuhusu kumwamini Mungu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba, wakati wa kula na kunywa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, nilifurahia. Nilihisi kwamba maneno Yake yalikuwa mazuri sana, na nilipoimba au kuomba mara nyingi niliguswa na Roho Mtakatifu hadi kiwango cha kulia. Uzuri huo ndani ya moyo wangu, furaha hiyo ilikuwa ni kama kwamba tukio la furaha lilikuwa limenijia. Hasa katika mikusanyiko wakati wa kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, nilihisi kama nilikuwa nimevuka mipaka ya mwili na nilikuwa nikiishi katika mbingu ya tatu, kwamba kila kitu cha ulimwengu kilikuwa kimetupiliwa mbali. Siwezi kusema jinsi nilivyokuwa na furaha, jinsi nilivyoridhika moyoni mwangu. Nilihisi kwamba nilikuwa mtu mwenye furaha zaidi duniani. Kwa hivyo wakati huo niliamini kwamba kumwamini Mungu kulikuwa tu kufurahia neema Yake.

Wakati maneno mengi zaidi na zaidi ya Mungu yalikuwa yakitolewa (wakati huo yalikuwa yakitumwa kanisani siku zote, kifungu baada ya kifungu), pia nilijua zaidi na zaidi. Kisha, sikukamilishwa tena na kufurahi tu neema ya Mungu. Nilipoona “wazaliwa wa kwanza” wakitajwa katika maneno Yake na nikajifunza kwamba Mungu hutoa baraka kubwa kwa wazaliwa Wake wa kwanza, nilitafuta kuwa mmoja, nikitumaini kuwa siku zijazo ningeweza kutawala na Mungu. Baadaye, nilipoona katika maneno Yake kwamba muda Wake ulikuwa ukija hivi karibuni, nilihisi dharura zaidi, na kudhani: Nilikawia sana kumwamini Mungu; Je, sitakuwa na uwezo wa kupata baraka hii? Ninahitaji kuweka juhudi zaidi ndani ya hili. Kwa hivyo, nyumba ya Mungu iliponipangia kutekeleza wajibu, nilikuwa mwenye bidii sana. Sikuogopa shida. Niliamua kuacha kila kitu kumfuata Mungu ili niweze kupata baraka ya kuwa mwana wa kwanza. Kwa kweli, Mungu hakuwa amesema waziwazi katika maneno Yake kwamba tungeweza kuwa wazaliwa wa kwanza. Ilikuwa tu kwa sababu tulikuwa na malengo na tamaa zilizopita kiasi, tuliamini kwamba kwa kuwa Mungu alikuwa ametuita “wana” Wake na kwamba sasa Ametuinua, kwamba hakika tungekuwa wazaliwa wa kwanza. Hivi ndivyo nilivyoamini kwamba nilikuwa, kwa kawaida, nimekuwa mzaliwa wa kwanza. Baadaye niliona maneno ya Mungu ambayo yalikuwa yametolewa karibuni ambayo mara kwa mara yalitaja “watendaji-huduma,” na kulikuwa na maelezo zaidi na zaidi ya hukumu ya watendaji-huduma. Nilidhani mwenyewe: Kwa bahati ninamfuata Mwenyezi Mungu, vinginevyo ningekuwa mtendaji-huduma. Niliposoma kuhusu baraka za Mungu na ahadi za wazaliwa wa kwanza, niliamini kuwa sehemu ya hiyo ingekuwa yangu. Nilipoyasoma maneno Yake ya faraja na ya kuhimiza kwa mzaliwa Wake wa kwanza, nilihisi pia kwamba yalikuwa yakielekezwa kwangu. Nilihisi furaha hata zaidi hasa nilipoona yafuatazo “Maafa makuu hakika hayatawafikia wana Wangu, wapendwa Wangu. Nitawatunza wana Wangu kila wakati na kila sekunde. Hakika hamtavumilia uchungu na mateso hayo; badala yake, ni kwa ajili ya ukamilishwaji wa wana Wangu na utimizaji wa neno Langu ndani yao, ili kwamba muweze kutambua kudura Yangu, mkue zaidi katika maisha, mbebe mizigo kwa ajili Yangu karibuni, na kujitolea kabisa kwa ukamilisho wa mpango Wangu wa usimamizi. Mnapaswa kuwa na furaha na kuridhika na kushangilia kwa sababu ya hili. Nitawapa kila kitu, Nikiwaruhusu kuchukua usukani. Nitaiweka mikononi mwenu. Mwana akirithi mali nzima ya babake, je, ninyi wana Wangu wazaliwa wa kwanza mtaridhi zaidi kiasi gani? Kweli mmebarikiwa. Badala ya kuteseka kutokana na maafa makuu, mtafurahia baraka za milele. Utukufu ulioje! Utukufu ulioje!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 68). Nilidhani: Je, ninaota? Mana hii ya ajabu kutoka mbinguni imeshuka juu yangu? Sikuweza kabisa kuthubutu kuamini, lakini nilihofu kuwa kaka zangu na dada wangesema kuwa imani yangu ilikuwa ndogo sana, kwa hivyo sikuthubutu kutoamini.

Siku moja, nilikwenda kwa furaha kushiriki katika mkutano, na nikaona kwamba viongozi wawili walikuwa wamekuja kanisani. Nilipokuwa katika ushirika nao, walisema kuwa walikuwa watendaji-huduma. Baada ya kusikia hayo, nilikuwa na hofu, na nikawauliza: “Ikiwa ninyi ni watendaji-huduma, si sisi wote ni watendaji-huduma?” Walisema ukweli bila kusita: “Takribani sisi sote nchini China ni watendaji-huduma.” Niliposikia wakisema hivi, moyo wangu ulihofu. Haiwezekani! Je, huu ni ukweli? Lakini nilipoona maonyesho yao nzito, yenye uchungu na kwamba nyuso za wengine pia zilikuwa za majonzi, sikuweza kuamini. Lakini nilibadili mawazo yangu na kufikiri: Kama viongozi, walikuwa wameacha familia zao na kazi zao, walikuwa wameteseka sana na kulipa thamani kuu sana kwa ajili ya kazi ya Mungu. Nilipungukiwa kabisa ikilinganishwa nao; kama wao ni watendaji-huduma, ningesema nini kingine? Mtendaji-huduma ni mtendaji-huduma, hivyo wakati huo, sikuhisi vibaya mno.

Baada ya kwenda nyumbani, nilichukua neno la Mungu tena na kuangalia kile Mungu alichokuwa na kusema kuhusu watendaji-huduma, na nikaona haya: “Wale wanaonitumikia, sikilizeni! Mnaweza kupokea baadhi ya neema Yangu wakati mnanitumikia. Yaani, ninyi mtajua kwa wakati kuhusu kazi Yangu ya baadaye na mambo ambayo yatatokea baadaye, lakini hamtafurahia hilo kabisa. Hii ni neema Yangu. Wakati huduma Yako imekamilika, ondoka mara moja na usikawie. Wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza hawapaswi kuwa wenye kiburi, lakini mnaweza kujivunia, kwa kuwa Nimewapa baraka za milele kwenu. Wale ambao ni walengwa wa uangamizaji hampaswi kujiletea shida au kuhisi huzuni kwa ajili ya hatima yenu; ni nani aliyekufanya kuwa mzawa wa Shetani? Baada ya kufanya huduma yako kwa ajili Yangu, unaweza kurudi tena kwenye shimo lisilo na mwisho kwa sababu hutakuwa tena na matumizi Kwangu na Nitaanza kuwashughulikia na kuadibu Kwangu. Mara Ninapoanza kufanya kazi, Nitaishughulikia mpaka mwisho; matendo Yangu yatakamilishwa, na mafanikio Yangu yatadumu milele. Hili linatumika kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu, watu Wangu, na hili linawahusu ninyi pia—Mimi kuwaadibu ninyi kutakuwa kwa milele(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 86). Mara tu nilipoyasoma maneno haya nilizongwa na uchungu ambao sikuwa nimewahi kuhisi hapo awali. Nilifunga haraka kitabu cha maneno ya Mungu na sikujaribu kukitazama tena. Mara moja hisia za kusikitisha, za kuchanganyikiwa, za kutoridhika zote zilichemka ndani ya moyo wangu mara moja. Nilidhani: Jana nilikuwa katika susu ya furaha, lakini leo nimesukumwa nje ya nyumba ya Mungu. Jana nilikuwa mwana wa Mungu, lakini leo nimekuwa adui wa Mungu, mzao wa Shetani. Jana, baraka zisizo na kikomo za Mungu zilikuwa zikinisubiri, lakini leo shimo la kuzimu ni hatima yangu, nami nitaadhibiwa hata milele. Ikiwa Hatoi baraka, basi haijalishi, lakini kwa nini bado lazima Aniadibu? Nimekosea vipi tena? Haya yote ni ya nini tena? Sikuwa tayari kukabiliana na ukweli huu; sikuweza kukabiliana na aina hii ya ukweli. Niliyafumba macho yangu na sikuwa radhi kufikiri juu ya hayo tena. Nilitumaini sana kwamba ilikuwa ndoto tu.

Kuanzia hapo kuendelea, mara tu nilipojifikiria kuwa mtendaji-huduma, nilisikia maumivu yasiyoelezeka moyoni mwangu, na sikuthubutu kuyasoma maneno ya Mungu tena. Lakini Mungu ni mwenye hekima sana, na maneno Yake ambayo huwaadibu na kuwafichua watu hayaenei tu kwa fumbo, lakini pia ni unabii wa maangamizi ya siku za baadaye na vilevile mtazamo wa ufalme na mambo yanayofanana na hayo. Hivi vyote vilikuwa vitu ambavyo nilitaka kuvijua, hivyo bado singekwepa maneno Yake. Wakati wa kusoma maneno ya Mungu, maneno Yake makali sana yaliuchoma moyo wangu mara kwa mara, na sikuwa na budi ila kukubali hukumu na kuadibiwa na Yeye. Nilihisi kwamba ghadhabu kubwa ya hukumu ya Mungu ilikuwa daima juu yangu. Kando na maumivu, nilijua ukweli halisi wa kupotoshwa kwangu na Shetani. Ilibainika kuwa nilikuwa mtoto wa joka kubwa jekundu, uzao wa Shetani, na lengo la uharibifu. Katika kukata tamaa, sikuthubutu tena kutumaini kwa tamaa baraka zozote, na nilikuwa tayari kukubali majaaliwa ya Mungu kwamba nilikuwa mtendaji-huduma. Nilipohisi kwamba ningeweza kutoa moyo wangu katika kuwa mtendaji huduma, Mungu tena aliyapanga mazingira yaliyofichua tabia potovu ambayo ilikuwa imefichwa ndani yangu. Siku moja nilipokuwa nikiyasoma maneno ya Mungu, niliona: “Baada Yangu kurudi Sayuni, wale walio duniani wataendelea kunisifu Mimi kama zamani. Wale watendaji huduma waaminifu wanabaki wakisubiri kutoa huduma Kwangu lakini kazi yao itakuwa imefika mwisho. Jambo bora zaidi wanaloweza kufanya ni kutafakari hali Yangu kuwa duniani. Wakati huo, Nitaanza kushusha maafa juu ya wale ambao watakabiliwa na maafa makubwa; ilhali kila mtu anaamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye haki. Bila shaka Sitawaadhibu wale watendaji-huduma waaminifu, bali nitawaruhusu tu wapokee neema Yangu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 120). Nilipoona hili, nilifikiri kwa siri: Sitafikiri tena juu ya haki ya mzaliwa wa kwanza na sitahitaji tena baraka nyingi. Sasa nitafuatilia tu kuwa mtendaji-huduma mwenye kumcha Mungu. Huu sasa ndio ufuatiliaji wangu wa pekee. Katika siku zijazo, bila kujali ni nini ambacho nyumba ya Mungu atanipangia mimi kufanya, nitakifanya kwa kujitolea kadiri ninavyoweza. Mimi kabisa siwezi kupoteza nafasi ya kuwa mtendaji-huduma mwaminifu tena. Kama hata sina uwezo wa kuwa mtendaji-huduma mcha Mungu lakini bali mtendaji-huduma tu, baada ya kumaliza huduma yangu ni lazima nirudi katika shimo la kuzimu au ziwa la moto wa jahanamu. Kwa hivyo yote ni ya nini? Sikuthubutu kuonyesha mawazo haya kwa mtu yeyote, lakini sikuweza kuepuka uchunguzi kutoka kwa macho ya Mungu. Niliyasoma maneno ya Mungu yaliyosema: “Hakuna awezaye kuielewa asili ya mwanadamu isipokuwa Mimi, na wote wanafikiria kwamba wao ni watiifu Kwangu, pasipo kujua kwamba utiifu wao ni mchafu. Uchafu huu utawaangamiza watu kwa kuwa wao ni njama ya joka kubwa jekundu. Hilo lilidhihirishwa na Mimi zamani sana; Mimi ni mwenyezi Mungu, na je, Mimi singeweza kufahamu jambo rahisi kama hili? Mimi ninaweza kupenyeza damu yako na mwili wako ili kuziona nia zako. Si vigumu Kwangu kuielewa asili ya mwanadamu, lakini watu hujaribu kuwa wajuaji, wakifikiria kwamba hakuna mtu ajuaye nia zao isipokuwa wao wenyewe. Je, hawajui kwamba, mwenyezi Mungu anaishi ndani ya mbingu na dunia na vitu vyote?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 118). “Watu wengi zaidi sasa wanahodhi matumaini haba, lakini matumaini hayo yanapogeuka na kuwa masikitiko hawataki kuendelea zaidi na wanaomba kurudi. Nimekwisha kusema awali kwamba Simweki yeyote hapa kinyume cha mapenzi yake, lakini tahadhari kufikiria matokeo yatakavyokuwa kwako, ni huu ni ukweli, si Mimi kukutisha wewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 118). Baada ya kusoma haya, moyo wangu ulikuwa ukipapa kwa nguvu. Nilihisi kwamba Mungu kwa kweli hubaini kila kipengele cha nafsi ya mwanadamu. Tunafikiria kitu na Mungu anajua; tunaweka tumaini kidogo katika mioyo yetu na Mungu anachukizwa. Wakati huo tu ndipo nilikuwa na moyo wa kumcha Mungu. Niliamua kwamba singeendesha tena shughuli na Mungu, ila kwa uaminifu, ningetenda kama mtendaji-huduma na kutii miundo Yake.

Baadaye tu ndipo nilijua kwamba uzoefu wangu kwa miezi hii mitatu ilikuwa jaribio la watendaji-huduma. Ilikuwa kazi ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ndani ya watu ya jaribio kwa maneno Yake. Baada ya kupitia jaribio la watendaji-huduma, nilielewa kuwa Mungu sio Mungu mwenye huruma na upendo tu, bali ni Mungu mwenye haki, Mungu mwenye uadhama ambaye havumilii makosa ya wanadamu. Maneno Yake yana mamlaka na nguvu, ambayo hayana budi ila kuzalisha moyo wa hofu kwa mwanadamu. Nilijua pia kwamba wanadamu ni viumbe wa Mungu, kwamba tunapaswa kuamini katika Mungu na kumwabudu Yeye. Hili ndilo lililo sawa na sahihi. Hakuna haja ya sababu, ya masharti, na hakupaswi kuwa na tamaa ya makuu au hamu iliyopita kiasi. Ikiwa watu wanaamini katika Mungu ili kupata kitu kutoka Kwake, basi aina hii ya imani ni kumtumia vibaya na kumdanganya. Ni maonyesho ya kukosa dhamiri na mantiki. Hata kama watu humwamini Mungu lakini hawapati chochote na baadaye kupata adhabu Yake, wanapaswa kumwamini. Wanadamu wanapaswa kumwamini na kumtii Mungu kwa sababu Yeye ni Mungu. Nilitambua pia kwamba mimi mwenyewe ni mwana wa joka kuu jekundu, kizazi cha Shetani, na mmoja wa wale watakaoangamia. Mungu ni Bwana wa viumbe vyote, na bila kujali Anavyonitendea mimi inastahili. Yote ni ya haki, na ninapaswa kuitii mipango na mipangilio Yake bila masharti. Sipaswi kujaribu kujadiliana na Yeye, na hata zaidi sipaswi kumpinga. Nilipokumbuka uzuzu wangu mwenyewe uliofichuliwa katika jaribio hili, niliona kwamba nilikuwa kweli mwenye aibu, na kwamba nilitaka tu kupata hadhi fulani ya juu, baraka nyingi, au hata kukaa bega kwa bega na Mungu na kutawala pamoja na Yeye. Nilipoona kwamba singepata baraka nilizozitarajia bali badala yake kupitia maangamizi, nilifikiria kuhusu kumsaliti Mungu. Mafafanuzi hayo ya wazi kabisa yalinifanya nione wazi kwamba lengo langu katika kumwamini Mungu lilikuwa kubarikiwa. Nilikuwa nikijaribu kufanya shughuli za kibiashara na Mungu kwa dhahiri. Kweli nilikuwa asiye na aibu, na nilikuwa nimepoteza kabisa mantiki ambayo mtu anapaswa kuwa nayo. Isingekuwa hekima hiyo katika kazi ya Mungu—kutumia jaribio la watendaji-huduma ili kunishinda, kuvunja tamaa yangu ya kupata baraka—bado ningekuwa nikikimbia katika njia isiyo sahihi ya kutafuta baraka. Nisingeweza kuelewa asili yangu iliyopotoka, na hasa singekubali hukumu na adhabu ya maneno ya Mungu kwa utiifu. Katika hali hiyo, nisingeweza kamwe kuokolewa au kukamilishwa.

Baada ya kupitia jaribio la watendaji-huduma, nilidhani sikuthubutu tena kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu ili kupata baraka, na nilidhani sikuthubutu tena kufanya mambo kwa nia ya kufanya shughuli na Mungu. Nilihisi kuwa kumtumia vibaya na kumdanganya Mungu kwa njia hii kulistahili kudharauliwa sana. Lakini wakati huo huo, nilikuwa na ufahamu kwamba Mungu kutumia jaribio hili kuokoa wanadamu ni nia Yake ya fadhili, na nilijua kuwa hakuna sehemu Yake ambayo humchukia mwanadamu. Upendo Wake kwa wanadamu haujabadilika tangu Alipoumba ulimwengu, hivyo, moyoni mwangu, nilikuwa tayari kufuatilia njia ya kuridhisha na kulipiza upendo wa Mungu katika imani yangu ya baadaye Kwake na kutimiza wajibu wangu. Hata hivyo, kwa sababu nia ya kupata baraka na kuendesha shughuli na Mungu imefanywa madhubuti sana katika mioyo ya watu, haiwezekani kutatua kabisa kwa kupitia jaribio moja tu. Baada ya muda fulani kupita, mambo haya yatajidhihirisha tena. Kwa hivyo, ili kutushinda zaidi na kabisa na kutuokoa, Yeye hufanya majaribio kadhaa ya mfululizo kwetu—jaribio la nyakati za kuadibiwa, jaribio la kifo, na majaribio ya miaka saba. Kati ya majaribio haya, nililopitia zaidi na kufaidika zaidi kutokana nalo lilikuwa jaribio la miaka saba la 1999.

Mnamo mwaka wa 1999, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Hii ilikuwa ni mwaka ambao injili ya ufalme ilienea sana, na nyumba ya Mungu ilihitaji kwamba tujaribu kumwokoa kila mtu aliyekuwa na uwezekano wa kuokolewa. Nilipoona utaratibu huu kutoka kwa nyumba ya Mungu, nilifikiri kazi ya Mungu ingekamilika mwaka wa 2000. Ili kujipatia roho zaidi na kupata hatima nzuri wakati ulipofika, nilijipa shughuli za injili kuanzia asubuhi hadi usiku. Kwa mintarafu ya maisha ya kanisa, nilikuwa nikihudhuria tu na kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati. Hata ingawa nilitambua kuwa nia zangu hazikuwa sawa, sikuwa na uwezo wa kudhibiti tamaa yangu ya kupata baraka. Wakati huo nilikuwa na shughuli nyingi, na nilihisi kuwa kufanya chochote kando na kazi ya injili kulikuwa kunanizuia, hata kula na kunywa neno la Mungu. Hivi ndivyo nilivyoanza kufanya kazi kwa ari kubwa, na bila ya kujua mwaka ulikuwa umekwisha. Nyumba ya Mungu ilikuwa imemchagua mtu wa mahali palepale ili kusaidia katika kazi, kwa hivyo nikarudi eneo la makazi yangu ya kudumu.

Nilidhani kwamba kazi ya Mungu itakapomalizika, janga kubwa hakika lingetokea, na hivyo baada ya kurudi nyumbani, nilisubiri tu janga nikiwa nyumbani kila siku, nikisubiri mwisho wa kazi ya Mungu. Nilipoona kwamba Sherehe ya Majira ya Kuchipua ilikuwa ikiwadia, kulikuwa na ushirika kutoka kwa kiongozi wa kanisa uliosema kuwa ni jambo la lazima kupitia miaka saba ya majaribio. Baada ya kusikia ujumbe huu, nilihisi kushtuka na moyo wangu ulikuwa katika msukosuko. Sikuwa na budi ila kuanza kujadiliana na Mungu: Miaka mingine saba imenikaribia—je, hii ni njia gani ya kuishi? Ee Mungu, ninakuomba Uniangamize mimi. Kwa kweli siwezi kuvumilia mateso haya tena! Siku iliyofuata, bado sikuweza kuepukana na mfadhaiko wangu. Nilidhani: Vyovyote vile, imekuwa miaka saba. Kesho ni siku nyingine—nitatoka na kuiondoa kutoka mawazo yangu. Mara tu nilipoingia kwenye basi, nilihisi Roho Mtakatifu alikuwa ndani yangu akishutumu: Wakati ulikuwa unatafuta bila kusita, ulikuwa umelipa gharama yako, na kusema kwamba ungempenda Mungu hadi mwisho, kwamba hungewahi kumwacha, kwamba ungevumilia ugumu wowote na kushiriki furaha zozote kwa pamoja. Ulikuwa mnafiki uliyejidanganya mwenyewe! Huku nikikabiliana na shutuma ya Roho Mtakatifu, sikuwa na budi ila kuning’iniza kichwa changu. Ilikuwa kweli. Awali, nilipokuwa nimefurahia neema ya Mungu, nilimpa ahadi, lakini sasa wakati ambapo kuna matatizo na ni lazima niyapitie, nataka kughairi neno langu. Hivyo si ahadi zangu ni za uongo tu? Mungu alinipa upendo mwingi sana, na sasa ninapokutana na mazingira ambayo sio kabisa kama ambavyo ninapenda nina hasira kubwa sana kiasi kwamba nataka kumghairi Mungu. Kwa kweli mimi ni mnyama asiye na shukrani, asiye bora kuliko mnyama! Nilipofikiri juu ya jambo hili, sikukuwa tena na hisia za kwenda nje, lakini nilirudi nyumbani na moyo mzito. Hata ingawa nilikuwa nimelazimishwa kuwa “mtiifu,” nilipofikiria ukweli kwamba bado kulikuwa na miaka saba iliyobaki katika kazi ya Mungu, niliweka huru katika moyo wangu na chochote nilichokifanya, sikuwa na haraka au wasiwasi. Nilitia bidii kila siku katika kutimiza wajibu wangu kana kwamba ilikuwa siku nyingine yoyote. Aina hii ya hali mbaya na yenye makabiliano ilinifanya nipoteze kazi ya Roho Mtakatifu hatua kwa hatua, na ingawa nilitaka kubadilisha hali yangu mwenyewe, sikuweza.

Siku moja, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno Yake yaliyosema: “Wakati baadhi ya watu walipotenda wajibu wao mara ya kwanza, walijaa nguvu, kana kwamba haingewahi kuishiwa na nguvu hizo. Lakini inakuwaje kwa kadri wanapoendelea ndipo wanapoonekana kupoteza nguvu hizo? Mtu waliokuwa wakati huo na mtu waliye sasa ni sawa na watu wawili tofauti. Kwa nini walibadilika? Sababu ilikuwa gani? Ni kwa sababu imani yao kwa Mungu ilienda njia mbaya kabla ya kufikia njia sahihi. Waliichagua njia mbaya. Kulikuwa na jambo lililokuwa limefichwa ndani ya kufuatilia kwao kwa kwanza, na kwa wakati mwafaka jambo hilo likaibuka. Nini kilikuwa kimefichwa? Ni matarajio yanayokuwa ndani ya mioyo yao wakati wakimsadiki Mungu, matarajio kwamba siku ya Mungu inawadia hivi karibuni ili taabu yao itafika mwisho; matarajio kwamba Mungu atabadilika na kwamba mateso yao yote yataisha(“Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinifanya nitafute mzizi wa tatizo hilo. Ilibainika kuwa nilikuwa na matumaini yaliyofichika ndani ya ufuatiliaji wangu, nikitumaini kwamba siku ya Mungu ingewadia hivi karibuni na kwamba singeweza kuteseka tena, kwamba ningekuwa na majaaliwa mazuri. Wakati huo wote, ufuatiliaji wangu ulitawaliwa na tumaini hili, na wakati ambapo matumaini yangu yalikuwa bure, niliteseka na kuvunjika moyo kiasi cha kumsaliti Mungu, hata kufikiri juu ya kuponyoka kupitia kifo. Ni wakati ule tu ndipo niliona kwamba nilikuwa nimemfuata Mungu kwa miaka mingi, lakini asili yake haikuwa kufuatilia njia ya kweli; daima nililenga siku ya Mungu, na nilikuwa nimefanya biashara na Yeye ili nipate baraka Zake. Hata ingawa wakati huo sikuwa na budi ila kukaa ndani ya nyumba ya Mungu na kutomwacha, ikiwa sikutatua uchafu ndani yangu, mapema au baadaye ningempinga na kumsaliti Mungu. Baada ya kuona hali yangu hatari, ndani ya moyo wangu nikamwuliza Mungu: Ninaweza kufanya nini ili kuondoa uchafuzi wa kutumaini siku ile? Kisha, nilisoma tena maneno ya Mungu, ambayo yalisema: “Je, ulijua kwamba kwa kumwamini Mungu huko Uchina, kuweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, kwamba wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. … Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi wa Mungu. Iliwahi kusemwa: ‘Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo.’ Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa? Mnafaa kuitembelea vipi njia iliyo mbele? Mnafaa kuufuatilia vipi ukweli? Kama hamfuatilii ukweli basi mnawezaje kuipata kazi ya Roho Mtakatifu? Pindi utakapopoteza kazi ya Roho Mtakatifu, basi utakuwa katika hatari kubwa zaidi. Mateso ya sasa si muhimu. Je, wajua yatakufanyia nini?(“Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kutoka kwa maneno haya ya Mungu, niliweza kuona kwamba kuna maana kubwa kwa watu leo kuwa na uwezo wa kuteseka, lakini sikuweza kutambua maana ya mateso hayo kweli ilikuwa nini. Nilijua tu kwamba kama ningeweza tu kubaini maana ya mateso ndio ningeweza kwa kweli kubadilisha hali yangu ya kutarajia siku ya Mungu. Hii ilikuwa njia ya kuelekea katika azimio. Ingawa sikufahamu maana ya mateso wakati huo, jambo pekee ambalo ningeweza kufanya ilikuwa kufuatilia ukweli kabisa, kutafuta ukweli zaidi, kwa sababu ikiwa tu ningepata ukweli ndio ningeweza kuelewa kweli maana ya mateso, na ndipo basi ningeweza kuondoa uchafuzi huu ndani yangu.

Kama kwamba muda ulikuwa umeongeza kasi, nilipepesa na tayari ilikuwa mwaka wa 2009. Hiyo miaka saba ilikuwa imepita muda mrefu, bila mimi kugundua. Nilikuwa nimefika mbali hivyo na hatimaye nilihisi kwamba miaka hiyo saba haikuwa muda mrefu kama nilivyofikiri. Hiyo miaka michache, katika hukumu iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu, katika ufunuo wa majaribu ya Mungu na usafishaji, nilikuwa nimeuona uso wangu wa kweli. Niliona kwamba nilikuwa, mtoto wa joka kuu jekundu kabisa, kwa sababu nilijawa na sumu lake, kama vile sumu ya “Usiamke mapema ikiwa hakuna faida, faida huongoza katika kila kitu.” Huu ni uwakilishi bora zaidi wa sura ya joka kuu jekundu. Chini ya utawala wa sumu hii, imani yangu kwa Mungu ilikuwa tu kubarikiwa. Niliyotumia kwa ajili ya Mungu kilikuwa na mpaka wa muda, na nilitamani kuteseka kidogo na kupata baraka kubwa. Ili kuniondolea nia hii thabiti ya kubarikiwa na mtazamo wa kibiashara uliokuwa ndani yangu, Mungu alikamilisha majaribio mengi na usafishaji kwangu. Wakati huo tu ndipo uchafu katika imani yangu kwa Mungu ulipotakaswa. Na nikaona ndani ya ufunuo wa Mungu kwamba nilikuwa nimejaa tabia mbaya ya Shetani. Nilikuwa na kiburi, udanganyifu, ubinafsi na mwenye kustahili dharau, mzembe, na mwenye shingo upande. Yalinifanya nione wazi zaidi na zaidi hali yangu halisi, kuona kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani, kwamba nilikuwa mwana wa kuzimu. Kwamba ningeweza kumwamini Mungu na kumfuata Mungu wakati huo ilikuwa kweli kukuzwa na Yeye na neema, na kwamba ningeweza kukubali hukumu na kuadibiwa na Yeye vilikuwa baraka kubwa zaidi. Shukrani yangu kwa Mungu ilikua, mahitaji yangu yakawa madogo, utiifu wangu Kwake ukakua, na kujipenda kwangu mwenyewe kukapungua. Niliomba tu kuwa na uwezo wa kupoteza tabia yangu potovu ya kishetani, kuwa mtu ambaye anamtii na kumwabudu Mungu kweli. Tokeo hili dogo lilipatikana baada ya kazi nyingi ya Mungu isiyojulikana kiasi, ikiwa ni pamoja na jitihada Zake nyingi sana. Hadi leo, kupitia kazi ya Mungu, nimekwisha kufahamu kwamba wokovu wa watu kwa kweli si rahisi. Kazi Yake ni ya vitendo sana—kazi Yake ya kuwabadilisha na kuwaokoa wanadamu sio rahisi kama ambavyo watu wangefikiria. Hivyo, sasa mimi si kama mtoto mjinga, kutumaini tu kwamba siku ya Mungu itakuja kwa haraka, lakini daima ninahisi kuwa upotovu wangu ni mkubwa sana, kwamba ninahitaji sana wokovu wa Mungu na ninahitaji sana kupitia hukumu na kuadibiwa na Yeye, majaribio Yake na usafishaji Wake. Lazima sasa niwe na dhamiri kidogo na mantiki ambavyo vinapaswa kuwepo katika ubinadamu wa kawaida, na kikamilifu kuipitia kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu. Mwishoni wakati ambapo nitaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli na kupokea furaha ya Mungu, moyo wangu utatimizwa. Sasa, ninapoangalia nyuma na kufikiri juu ya kile nilichofichua juu yangu wakati ambapo miaka hiyo saba ya majaribio ilinijia, ninahisi kwamba nina deni kubwa kwa Mungu, kwamba niliujeruhi moyo Wake sana. Kama kazi ya Mungu ingekamilika mwaka 2000, mimi, ambaye nilikuwa mchafu sana kabisa, hakika ningeangamizwa. Miaka saba ya majaribio kweli ilikuwa uvumilivu wa Mungu na huruma kwangu, na aidha, ilikuwa ni wokovu wa Mungu wa kweli zaidi na halisi zaidi kwangu.

Mara nilipokuwa nimetoka katika miaka hiyo saba na nilitafakari maneno hayo kutoka kwa Mungu ambayo sikuwa nimeyaelewa awali: “Je, ulijua kwamba kwa kumwamini Mungu huko Uchina, kuweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, kwamba wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. … Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi wa Mungu. Iliwahi kusemwa: ‘Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo.’ Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa?” Niliweza kuelewa maana kidogo ya maneno haya; niliweza hatimaye kuhisi kuwa mateso ni yenye umuhimu kweli. Ingawa niliteseka nilipopitia majaribio haya, baada tu ya kuteseka ndipo niliona kwamba kile nilichopata kilikuwa cha thamani sana, muhimu sana. Kwa kupitia majaribio haya, niliona tabia yenye haki ya Mwenyezi na uweza wa Mungu na hekima. Nilielewa ukarimu wa Mungu, na nilionja upendo wa kina, wa baba wa Mungu kwa watoto Wake. Pia nilipitia mamlaka na nguvu katika maneno Yake, na niliona ukweli wa kupotoshwa kwangu na Shetani. Niliona dhiki ya Mungu katika kazi Yake ya wokovu, kwamba Yeye ni mtakatifu na mwenye kuheshimiwa, na kwamba watu ni wabaya na wa kudharauliwa. Pia nilipitia jinsi Mungu anavyoshinda na kuwaokoa wanadamu ili kuwaleta kwenye njia sahihi ya kumwamini. Ninapolifikiria sasa, kama Mungu hakuwa amefanya kazi hii ngumu ya majaribio kwangu baada ya majaribio, nisingeweza kuwa na ufahamu huu. Dhiki na usafishaji vina manufaa katika ukuaji wa watu katika maisha yao. Kwa kuvipitia, watu wanaweza kupata kitu cha maana na cha thamani sana katika kipindi chao cha kumwamini Mungu—ukweli. Baada ya kuona thamani na maana ya mateso, mimi tena sina ndoto ya kuingia katika ufalme nikiwa nimeabiri motokaa, lakini nina nia ya kusimamisha imara miguu yangu na kupitia kazi ya Mungu, kufuatilia kwa kweli ukweli ili kujibadili.

Kwa kupitia miaka kadhaa ya kazi ya Mungu, ndipo sasa tu nina ufahamu mdogo wa vitendo wa maneno haya kutoka kwa Mungu: “Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Kabla ya kupitia majaribio haya kutoka kwa Mungu, nilikuwa nimejaa nia kali ya kubarikiwa na mtazamo wa kishughuli. Hata ingawa nilijua kikanuni kuamini katika Mungu kulikuwa nini na lengo la imani katika Mungu lilikuwa nini, bado nilikuwa nimelenga tu kubarikiwa. Sikujali ukweli, sikuondoa tabia yangu potovu ili kuyakidhi mapenzi ya Mungu, au kumtambua Mungu kama lengo la ufuatiliaji wangu. Ni wakati ule tu ndipo nilielewa kwamba Mungu alipokuwa mwili kazi Yake ya msingi ilikuwa kutatua nia ya wanadamu ya kubarikiwa na mtazamo wao wa kishughuli. Ilikuwa ni kwa sababu mambo haya kweli ni vikwazo kati ya wanadamu na kuingia kwao kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Mambo haya yanapofichwa ndani ya wanadamu, hawatafuatilia ukweli. Hawatakuwa na lengo sahihi katika ufuatiliaji wao; watatembea katika njia isiyo sahihi. Hii ni njia ambayo haitambulikani na Mungu. Sasa, kazi ya Mungu ya kushinda na wokovu imeharibu ngome ya Shetani ndani yangu. Hatimaye sina wasiwasi tena, sina tena fikira za kupatia baraka au kupitia janga. Sifuatilii tena kwa uchungu tamaa zilizopita kiasi, na sizungumzii tena masharti au kutoa mahitaji ili kuepuka janga hilo. Bila uchafu huu, najihisi mwepesi, huru. Ninaweza kufuatilia ukweli kwa utulivu na kikamilifu. Hili ndilo tunda lililotokana na majaribio na usafishaji wa Mwenyezi Mungu. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu ya majaribio na usafishaji ambavyo vimeniongoza kwenye njia ya kweli ya kumwamini Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali kazi zaidi ya majaribio ambayo Mungu hufanya, bila kujali jinsi usafishaji wenye maumivu ninaoupitia, nitatii na kukubali, na kuyapitia kwa kweli. Nitatafuta ukweli kutoka kwazo, na kufikia tabia isiyo na upotovu ili kukidhi mapenzi ya Mungu, ili kulipiza miaka mingi ya Mungu ya juhudi ya bidii.

Iliyotangulia: Utajiri wa Maisha
Inayofuata: Hukumu ni Mwanga

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nilifurahia Karamu Kubwa

Xinwei Mkoa wa Zhejiang Juni 25 na 26, mwaka wa 2013 zilikuwa siku zisizosahaulika. Eneo letu lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na...

Ulinzi wa Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp