Kwa Nini Ulimwengu wa Kidini Daima Unaipinga na Kuishutumu Kazi Mpya ya Mungu kwa Hasira
Nyakati mbili ambapo Mungu amekuwa mwili ili kutembea duniani na kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu, Amekumbana na upinzani mkubwa sana, lawama na mateso yenye hasira kutoka kwa viongozi katika ulimwengu wa kidini. Huu ukweli umewakanganya na hata kuwashtua watu: Kwa nini kila wakati Mungu anafichua hatua ya kazi mpya kila mara Yeye hutendewa kwa namna hii? Mbona wale ambao humpinga Mungu kwa hasira na hima ni viongozi wa kidini ambao husoma Biblia tena na tena na ambao wamemtumiia Bwana kwa miaka mingi? Kwa nini viongozi hao wa kidini ambao watu huwaona kama wanaomcha Mungu sana, walio waaminifu sana na watiifu sana kwa Bwana kwa hakika hushindwa kulingana na Mungu, bali badala yake ni maadui wa Mungu? Je, inawezekana kuwa kwamba kazi ya Mungu si sahihi? Je, inawezekana kuwa kwamba matendo ya Mungu hayafuati mantiki? Hakika hiyo si kweli! Kuna sababu mbili za msingi mbona viongozi wa kidini wanaweza kuchukua wajibu wa kumpinga Mungu na kuwa maadui wa Mungu, na hizi ni: Sababu ya kwanza inategemea watu hawa kukosa maarifa ya kazi ya Roho mtakatifu, wala hawana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu. Kila mara wao hutegemea maarifa yao kidogo ya Biblia, nadharia za teolojia na dhana na mawazo ya watu ili kuiwekea mipaka kazi ya Mungu ambayo ni mpya daima na si ya kale kamwe; sababu ya pili ni kuwa, kwa kuwa wanadamu wamepotoshwa sana na Shetani, asili yao ni yenye kiburi na ya kujipenda, wanadharau na kuuchukia ukweli, na haswa wathamini cheo. Zikiwekwa pamoja, sababu hizi mbili zimesababisha janga la wanadamu kuiacha na kuishutumu njia ya kweli kila wakati na pia kote katika historia.
Tukikumbuka miaka elfu mbili iliyopita wakati ambapo Bwana Yesu alikuwa miongoni mwa watu wa Kiyahudi, Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, akisema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17). Alionyesha ukweli, Akaleta njia ya kutubu, Akamsaidia mwanadamu kwa kuwaponya wagonjwa na kufukuza pepo, Akafanya ishara, maajabu na miujiza mingi, na Akampa mwanadamu neema na amani na furaha nyingi na tele. Haya yote ni mambo ambayo hayakunukuliwa katika Agano la Kale, na pia ilikuwa kazi ambayo hakuna mtu aliwahi kuifanya awali. Bila shaka, pia lilikuwa jambo ambalo hakuna mwanadamu angeweza kulitekeleza, kwa sababu kando na Mungu hakuna mtu aliye na mamlaka na uwezo wa kufanya mambo kama hayo. Kile ambacho Bwana Yesu alifanya wakati huo kilikuwa kazi ya kuzichukua dhambi za mwanadamu binafsi kwa kusulubiwa msalabani na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi, ili Aweze kumwongoza mwanadamu kutoka kwenye vifungo vya kanuni na sheria, na kumruhusu mwanadamu asiadhibiwe kwa kutoweza kuifuata sheria; wale watu walio chini ya sheria wangeweza tu kupata wokovu wa Mungu na kutoangamizwa kwa kuikubali kazi ya Bwana Yesu. Lakini makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa dini ya Kiyahudi hawakuitambua kazi ya Roho Mtakatifu na hawakuelewa ni kazi gani ambayo Bwana Yesu alikuwa akiitekeleza. Katika dhana zao waliamini kwamba mtu yeyote ambaye hakuomba kwa jina la Yehova Mungu alikuwa akimsaliti Mungu, mtu yeyote ambaye alihubiri ujumbe usiopatana na sheria alikuwa akiwadanganya watu, na chochote ambacho kilikuwa nje ya Biblia kilikuwa uzushi. Zaidi ya hayo, walijishaua kuwa wanazijua sheria vizuri na kuwa watumishi wa Yehova Mungu katika hekalu kwa miaka mingi, na waliamini kwamba kile walichokizingatia kilikuwa ukweli na njia safi kabisa. Kwa maoni yao, kazi ya Bwana Yesu ilikiuka sheria na kwenda nje ya Biblia, kama njia kando na Biblia. Na hata walisema kuwa Bwana Yesu alinena maneno ya kukufuru kwa kulinyang’anya jina la Mungu na kwamba Alikuwa Akimsaliti Yehova Mungu. Kwa sababu ya jambo hili, heri wangekufa kuliko kuikubali njia ambayo ilikuwa ikihubiriwa na Bwana Yesu. Hata waliiona kazi ya Bwana Yesu kama “uzushi,” “dhehebu baya” na “kumdanganya mwanadamu.” Ingawa kazi na neno la Bwana Yesu lilikuwa na mamlaka, nguvu na hekima, ingawa miujiza ambayo Bwana Yesu alidhihirisha ilikuwa ya kipekee katika historia, ingawa watu wengi zaidi walikuja kushuhudia matendo ya Bwana Yesu na kushuhudia ukweli kwamba Bwana Yesu alikuwa ni kuja kwa Masihi, bado walishikilia mawazo yao kwa ukaidi na kwa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria, na waliipinga na kuishutumu kabisa kazi mpya ya Mungu kwa ukaidi—kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu. Mtazamo wao kuhusu kazi mpya ya Mungu ulikuwa jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu amefichua: “Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko—lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu). Kama mtu anayemwamini Mungu, angalau mtu anapaswa kuwa na moyo unaomcha Mungu na kuwa na njaa na kiu ya haki. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu ataweza kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu, kutimiza ufahamu wa kazi mpya ya Mungu na kuzifuata hatua za Mungu kwa karibu. Lakini wale makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo waliwasiliana na Bwana Yesu na kukutana naye mara nyingi, ilhali haikuwa kuufuatilia ukweli kamwe. Walikuwa wakibuni njia na mbinu za kumjaribu Bwana Yesu na kupata kitu cha kutumia dhidi ya Bwana Yesu (tazama Mathayo 22: 15-46), wakijaribu kuiharibu na kuikomesha kazi ya Bwana Yesu. Wote walikuwa sawa kwani hawakumjua Mungu, na kwamba walishikilia dhana kuhusu kazi mpya ya Mungu, lakini Nathanaeli na mwanamke Msamaria na wanafunzi na watu wa kawaida waliomfuata Bwana Yesu waliweza kuweka kando dhana zao na kuutafuta ukweli. Kwa njia hii, waliweza kuisikia sauti ya Mungu kupitia kwa kazi na maneno ya Bwana Yesu, kutambua kwamba Bwana Yesu alikuwa ni kuja kwa Masiya, na kurudi kwa Mungu. Kupitia kwa mlingano huu tunaweza kuona kwamba watu wa ngazi za juu za ulimwengu wa dini wa Kiyahudi hawakuwa tu wasiopenda kubadili mambo kwa ukaidi na bila maarifa ya kazi ya Mungu, lakini pia wenye kiburi na wa kujidai, na walikataa kabisa kuukubali ukweli. Hii ilikuwa moja ya sababu za wao kumpinga Mungu.
Sababu nyingine ilikuwa kwamba, kwa kuwa maneno na kazi ya Bwana Yesu yalikuwa na ukweli na mamlaka na yangeweza kukimu mahitaji ya maisha ya mwanadamu, watu wengi zaidi wa kawaida wa Kiyahudi walianza kumfuata Bwana Yesu, na hivyo makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo walikuwa na wasiwasi kuhusu watu wote wa kawaida kumfuata. Watu walipokuwa hawawaabudu au kuwafuata tena walikuwa na wasiwasi zaidi, kwa sababu walijua wazi katika mioyo yao kwamba hawangeweza kabisa kufikia mamlaka na nguvu ya maneno na kazi ya Bwana Yesu, na kwamba mradi Bwana Yesu angebaki duniani, watu wengi zaidi wa kawaida wangewaacha na kumfuata Bwana Yesu, na kungekuwa na watu wachache zaidi hekaluni, ikiwasababisha kutoweza kuendelea kufurahia maisha yao ya mamlaka ya juu kabisa, kuungwa mkono na wengine na wao kuwakimu. Kwa hiyo, Bwana Yesu alikuwa kama sindano katika jicho lao au mwiba katika mwili wao, na Akawa adui Aliyechukiwa ambaye hawangeweza kuishi naye kwa amani. Kwa hiyo walizungumza kuhusu Yesu, wakisema: “Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamsadiki: nao Warumi watafika na kuichukua nafasi yetu na taifa letu” (Yohana 11:47-48). Ili kuzilinda nafasi zao, walifikiri kuhusu kila kitu ambacho wangeweza kufanya na kutumia kila namna za mbinu zenye kustahili dharau ili kuleta mashtaka ya uwongo dhidi ya Bwana Yesu. Waliikufuru na kuishutumu kazi ya Bwana Yesu, walimsingizia na kumkashifu Bwana Yesu, wakisema kwamba Alimtegemea Beelzebuli ili kutoa pepo (tazama Mathayo 12:24), na wakatoa ushuhuda wa uwongo, wakimhukumu na kumsingizia Bwana Yesu (tazama Marko 14: 55-58). Hata walishirikiana na watu wenye mamlaka wa Kirumi kumsulubisha msalabani kikatili. Bwana Yesu alipofufuliwa, Aliwaonekana mbele ya wanafunzi Wake kwa siku 40 na kisha Akapaa mbinguni, na nguvu na miujiza ziliandamana na kuenezwa kwao kwa injili. Ukweli huu ulitosha kuthibitisha kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu wa kweli, kwamba kazi Yake ilikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake, kwamba ilithibitishwa na Roho Mtakatifu, na kwamba ilikuwa njia ya kweli! Katika hali hizi, wale makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo hawakukosa kufikiria tena tu kuhusu hali yao, lakini badala yake walitenda kwa kisingizio cha “kudumisha sheria na kuilinda njia ya kweli” na waliendelea kutumia nguvu zao kwa kupanga njama na watawala wao ili kuzidisha ukandamizaji wao, mateso na kuchinjwa kwa wafuasi wa Bwana Yesu kwa hasira. Walifanya kila wawezalo ili kuwazuia watu wasimfuate Bwana Yesu, hata walimzuia kabisa mtu yeyote asilieneze jina la Bwana Yesu.... Ili kuzilinda nafasi zao wenyewe na riziki zao, hakika hakukuwa na uhalifu ambao hawangetenda, jambo ambalo lilionyesha kabisa asili yao ya kishetani ya kuuchukia ukweli na kuwa maadui wa Kristo. Hii ndiyo ilikuwa sababu nyingine ya upinzani na shutuma yao yenye hasira kwa Bwana Yesu. Matendo yao maovu yaliikosea tabia ya Mungu na kuchochea ghadhabu ya Mungu. Mwishowe, jamii nzima ya Wayahudi ilipitia maumivu ya pekee ya kutiishwa kwa kitaifa, ambayo ilikuwa ni gharama ya uchungu waliyolipa kwa kumpinga Mungu na kumshutumu Mungu.
Sasa tuko katika siku za mwisho, na Mungu ameandaa wokovu mkubwa zaidi kwa wale ambao wamekombolewa na Yeye. Wokovu huu ni Mungu kupata mwili tena na kuuonyesha ukweli ili kumhukumu na kumtakasa mwanadamu. Sasa Anatenda kazi mpya ya hukumu Akiianzia nyumba ya Mungu. Hatua hii ya kazi itamwondolea kabisa mwanadamu tabia yake potovu ya kishetani. Itamweka mwanadamu huru kutokana na ushawishi wa giza wa Shetani na kuwageuza wanadamu wawe jamii inayomjua Mungu, inayolingana na Mungu na iliyo ya Mungu kweli, ili kwamba wanadamu watapata wokovu na kupatwa na Mungu. Hii ndiyo hatua ya mwisho ya kazi katika mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu alionekana na kuanza kazi Yake, wale kutoka katika madhehebu mbalimbali wanaoupenda ukweli na ambao wametamani kuonekana kwa Mungu, wamesoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na kuamua kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu yana mamlaka na nguvu, na kwamba hayo ni maonyesho ya ukweli, na kwa hakika ni sauti ya Mungu, na hivyo mmoja baada ya mwingine wameikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Mwonekano wa pekee wa mataifa yote yakimiminika kwenye mlima umeonekana. Sasa, injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu inaenea katika kila taifa na kila upande duniani kote hivi sasa; matawi mapya ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanaanzishwa moja baada ya lingine katika nchi na mikoa ya kigeni; watu wengi zaidi duniani kote wameanza kuikubali injili ya Mungu ya siku za mwisho. Hii inafichua kabisa uweza na hekima ya Mungu. Hata hivyo, wakiwa wamekabiliwa na ukweli huu wote, wakiwa wamekabiliwa na ajabu kubwa sana na ushuhuda wa kazi ya Roho Mtakatifu, viongozi katika ulimwengu wa kidini wamepuuza na hawazijali hata kidogo. Watu hawa ni sawa na Mafarisayo, hawatambui kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inaendelea kusonga mbele, na kwamba kazi ya Mungu ni mpya daima nayo si nzee kamwe. Wanaikubali tu kanuni moja isiyobadilika: Mahubiri yoyote ambayo yanasema kwamba Bwana amekuja katika mwili ni ya uwongo; wote wanaohubiri kuhusu Mungu aliye na jina tofauti na Bwana Yesu ni wazushi; maneno yote ya Bwana yamo katika Biblia, chochote kilicho nje ya Biblia si njia ya kweli, na kutofuata masharti ambayo Mungu alimhitaji mwanadamu ayafuate katika Enzi ya Neema ni kwenda nje ya mafundisho ya Kristo. Zaidi ya hayo, hata wanasadiki kwa kujiamini sana kwamba wao ni stadi katika Biblia na wameyapata maisha baada ya kufanya kazi na kuhubiri kwa miaka mingi, kwamba mambo tu wanayoyakubali, walio na ufahamu kuyahusu na wanaoishikilia njia ya kweli, na chochote zaidi ya hili ni uzushi au dhehebu baya. Watu hawa wamemwekea Mungu mipaka kabisa ndani ya Biblia, na wamemwekea mipaka ndani ya kazi ya Mungu ya zamani. Haijalishi ni kiasi gani cha ukweli ambacho kazi iliyoletwa na Mwenyezi Mungu ilicho nacho, kiasi gani cha kazi ya Roho Mtakatifu ilicho nacho, jinsi inavyoweza kukimu mahitaji ya watu, na ni kweli ngapi zilizoko ili kuithibitisha, hawatambui kwamba inatoka kwa Mungu. Hawakosi kutafuta na kuchunguza tu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini wana uhasama kuihusu na wanaikataa, sana kiasi kwamba wanaukufuru mwili wa Mungu na kuikashifu na kuishutumu kazi na neno la Kristo katika siku za mwisho. Wao ni sawa tu na Mafarisayo wa zamani—wakaidi na wenye kiburi, wakiudharau ukweli na kumkufuru Roho Mtakatifu! Ni jinsi tu Mwenyezi Mungu anavyosema: “Kama unapata kumjua Mungu kutokana na hatua moja ya kazi Yake tu, basi maarifa yako ni kidogo, kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama si hivyo, kwa nini wengi wa walinzi wa kidini wa kale walimtundika Mungu msalabani akiwa hai? Je, si kwa ajili mwanadamu humwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani? Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasiojua na wasio na habari ya kutosha jinsi na wanajaribu kuonyesha walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha ‘wasomi’; wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu)
Watu wengi wanaomwamini Bwana kwa kweli wanaporudi kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu, upanuzi wa taratibu wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho unafikia kilele chake. Lakini hata kazi ya Roho Mtakatifu ikiwa inasitawi sana, haijasababisha viongozi wa kidini ambao wamezoea kuwa wenye majivuno sana na wataalam wa kidini ambao huwaamuru wengine kutafakari kujihusu, wala kuinamisha vichwa vyao vyenye kiburi kutafuta na kuchunguza. Badala yake, watu hawa wanafahamu kuwa nafasi zao zinakuwa zenye kupinduliwa zaidi na zaidi na wanaweza kupinduka wakati wowote, na hata zaidi wanaogopa kwamba kila mtu atamgeukia Mwenyezi Mungu na hakuna mtu atakayewafuata, na makanisa yao yatafungwa na kufilisika. Kwa hiyo, ili “kuiokoa siku,” wachungaji, wazee, viongozi na wafanyakazi wenzi kutoka madhehebu mbalimbali hutenda kwa kisingizio cha “kulichunga kundi kwa ajili ya Bwana na kuidumisha njia ya kweli.” Wamebuni na kusambaza vifaa vya propaganda ambavyo vinamkufuru na kumshambulia Mwenyezi Mungu kwa utundu, na wamevibandika kwenye aina mbalimbali za majukwaa ya mtandao wakiwashawishi watu kumpinga Mungu. Hata wao husema mambo ambayo hupotosha na kutafsiri ukweli vibaya na kulikashifu Kanisa la Mwenyezi Mungu kama dhehebu la uzushi, na wao huwazuia kabisa waumini wao wasivisome vitabu vya Umeme wa Mashariki au kusikiliza mahubiri ya Umeme wa Mashariki. Hawawaruhusu waumini wawapokee watu wanaohubiri wokovu wa Mungu katika siku za mwisho au hata wageni wowote, na wao huenda kinyume cha mafundisho ya Mungu kabisa katika Enzi ya Neema wakati Alipomtaka mwanadamu kuwakaribisha wageni kwa huruma. Watu hawa wanafahamu kikamilifu kwamba wale wanaomfuata Mwenyezi Mungu ni watu wakarimu ambao wanamwamini Mungu kweli, na hata wanafahamu zaidi kwamba hakuna madhumuni mabaya yoyote katika watu hawa kuhubiri kuhusu wokovu wa Mungu katika siku za mwisho, ilhali bado wanawatukana na kuwafukuza kwa njia isiyo na ustaarabu na ya kikatili, na hata kuwashambulia ndugu na dada ambao huieneza injili. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba, licha ya kuwa waumini katika Mungu, watu hawa wanashirikiana na utawala wa kishetani wa Chama cha Kikomunisti cha China, wakijihusisha katika shughuli ya hila na mbovu ya kumsaliti Bwana na kuwasaliti marafiki zao, wakiwafuatilia, kuwasimamia na kuwaripoti ndugu na dada ambao hueneza injili ya siku za mwisho, na hata wao hutumika kama wapelelezi katika kanisa ili kukusanya habari kwa ajili ya Chama cha Kikomunisti cha China kuwakamata Wakristo kwa siri. Inaonekana kwamba wanaweza tu kuhisi afueni kutokana na chuki iliyo mioyoni mwao kwa kuwaua kwa mkupuo mmoja wale wanaomshuhudia Mungu na kuikomesha kazi mpya ya Mungu. Je, si hawa viongozi wa kidini ni watumwa wabaya ambao Bwana Yesu alizungumzia? Bwana Yesu akasema: “Kulikuwa na mwenye nyumba fulani, aliyepanda shamba la zabibu, na akalizingira kwa ua, na akachimba kishinikizo cha zabibu ndani yake, na akajenga mnara, na akalipangisha kwa wakulima, na akasafiri kwenda nchi ya mbali: Na wakati wa matunda ulipokaribia, aliwatuma watumwa wake kwa wakulima, ili waweze kupokea matunda yake. Na wakulima wakawachukua watumwa wake, wakampiga mmoja, na kumuua mwingine, na kumpiga mwingine kwa mawe. Tena, akawatuma watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza: na wakawafanyia vivyo hivyo. Lakini mwishowe kabisa alimtuma mwanawe kwao, akisema, Watamheshimu mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona mwana huyo, walisema miongoni mwao, Huyu ndiye mrithi; njooni, tumuue, na tutwae urithi wake. Na wakamshika, wakamtupa nje ya shamba la zabibu, na wakamchinja. Basi wakati bwana wa shamba la zabibu atakapokuja, atawafanyaje wakulima hao? Wakamwambia, atawaharibu kabisa watu hao waovu, na atapangisha shamba hilo la zabibu kwa wakulima wengine, ambao watampa matunda wakati wa kipindi chake” (Mathayo 21:33-41). Kwa hiyo inaweza kuonekana kwamba sababu ya msingi ya wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini kumshutumu na kumpinga Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni sawa na ile ya Mafarisayo wa Kiyahudi ambao walimpinga Bwana Yesu—daima wao hupanga njama kwa ajili ya nafasi zao wenyewe, wakikimbia hapa na pale kwa ajili ya maslahi yao wenyewe, na kuweka mioyo na nguvu zao zote katika kuridhisha tamaa zao wenyewe. Asili na kiini chao cha kishetani kinachowafanya kuchoshwa na ukweli, kuuchukia ukweli na kupinga Mungu basi kinafichuliwa. Bwana Yesu alipokuja, Aliwafichua Mafarisayo wa Kiyahudi waliokuwa wanafiki; sasa Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho naye Anazifichua kabisa nguvu zinazompinga Kristo za ulimwengu wa dini! Isingekuwa Mungu kuonekana na kutekeleza kazi Yake, hakuna mtu ambaye angeweza kuubaini uso wa kweli unaomwasi Mungu wa wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini. Kuonekana na kazi ya Mungu mwenye mwili humfichua mwanadamu kweli.
Baada ya ushirika huu, naamini kwamba kila mtu atakuwa na ufahamu kidogo kuhusu sababu ya msingi ya kwa nini ulimwengu wa dini huipinga kazi mpya ya Mungu daima! Watu wa kawaida wa Kiyahudi katika siku za Yesu hawakuwa na ufahamu kuhusu kiini cha Mafarisayo, kilichompinga Mungu na kuuchukia ukweli, na hivyo waliwaabudu na kuwafuata. Hawakuitafuta au kuchunguza kazi mpya ya Mungu, bali waliikataa na kuipinga tu bila kufikiri na hatimaye waliadhibiwa na Mungu. Hii ilisababisha taifa la Israeli kutiishwa kwa karibu miaka elfu mbili na kuchinjwa kwa Wayahudi wengi mno. Sasa, kazi ya hukumu inayoanza katika nyumba ya Mungu inayotekelezwa na Mwenyezi Mungu imefikia tukio la pekee, na hivi karibuni itaisha katika utukufu kwa kuwa Mwenyezi Mungu ataonekana wazi kwa mataifa yote na watu wote. Sasa katika wakati huu muhimu, tunasikiliza maneno ya wachungaji na wazee, au tunachunguza kazi mpya ya Mungu? Swali hili linahusiana moja kwa moja na ikiwa tunaweza kupata wokovu wa Mungu au la. Bwana Yesu alisema: “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata” (Yohana 10:27). Je, wewe ni mmoja wa kondoo wa Mungu? Kwa hiyo unapaswa kuchagua kwa namna gani?
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?