Kanisa la Kweli ni Nini? Tunaweza Kulipataje Kanisa Litakalonyakuliwa Kabla ya Maafa?

19/07/2020

Na Baoda, Australia

Ulimwengu uko katika hali ya machafuko, kila aina ya maafa yakiwakumba wanadamu. Watu wengi wanajiuliza: “Je, Bwana amerudi tayari? Na ikiwa Amerudi, kwa nini hatujanyakuliwa kabla ya maafa makubwa?” Wengine huona wachungaji na wazee wao wakihubiri juu ya mambo yale yale ya zamani kila wakati, imani ya waumini ikififia, waumini wakifuata mienendo ya kidunia na wakishindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Bwana. Kisha wanajiuliza ikiwa kanisa la Kikristo ni kama kanisa la Laodikia ambalo liliachwa na Bwana. Katika barua kwa kanisa la Filadefia katika Ufunuo, inasema, “Navijua vitendo vyako: tazama, nimeweka mlango ulio wazi mbele yako, na hakuna mtu anayeweza kuufunga: kwani una nguvu kidogo, na umelishikilia neno Langu, na hujalikana jina Langu(Ufunuo 3:8). Tunaweza kuona kwamba wale walio katika kanisa la Filadelfia peke yao ndio wanaoweza kushikilia maneno ya Bwana katika hali yoyote na kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wao tu ndio ambao wamenyakuliwa kwa kweli kabla ya maafa makubwa, na ni kanisa la aina hii pekee, lililo na kazi ya Roho Mtakatifu, ndilo kanisa pekee la kweli. Watu wengine hulinganisha hili na hali ya sasa ya kanisa la Kikristo na wanatamani kuondoka ili watafute kanisa la kweli. Hata hivyo, kuna wengine wanaoamini kwamba kanisa linasitawi, mashindano ya ufahamu wa watu kuhusu Biblia yakifanywa kukiwa na hali ya kusisimua ya kila aina ya sherehe za likizo. Wao huwaza, “Je, hii siyo kazi ya Roho Mtakatifu? Kanisa la aina hii ndilo kanisa la kweli na hakika litanyakuliwa.” Lakini ni mtazamo upi ulio sahihi? Kanisa la kweli ni nini? Na, je, tunapaswa kutofautishaje kati ya kanisa la kweli na makanisa ya uwongo? Hebu tufanye ushirika juu ya maswali haya.

Kanuni ya kwanza ya kutambua kati ya kanisa la kweli na makanisa ya uongo: Je, lina kazi ya Roho Mtakatifu na, je, washiriki wake hufuatilia ukweli?

Biblia inasema, “[Kanisa] … ni mwili Wake, ukamilifu wa Yeye anayekamilisha yote katika yote” (Waefeso 1:23). Yehova Mungu alimwambia Sulemani, “Kwa kuwa sasa Nimechagua na kutakasa nyumba hii, ili jina Langu liwe hapo milele: na macho Yangu na moyo Wangu yawe hapo kwa kudumu(2 Mambo ya Nyakati 7:16). Na neno la Mungu linasema, “Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo pia matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikiwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo katika mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na hali ikiwa mbaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee utunzaji na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda hata wakaadhibiwa. Bila kujali wao ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo katika mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake(“Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba kanisa ni hekalu la Mungu, kwamba Mungu hulitunza na kwamba linatambuliwa na Mungu. Kanisa la kweli lina kazi ya Roho Mtakatifu; linajuimuisha watu wanaoikubali kazi ya sasa ya Mungu, na wanaoishi ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu na wanaofuatilia ukweli. Katika kanisa kama hili, waumini hukusanyika pamoja ili kushiriki juu ya matamko ya sasa ya Mungu; wanapata nuru na mwangaza kutoka kwa Roho Mtakatifu, wanayaelewa mapenzi na matakwa ya Mungu, wanaendelea zaidi na zaidi katika maisha yao, na wanaweza kushiriki ushuhuda juu ya kutenda maneno ya Mungu katika maisha yao ya kila siku. Bwana Yesu alipokuja kutekeleza kazi Yake, wale waliomwamini Mungu kwa dhati na kumfuata Bwana Yesu waliungana pamoja kuunda kanisa. Waliikubali njia ya toba iliyohubiriwa na Bwana na hawakuwa chini shutuma za sheria kama walivyokuwa hapo awali. Tabia yao ilifanywa kulingana na maneno ya Bwana, wakionyesha uvumilivu, ustahimilivu na msamaha kwa wengine, na kadhalika. Chini ya mwongozo wa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, ubinadamu wao na kile walichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yao kikawa kinachofaa zaidi na zaidi. Pia waliona jinsi ambavyo Bwana alivumilia mateso na udhalilishaji mkubwa na Alisulibiwa kwa ajili ya mwanadamu, jinsi Alivyowakomboa wanadamu, na walielewa kwamba tabia ya Mungu ni yenye huruma na upendo. Imani yao katika Mungu ilikua zaidi na zaidi. Hili linatuambia kwamba kanisa la aina hii lina kazi ya Roho Mtakatifu, kwamba ndilo kanisa la kweli. Kinyume chake, kanisa lolote ambalo linakosa kazi ya Roho Mtakatifu ni kanisa la uwongo. Kwa mfano, mwishoni mwa Enzi ya Sheria, Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, na kisha kazi ya Roho Mtakatifu ilibadilika. Hekalu likawa lenye ukiwa. Makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa Kiyahudi hawakukubali kazi ya wakati huo na maneno ya Bwana Yesu. Ingawa walionekana kufuata mari na sheria, walikosa kazi ya Roho Mtakatifu, hadi mwishowe hawakuweza kufuata sheria zao wenyewe. Vitendo visivyo halali kama vile wizi, mauaji na uzinzi vilikuwa vimeenea pote. Hekalu halikuwa tena mahali pa kuabudu, lakini badala yake lilikuwa pango la wezi ambapo pesa zilibadilishwa na ng'ombe na njiwa walinunuliwa na kuuzwa. Sasa hebu tuangalie hali ya kanisa la Kikristo leo: Wachungaji wanaweza tu kufafanua maarifa na mafundisho kiasi ya kibiblia katika mahubiri yao, na hawana nuru na mwanga wa Roho Mtakatifu; waumini hujikuta bila unyunyiziwaji na lishe ya kweli, wanakuwa hasi na baridi, na imani yao inafifia; katika mikutano watu huwa bila shauku ya kufurahia maneno ya Mungu; iwe ni mchungaji au mzee, au muumini wa kawaida tu, mara nyingi hakuna mtu anayeweza hata kufuata mafundisho ya Bwana. Kanisani, wachungaji na wazee wanazidi kushiriki katika mizozo ya wivu, wanapigana madhabahu, ni walafi, na hawana moyo wa kumcha Mungu kabisa. Wengi wa waumini huanguka na kurejea ulimwenguni na kujishughulisha katika kuchuma pesa, wanatamani raha za mwili, na watu wanaohudhuria ibada wanazidi kupungua. Watu huenda tu kanisani wakati kuna tamasha fulani linalofanyika au kuna mlo, au wanapokabiliwa na hatari kubwa. Hawatafuti ukweli kwa dhati, lakini sanasana wanataka tu kushiriki katika raha, au kupata neema na kuhakikisha kwamba kuna amani maishani mwao. Haijalishi kanisa kama hilo linaonekana kuwa la kusisimua namna gani kutoka nje, hilo ni kama tu dimbwi la maji yasiyosonga, sawa na hekalu la mwishoni mwa Enzi ya Sheria. Ni wazi kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi katika kanisa kama hilo, na Mungu halitunzi.

Kwa hivyo, ili kutofautisha kati ya kanisa la kweli na makanisa ya uwongo, kimsingi lazima tuangalie ikiwa lina kazi ya Roho Mtakatifu, ikiwa Roho Mtakatifu analitunza, ikiwa watu wanasoma matamko ya sasa ya Mungu, na ikiwa kwa kusoma maneno ya Mungu, wanaelewa ukweli zaidi na kukuza imani yao katika Mungu. Kanisa lisipoenda kwa mwendo sawa na kazi ya sasa ya Mungu na halina mwongozo wa Roho Mtakatifu, basi haijalishi lina washiriki wangapi au kasi yake inavyoonekana kwa kuwa linafanya sherehe za kila aina, bado hilo ni kanisa la uwongo na litaachwa na Mungu hivi karibuni. Kama tu vile Mungu alivyompa Yohana ufunuo kuandika katika barua yake kwa kanisa la Laodikia: “Navijua vitendo vyako, kwamba wewe si baridi wala moto: heri ungekuwa baridi au moto. Kwa hiyo basi kwa vile wewe ni vuguvugu, na wala si baridi au moto, nitakutema kutoka kinywani mwangu(Ufunuo 3:15-16).

Kanuni ya pili ya kutambua kati ya kanisa la kweli na makanisa ya uongo: Je, ni ukweli au wachungaji wa uongo wanaoshikilia mamlaka?

Kanuni ya pili ya kutambua kati ya kanisa la kweli na makanisa ya uongo: Je, ni ukweli au wachungaji wa uongo wanaoshikilia mamlaka?

Kuna kanuni nyingine muhimu ya kutofautisha kati ya kanisa la kweli na makanisa ya uwongo, ambayo ni kuona ikiwa ukweli unashikilia mamlaka au ikiwa wachungaji wa uwongo ndio wanaoshikilia mamlaka. Kanisa ni mahali pa watu wanaotafuta ukweli kuishi maisha ya kanisa na kumwabudu Mungu, na kanisa lolote ambalo linajumuisha watu wanaomwamini Mungu kwa dhati na ambao Roho Mtakatifu hufanya kazi kwao ndilo kanisa la kweli. Ukweli unashikilia mamlaka katika kanisa la aina hii; kila mtu husoma na kutenda maneno ya Mungu, na wanatii ukweli. Linaongozwa na wale wanaofuatilia ukweli, na wafuatiliaji wa ukweli huungwa mkono. Yeyote anayeenda kinyume na maneno ya Mungu na ukweli, anayefanya uovu na kucharuka kanisani, hukataliwa na kufukuzwa. Kwa sababu wale wanaofuatilia ukweli wana kazi na mwongozo wa Roho Mtakatifu, mapenzi ya Mungu yanafanywa katika kanisa linalojumuisha watu kama hao, na lina uwepo wa Mungu. Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi na kunena katika Enzi ya Neema, Aliwachagua mitume 12 Yeye mwenyewe, na Yeye binafsi alimshuhudia na kumteua Petro kama mchungaji wa makanisa. Mitume waliwaongoza waaminifu wa wakati huo kulingana na maneno ya Bwana na walishiriki injili ya wokovu wa Bwana Yesu. Na hivyo mapenzi ya Mungu yalitendeka na jina takatifu la Bwana Yesu likaenea kote kote.

Sasa katika siku za mwisho, waumini katika Bwana Yesu wamegawanyika katika madhehebu mbalimbali, kila moja likiwa na kiongozi wake. Hata hivyo, katika Biblia Mungu hakuwashuhudia wachungaji na viongozi hawa Yeye mwenyewe, sembuse kudai kwamba Aliwateua kama viongozi. Wachungaji na wazee wengi katika madhehebu haya ni wahitimu kutoka shule za seminari ambao huwa viongozi na wachungaji mara wanapothibitishwa—hawatokani na kukamilishwa na kuadilishwa na Roho Mtakatifu wakati wanapitia kazi ya Mungu. Katika kazi na mahubiri yao, huwa hawashuhudii au kuyatukuza maneno ya Bwana, wala hawafanyi ushirika juu ya mapenzi ya Bwana. Kwa jumla wao hufanya kazi kwa kutegemea vipaji na ubora wao wa tabia, na yote wanayozungumzia ni maarifa ya Biblia na nadharia ya kiroho. Wao huiinua na kuishuhudia Biblia na wanambadilisha Bwana Yesu na maneno kutoka katika Biblia. Kazi kama hiyo inampinga Bwana. Hivyo basi, Roho Mtakatifu anawezaje kuyatunza makanisa yao? Hawawezi kushiriki maarifa ya kweli ya Mungu na hawawezi kuwaongoza watu kuingia katika uhalisi wa ukweli. Kile wanachojua kufanya ni kuwaongoza watu katika sheria na mafundisho, kuwapotosha, na kuwaelekeza katika maangamizi tu. Aidha, katika kazi yao kanisani kila wakati wao hujiinua na hujijengea fahari yao wenyewe ili wawafanye wengine wawaheshimu; hawatendi au kuwatendea watu kulingana na maneno ya Mungu, lakini badala yake wanajipendekeza kwa mtu yeyote anayetoa pesa nyingi, na huwateua wanaowapendelea katika nyadhifa muhimu. Ndugu wengine hawaelewi ukweli. Wamechanganyikiwa na hawana utambuzi, kwa hivyo wanawaabudu wachungaji na wazee hawa na kuwatafuta ili wawaulize juu ya kila jambo lililopo, kana kwamba ni wao tu wanaoweza kuwaongoza watu kuingia katika ufalme wa Mungu. Ingawa waumini hawa wanaonekana kumwamini Mungu na kumfuata Mungu, kiasili kwa kweli wanawaamini wachungaji na wazee. Hasa, kanisa linapokuwa lenye ukiwa na ndugu ambao wanaojishughulisha zaidi katika ufuatiliaji wao wanaenda kutafuta kanisa lililo na kazi ya Roho Mtakatifu, na kutafuta matamko ya Bwana aliyerejea, wachungaji na wazee hufanya kila kitu wawezacho kuwazuia na kuwashutumu. Wanaona ni afadhali waumini wafe kwa njaa na kiu ya kiroho kuliko kuwaruhusu watoroke kutoka katika utawala wao. Ni wazi kwamba ukweli haushikilii mamlaka katika makanisa kama haya, lakini badala yake yanadhibitiwa na wachungaji hao wa uongo, wapinga Kristo na watumishi hao waovu wasio na kazi ya Roho Mtakatifu. Makanisa kama haya yaliichukiza tabia ya Mungu zamani na yameachwa na Roho Mtakatifu, na hivi karibuni yataondolewa kabisa. Kama Biblia inavyosema, “Naye akalia sana kwa sauti kubwa, akisema, Babeli mkuu umeanguka, umeanguka, na umekuwa makazi ya pepo, ngome ya kila pepo mwovu, na tundu la kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza. Kwani mataifa yote yamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa ulimwengu wamefanya uasherati naye, na wafanya biashara wa ulimwengu wametajirika kupitia kwa utele wa uzuri wake(Ufunuo 18:2-3).

Jinsi ya Kulipata Kanisa la Kweli

Kufikia hatua hii katika ushirika wetu, pengine wengi wenu sasa wanagundua kuwa makanisa ya ulimwengu wa kidini hayana kazi ya Roho Mtakatifu tena. Kwa hivyo basi, tunawezaje kupata kanisa ambalo lina kazi ya Roho Mtakatifu na uwepo wa Mungu? Tunaweza kutafuta katika historia ili tupate jibu la swali hili. Bwana Yesu alipoonekana ili kufanya kazi na kunena miaka hiyo yote iliyopita, hekalu lilikuwa lenye ukiwa. Sababu moja ya hilo ilikuwa kwamba makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo hawakuwa wakiwaongoza waumini kwenye njia sahihi, ambalo kasha lilimfanya Roho Mtakatifu awaache; sababu nyingine ni kwamba Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi mpya, kwa hivyo Roho Mtakatifu aliondoa kazi Yake kutoka hekaluni na Akaanza kufanya kazi ndani ya wale watu ambao walienda sambamba na nyayo za Mungu. Wale ambao walimfuata Bwana Yesu waliposikia maneno Yake ya wakati huo, walipokea riziki ya maji yaliyo hai, ilhali wale waliobaki hekaluni waliingia gizani. Jambo hilo hilo linatendeka sasa katika siku za mwisho. Dini imekuwa yenye ukiwa na haina kazi ya Roho Mtakatifu, kwa hivyo tunapaswa kutafuta matamko ya Roho Mtakatifu na twende sambamba na nyayo za Mwanakondoo, kama tu inavyosema katika Biblia: “Na pia nimeizuia mvua isije kwenu, ilipokuwa miezi mitatu kabla ya wakati wa mavuno: Na nimefanya kunyeshe katika mji mmoja, na kufanya kusinyeshe katika mji mwingine: kulinyesha katika sehemu moja, na sehemu ambayo haikunyesha ikanyauka. Basi watu kutoka miji miwili au mitatu wakazurura kuingia mji mmoja, ili kunywa maji; lakini hawakutosheka: hata hivyo hamjanirudia. Atamka Yehova(Amosi 4:7-8). Kwa hivyo tunaweza kuona kwamba Mungu anapokuja kufungua kazi mpya, makanisa ya enzi ya zamani hayana budi kuwa yenye ukiwa. Mapenzi ya Mungu yamo ndani ya hili; yaani, ni kwa sababu ya ukiwa wa makanisa ndiyo tunalazimika kwenda kutafuta nyayo Zake. Kiwango cha maafa kinazidi kukua na unabii wa kuja kwa Bwana sasa umetimia kwa kiasi kikubwa. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Bwana amekwisha rudi, ya kwamba Ameonekana na anafanya kazi katika kanisa moja. Tukiweza kupata nyayo za Mungu, basi tutalipata kanisa la kweli kwa hakika.

Kwa hivyo tunaweza kuzipataje nyayo za Mungu? Kuna kifungu cha maneno ya Mungu kinachoeleza hili waziwazi: “Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya). Hii inamaanisha kwamba tukitaka kulipata kanisa la kweli ambalo litanyakuliwa kabla ya maafa, basi lazima tafuta nyayo za Mungu, tutafute matamko ya Mungu, na tuzingatie kusikilize sauti ya Mungu. Kama tu vile Biblia inavyosema: “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa. Kwa yule ambaye anashinda, nitampa matunda ya mti wa uzima ale, ambao uko katikati ya bustani ya Mungu(Ufunuo 2:7). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20).

Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba Bwana atakaporudi, Ataonyesha maneno mapya kwa makanisa. Ulimwenguni kote, leo kuna Kanisa la Mwenyezi Mungu tu linaloshuhudia kwamba Bwana amerudi, kwamba Anafanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu, na kwamba Ameonyesha mamilioni ya maneno na kufunua siri zote za mpango wa Mungu wa usimamizi. Siri kama hizo ni pamoja na hali halisi ya hatua Zake tatu za kazi, siri ya kupata mwili, umuhimu wa majina ya Mungu, hadithi ya ndani ya Biblia, jinsi Shetani anavyowapotosha wanadamu, jinsi Mungu anavyowaokoa watu, na hatima ya mwisho ya kila aina ya mtu, jinsi watu wanavyoweza kupata wokovu kamili, na zaidi. Siri hizi zimefunuliwa ili macho yetu yaweze kufunguliwa na tufurahie yale tunayoona. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho kufanya kazi Yake ya hukumu, na kwa hivyo Kanisa la Mwenyezi Mungu limeanzishwa, kama tu vile kanisa la Enzi ya Neema lilivyotokea baada ya Bwana Yesu kuja kufanya kazi katika Enzi ya Neema. Kanisa la Mwenyezi Mungu linajumuisha watu wanaokubali kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho, wanaomwamini Mungu kwa dhati, na wanaofuatilia ukweli. Wanakubali unyunyizaji na uchungaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, wanasoma maneno ya sasa ya Mungu, na wanamwomba na kumwabudu Mwenyezi Mungu, Bwana Yesu aliyerudi. Kundi hili la watu limepitia mateso na kukandamizwa na CCP; wengine wamekamatwa na kufungwa gerezani, wakikabiliwa na ukatili na mateso yake, lakini wamemfuata Mwenyezi Mungu kwa uthabiti na wamekuwa na ushuhuda wa washindi. Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, kikundi hiki kimeijua asili yao ya kishetani. Wamehisi majuto ya kweli na chuki ya kweli kwao wenyewe. Tabia zao potovu zimebadilishwa, na wamekuwa na ushuhuda mwingi kuhusu tabia zao potovu kutakaswa kupitia hukumu na kuadibu. Ni dhahiri kwamba kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho tayari imefanyiza kikundi cha washindi; ni hawa washindi wanaoyakuliwa kabla ya maafa na ndio wanaostahili kurithi ahadi na baraka za Mungu. Kitabu kilichoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, Neno Laonekana katika Mwili, sasa kinapatikana waziwazi mtandaoni, na ushuhuda wa matukio wa wateule wa Mungu na vile vile sinema na video ambazo hutolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu zinaweza kupatikana kwa wingi mtandaoni. Wengi wanaotamani ukweli wanakuwa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu na ushuhuda mwingi wa matukio wa wateule wa Mungu. Wanapata ufahamu mpya wa kazi ya Mungu na jinsi ya kutenda ukweli. Tunaweza kuona, basi, kwamba Kanisa la Mwenyezi Mungu hakina linayo kazi ya Roho Mtakatifu; Kanisa la Mwenyezi Mungu ndilo kanisa la Filadelfia—ndilo kanisa linalonyakuliwa kabla ya maafa! Siku hizi, ulimwengu mzima wa kidini umeingia katika ukiwa; ni Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee ambalo linazidi kukua thabiti siku kwa siku. Kuna matawi mapya ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanayoanzishwa moja baada ya lingine katika nchi kote ulimwenguni. Yanaendelea kukua na kuwa thabiti, yakituonyesha kuwa yote yatokayo kwa Mungu lazima yasitawi!

Kwa kuwa kuna maafa makubwa zaidi na zaidi, na ni muhimu tulipate kanisa la Filadelfia ambalo litanyakuliwa kabla ya maafa makubwa. Hili lina athari ya moja kwa moja kwa jambo muhimu la ikiwa tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni. Ikiwa hatuwezi kwenda sambamba na nyayo za Mungu na kulipata kanisa la kweli, mwishowe tutasombwa na misiba hiyo tukilia na kusaga meno sana. Katika wakati huu mgumu, tunapaswa kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu ili kubainisha kama hayo ni sauti ya Mungu. Tukiyatambua kuwa sauti ya Mungu, lazima tufanye hima kuyakubali, kwa sababu ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo tunaweza kuenda sambamba na nyayo za Mwanakondoo.

Je, ushirika huu umekuonyesha njia ya kutambua kanisa la kweli kutoka kwa makanisa ya uwongo, na kupata kanisa la Filadelfia ambalo litanyakuliwa kabla ya majanga, kama ilivyotabiriwa katika Biblia? Ikiwa makala haya yamekuwa na msaada kwako, tafadhali yashiriki na rafiki zako ili watu zaidi waweze kulipata kanisa la kweli katikati ya maafa, na ili kwamba siku moja hivi karibuni waweze kunyakuliwa mbele ya Mungu wapokee utunzaji na ulinzi Wake.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp