Ukombozi wa Moyo

24/01/2021

Na Zheng Xin, Marekani

Mnamo Oktoba ya 2016, mimi na mume wangu tulikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho wakati tulikuwa ughaibuni. Miezi michache baadaye, Dada Wang, ambaye alikubali kazi ya Mungu pamoja nami, alikuwa anaendelea kwa haraka. Nakumbuka, wakati huo, kila mtu alikuwa akimpongeza kwa sababu ya ubora wake mzuri wa tabia. Nakumbuka pia jinsi, baada ya mkutano mmoja, nilimsikia Dada Lin akisema, “Kila kitu ambacho Dada Wang ameshiriki leo, kuhusu kukubali kwake na kuyaelewa maneno ya Mungu, kilizungumzwa kutoka moyoni. Alichokisema pia kina nuru, na kwangu ni cha msaada sana.” Kwa kweli, mwanzoni, nilimposikia kila mtu akisema hivyo kulinifanya nimwonee wivu. Lakini muda mfupi baadaye, nilianza kuhisi mwenye chukichuki: Inakuwaje kwamba kila mtu alikuwa akimsifu yeye, na siyo mimi? Sikuwa nimekua hata kidogo? Je, kulikuwa na kitu kibaya na ushirika wangu? Hatua kwa hatua, sikutaka kukubali ukweli kwamba yeye alikuwa bora kuniliko, na nikaanza kuwa mpinzani wake kwa siri. Nilijiwazia, unaweza kushiriki kuhusu maneno ya Mungu, lakini mimi pia naweza. Siku itakuja ambapo mimi nitakushinda. Nitashikilia ufahamu na maarifa ninayopata kutoka katika maneno ya Mungu na kuyashiriki tu nikiwa mikutanoni. Hivyo, kila mtu ataona kuwa ushirika wangu ni mzuri sana na wa vitendo pia.

Kwa kipindi cha muda baada ya hapo, niliandika kila kitu nilichokuwa nimepata na kuelewa kutoka katika maneno ya Mungu katika daftari. Wakati wa mkutano ulipofika, ilibidi niyatafakari kwa uangalifu moyoni mwangu, kuona jinsi ambavyo ningeweza kuyashiriki katika ushirika kwa njia ambayo ingekuwa wazi, taratibu na ya mpangilio kama ya Dada Wang. Lakini kwa sababu fulani, kadiri nilivyojaribu kujionyesha mbele ya ndugu, ndivyo nilivyoonekana mpumbavu zaidi. Mara tu ilipofika zamu yangu kufanya ushirika, mawazo yangu yangekuwa tupu au maneno yangu yangetoka yakiwa yamevurugika kabisa. Sikuweza kusema wazi mitazamo niliyonuia kuelezea. Mkutano huo uliishia kuwa wa aibu sana kwangu. Baada ya kufika nyumbani siku moja, nilimwambia mume wangu, “Kila ninaposikia kuna nuru katika ushirika wa Dada Wang kuhusu maneno ya Mungu wakati wa mikutano, najisikia niliyesumbuka kweli—” Lakini kabla sijamaliza kuongea, mume wangu alinitazama kwa jicho la ukali na kuniambia kwa dhati, “Ushirika wa Dada Wang una nuru, na ni wa msaada kwetu. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa ajili ya hili.” “Kusumbuka unakohisi huku—sio wivu tu?” Maneno yake yalikuwa kama kofi usoni. Nilitikisa kichwa changu haraka kwa kukana: “Hapana, sivyo. Mimi siko hivyo.” Mume wangu aliendelea kusema, “Ndugu zetu wote wamepata furaha kutoka katika ushirika wa Dada Wang, lakini wewe kuusikia unakufanya uhisi ukosefu wa amani. Hiyo inamaanisha tu kuwa una wivu kwa sababu yeye ana uwezo zaidi kukuliko, sivyo?” Kusikia hili kulinikasirisha zaidi. Inawezekana kuwa mimi kweli nilikuwa mtu mwenye wivu vile? Nikamwambia, “Acha kuongea sasa. Acha nitulie, nami nitalifikiria mwenyewe.” Baada ya hayo, mume wangu alimwambia Dada Liu kanisani kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea upande wangu, akitumai kwamba Dada Liu angenisaidia. Niliposikia habari hiyo, nilimkaripia: “Unawezaje kuzungumza naye bila kuniuliza kwanza? Akimwambia kila mtu kuhusu hili, watanionaje?” Kadiri nilivyofikiria zaidi kuhusu hilo, ndivyo nilivyokasirika zaidi. Nilichoweza kufanya kilikuwa kumwomba Mungu kimyakimya: “Ee Mungu! Tafadhali nipe mwongozo. Tafadhali nisaidie.”

Siku iliyofuata, nilitafakari kuhusu kile nilichokuwa nimefichua katika kipindi hicho cha wakati. Ilinitokea kwamba kwa kawaida niliposoma maneno ya Mungu, ningejiwekea nuru yoyote ambayo nilipata, na kisha niishiriki wakati wa mikutano yetu. Kwa kweli hii ilikuwa tu tamaa ya kuongea kuhusu vitu ambavyo watu wengine hawakujua kuvihusu ili ndugu zangu wawe na maoni ya juu kunihusu. Nilipoona kuwa Dada Wang alikuwa na nuru katika ushirika wake, kila mara nilikosa amani na nilitaka kumshinda. Nilikuwa nikifikiri kwamba nilikuwa mtu asiye mgumu kuongea na wengine na sikuwahi kuonekana mwenye kujadili kila jambo dogo, kwamba nilikuwa mtu wa kawaida moyoni. Lakini sasa ilitukia kuwa naweza kumwonea mtu wivu, na kwamba ningeweza kuwa mpinzani wake na kushindana naye kwa siri. Iliwezekanaje niwe mtu kama huyo? Nilimpigia dada mmoja simu na nikamuuliza, “Dada, je, wewe huhisi wivu wakati wa mikutano baada ya kusikia nuru katika ushirika wa ndugu wengine kuhusu maneno ya Mungu?” Akajibu, “Hapana, huwa sihisi hivyo. Ikiwa ndugu zetu wana nuru katika ushirika wao, hiyo ni ya msaada kwangu. Inanifurahisha sana, na ninafurahia hilo sana!” Kumsikia akisema hivyo kulinifanya nihisi vibaya zaidi. Nilihisi vikali jinsi nilivyokuwa na wivu nyingi sana. Hakuna mtu mwingine aliyemwonea wivu dada huyo; ni mimi pekee niliyehisi vile. Nikiishi katika hali kama hii, sikuwa na lingine ila kumwomba Mungu. Nilimwambia, “Ee Mungu! Sitaki kuwa mtu mwenye wivu, lakini kila wakati ninaposikia ushirika mzuri wa dada huyu, huwa nahisi wivu kwake bila kutaka. Ee Mungu! Sijui la kufanya. Tafadhali, naomba Uniongoze nitupilie mbali pingu zangu za wivu…”

Baadaye, Dada Liu kutoka kanisani kwetu alikuja kunitembelea. Alifanya ushirika nami kulingana na hali yangu, na pia akasoma kifungu cha maneno ya Mungu. “Watu wengine daima wana hofu kwamba wengine wataiba maarufu wao na kuwashinda, wakipata utambuzi ilhali wao wenyewe wanatelekezwa. Hili huwasababisha kuwashambulia na kuwatenga wengine. Je, huku si kuwaonea wivu wale walio na talanta? Je, huku si kuwa wabinafsi na wachoyo? Je, mwenendo kama huu si wa binafsi na wa kudharauliwa? Hii ni tabia ya aina gani? Ni ovu! Kujifikiria tu, kuridhisha tu tamaa zako mwenyewe, kutofikiria wajibu wa wengine, na kufikiria tu kuhusu maslahi yako mwenyewe na sio maslahi ya nyumba ya Mungu—watu kama hawa wana tabia mbaya, na Mungu hawapendi(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliposikia maneno haya ya Mungu, nilihisi kwamba hii ilikuwa hali niliyokuwa ndani hasa. Ushirika wa Dada Wang juu ya maneno ya Mungu ulikuwa wa kutia nuru, lakini sikujaribu kuelewa ukweli au kutafuta njia ya kutenda kutoka katika yale aliyokuwa ameyasema. Badala yake, nilimwonea wivu. Wakati ushirika wangu mwenyewe haukuwa mzuri, na wakati sikuweza kujionyesha na badala yake nikaishia kujidhalilisha, mawazo yangu yangevurugika na ningekuwa hasi sana na mwenye kukasirika. Ningeogopa sana kwamba ndugu zangu wangenidharau. Nilikuwa mbinafsi na mwenye kustahili dharau, na kila nilichofikiria kilikuwa kuweza kutokezea—lakini sikuweza kabisa kuvumilia kumwona mtu aliyefanya vizuri kuniliko. Je, huko hakukuwa kuwa mwenye wivu na husuda? Hakukuwa na hata chembe ya ubinadamu wa kawaida katika hilo! Nikikumbuka nyuma, nilikuwa vile vile kabla ya kumwamini Mungu. Nilipokuwa naingiliana na jamaa na marafiki, majirani, na wafanyakazi wenza, siku zote nilikuwa nawataka wengine wazungumze mema kunihusu. Wakati mwingine, mfanyakazi mwenza alipoisifu kazi ya mtu mwingine mbele yangu, ningeanza kuhisi niliyesumbuka, na ili kuwafanya wengine wazungumze mema kunihusu, ningejitolea kufanya kazi yangu vizuri, na nilifurahia kuifanya bila kujali ilikuwa ngumu au ya kuchosha vipi. Sikuwa na ufahamu wa hilo, lakini niliifikiria tu kama aina fulani ya tamanio la maendeleo. Ni sasa tu ndipo nimegundua kuwa hayo yalikuwa udhihirisho wa tabia potovu ya Shetani. Baada ya hapo, nilikuja mbele za Mungu mara kwa mara na kufanya maombi Kwake kuhusu shida zangu. Wakati wa mikutano, nililenga kuutuliza moyo wangu na kusikiliza ushirika wa wengine. Ilipofika zamu yangu kufanya ushirika, sikufikiria tena jinsi ya kutoa ushirika bora kuliko vile Dada Wang alivyofanya. Badala yake, nilitafakari maneno ya Mungu kwa utulivu na kushiriki katika ushirika kile nilichoelewa kuhusu. Nilipotenda kwa njia hii, kwa kweli nilihisi huru zaidi na mwenye kuachiliwa.

Baada ya kipindi cha muda, kwa kweli nilihisi kwamba wivu wangu ulikuwa umepungua ikilinganishwa na ulivyokuwa, lakini tabia potovu ya kishetani imekita mizizi sana, na hujifichua wakati wowote ambapo hali inayofaa inatokea. Baadaye, wakati wa mikutano michache, kila nilipoona kuwa wale ndugu wengine walikuwa wakiusifu ushirika wa Dada Wang, nilianza tena kuona wivu kiasi. Baada ya hapo, nilihisi umbali kati yangu na yeye. Hata hivyo, nikiishi katika hali hiyo, sikuthubutu kuwaambia wengine. Niliogopa kwamba kama ningefanya hivyo, wangenichukia. Kwa hivyo, wakati wa mikutano kadhaa, nilihisi aliyezuiliwa sana.

Jioni moja, Dada Liu alinipigia simu. Akiwa ametatizika, aliniuliza kama nilikuwa nikipitia shida yoyote hivi karibuni. Nilijibu kwa wasiwasi, “Je, mimi ni mpotovu mno? Je, Mungu atakataa kumwokoa mtu kama mimi?” Nikiogopa angenidharau, sikusema chochote zaidi. Kisha Dada Liu alinisomea kifungu cha maneno ya Mungu kuhusiana na hali yangu: “Watu wengine wanaposikia kwamba kuwa mtu mwaminifu, mtu lazima ajifunue na kujiweka wazi, wao husema, ‘Ni vigumu kuwa mwaminifu. Ni lazima niseme vyote ninavyofikiri kuwahusu wengine? Je, haitoshi kuwasiliana kuhusu mambo mazuri? Sihitaji kuwaambia wengine kuhusu upande wangu mwovu ama mpotovu, nahitaji?’ Usipowaambia wengine mambo haya, na hujichambui, basi hutawahi kujijua; hutawahi kutambua wewe ni kitu cha aina gani, na watu wengine hawataweza kukuamini. Huu ni ukweli. Iwapo unawataka wengine wakuamini, kwanza lazima uwe mwaminifu. Kuwa mwaminifu, lazima kwanza uuweke wazi moyo wako ili kila mtu aweze kuuona moyo wako, kuona vyote unavyofikiri, na kuuona uso wako wa kweli; hupaswi kujifanya ama kujaribu kujificha. Hapo tu ndipo watu watakuamini na kukuchukua kuwa mwaminifu. Hili ndilo tendo la msingi kabisa, na sharti, la kuwa mwaminifu(“Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno hayo kutoka kwa Mungu, alifanya ushirika nami, “Lazima tujiweke wazi na kufanya ushirika ili tutafute ukweli; hii ni njia moja ya kupata kuachiliwa kwa kiroho. Pia ni njia ya kutenda ukweli na kuwa mtu mwaminifu. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kupokea msaada kutoka kwa ndugu zetu. Hii inaziruhusu tabia zetu potovu kutatuliwa kwa haraka zaidi, na inatupa hisia za kuachiliwa. Kama hatuko tayari kuweka wazi shida zetu, tutaanguka kwa urahisi katika hila za Shetani, na maisha yetu yatakuwa katika hatari ya kupata hasara.” Baada ya kusikiliza ushirika wa Dada Liu, nilipata ujasiri na kumwambia nilichokuwa nikipitia. Kisha Dada Liu alisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Watu ambao Mungu huwaokoa ni wale ambao wana tabia potovu kwa njia ya kupotoshwa na Shetani; sio watu safi wasio na dosari hata kidogo, wala sio watu ambao wanaishi katika utupu. Kwa wengine, mara tu upotovu wao unafunuliwa, wanawaza, ‘Kwa mara nyingine tena, nimempinga Mungu; nimemwamini kwa miaka mingi, lakini bado sijabadilika. Kwa kweli Mungu hanitaki tena!’ Huu ni mtazamo wa aina gani? Wamejikatia tamaa, na kufikiria kuwa Mungu hawataki tena. Je, hii si hali ya kumwelewa Mungu vibaya? Wakati wewe uko hasi sana, ni rahisi zaidi kwa Shetani kupata dosari ndogo kwako, na mara tu anapofanikiwa, matokeo yake ni mabaya sana. Kwa hivyo, bila kujali uko katika shida kiasi gani au unahisi ukiwa hasi kiasi gani, lazima usikate tamaa! Katika mchakato wa ukuaji wa maisha na wakati wanaokolewa, watu wakati mwingine huchukua njia mbaya au kupotoka. Wanaonyesha kutokomaa kiasi katika maisha yao kwa muda, au wakati mwingine wanakuwa dhaifu na hasi, husema vitu vibaya, huteleza na kuanguka, au kushindwa. Kutoka katika mtazamo wa Mungu, vitu kama hivyo vyote ni vya kawaida, na hawezi kuhangaika juu ya hivyo(“Uingiaji Katika Maisha ni Muhimu Zaidi Katika Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Dada huyo alishiriki ushirika huu na mimi: “Sote tumepotoshwa kwa kina na Shetani. Sisi ni wenye kiburi, hila, ubinafsi, na wivu. Tabia hizi za kishetani zimekita mizizi kwa kina ndani yetu sote, na hata zimekuwa maisha yetu. Kwa sababu hii, tabia na mitazamo yetu hufichua upotovu mara kwa mara. Ilikuwa ikinikera sana: Nilikuwa na ufahamu kiasi kuhusu tabia yangu potovu na nilijuta baada ya kuifichua, hivyo kwa nini ningerudia kuifanya tena wakati uliofuata? Baada ya kusoma maneno ya Mungu, mwishowe niligundua kuwa tabia yangu ya kishetani ilikuwa ya kina sana, na nilianza kufahamu kuwa mabadiliko katika tabia si jambo linalofanyika ghafla. Watu hawawezi kubadilika tu baada ya kujitambua kidogo. Bila hukumu na kuadibu kwa muda mrefu kutoka kwa Mungu, bila kupogolewa na kushughulikiwa, na bila majaribio na usafishaji, mabadiliko ya kweli hayawezekani. Kusudi la kuja kwa Mungu kutekeleza hukumu na kuadibu ni ili kututakasa na kutubadilisha. Anajua jinsi ambavyo Shetani ametupotosha kwa kina, na Yeye anajua kimo chetu na shida tunazokumbana nazo katika kujaribu kubadili tabia zetu, kwa hivyo ni Mwenye msamaha na subira kwa wale wanaofuatilia ukweli. Mungu anatumai kuwa tuna azimio la kufuatilia ukweli, na kwamba tunatafuta kuzibadili tabia zetu kwa moyo wote. Kwa hivyo, lazima tujichukulie kwa njia inayofaa. Lazima tule na kunywa maneno ya Mungu zaidi, tukubali hukumu na kuadibu kwayo, tuukane mwili, na tuweke ukweli katika vitendo. Kisha siku moja, tabia zetu potovu zitabadilika.”

Kisha tulisoma kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Watu wote hawataki kushindwa, bali daima wanataka kushindana—hata ingawa kushindana kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. ‘Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?’ Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi. Unamwomba Mungu na unahisi nafuu kwa muda, lakini punde unapokumbana na hali ya aina hii tena, huwezi kulishinda. Je, hii haionyeshi kimo kisicho komavu? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu. … Lazima ujifunze kuacha na kuweka kando vitu hivi, kuwapendekeza wengine, na kuwaruhusu wengine kutokeza. Using’ang’ane au kukimbilia kujinufaisha punde unapopata nafasi ya kutokeza au kupata utukufu. Lazima ujifunze kujiondoa, lakini hupaswi kuchelewesha utekelezaji wa wajibu wako. Kuwa mtu anayefanya kazi kwa ukimya bila kuonekana, na ambaye hajionyeshi kwa wengine unapotekeleza wajibu wako kwa uaminifu. Kadiri unavyoacha ufahari na hadhi yako, na kadiri unavyoacha masilahi yako mwenyewe, ndivyo utakavyokuwa mwenye amani zaidi, na ndivyo nafasi itakavyofunguka zaidi ndani ya moyo wako na ndivyo hali yako itakuwa bora zaidi. Kadiri unavyopambana ana na kushindana zaidi, ndivyo hali yako itakuwa mbaya zaidi. Ikiwa huamini hili, jaribu na uone! Ikiwa unataka kugeuza hali hii, na usidhibitwe na vitu hivi, basi lazima uviweke kando kwanza na kuviacha. Vinginevyo, kadiri unavyong’ang’ana, ndivyo giza litakuzingira zaidi, na ndivyo utakavyohisi wivu na chuki, na hamu yako ya kupata itaongezeka na kuongezeka tu. Kadiri hamu yako ya kupata ilivyo kuu, ndivyo utakaavyopunguza kuweza kufanya hivyo, na unapopata kidogo chuki yako itaongezeka. Chuki yako inapoongezeka, utakuwa mbaya zaidi. Kadiri ulivyo mbaya ndani yako, ndivyo utakavyotekeleza wajibu wako vibaya zaidi; kadri unavyotekeleza wajibu wako vibaya, ndivyo utakuwa mwenye manufaa kigogo zaidi. Huu ni mzunguko mwovu uliofungamana. Ikiwa huwezi kamwe kutekeleza wajibu wako vizuri, basi, utaondolewa polepole(“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Ushirika wa dada huyo kuhusu maneno ya Mungu ulinifanya nitambue kwamba wivu wangu uliibuka kutokana na kuwa na tamaa kuu sana ya sifa na hadhi, na kwamba tabia yangu ilikuwa ya kiburi sana. Nilikuwa nimeelimishwa na elimu ya CCP na kila aina ya falsafa za maisha ya kishetani na sumu tangu utotoni, kama vile, “Kila mtu ajitetee, ole wake ashikaye mkia,” “Mtu hujitahidi kwenda juu; maji hububujika kwenda chini” na “Kujipatia sifa na kuleta heshima kwa mababu zake” Sumu hizi za kishetani zilikuwa zimepandwa ndani kabisa ya moyo wangu, zikiisababisha tabia yangu kuwa ya kiburi, ya kujidai, ya ubinafsi, na ya kustahili dharau. Nikidhibitiwa na tabia hii ya kishetani, nilikuwa nimekuwa mwenye kutamani makuu na asiyekata tamaa; bila kujali nilichofanya, nilihisi kulazimika kuwashinda wengine. Nilikuwa nimekuwa hivyo katika jamii, na nilikuwa nimekuwa hivyo kanisani pia. Hata wakati wa kufanya ushirika na kuomba wakati wa mikutano, bado nilitaka tu kuwa bora kuliko watu wengine, na nyakati pekee ambazo nilikuwa na furaha ni wakati wengine walinipongeza. Mara tu mtu mwingine alionekana kuwa bora kuniliko mimi, sikulikubali hilo, na ningekuwa na wivu. Ndani mwangu, ningepinga na kufanya kazi dhidi ya mtu huyo. Wakati sikuweza kumshinda kweli, ningeshinda tu katika uhasi na suitafahamu, kutoweza kujitendea vizuri. Hata nilimwelewa Mungu visivyo, na nilidhani kwamba sikuwa mlengwa wa wokovu wa Mungu. Niliona kwamba upotoshaji wa Shetani ulikuwa umenifanya niwe mwenye kiburi na dhaifu, mwenye ubinafsi na mwenye kustahili dharau, na maisha yangu yalikuwa ya kusikitisha sana. Baadaye, nilipata njia ya kutenda kutoka katika maneno ya Mungu. Lazima nijifunze kuachilia, kuweka vitu kando, na kutenda kulingana na maneno ya Mungu. Lazima nijifunze kuukana mwili wangu mwenyewe na kukandamiza ubinafsi na hadhi yangu, na nijifunze zaidi kutoka katika uwezo wa za Dada Wang, na kufidia udhaifu wangu mwenyewe. Hii ilikuwa ndiyo njia pekee ya kuelewa na kupata ukweli zaidi.

Baadaye, nilisoma kifungu hiki kutoka katika maneno ya Mungu: “Shughuli si za aina moja. Kuna mwili mmoja. Kila mmoja hufanya kazi yake, kila mmoja kwa nafasi yake na kufanya kadiri ya uwezo wake—kila cheche ya shauku mwako wa mwanga—kutafuta ukomavu katika maisha. Ni hivyo ndivyo nitakavyoridhika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 21). Mara tu niliposoma maneno haya kutoka kwa Mungu, nilielewa kwamba kwa sababu ubora wa tabia na vipaji ambavyo Mungu hutoa ni tofauti kwa kila mtu, mahitaji Yake kwa kila mtu ni tofauti. Kwa kweli, mradi tunafanya kila kitu tuwezacho kutimiza wajibu wetu, moyo wa Mungu utafarijika. Ni kwa neema ya Mungu kwamba Dada Wang ni mwenye ubora mzuri wa tabia na ni mwepesi sana kuelewa ukweli. Leo Mungu amepanga sisi kukusanyika pamoja, na kusudi Lake ni sisi tujifunze kutoka katika uwezo wa kila mmoja na kufidia udhaifu wetu wenyewe ili tuweze kuelewa ukweli na kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu pamoja. Napaswa kushughulikia vyema uwezo wangu na upungufu wangu mwenyewe. Haijalishi ni aina gani ya ubora wa tabia ambayo Mungu amenipangia niwe nayo, lazima nitii sheria na mipango Yake, nirekebishe nia zangu, na nifuatilie ukweli kwa moyo wangu wote. Napaswa kushiriki kiasi chochote ninachoelewa, na nitende kiasi chochote ninachojua. Ninapaswa kufanya bidii yangu yote, na kwa njia hii, Mungu atanipa nuru na kunielekeza. Ili kutimiza haya, nilifanya azimio lifuatalo mbele za Mungu: Kuanzia sasa kuendelea, niko tayari kuweka jitihada katika kufuatilia ukweli, kuacha kuwa mwenye mawazo finyu na mwenye wivu kwa watu wenye uwezo kunishinda, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu wa kweli ili kutimiza mapenzi ya Mungu.

Mkutano uliofuata wa kanisa ulifika kwa haraka sana. Nilitaka kuwaambia ndugu kuhusu jinsi nilivyokuwa mwenye wivu kwa Dada Wang, na ni vipengele vipi vya tabia yangu potovu ambayo nilikuwa nimefichua, lakini mara tu nilipofikiria hili, nilihofu kuhusu jinsi ambavyo wangeniona, na kile ambacho Dada Wang angefikiria kunihusu ikiwa angejua jinsi nilivyokuwa mwenye wivu kwake. Ndani mwangu, nilihisi mwenye kusita kukabili hali hiyo. Kimyakimya ndani yangu, nilimwomba Mungu. Nikasema, “Ee Mungu! Naomba Unipe imani na ujasiri. Niko tayari kuweka kando ubatili na hadhi yangu, kushiriki katika ushirika waziwazi na ndugu zangu, na kutatua vikwazo vilivyopo kati yetu. Mungu, naomba Uwe mwongozo wangu.” Baada ya kuomba, nilihisi mwenye amani zaidi, na kwa hivyo nilizungumza kuhusu hali gani niliyokuwamo na kuhusu yale yote niliyokuwa nikipitia. Baada ya kunisikiliza, sio tu kwamba ndugu zangu hawakunidharau, lakini kwa kweli wao wote pia walivutiwa na ujasiri wangu wa kuweza kutenda uaminifu. Walisema kwamba niliyoyapitia yaliwafanya watambue kwamba ni kwa kutenda kulingana na maneno ya Mungu tu ndiyo wanaweza kutupilia mbali tabia zao wenyewe za kishetani na wapate kuachiliwa na uhuru. Pia walisema kwamba sasa walijua la kufanya wakati mwingine watakapokumbana na hali kama hiyo. Wakati wa mikutano iliyofuata, niligundua uwezo mwingi wa Dada Wang: Wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu, aliweza kujumuisha hali yake mwenyewe katika ushirika wake. Kila alipokumbana na tatizo, aliweza kulenga kuja mbele za Mungu na kutafuta makusudi Yake, na kuhusu kupata njia ya kutenda kutoka katika maneno Yake. Ni baada tu ya kuona huu uwezo wake ndipo nilielewa kwamba yeye hakuwa mpinzani wangu, bali alikuwa mtu anayeweza kunisaidia. Hapo ndipo nilipohisi, kwa dhati, kwamba kusudi la mpango wa Mungu la sisi kufanya kazi pamoja ni ili tujifunze kutoka kwa uwezo wa kila mmoja ili kufidia udhaifu wa kila mmoja. Nilipolifikiria hivyo, nilihisi nimeachiliwa kabisa. Sasa nahisi kwamba kila mkutano ni aina fulani ya kufurahia. Sishawishiwi tena na wivu, lakini ninaweza kutumia uwezo wa wengine kufidia udhaifu wangu mwenyewe, kuishi kwa amani pamoja nao, na kuhisi nimeachiliwa katika roho.

Iliyotangulia: Baada ya Uwongo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kurudi kwenye Njia Sahihi

Chen Guang, Marekani Mwenyezi Mungu anasema, “Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp