Miaka Saba ya Majaribio Imefichua Hali Yangu Halisi

18/10/2019

Na Chen Hui, Mkoa wa Heilongjiang

Mnamo mwaka wa 1994, pamoja na mama yangu, nilikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nilipopata habari kuhusu jinsi Mungu alivyokuwa amejitokeza tena katika mwili ili kufanya kazi ya wokovu, nilifurahi mno, na hasa nilikuwa na heshima kuwa mnufaishwa wa wokovu wa Mungu. Katika wakati uliofuata, nilihudhuria mikutano mara nyingi na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja na ndugu zangu. Nilipokuwa na wakati, ningesoma neno la Mungu, na baada ya kupata ufahamu kiasi wa makusudi Yake, niligawanya muda wangu kati ya kazi na kutimiza wajibu wangu mwingi kanisani kadiri ya uwezo wangu. Muda fulani baadaye, nilisikia kwamba kazi ya Mungu ingetamatika karibuni sana. Huku nikisisimuka sana, nilijiwazia, “Ni afadhali nitie bidii katika ufuatiliaji wangu wa ukweli na kufanya vitendo vizuri zaidi kabla ya kazi ya Mungu kumalizika. Lazima nisikose fursa hii itokeayo mara moja katika maisha.” Kwa hiyo, nilifanya uamuzi thabiti kuacha kazi yangu na kujiwekeza kabisa katika kazi ya kueneza injili ya ufalme. Niliamua kutoa maisha yangu yaliyobaki yote kwa Mungu kabisa, kwa imani kwamba kwa kufanya hivyo tu ndipo ningepata sifa na baraka Zake. Wakati huo, kila siku, nilijipa shughuli nyingi siku zote kuanzia alfajiri hadi usiku sana licha ya upepo au mvua. Hata kama ningelazimika kuendesha baiskeli yangu kilomita nyingi, sikuwahi kuhisi hoi au kufanyishwa kazi nyingi kupita kiasi. Kulikuwa na nyakati ambapo nilihisi uchungu na udhaifu nilipokabiliwa na kashfa ya watu wa dunia au kuachwa na wapendwa, lakini almradi wazo lilinijia akilini kwamba sio tu kwamba nitaokolewa majanga makubwa yatakaposhuka duniani na kupata uzima wa milele, lakini pia nitafurahia baraka nyingi za Mungu, nilijawa na hisia ya furaha, na hisia kwamba juhudi zangu zote zilikuwa na thamani. Kwa njia hii, nilihisi mwenye hakika kwamba kama niliweza kutumia kila kitu kwa ajili ya Mungu, basi hii ilimaanisha kuwa nilikuwa mtu aliyempenda Mungu na aliyestahili baraka Zake, na kwamba hakika kungekuwa na mahali pangu katika ufalme. Kuanzia wakati huo, hata nilipokuwa nikiendelea kutumia rasilmali na kutoa, nilikuwa nikisubiri bila kutulia siku ambayo kazi ya Mungu ingefika mwisho ili niweze kudai furaha yangu katika ufalme haraka iwezekanavyo.

Siku moja kuelekea mwisho wa mwaka wa 1999, nilipokuwa tu nikijiandaa kwa imani kuingia katika ufalme na kufurahia baraka zake kuu, dada mmoja aliniambia, “Mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu ameshiriki kwamba ikiwa tunataka kupata wokovu na kukamilishwa, lazima kwanza tupitie miaka saba ya majaribio.” Niliposikia haya, sikuweza kabisa kuamini masikio yangu. Huku nikitaka kuhakikisha kuwa sikuwa nimesikia vibaya, nilimuuliza dada huyo arudie alivyosema. Mara nilipothibitisha kwamba hivyo ndivyo alivyokuwa amesema, kichwa changu kilipepesuka na ghafla nikachanganyikiwa. Sikuweza kabisa kukubali yale aliyokuwa amesema kuwa ni ukweli. Ghafla, mawazo yalianza kukimbia kichwani mwangu: “Kwa nini bado lazima nipitie miaka saba ya majaribio? Waliposema kazi ya Mungu itaisha katika miaka miwili ijayo, niliacha kila kitu; ninapaswa kuendeleaje, sasa kwa kuwa bado kuna miaka saba? Je, nitafute kazi ili nichume pesa kiasi? Baada ya miaka saba, nitakuwa na umri wa miaka thelathini; vipi kuhusu suala hili la kufunga ndoa? …” Hapo awali nilidhani kuwa nilikuwa karibu kabisa kuingia katika ufalme wa Mungu, na kwamba mateso yangu yote ya mwili yangemalizika hivi karibuni. Hata hivyo, ilionekana sasa kwamba sio tu kwamba singeingia katika ufalme wa Mungu, lakini ilinilazimu bado nipitie miaka saba ya majaribio na usafishaji. Nilipofikiria kuhusu hili, moyo wangu ulivunjika, na huzuni isiyoelezeka ikajaa ndani yangu. Bila kujua nilianza kumlaumu Mungu, nikifikiri, “Mungu! Kwa nini Hukuniambia mapema kwamba lazima bado nipitie miaka saba ya usafishaji? Hapo awali nilikuwa nimedhani kwamba bila kujali mambo yanaweza kuwa magumu kiasi gani, yote yataisha baada ya miaka miwili au mitatu, na kwamba wakati huo ningeweza kuingia katika ufalme na kufurahia baraka ya ajabu milele. Sasa, hata hivyo, bado nina miaka saba ya majaribio na usafishaji mbele yangu. Natarijwa kuyashindaje hasa?” Kadiri nilivyozidi kuwaza, ndivyo nilivyozidi kuwa hasi. Nilianza kujutia maamuzi ambayo nilikuwa nimeyafanya, na hata nikakusudia kurudi katika ulimwengu wa kidunia kutafuta kazi na kuchuma pesa, na kushiriki tu katika maisha ya kanisa wakati wowote muda utakaponiruhusu. Hivyo, niliishi katika taabu tupu, na nilisononeka kila wakati: Nikisinzia katika mikutano, na kutimiza wajibu wangu shingo upande. Sikuhisi kuwa nilikuwa na nguvu ya kuendelea mbele sawa na ile niliyokuwa nayo hapo zamani, lakini sikuthubutu kuchukua hatua kurudi nyuma; kwa kweli sikuwa na mbele wala nyuma. Karibu wakati huo, kulikuwa na watu ambao, kwa kutoweza kuvumilia dhiki ya miaka saba ya majaribio, walimkana Mungu na kupoteza imani yao. Niliposikia habari hii, nilishtuka, na ilikuwa kana kwamba saa ya kengele ilikuwa imelia kichwani mwangu. Nilipoangalia hali yangu ya sasa, niligundua kuwa kama singefanya kitu ili kujigeuza, basi, mimi pia, ningekuwa katika hatari kubwa—na hata hivyo, nilitarajiwa vipi kubadilisha hali yangu ya sasa na kujitokeza kutoka katika uhasi ambao nilikuwa nimezama ndani yake?

Muda mfupi baadaye, niliona kifungu kifuatacho cha maneno ya Mungu: “Kila wakati majaribu ya miaka saba yanapotajwa, kuna watu wengi kiasi wanaohisi hasa wasio na rah na kuvunjika moyo, na kuna wengine ambao hulalamika, na kuna kina aina ya hisia. Kutokana na hizi hisia ni dhahiri kwamba watu sasa wanahitaji majaribu haya; wanahitaji aina hii ya dhiki na utakasaji. Katika imani yao kwa Mungu, kile ambacho watu hutafuta ni kupata baraka kwa ajili ya siku zijazo; hili ndilo lengo lao katika imani yao. Watu wote wana kusudi na tumaini hili, lakini upotovu ulio katika asili yao lazima uondolewe kupitia majaribu. Katika hali ambazo bado hujatakaswa, hizi ndizo hali ambamo lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili uweze kujua upotovu wako mwenyewe. Hatimaye, unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu(“Jinsi Mtu Anapaswa Kumridhisha Mungu Katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa maelezo sahihi ya mashaka yangu ya sasa. Mara tu niliposikia kwamba bado ningehitaji kupitia miaka saba ya majaribio, nilikuwa nimeingia kwenye shimo la uhasi na, nikiwa nimejaa malalamiko, nilikuwa nimemwasi Mungu. Hapo awali nilikuwa nimefikiri kwamba kwa kuwa nilikuwa nimeacha kazi yangu na kutelekeza maisha ya familia yangu, nilikuwa nimewekeza zaidi ya wafuasi wa kawaida, kwa hivyo mimi ndiye niliyekuwa ninampenda Mungu kuliko mtu mwingine yeyote, na niliyestahili zaidi baraka Zake. Wakati huo tu ndipo niligundua kuwa ufuatiliaji wangu ulikuwa wenye najisi. Mungu huchunguza mioyo na akili za watu, na Alitumia majaribio na usafishaji kufunua kwamba imani yangu Kwake ilikuwa kweli kwa msingi wa tamaa ya baraka. Aliniruhusu nipate ufahamu wa kweli juu ya mtazamo usio sahihi wa ufuatiliaji wangu na kuondoa tamaa yangu ya baraka. Baadaye, niliona kifungu kingine cha maneno ya Mungu: “Je, si bado mnaendeleza picha ya uongo ili kunidanganya Mimi, kwa ajili ya hatima yenu, na kuwa na hatima nzuri na ya furaha? Nafahamu kwamba ibada yenu na unyofu wenu ni wa muda tu; je, matamanio yenu na gharama mnayolipa ni ya sasa tu na si ya baadaye? Mnataka tu kutumia nguvu moja ya mwisho ili kupata hatima nzuri. Azma yenu ni kubadilisha tu; siyo ili msiwe wenye deni kwa ukweli, na ni hasa msinilipe kwa ajili ya gharama Niliyolipa. Kwa neno, mko tu tayari kutumia ujanja wenu, lakini hamtaki kuipigania. Je, si haya ni matakwa yenu ya dhati? Sio lazima mjifiche, na hata zaidi, sio lazima mpige mbongo zenu juu ya hatima yenu hadi pale ambapo hamuwezi kula au kulala. Je, si ni kweli kwamba matokeo yenu yatakuwa yameamuliwa mwishowe?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima). Hukumu na kuadibu vilivyokuwa katika maneno ya Mungu vilinifanya nihisi aibu na kufikiri kuhusu mawazo na vitendo vyangu, nikigundua kuwa vilikuwa sawa na vile ambavyo Mungu alikuwa ameviweka wazi. Nikifikiri nyuma juu ya wakati ambapo nilikuwa nimeingia kanisani kwa mara ya kwanza na nilikuwa bado nikifanya kazi huku nikitimiza wajibu wangu. Nilipokuwa nimepata habari kwamba kazi ya Mungu ingeisha hivi karibuni, nilikuwa nimedhani kwamba ili kupata baraka Zake na kupata thawabu, nilihitaji tu kujiwekeza kabisa katika kutumia rasilmali kwa ajili Yake kwa muda mfupi. Ili kuhakikisha kuwa ningeingia katika ufalme mara kazi ya Mungu itakapohitimishwa, nilikuwa nimeachana na raha zote za mwili na bila kufikiri nikazama katika kutimiza wajibu wangu. Hata hivyo, niliposikia kwamba bado nilihitaji kupitia miaka saba ya majaribio, nilihisi kuwa nilikuwa nimekutana na kizuizi kisichorekebishika, na nikawa hasi sana kwamba sikuwa hata na msukumo wa kutekeleza wajibu wangu. Moyo wangu ulijawa na lawama na upinzani dhidi ya Mungu. Nilijutia kila kitu ambacho nilikuwa nimeacha na kazi yote ngumu ambayo nilikuwa nimefanya; hata nilikusudia kumsaliti Mungu na kumkana. Niligeuka na kuwa mtu tofauti kabisa na yule niliyekuwa hapo awali! Ilikuwa tu kupitia ufunuo wa jaribio ndipo niligundua kuwa kwa kweli sikuwa nimewahi kumwabudu Mungu kama Muumba wa viumbe vyote. Niligundua pia kuwa sikuwa nimejitumia au kuacha vitu vya dunia ili kutekeleza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa ili kufuatilia upendo wangu wa Mungu na kumridhisha Mungu. Badala yake, nilikuwa nimefanya juhudi hizi zote kwa ajili tu ya hatima yangu ya baadaye. Kila kitu nilichokuwa nimekifanya kilikuwa ili kufanya maafikiano na Mungu; hivyo, nilikuwa nikimdanganya na kumtumia kufikia lengo langu la mwisho la kuingia katika ufalme ili kupokea baraka tele. Nilikuwa mbinafsi, mwenye kustahili kudharauliwa, na mbaya sana! Ilikuwa tu kama maneno ya Mungu yalivyofunua: “Bila kujali jinsi wanavyojaribiwa, utii wa wale wenye Mungu ndani ya mioyo yao hubaki vile vile; lakini kwa wale wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao, wakati kazi ya Mungu hainufaishi miili yao, wanabadilisha mtazamo wao kwa Mungu, na hata kumkimbia Mungu. Hawa ndio wale hawatasimama imara mwishoni, wanaotafuta baraka za Mungu na hawana tamaa ya kujitolea wenyewe kwa Mungu na kujikabidhi wenyewe Kwake. Watu duni wa aina hii watafukuzwa wakati kazi ya Mungu itakapofikia kikomo, na wao hawafai kuonewa huruma yoyote. Wale wasiokuwa na ubinadamu, hawawezi kumpenda Mungu kwa kweli. Wakati mazingira ni mema na salama, au kama kuna faida inayoweza kupatwa, wao ni watiifu kabisa kwa Mungu, lakini wakati walilokuwa wanataka limepatikana au hatimaye kukataliwa, wanageuka mara moja. Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye ‘mioyo mikunjufu’ hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu. Ikiwa mapepo haya hayatarushwa nje, mapepo haya ambayo yanaweza kuua bila kusita, je, hayatakuwa hatari iliyofichika?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu). Kutoka kwa maneno ya Mungu ilikuwa dhahiri kwamba watu wabinafsi na wasaliti hawana ubinadamu na huishi kabisa kwa ajili ya faida, wakisaliti uaminifu na imani kwa sababu ya faida ya mtu binafsi. Wale wanaoishi kulingana na asili ya Shetani hawawezi kabisa kulingana na Mungu; watu kama hao wanampinga na kumsaliti Mungu siku zote, na hata humchukulia Mungu kama adui wao. Mungu anawachukia na kuwakirihi watu hawa, na wakiendelea kukataa kufuatilia ukweli, hatimaye wataondolewa. Nilifikiria jinsi, katika nyakati mbili ambazo Mungu mwenye mwili anakuja duniani kufanya kazi ya wokovu wa wanadamu, Amepitia fedheha ya ajabu sana na Alilipa gharama kuu ili kutukomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza—na bado, Hajawahi kutaka chochote kutoka kwetu. Kinyume chake, sio tu kwamba sikuwa nimegundua upendo wa Mungu au kuwa bila shukrani hata kidogo au kujitoa Kwake kwa kweli, lakini pia nilikuwa nimejishughulisha tu na jinsi ambavyo ningepata baraka. Kazi ya Mungu ilipokosa kulingana na dhana na mawazo yangu au ilipokosa kuhusisha kuninufaisha kimwili, nilikuwa nimemwacha mara moja, hata nikajutia juhudi zangu zote na yote niliyokuwa nimeacha na nikataka kumtelekeza Mungu kabisa. Niliweza kuona kuwa sikuwa na ubinadamu hata kidogo; asili yangu ilikuwa kiasi kwamba nilikuwa nimempinga na kumsaliti Mungu, na uasi kama huo ulikuwa tu unastahili laana ya Mungu. Baada ya kugundua yote haya, nilijawa na hatia na kujilaumu, na nikaahidi kamwe kutokuwa fidhuli tena. Nilijua kuwa, haraka iwezekanavyo, lazima nitubu, nijitahidi kufuatilia ukweli ili kumridhisha Mungu.

Baadaye, nilisoma maneno yafuatayo katika mahubiri: “Leo kuna wengi ambao mioyo yao huzua malalamiko na ambao hutenda kwa kutokuwa na imani kwenye mawazo maovu wanapokabiliwa na miaka hiyo saba ya majaribio. Hii inashangaza sana, na imenifanya nigundue kuwa wale walio katika familia ya Mungu sasa si bora kuliko Waisraeli wa siku za zamani. Inaweza kusemekana kuwa kazi ya Mungu siku hizi inafaa zaidi kwa binadamu waliopotoka, na ni ya haja sana kwao. Mungu asingetenda kwa njia hii, binadamu wasingekuja kumjua, wasingepata imani ya kweli, au kumsifu kwa kweli. Siku hizi binadamu ni dhaifu, wanyonge na ni vipofu. Hawana maarifa ya kweli kumhusu Mungu. Kabla ya majaribio kuanza, asili ya watu wengi ya uasi, upinzani, na usaliti kwa Mungu ilikuwa imefunuliwa hadharani ili wote waone. Watu kama hao wanawezaje kutarajia kuingia katika ufalme? Wanawezaje kuchukuliwa kuwa wanaostahili kupokea ahadi za Mungu? Kama mwanadamu angeelewa kwa kweli kasoro, udhaifu, na unyoge wake—kama angeona jinsi asili yake ilivyokuwa kaidi na kinzani kwa Mungu—basi angetii mateso na usafishaji mbalimbali ambao Mungu amepanga, na angekuwa tayari kutii mipangilio ya Mungu na kazi Yake yote. Ni wenye kiburi kingi pekee, baada ya kusoma vifungu vichache vya neno la Mungu, ndio wanaweza kudhani kwamba wameelewa ukweli, wana ubinadamu, hawahitaji kupitia majaribio na usafishaji, na wanapaswa kuinuliwa moja kwa moja hadi katika mbingu ya tatu. Mtu yeyote aliye na uzoefu wa maisha atakuwa amegundua kuwa ikiwa mtu husoma tu neno la Mungu lakini hapitii usafishaji wa kila aina wa majaribio na mateso, mtu kama huyo hawezi kufikia mabadiliko ya tabia. Kwa sababu tu mtu ameelewa mafundisho mengi haimaanishi kwa lazima kuwa ana kimo cha kweli. Kwa hivyo, katika siku zijazo, mwanadamu lazima apitie majaribio mengi: Hii ni neema ya Mungu na kukuzwa na Mungu, na hata zaidi ni wokovu wa Mungu, na wote wanapaswa kumshukuru na kumsifu Mungu kwa sababu ya hilo” (Ushirika kutoka kwa Aliye Juu). Baada ya kusoma mahubiri haya, nilipata ufahamu mkubwa hata zaidi kuhusu nia ya Mungu. Maisha yangu yalihitaji hasa kukutana na majaribio na usafishaji kama huu; nisingefunuliwa kwa njia hii, nisingechunguza kwa makini nia mbaya ambazo zilikuwa zimetia hamasa imani yangu au kutambua asili yangu ya kishetani yenye ubinafsi na ya kuleta hizaya. Nilikuwa hata nimedhani kuwa nilikuwa na imani ya kweli katika Mungu, na nikajivisha taji kama mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli. Nilikuwa nimejidanganya na kujighilibu. Kazi ya Mungu ya ajabu ilikuwa imenifunua kikamilifu, ikiniwezesha nione wazi ukweli wa upinzani wangu Kwake, na kuona uovu wangu na ubaya wangu. Ilikuwa imenionyesha kuwa nilikuwa mfuata upepo na dhuria wa Shetani anayeishi na anayepumua. Imani yangu katika Mungu ilikuwa yenye najisi kabisa na yenye alama za mapatano ya kibiashara. Kama ningeendelea kutenda imani yangu kwa njia hiyo, kamwe singepokea sifa ya Mungu, na ningeishia kushindwa. Kupitia hukumu na kuadibu kulinisaidia kugundua kuwa imani katika Mungu si rahisi kama vile nilivyokuwa nimefikiria; mtu hapokei baraka za Mungu mara tu baada ya kumwamini Mungu, wala mtu hafiki katika hatima ya furaha kwa sababu tu amefanya kazi na kutega wakati na nguvu. Asili yangu ya kishetani isipotakaswa na kubadilishwa, naweza kutenda imani katika Mungu kwa miaka mia moja na bado nisipate wokovu. Hii imebainishwa na asili ya Mungu ya haki, na hakuna mtu anayeweza kuibadilisha. Niligundua pia kwamba kupitia majaribio na usafishaji ni hatua muhimu kwenye njia ya kupata wokovu wa Mungu. Sasa simlaumu tena au kumwelewa vibaya Mungu, lakini badala yake naitii kazi Yake kwa furaha. Nimeamua kuanza upya, na kutia bidii katika ufuatiliaji wangu wa ukweli, ili siku moja hivi karibuni nipate kufikia mabadiliko ya tabia na uwiano na Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ulinzi wa Mungu

Mwenyezi Mungu anasema: “Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp