Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ni kwa Nini Ulimwengu wa Kidini Wenye Wayowayo kwa Hasira Unaipinga na Kuishutumu Kazi Mpya ya Mungu Daima?

34

Ni kwa Nini Ulimwengu wa Kidini Wenye Wayowayo kwa Hasira Unaipinga na Kuishutumu Kazi Mpya ya Mungu Daima?

Mara mbili ambapo Mungu amepata mwili kutembea duniani na kufanya kazi ya kumwokoa mwanadamu Amekumbana na upinzani mkubwa, shutuma na mateso ya hasira kutoka kwa viongozi katika dunia ya kidini, ukweli ambao umewakanganya na hata kuwashtua watu: Ni kwa nini kila wakati Mungu anapoonyesha hatua ya kazi mpya Yeye daima hukumbana na aina hii ya utendewaji? Ni kwa nini wale ambao humpinga Mungu kwa hasira zaidi na ujeuri ni viongozi wa dini wanaosoma Biblia tena na tena na ambao wamemhudumia Mungu kwa miaka mingi? Ni kwa nini viongozi hao wa kidini ambao watu huona kuwa wacha Mungu zaidi, waaminifu zaidi na watiifu kwa Mungu kwa hakika hawawezi kulingana na Mungu, na badala yake daima wanatenda kwa ukaidi, na kuwa maadui wa Mungu? Inawezekana kuwa Mungu alifanya makosa katika kazi Yake? Inawezekana kuwa matendo ya Mungu siyo ya kufuata mantiki kwa kawaida? Hakika huo si ukweli! Kuna sababu mbili za msingi ambazo kwazo madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini yana watu ambao wana uwezo wa kumpinga Mungu, kugeuka kuwa maadui wa Mungu, na hizi ni: Kwanza, pamoja na watu hawa kutomiliki ukweli na kutokuwa na maarifa ya kazi ya Roho Mtakatifu, wao pia hawana maarifa ya Mungu, wao daima hutegemea maarifa yao duni ya Biblia, nadharia za kiteolojia na dhana na mawazo ya watu kueleza kazi ya Mungu ambayo daima ni mpya na kamwe si nzee; Pili, kwa kuwa wanadamu wamepotoshwa kwa kina na Shetani, asili yao ni ya kiburi na kujipenda, wameshindwa kutii ukweli, na hasa huthamini hadhi. Mchanganyiko wa mambo haya mawili husababisha majonzi ya wanadamu kutelekeza na kushutumu njia ya kweli mara kwa mara kote katika historia.

Angalia nyuma kwa miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu alipokuwa miongoni mwa watu wa Kiyahudi Alifanya miujiza mingi, Alimsaidia mwanadamu kwa kuwaponya wagonjwa na kutoa pepo, Alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, Akawafundisha watu kuhusu kutubu, na kuwasamehe dhambi zao. Haya ni mambo yote ambayo hayakuandikwa katika Agano la Kale, na pia ilikuwa kazi ambayo hakuna mtu aliyewahi kuifanya kabla. Bila shaka, pia kilikuwa kitu ambacho hakuna mtu angeweza kutekeleza, kwa sababu mbali na Mungu hakuna mtu aliye na mamlaka na nguvu ya kufanya mambo kama hayo. Kile Bwana Yesu alichotimiza wakati huo kilikuwa binafsi kuchukua dhambi za mwanadamu kwa kutundikwa msalabani ili mwanadamu angeweza kuokolewa na kukombolewa kutoka kwa dhambi, Akiwafadhili wanadamu kwa neema na amani na furaha maridhawa na kwa wingi, na Akimleta mtu kutoka kwa kanuni za sheria kupitia kazi ya enzi mpya, ambapo mwanadamu haadhibiwi tena kwa kuwa hawezi kuzingatia sheria. Watu hao chini ya sheria wanaweza tu kupata wokovu wa Mungu na kutoangamizwa kwa kufuata kazi ya Bwana Yesu. Lakini makuhani wakuu, walimu wa sheria na Mafarisayo wa Kiyahudi hawatambui kazi ya Mtakatifu Roho, hawaelewi ni kazi ya aina gani ambayo Bwana Yesu hutekeleza, katika fikira zao wanaamini: Kutofuata sheria, kutoomba katika jina la Yehova Mungu ni sawa na kumsaliti Mungu, ambalo ni jambo la kufedhehesha kabisa. Aidha, wao hujishaua kuwa ni wasomaji motomoto wa Biblia na watumishi wa Yehova Mungu katika hekalu kwa miaka mingi, na wanaamini kwamba wanayoyashikilia ni ukweli na njia iliyo safi zaidi, na almradi wanahusika, kazi ya Bwana Yesu huenda kinyume na Biblia na hukiuka sheria, ni njia mbali na Biblia, na kwa sababu hiyo wao ni afadhali wafe kuliko kuikubali njia inayoenezwa na Bwana Yesu. Wao hata huifikiria kazi ya Bwana Yesu kama “uasi,” “dhehebu bovu” na kama ya “kumdanganya mwanadamu.” Ingawa kazi na neno la Bwana Yesu zina mamlaka, nguvu na hekima, hata kama miujiza Bwana Yesu aliyoonyesha ni ya pekee katika historia, hata kama watu zaidi na zaidi huja kutoa ushahidi juu ya matendo ya Bwana Yesu na kushuhudia ukweli kwamba Bwana Yesu ni Masihi ambaye atakuja, bado ni wasiotaka kuchunguza na kutafuta njia ya juu, badala yake wanashikilia maoni yao, na kwa kiburi wanakana katakata kwamba Bwana Yesu ni Kristo, kwamba Bwana Yesu ni Masihi ambaye atakuja. Ni kama tu vile Mwenyezi Mungu amefichua: “Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko —lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa” (“Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutenda kama mtu ambaye huamini katika Mungu, angalau sana tunapaswa kumiliki moyo ambao humcha Mungu na kuwa na njaa na kiu ya haki, ni kwa njia hii tu ambapo tutaweza kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu, kufanikisha ufahamu wa kazi mpya ya Mungu na kufuata kwa karibu nyayo za Mungu. Lakini hao makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo kutoka Uyahudi wamekutana na Bwana Yesu mara nyingi, lakini kamwe si katika ukimbizaji wa ukweli. Kila wakati wao hubuni njia na namna za kumpima Bwana Yesu, kupata umiliki wa kitu cha kutumia dhidi ya Bwana Yesu. Wao wote wako sawa kwa kuwa hawana elimu ya Mungu, na kwamba hushikilia dhana kuhusu kazi mpya wa Mungu, wakati ambapo Nathanaeli na mwanamke Msamaria na wanafunzi na watu wa kawaida ambao humfuata Bwana Yesu wanaweza kuweka kando dhana zao ili kutafuta ukweli. Kwa njia hii wanaweza kujua utambulisho wa Kristo, kuitambua sauti ya Mungu, kutii na kukubali ukweli, na kurudi mbele ya Mungu. Kwa njia ya ulinganifu huu tunaweza kuona wazi kuwa watu wa kiwango cha juu katika ulimwengu wa kidini wa Uyahudi hawashikilii ukale kwa ukaidi tu, lakini pia ni wenye kiburi na wa kujipenda, kwa maana kimsingi hawakubali ukweli, na waziwazi hawatii ukweli. Humo mle mna sababu za upinzani wao kwa Mungu.

Aidha, kama watu zaidi wa kawaida wa Kiyahudi wanapoanza kumfuata Bwana Yesu, makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wanaanza kuwa na mahangaiko juu ya kupoteza nafasi yao katika mioyo ya watu wa kawaida. Watu wakiwa hawawaabudu tena au kuwafuata wao wanakuwa na wasiwasi kwa ongezeko, kwa sababu mamlaka na nguvu ya maneno na kazi ya Bwana Yesu hayafikiki nao, huwafanya kukwajuka kwa ulinganishi, na kuwafanya waaibike wenyewe, na katika njia hii huzidi kuhisi hali ya hatari: Yote ambayo ingechukua ni kwa Bwana Yesu kuishi kwa siku moja, na kisha hata watu zaidi wa kawaida wangewaacha na kwenda kumfuata Bwana Yesu, na kungekuwa na watu wachache katika hekalu, likiwasababisha kushindwa kuendelea kufurahia maisha ambapo wanaungwa mkono na kufadhiliwa na wengine kwa njia ambayo haina kifani na mtu mwingine yeyote. Hili humfanya Bwana Yesu kuwa kama sindano katika jicho lao au mwiba katika mwili wao, hili humgeuza Yeye kuwa adui ambaye hawezi kuishi katika dunia moja na wao. Ili kulinda nafasi yao, wao hufikiria kila kitu wanachoweza kufanya na kutumia kila aina ya mbinu ya kudharauliwa ili kuleta mashtaka ya uongo dhidi ya Bwana Yesu. Wao huikufuru na kuishutumu kazi ya Bwana Yesu, wao humtukana na kumkashifu Bwana Yesu, wakisema kuwa yeye hutegemea uwezo wa Beelzebuli kutoa pepo, na wao huleta ushahidi wa uongo wakimlaumu Bwana Yesu kwa kuongea dhidi ya mahali patakatifu na kinyume cha Sheria (Kwa marejeleo ona Matendo 6: 10-14). Kwa vyovyote vile wangemfuta Bwana Yesu kutoka kwa watu wa Kiyahudi, na mwishowe wakamsulubisha Yesu kikatili. Wakati Bwana Yesu alipofufuliwa, Alionekana mbele ya wanafunzi wake, na pamoja na kueneza kwao kwa injili kulikuwa na nguvu na miujiza, ukweli ambao unatosha kuthibitisha kuwa njia hii ina kazi ya Roho Mtakatifu, ambao unaungwa mkono na Roho Mtakatifu, na kwamba ndiyo njia ya kweli! Katika hali hii, hao makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo bado hawakutafakari juu ya hili: Je, injili ya Bwana Yesu inawezaje kuwa na mafanikio hivyo? Kwa kweli, wale watu ambao ni stadi katika Biblia na ambao wanajidhani kuwa “wa heshima” hasa huhisi kuwa ni kudunishwa kwao kutafuta na kutalii mambo kama hayo na wale wavuvi wa kijiji na watu wajinga wa kawaida ambao hawana elimu au hadhi, na wao hata kwa unafiki hutenda kwa kisingizio cha “kuunga mkono sheria na kulinda njia ya kweli” wakati huo wakiendelea kutumia nguvu mikononi mwao kwa kula njama na viongozi ili kuzidisha ukandamizaji wao na hasira, mateso na kuchinjwa kwa mitume na watu wa kawaida wa Kiyahudi ambao ni wafuasi wa Bwana Yesu. Wao kufanya kila kitu katika uwezo wao ili kuwazuia watu kumfuata Bwana Yesu, wao hata hupiga marufuku kabisa mtu yeyote kueneza jina la Bwana Yesu. … Ili kulinda nafasi zao wenyewe na riziki yao, kwa kweli hakuna uhalifu ambao hawawezi kuutenda, ambayo ni sababu nyingine ya upinzani wao wa hasira na shutuma ya Bwana Yesu. Bila shaka, matendo yao maovu yameichochea hasira kali ya Mungu, wamepitia adhabu ya Mungu. Jamii nzima ya Wayahudi imekuwa taifa lililoshindwa kwa karibu miaka 2000, ambayo ni thamani chungu wao wamelipa kwa kumpinga Mungu na kumshutumu Mungu.

Hebu turejelee wakati wa sasa ambapo tupo katika siku za mwisho. Mungu ameandaa wokovu mkubwa kwa wale ambao wamekombolewa na Yeye. Wokovu huu ni Mungu akitumia maneno kuhukumu na kumtakasa mwanadamu. Ni kazi mpya, ya juu zaidi. Hatua hii ya kazi itamwondolea mwanadamu kabisa tabia yake potovu ya kishetani. Itamkomboa mwanadamu kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani na kuwageuza wanadamu kuwa jamii inayomjua Mungu, inalingana na Mungu na kweli ni milki ya Mungu, ambapo itapata ukombozi na kukamiliswa. Hii ni hatua ya mwisho ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita. Katika kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Kristo mwenye mwili huonyesha ukweli wote ambao humtakasa mtu na kumwokoa mtu, Yeye hufichua na kukihukumu kiini na asili potovu ya mwanadamu, na Yeye huonyesha njia ambayo mtu anaweza kuipitia ili kuuachaa upotovu wake. Yeye pia hufichua aina zote za mafumbo ya mbinguni. Zaidi ya hayo, Mungu hutumia hekima Yake, nguvu na mamlaka kueneza injili ya siku za mwisho kwa kila familia duniani kote, na milioni nyingi za watu ambao hutafuta na kuonea kiu ukweli wamerejea mmoja kwa mmoja kutoka madhehebu na makundi mbalimbali ya kidini hadi kwa uwepo wa Mwenyezi Mungu. Maono yasiyowahi kutokea ya mataifa yote kufurikia mlima huu yameonekana, na injili ya siku za mwisho kwa sasa inaenea kuvuka kila taifa na kila mahali duniani kote. Hata hivyo, wakati wakikabiliwa na ukweli huu wote, maajabu haya makubwa na ushuhuda wa kazi ya Roho Mtakatifu, viongozi katika dunia ya kidini wamejifanya kuwa hawaoni na mambo haya hayawagusi hata kidogo, na hawayatafiti kwa makini, na kwa hakika hawayakubali kwa unyenyekevu. Watu hawa ni sawa na Mafarisayo,hawatambui kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inaendelea kusonga mbele, wao hawatambui kwamba kanuni ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kwamba ni mpya daima na kamwe si nzee, hawana elimu hata kidogo juu ya kazi Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, na wao hata husadiki kwa kujiamini mno kwamba: Kwa kuwa tayari wao hufurahia njia ambayo ni ya juu zaidi kuliko ile kutoka kwa Enzi ya Sheria, kwa kuwa wao ni stadi katika Agano la Kale na Jipya kwa ukamilifu wao na wamefanya kazi na kufanya mahubiri kwa miaka mingi, tayari wamepata ukweli na kumjua Mungu. Zaidi ya hayo, wao kwa ukaidi huamini katika dhana isiyo sahihi ambayo wanaamini kuwa ni kweli: Kwamba maneno yote ya Bwana, yanapatikana katika Biblia, kwamba kama inapita mawanda ya kazi ya Bwana Yesu, kama inapita Biblia, basi si njia ya kweli. Kupotea kutoka kwa masharti ya Mungu kwa mwanadamu katika Enzi ya Neema itakuwa kuvunja sheria ya mafundisho ya Kristo, mambo wanayoyakubali tu, walio na elimu juu yake na kushikilia ndiyo njia ya kweli, kitu chochote zaidi ni uasi au dhehebu bovu. Watu hawa wamemweleza Mungu kwa udhabiti ndani ya Biblia, wamemweleza Yeye katika dhana na mawazo ya mwanadamu. Bila kujali kazi iliyoletwa na Mwenyezi Mungu ni ya juu kiasi gani, ni kiasi gani cha kazi ya Roho Mtakatifu inayo, ni njia ngapi za matendo inaleta, na ni ukweli kiasi gani upo kuithibitisha, hawakiri kwamba imetoka kwa Mungu, na kwa hiyo wote hudumisha maoni ya uhasama na msimamo wenye shaka juu ya kurudi kwa Bwana Yesu, hivyo kiasi kwamba wao huukufuru mwili wa Mungu mwenye mwili na kuishushia hadhi na kuishutumu kazi na neno la Kristo katika siku za mwisho. Je, wao si ni sawa kama Mafarisayo ambao katika wakati wao walikuwa wakaidi, wa kushikilia ukale na wenye kiburi na wa kujipenda, kuangalia ukweli kwa dharau na kumkufuru Roho Mtakatifu? Ni kama kile Mwenyezi Mungu alichokisema: “Kama unapata kumjua Mungu kutokana na hatua moja ya kazi Yake tu, basi maarifa yako ni kidogo, kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama si hivyo, kwa nini wengi wa walinzi wa kidini wa kale walimtundika Mungu msalabani akiwa hai? Je, si kwa ajili mwanadamu humwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani? Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha ‘wasomi’ wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Je, watu hawa wana mantiki yoyote ya kuzungumzia? Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru —je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu?” (“Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Watu ambao kweli wanaamini katika Bwana wanaporudi kwa wingi kwa nyumba ya Mungu, uenezi wa polepole wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho umefanikisha kilele chake, lakini hata na kazi ya Roho Mtakatifu kustawi sana, viongozi wa kidini ambao wamezoea kuwa wenye kujigamba na wataalam wa kidini ambao huwaelekeza wengine hawajiakisi wenyewe, wala hawashushi vichwa vyao vyenye kiburi kutafuta na kutafiti. Kwa kinyume, watu hawa wanatambua kwamba nafasi zao zinakuwa zaidi na zaidi za mashaka, kwamba wao si imara wakati wote, na wao huanza kuhofia kwamba kila mtu mwingine atarejea kwa Mwenyezi Mungu na atawakataa na dharau. Kwa sababu hiyo, ili “kukomboa hali ya sasa,” wachungaji, wazee wa kanisa, viongozi na wafanyakazi wenza kutoka madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini hutenda kwa kisingizio cha “kuwachunga kondoo kwa ajili ya Bwana na kuitetea njia ya kweli.” Wameanza kuchukua hatua kama vile kubuni na kusambaza vifaa vya propaganda, wakitumia mtandao kueneza uvumi na njia zingine za kudharauliwa kumkufuru na kushambulia Mwenyezi Mungu kwa utukutu. Wanaeneza uvumi wa kushusha hadhi, wakidai kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu si neno la Mungu, kwamba yameandikwa na mwanadamu, na hata wanasema upuuzi kama vile “kitabu hiki ni kama dawa inayokuduwaza, ukikisoma kitakutia kasumba,” na vitu vingine ambavyo hupotosha na kuwasilisha visivyo ukweli na kulikashifu Kanisa la Mwenyezi Mungu kuwa “kikundi cha Umeme wa Mashariki,” ambalo ni shirika la jinai. Kwa kuwadanganya na kuwatisha waumini kwa njia hii, kunawasababisha watu wapumbavu na wajinga kutothubutu kuikaribia na kugusana na injili ya Mungu, kuzingia madhehebu mbalimbali na makundi ya kidini kwa kiasi kwamba sindano haingeweza hata kuchoma moja kwa moja, wala maji kupenya ndani. Viongozi hawa wa kidini wamewapiga marufuku kabisa waumini wao kusoma vitabu vya Umeme wa Mashariki au kusikiliza mahubiri ya Umeme wa Mashariki, hawaruhusu waumini kuwapokea watu ambao huhubiri wokovu wa Mungu katika siku za mwisho au hata wageni wowote, na wao kabisa huenda kinyume na mafundisho ya Mungu katika Enzi ya Neema ambapo Yeye humuuliza mwanadamu kuwakaribisha wageni. Kitu ambacho ni cha kutisha zaidi kwa wanadamu ni kwamba, licha ya kuwa waamini katika Mungu, watu hawa hushirikiana na serikali ya kishetani ya CCP, wakiwasaidia katika shughuli yao mbovu na danganyifu kwa kufuatilia, kufuatia na kutoa taarifa juu ya ndugu wa kiume na wa kike ambao hueneza injili ya siku za mwisho, na wao hata hutumika kama wasaliti wsiogunduliwa ndani ya kanisa kukusanya taarifa kwa ajili ya kukamatwa kwa Wakristo kisiri na CCP. Inaonekana kuwa wanaweza tu kuhisi tulizo kutoka kwa chuki katika mioyo yao kwa kuwaondoa wanaomshuhudia Mungu kwa pigo moja na kukomesha kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wanaelewa kabisa kwamba wale wanaofuata Mwenyezi Mungu ni watu wenye tabia njema ambao kweli huamini katika Mungu, na wao hata wanajua zaidi kwamba hakuna nia mbaya hata kidogo kwa watu hawa kuhubiri juu ya wokovu wa Mungu katika siku za mwisho, lakini bado huwatusi kwa njia ya kishenzi na katili, wakiwafukuza na hata kuwashambulia kimwili ndugu wa kiume na wa kike ambao hueneza Injili. Ni wazi kuwa viongozi hawa wa kidini waliacha kumiliki kazi ya Roho Mtakatifu zamani sana, na ni wazi pia kwamba wao hawakubali ukweli, kwamba wao husinywa na ukweli, na kwamba wao huchukia ukweli katika asili na kiini. Kwa nje watu hawa hukimbia kote wakijitahidi kutekeleza kazi, lakini kwa ndani wao wamechanganyikiwa na malengo yasiyowezekana na kutotii. Kweli wanajaribu tu kupanga njama kwa ajili ya hadhi, wakikimbia kote kwa faida yao wenyewe, na kufanya kila wawezalo kuridhisha tamaa zao ubinafsi.

Ni wazi kuona kwamba bila kujali kama ni dunia ya kidini ya Kiyahudi kwa wakati wake au viongozi wa kidini kutoka madhehebu mbalimbali kutoka kwa makundi ya kidini ya leo, sababu kwamba wanaweza kumpinga Mungu mara kwa mara, ukweli na njia ya kweli, sababu ambayo ni “afadhali wafe kuliko kutii” na “kukabili kifo kwa utulivu” hatimaye ni kwa sababu hawatambui kanuni kwamba kazi ya Mungu daima ni mpya na kamwe si nzee, wala hawana ujuzi wa kazi mpya ya Mungu, na zaidi ya hayo hawafuatilii ukweli kamwe, ni wakaidi na wenye kushikilia ukale, ni wenye majivuno na wa kujipenda. Pia yote haya yanahusiana na wao kuwa na wasiwasi kupita kiasi kuhusu hadhi yao na kuwa wa ubora duni sana. Siku hizi, katika wakati huu muhimu wakati enzi mpya inachukua nafasi ya ile ya zamani, vita katika dunia ya kiroho imefikia kilele chake. Kama watu bado huamini uvumi na ushuhuda wa uwongo unaoenezwa na viongozi wa kidini na kukubali wenyewe kutawaliwa nao, wasipotilia maanani au hata kudharau na kudunisha kazi inayotekelezwa na maneno yanayosemwa na Mungu katika siku za mwisho, kama hawachukui jukumu kwa maisha yao wenyewe na hufanya watu wengi wanavyofanya tu na kwenda na mtiririko huku wakikosoa zaidi kazi ya Roho Mtakatifu na kusafihi kusikozuiwa, kama hawajihusishi na ufahamu na huabudu tu kwa upofu, kusikiliza na kutii uvumi na udanganyifu wa wachungaji na wazee wa kanisa, kama hawana uwezo wa kugeuka kuelekea kwa haki na kujitoa kwa udhibiti wa majeshi ya Shetani na kutafuta njia ya kweli na kusikiliza sauti ya Mungu, kama hawawezi kufanya vitu hivi, basi hawatakuwa na uwezo kamwe wa kukaribisha kurejea kwa Bwana, hawatakuwa na uwezo kamwe wa kuushuhudia uso wa Muumba, hawatapata fursa ya kumjua Mungu kamwe, watashushwa kuwa karagosi tu katika historia, kitu cha sadaka cha Shetani, na watazama katika giza ambapo watalia na kusaga meno yao mpaka waangamie, kama tu ambavyo imetabiriwa katika Maandiko: “Kwa sababu hiyo Bwana atakata kichwa na mkia kutoka Israeli, tawi na tete, mnamo siku moja. Mkongwe wa heshima, yeye ndiye kichwa; na nabii afundishae uongo, yeye ndiye mkia. Kwa sababu viongozi wa watu hawa huwasababishia kukosa; na wale wanaoongozwa nao wanaangamizwa” (Isa 9:14-16). Ni lazima tujue kwamba Mungu hatamchagua mtu yeyote ambaye hana kiu ya ukweli, ambaye si dhahiri juu ya imani yake katika Mungu, ambaye hana msimamo wa hakika juu ya mitazamo yake, ambaye huabudu nguvu na ushawishi au ambaye hutumia hali kwa manufaa yake. Kinyume cha hicho, Mungu hutafuta, hukamilisha na kuchuma wanawali mabikira ambao humheshimu Mungu kama mkuuu, ambao ni wenye akili wazi, walio na utii safi, ambao kweli huona kiu kwa Mungu na kumtafuta. Huu ni ukweli wa namna nyingi! Inawezekana kuwa kwamba damu iliyomwagwa na Waisraeli haikuwa ya kutosha kukufanya uwe na ufahamu wa somo hili?