Ukweli Kuhusu Kunyakuliwa

19/05/2021

Li Huan

Kama tu ndugu Wakristo wengine wengi, natamani sana kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Tunafuata fungu lifuatalo kutoka kwa Biblia: “Baada ya hayo sisi ambao tuko hai na kusalia tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa: na hivyo tutakuwa naye Bwana daima” (1 Wathesalonike 4:17). Kwa sababu hii, kwa upumbavu tunaangalia anga tukitamani sana siku ambayo Yesu atarudi na kutuchukua juu katika mawingu ili tuweze kuwa na Bwana. Hata hivyo, baada ya miaka mingi sana imepita, miezi minne ya damu imeonekana tayari; mitetemeko ya ardhi, njaa, tauni na vita na aina zote za maafa mengine zinakuwa kali zaidi na zaidi. Unabii wa kuja kwa mara ya pili kwa Bwana umetimizwa kimsingi. Hata hivyo, bado hatujashuhudia Mkristo mmoja akinyakuliwa hadi mbinguni. Siwezi kujizuia kufikiri, “Kwa nini Bwana hakuji kutupokea? Bwana ni mwaminifu. Bwana aliahidi kwamba Angetuchukua hadi katika ufalme wa mbinguni katika siku za mwisho. Hakika ahadi ya Bwana itatimizwa na kufanikishwa. Sishuku hili hata kidogo. Ilhali, kwa nini hadi sasa, bado hatujanyakuliwa na Bwana hadi mbinguni? Inaweza kuwa hamu yetu ina shida fulani?”

Ilhali, kwa nini hadi sasa, bado hatujanyakuliwa na Bwana hadi mbinguni?

Wakati tu nilipokuwa nikihisi kukanganyikiwa, mhubiri ambaye alikuwa amefanya kazi katika maeneo ya kigeni kwa miaka mingi alirudi na nikapokea ufahamu mpya kutoka kwake. Dada huyo alijibu maswali yangu moja kwa moja: “Fungu la Biblia ambalo umelirejelea lilikuwa jambo ambalo Paulo alisema. Halikuwa jambo ambalo Yesu alisema. Paulo alikuwa mtume tu. Hata kama maneno yake yalirekodiwa katika Biblia, ni baadhi ya maneno yake tu yangeweza kuelezwa kama nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hata kama maneno yake yalilingana na ukweli, hayakuwa maneno ya Mungu na hayawezi kutajwa kana kwamba yalikuwa sawa na maneno ya Mungu. Aidha, baadhi ya yale ambayo Paulo alisema hayangeweza kuelezwa kama nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Badala yake, yalitokana kutoka kwa fikira na wazo na linaleta maana ya mwanadamu nalo. Maneno haya hayana msingi katika maneno ya Mungu. Kwa hiyo, inapofika suala la kukaribisha kurudi kwa mara ya pili kwa Bwana, ni lazima tusitumie maneno ya Paulo kama msingi. Badala yake, tunapaswa kutumia maneno ya Bwana kama msingi na kutafuta nia Zake kwa sababu ni maneno ya Bwana tu ni ukweli na sahihi 100%.” Baada ya kusikia hili, nilifikiri, “Ndiyo, Yesu kweli hakuwahi kusema “kunyakuliwa hadi mbinguni.” Haya yalikuwa maneno ya Paulo. Paulo alikuwa mwanadamu tu. Maneno yake kweli hayawezi kulinganishwa na maneno ya Mungu. Lazima tusitumie maneno ya Paulo kama msingi kwa kukaribisha kurudi kwa mara ya pili kwa Bwana. Kama mtu anayemwamini Mungu, napaswa kutumia maneno ya Mungu na kazi ya Mungu kama msingi. Hili ndilo linapatana na nia za Mungu!”

Dada huyo aliendelea kuzungumza, “Yesu alisema: ‘Na hakuna mwanadamu amepaa hadi mbinguni, isipokuwa yeye ambaye alishuka chini kutoka mbinguni, ambaye ni Mwana wa Adamu aliye mbinguni(Yohana 3:13). Kutoka kwa maneno ya Yesu, tungeweza kuona kwamba kando na Mwana wa Adamu ambaye alishuka chini kutoka mbinguni, ambaye ni Mungu mwenye mwili, hakuna mtu mwingine alipanda mbinguni. Mbinguni ni kiti cha enzi cha Mungu. Mungu Mwenyewe pekee ndiye anaweza kupanda hadi mahali hapa pakuu. Kama wanadamu, hatuwezi kupanda hadi mahali hapa pakuu kumwona Mungu. Badala yake, wakati ambapo Mungu alimwumba mwanadamu kwanza, Aliamua kabla kwamba binadamu wangeishi duniani. Mungu alitumia dunia kuwaumba mababu za wanadamu Adamu na Hawa na kuwasaidia kuishi katika Bustani ya Edeni. Walisikiza maneno ya Mungu, wakapokea baraka za Mungu na kusimamia kila kitu ndani ya bustani. Baadaye, binadamu pia wangesimamia kila kitu duniani lakini si mbinguni. Wakati ambapo binadamu walipotoshwa sana na dunia ilijaa upotovu na vurugu, Mungu aliamua kutumia gharika kuuharibu ulimwengu. Mungu alimwokoa Nuhu mtu wa haki anayemwabudu Mungu lakini Mungu hakumnyakua hadi mbinguni ili aweze kuepuka maji ya gharika. Badala yake, Mungu alimfanya Nuhu ajenge safina. Wakati gharika lilikuja, Nuhu na familia yake ya watu wanane walijikinga katika safina. Baada ya wao kuondoka kutoka kwa safina, Nuhu na familia yake waliendelea kuishi duniani na kuongezeka. Katika Enzi ya Sheria, Waisraeli waliteseka chini ya utumwa wa mikono ya Farao wa Misri. Wakati ambapo Mungu aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri na kuwasaidia kutoroka kuwindwa na Farao, Mungu hakuwanyakua Waisraeli hadi mbinguni. Badala yake, Mungu alionyesha mamlaka Yake duniani kwa kufanya aina zote za miujiza ili watu wangeweza kushuhudia uweza wa Mungu na kujua hekima ya Mungu na jinsi Alivyo wa ajabu. Baadaye, Mungu alitoa sheria na amri Zake kupitia Musa na kuwaelekeza Waisraeli kuhusu jinsi ya kuishi duniani. Katika wakati wa Enzi ya Neema, wakati ambapo binadamu hawakuweza kushika sheria na walikabiliwa na hatari za kuuwawa, mwanadamu hakuenda mbinguni kulipia kosa la dhambi zake. Badala yake, Mungu alipata mwili wa sura ya Yesu na akashuka chini duniani. Ili kuwaokoa wanadamu, Alisulubiwa. Hii ilikuwa njia pekee ya mwanadamu kupata wokovu wa Bwana. Kwa dhahiri, sisi, kama wanadamu, ni wa dunia. Mungu alituamulia kabla kuishi duniani. Aidha, Yesu alitufundisha: ‘Ombeni basi kwa namna hii: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni(Mathayo 6:9-10). Maneno ambayo Bwana anazungumza yana nia Zake. Bwana anataka tumwabudu duniani. Ufalme wa Kristo utashuka duniani pia. Kuna unabii katika Kitabu cha Ufunuo unaosema: ‘Na nikasikia kutoka mbinguni sauti kuu ikisema, Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao(Ufunuo 21:3). Kwa dhahiri, tamaa yetu ya kunyakuliwa hadi mbinguni kukutana na Bwana ni fikira na wazo letu kabisa na si ukweli hata kidogo.” Baada ya kumsikiza dada yangu akijadili, nilielewa wazi sana kwamba bila kujali kama tunaangalia kazi ambayo Mungu alifanya zamani au unabii wa Bwana, Mungu hakuwahi kutaja kwamba tungenyakuliwa hadi mbinguni. Kama bado tunaamini kwamba Mungu atarudi na kutunyakua hadi mbinguni, je, hii si fikira na wazo letu wenyewe? Je, huku si kufikiri kwetu kwa uwongo? Kimsingi, hili halikubaliani na maneno na nia za Mungu! Moyo wangu ulihisi kama mambo yalikuwa yamefanywa wazi. Hata hivyo, bado nilikuwa na swali moja: Hata kama kukubali kwetu kwa kunyakuliwa si sahihi, kunyakuliwa kunamaanisha nini kweli? Niliendelea kumwuliza dada huyu kutafuta kuhusiana na swali hili.

Dada huyo alisema, “Kuhusiana na kunyakuliwa, hili ni fumbo na sisi, kama wanadamu, hatuwezi kuielewa. Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, amekuja na kuonyesha mamilioni ya maneno na kufichua aina zote za ukweli na mafumbo. Nilipata kuelewa nilichowasilisha kutoka tu kusoma maneno ya Mungu. Kuhusiana na suala la kunyakuliwa, hebu tuangalie maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: ‘“Kunyakuliwa” si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanaweza kufikiria; hiyo ni fikira potovu sana. “Kunyakuliwa” kunaashiria kujaaliwa Kwangu halafu kuchagua. Hii inawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale wote wataonyakuliwa ni watu waliopata hadhi ya wazaliwa wa kwanza, au wana, auwale ambao ni watu wa Mungu. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu(“Sura ya 114” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa maneno ya Mungu tunaweza kuona kwamba kunyakuliwa hakukuwa jinsi tulivyokudhania kuwa. Hakukuwa kupaa kutoka duniani hadi mbinguni kumwona Mungu. Badala yake, inamaanisha wale ambao Mungu amewaamua kabla na kuwachagua. Hili linajumuisha wale ambao wanaweza kusikia sauti ya Mungu na kukubali kazi ya Mungu. Watakuja mbele ya Mungu wakati ambapo Mungu anakuja duniani kufanya kazi Yake. Hawa ndio watu wanaoletwa mbele ya Mungu. Hili ni sawa na kipindi cha mwisho cha Enzi ya Sheria. Wakati ambapo Yesu alikuja kufanya kazi Yake, wale wote ambao wangeweza kujua kwamba maneno ya Yesu yalikuwa sauti ya Mungu na walimkubali Yesu kama Bwana wa wokovu waliletwa mbele ya Mungu. Hili lilijumuisha Petro, Yohana, Mathayo na wanafunzi wengine, mitume na wale wote waliokubali wokovu wa Bwana. Wote waliletwa mbele ya Mungu. Na kuhusu wale walioshikilia Biblia ya Agano la Kale kama vile Mafarisayo na watu wa kawaida, hawakukataa kukubali wokovu wa Mungu tu, walihukumu, kupinga na kukufuru kazi mpya ya Mungu. Watu hawa hawakukosa kuletwa mbele ya Mungu tu, badala yake, walifichuliwa, kuondolewa na kuachwa na kazi mpya ya Mungu. Sasa, tayari ni siku za mwisho na Mwenyezi Mungu amefanya kazi mpya na kuonyesha maneno yanayotakasa na kumwokoa mwanadamu. Wale ambao wanaweza kujua kwamba ni sauti ya Mungu inayosema maneno ya Mungu, hufuata nyayo za Mwanakondoo na kukubali kazi mpya ya Mungu ya siku za mwisho wataletwa mbele ya Mungu. Tangu kazi ya Mungu ya siku za mwisho ionekane, zaidi na zaidi ya ndugu waaminifu, baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, wanaamini kwa uthabiti kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni ukweli na kwamba ni maneno ambayo Roho Mtakatifu anasema kwa makanisa. Mmoja baada ya mwingine, wamerudi mbele ya Mwenyezi Mungu. Wote ni wanawali wenye busara na wamekubali unyunyizaji, ustawishaji, hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu. Tabia zao potovu zimetakaswa hatua kwa hatua na wanamjua Mungu kweli. Watu hawa wote wanaletwa mbele ya Mungu. Kuhusu wale wanaosubiri kwa upumbavu Bwana aje na kuwanyakua hadi mbinguni ambapo watakutana na Mungu, wanashikilia fikira na wazo lao kabisa. Hawakosi kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho pekee, wanahukumu, kukashifu na kupinga kazi mpya ya Mungu. Wote ni wanawali wapumbavu. Sio tu kukosa kuletwa mbele ya Mungu, lakini mwishowe, wataanguka kwa majanga na kuadhibiwa na Mungu.”

Ukweli Kuhusu Kunyakuliwa

Baada ya kusikia mambo haya kutoka kwa dada huyu, nilipata ufahamu ghafla. Kama ilivyo, kunyakuliwa kunamaanisha sisi kukubali kazi mpya ya Mungu, kufuata nyayo za Mwanakondoo na kuja mbele ya Mungu. Jinsi alivyowasilisha hili kuliangaza kweli. Ni lenye uhalisi zaidi sana kuliko jinsi tulivyoamini mwanzoni kwamba tungenyakuliwa hadi mbinguni ambapo tungekutana na Bwana. Kama haingekuwa maneno ya Mungu kufichua mafumbo haya, bila kujali tunamwamini Bwana kwa muda upi, hatungeweza kuelewa. Tungekuwa tukiishi ndani ya fikira na wazo letu na kwa upumbavu tungesubiri Bwana atunyakue hadi ufalme wa mbinguni!

Baada ya dada huyu kuondoka, niliwaza tena na tena kuhusu kile alichosema. Nilitambua kwamba kama tunataka kuletwa mbele ya Mungu, cha umuhimu ni kwamba ni lazima tutafute maneno ambayo Roho Mtakatifu anasema kwa makanisa kwa kuwa tayari kupokea mawazo mapya. Ni lazima tuwe wanawali wenye busara na kutafuta kwa vitendo na kuchunguza sauti ya Bwana. Kwa njia hii, tutaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana na kuletwa mbele ya Mungu! Wakati huu, nilifikiri kuhusu moja ya mafunzo ya Yesu: “Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao. … Heri wenye moyo safi; kwa kuwa hao watamwona Mungu(Mathayo 5:3, 8). Nashukuru kwamba nuru ya Mungu imenisaidia kupata njia ya utendaji. Naelewa hatimaye maana ya kweli ya kunyakuliwa. Kwa sasa, aina zote za maafa zinatokea moja baada ya nyingine katika nchi ulimwenguni kote. Maafa makuu yako mbele yetu na kutafuta kuonekana kwa Mungu kunakaribia sana. Leo, ni Kanisa la Mwenyezi Mungu tu linashuhudia ukweli kwamba Bwana amerudi tayari. Aidha, injili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu tayari imefikia pembe zote za dunia. Vitabu vyake, video na filamu zinapatikana mtandaoni na watu kutoka ulimwengu mzima wanaweza kuzifikia na kuzichunguza. Sasa hivi, kitu cha pekee ambacho napaswa kufanya ni kuchunguza maneno ya Mwenyezi Mungu mara moja na kuona iwapo maneno ya Mwenyezi Mungu ni sauti ya Mungu na ukweli au la. Hili ni tukio kuu na muhimu sana zaidi inapofikia kukaribisha kurudi kwa Bwana!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Unyakuo wa kweli ni nini?

Aya za Biblia za Kurejelea: “Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki. Kisha mabikira...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp