Kondoo wa Mungu Wasikia Sauti Yake: Tunapaswa Kusikia Neno la Mungu Tunapochunguza Njia ya Kweli

19/07/2020

Na Su Xing, Uchina

Maradhi yameendelea kuenea katika miezi ya karibuni na idadi ya waliothibitika kuugua na vifo inazidi kupanda. Maafa yamejaa duniani nzima, kama vile kundi kubwa la wadudu, mafuriko na moto na tishio la vita linakaribia. Wakristo wengi wameanza kutambua kwamba Bwana amerudi tayari na sasa wanatafuta kuonekana Kwake. Siku hizi, ni Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee linaloshuhudia kwamba Bwana amerudi, na sasa wengi wanatafuta na kuchunguza kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu. Idadi inayoongezeka ya watu wanakuwa na uhakika kwamba hayo ndiyo sauti ya Mungu baada ya kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu, na kisha wanakubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Lakini kuna watu wengine ambao wanapoona kazi ya Mwenyezi Mungu ikikashifiwa na kushutumiwa na serikali ya CCP na wachungaji na wazee wa dunia ya dini wanaamua kuwafuata. Hawaamini kwamba hii ndiyo njia ya kweli na hawathubutu kuitafuta ama kuichunguza. Japokuwa tunapaswa kujitahadhari tunapochunguza njia ya kweli, je, inaambata na ukweli kuyachukulia maneno ya serikali ya CCP na wachungaji na wazee kuwa kiwango cha kuamua iwapo kitu fulani ndiyo njia ya kweli ama njia isiyo kweli? Ni nani hasa tunayepaswa kumsikiliza tunapochunguza njia ya kweli ili tuweze kukaribisha kurudi kwa Bwana? Tutashiriki na kuchunguza masuala haya hapa.

Kuamini Shutuma ya CCP ni Kuyaamini Maneno ya Shetani

Sote tunajua kwamba serikali ya CCP ni serikali inayomkana Mungu. Tangu ishikilie madaraka, CCP imekuza ukanaji Mungu, uyakinifu na kufuata nadharia ya mageuko. Daima imekana kuwepo kwa Mungu na imetetea uwongo wa kishetani kama “Hakujawahi kuwa na Mwokozi yeyote,” “Kudura ya mtu imo mkononi mwake mwenyewe” na “Mwanadamu anaweza kutengeneza nchi ya asili ya kufurahisha kwa mikono yake mwenyewe”. Pia CCP imeshutumu Ukristo hadharani kama “xie jiao,” na Biblia kama kitabu cha “xie jiao”. Imebomoa makanisa mengi sana, ikachoma nakala nyingi sana za Biblia na kuwakamata na kuwatesa Wakristo na Wakatoliki kwa utukutu. Tunaweza kuona kutokana na jinsi inavyotesa Ukristo na Ukatoliki kwa mhemuko kwamba CCP inadharau ukweli na Mungu kabisa. Je, utawala wa kishetani unaompinga Mungu unawezaje kukubali kuonekana na kazi ya Mungu? CCP inakataa kabisa kukubali kwamba kuna kitu kama njia ya kweli, sembuse kwamba kuna Mungu. Inapofikia kuamua iwapo njia fulani ni njia ya kweli ama la basi kuna tofauti ipi kati ya kuamini uvumi na uongo wa CCP na kuyaamini maneno ya Shetani ibilisi?

Aidha, sote tunajua kwamba njia ya kweli imepitia mateso tangu zama za kale. Utawala wote wa kishetani unamchukia Mungu na ukweli kabisa, na kadiri kitu fulani ni cha Mungu, ndivyo wanavyokipinga kwa hasira zaidi. Hiyo ndiyo maana kila wakati Mungu huja kutekeleza kazi Yake, Anateswa na kushutumiwa bila kuepukika na utawala wa kishetani—huu ni ukweli usiopingika. Bwana Yesu alipowasilisha mahubiri Yake na kufanya kazi Yake miaka hiyo yote iliyopita, makuhani wakuu na Mafarisayo wa imani ya Kiyahudi walishirikiana na mamlaka ya Kirumi kumsulubisha Yesu. Je, basi tunaweza kukana ukweli kwamba Bwana Yesu ni Kristo kwa sababu ya shutuma, mateso, uongo na kashfa ya utawala ulio mamlakani? Vivyo hivyo, Mungu amerudi sasa kufanya kazi Yake na CCP imezidi kushutumu na kukufuru kuonekana na kazi ya Mungu kwa ukali. Inawakamata na kuwatesa Wakristo kwa utukutu, na kutumia vyombo vya habari vya mtandaoni huko nyumbani na ugenini kueneza uongo wake unaokashifu kazi ya Mungu na kuwapotosha wale wasiojua ukweli. Inafanya hivi kwa sababu ya hofu, kwa sababu inaogopa kwamba Mungu ameonekana na anafanya kazi kuwaokoa wanadamu, na kwamba wanadamu wote watakubali ukweli na kumgeukia Mungu. Hata zaidi, inahofia kwamba maneno ya Mungu yatatimika duniani, kwamba ufalme Wake utaonekana duniani, na kisha wanadamu wote wataikataa CCP. Hii ndiyo sababu serikali ya Kichina inakandamiza kwa hasira na kutesa kikatili Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo sababu yake ya msingi kukashifu na kushutumu kazi ya Mungu. Ikiwa kweli tuna utambuzi, basi tunapaswa kuamua njia ya kweli ni ipi kwa kutumia kile kinachopingwa na kuchukiwa zaidi na utawala huu wa kishetani. Kinyume chake, tukiacha kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho kwa sababu inapingwa na kushutumiwa na serikali ya Kichina, basi tutakuwa wapumbavu wakubwa kweli.

Je, ni Sahihi Kuamini Kile Ambacho Wachungaji na Wazee Husema Wakati wa Kuchunguza Njia ya Kweli, na Kutosikiliza Neno la Mungu?

Watu wengine wanafikiri kwamba serikali ya CCP daima imempinga Mungu na kwamba hakuna kitu chochote inachoweka mtandaoni kinaweza kuaminika, lakini kwamba kwa upande mwingine, wachungaji na wazee wana maarifa mengi ya Biblia na wanaielewa, kwa hivyo kwa kuwasikiliza wanapochunguza njia ya kweli, hawawezi kukosea. Lakini, je, tumewahi kuzingatia yafuatayo: Je, mtu kuwa na maarifa mengi ya Biblia kunaweza kuthibitisha kwamba anaelewa ukweli? Je, kunaweza kuthibitisha kwamba anamjua Mungu? Tukifikiria nyuma kwa makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo wa imani ya Kiyahudi, walikuwa na maarifa mengi ya Maandiko na waliwaelezea wengine Maandiko mara kwa mara. Lakini wakati Bwana Yesu alionekana na kutekeleza kazi Yake, je, walimtambua kuwa Masihi? Je, walitambua maneno Yake kuwa ukweli, sauti ya Mungu? Hawakukosa tu kumtambua Bwana, lakini kwa ajili ya vyeo na riziki zao, walitumia maana halisi ya Maandiko kumtathmini Bwana, na wakabuni uvumi kumhusu na kumpunguzia sifa. Walimtesa na kumkufuru kwa ukali, na hatimaye walishirikiana na mamlaka ya Kirumi kumsulubisha Bwana Yesu. Ukweli huu unathibitisha vya kutosha kwamba kwa sababu tu mtu fulani ana maarifa mengi ya Biblia na anaielezea mara kwa mara, hii haimaanishi kwamba anaelewa ukweli, sembuse kwamba anamjua Mungu. Hili lilikuwa jambo ambalo waumini wa Kiyahudi wa wakati huo hawakuelewa kikamilifu, na hawakuwa na utambuzi ilipofikia suala la Mafarisayo. Kuhusu kumkaribisha Bwana, waliamini bila kufikiri kile ambacho viongozi wa kidini walisema, na ingawa wengine walijua vyema kwamba maneno na kazi ya Bwana Yesu yalikuwa na mamlaka na uwezo, bado waliamini uvumi na kashfa zilizotolewa na Mafarisayo wa kidini. Kwa hivyo walidanganywa na wakaungana na viongozi wao wa kidini katika kumshutumu na kumkataa Bwana Yesu. Hawakukosa tu kupokea wokovu wa Bwana, lakini badala yake waliadhibiwa na Mungu.

Kwa njia hiyo hiyo, ingawa wachungaji na wazee wa leo ni wana maarifa mengi ya Biblia, hili halithibitishi kwamba wanaelewa ukweli ama wanamjua Mungu. Kwa kawaida, mengi ya yale wanayohubiri ni maarifa ya Biblia na nadharia ya kitheolojia; ni nadra sana ambapo wanahubiri ama kushuhudia maneno ya Bwana Yesu. Maarifa yao ya Biblia na nadharia ya kitheolojia hayawezi kuruzuku maisha ya watu, na bila kujali kiasi wanachojua, hayaonyeshi hata kidogo kwamba wanaelewa ukweli ama kumjua Bwana. Tunachohitaji sasa zaidi ni kuelewa ukweli fulani, kama vile sababu ya dunia ya kidini kuwa na ukiwa sana, jinsi ya kutatua chanzo cha asili cha ukiwa wa kanisa, jinsi ya kutafuta nyayo za Mungu, jinsi ya kumkaribisha Bwana, jinsi ya kutenda mapenzi ya Mungu na kumtii Bwana, jinsi ya kujiweka huru dhidi ya pingu na minyororo ya dhambi na kutakaswa ili kulingana na Kristo na kadhalika. Wachungaji na wazee hawajawahi kuhubiri ukweli kama huu kwa sababu wao wenyewe hawauelewi. Iwapo wangeuelewa ukweli huu, basi waumini wangenyunyizwa na kuruzukiwa. Wakati wachungaji na wazee wao wenyewe hawauelewi ukweli ama kumjua Bwana, basi wanawezaje kutuongoza kukaribisha kurudi kwa Bwana? Biblia inasema, “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia(Mathayo 4:10). “Watu hawa wananikaribia kwa vinywa vyao, na wananiheshimu kwa midomo yao; lakini moyo wao uko mbali nami. Lakini wananiabudu bure, wakifunza mafundisho ya dini ambayo ni amri za wanadamu(Mathayo 15:8–9). “Amelaaniwa mtu amwaminiye mwanadamu, na amfanyaye mwanadamu kinga yake na ambaye moyo wake umeondoka kutoka Yehova(Yeremia 17:5). Bwana anatushauri kwamba ni lazima tumtukuze Mungu kama aliye mkuu katika imani yetu, na tumwabudu Mungu kwa moyo wa kweli. Hatupaswi kuwathamini watu wengine ama kuamini kwa urahisi kile wanachosema watu wengine, vinginevyo Bwana hatawahi kutusifu bila kujali jinsi tunavyomfuata. Tunapomwamini Mungu, tukiwaamini wachungaji na wazee bila kufikiri inapofikia suala muhimu la kuchunguza njia ya kweli, na tuwaachie majaliwa na hatima zetu wazipange, hii ni shida ya aina gani? Je, huko ni kumwamini Mungu, ama ni kuwaamini watu? Tunapochunguza njia ya kweli, tunapaswa kusikiliza kile ambacho Mungu husema, ama kile ambacho wachungaji na wazee husema? Ikiwa hatuna maoni yetu wenyewe bali tunaamini maneno ya wengine tu bila kufikiri tunapochunguza njia ya kweli, je, huku si kukosa kuwajibikia maisha yetu wenyewe? Basi tutakuwa wenye kuelekea kutenda makosa yale yale kama walivyofanya watu wa kawaida wa Kiyahudi miaka hiyo yote iliyopita, na tutaachwa na kuondolewa na Bwana!

Tunapaswa Kusikiliza Sauti ya Mungu Tunapochunguza Njia ya Kweli

Tunapaswa Kusikiliza Sauti ya Mungu Tunapochunguza Njia ya Kweli

Tunapaswa kuwa na maoni yetu wenyewe inapofikia kuchunguza njia ya kweli badala ya kuamini bila kufikiri kile ambacho wachungaji, wazee ama serikali ya Kichina husema. Ni lazima tutende kulingana na maneno ya Bwana, kwa maana ni hapo tu ndipo tutaweza kukaribisha kuonekana kwa Bwana. Bwana Yesu alisema, “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Sura za 2 na 3 za Kitabu cha Ufunuo zinatabiri mara nyingi: “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa.” Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema, “kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa ‘Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.’ Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani!(“Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Tunaweza kuona kutoka kwa hili kwamba Mungu hunena maneno zaidi Anaporudi katika siku za mwisho, na tunapaswa kuwa wale wanawali wenye busara wanaolenga kusikia sauti ya Mungu. Wanawali wenye busara wana ubora wa tabia na wana utambuzi wa kiroho; wanaweza kufahamu kutoka kwa matamshi ya Kristo kwamba maneno haya ndiyo ukweli, njia ya uzima, na kwa hivyo wanaweza kutambua sauti ya Mungu na kukaribisha kuonekana Kwake. Kwa mfano, Bwana Yesu alipoonekana na kufanya kazi Yake katika Enzi ya Neema, Alionyesha njia ya “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). Petro, Yohana na wale wanafunzi wengine waliomfuata Bwana Yesu wote walimtambua Bwana kupitia sauti ya Mungu. Waliweza kusikia kwamba kile ambacho Bwana alikuwa akionyesha kilikuwa ukweli, na kwa hivyo waliwacha wazazi na nyumba zao bila kusita ili wamfuate Bwana, na wao walinyunyiziwa na kuchungwa na Yeye binafsi. Katika kipindi walipomfuata Bwana Yesu, walisumbuliwa na kuzuiwa kwa njia za kila namna na Mafarisayo, na wakakashifiwa na kushutumiwa na mamlaka ya Kirumi. Lakini walisikiliza tu maneno ya Mungu na kumtii, wakikataa kusumbuliwa ama kudanganywa na mamlaka tawala ama Mafarisayo wa kidini. Baada ya kumtambua Kristo, walimfuata hadi mwisho, walisali Kwake, na wakapitia maneno Yake. Walipevuka polepole maishani na wakaja kuwa na maarifa kiasi juu ya Mungu. Hata hivyo, waumini wa Kiyahudi walikuwa wagumu, wasiojua na wakaidi, ingawa walisikia mamlaka na uwezo katika maneno ya Bwana Yesu, na walijua kwamba hakuna mtu ambaye angeweza kusema mambo kama hayo, bado hawakuweza kumwamini ama kumfuata. Walitikisika walipopata dalili ya kwanza ya kusumbuliwa na kudanganywa na Mafarisayo; walimwamini Mungu lakini hawakuweza kusikia maneno Yake, hawakuwa na utambuzi ama maoni yoyote yaliyokuwa yao wenyewe, na hata wakafika kiwango cha kusimama kwenye upande wa Shetani kumpinga Mungu. Mwishowe, watu kama hao wangeweza tu kuachwa na kuondolewa na Mungu, wakitumbukia kuzimu ili waadhibiwe milele. Kwa hiyo, tunapochunguza njia ya kweli, hatupaswi kuamini kile ambacho watu wengine wanasema bila kufikiri, lakini tunapaswa kulenga kusikia sauti ya Mungu na kutambua kwamba Kristo ndiye ukweli, njia na uzima. Hili ndilo muhimu kabisa.

Injili ya siku za mwisho ya Mwenyezi Mungu sasa inaenea katika ulimwengu mzima, na kitabu cha maneno bora yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu—Neno Laonekana Katika Mwili—kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 20, na kinapatikana hadharani mtandaoni kwa wanadamu wote kutafuta na kuchunguza. Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli wote ili kuwaokoa wanadamu, kama vile imani ya kweli katika Mungu ni nini, kumtii Mungu na kumpenda Mungu ni nini, jinsi tunavyoweza kumcha Mungu na kuepuka maovu, jinsi tunavyoweza kulingana na Kristo, jinsi tunavyoweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana na zaidi. Watu kutoka mataifa yote duniani kote ambao wametamani sana Mungu aonekane wameitambua sauti ya Mungu katika maneno ya Mwenyezi Mungu na mmoja baada ya mwingine wamerudi kwa nyumba ya Mungu. Bila kujali jinsi wachungaji na wazee hujaribu kuzuia, ama ni kashfa na kufuru ya aina gani ambayo serikali ya Kichina hueneza, wanamfuata Mungu kwa uthabiti. Watu hawa ndio wanawali wenye busara, wale ambao wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, wale walio na fursa ya kutakaswa na kukamilishwa na Mungu, na kufanywa kuwa washindi na Mungu katika siku za mwisho. Kisha kuna wale wanaoona kwamba maneno yote ambayo Mwenyezi Mungu huonyesha ni ukweli, kwamba ni sauti ya Mungu, lakini wanadanganywa na kuzuiwa baada ya kusikia ilani zilizonenwa na wachungaji na wazee, na hawathubutu kuchunguza kazi ya Mungu. Hata wanafika kiwango cha kushuku njia ya kweli na kazi ya Mungu—je, wanawali wenye busara wanatenda hivi? Mungu anaweza kuzungumza maneno mia mja na wakose kuyaamini kikamilifu, lakini mtu mmoja kati ya wanadamu wapotovu anaposema neno moja tu, wanalikubali kikamilifu—je, wao si wanawali wapumbavu? Wanapochunguza njia ya kweli, wanawali wapumbavu hawasikilizi sauti ya Mungu, lakini badala yake wanasikiliza sauti ya mwanadamu. Wanasumbuliwa na kudanganywa siku zote na Shetani, na mwishowe watateketezwa na Shetani. Watapoteza wokovu wa Mungu, na wataachwa na kuondolewa na Mungu, na wataangamizwa na maafa. Hili linatimiza kabisa maneno haya katika Biblia: “Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa(Hosea 4:6) na “Wapumbavu hukufa kwa ajili ya ukosefu wa hekima” (Mithali 10:21).

Sasa, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho itakamilika karibuni. Je, tunataka tuwe kama Petro, tuwe watu wanaosikia sauti ya Mungu na kumkaribisha Bwana? Ama tunataka tuwe kama waumini wa Kiyahudi, tukifuata bila kufikiri kile ambacho wachungaji, wazee na utawala wa kishetani husema, na hivyo tupoteze wokovu wa Mungu? Iwapo tumeamua kusikiliza maneno ya Mungu ama maneno ya mwanadamu tunapochunguza njia ya kweli kutaamua majaliwa na hatima zetu za mwisho! Jinsi Mwenyezi Mungu anavyosema, “Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote).

Maelezo ya Mhariri: Iwapo una maswali ama matatizo yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia mazungumzo ya moja kwa moja na tunaweza kuyachunguza na kuyajadili pamoja.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp