Mateso na Maafa Yalinisaidia Kukua

14/01/2018

Baituo Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong

Kabla, nilijua tu kwamba hekima ya Mungu ilitumiwa kwa msingi wa njama za Shetani, kwamba Mungu ni Mungu mwenye hekima na kwamba Shetani milele atakuwa adui mshinde wa Mungu katika nadharia, lakini sikuwa na ufahamu halisi au maarifa. Baadaye, ni ndani tu ya mazingira yaliyopangwa na Mungu nilipopata uzoefu halisi wa kipengele hiki cha kweli.

Nilikuwa kwa mkutano fulani alasiri moja, wakati ghafla kiongozi wa wilaya alikimbia kwangu kwa haraka na kusema, “Mama yako amechukuliwa na joka kubwa jekundu. Usiende nyumbani kwa muda. Kanisa litakutayarishia familia mwenyeji.” Habari hii ilinipiga kama tukio la ghafla lisilotarajiwa na kunitetemesha sana kiasi kwamba niliduwazwa ghafla: Ati nini? Mama yangu amechukuliwa na joka kubwa jekundu? Je, joka kubwa jekundu litamtesa vipi? Je, ataweza kuvumilia? Huenda nisimuone mama yangu tena kamwe. Napaswa kufanya nini? Nikifikiria mambo haya, moyo wangu ulikuwa katika mateso na sikuweza kuyazuia machozi yangu. Baada ya mkutano kukamilika, nilipelekwa kwa familia mwenyeji niliyopangiwa na, baada ya kutulia, mawazo yangu yalirudi tena kwa mama yangu. Nyumbani, nilikuwa karibu mno na mama yangu. Ingawa baba yangu asiyemwamini Mungu alijaribu kunilazimisha kuachana na Mungu, dada yangu mkubwa alinipuuza kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu na jamaa zangu wengine wote walinitelekeza, sikuwahi kujihisi mpweke, kwa sababu bado nilikuwa na mama yangu ambaye pia alimwamini Mungu. Kama kwa kiroho au kwa kimwili, mama yangu alinitunza daima, alinipenda sana, na alinisaidia mara nyingi. Wakati wowote nilipokuwa na shida fulani niliweza kuzungumza naye kuihusu; unaweza kusema kwamba alikuwa mwamba wangu. Bali sasa yule tu ambaye niliweza kumtegemea alikuwa amechukuliwa na joka kubwa jekundu. Nilihisi kana kwamba tayari nilikuwa nimegeuka yatima kwa ghafla, bila kujua jinsi ya kuitembea barabara iliyo mbele, wala kujua ni nani wa kumwendea wakati nilipokabiliwa na matatizo. Kwa siku chache zilizofuata, nililia mchana kutwa, niliishi katika maumivu ya siku zote na kujihisi kushuka sana. Nilipokuwa nikiishi katika hali hii, bila kuweza kujiweka huru, kulikuwa na mwongozo ndani: “Je, kwa kweli uko radhi kuishi daima katika giza, ukimruhusu Shetani kukudanganya? Na je, kwa kweli huko radhi kumwelewa Mungu katika kazi Yake na kuishi katika mwanga?” Maneno haya yalinizindua mara moja. Hilo ni sawa, nilifikiri. Kwa kweli nitaendelea kuishi daima jinsi hii katika giza, nikimruhusu Shetani kunidanganya? La, siwezi! Hali hii ambayo imenifika ni lazima hakika imeshikilia wema wa Mungu. Baadaye, nilikwenda mbele ya Mungu mara nyingi kuomba na kumtafuta Mungu, kumwomba Mungu anipatie nuru ili nipate kuyaelewa mapenzi Yake.

Baada ya muda, niligundua kuwa nilikuwa nimeanza kuingia katika baadhi ya ukweli ambao sikuwa nimeuelewa awali au ambao sikuwa nimeweza kuuweka katika matendo. Nilikuwa nikidekezwa nyumbani na chakula, nguo na kujifurahisha vilichukua muda wangu mwingi. Mwili wangu haungeweza kudhulumiwa na haungeweza kuvumilia shida hata kidogo. Katika siku chache baada ya kuondoka nyumbani na nilikuwa nikiishi na familia mwenyeji, sikuweza kufanya chochote nilichotaka, sikuweza tena kufanya kama nilivyotaka kama nilivyokuwa nimefanya nyumbani. Hatua kwa hatua, asili yangu ya kudekezwa na tabia mbaya zilipungua, na nikaja kujua kwamba kuwa na chakula na mavazi katika maisha ni kuridhika. Pia nilipata umaizi juu ya kiini cha mwili, kamwe kutoendelea tena kufuatilia ridhaa ya mwili, na nilikuja kujua kuwa kutafuta kumridhisha Mungu ndilo jambo muhimu zaidi ambalo kiumbe anaweza kulifanya. Kabla, wakati mama yangu alikuwa nyumbani, bila kujali kama nilikuwa na masuala ya kimwili au matatizo katika maisha yangu, siku zote nilimtegemea na kumwacha anisaidie kuyatatua. Nilipokumbana na matatizo, sikumwomba Mungu, sikutafuta ukweli, wala sikuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Baada ya mama yangu kuchukuliwa, sikuwa na yeyote wa kumtegemea nilipopata matatizo. Ningeweza tu kwenda mbele ya Mungu aghalabu kumwomba, kula na kunywa zaidi ya maneno ya Mungu, aghalabu kutafuta mapenzi Yake. Hatua kwa hatua, mahali ambapo mama yangu alikuwa ameshikilia moyoni mwangu paliendelea kuwa padogo, wakati nafasi ya Mungu katika moyo wangu iliendelea kuwa kubwa sana. Nilihisi kwamba Mungu angeweza kunisaidia wakati wowote niliohitaji, kwamba sikuweza kumwacha Mungu hata kwa wakati mmoja. Aidha, nilijifunza pia kutegemea sala na kutegemea ukimbizaji wangu wa ukweli ili kutatua shida zangu, na nilionja hisia ya amani, uhakika na kutegemewa inayotokana na kuwa na Mungu pamoja nami. Nilipoishi nyumbani, ingawa nilijua kwamba waumini na wasiokuwa waumini walikuwa aina mbili za watu ambao walikuwa si wa kutangamana, bado nilihisi kana kwamba ni wazazi wangu tu na dada yangu mkubwa waliokuwa familia yangu, na daima niliwaona ndugu zangu wa kiume na wa kike katika kanisa kama watu wa nje, daima nikihisi umbali kati yetu. Baada ya Mungu kutumia mazingira “kunifukuza” kutoka kwa nyumba yangu, nilikuwa pamoja na ndugu zangu wa kiume na wa kike katika familia mwenyeji wangu kutoka asubuhi mpaka usiku, na nilihisi wasiwasi wao na utunzaji wao kwangu, uvumilivu wao na wao kuelewa hisia zangu. Tulizungumza lugha moja, tulikuwa na malengo sawa na tulisaidiana katika maisha; kutoka moyoni mwangu, nilihisi kwamba hii ndiyo iliyokuwa familia yangu ya kweli tu, kwamba ni ndugu zangu wa kiume na wa kike katika kanisa tu waliokuwa baba yangu, mama na ndugu zangu. Hakukuwa tena na utengano wowote kati yangu na ndugu zangu wa kiume na wa kike katika kanisa, hakukuwa na umbali, na nilipitia wema mwingi unaotokana na kuwa na familia kubwa. Kupitia mazingira haya na ndugu zangu wa kiume na wa kike, nilijifunza pia jinsi tungeweza kupendana, kusameheana na kusaidiana katika maisha, ili ubinadamu wangu wa kawaida ulipona. Ukweli huu ni ule ambao sikuweza kuutia katika matendo kabla, wakati nilipoishi nyumbani na kutegemea mikutano na mahubiri. Baada ya mama yangu kuchukuliwa na joka kubwa jekundu na nikalazimika kuondoka nyumbani, katika mazingira haya ya kipekee na bila mimi kujua, Mungu aliugusisha ukweli huu ndani yangu na hatua kwa hatua akaimarisha ufahamu wangu. Baada ya kuingia kwangu katika ukweli huu, moyo wangu uliotafuta kumpenda na kumridhisha Mungu ukawa na nguvu wakati wote na nia yangu ya kuishi maisha yangu yote kwa ajili ya Mungu ikawa imara hata zaidi. Yule mtu niliyekuwa—ambaye alimwamini Mungu lakini hakuwa na kusudi, ambaye alikuwa dhaifu wakati wowote tatizo lilipokuja—alikuwa akipitia mabadiliko asteaste. Kile Mungu alichonipa kwa kweli kilikuwa zaidi kuliko jinsi ambavyo ningeweza kufikiri, na moyo wangu ukajawa na shukrani na sifa Kwake.

Siku moja, wakati wa ibada yangu ya kiroho, nilisoma maneno ya Mungu yanayosema: “Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema. Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. … Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake …(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo). Maneno ya Mungu ghafla yaliuwasha moyo wangu, na sikuweza kujizuia kushusha pumzi kutoka ndani: Mungu kwa kweli ni Mungu mwenye hekima! Matendo ya Mungu kwa kweli ni ya ajabu na yasiyotarajiwa! Hali hii imenifika leo na, kwa juu juu, inaonekana kana kwamba joka kubwa jekundu limemchukua mama yangu, limechukua mwamba wangu wa pekee, limefanya vigumu kwangu kurudi nyumbani, limejaribu bila kufaulu kutumia tukio hili ili kuzuia imani yangu kwa Mungu na kunifanya kusalimu amri, au kuwa dhaifu na kusalimu amri kwa kuniogofya kwa ushawishi wake. Lakini hekima ya Mungu hutumiwa kwa msingi wa njama za Shetani, na Mungu aliitumia kwa athari kubwa. Yeye alinirusha nje ya mahali pangu pa kupumzika pa kustarehesha na, kwa njia ya mazingira haya, Akaituliza dhamira yangu, Akaboresha dhamira yangu kupitia mateso, Akanifundisha kuwa na uwezo wa kuishi kwa kujitegemea, Akanifundisha jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida na jinsi ya kuwa mtu halisi; ukweli huu ni kitu ambacho sikuwa na njia ya kukielewa, sikuwa na njia ya kuupata katika mazingira ya raha na faraja. Kwa njia ya mazingira haya, Mungu aliugusisha ukweli Wake na kile Alicho ndani ya maisha yangu, ili kwamba sikukosa kusalimu amri tu kwa sababu ya mateso ya joka kubwa jekundu lakini, kwa kinyume, nilipata ukweli ambao Mungu alikuwa amenipa na nililetwa chini ya wokovu wa Mungu. Aidha, kupitia kwa mateso ya joka kubwa jekundu, niliona uso wake mshenzi, mkatili na asili yake ya kupinga maendeleo inayompinga Mungu hata kwa dhahiri zaidi. Kutoka moyoni mwangu, nililichukia hata zaidi, na moyo wangu ambao ulitaka kumpenda Mungu ukawa na nguvu hata zaidi.

Ninamshukuru Mungu! Kutoka kwa uzoefu huu, nilipata ufahamu kiasi wa kivitendo wa uweza na ukuu wa Mungu, na kupata uzoefu wa kivitendo wa ukweli kwamba hekima ya Mungu hutumiwa kwa msingi wa njama za Shetani. Nilielewa kuwa kila kitu kinachofika ambacho hakipatani na dhana za mwanadamu kina nia njema ya Mungu. Haijalishi jinsi Shetani hutiisha njama zake, Mungu atakuwa Mungu mwenye hekima wakati wote, na Shetani atakuwa adui mshinde wa Mungu milele. Kwa kuelewa hili, mapenzi yangu ya kumfuata Mungu sasa ni dhabiti zaidi, na nimejawa na imani kwa njia iliyo mbele!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp