Upendo wa Aina Tofauti
Nafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na matukio mapya na tofauti na kujawa na upekuzi, na nilikuwa na hisia nzuri kuhusu siku zijazo. Lakini baada ya muda fulani, hisia hii mpaya na tofauti ilibadilishwa haraka kwa upweke na uchungu wa kujipata katika nchi ya mbali ya kigeni. Kila siku nilirudi nyumbani peke yangu na kula peke yangu, nikikodolea kuta macho siku baada ya siku bila kuwa na yeyote hata wakuzungumza naye. Nilihisi mpweke mno, na mara nyingi ningelia kisirisiri. Nilipokuwa tu nikihisi kuhuzunishwa sana na asiyejiweza kabisa, Bwana Yesu alinipeleka kwenye mkutano kupitia rafiki mmoja. Kupitia kusoma maneno ya Mungu, kuimba nyimbo, na kuomba katika mikusanyiko, moyo wangu wenye ukiwa ulifarijiwa na Bwana. Nilipata habari kutoka katika Biblia kwamba mbingu na nchi na vitu vyote viliumbwa na Mungu, na kwamba mwanadamu pia ni kiumbe wa Mungu. Niligundua pia kuwa Bwana Yesu alisulubiwa kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu, kwamba ilikuwa ni Bwana Yesu ambaye alitukomboa kutoka kwa dhambi, na kwamba Yeye tu ndiye Mkombozi wa wanadamu. Baada ya kuja mbele za wokovu wa Bwana, ambao ni mkuu kuliko mengine yote, nilihisi kuguswa sana na niliazimia kumfuata Bwana kwa maisha yangu yote. Kwa hivyo nilibatizwa mnamo Sikukuu ya kutoa shukrani na nikawa Mkristo rasmi. Kwa sababu nilipenda kuimba, hususa kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, baada ya kubatizwa nilianza kuhusika kwa bidii katika kufanya kazi kwa ajili ya kanisa kwa kujiunga na kwaya. Kwa sababu ya mwongozo na baraka za Mungu, niliishi kwa amani na furaha. Kila nilipokwenda kwenye mkutano au kumsifu Mungu katika ibada, nilihisi kujawa na nguvu.
Lakini nyakati nzuri hazidumu milele, na nilipoingia katika safu ya huduma ya kanisa, pole pole nilikuja kuona kwamba ndugu kanisani walionekana kijuujuu wenye kupendana na wenye kutunzana, na wote walionekana kupatana vizuri, lakini kwamba kwa kweli kila kitu walichosema na kufanya kilikuwa kwa ajili ya maslahi yao wenyewe. Hawakutaka kupata hasara yoyote ya kibinafsi walipokuwa wakifanya kazi katika huduma ya kanisa, na mara kwa mara walisengenyana kuhusu ni nani aliyekuwa akifanya mengi na ni nani aliyekuwa akifanya machache. Hata mchungaji alikuwa mwenye madharau sana. Aliwatendea watu kulingana na kiasi cha michango yao, na alifanya tangazo maalumu la michango kila alipotoa mahubiri. Kila alipokuja kwenye mkutano, suala ambalo mchungaji alijishughulisha nalo lilikuwa ikiwa watu walikuwa wakitoa michango au la na walikuwa wakitoa kiasi gani, na hakutaka kusikia lolote kuhusu maisha ya kina ndugu. Alizungumza kuhusu upendo lakini sikuwahi kumwona akichukua hatua yoyote halisi. Wakati wowote ndugu au dada alikuwa na tatizo, mchungaji hangemsaidia au kumhimili. Lakini kilichokuwa cha kufedhehesha zaidi ni kwamba bado angewakosoa watu na kuwadharau wale ndugu fukara na wasio na uwezo. Nilipoona hali hii kanisani, nilivunjwa moyo lakini pia nilichanganyikiwa: Je, kanisa lilikuwa limebadilikaje na kuwa lisilo tofauti na jamii kwa ujumla? Pole pole, nilipoteza upendo na imani ambayo nilikuwa nayo mwanzoni, na sikushiriki tena kwa bidii nilipoenda kanisani Jumapili. Hata sikutaka kuimba. Kila wiki nilipoenda kanisani, ningesimama nje nikikunywa kahawa au kulala kidogo katika benchi za kanisa. Mahubiri yalipokwisha, ningetoa mchango wangu na kuondoka, na daima ningeondoka nikiwa na hisia ya huzuni na kukosa msaada moyoni mwangu.
Jumapili moja mnamo Agosti ya mwaka wa 2016, nilikutana na Dada Li Min kwenye bustani moja. Alikuwa amekuja kutoka Marekani na alikuwa mwanafunzi mwenza wa kina dada Gao Xiaoying na Liu Fang. Sote tulimwamini Bwana, na tulizungumza tulipokuwa tukiketi kwenye nyasi. Tulizungumza na kuzungumza na kufikia kwenye mada ya hali ilivyo kanisani, na niliwaambia kila kitu nilichokuwa nimekiona kanisani. Nilipomaliza kuzungumza, Dada Li Min alikubali kwa kichwa akiwaza na kusema “Siku hizi, sio tu kwamba kanisa lenu limekuwa namna hii, lakini ulimwengu wote wa kidini umepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, na umeanguka katika giza na ukiwa. Bwana Yesu alitabiri hapo nyuma: ‘Na kwa kuwa uovu utaongezeka, mapenzi ya wengi yatakuwa baridi’ (Mathayo 24:12). Sasa tuko katika siku za mwisho, na uhalifu unaongezeka kwa kuenea pote katika dini. Wachungaji na wazee hawazingatii amri za Bwana, hawatendi njia ya Bwana, na wanadhani kwamba sio suala kuu kuishi katika dhambi hivyo. Sote twajua kwamba kufanikiwa kwa kanisa ni tokeo linalotimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, Mungu ametekeleza kazi mpya tayari, na kazi ya Roho Mtakatifu imehamia kwa kikundi cha watu wanaokubali na kutii kazi mpya ya Mungu. Wachungaji na wazee katika dini hawawaongozi waumini kutafuta na kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, lakini badala yake wanapinga na kuilaani kazi mpya ya Mungu kwa kueneza kila aina ya uvumi na uwongo ili kuwazuia watu kumgeukia Mungu. Wanakumbana na chuki na kukataliwa kwa Mungu na kwa hivyo ulimwengu mzima wa kidini hauna baraka za Mungu, umepoteza kabisa kazi ya Roho Mtakatifu, na umetelekezwa na kuondolewa na Bwana. Kanisa basi linakuwa lenye ukiwa na kuhuzunika zaidi na zaidi. Ni kama tu Bwana Yesu alipopata mwili ili kutekeleza kazi Yake. Kazi ya Bwana Yesu ilianzisha Enzi ya Neema na kutamatisha Enzi ya Sheria. Kwa sababu wale waliomfuata Bwana Yesu walikubali na kutii kazi mpya ya Mungu, kisha walipata kazi ya Roho Mtakatifu, ilhali Roho Mtakatifu hakufanya kazi kati ya wale ambao hawakumkubali Bwana Yesu na ambao walisalia hekaluni. Na kwa hivyo, hekalu ambalo wakati mmoja lilikuwa limejawa na utukufu wa Mungu na ambapo waumini walimwabudia Mungu liligeuka kuwa mahali pa kufanyia biashara na tundu la wezi. Yaani, kuna sababu mbili za kanisa kuwa lenye ukiwa: Ya kwanza ni kwa sababu wachungaji na wazee hawafuati amri za Mungu au kutenda kulingana na neno la Mungu, na kwa sababu wao wanatenda dhambi na kutenda maovu siku zote; sababu ya pili ni kwa sababu Mungu anatekeleza kazi mpya, kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu imehama, na kwa sababu watu hawaendi kwa mwendo sawa na nyayo za Mungu. Hata hivyo, mapenzi ya Mungu ndicho chanzo cha ukiwa wa kanisa, na kuna ukweli wa kutafutwa hapa. Kupitia ukiwa wa kanisa, Mungu anawalazimisha wale wote wanaomwamini kwa mioyo ya kweli na ambao wana kiu ya ukweli kuacha dini, ili waweze kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu, waende kwa mwendo sawa na nyayo za Mungu, waje mbele za Mungu, na wapate kazi ya Mungu ya sasa na wokovu Wake.”
Baada ya kusikiliza ushirika wa Dada Li, nilikubali kwa kichwa na kusema, “Unayoyasema ni sahihi. Bila shaka ni kama tu unavyosema. Sikuwahi kuweza kuelewa tatizo hili. Kanisa hapo mwanzo lilikuwa mahali pa kumwabudia Mungu, lakini hakuna tofauti tena kati ya kanisa na jamii kwa jumla. Zaidi ya hayo, hakuna nuru mpya katika yale ambayo wachungaji wanahubiri, wala raha yoyote katika kuwasikiliza, na sasa watu wote wanaishi gizani. Inavyobainika, ni kwa sababu hatujaendelea kwa mwendo sawa na kazi mpya ya Mungu, kwa hivyo je, tunapaswa kufanya nini ili kuendelea sawa na kazi mpya ya Mungu?” Dada Li alisema, “Bwana Yesu alirudi zamani. Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili kama Mwana wa Adamu ili kuonyesha ukweli chini ya jina la Mwenyezi Mungu, na ili atekeleze hatua ya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu. Lazima tuendelee sawa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho na tukubali hukumu ya neno la Mungu, na ni wakati huo tu ndipo tutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu.” Niliposikia kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi tayari na alikuwa akitekeleza kazi ya hukumu, nilishangazwa. Niliwaza: “Je, si hukumu ni kumwadhibu mtu baada ya yeye kutangazwa kuwa mwenye dhambi? Mungu anakuja katika siku za mwisho kuwahukumu wale ambao hawamwamini Mungu, na sisi tunaomwamini Bwana Yesu tumesamehewa dhambi zetu tayari na tumetunukiwa wokovu. Hatuhitaji kupokea hukumu ya Mungu, kwa ajili Bwana atakaporudi, Atatuinua moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni. Angewezaje kuja kutuhukumu?” Kwa wazo hilo, nilishiriki mawazo yangu, wakati Dada Liu Fang alisema, “Ndugu, tayari nimekuwa nikichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho pamoja na Dada Gao kwa muda wa wiki moja. Kwa kusoma neno la Mwenyezi Mungu, tumelitambua kuwa ni sauti ya Mungu. Mwenyezi Mungu kweli ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Soma maneno ya Mwenyezi Mungu, na kisha utaelewa. Sababu Bwana Yesu amerudi kutekeleza kazi ya hukumu ni kwa sababu, ingawa sisi tunaomwamini Bwana tumesamehewa dhambi zetu, bado daima tunaishi katika dhambi ambayo hatuwezi kujiondoshea. Hatuwezi kujiweka huru kutoka kwa utumwa na udhibiti wa dhambi, na kwa kweli tunahitaji Mungu aonyeshe ukweli ili Atuhukumu na kututakasa, na ili aondoe kabisa asili zetu zenye dhambi na tabia zetu potovu za kishetani. Kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ni kazi mpya zaidi na muhimu zaidi iliyojengwa kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya kuokoa. Inamtakasa kabisa na kumwokoa mwanadamu kupitia hukumu ya ulimwengu, na inawaongoza watu hadi kwenye hatima nzuri.” Baadaye, walishiriki kwa subira kuhusu ukweli mwingi zaidi pamoja nami. Lakini bila kujali waliyoyasema, sikuweza tu kukubali kuwa Bwana alikuwa amerudi kuwahukumu wale waliomwamini. Nilipokuwa nikishughulikia ugomvi huu wa ndani, pia nilihisi kukanganyikiwa: Kina dada Gao na Liu walikuwa waumini wacha Mungu sana, na kila mtu alitambua imani yao na upendo wao kwa Bwana, kwa hivyo je, wangewezaje kuamini kwamba Bwana Yesu alikuwa akirudi kuwahukumu wale kati yetu ambao wanamwamini, na kwamba hangeweza kutuinua moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni? Je, kunaweza kuwa kwamba kulikuwa na siri au ukweli fulani katika swala hili ambalo sikujua?
Nilipokuwa nikiwaza, Dada Li Min alitoa kitabu na kuniambia kwa dhati, “Ndugu, Bwana Yesu alisema: ‘Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao’ (Mathayo 5:3). Usiamue jambo upesi bila kuzingatia swala nzima, sawa? Hebu kwanza tuone iwapo neno la Mwenyezi Mungu ni sauti ya Mungu, na iwapo linaweza kukimu maisha yetu, na iwapo linaweza kututakasa na kutuokoa, na kisha tutajua iwapo Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi au la. Naamini kwamba kondoo wa Mungu wataisikia sauti ya Mungu, kwa hivyo hebu tusome neno la Mungu pamoja!” Nilihisi kusita kidogo na sikumjibu. Dada hao watatu walihuzunika kidogo walipoona mtazamo wangu. Dada Liu alipendekeza ghafla: “Kwanza hebu tuombe, na kisha tusome neno la Mungu.” Dada hao watatu kisha walianza kuomba, na sikuwa na lingine la kufanya ila kuandamana nao. Hata hivyo, nilipokuwa nikiomba, sikuweza kuutuliza moyo wangu. Hata ingawa sikuweza kusikia kile ambacho kina dada hao walikuwa wakiomba kuhusu, niliguswa na jinsi walivyojiendesha. Mtazamo wao kwa Mungu ulikuwa wa kweli sana, na walitafuta mapenzi ya Mungu katika kila jambo. Walitumaini kuwa ningeweza kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na tumaini hili pia lilitokana na upendo wa Mungu. Baada ya kuomba, Dada Li alinipa kitabu na kuniambia kwa dhati, “Maswali mengi katika kitabu hiki, Maswali na Majibu Mia Moja Kuhusu Kuichunguza Njia ya Kweli, yanaulizwa miongoni mwa watu wa madhehebu yote. Vifungu husika vimechaguliwa kutoka katika neno la Mungu ili kujibu kila swali. Hebu kiangalie.” Sikutaka kukichukua kitabu hicho, lakini nilipoona jinsi alivyokuwa amezungumza kwa kweli, niliwatazama tena Dada Gao na Dada Liu, na nikaona kiasi walichokuwa wametumaini ningechunguza na kutafuta hiki. Nilifikiria jinsi kupokea ujio wa Bwana kulikuwa jambo muhimu, na kwamba sipaswi kulichukulia ovyo ovyo. Kwa hivyo, nilikikubali kitabu hicho na kusema, “Sawa, niko tayari kukikubali kitabu hiki. Tusikizungumzie tena leo. Nitakisoma kitabu hiki kwanza, na kisha tutazungumza zaidi.”
Baada ya kurudi nyumbani, nilikiweka kitabu hicho upande mmoja—akili yangu ilikuwa katika msukosuko. Nilifikiria kuhusu yale ambayo Dada Li Min alikuwa ameshiriki na yote yalionekana wazi na bayana kwangu. Kila kitu alichosema kilikuwa kweli, lakini kile ambacho sikukielewa kilikuwa ni kwa nini Bwana atekeleze kazi ya hukumu Atakaporudi? Nilitafakari kuhusu jambo hilo kwa makini, lakini bado sikuelewa. Kuhusu suala la ujio wa pili wa Bwana, hata hivyo, kwa kuwa nilikuwa sasa nimesikia kulihusu, sikuweza tu kufanya maamuzi yangu mwenyewe kulihusu pasipo kufikiria na kukaa nikiwa nimekubali hatima yangu. Nilifikiria lingekuwa wazo zuri kukisoma kitabu hicho kwa kukipitia na kuanza kuwa na utambuzi fulani. Kwa hivyo nilitumia muda wa siku sita nikisoma kitabu hicho chote. Niliona kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amefichua ukweli mwingi sana na siri nyingi sana ambazo sikuwa nimewahi kusikia kuhusu hapo awali na nilihimiliwa sana kwa kuzisoma. Pia, niliposoma maneno ya Mwenyezi Mungu, nilihisi kwamba kulikuwa na mambo mengi ambayo yalikuwa yamesemwa kwa sauti ile ile ya Bwana Yesu. Maneno hayo yalikuwa na mamlaka na nguvu, kana kwamba Mungu Mwenyewe alikuwa akizungumza. Na kwa hivyo, baada ya kumaliza kukisoma kitabu hicho, nilitaka kuelewa vyema zaidi kazi ya hukumu iliyofanywa na Mwenyezi Mungu ilihusu nini hasa, na niliamua kwenda kumtafuta Dada Gao ili nimuulize kuihusu.
Siku iliyofuata, nilienda nyumbani kwa Dada Gao, na ilitokea kuwa nilikutana na baadhi ya marafiki zake. Wote walikuwa wamekubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na walikuwa wakifanya mkutano na kushiriki wao kwa wao. Tulisalimiana, na papo hapo Dada Li Min aliniuliza moja kwa moja, “Ndugu, bado una mawazo gani? Je, ni kipengele kipi cha kazi ya Mungu ya siku za mwisho unachotaka kuelewa? Tunaweza kufanya ushirika pamoja.” Nilisema, “Ulisema kuwa kanisa limekuwa lenye ukiwa katika siku za mwisho kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu imehama. Ninaweza kulikubali hili, lakini sisi tunaomwamini Bwana tumesamehewa dhambi zetu tayari, na Bwana hatuoni kuwa wenye dhambi. Je, mbona Mungu bado anataka kutekeleza kazi ya hukumu? Je, hatutaweza kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni kama Mungu hatatekeleza hatua hii ya kazi? Mungu anapomhukumu mtu, je, mtu huyo basi hajalaaniwa? Je, lazima sote tuadhibiwe? Je, basi tutawezaje kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni?” Dada Li Min alisema, “Kulingana na maoni ya watu wengi, watu ambao Bwana aliyerudi anahukumu ni wasiomanini ambao hawamwamini Mungu. Wanaamini kuwa, kwa sababu Mungu anamhukumu mtu, mtu huyo basi analaaniwa na kuadhibiwa. Wanaamini kwamba wale wanaomwamini Bwana wamesamehewa dhambi zao, na kwamba Bwana atakapokuja, Atawainua moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni, na bila shaka hatawahukumu. Kwa hivyo wanakataa kupokea kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa kufanya hili, wanaelewa mapenzi ya Mungu visivyo kabisa na kuonyesha kwamba hawajui kazi ya Mungu. Kwa kweli, kazi ya Mungu katika siku za mwisho—ile ya kuonyesha ukweli na ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu—inatekelezwa hasa kwa ajili ya kuwainua waumini hadi katika ufalme wa mbinguni. Sote twajua Biblia inasema: ‘Lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu’ (1 Petro 4:17). Utabiri huu unatuambia waziwazi kwamba kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inaanza kwanza katika nyumba ya Mungu. Yaani, inaanza na wale watu ambao wanamwamini Mungu kwa mioyo ya kweli na kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Kwa hivyo, tunadhani kwamba kumwamini Bwana Yesu kunamaanisha kwamba hatuhitaji kukubali hukumu ya Mungu, lakini mtazamo huu si sahihi. Katika siku za mwisho, Mungu anatumia maneno Yake kuwahukumu wale wote ambao wamekuja mbele ya kiti Chake cha enzi, na Anawatakasa na kuwaokoa watu hawa, na kufanya kikundi cha watu kuwa washindi kabla ya majanga kuja. Baadaye, majanga makubwa yatakapokuja, Atatuza mema na kuadhibu mabaya. Hivi ndivyo kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho inaanza. Hakuna yeyote anayeweza kuikimbia kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, lakini kwa wale ambao wanakubali na kutii hukumu ya Mungu ni utakaso, wokovu, na ukamilifu. Kwa wale wanaokataa na kupinga kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, ingawa wanaweza kujificha kutoka kwa hukumu ya neno la Mungu, bado hawawezi kuikimbia hukumu ya majanga makubwa mwishowe. Huu ni ukweli! Sababu ya Mungu kutaka kutuhukumu katika siku za mwisho imeelezewa dhahiri shairi katika neno la Mwenyezi Mungu. Hebu tusome pamoja kifungu cha maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu anasema: ‘Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja’ (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho). Tunafahamu kutoka katika neno la Mungu kwamba kwa kumwamini Bwana Yesu tunasamehewa tu dhambi zetu. Hili halimaanishi kwamba hatutendi dhambi, wala kwamba hatuna dhambi. Kwa uhalisia, sote tunaishi katika mfuatano mbaya wa kutenda dhambi na kukiri, na bado tunahitaji Mungu aonyeshe maneno Yake ili Atuhukumu na kututakasa. Ni wakati tu ambapo tumetakaswa ndipo tutaweza kuwa wenye sifa zinazostahili ili kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Imeandikwa katika Biblia: ‘Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu’ (Walawi 11:44). ‘Utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana’ (Waebrania 12:14). Mungu ni mtakatifu. Watu wenye najisi na wapotovu wanaweza kukosa kuona uso wa Mungu na hawastahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Kazi ya ukombozi inayofanywa na Bwana Yesu ilitusamehe tu dhambi zetu, lakini haikutusamehe tabia zetu potovu na asili zenye dhambi. Kwa hivyo, tabia zetu potovu za kishetani bado zimebaki, kama zile za kuwa wenye kiburi na wenye majivuno, wasio waaminifu na wajanja, wenye ubinafsi na wenye kustahili dharau, waovu na walafi, wenye chuki kubwa kwa ukweli na wanaofurahia udhalimu. Tabia hizi potovu ndizo sababu ya kimsingi hasa inayotusababisha kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Kama hazitatatuliwa, tutatenda dhambi mara kwa mara, tutashindana sisi kwa sisi kwa ajili ya umaarufu na faida, tutajihusisha na ugomvi wa wivu, tutasema uongo na kulaghai, tutajiinua, tutakuwa na ushuhuda kwetu wenyewe, na mengine mengi. Hasa kazi ya Mungu isipokubaliana na mawazo yetu, bado tutategemea mawazo yetu na dhana zetu kumhukumu, kumkana, na kumlaani Mungu, na kupinga kazi ya Mungu. Je, watu kama hawa wanaompinga Mungu wanawezaje kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni? Mungu anaonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na lengo Lake kwa kufanya hivyo ni kututakasa kutokana na tabia zetu potovu na za kishetani na kutimiza ndoto zetu za kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Tunapokubali hukumu ya Mungu, kuacha tabia zetu potovu, na kutakaswa na kubadilishwa, basi tunakuwa wenye sifa zinazostahili ili kurithi ahadi ya Mungu na kuongozwa na Mungu hadi katika ufalme wa Mbinguni.”
Baada ya kusikiliza ushirika wa dada na neno la Mwenyezi Mungu, niliwaza: “Mtu anapomwamini Bwana, dhambi zake zinasamehewa, lakini hilo halimaanishi kwamba hatendi dhambi tena. Hili ni kweli kabisa! Kuangalia wale walio kanisani, kuanzia kwa wachungaji na wazee hadi tabaka la chini kwa washiriki wa kawaida, pamoja nami, kila mtu anaishi katika hali ambapo tunatenda dhambi mchana na kukiri dhambi zetu usiku, na hatuwezi kutoroka kutoka katika utumwa na udhibiti wa dhambi. Inaonekana kuwa watu bila shaka hawataweza kuona uso wa Bwana bila kwanza kuhukumiwa na kutakaswa na neno la Mungu. Mtu anapolisema kwa namna hiyo, ni lazima kabisa Mungu aje na kutekeleza kazi ya hukumu na utakaso wa mwanadamu! Hapo nyuma niliamini kwamba iwapo mtu angekuwa na imani katika Bwana Yesu, basi hakuhitaji kuhukumiwa. Nilidhani kuwa Bwana angekuja kuwahukumu wale ambao hawakumwamini. Sasa ninafahamu kuwa wazo hili halikubaliani na mapenzi ya Mungu hata kidogo, na kwamba ni suitafahamu.” Wakati huo tu, Dada Gao alinichezea video ya kuimba na kucheza kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu inayoitwa Furaha Katika Nchi ya Kanaani. “Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu kuingia katika Enzi ya Ufalme. Maneno Yake yananionyesha njia, na naielewa njia ninayopaswa kuchukua kama mtu. Nimenyunyiziwa na Mungu kwa maji yaishiyo ya uzima. Kuwa ana kwa ana na Yeye ni starehe, starehe isiyo na kifani. Sitafutitafuti tena, ndoto yangu ya ufalme wa mbinguni hatimaye imetimia” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo wote ulikuwa mchangamfu na wa kusisimua, na ulikuwa wa kutia moyo sana. Niliona kwamba uso wa kila ndungu katika video ulikuwa umejawa na furaha, na hatukuweza kujizuia kujiunga katika kuimba wimbo huo. Tulianza kudansi kufuatana na muziki na mioyo yetu ilijawa na furaha. Niliona kuwa ndugu waliokuwa na riziki ya neno la Mungu walikuwa wenye baraka na wenye furaha. Ingawa walikuwa wamepitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, bado hawakuwa na wasiwasi hata kidogo, lakini badala yake walikuwa wamekombolewa, huru, wenye shangwe, na wenye furaha. Niliwaza kuhusu jinsi imani na shauku yangu mwenyewe katika dini ilikuwa imepotea yote, na kile nilichoona tu kilikuwa ukiwa na giza la kanisa. Ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, kwa upande mwingine, walijawa na kazi ya Roho Mtakatifu. Nuru iliangaza kutoka katika ushirika wao kuhusu ukweli, walimsifu Mungu kwa nguvu, na walishuhudia kwa Mungu kwa msisimko mkubwa na nguvu kubwa. Kwa kulinganisha, walionekana wakiishi katika ulimwengu mwingine tofauti kabisa nami. Wakati huo huo, nilihisi kama yatima anayezurura ambaye alikuwa amerejea nyumbani na alikuwa akifurahia ukunjufu wa kumbatio la mama yake. Niliwaza: “Kwa kweli kuna ukweli unaopaswa kutafutwa hapa. Lazima nisikilize vizuri ushirika unaotolewa na kina ndugu kuhusu ukweli wa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ili nisikose nafasi yangu ya kupokea ujio wa Bwana na kuinuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni.”
Kufuatia hayo, Dada Li alitusomea vifungu viwili zaidi kutoka katika maneno ya Mungu: “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema, ‘Kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu?’ Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). “Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).
Dada Li alifanya ushirika kwetu, akisema, “Baada ya kupotoshwa na Shetani, sote tuliishi chini ya utawala wa Shetani na tukakuwa wapotovu waliompinga Mungu. Kulingana na asili ya Mungu yenye haki na takatifu, sote tulikuwa walengwa wa laana na maangamizo ya Mungu, lakini sio mapenzi ya Mungu kuwaangamiza wanadamu, lakini badala yake ni kuwaokoa wanadamu. Kwa hivyo, ili kuwaokoa watu kikamilifu kutoka kwa miliki ya Shetani, Mungu anaonyesha maneno Yake na kutekeleza kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu katika siku za mwisho. Kazi ya hukumu kwa kweli ni Mungu kutumia neno Lake kuweka wazi kiini, asili, hotuba na matendo ya watu ya uasi na ya kumpinga Mungu, ili watu waweze kuja kufahamu asili yao potovu na ukweli wa upotovu wao, watambue tabia ya Mungu ya haki na utakatifu, na kufanikisha kujichukia. Kisha, watu wanaweza kutubu na kubadilika kwa kweli, na wanaweza kuacha tabia zao potovu za kishetani na kupatwa na Mungu. Kwa njia hii, watu watapata wokovu kamili. Ni kupitia kwa hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu tu ndiyo tunaweza kuona kwamba tumejawa na upotovu, na kwamba nyakati zote na katika kila mahali, tunaonyesha tabia potovu kama ubinafsi, majisifu, udanganyifu, na ulafi, na kwamba tumejawa na mawazo na dhana, tamaa za kupita kiasi, na madai yasiyo na mantiki kuhusu Mungu, na kwamba hatuna dhamiri au mantiki, uaminifu au utiifu. Kadiri tunavyozidi kukubali hukumu ya Mungu, ndivyo tunavyozidi kutambua jinsi ambavyo tumepotoshwa sana na kwamba kweli hatuna utu. Tunaanza kuhisi kuchukizwa nasi wenyewe, na kujichukia mioyoni mwetu. Kadiri tunavyozidi kukubali hukumu ya Mungu, ndivyo tunavyozidi kuona utakatifu na haki ya Mungu, na ndivyo mioyo yetu inayvozidi kumtukuza Mungu. Tunakuwa tayari kuacha tamaa zetu za miili na kuishi kulingana na neno la Mungu. Baadaye, badiliko linatokea katika taswira zetu kuhusu mambo na katika tabia zetu potovu, na tunaanza kuishi kwa kudhihirisha mfano fulani wa mwanadamu wa kweli. Kisha tunakuja kutambua kwa kweli kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu ni upendo mkubwa na wokovu mkubwa wa Mungu kwetu. Bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, sote tungekuwa walengwa wa maangazimo.”
Dada huyo alimaliza ushirika wake hapa, na nilihisi nimeguswa sana na yale aliyosema na kuona jinsi upendo wa Mungu ulivyo mkubwa na wa kweli. Yeye ni Mungu anayewapenda wanadamu! Ni mimi ndiye nilikuwa nimeelewa visivyo nia nzuri ya Mungu ya kuwaokoa watu. Nilikuwa nimefikiria kuwa Mungu aliwahukumu watu ili kuwalaani na kuwaadhibu, na sikuwahi kufikiria kwamba Mungu kuonyesha neno Lake na kumhukumu mwanadamu katika siku za mwisho kungeweza kuwa hata upendo wa kweli zaidi, au kwamba kulikuwa hata wokovu mkubwa zaidi kwetu! Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu! Kupitia kusoma neno la Mwenyezi Mungu na kutoka kwa ushirika wa kina dada wale, nilipata ufahamu fulani wa kazi ya Mungu ya hukumu na suitafahamu yangu kuhusu Mungu iliondolewa. Nilikuja kuwa na imani thabiti kwamba Mwenyezi Mungu si mwingine ila Bwana Yesu aliyerudi, na nilikuwa tayari kukubali kazi ya hukumu. Nilikuwa nimeibuka kikamilifu kutoka katika hali ya mkanganyiko, na uso wangu ulijawa na tabasamu la furaha. Dada Li alisema kwa furaha: “Shukrani ziwe kwa Mungu kwa kukuongoza. Haya yote ni matokeo ya neno la Mungu. Kutokana na haya, tunaweza kuona kwamba, kabla hatujakuja kuelewa ukweli, ingawa mawazo kuhusu Mungu na kazi ya Mungu yanaweza kuibuka, mradi tu tuutafute na kuukubali ukweli, na kusikiliza neno la Mungu, basi tutaelewa ukweli na kuwa na ufahamu wa kazi ya Mungu, na mawazo yetu na dhana zetu zitaondolewa kama mawingu ya moshi. Kisha tutaweza kufahamu mapenzi ya Mungu na hatutamwelewa Mungu visivyo tena.” Niliamkia kwa kichwa kwa furaha na kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuniokoa.
Baada ya kukubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, nilisakinisha programu ya ujumbe katika simu yangu ili Dada Gao na wengine wangeweza kushiriki nami filamu za injili, video za muziki, na nyimbo kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilipotazama filamu ya injili kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu inayoitwa Kutoka kwa Kiti cha EnziHububujika Maji ya Uzima, ilikuwa na athari kubwa kwangu. Hali ya ukiwa wa kanisa katika filamu hiyo ilikuwa tu kama hali katika kanisa letu wenyewe, na filamu hiyo ilionyesha sababu ya kimsingi ya ukiwa huu kwa uwazi kamili. Kwa sababu kazi ya Mungu ilikuwa imehama, na Mungu hakuwa akifanya kazi tena ndani ya kanisa la kidini, watu ambao walikataa kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho wote walikuwa wakitaabika kwa njaa. Wale watu waliokubali neno la Mwenyezi Mungu walipata ruzuku ya maji ya uzima na hawakuwa na kiu tena, na waliishi maisha yaliyobarikiwa na Mungu. Nilipotazama filamu iitwayo Kusubiri, sikuweza kujizuia kushusha pumzi. Mchungaji mkongwe katika filamu hii alikuwa amemwamini Bwana maisha yake yote na alidhani kwamba bidii yake ilikuwa yenye kustahili pongezi. Alikuwa tu akimsubiri Mungu aje ili aweze kuinuliwa hadi mbinguni. Lakini alishikilia kwa ukaidi imani kwamba wakati Bwana angekuja angeshuka juu ya wingu na kumpa ufunuo kwanza. Kwa sababu ya ukaidi wake, alipinga na kukataa kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, kwa hiyvo mwishowe aliachwa akikodolea tu mbingu, akingojea wingu, na alifariki akiwa na majuto. Funzo hili la kuleta huzuni kwa kweli lilimpa mtazamaji kitu cha kutafakari! Wakati huo huo, nilishangilia moyoni mwangu na kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuniokoa, mtoto wa kiume mkaidi ambaye alitafuta tu kupata baraka kutoka Kwake lakini alisita kukubali hukumu na utakaso Wake, na kwa ajili ya kuniongoza hadi mbele ya kiti Chake cha enzi ili kupata wokovu Wake katika siku za mwisho.
Sasa ninaishi maisha ya kanisa katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kwa sababu ya kupitita kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, nimeanza kutambua polepole jinsi ilivyo halisi na ya utendaji kwa Mungu kutekeleza kazi ya hukumu. Mungu alipochangua asili danganyifu ya mwanadamu, nilihisi kwamba kwa sababu mimi mwenyewe sikuwahi kudanganya, kwa hivyo nilikataa kutambua hali halisi iliyofichuliwa na maneno ya Mungu. Nilipokabili hali ya utendaji ambayo Mungu alikuwa ameniandalia, niliropoka uwongo bila kujua ili kulinda masilahi yangu mwenyewe na kulinda majivuno yangu. Zaidi ya hayo, nilihisi udanganyifu na ulaghai moyoni mwangu, na pia nilikuwa na siri nyingi ambazo sikutaka zijulikane hadharani. Hili lilinisababisha nione kwamba kila kitu kilichofichuliwa na neno la Mungu ni ukweli na hali halisi, na kwamba ni asili na kiini cha mwanadamu. Hapo tu ndipo niliridhika na neno la Mungu, na nilikuwa na hamu ya haraka ya kutafuta ukweli na kubadilisha asili yangu mwenyewe danganyifu. Baada ya tukio hili, nilikuja kugundua kwamba kama haingekuwa kwa ajili ya hukumu ya utendaji na kuadibu kwa Mungu, singewahi kujua asili yangu mwenyewe danganyifu na singewahi kuweza kutenda kulingana na ukweli ili kubadilisha tabia yangu danganyifu. Hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa kweli vilikuwa vikinitakasa na kuniokoa, na kulikuwa aina tofauti ya upendo. Ninataka kutunza vizuri aina hii maalumu ya upendo na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, na ninataka kubadilika haraka iwezekanavyo kuwa mtu mpya ili niweze kumridhisha Mungu.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?