Vurugu Kutoka kwa Uvumi wa “Mei 28” (Sehemu ya 2)

30/05/2021

Xingwi, Ufaransa

Yaliyomo
Huku Nikitafuta Ukweli wa Mambo ya Hakika, Niliona Dhahiri Chanzo cha CCP Kusogeza Lawama kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu
Familia Yangu Ilijaribu Kunikomesha Kueneza Injili, Lakini Neno la Mungu Liliniongoza kwa Ushindi Dhidi ya Kuzingirwa na Shetani

Vurugu Kutoka kwa Uvumi wa “Mei 28” (Sehemu ya 2)

Huku Nikitafuta Ukweli wa Mambo ya Hakika, Niliona Dhahiri Chanzo cha CCP Kusogeza Lawama kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu

Baada ya hilo, sikujihadhari tena dhidi ya ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wowote nilipokuwa na muda ningesoma neno la Mungu na kutazama video, filamu, video za muziki, nyimbo, filamu za muziki na maonyesho mengine yaliyotolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kadiri nilivyozidi kutazama haya yote, ndivyo nilivyozidi kuhisi kupewa, na ndivyo nilivyozidi kuhisi raha. Nilidhibitisha kutoka kwa moyo wangu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kuonekana kwa Bwana Yesu. Sasa, hatimaye nilielewa kwa nini CCP na wachungaji na wazee kutoka dunia ya dini waliazisha uvumi kwamba “punde unapokubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho huwezi kutoka.” Kama inavyotukia, si kwamba huwezi kutoka, badala yake ni kwamba kazi ya Roho Mtakatifu na utoaji na mwongozo wa neno la Mungu yako katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, kwa hivyo kama unaweza kufurahia maji hai ya uzima ambayo Mungu anakupa, na kupata njia ya uzima wa milele, basi mbona utake kutoka? Sasa mimi pia siko tayari kutoka, aidha, nimeamua kumfuata Mwenyezi Mungu ifaavyo, na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu ili kupata wokovu na kuletwa na Mungu katika ufalme Wake. Kisha nikafikiri kuhusu jinsi dada zangu wakubwa bado walikuwa wakidanganywa na kufungwa na uvumi mbalimbali, wakikosa kufuata kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na nikawa na wasiwasi sana, hivyo niliwakusanya dada zangu wawili kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu pamoja ili kueneza injili kwao. Nilishangaa kwamba mume wake dada yangu mkubwa wa pili, ambaye ni muumini wa Kanisa la Nafsi Tatu, hangeniruhusu niwe karibu na dadangu, na hata alinikaripia kwa uso uliojaa hasira kali: “Nakuonya usije nyumbani kwetu kueneza injili! Huko nyumbani habari ya CCTV ilisam baza Kesi ya Mauaji ya Mei 28 ya Zhaoyuan, Shandong. Hili kweli halikupi wasiwasi? Kutoka sasa kwendelea, usitufanye tukutane na watu kutoka Umeme wa Mashariki, na hakika usiwalete nyumbani kwetu.” Niliweza kuona kwamba mume wa dadangu hakuona ukweli wa mambo yaliyokuwa ya hakika na kuwa alikuwa amedanganywa na uvumi, jambo lililonifanya kuwa na wasiwasi sana, lakini sikujua jinsi ya kumshawishi kusikiza. Baadaye, wakati ambapo mume wangu pia alijua kuwa nilikuwa nimekubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, alifanya hata juhudi zaidi kunikomesha, na hata angeenda mtandaoni daima kutafuta video kuhusu Kesi ya Mauaji ya Mei 28 ya Zhaoyuan na kunifanya nizitazame. Nilipoona kuwa familia yangu na jamaa wengine waliendelea kudanganywa na Kesi ya Mei 28 ya Zhoyuan na hawakutaka kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho, nilihisi huzuni sana. Na, kwa sababu kimo changu ni kidogo, wakati wowote ambapo wanafamilia wangu walinijia kwa nguvu, sikujua jinsi ya kukanusha na kufichua uongo wa CCP; kinyume chake nilihisi kama nilikuwa mhasi na dhaifu. Wakati huo huo nilihisi kukanganywa ndani: Kwa nini CCP kililaumu Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Mauaji ya Zhaoyuan ya Mei 28? Ukweli wa hakika wa siri ya kufanya hili ulikuwa upi?

Punde ndugu walzipojua kuhusu hali yangu walikuja kunisaidia na kunihimili. Niliwaambia: “Naamini kwamba Mwenyezi Mungu ni kuonekana kwa Bwana Yesu, kwamba Yeye ndiye Kristo mwenye mwili katika siku za mwisho, kwamba maneno yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yote ni ukweli, na nina hakika kwamba uvumi huo si ukweli. Lakini kuna jambo moja ambalo silielewi. Kwa nini CCP kiliripoti kwa habari ya CCTV kwamba Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 ilisababishwa na Kanisa la Mwenyezi Mungu? Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 ni nini kweli? Tafadhali mnaweza kushiriki kuhusu hili nami?”

Ndugu Chen alisema: “Mshukuru Mungu! Umeuliza swali zuri sana. Tusipotambua ukweli wa uvumi huo, basi tutadanganywa kwa urahisi na uongo na upuuzi wa CCP, kuathiriwa na hila za Shetani, kumkana Mungu na kumsaliti Mungu, na kukosa kupata wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Ni kwa kuelewa ukweli wa mambo ya hakika pekee huku tukiweza kutambua nia bovu za wanaoanzisha uvumi kwa wakati ule ule ndio tutaweza kufanya uchaguzi wa busara na kutodanganywa na Shetani. Acha tuanze kwa kuzungumza kuhusu kile kilichofanyika kwa kweli katika Kesi ya Mauaji ya McDonald huko Zhaoyuan, Shandong. Mnamo Mei 28, 2014, katika mkahawa wa McDonald huko Zhaoyuan, Shandong, Zhang Lidong na washukiwa wengine kadhaa walimchapa mwanamke hadi kufa, na baada ya siku tatu tu kutoka wakati kesi ya jinai ilipoanza, mbele ya mahakama ya sheria na kuhukumu kesi hiyo, CCTY, msemaji wa vyombo vya habari vya CCP, iliripoti hadharani kuhusu na kuamua asili ya kesi hii, ikilishutumu Kanisa la Mwenyezi Mungu moja kwa moja. Acha tufikirie kuhusu hili, je, vyombo vya habari vinaweza kuhukumu kesi na kufikia uamuzi? Jambo hili ni la busara na linafuata sheria? Kuna kiwango cha kusadikika katika matokeo kama hayo? Baadaye, wakati washukiwa kadhaa wa jinai walipohojiwa na vyombo vya habari, wote walisema tena na tena kwamba hawakuwa washirika wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, wala hawakuwahi kuwasiliana na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Mnamo Agosti 21, 2014, wakati ambapo daawa ya umma ya kesi hiyo ilianza, Lü Yingchun, mmoja wa wakosaji, pia alisema wazi: “Mimi na Zhang Fan ni wasemaji wa pekee wa “Mwenyezi Mungu” wa kweli. Serikali imekuwa ikichukulia hatua kali Mwenyezi Mungu wa Zhao Weishan, sio “Mwenyezi Mungu” wetu. Hili linatosha kuonyesha kwamba hawa washukiwa wa jinai hawashirikishwi kwa njia yoyote na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, majaji wa CCP hawakukubali ushuhuda huu kutoka kwa hao washukiwa wa jinai, na wakasisitiza kusema kwamba walikuwa washirika wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Aidha, wakosaji Zhang Fan na Lü Yingchun walidai kuwa “Mungu,” na kusema mambo kama jinsi wao ni miili mbili inayoshiriki nafsi moja, kwamba ndani ya muda wa dakika chache waliweza kuamua kwamba mwathitriwa alikuwa roho ovu na kwamba iliwabidi wamchape hadi kufa. Na washukiwa wale wengine wote waliamini mambo haya kwa thabiti bila shaka. Ushuhuda ambao kundi hili la watu liliwapa mahakama ulikuwa usioeleweka, na ulikuwa upuuzi, na kwa wazi wale waliodai kuwa ‘Mungu’ na wale waliofuata hawakuwa na akili na urazini wa binadamu wa kawaida, walikuwa kundi la wagonjwa wa akili.

“Katika “Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii,’ Mwenyezi Mungu anasema wazi kwamba: ‘Mwanadamu hapaswi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.’ Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, Muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vilivyoko ndani yake, na hakuna mwanadamu anayeweza kuchukua nafasi Yake au kujifanya kuwa Yeye. Lakini Zhang Lidong na kundi lake hawakuwa na Mungu mioyoni mwao, mioyo yao haikuwa na uchaji hata kidogo wa Mungu. Hata walifika kiwango cha kumwua mtu katika mahali palipojaa pa umma huku wakithubutu kujifanya kuwa Mungu Mwenyewe. Hawa kwa wazi ni watu ambao wamepoteza dhamiri na mantiki ya binadamu wa kawaida, na kwa wazi wao wenyewe wamepagawa na roho waovu. Kanuni za kiinjilisti za Kanisa la Mwenyezi Mungu zaelezea wazi kwamba hakuna yeyote anayeruhusiwa kuhubiri kwa wale walio na kazi ya roho waovu na ambao wamepagawa na roho waovu. Hata hakuna sababu ya kuongea kuhusu wao kuingizwa katika kanisa—jambo hili linajulikana na kila mtu! Hivyo, wale wote wanaotambua kiasi wanaweza kuona kwamba Kesi ya Shandong Zhaoyuan ni kesi ya kisheria iliyobuniwa na CCP ili kusingizia, kulilaumu na kulipunguzia sifa Kanisa la Mwenyezi Mungu.”

Hatimaye niliweza kuwa na utambuzi kiasi kuhusu kilichofanyika katika Kesi ya Zhaoduang ya Mei 28 baada ya kusikiza ushirika wa Ndugu Chen. Ilitokea kuwa njama iliyobuniwa na mikono ya CCP. Niliona jinsi CCP kilivyokuwa katili na kisicho na aibu kweli; kilifika kiwango cha kubuni kesi ya sheria ili kuunda mashtaka ya uongo dhidi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, na bila haya kuwadanganya na kuwapumbaza watu wa China na watu duniani kote! Ni kiovu sana!

Dada Liu aliendelea kushiriki, akisema: “Sasa kwa nini CCP bila haya kitake kusingizia na kulilaumu Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Kesi ya Mauaji huko Zhaoyuan? Sote tunajua kwamba CCP ni chama cha kisiasa kinachomkana Mungu, kwamba kinauchukia ukweli na kumchukia Mungu, kwamba tangu kije mamlakani daima kimekandamiza na kutesa imani ya dini kwa hasira, kwamba ili kupiga marufuku imani ya dini kabisa kimeupachika jina Ukristo kama dhehebu ovu na Biblia Takatifu kama kazi ya dhehebu ovu, na kwamba kimewakamata, kuwakandamiza na kuwatesa Wakristo kwa wayowayo. Huu ni ukweli ambao mtu yeyote anaweza kuuona! Sasa Mungu amekuja tena katika mwili kuonekana Uchina kutekeleza kazi Yake; yaani, Mwenyezi Mungu anatekeleza kazi ya maneno ili kumhukumu mwanadamu, kumtakasa mwanadamu na kumwokoa mwanadamu. Maneno yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu tayari yamechapishwa mtandaoni, ili watu kutoka mataifa yote na nchi zote watafute na kuchunguza. Ndugu kutoka kila madhehebu na vikundi wanaomwamini Mungu kwa kweli na hata wengi wasioamini, baada ya kusoma neno la Mwenyezi Mungu, wote wanatambua kwamba ni ukweli, kwamba ni sauti ya Mungu, na mmoja baada ya mwingine wanarudi mbele ya Mwenyezi Mungu. CCP, kwa kuona injili ya Mwenyezi Mungu ya ufalme ikienea na kusitawi hivi, kinashtuka sana na kuwa na wasiwasi. Kinaogopa watu kusoma neno la Mwenyezi Mungu, kwa sababu mara watu wanapotambua ukweli wataona kwa wazi kiini cha shetani na kiovu cha CCP cha kuidanganya na kuipotosha jamii ya binadamu na kumpinga Mungu, na watakitelekeza na kukisaliti, hivyo kuja mbele ya Mungu, na kwa njia hii hawatakiamini CCP tena au kukifuata. Ili kulinda utawala wake wa kidikteta, ili kuwa na uthibiti wa milele juu ya watu wa Kichina, na kuimarisha Uchina kama eneo linalomkana Mungu, CCP kimetumia Kesi ya Zhaoyuan ya Mei 28 kuunda wasiwasi wa umma ili kuleta mashtaka ya uongo dhidi ya na kulipunguzia sifa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kwa upande mmoja, hili linawadanganya wale watu wasioelewa ukweli, na huleta suitafahamu na nia mbaya kuelekea kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa umma, kuwasababisha kulichukia Kanisa la Mwenyezi Mungu na wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu, kuwaf anya wasithubutu kutafuta na kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho; kwa upande mwingine, hili linakipa CCP kisingizio cha maana na kuongeza maoni ya umma ya chama hicho kukandamiza na kupiga marufuku Kanisa la Mwenyezi Mungu katika siku za baadaye. Kama anavyojua kila mtu, CCP, kabla ya kuikandamiza imani ya dini, walio wachache wa kabila au wanafunzi wa chuo kikuu, kitaunda tukio katili au kubuni mashtaka ya uongo dhidi ya vikundi hivi, na kisha kitawakandamiza kwa nguvu za kijeshi. Chukua mfano wa tapo ya wanafunzi ya Juni 4. CCP kwanza kiliwachochea wachochezi fulani kuchanganyika na wanafunzi, ili kuanzisha mapigano na vurugu, kisha kikabuni uongo na kubuni kesi za sheria ili kuhamisha lawama kwa wanafunzi hao wa chuo kikuu, na baada ya hilo kikatumia nguvu kuwakandamiza. Hii ni mbinu ambayo CCP kinachukua daima ili kuwaondoa wapinzani na kulinda utawala wake wa kidikteta. Kulipokuwa na malalamiko ya umma ya watu wa Tibet CCP kilifuata mkondo huu huu, na ilikuwa vivyo hivyo na Kesi ya Zhaoyuan. Hivyo, tukiona wazi uso mbaya wa kishetani na katili wa CCP na nia yake ye makusudi katika kuanzisha uvumi, hatutaamini uvumi wa CCP, au kudanganywa nacho, au kuathiriwa na hila zake.”

Vurugu Kutoka kwa Uvumi wa “Mei 28” (Sehemu ya 2)

Baada ya kusikiza ushirika kutoka kwa ndugu niligundua ghafla: Ilikuwa CCP ambacho muda huu wote kilikuwa kikitumia msemaji wake wa vyombo vya habari kueneza uvumi, na kilifanya hili ili kukandamiza na kutesa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kutudanganya na kutuzuia kuichunguza njia ya kweli na kumrudia Mungu. CCP, ili kuimarisha nguvu zake na kulinda maslahi yake, ili kutimiza lengo lake la kuwadhibiti watu milele, kweli kilitumia hila kilizokuwa nazo, kwa kweli ni kidanganyifu na kiovu sana! Isingalikuwa ushirika wa ndugu hawa nisingaliweza kuona ukweli wa mambo haya ya hakika, bado ningedanganywa na uvumi huu. Nilifikiri nyuma kwa jinsi zamani niliuamini uvumi ulioenezwa bila kufikiri kwa sababu sikuelewa ukweli wa mambo haya ya hakika, jinsi nilivyouchukua uvumi na kusisitiza kwamba yalikuwa mambo ya hakika, na jinsi hata nilivyohudumu kama mtumishi wa Shetani ambaye mara kwa mara alijaribu kumkomesha mamangu kumwamini Mwenyezi Mungu. Kweli nilimwasi Mungu sana! Nilikuwa na haya kuonyesha uso wangu mbele ya ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na hata zaidi sikustahili kuja mbele ya Mungu. Kweli nilitaka tu kuuficha uso wangu mchangani. Nikikumbuka wakati huo, nilishangaa jinsi nilikuwa mpumbavu hivyo. Nilipagaliwa vipi kuamini uvumi wa CCP, bila kutafuta kuisikia sauti ya Mungu? Sikuweza kujizuia machozi ya majuto kutiririka kwa mashavu yangu, niliinama mbele ya Mungu na kuomba: “Mwenyezi Mungu, zamani nilikuwa mjinga na asiyejua na sikutambua vitu, bila kufikiri niliamini uvumi na kumfuata Shetani katika kukupinga, na hata niliufungia mlango wokovu Wako tena na tena, kweli nilikuwa asiyefikiri kabisa! Isingalikuwa rehema Yako na Usingaliwasisimua ndugu hawa kunihubiria mara kwa mara, basi ningepoteza wokovu huu mkubwa. Ewe Mungu, kutoka sasa kuendelea niko tayari kushirikiana na Wewe katika kueneza injili, kuwaleta wale wanaoishi gizani na ambao wamedanganywa na uvumi Kwako, ili niweze kulipiza upendo Wako mkubwa. Haijalishi ni aina gani ya mateso na majaribu naweza kukabili, nimedhamiria kukufuata, sitavutwa!”

Familia Yangu Ilijaribu Kunikomesha Kueneza Injili, Lakini Neno la Mungu Liliniongoza kwa Ushindi Dhidi ya Kuzingirwa na Shetani

Baadaye nilipokuwa nikieneza injili kwa dada zangu wawili, nilikutaka na kizuizi kikubwa sana. Kwa kuwa mume wa dadangu alikuwa amedanganywa kwa kina na uvumi wa CCP, hakukataa kuniruhusu kumpa dadangu ushuhuda wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho pekee, lakini pia alisema mambo mengi ya kuchukiza ili kunishambulia na kutisha kuvunja uhusiano wetu wa kifamilia. Kwa kuwa mume wangu aliamini uvumi na uongo wa CCP, kunitesa kwake mimi pia kuliendelea kuongezeka. Hangepigana nami nyumbani pekee, lakini angenifuata kisiri, na hata kutumia kila aina ya mbinu kunitesa na kunitisha, akisema kwamba kama ningeendelea kumwamini Mungu basi angeniripoti kwa ubalozi. Kwa kukabiliwa na vizuizi na mateso kama haya, nilikuja kukichukia CCP kwa ukali, kwani daima kilikuwa ndicho kilianza uvumi kusingizia na kupunguza sifa za Kanisa la Mwenyezi Mungu, jambo lililosababisha wanajamii wangu kudanganywa hadi kiwango ambacho walijaribu kunikomesha na kunitesa kwa njia hii. Nilitaka kupaza sauti ya juu sana: “Mimi ni mtu tu anayemwamini Mungu na anayetembea katika njia sahihi ya maisha, mbona hili ni gumu sana!” Wakati wangu wa mateso na udhaifu, nilifikiri kuhusu maneno ya Bwana Yesu ambapo linasema: “Mmebarikiwa ninyi wakati wanadamu watakapowalaani, na kuwatesa, na kusema kila aina ya uovu dhidi yenu kwa udanganyifu, Shangilieni kwa sababu yangu(Mat 5:11). Neno la Mungu liliniwezesha kutambua kwamba wale wanaoteswa katika jina la haki wamebarikiwa. Ni jambo la baraka kwamba ninashutumiwa na kuteswa leo kwa sababu ya imani yangu kwa Mungu, sipaswi kuhuzunika kwa sababu ya mateso haya, yanapaswa kunifanya niwe na furaha, kwa sababu kuna thamani na maana katika hili, na linasifiwa na Mungu kuvumilia mateso kama haya. Baadaye, ndugu wengine kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu walinipa neno zaidi la Mwenyezi Mungu nilisome, na pia filamu na video nyingine kuhusu ndugu kuwa na ushuhuda wanapopitia mateso na majaribu, na kwa kufanya hili, walinihimili na kuniliwaza, na kuniwezesha kuyafahamu mapenzi ya Mungu. Nilisoma neno la Mwenyezi Mungu ambapo linasema: “Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita” (“Kumpenda Mungu Tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Futa machozi yako, na usihisi uchungu au huzuni tena. Vitu vyote vimepangwa na mikono Yangu, na lengo Langu ni kuwafanya ninyi muwe washindi na kuwaleta katika utukufu pamoja na Mimi. Kwa yote yanayokutendekea, unapaswa kushukuru sawasawa na uwe uliyejawa na sifa; hilo litanifanya Niridhike sana. … Kuwa mwaminifu Kwangu bila kujali chochote, na usonge mbele kwa ujasiri; Mimi ni mwamba wako wa nguvu, kwa hivyo Nitegemee Mimi!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). Mwongozo wa maneno ya Mungu ulinifanya niyaelewe mapenzi ya Mungu. Kwa kweli, hali niliyomo ndani inaonekana kwa nje kuwa familia yangu ikinizuia kumwamini Mungu na kuieneza injili, lakini, kwa kisiri, ni Shetani ambaye anatengeneza vurugu hiyo. Ni vita katika dunia ya roho. Shetani anataka kunifanya kuwa hasi na dhaifu kupitia uvumi na mateso ya familia yangu, na anataka nipoteze imani yangu na kumwacha Mungu na kumsaliti Mungu, lakini ni mapenzi ya Mungu kunijaribu kupitia hali ya aina hii, kuona iwapo naweza kuangalia vitu kulingana na neno la Mungu au la, kubaini hila za Shetani, na kukita mizizi na kusimama imara katika njia ya kweli. Ingawa kimo changu ni kidogo na kuna ukweli mwingi ambao siuelewi, siwezi kujikunyata kwa sababu ya mambo haya. Mungu hutawala kila kitu, mambo yote na viumbe wote wamo mikononi mwa Mungu. Almradi nina msaada wa Mungu sina chochote cha kuogopa, bila kujali jinsi mume wangu anavyoendelea kunitisha kwa kweli hawezi kunidhuru kama halijakubaliwa na Mungu. Lazima nisiathiriwe na hila za Shetani hata kidogo. Lazima nimtegemee Mwenyezi Mungu kwa dhati na kuishi kwa kutegemea neno la Mungu, na naamini Mungu hakika ataniongoza hadi kwa ushindi dhidi ya kuzingirwa na Shetani. Kwa hivyo nilimwomba Mungu: “Ee Mwenyezi Mungu, nakupa shukrani zangu na sifa yangu! Ingawa hali hii niliyomo ndani sasa haikubaliani na dhana zangu, ninashawishika kwamba mapenzi Yako mema yako ndani yake; ingawa nimeteseka sana na nahisi dhaifu, niko tayari kushirikiana na Wewe na kushikilia imani yangu Kwako, niko tayari kuwa na ushuhuda na kumwaibisha Shetani nikiwa nimekabiliwa na mateso, kwa ajili Yako nitakuwa na ushuhuda mkubwa ili kuuliwaza moyo Wako!” Baada ya kuomba, nilihisi nguvu kubwa ndani yangu, na nikahisi mwenye imani katika kukabiliana na vichocheo na kuzingirwa na Shetani. Baadaye, wakati ambapo mume wangu alikuwa akitumia uvumi mara nyingine ili kujaribu kunidanganya, nilimwambia kwa sauti jasiri na ya haki: “Unaweza kuendelea kuniambia mambo haya mara elfu kumi na bado itakuwa bure; hata ukinifunika kwa uvumi, usidhani kwamba nitadanganyika.”

Baada ya kupitia vurugu hizi, niliona kwamba kwa asili huu uvumi ulikuwa uongo, kwamba ulikuwa mashimo na mitego iliyowekwa na Shetani kwa ajili ya mwanadamu, na kwamba ulikuwa sumu unaomdanganya mwanadamu, chanzo cha familia yangu kutenganishwa, na kikwazo katika njia yangu kumrudia Mungu. Siku hizi naona ukweli, ninaridhika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kuonekana kwa Bwana Yesu, na sitaamini uvumi tena, wala sitadanganywa na kudhibitiwa nao. Nikiwa nimesimama thabiti katika ushuhuda wangu, niliona matendo ya Mungu ya ajabu, kwa sababu baada ya muda, nilipokuwa nikieneza injili kwa dada yangu mkubwa wa pili, mume wangu aliacha kujaribu kunizuia, na hata alinipeleka kwa nyumba yake kwa gari. Baada ya yeye kusikiza neno la Mungu, pia aligundua kwamba ilikuwa sauti ya Mungu, na akawa tayari kutafuta na kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, na hata alimwita dada yetu mkubwa kabisa kupanga mkutano ili tukusanyike kuchunguza na kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Nilipokuwa nikiangalia yote yaliyofanyika, nilimshukuru Mungu kwa dhati, kwani Mungu aliniongoza nilipokuwa nikipitia siku zangu za shida kabisa na kutuleta Kwake, tukipokea wokovu Wake katika siku za mwisho. Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu! Amina!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp