Kusadiki Uvumi Kunamaanisha Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho

17/01/2021

Ndugu wengi hawana uwezo wa kutilia maanani wakati wowote wanapomsikia mtu akizungumza kuhusu injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na hawathubutu kukubali kile kinachohubiriwa kwa sababu wametishiwa na uvumi na mihemko iliyobuniwa katikati ya jamii za kidini. Wanaweza kumsikia mtu akisema: “Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu ni wa ajabu kweli—utadanganywa punde utakapowasiliana nao. Kuna waumini wengi wa kweli kutoka katika kila dhehebu ambao ni kondoo wazuri na hata viongozi wenye ubora mzuri wa tabia, lakini wanaibiwa na wanaomwamini Mwenyezi Mungu...” Au wengine wamesema: “Wanaomwamini Mwenyezi Mungu kweli ni wenye shauku kuhusu kueneza injili. Wakimbadilisha muumini dini wanapata zawadi ya RMB 2,000, wakimbadilisha kiongozi wa kanisa dini wanaweza kupata RMB 10,000 hadi 20,000....” Na hata wengine wamesema: “Hawadumishi mipaka mizuri kati ya wanaume na wanawake—wote ni wazinzi....” Wengine hata wamesema: “Umeme wa Mashariki ni shirika halifu la watu waovu. Ukijihusisha nao, hutawahi kukwepa. Ukijaribu, watang’oa macho yako na kukata masikio yako, au watavunja miguu yako....” na kadhalika. Ni uvumi kama huu unaowazuia ndugu wengine ambao hawana uhakika kuhusu ukweli kutokana na kuitafuta na kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Ndugu mnaouamini uvumi huu, je, mmezingatia au kuchunguza kwa bidii iwapo kuna msingi wowote wa mambo haya, na kama yanaambatana na ukweli? Mmewahi kufikiri kuhusu kutakuwa na matokeo gani mabaya mkiamini uvumi wote mnaosikia bila kufikiria na kupoteza fursa ya kukaribisha kuwasili kwa Bwana? Kwa sasa, kwanza tutakuwa na ushirika wa kawaida kuhusu uvumi huu ili ndugu zetu waweze kuona asili yao kwa wazi, na kuwa na utambuzi dhahiri kuhusu ni nani ambaye kweli anaueneza, sababu za yeye kuzibuni ni zipi, na ni lengo gani analotaka kutimiza.

Uvumi unasema: “Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu kweli ni wa ajabu—utadanganywa punde utakapowasiliana nao. Kuna waumini wengi wa kweli kutoka katika kila dhehebu ambao ni kondoo wazuri na hata viongozi wa ubora mzuri wa tabia, lakini wanaibiwa na wanaomwamini Mwenyezi Mungu.…” Leo, waumini wengi wa Mwenyezi Mungu kweli wanatoka katika madhehebu mengi tofauti na miongoni mwao, wengi ni wale kutoka katika madhehebu yao ambao wana ubora wa tabia, umaizi, na ni wanaotafuta kwa kujitolea, lakini kusema kwamba wote wamedanganywa ni kashfa mbovu tupu kabisa. Lifikirie jambo hili: Je, watu wengi sana wenye kumcha Mungu wanaotoka katika madhehebu mbalimbali wangeweza kudanganywa kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Inaleta maana kwamba wangekuwa waumini kwa miaka mingi sana na kuijua Biblia vizuri bila kuwa na utambuzi kiasi? Hata kama watu wanadanganywa, wangekuwa tu wale ambao hawatafuti pekee, wale wanaokula mikate na wanashiba, na wale waliokanganywa katika imani yao. Inawezekanaje hata kwamba watu wengi sana wanaotafuta na watu wengi sana wenye imani ya kweli katika Mungu wamedanganywa? Kama kila mtu anavyojua, ilitabiriwa katika Biblia kitambo kwamba Mungu angekuja katika siku za mwisho “kama mwizi” “kuiba” hazina, kwamba “Angeiba” wale ambao ni “hazina.” Hii inamaanisha kwamba wale wote ambao “wanaibiwa” ni wenye ubora mzuri wa tabia, wanaweza kuuelewa na kuukubali ukweli, na kuijua sauti ya Mungu. Wale wote ambao “wameibiwa” ni kondoo wazuri na kurudi kwa Bwana ni kwa ajili ya kuwaokoa na kuwakamilisha. Ni dhahiri kwamba “kuibiwa” kweli ni kunyakuliwa ili kukutana na Bwana. Wale kutoka madhehebu tofauti wenye imani ya kweli katika Bwana huyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na huona kwamba Amefunua siri za mpango wa Mungu wa usimamizi wa kuwaokoa wanadamu na vile vile uhusiano kati ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, Enzi ya Ufalme (hatua tatu za kazi ya Mungu), ukweli na maelezo ya ndani ya Biblia, umuhimu wa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, jinsi Mungu huwaainisha watu kulingana na aina zao na kuamua matokeo yao, na hatimaye jinsi Mungu atakavyohitimisha enzi na jinsi ufalme wa Kristo utakavyofanikishwa. Wakishaona haya, wanaweza kuthibitisha mioyoni mwao kwamba hii ni sauti ya Mungu, na kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni yale yaliyotabiriwa mara nyingi katika Ufunuo: “ambayo makanisa yaliambiwa na Roho.” Yote ni ukweli, na wametambua kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi na hivyo wamemgeukia, mmoja baada ya mwingine. Isingekuwa kuonekana na kazi ya Mungu, ni nani mwingine angekuwa na mamlaka na uwezo wa kuwashinda ndugu kutoka katika madhehebu yote na kufanya imani zote kuwa moja? Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu, ambaye Amerudi na hufanya kazi katika siku za mwisho, ndio wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli wameisikia sauti ya Mungu na kuona kuonekana kwa Mungu na hivyo wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Ni nani asingetaka kuwa bikira mwenye hekima na kufuata nyayo za Mwanakondoo? Hii ndiyo sababu wengi sana wanaotafuta kutoka katika madhehebu tofauti wameikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Wazo kwamba watu ambao wameikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho wamedanganywa ni uongo mtupu wa wazi, linakashifu, na linamkufuru Mungu.

Watu wengine wamesema: “Wanaomwamini Mwenyezi Mungu kweli ni wenye shauku kuhusu kueneza injili. Wakimbadilisha muumini imani wanapata zawadi ya RMB 2,000, wakimbadilisha kiongozi wa kanisa imani wanaweza kupata RMB 10,000 hadi 20,000.…” Ndani ya uongo huu, kumetajwa kwamba wanaomwamini Mwenyezi Mungu ni wenye shauku sana kuhusu kuieneza injili ya Mwenyezi Mungu. Ingawa sehemu hii ni yenye ukweli hasa, zingine kuhusu kuhongwa kwa pesa ili kueneza injili Yake na kuhusu shauku yao kusababishwa na manufaa ya mtu binafsi, ni upuuzi uliobuniwa kabisa na uvumi unaokashifu. Ukweli ni kwamba, wanaomwamini Mwenyezi Mungu wanaoieneza injili Yake hawapokei tuzo ya aina yoyote. Kinyume na hayo, wanatumia akiba zao wenyewe ili kufanya hivyo, na wakati mwingine yote waliyo nayo. Sababu ya wao kuwa na shauku sana si kwa sababu wanahongwa kwa pesa, badala yake, ni kwa sababu wameuelewa ukweli kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu, kweli wameona kuonekana kwa Mungu, wameupokea wokovu Wake mkubwa, kupitia upendo wa Mungu, na kuhisi hamu ya Mungu ya kuwaokoa watu. Kwa hiyo, wako tayari kutumia yote waliyo nayo na kuvumilia taabu au fedheha yoyote ili kueneza injili ya ufalme wa Mungu. Wao ni kama wanafunzi wa awali wa Bwana Yesu Kristo, walioisikia sauti ya Mungu kupitia kazi na maneno ya Yesu, walitambua kwamba Bwana Yesu alikuwa Masiya ambaye walikuwa wakimsubiri, na kuona kwamba Alikuwa tayari kujitoa mhanga ili kuwaokoa wanadamu, kusulubiwa. Upendo wa Mungu ni mkuu sana, halisi sana! Wakiwa wameguswa na Roho Mtakatifu, kuhimizwa na upendo wa Mungu, walikuwa tayari kuacha nyumba na kazi zao na kustahamili kila aina za ukandamizaji na ugumu ili kuieneza habari, kumshuhudia Bwana. Ni kweli! Pengine ndugu wengine wameona na kusikia ni aina gani ya “fidia” wanaomwamini Mwenyezi Mungu hupata wanapoeneza injili: Wengine wanafedheheshwa, wengine wanapigwa kwa rungu, wengine wanafukuzwa, na wengine wamehukumiwa na kutiwa gerezani mikononi mwa wale walio mamlakani, wanapitia kila aina ya mateso.... Namhimiza kila mtu kuzingatia hili: Nani angekubali laana, mapigo, na fedheha kwa hiari ili kueneza injili ya Mungu ya siku za mwisho isingekuwa kwa ajili ya upendo mkuu wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu? Nani angejihatarisha kufungwa gerezani na hata maisha yake ili kueneza injili ya wokovu wa Mungu katika siku za mwisho isingekuwa kwa ajili ya kazi ya Mungu? Hivyo “Wakimbadilisha imani muumini wanapata zawadi ya RMB 2,000, wakimbadilisha imani kiongozi wa kanisa wanapata RMB 10,000 hadi 20,000” ni uongo tu, ubunifu mtupu.

Bado kuna wengine ambao wamesema: “Hawadumishi mipaka mizuri kati ya wanaume na wanawake—wote ni wazinzi sana....” Kuhusu hoja hii, hebu tuangalie maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mimi ndimi Mungu mtakatifu Mwenyewe, Siwezi kuchafuliwa, na Siwezi kumiliki hekalu najisi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 109). Na kanuni ni dhahiri sana katika “Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii”: “Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu bila kuwepo na mtu mwingine. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili.” Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba tabia ya Mungu ni takatifu na yenye haki na haivumilii kosa lolote kutoka kwa wanadamu. Haishi katika hekalu chafu. Mungu hamtaki mtu yeyote anayeshiriki katika tabia ya fujofujo. Lazima kila mfuasi wa Mwenyezi Mungu azishike amri za utawala za Mungu, au ataondolewa kutoka kwa kanisa—hakuna atakayeepuka. Aidha, ndugu ambao wanamwamini Mwenyezi Mungu kimsingi wametoka kwa wale wanaotafuta kwa kweli kutoka madhehebu mbalimbali; wengine wao ni viongozi na wafanyakazi wenza kutoka madhehebu tofauti. Wanajua kutoka Enzi ya Neema kwamba Mungu ni Mungu mwenye wivu na huchukia tabia ya fujofujo. Daima wamedumisha amri za Bwana Yesu, jambo ambalo watu wanaomcha Mungu kwa kweli wamekuwa wakifanya sikuzote. Je, mtu kama huyu angekiuka amri za utawala za Enzi ya Ufalme leo kwa makusudi? Kwa hiyo mnaweza kuona, chanzo cha uvumi huu ni cha upuuzi kabisa na kimenuiwa kuwapaka watu matope kabisa.

Watu wengine wamesema kwamba “Umeme wa Mashariki ni shirika halifu la watu waovu. Ukijihusisha nao hutawahi kukwepa. Ukijaribu, watang’oa macho yako na kukata masikio yako, au watavunja miguu yako....” Wanapotaja mashirika ya watu waovu, sote tunajua kwamba hayo yanahusisha wauaji, wanaochoma mali kwa makusudi, wezi, na wanyang’anyi wanaofanya kila aina ya mambo maovu. Hakuna anayetaka kukasirisha watu wa aina hizo. Hata serikali ya Kichina na polisi wake hawathubutu kuchezea wengine wao, sivyo? Kwa hiyo hebu tuwaangalie ndugu wanaoieneza injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Wanapoondoka kuwaleta watu kwa Mungu, wanavumilia kurushwa nje, kutukanwa, kuchapwa, kushambuliwa na mbwa, kukamatwa, kufungwa jela, na hata kuteswa. Wanapitia kila aina za kutendewa kikatili. Kama hawa ndugu kweli wangekuwa washirika wa shirika la watu waovu, yeyote angethubutu kuwatendea namna hiyo kweli? Wangevumilia kutukanwa na wasijibu? Wangepigwa na wasilipize kisasi? Je, mnawajua majambazi wowote walio hivyo? Je, mtu yeyote anayejihusisha na jambo la aina hiyo angeweza kumwamini Mungu kweli? Kama kweli angemwamini Mungu, angekuwa na kazi ya Roho Mtakatifu? Angeweza kuihubiri injili kwa wanaotafuta ambao wamejitolea kiasi? Zaidi ya hayo, kuna ndugu wengi kutoka katika madhehebu mbalimbali ambao wameisikia injili ya Mungu ya siku za mwisho. Wawe waliikubali injili na kisha kujiondoa kutoka katika kanisa kwa sababu yoyote ile, au hawakuwahi kuikubali kutoka mwanzo, nani kati yao ameng’olewa macho, kukatwa masikio, au kuvunjwa miguu? Kulingana na hili, lazima kuwe na idadi ya watu ambao wameng’olewa macho, kuvunjwa miguu. Je, mmeona hata mmoja? Kama kweli kungekuwa na mmoja, je, serikali ya CCP haingekuwa imeshamfikisha mahakamani, na kutoa hukumu, na kisha kuwahamasisha waandishi wote wa habari kueneza habari katika ulimwengu mzima? Kuna msingi wowote wenye ukweli wa mambo ambayo hawa wazushi wamesema? Wala hakuna msingi wowote wenye ukweli wanaposema mambo kama: “Ukijihusisha na kumwamini Mwenyezi Mungu, punde utakapoingia, hutawahi kutoka.” Imeandikwa katika “Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii”: “Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani.Kanisa la Mwenyezi Mungu halina haja kwa wale wasiomwamini Mungu kwa furaha ili kukamilisha idadi na wakati wa wanapoihubiri injili, hasa watu hawawezi kuwaburuta au kuwalazimisha kumwamini Mungu. Hii ni amri ya utawala ya Mungu na lazima kila mtu aishike hii—haiwezi kukiukwa. Ukweli ni kwamba mlango wa Kanisa uko wazi, na wale wanaotaka kuondoka kanisani na kuiacha imani yao wanaweza kwenda wakati wowote. Hakuna atakayewalazimisha. Kanisa la Mwenyezi Mungu daima humpa kila mtu uhuru wa kufanya uchaguzi wake mwenyewe. Kwa kweli, si kwamba wale wanaoikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho hawawezi kuondoka, lakini kwamba wao wenyewe hawataki kuondoka. Mbona hivi? Mwenyezi Mungu anasema, “Hali ya Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika dini na madhehebu yote, ‘imeparaganya’ mpangilio wa awali wa jamii ya kidini, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kujitokeza kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi sana, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu Mwenyewe amejitokeza, na Ameonyesha utambulisho Wake kwa watu—inawezekanaje hii isiupatie moyo wa mwanadamu furaha?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (10))Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. … Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Kuonekana na kazi ya Mungu mwenye mwili katika siku za mwisho kweli vimeitikisa dunia yote ya kidini na vimeitia shaka mioyo ya wale wanaotamani kuonekana kwa Mungu. Sababu ndugu kutoka katika madhehebu mbalimbali wamerudi kwa Mungu ni kuwa wameona kuonekana kwa Mungu, kusikia sauti Yake, kuelewa kwamba Kristo wa siku za mwisho ndiye ukweli, njia, na uzima, na kwamba imani katika Mwenyezi Mungu pekee ndiyo itawaruhusu kufanikisha wokovu na kuingia ndani ya ufalme wa mbinguni. Ni nani angetaka kuondoka baada ya kupokea wokovu kama huu? Kwa hiyo, ni rahisi kuona kwamba uvumi kuhusu watu kutotaka kuondoka kwa sababu ya kuogopa kung’olewa macho, kukatwa masikio, au kuvunjwa miguu unabuniwa tu na watu walio na nia zilizofichika.

Kutoka kwa kile tulichoshiriki kuhusu hapo awali, tunaweza kuona kwamba maoni yanayokashifu kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni uongo tu ambao ni ubunifu kamili usio na msingi wowote katika ukweli. Tukitumia utambuzi mdogo tu hapa uvumi huu unaanza kufumbuka kwa kweli. Muumini kubuni uongo na kuwa na ushuhuda wa uongo ni tabia ambayo Mungu huchukia zaidi; imeshutumiwa na Mungu, jinsi Biblia inavyosema: “Muongo huonyesha udanganyifu” (Mithali 12:17). “Midomo idanganyayo ni chukizo kwa Yehova” (Mithali 12:22). Bwana Yesu alisema: “Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na mtatimiliza tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo, na hakudumu katika ukweli, kwa sababu ukweli haupo ndani yake. Anaponena uwongo, anazungumza yaliyo yake mwenyewe: kwani yeye ni mwongo, na baba wa uwongo(Yohana 8:44). Kujua kwamba kubuni uongo na kuwa na ushuhuda wa uongo ni jambo ambalo Mungu huchukia sana, mbona washikiliekufanya hivi? Yohana sura ya 11 mstari wa 47-48 inasema: “Kisha makuhani wakuu na Mafarisayo walikonga baraza, na wakasema, Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamsadiki: nao Warumi watafika na kuichukua nafasi yetu na taifa letu.” Mathayo sura ya 28 inadokezea ukweli huu: Baada ya kufufuka kwa Bwana Yesu, makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi, na Mafarisayo waliogopa kwamba kila mtu angemwamini Bwana Yesu na kwamba kisha wangepoteza hadhi na mapato yao. Kwa hiyo walishirikiana kufunika ukweli kwamba Bwana Yesu alifufuka. Waliwahonga askari kwa fedha na kubuni uongo ili kuwashawishi watu kwamba Bwana Yesu hakuwahi kufufuka, wakisema kwamba wanafunzi Wake waliuondoa mwili Wake wakati askari walikuwa wakilala. Tunaona kutoka kwa hili kwamba watu wanaweza kubuni uongo kwa makusudi, na kuihukumu na kuikashifu kazi ya Mungu na pia kumkufuru Mungu. Wanafanya hivi ili kulinda sifa, hadhi na faida zao wenyewe. Hii inaonyesha asili yao mbovu, kwamba wanauchukia ukweli na ni maadui wa Mungu. Ni vivyo hivyo sasa, katika siku za mwisho. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameieneza kazi Yake ya siku za mwisho katika bara la Uchina, idadi kubwa ya waumini kutoka katika madhehebu mengi tofauti wamekuja kuikubali kazi mpya ya Mungu. Wakati viongozi wengine wa haya madhehebu wanawaona watu zaidi na zaidi wakimwamini Mwenyezi Mungu wakati waumini walio chini yao wanapungua, wanabuni aina zote za uongo na kashfa ili kuishutumu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ili waweze kulinda hadhi na mapato yao wenyewe. Hivi ndivyo wanavyowadanganya na kuwatisha ndugu ili kuwafanya waogope kuitafuta, kuichunguza, na kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho; kusudi lao ni kuwanasa na kuwadhibiti waumini wao milele. Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba viongozi wa madhehebu mbalimbali ni Mafarisayo wa kisasa waliofichuliwa na kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Wanabuni uvumi ili kulinda hadhi na mapato yao wenyewe—wana nia zao, malengo yao wenyewe katika hili.

Kama hatuwezi kutambua uongo huu unaobuniwa na jamii za kidini na tuufuate bila kufikiri, basi tunasimama katika upande wa wale wanaoikashifu, kuipinga, na kuikatiza kazi ya Mungu. Hili halimsababishi mtu kupoteza wokovu wa Mungu katika siku ya mwisho tu, lakini pia linamgeuza mtu kuwa mlengwa wa karaha, kukataliwa na adhabu ya Mungu. Hii ni kama kazi ya Bwana Yesu miongoni mwa watu wa Kiyahudi, ambapo Mafarisayo walibuni aina zote za uongo na kashfa dhidi Yake, kama kusema kwamba uwezo wa Bwana Yesu kuondoa pepo ulikuwa tu kwa sababu alikuwa Akimwita mkuu wa pepo, Beelzebuli, Akisema kwamba alikuwa Amepagawa na pepo, na vile vile mambo mengine ya kukufuru. Kwa sababu ya uongo na uvumi wa Mafarisayo, kwa sababu walikosa utambuzi, na kwa sababu hawakuchunguza kazi na neno la Bwana Yesu kwa makini, watu wengi wa Kiyahudi waliifuata njia mbovu ya kumpinga Mungu, kuukubali uongo wa Mafarisayo bila kufikiria na kuwaunga katika kumwacha na kumuua Bwana Yesu. Mafarisayo walieneza uongo na kumkashifu na kumkufuru Mungu, na sote tunaweza kukisia mwisho waliokumbana nao, lakini, je, wale watu wa Kiyahudi waliochukulia uongo na kashfa hizo kuwa ukweli—je, mwisho wao haukuwa wa huzuni hivyo? Walipitia maangamizi yasiyo ya kifani ya taifa na watu wa Kiyahudi walitawanyika pande zote. Hawakuwa na nyumbani pa kurudia kwa miaka 2,000. Je, haya siyo matokeo ya kuchukulia uongo wa Mafarisayo kuwa ukweli na kumpinga Mungu? Tunaweza kuona basi, kwamba wale wanaomwamini Mungu bila moyo wa uchaji, wasiotafuta au kuchunguza kazi mpya ya Mungu, na ambao wanaamini uongo kwa urahisi wanakuwa washirika kwa Shetani na watenda maovu wanaompinga Mungu. Mwishowe, wanazama katika maangamizi kwa sababu ya upinzani huu kwa Mungu. Hili lilitimiza kile ambacho kimeandikwa katika Biblia: “Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa(Hosea 4:6). “Wapumbavu hukufa kwa ajili ya ukosefu wa hekima” (Mithali 10:21).

Biblia inasema kwamba pepo hudanganya kuanzia mwanzo kabisa. Kudanganya na kukashifu ni hila mbili za kawaida ambazo Shetani hutumia kumpinga Mungu na kuwadanganya watu, na nia na ujanja wake mwovu umefichwa hapo ndani. Hata hivyo, hekima ya Mungu daima iko hatua moja mbele ya hila za Shetani. Shetani hawezi tu kuiharibu kazi ya Mungu, lakini kinyume chake, hutoa huduma yake kwa kazi ya Mungu. Kama wakati makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo walijitahidi sana kuipinga na kuishutumu kazi ya Bwana Yesu; walishirikiana na Roma kusababisha Bwana Yesu asulibiwe, wakifikiri kwamba walikuwa wakifanikiwa katika njama yao na wangeharibu kazi ya Bwana Yesu, lakini walishangazwa sana wakati Bwana Yesu alisema: “Imekwisha.” Hili linatuonyesha kwamba Mungu alitumia hila za Shetani kuutimiza mpango Wake wa usimamizi na kukamilisha kuwakomboa wanadamu. Leo si tofauti. Ingawa kuna viongozi katika madhehebu mbalimbali ambao watafanya lolote wawezalo kubuni uongo na uvumi ili kuipinga kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, haya yote hayawezi tu kuidhuru kazi ya Mungu, lakini kwa kweli, yanasaidia katika ufanikishaji wa kazi Yake ya siku za mwisho: kazi ya kuvuna na kupepeta, ya kutenga ngano kutoka miongoni mwa magugu, kondoo kutoka miongoni mwa mbuzi, kuwaainisha wanadamu kulingana na aina yao, na kuwatuza wazuri na kuwaadhibu waovu. Kupitia uzoefu wetu halisi, tumeona kwamba uongo wa serikali ya CCP na dunia ya kidini umewadanganya ndugu wengine ambao hawaelewi hali ya kweli. Hata hivyo, kupitia kuitafuta na kuichunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kuyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, wale wanaomwamini Mungu kwa kweli na kuupenda ukweli wanaona wazi ukweli kwamba njia ya kweli imepitia ukandamizaji tangu zama za kale. Wanaelewa kwamba kadri serikali ya CCP na dunia ya kidini huipinga na kuishutumu, ndivyo ilivyo njia ya kweli zaidi—hivyo wanamrudia Mungu. Lakini wale wanaochukia na kusinywa na ukweli husikiza uongo na uvumi bila kujali na kuwafuata watu wengine kwa sababu wanapenda uovu na kuhusudu mamlaka. Kwa hiyo, wamenaswa katika utando wa uongo na kukwama nje ya lango la ufalme. Je, hiyo si hekima na uweza wa Mungu? Uongo unaweza kufunga “magugu” kwa kukaza, lakini uongo huu haufanyi vivyo hivyo kwa “punje za ngano.” Upepo hupeperusha makapi, wakati mbegu nenezitakusanywa ndani ya ghala ya nafaka mwishowe. Kwa njia hii, hila za Shetani huishia kuwa vifaa tu, vyombo vya huduma vya kukamilisha kazi ya Mungu katika siku za mwisho ya kuwaainisha wanadamu kulingana na aina zao, na vile vile kuwatuza wazuri na kuwaadhibu waovu. Kazi ya Mungu ni ya ajabu na isiyoweza kueleweka kabisa.

Nifikiapo hapa, natumai kwamba mmepata maarifa kiasi kuhusu chanzo cha uvumi, asili yake, na madhara yake! Na sasa, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imefika vilele vipya visivyo na kifani—inakaribia hitimisho lake la kupendeza na Mwenyezi Mungu atajifichua kwa mataifa na watu wote ili waione. Katika wakati muhimu kama huu, mko tayari kupoteza uzima wenu kwa ajili ya kudanganywa tu na uvumi fulani? Mko tayari kuwa karibu kuukosa wokovu wa Mungu wa siku za mwisho kwa sababu ya jambo hilo? Naamini kwamba mtu yeyote mwenye akili hakika atafanya chaguo lenye busara.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp