Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Jinsi Nilivyomgeukia Mwenyezi Mungu Tena

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

24. Maneno ya Mungu Yaliniongoza Nikipitia Majaribu ya Shetani

Na Ma Xin, China

Kwa sababu mume wangu hakuwa akifanya kazi halali, alikunywa pombe sana, na hakujali masuala ya familia, mara nyingi nilikumbwa na uchungu na maumivu. Wakati ambapo sikuwa na nguvu ya kuendelea kung’ang’ana, jamaa yangu mmoja alishiriki injili ya Mwenyezi Mungu ya ufalme nami. Kupitia kusoma neno la Mungu, nilielewa kwamba Mungu anaonyesha ukweli na hufanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho ili kuokoa jamii ya binadamu kutoka kwa mikono ya Shetani. Anamruhusu mwanadamu kuelewa, kutii na kumgeukia ili kupokea ulinzi na utunzaji Wake. Kama matokeo, nilipokea kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa furaha na kuanza kuishi maisha ya kanisa haraka. Hata hivyo, nilipokuwa tu nikihisi mwenye bahati na furaha kwa sababu nilipata kitu ambacho ningekitegemea maishani, majaribu ya Shetani yalinivamia kama mnyama mwitu akikimbiza mawindo yake, na vita vya kiroho vikaanza...

Siku moja, binti yangu alikuja nyumbani kutoka shuleni na kuniambia, “Mama, leo nilipokuwa nikimsaidia mwalimu wangu kuleta vitu fulani katika ghorofa ya juu, kwa bahati mbaya niligonga mkono wangu kwenye chuma. Unauma sana.” Nikiwa na wasiwasi, niliuangalia mkono wake. Haukuwa mwekundu wala kuvimba. Kulikuwa na sehemu ndogo ya ngozi iliyopasuka eneo la chini la kidole chake cha gumba, nilimfariji binti yangu na kusema, “Usiwe na wasiwasi, utakuwa na afueni baada ya siku chache.” Nilifikiri, “Sasa namwamini Mwenyezi Mungu, kwa hivyo kwa ulinzi na utunzaji wa Mungu, mtoto wangu bila shaka atakuwa sawa.” Hata hivyo, siku kadiri kumi zilipita na kidole chake cha gumba na kiganja chake nusu vilikuwa vikivimba zaidi. Baada ya miezi miwili, sehemu hiyo yote ilikuwa nyeusi na zambarau. Kidole chake cha gumba kiligeuka kuwa kikubwa zaidi kuliko kidole chake kikubwa cha mguu. Basi nikaanza kuwa na wasiwasi sana. Mimi na mume wangu tulimpeleka binti yetu hospitalini mara moja, lakini hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichopatikana kupitia uchunguzi wote wa kawaida. Nilimwomba Mungu kimoyomoyo, “Mwenyezi Mungu. Mkono wa binti yangu una tatizo gani? Niko tayari kukutazamia Wewe na kukuaminia binti yangu. Tafadhali mtunze na umlinde.” Hata hivyo, wakati familia na marafiki waliona mkono wake, wote walisema, “Kuna jambo la kuogofya sana na mkono wa binti yako.” Bibi yake pia alisema kwa wasiwasi, “Huenda atakuwa na ulemavu mkononi mwake.” Kusikia mambo haya kuliibua mchanganyiko wa hisia; nilihisi mwenye wasiwasi sana. Binti yangu kweli akilemaa katika mkono huo, tutafanya nini kuanzia sasa kuendelea? Yeye ni mchanga sana. Anawezaje kuvumilia kipingamizi cha aina hii? Nilivyozidi kufikiri, ndivyo nilivyozidi kuhisi mwenye maudhi, wasiwasi na uchungu. Niliwaza, “Nimekuwa nikimwomba Mungu muda huu wote. Kwa nini mkono wa binti yangu haujapata afueni? Mungu hajajibu maombi yangu; Hajamlinda binti yangu!” Moyo wangu ulijawa na suitafahamu na malalamiko kwa Mungu. Na wakati huu, mume wangu aliharibu mambo kazini tena kwa sababu ya kulewa kwake na bosi wake akataka kumfuta kazi. Mambo yanapoharibika, yanaharibika sana—lilikuwa tu jambo moja baada ya jingine! Nilipopata habari hii, nilihangaika hata zaidi. Mume wangu akipoteza kazi yake, familia yetu ingejimudu vipi? Mambo haya yaliniacha nikihisi mwenye wasiwasi sana na singeweza kutulia bila kujali nilichofanya. Hata niliposoma neno la Mungu, sikuweza kuliingiza akilini hata kidogo. Niliwaza, “Namwamini Mungu. Kwa nini mambo haya yote mabaya yanaitendekea familia yangu? Kwa nini Mungu hatulindi?” Nilikuwa hasi sana kwa sababu ya hili.

Wakati jamaa yangu aliyeshiriki injili na mimi alijua kuhusu fikira zangu, alishiriki nami kwa subira, “Taabu tunazokabili leo ni kwa sababu ya usumbufu wa Shetani—kuna vita vinavyoendelea katika dunia ya kiroho. Kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni ili kuwaokoa wanadamu, kwa hivyo watu wanapomwacha Shetani na kumrudia Mungu, Shetani hatakubali kushindwa. Atamsumbua na kumdanganya mwanadamu katika kila namna iwezekanavyo. Atawaletea watu mateso na dhiki za kila aina ili waanze kuwa na suitafahamu na malalamiko kumhusu Mungu. Lengo lake ni kumfanya mwanadamu amkatae na kumwasi Mungu, kupoteza wokovu wa Mungu na kwa mara nyingine kurudi katika miliki ya Shetani. Tukiwa hasi hivi na kujitenga kutoka kwa Mungu, basi tumeanguka katika mtego mjanja wa Shetani! Kwa kweli, mambo haya hayangeweza kuepukika hata ikiwa tusingemwamini Mungu, lakini tunampa Shetani nafasi ya kutudhuru wakati mtazamo wetu kuhusu imani si sahihi. Hebu tuangalie kifungu cha maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu alisema, ‘Watu wengi huamini katika Mungu kwa ajili ya amani na manufaa mengine. Isipokuwa kwa manufaa yako, wewe huamini katika Mungu, na ikiwa huwezi kupokea neema za Mungu, wewe huanza kununa. Hiki kingekuwaje kimo chako halisi? Inapofikia matukio ya familia yasiyoepukika (watoto kuwa wagonjwa, mume kwenda hospitalini, mazao mabaya ya mimea, kuteswa kwa watu wa familia, na kadhalika), huwezi hata kufaulu katika mambo haya ambayo hufanyika mara kwa mara katika maisha ya kila siku. Wakati ambapo mambo hayo hufanyika, wewe huingia katika hofu kubwa, hujui la kufanya—na wakati mwingi, wewe hulalamika kuhusu Mungu. Wewe hulalamika kwamba maneno ya Mungu yalikudanganya, kwamba kazi ya Mungu imekuvuruga wewe. Je, hamna mawazo kama haya? Unadhani mambo kama haya hufanyika miongoni mwenu mara chache tu? Mnatumia kila siku kuishi katikati ya matukio kama haya. Hamfikirii hata kidogo sana kuhusu mafanikio ya imani yenu katika Mungu, na namna ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Kimo chenu halisi ni kidogo sana, hata kidogo zaidi kuliko cha kifaranga mdogo. … Tumbo lako limeshindiliwa pomoni na malalamiko, na wakati mwingine wewe huendi katika mikutano au kula na kunywa maneno ya Mungu kwa sababu ya hili, wewe huelekea kuwa mbaya kwa muda mrefu sana’ (“Utendaji (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili).”

Niliposikia maneno haya ya Mungu, moyo wangu ulitetema: Mungu kweli huchunguza vina vya mioyo ya wanadamu! Kila neno lilifika ndani sana ya moyo wangu. Sababu ya imani yangu kweli ilikuwa kwa ajili nilitaka familia yangu iwe salama! Nilipokumbana na taabu, nilimwelewa Mungu visivyo, nililalamika kumhusu Mungu na kupoteza imani yangu Kwake. Nilikuwa nikiishi katika hali hasi na kimo changu kilikuwa kidogo sana. Jamaa yangu aliendelea katika ushirika, “Maneno ya Mungu yanaonyesha mtazamo wetu wenye makosa wa kuwa na imani ili tu kutafuta baraka. Kwa sababu ya fikira na mawazo yetu, tunafikiri kwamba alimradi tumwamini Mungu, Atatubariki na kuhakikisha tuko salama salimini, kwamba kila kitu kinaendelea vizuri. Kwa kuwa fikira hii iko ndani ya mioyo yetu, punde tunapokumbana na hali zisizofurahisha maishani mwetu, tunamlaumu Mungu mara moja. Kama matokeo, tunaweza kumkataa, kumsaliti ama kumwacha Mungu wakati wowote. Shetani anaelewa vyema udhaifu huu wetu mbaya sana; hii ndiyo maana anatuletea kila aina za misiba na mateso ili kutuvuruga. Ikiwa hatuwezi kubaini hila janja za Shetani, tutampinga, kumlaumu na kumkataa Mungu bila kutaka, na hata tunaweza kumwacha na kumsaliti Mungu. Hatimaye tutakamatwa na kumezwa na Shetani. Maneno ya Mungu yanasema, ‘Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, bila kusita wanatafuta maiti za watu wazile’ (“Sura ya 10” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Kile kinachofichuliwa na maneno ya Mungu ni ukweli mtupu wa dunia ya kiroho! Punde tunapomezwa na Shetani, tunapoteza nafasi yetu ya kuokolewa na Mungu. Lazima tubaini njama janja za Shetani!” Moyo wangu ulichangamka sana punde nilipomsikia akisema mambo haya. Nilitambua kwamba mambo ambayo familia yangu ilikuwa ikikumbana nayo kweli yalikuwa usumbufu na msiba wa Shetani. Wakati uo huo, Mungu alifichua mtazamo wangu wenye makosa kuhusu imani. Nilimwambia jamaa yangu, “Tangu nianze kumwamini Mungu, nimefikiri kwamba Mungu ni Mungu anayempa mwanadamu neema na kwamba alimradi umwamini Mungu, mambo yataenda shwari katika familia yako na utapokea utunzaji na ulinzi wa Mungu. Nilipokumbana na shida maishani mwangu, nilifikiri kwamba kitu hakikuwa sawa, na kwamba kuwa na imani kunamaanisha kwamba sifai kuwa na shida za aina hii. Ni baada tu ya kukusikia ukisoma vifungu hivyo vya maneno ya Mungu ndiyo nilielewa kwamba mtazamo wangu kuhusu imani umekuwa usio sahihi na kwamba Shetani amekuwa akitumia hili kama njia ya kunivuruga na kunifanya niibue fikira na suitafahamu kumhusu Mungu, na kunitenga na Yeye. Kweli nilianguka katika njama janja za Shetani! Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali kile Shetani anafanya kunisumbua, lazima nibaini njama zake. Sitamlaumu, kumwelewa visivyo ama hasa kumsaliti Mungu tena. Lazima nimshuhudie Mungu. Bila kujali iwapo mkono wa mwanangu utapata afueni ama iwapo mume wangu anaweza kufanya kazi, niko tayari kumwaminia Mungu vitu hivi na kumwacha Mungu afanye mipango Yake.” Nilishangaa kwamba, punde nilipokuwa tayari kutii mipango na utaratibu wa Mungu, baada ya muda mfupi, mkono wa binti yangu ulianza kutunga usaha. Daktari alipoondoa usaha, aligundua kwamba kulikuwa na kibanzi kilichokwama kwenye sehemu ya chini ya kidole chake. Baada ya kibanzi hicho kuondolewa, haukuwa muda mrefu kabla ya mkono wa binti yangu kupona. Baada ya tukio hili, niliweza kuona kwamba punde nilipogeuza mtazamo wangu wenye makosa na kuwa tayari kumtii Mungu, Shetani aliaibika na kushindwa. Mungu aliondoa ugonjwa wa binti yangu. Kweli Mungu ni mwenye miujiza na uweza!

Hata hivyo, Shetani mbaya hangekubali kushindwa. Hila yake moja inaposhindwa, atajaribu nyingine. Usiku mmoja mnamo saa mbili usiku, mume wangu aliniita ghafla na kunitaka niende ghorofa ya chini ili nimpe fedha kiasi. Nilimvalisha nguo mtoto wetu mchanga, aliyekuwa na umri wa kadiri mwaka mmoja wakati huo, na kuenda ghorofa ya chini, ambapo nilimwona mume wangu akitoka nje ya teksi kwa jitihada kidogo. Hata alikuwa na shida kubwa kutembea. Nilipomwona katika hali hii, nilihisi mwenye wasiwasi sana na sikujua la kufanya. Nilichoweza kufanya ni kumwita Mungu bila kusita, “Mwenyezi Mungu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, nakuomba Uulinde moyo wangu. Kimo changu ni kidogo. Tafadhali nipe imani ya kuwa na ushuhuda katika hali ya aina hii na kutokulaumu.” Nilihisi mwenye imani zaidi baada ya kuomba. Lakini baada ya hapo miguu ya mume wangu ilidhoofika zaidi hadi kiwango ambapo hakuweza hata kutembea. Sikuwa na chaguo ila kumwacha ndugu yake mkubwa na bibi yake wampeleke hospitalini. Nilikuwa na wasiwasi sana nilipofikiri kuhusu jinsi Mume wangu hakuweza kutumia miguu yake, kwa hivyo nilimwomba Mungu tena, “Mungu! Mume wangu hayuko sawa. Ni Shetani anayekuja kunivuruga ili nikulalamikie na kukusaliti. Nataka kubaini hila za Shetani. Bila kujali jinsi matibabu ya mume wangu yalivyo ghali, sitakulaumu. Niko tayari kukutii. Nakuomba Unilinde ili niweze kukushuhudia.” Baada ya kuomba nilihisi mwenye amani zaidi. Muda mfupi baadaye, wifi wangu alipiga simu na kusema kwamba mume wangu alikataa kwenda hospitalini; alisisitiza kwenda nyumbani. Nikiamini hili kuwa mapenzi ya Mungu, nilikubali. Baada ya wao kurudi, shemeji yangu na mke wake walijaribu kuchuna miguu yake na kuiosha kwa maji ya fufutende. Walijishughulisha kwa muda mrefu sana, lakini mume wangu bado hakuweza kuhisi chochote katika miguu yake. Kwa sababu ya kukata tamaa, alisema, “Mambo ni mabaya. Sina hisi yoyote katika miguu yangu!” Niliposikia haya, machozi yalianza kutiririka usoni mwangu ghafla na nikawaza, “Mambo kwisha. Hataweza kutembea tena. Tutafanya nini ikiwa amepooza? Familia yetu itajimudu vipi?”

Nilipokuwa tu karibu kujawa na uchungu na kufa moyo, nilifikiri kuhusu maneno ya Mungu: “Kama mambo mengi yanakuja kwako ambayo si sambamba na dhana zako lakini unaweza kuyaweka kando na kujua matendo ya Mungu kutoka kwa mambo haya, na katikati ya usafishaji unadhihirisha moyo wako wa upendo kwa Mungu, huku ni kuwa shahidi. Kama nyumba yako ina amani, unafurahia starehe za mwili, hakuna mtu anayekutesa, na ndugu na dada zako katika kanisa wanakutii, je, unaweza kuonyesha moyo wako wa upendo kwa Mungu? Je, hili linaweza kukusafisha? Ni kwa kupitia katika usafishaji tu ndiyo upendo wako kwa Mungu unaweza kuonyeshwa, na ni kwa mambo yasiyo sambamba na dhana yako kutokea tu ndiyo unaweza kufanywa mkamilifu. Ni kupitia mambo mengi hasi, matatizo mengi ndipo Mungu anakukamilisha. Ni kupitia kwa matendo mengi ya Shetani, shutuma, na udhihirisho wake kwa watu wengi kwamba Mungu anakuruhusu upate ujuzi, hivyo kukufanya uwe mkamilifu” (“Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupitia maneno ya Mungu, nilielewa kwamba Shetani alikuwa akitumia hali ya mume wangu kufanya hila zake. Kwa kuwa mtazamo wangu wa kupata baraka kutoka kwa Mungu na kufanya mabadilishano na Yeye ili nimpe imani haukuwa umetatuliwa kabisa, Shetani alifanya hili ili kunifanya nielewe visivyo, nimlaumu, nimkatae, na kumsaliti Mungu, hatimaye kupoteza wokovu wa Mungu. Lakini Mungu alitumia hali tu kama hiyo ili kuikamilisha imani yangu Kwake, Akiniruhusu kuona vitu kulingana na maneno ya Mungu na kubaini kula njama kwa Shetani ili nisibishane tena na Mungu kwa lengo la kupata baraka. Hili liliniruhusu kusimama upande wa Mungu na kuwa na ushuhuda thabiti Kwake katika vita kati ya Mungu na Shetani. Punde nilipoelewa mapenzi ya Mungu, nilimwomba Mungu kimoyomoyo, “Mungu, linda moyo wangu ili niweze kusimama imara katika hali hii. Bila kujali kitakachomfanyikia mume wangu, sitakulaumu. Hata akipooza, niko tayari kuendelea kukufuata.” Kwa mshangao, punde nilipomaliza kuomba, nilimsikia mume wangu akisema kwa furaha, “Niko afadhali sasa. Naweza kusongeza miguu yangu.” Nilisisimka sana—kweli Mungu ni mwenye hekima na uweza! Mungu hakufanya nipitie mambo haya kwa makusudi. Badala yake, Alitumia hali hizi kunijaribu na kubadili mitazamo yangu yenye makosa niliyokuwa nayo katika imani yangu!

Baadaye, niliendelea kusoma maneno ya Mungu, “Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayewapotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajaruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu waovu na kuwatuza wema. Amepambana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kitii mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu duniani kipumzike chini ya kigonda Chake, na pia Huwafanya wale watenda maovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu wajipate katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake” (“Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilielewa kutoka maneno ya Mungu kwamba tangu wanadamu wapotoshwe na Shetani, Shetani amekuwa akimvuruga na kumdhuru mwanadamu wakati huo wote. Na wakati huo wote, Mungu amekuwa akimwokoa mwanadamu ili aweze kujiweka huru dhidi ya madhara ya Shetani. Nikikumbuka uzoefu wangu mwenyewe, tangu nilipopata imani, Shetani hakuwahi kuacha kubuni njama ili kunisumbua. Alitumia shida za afya za binti yangu na mume wangu kunifanya niwe hasi na dhaifu, kunifanya nimwelewe Mungu visivyo na kumlaumu. Alijaribu bila mafanikio kunifanya nimwache na kumsaliti Mungu, kunivuta kuzimu. Pia, hekima ya Mungu daima hutegemezwa kwa njama za Shetani. Mungu alitumia vurugu za Shetani kufichua mtazamo wangu usio sahihi kuhusu imani huku pia akitumia maneno Yake kunipa nuru na kuniangaza. Hili lilinisaidia kutambua lengo langu la kupata baraka kutoka kwa Mungu na kufanya mabadilishano naye. Kupitia watu, matukio na mambo halisi, Mungu ameniruhusu kubaini asili ovu na malengo yanayostahili dharau ya Shetani, akiniwezesha kukana uovu na kuugeukia wema. Sitaishi tena kwa kufuata tamaa yangu ya kupata baraka. Kwa imani ya kweli katika Mungu, naweza kumshinda Shetani na kupatwa na Mungu.

Matukio haya yalinionyesha jinsi upendo na wokovu wa Mungu kwa mwanadamu ulivyo wa kweli! Kuanzia sasa kuendelea, nitamwomba Mungu na kumtegemea Mungu zaidi, na nitashuhudia katika majaribu. Nimedhamiria kumfuata Mungu kwa uthabiti mpaka mwisho kabisa!

Iliyotangulia:Vita

Inayofuata:Nilichopata kwa Sababu ya Kupitia Majaribu ya Shetani Mimi Mwenyewe

Maudhui Yanayohusiana

 • Kupenya Ukungu ili Kuona Mwanga

  Wakati tu nilipokuwa nikipoteza njia yangu, ilikuwa ni neno la Mungu lililoniongoza kubaini mpango wa Shetani, na kupenya ukungu na kuingia kwenye njia angavu na sahihi kwa uzima.

 • Bahati na Bahati Mbaya

  Kama haingekuwa kwa ajili ya ugonjwa wangu ambao umenizuia kutafuta umaarufu na kupata, bado ningekuwa mashine ya kutengeneza fedha duniani. Ningekuwa kipofu kwa hili mpaka uharibifu wa Shetani uniue. Shetani alinidhuru mimi kwa kutumia umaarufu, faida, na magonjwa. Kinyume na hilo, Mwenyezi Mungu alitumia ugonjwa yangu kunileta mbele Yake. Kupitia kwa maneno Yake, niliona wazi kwamba Shetani anahusika na upotovu wa mwanadamu. Niliona pia wazi jinsi ilivyo vibaya na cha kudharauliwa kwa Shetani kutumia umaarufu na faida kuwameza watu. Hatimaye nilikuwa katika nafasi ya kutupa mbali pingu za umaarufu na faida na kuanzisha mtazamo sahihi wa maisha. Roho yangu iliwekwa huru. Mungu ni mwenyezi sana na mwenye busara!

 • Nimepata Makazi ya Kweli

  Sasa, kila siku ninafurahia kunyunyiziwa na kukimiwa na neno la Mwenyezi Mungu. Maumivu ambayo nilihisi ndani yangu yametoweka, na nimepata mwelekeo katika maisha yangu na kupata uhuru na furaha ya kweli. Shukrani kwa Mungu kwa kuniokoa. Nitajitahidi kufuatilia ukweli na kutimiza wajibu wangu kama kiumbe kadiri niwezavyo ili kulipisha upendo wa Mungu!

 • Kutembea Katika Njia Ng’avu ya Maisha

  Kila siku ningekula, kunywa na kufuatilia anasa hadi nilipokuwa nimetosheka na moyo wangu ulikuwa umeridhika. Nilidhani kwamba ilikuwa tu kwa kuishi kwa njia hii ndiyo maisha yalikuwa na maana yoyote, na hiyo ni mpaka nilipopokea kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Ni baada tu ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu ndipo nilipata utambuzi wa maisha muhimu kwa kweli ni yapi, na kisha nilianza kutembea katika njia ng’avu ya maisha.