Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Jinsi Nilivyomgeukia Mwenyezi Mungu Tena

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

25. Nilichopata kwa Sababu ya Kupitia Majaribu ya Shetani Mimi Mwenyewe

Na Xinzhi, Australia

Nilipokuwa nikirudi nchini Afrika Kusini kushughulikia mambo fulani mnamo Disemba mwaka wa 2017, nilikutana na dada katika Bwana, ambaye aliniambia kwamba Bwana Yesu alikuwa amerudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Pia alishiriki nami kinaganaga kuhusu ukweli na siri kama mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, kusudi la hatua tatu za kazi ya Mungu na umuhimu wa jina la Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika wake, nilistaajabu na kusisimka. Sikuwahi hapo awali kusikia ukweli huu, lakini nilijua kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye angeweza kufichua siri za kazi Yake. Kwa hivyo nilikuwa na uhakika moyoni mwangu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na nilikubali kwa furaha kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Kila siku, nilifurahia kunyunyiziwa na ruzuku ya maneno ya Mungu na nilihisi mtulivu na aliyesaidiwa sana. Hata hivyo, sikujua hata kidogo kwamba majaribu ya Shetani yalikuwa yamejificha karibu sana …

Baada ya kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, nilihudhuria mikutano ya kanisa kwa bidii. Hata hivyo, kwa ajili ya sababu ambazo sikujua, kila ndugu zangu walipoanza kusoma maneno ya Mungu, ningeanza kusinzia. Jambo hili lingetendeka hata nilipopumzika kabla ya mkutano. Ndugu zangu wangelazimika kuniamsha mara nyingi, lakini mara waliponiamsha ningelala tena mara moja. Kwa hivyo, ningesinzia mfululizo karibu mkutano mzima, akili yangu ilichanganyikiwa daima, hakuna chochote ambacho kingeeleweka, na jambo hili lilinifadhaisha sana. Nilikanganyikiwa sana: Kwa kawaida singehisi mwenye usingizi nilipokuwa nikifanya kitu kingine, kwa hivyo, je, ni kwa nini nilihisi mwenye usingizi sana mara nilipofika katika mkutano wa kanisa? Niliishia kutumaini mikutano imalizike haraka iwezekanavyo, na mwishowe ilifikia kiwango ambacho hata sikutaka kuhudhuria mikutano hiyo tena. Dada mmoja aliona kwamba nilikuwa nikisinzia daima katika mikutano, na kwa hivyo alishiriki ushirika nami, akisema kwamba hivi vilikuwa vita vya kiroho. Kisha alinisomea kifungu cha maneno ya Mungu, “Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu …” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Alitoa ushirika, akisema, “Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha maneno na kutekeleza kazi ya hukumu ili kugeuza na kutakasa tabia zetu za kishetani, ili kutuwezesha kuwa huru kabisa kutokana na minyororo ya dhambi na kutakaswa na kuokolewa na Mungu. Hata hivyo, Shetani hataki tuokolewe na Mungu, na kwa hivyo anajaribu kutuvuruga kwa kila njia iwezekanayo. Kwa mfano, tunapohisi wenye usingizi mara tunapoanza kusoma maneno ya Mungu katika mkutano, na bado tuna nguvu nyingi tunapofanya kitu kingine chochote—hii bila shaka ni Shetani anayejaribu kutuvuruga. Shetani hutuvuruga sana kiasi kwamba hatuwezi kujituliza mbele za Mungu ili kusikia na kutafakari maneno Yake. Kwa hivyo, kamwe hatutaweza kufahamu ukweli au kufahamu mapenzi ya Mungu bila kujali tunahudhuria mikutano kwa muda gani. Badala yake, kwa sababu ya kuteseka kwa miili yetu, sisi huzidi kuchoshwa na kuhudhuria mikutano, na hata inaweza kufikia kiwango hatari kiasi kwamba tunatamani kumsaliti na kumwacha Mungu na kurudi chini ya utawala wa Shetani. Hii ni njama ya hila na nia mbaya ya Shetani. Dada, hatuna budi kung’amua njama za Shetani za hila, tumwombe na kumtegemea Mungu zaidi, na tuwe na azimio la kumwacha Shetani, kwa kuwa ni kwa njia hii tu ndiyo tutaweza kushinda vurugu na mashambulio ya Shetani!”

Baada ya kusikiliza ushirika wa dada huyo, kila kitu ghafla kilianza kuwa wazi, na niliogopa kidogo na kukasirika kidogo pia. Niliwaza: “Shetani ni mbaya sana kwa kweli! Si ajabu mimi huhisi mwenye usingizi mara ninapofika katika mkutano. Inatokea kuwa huyu ni Shetani anayejaribu kunisumbua.” Nilifikiria kuhusu jinsi ambavyo nilikuwa nikipata usingizi wa kimang'amung'amu mara nilipofika katika mikutano, jinsi akili yangu ingehisi kama kinamasi hata baada ya ndugu kuniamsha, na jinsi hata nilivyokuwa nimekubali wazo la kutohudhuria mikutano tena; kama ilivyotokea, nilikuwa nimeshindwa na njama za hila za Shetani. “La,” niliwaza. “Wakati ujao nikihudhuria mkutano, nitauacha mwili wangu na kupigana na Shetani, na nitasimama kidete katika ushuhuda wangu katika vita hivi vya kiroho!” Kisha mimi na dada huyo tulimwomba Mungu, na nilimjulisha Shetani kuwa, bila kujali jinsi anavyoweza kujaribu kunivuruga, daima ningeendelea kuhudhuria mikutano na kumwabudu Mungu, na kwamba singepumbazwa naye tena. Hivyo, nilipojisikia mwenye usingizi tena katika kipindi cha mkutano, kila wakati ningemjulisha Shetani azimio langu. Wakati huo huo, ningeendelea kumwomba Mungu, nikimsihi Aulinde moyo wangu, na ningefanya bidii ya makusudi kutuliza moyo wangu mbele za Mungu na kutafakari maneno Yake. Wiki moja baadaye, sikuhisi tena mwenye usingizi, na niliweza kuhudhuria mikutano vizuri pamoja na akina ndungu na kushiriki maneno ya Mungu.

Tukio hili liliniwezesha kufahamu kwamba Shetani alikuwa akitumia mbinu hii yenye kustahili dharau kunivuruga ili anifanye niachane na njia ya kweli—Shetani ni mwovu sana na wa kudharauliwa mno! Pia nilikuja kutambua kwamba, tusipokuja mbele za Mungu na kukubali wokovu Wake, tutaweza tu kuishi chini ya utawala wa Shetani, kudhuriwa na kudhibitiwa naye. Kwa kufikiria jambo hili, nilifanya azimio kwa Mungu: Bila kujali jinsi Shetani anavyoweza kujaribu kunivuruga, sitajisalimisha kamwe. Nitamwamini na kumfuata Mungu kwa dhati, na nitaeneza injili ya ufalme wa Mungu kwa watu wengi hata zaidi wanaoishi chini ya utawala wa Shetani, ili wao pia waweze kupata wokovu wa Mungu wa siku za mwisho na kuondolewa madhara ya Shetani.

Siku moja, nilitoa ushuhuda kwa rafiki mmoja kuhusu kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Alitaka kuchunguza kuhusu jambo hilo zaidi, kwa hivyo nilipanga kuzungumza naye kulihusu tena katika kipindi cha siku kadhaa baadaye. Hata hivyo, bila kutarajia, siku mbili baadaye ghafla nilianza kujisikia mwenye kusinzia sana na sikio langu la kulia lilivimba ndani na nje. Liliuma sana kiasi kwamba hata singeweza kuligusa. Nilidhani huenda ikawa ishara ya homa, kwa hivyo sikuwaza sana kulihusu.

Asubuhi moja wiki moja baadaye, nilipokuwa nikinawa uso wangu, niligundua kuwa upande wa kulia wa uso wangu ulikuwa umeganda, na singeweza kufumba macho yangu kikamilifu, na singeweza kusongesha kisashi changu na mdomo wangu ulionekana wa mshazari. Nilipojiangalia katika kioo, niligundua kuwa nilikaa kama mtu mzee mwenye ugonjwa wa Alzheimer, na nilishikwa na hofu, nikiwaza: “Uwezo wangu wa kusikia haujapata nafuu bado na sasa uso wangu wote ni wa mshazari. Sijawahi kuwa na hali hii kabla. Je, hali hii ingewezaje kutokea?” Niliogopa sana, kwa hivyo nilienda hospitalini haraka. Daktari alisema kwamba nilikuwa na kiharusi cha uso na hali yangu ilikuwa mbaya sana, na kwamba hakukuwa na uhakika ikiwa ningeponywa au la. Wakati huo, niligubikwa na woga kabisa, na niliwaza: “Je, ningewezaje kuwa nimepata ugonjwa hatari kama huu? Nitafanya nini iwapo hautaweza kuponywa?” Nilijawa na hofu na nilimwomba mungu wakati wote: “Ee Mungu, ninaogopa sana. Ee Mungu, tafadhali nisaidie, tafadhali kuwa nami….” Baada ya kuomba, maneno ya Mungu yalinijia akilini. “Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako. Wakati ugonjwa hutokea ni kwa sababu ya upendo wa Mungu, na nia Yake nzuri kwa hakika inaiunga mkono. Hata wakati mwili wako unavumilia mateso, usichukue ushauri kutoka kwa Shetani. Sifu Mungu katikati ya ugonjwa na furahia Mungu katikati ya sifa yako. Usikate tamaa unapokabiliwa na ugonjwa, endelea kutafuta na kamwe usisalimu amri, na Mungu Ataangaza nuru Yake kwako. Ayubu alikuwa mwaminifu kiasi gani? Mwenyezi Mungu ni daktari mwenye nguvu zote! Kukaa katika ugonjwa ni kuwa mgonjwa, lakini kukaa katika roho ni kuwa mzima. Kama unayo pumzi moja tu, Mungu hatakuacha ufariki” (“Sura ya 6” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno Mungu yenye mamlaka yalinipa imani na nguvu. “Naam,” niliwaza. “Mungu ni mwenye uwezo, na vitu vyote vimo mikononi Mwake. Anashikilia pia maisha yangu na kifo changu mikononi Mwake, na ikiwa uso wangu utapata nafuu au la ni uamuzi wa Mungu. Ingawa sielewi ningewezaje kupatwa na ugonjwa huu ghalfa sana, ninaamini kwamba mapenzi ya Mungu ndiyo kiini chake. Lazima nisimuelewe Mungu visivyo lakini badala yake niwe na imani Kwake. Ayubu alipopoteza kila kitu na mwili wake mzima kutokewa na majipu machungu, bado alidumisha imani yake kwa Mungu na mwishowe alisimama kidete katika ushuhuda wake kwa Mungu. Sina budi kuwa kama Ayubu!” Baada ya kufikiria jambo hili, moyo wangu uliokuwa na wasiwasi ulitulizwa.

Baadaye, niliona maneno yafuatayo kutoka kwa Mungu: “Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya yanaweza kumshawishi binadamu kikamilifuHafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba ‘ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano’ ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli” (“Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Shukrani ziwe kwa Mungu! Kwa kusoma maneno ya Mungu, nilifahamu kwamba Mungu hampongezi kila mtu anayemwamini. Wale ambao Mungu atawaokoa ni wale wanaomfuata kwa kweli, ambao hawamwachi bila kujali ni maumivu au taabu gani wanazokumbana nazo, na wanaoweza kuwa na ushuhuda Kwake katika kipindi cha majaribu. Waumini wale wa uwongo, kwa upande mwingine, wanaomwamini Mungu tu kwa kusudi la kupata baraka Zake watawekwa wazi na kuondolewa wakati wa majaribu. Nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu, nilifikiria tena kuhusu Ayubu. Wakati wa majaribu yake, alipoteza mali yake, watoto wake, na mwili wake wote ulitokwa na majipu machungu, bado hakupoteza imani yake kwa Mungu, lakini aliendelea kuwa na moyo wa kumcha Mungu na kumtii Mungu, akitukuza jina takatifu la Yehova Mungu, akisema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” (Ayubu 1:21). “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:10). Kwa kusema maneno haya, alikuwa na ushuhuda mkubwa sana na mzuri kwa Mungu, na alimfanya Shetani kutiwa aibu. Kisha kulikuwa na Ibrahimu. Mungu alipomwambia amtoe mtoto wake wa pekee Isaka kama sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu, ingawa moyo wake ulikuwa umejawa na uchungu, hakulalamika au kupinga, wala hakubishana na Mungu. Badala yake, alimtii Mungu bila masharti, akawa na ushuhuda wa kweli, na kupata baraka na ahadi ya Mungu. Kisha nilielewa kuwa ugonjwa huu ambao ulikuwa umenipata ulikuwa vita vingine vya kiroho, ambavyo Shetani alikuwa akijaribu kunishawishi. Pia ni Mungu aliyekuwa akinijaribu ili aone kama nilikuwa na imani ya kweli kwa Mungu na ikiwa nilikuwa muumini wa kweli kwa Mungu au la. Nikikumbuka tangu nilipoanza kumwamini Mungu, niligundua kwamba Shetani alikuwa amejaribu daima kunivuruga, kuanzia kuhisi mwenye usingizi wakati wa mikutano ya kanisa hadi kwa kichwa changu kuhisi kizito kwa usingizi na sikio langu kuvimba, na kisha kupatwa na ugonjwa wa kiharusi cha uso—kila moja ya vurugu za Shetani ilikuwa mbaya zaidi kuliko ya awali. Shetani hakukubali kuniruhusu nipokee wokovu wa Mungu ila alitaka kuniweka chini ya udhibiti wake ndani ya mfumbato wake, kupotoshwa na kuchezewa naye apendavyo. Kupitia mwongozo wa maneno ya Mungu, nilikuja kuwa na utambuzi kiasi wa nia za Shetani zenye kustahili dharau, na nilijua kuwa ni lazima nisidanganywe tena na njama zake za hila, lakini kwamba ni lazima nitoe moyo wangu wa kweli kwa Mungu na kujisalimisha kwa mipango na utaratibu Wake. Nikifikiria kuhusu jambo hili, sikuhisi tena aliyebanwa na ugonjwa wangu, na nilihisi hali nzuri ya utulivu na uhuru. Kisha nilikabidhi ugonjwa wangu kwa Mungu, na nilifanya azimio hili: Nikipata afueni au la, sitamlaumu Mungu au kumkataa Mungu, lakini nitamfuata Mungu hadi mwisho kabisa!

Nilipokuwa tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu, nilishuhudia matendo Yake ya kustaajabisha. Wiki moja baadaye, rafiki yangu mmoja daktari alipata habari kuhusu hali yangu na alipendekeza niende kwake kupata tiba vitobo. Nilidhani kwamba pendekezo la rafiki yangu lingeweza kuwa limetoka kwa Mungu, kwa hivyo nilikubali kulijaribu. Lililonishangaza, baada ya wiki tatu tu za matibabu ya vitobo, uso wangu ulianza kupona pole pole. Kisha niliacha kwenda kwa matibabu ya vitobo, na nilimwomba Mungu siku zote tu, nikiukabidhi ugonjwa wangu mikononi Mwake, na kumwamini Mungu kuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu nitakapopata nafuu. Shukrani ziwe kwa Mungu! Kabla ya muda wa mwezi mmoja kupita, kiharusi cha uso wangu kilipona kabisa. Hata rafiki yangu alishangazwa na kusema kwamba katu hali yangu haingeweza kuwa imekuwa bora haraka hivyo. Nilijua kwamba Mungu alikuwa amenifungulia njia, na imani yangu kwa Mungu iliongezeka.

Muda fulani baadaye, nilihamia nchini Australia baada ya kuhamishiwa kwa kazi mpya. Baada ya kuwasiliana na ndugu kanisani, walikuja nyumbani kwangu kunisaidia kupakua maneno ya Mwenyezi Mungu na programu iliyohitajika kuhudhuria mikutano ya mtandaoni. Kilichonishangaza, mara nilipokuwa nimeipakua programu hii, ghafla na bila kutarajia nilianza kuhisi maumivu kichwani mwangu na mwili wangu wote ulitokwa na jasho mara moja. Nililala kwenye sofa haraka, nilikuwa nimedhoofishwa kabisa na nilihisi hasa kama nilikuwa nikivurugika. Ilihisi kana kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikimea kichwani mwangu, na nilishika kichwa changu kwa mikono yote miwili kwa ajili ya maumivu. Mmoja wa ndungu wa kanisa aliona hali niliyokuwa na alinipa ushirika haraka, akisema kwamba huyu alikuwa ni Shetani aliyekuwa akijaribu kunivuruga. Aliniambia nimwombe Mungu zaidi, nidumishe imani yangu na niwe na ushuhuda kwa Mungu, na nisidanganywe na njama za hila za Shetani. Kumbusho la ndugu huyo lilinifanya nigundue kwamba vita vya kiroho kwa mara nyingine vilikuwa vimeanza kwangu tena, kwa hivyo nilimkaribia Mungu haraka moyoni mwangu na kumsihi ndugu yangu anichezee masimulizi ya maneno ya Mungu ili niyasikilize. Kupitia kusali na kusikiliza maneno ya Mungu mfululizo, maumivu yalianza kupungua kidogo. Jioni hiyo, hata hivyo, maumivu kichwani mwangu yalizidi kuwa mabaya. Nilihisi kana kwamba kichwa changu kilikuwa karibu kupasuka, na maumivu yaliambatana na hisia ya kisulisuli ambayo ilinifanya kushikwa na kizunguzungu kiasi kwamba nilitapika. Nilikuwa na uchungu mwingi na mateso, na sikuweza kujizuia kulia, nikiwaza: “Nahisi kizunguzungu sana. Je, nitaendelea kuishi hadi mwisho wa usiku?” Kadiri nilivyozidi kuwaza kuhusu jambo hilo, ndivyo nilivyozidi kuogopa, na nilikuwa na wasiwasi sana kuwa ningezimia ghafla na kufa. Lakini nilijua kuwa mawazo haya yalikuwa Shetani akijaribu kunivuruga, na nilijua lazima nisimlaumu Mungu tena kama nilivyokuwa nimefanya hapo awali. Na kwa hivyo, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu, nateseka sana hivi sasa. Sijui ni kwa nini Shetani hawezi kuniachilia kamwe, na sijui ugonjwa huu utadumu kwa muda gani. Lakini sijutii kukuamini katika maisha haya, na bila kujali nitateseka kiasi gani, sitawahi kukulaumu, kwa ajili nina uhakika kuwa Wewe ndiwe Mungu wa pekee wa kweli, nami nitakuamini na kukuabudu!” Nilimwomba Mungu hivi moyoni mwangu tena na tena. Wakati huo huo, nilikumbuka ghafla mstari wa maneno ya Mungu: “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi” (“Sura ya 6” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalituliza msukosuko wangu, na yalituliza moyo wangu uliokuwa ukiteseka na usiotulia. Pia yalinionyesha njia ya utendaji: Ni kwa kuwa tayari tu kutoa maisha yangu ndiyo ningeweza kumwaibisha Shetani na kumfanya akubali kushindwa. Nilifikiria kuhusu jinsi nilivyokuwa nimethamini mwili wangu daima kwa kiasi kikubwa na nilikuwa nimechukulia maisha yangu kuwa ya maana zaidi kuliko kitu kingine chochote. Shetani alijua udhaifu wangu, na kwa hivyo alitumia ugonjwa wa mwili wangu kunivuruga na kunishambulia, akijaribu kunifanya nimlaumu Mungu na kumsaliti Mungu. Lakini baada ya kupitia majaribu na vurugu ya Shetani mara kwa mara, nilifahamu kuwa haya yote yalikuwa njama za hila zilizotumiwa na Shetani kujaribu kunizuia kuja mbele za Mungu, na kwamba pia zilikuwa njia ya Mungu ya kunijaribu. Kwa hivyo nilifanya azimio kwa Mungu: “Bila kujali jinsi Shetani anavyoweza kujaribu kunivuruga au jinsi mwili wangu unavyoweza kuteseka, nitashikilia imani yangu na kukufuata hadi mwisho kabisa!” Shukrani ziwe kwa Mungu, kwa kuwa nilipokuwa tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu hata kwa kupoteza maisha yangu mwenyewe, maumivu kichwani mwangu yalitoweka pole pole, na afya yangu imesalia nzuri tangu wakati huo.

Katika kipindi cha majaribio ya kila siku ya Shetani ya kunivuruga na kunijaribu, mwili wangu uliteseka kweli kwa kiwango fulani, lakini nahisi kana kwamba yote yalikuwa ya thamani na yenye maana. Kwa kupitia majaribu ya Shetani, niliona waziwazi sura mbaya ya Shetani ya uovu na yenye kustahili dharau, pamoja na ukweli wa jinsi anavyowadhuru na kuwaumiza watu. Niliona kwamba Shetani hutumia njia zote za hila, hata kutumia udhaifu wetu, ili kutushambulia na kutujaribu, akijaribu bila mafanikio kutufanya tumwelewe Mungu visivyo na kumlaumu na hata kumsaliti Mungu na kupoteza wokovu wa Mungu wa siku za mwisho. Shetani ni mwovu sana na mwenye kustahili dharau! Wakati wa matukio yangu, kila wakati nilihisi Mungu akiwa kando yangu, Akitumia maneno Yake kunipa nuru na kuniongoza, Akiniwezesha kuelewa mapenzi Yake, kufahamu njama za Shetani za hila na kuwa na imani ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu! Kwa kweli nilishuhudia ukweli kwamba hekima ya Mungu hutekelezwa milele kulingana na njama za Shetani za hila, na kwamba Mungu hutumia majaribu ya Shetani na njama zake za hila kutujaribu, na kukamilisha imani yetu Kwake na upendo wetu Kwake—kweli nimekuja kutambua vyema upendo ambao Mungu anao kwangu, na ninamshukuru na kumsifu Mungu!

Iliyotangulia:Maneno ya Mungu Yaliniongoza Nikipitia Majaribu ya Shetani

Inayofuata:Ni Nani Aliye Kizuizi kwenye Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni?

Maudhui Yanayohusiana

 • Kupenya Ukungu ili Kuona Mwanga

  Wakati tu nilipokuwa nikipoteza njia yangu, ilikuwa ni neno la Mungu lililoniongoza kubaini mpango wa Shetani, na kupenya ukungu na kuingia kwenye njia angavu na sahihi kwa uzima.

 • Nimepata Makazi ya Kweli

  Sasa, kila siku ninafurahia kunyunyiziwa na kukimiwa na neno la Mwenyezi Mungu. Maumivu ambayo nilihisi ndani yangu yametoweka, na nimepata mwelekeo katika maisha yangu na kupata uhuru na furaha ya kweli. Shukrani kwa Mungu kwa kuniokoa. Nitajitahidi kufuatilia ukweli na kutimiza wajibu wangu kama kiumbe kadiri niwezavyo ili kulipisha upendo wa Mungu!

 • Bahati na Bahati Mbaya

  Kama haingekuwa kwa ajili ya ugonjwa wangu ambao umenizuia kutafuta umaarufu na kupata, bado ningekuwa mashine ya kutengeneza fedha duniani. Ningekuwa kipofu kwa hili mpaka uharibifu wa Shetani uniue. Shetani alinidhuru mimi kwa kutumia umaarufu, faida, na magonjwa. Kinyume na hilo, Mwenyezi Mungu alitumia ugonjwa yangu kunileta mbele Yake. Kupitia kwa maneno Yake, niliona wazi kwamba Shetani anahusika na upotovu wa mwanadamu. Niliona pia wazi jinsi ilivyo vibaya na cha kudharauliwa kwa Shetani kutumia umaarufu na faida kuwameza watu. Hatimaye nilikuwa katika nafasi ya kutupa mbali pingu za umaarufu na faida na kuanzisha mtazamo sahihi wa maisha. Roho yangu iliwekwa huru. Mungu ni mwenyezi sana na mwenye busara!

 • Kutembea Katika Njia Ng’avu ya Maisha

  Kila siku ningekula, kunywa na kufuatilia anasa hadi nilipokuwa nimetosheka na moyo wangu ulikuwa umeridhika. Nilidhani kwamba ilikuwa tu kwa kuishi kwa njia hii ndiyo maisha yalikuwa na maana yoyote, na hiyo ni mpaka nilipopokea kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Ni baada tu ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu ndipo nilipata utambuzi wa maisha muhimu kwa kweli ni yapi, na kisha nilianza kutembea katika njia ng’avu ya maisha.