Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

37. Hekima Kubwa Mno ni Kumwinua Mungu na Kumtegemea Yeye

Lingxin    Mji wa Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei

Siku chache zilizopita, nilisoma kifungu kutoka "Njia ya Kuingia Katika Uhalisi" katika Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia Katika Maisha (IV): "Kwa mfano, sasa kuna mtu ambaye amechukua mzunguko mbaya. Kutumia hili kama hoja ya kuzungumza ili kuwasiliana ukweli, ungefanyaje hivyo? ... Kwanza, unapaswa kushuhudia kazi ya Mungu, kushuhudia jinsi Mungu huwaokoa wanadamu. Kisha, unaweza kuzungumza juu ya kama barabara anayotumia inaongoza kwa wokovu wa Mungu, kama anaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu, na kama hii ni barabara ambayo Mungu huikubali. Hivyo, kwanza unashuhudia kazi ya Mungu, na kisha ushuhudie barabara ambayo Mungu anatuongozea, yaani, barabara ya wokovu. Mwache aone upendo wa Mungu na wokovu Wake, na ni hapo tu anapoweza kufuata njia sahihi. Ili kutatua tatizo hili, ni sawa kwako kutomshuhudia au kumwinua Mungu? Kama unaongea tu kuhusu ni barabara ipi inayoelekea kwa wokovu na barabara ipi ambayo hailekei kwa wokovu, lakini hushuhudii kazi ya Mungu, bado unazungumzia tu mafundisho. Hata hivyo, ukishuhudia kwanza kazi ya Mungu, kisha uzungumzie barabara hizi mbili, basi huongei tena juu ya mafundisho." Niliposoma maneno haya, nilikanganyika ndani. Katika moyoni mwangu niliwaza: Njia zote mbili zinazungumzia jinsi mtu anavyopaswa kutenda ukweli. Kwa nini ile isiyotaja kazi ya Mungu inaongea juu ya mafundisho, lakini ile ambayo inazungumzia kazi ya Mungu na kisha inataja vitu hivi haiongei juu ya mafundisho? Nilipokuwa nikizingatia jambo hili, niliwaza juu ya hadithi iliyo katika Biblia ya Daudi akilishinda jitu la Kifilisti, Goliathi. Wakati huo, Daudi kwanza alimwinua Yehova, kisha akavurumisha jiwe, na hatimaye akamshinda Goliathi. Kama Daudi hakuwa amemwinua Yehova wakati huo, na akaendelea tu na kuvurumisha jiwe moja kwa moja, angeweza kumshinda Goliathi? La hasha. Hii ni kwa kuwa sababu tu Daudi aliweza kumshinda Goliathi ilikuwa kabisa ni kwa sababu alimwamini Yehova, alimtegemea Yehova, na kwa sababu Yehova alimsaidia. Kama hakumwinua Yehova, hangeweza kupata msaada wa Yehova. Bila kujali ujuzi wake mkubwa wa kuvurumisha mawe, hangeweza kumshinda Goliathi. Ninapofikiri juu ya hili, ghafla inakuwa wazi moyoni mwangu. Sababu Mungu huwauliza watu kumwinua na kumtegemea sio kuwauliza watu kuzingatia sheria au mila, lakini badala yake ni kuwa na mahali pa Mungu katika mioyo yao, kumheshimu Mungu kama mkuu zaidi katika mioyo yao. Kama mtu kwa uhalisi humruhusu Mungu kuinuliwa na kumtegemea, hili huonyesha kwamba ana mahali pa Mungu na anaweza kumheshimu Mungu kama mkuu zaidi katika moyo wake. Kwa njia hii, watu wanapokwenda mbele ya uso wa Mungu wanaweza kupata furaha na baraka Zake, na Roho Mtakatifu atafanyia kazi ndani yao. Kazi yote wanayofanya haitategemea matendo yao wenyewe, bali mwongozo wa Mungu wa kazi zao. Na athari itakuwa nzuri kwa kawaida. Kama mtu hamwinui Mungu na kumtegemea, hili linaonyesha kwamba moyo wake hauna mahali pa Mungu, na kwamba kila kitu anachokifanya ni kwa sababu ya kazi yake mwenyewe. Mtu kama huyo ni chukizo kwa Mungu na hakika hawezi kupata baraka zake au kupata kazi kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hivyo, kazi yake haitakuwa na ufanisi. Wakati huu, siwezi kujizuia kushangaa: Je, udhaifu wa moja kwa moja wa matendo yangu ya ukweli unahusiana na ukweli kwamba mimi simwinui Mungu au kumtegemea katika kila kitu nikifanyacho? Nikikumbuka miaka ya nyuma, naona kwamba sala zangu mbele ya Mungu na njia yangu mwenyewe ya kutenda ukweli vilikuwa vimetangulika kabisa. Katika kutenda ukweli, ni mara chache sana nilipomtumainia Mungu au kumtegemea. Kwa kuitegemea nguvu yangu mwenyewe kutenda ukweli, sikuweza kupata msaada kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hii ndiyo sababu mambo daima yalionekana kuwa magumu hasa, yenye kutumia nguvu nyingi na sikuweza kuona matokeo tofauti.

Tangu wakati huo, nimeanza kuzoea kumwinua Mungu na kumtegemea Yeye katika kila suala katika maisha halisi. Kila asubuhi ninapoomba, mimi hujiweka kikamilifu mikononi mwa Mungu, nikimruhusu Mungu awe na udhibiti kamili juu ya maisha yangu siku hiyo. Kuhusu jambo muhimu la wokovu wangu mwenyewe, nitadiriki kikamilifu kwa sala na kumtegemea Mungu. Sijui kile ninachokosa au kile ninachohitaji. Hata hivyo, kila kitu ni wazi sana kwa Mungu. Ananielewa vizuri zaidi. Mungu anajua vyema sana ni mazingira gani ninayoyahitaji katika ukimbizaji wangu wa wokovu, kile ninachohitaji ili kuwa na uzoefu, kile ninachohitaji kuingia ndani. Kwa hivyo, ninajitoa kabisa katika mikono ya Mungu, kumruhusu Mungu "kunichonga" na kunidhibiti. Ninataka tu kuwa mtu anayemtii Mungu, na kufuata mwongozo wa Mungu kwa njia ya wokovu. Aidha, katika kila jambo katika maisha halisi, nitamtegemea Mungu kwanza, kumruhusu Mungu aende mbele yangu kuniongoza, na nitafuata baada Yake, kufuata mapenzi ya Mungu katika neno langu na tendo langu lote. Baada ya muda fulani, niliona kwamba sikupitia kila siku kama nafsi yangu ya zamani iliyochanganyikiwa. Sasa wakati ninapokabiliana na jambo fulani, najua ni kipengele kipi cha kweli ambacho ni lazima nikitende, ni kipengele kipi cha uhalisi ambacho ninapaswa kukiingia, na kile mapenzi ya Mungu yalicho. Yote haya yako wazi zaidi kuliko hapo awali. Bila kujua, ninaweza kutenda ukweli fulani kwa urahisi. Kwa mfano: Katika kipengele cha kuutuliza moyo wangu mbele ya Mungu, ingawa kabla pia nilitaka kuwa mtulivu nilipokwenda mbele ya Mungu, siku zote nilihisi kama moyo wangu haukuwa chini ya udhibiti wangu mwenyewe, na bila kufahamu ulikuwa unamilikiwa na vitu visivyo na maana . Wakati mwingine hata wakati nilipokuwa nikihariri makala, mawazo yangu yangeweweseka, na sikuweza kuyadhibiti. Leo, silazimiki kujitahidi sana ili kujidhibiti. Bila hata kujua, matukio ya wakati moyo wangu umemilikiwa na vitu vya nje yamepungua. Ingawa mawazo yangu bado yanaweweseka mara chache, naweza kutambua mara moja, na ni rahisi kwangu kuyarejesha mawazo yangu. Katika kipengele cha kujijua mwenyewe, awali pia nilitaka kufanya maendeleo kiasi kila siku, nikijijua mwenyewe kidogo zaidi. Hata hivyo, daima nilishindwa kushikilia mawazo yangu ya ndani. Daima nilisahau kuyadhibiti ili nijijue mwenyewe. Mara nyingi usiku nilifikiria, "Nimeshindwaje kujijua mwenyewe tena leo?" Kwa uendelevu kila siku niliishi jinsi hii bure. Sasa, wakati wowote fikira fulani zinapoonekana katika mawazo yangu, ni rahisi sana kwangu kuzidhibiti. Baada ya kutambua fikira hizi, nitamwomba Mungu ili kujijua mwenyewe vizuri, na moyoni mwangu ninajichukia hasa, na nina nguvu za kuunyima mwili wangu. Wakati ninapokabiliwa na mazingira fulani, najua pia kwamba Mungu hutumia mazingira haya kufichua kipengele ambacho kwacho mimi ni mpotovu au nina upungufu. Kisha, nitajiandaa mwenyewe na ukweli katika kipengele hiki. Kuhusu kipengele cha kutimiza wajibu wa mtu badala ya kufanya tu kiwango cha chini kabisa, katika siku za nyuma nilipofichua mwelekeo wangu bila kusudia mintarafu ya kufanya tu vya kutosha ili kwendelea kuishi, wakati mwingine mimi mwenyewe sikuwa na ufahamu. Wakati mwingine nilikuwa na ufahamu, lakini sikulenga kulitatua kabisa. Sasa, wakati nina mwelekeo huu moyoni mwangu, nina utambuzi katika moyo wangu. Kisha, kwa njia ya maombi ninaweza kugeuza hali hii ndani yangu. Ninafahamu kwa kina kwamba haya yote hutokana na Mungu kuniongoza na kunifungua. Ni kwa njia tu ya Roho Mtakatifu kunipa nguvu ninapofanikisha hili. Utukufu wote unaenda kwa Mungu!

Baada ya utambuzi huu, nilielewa kwamba sababu ya kuhisi kuwa ilikuwa vigumu kutenda ukweli katika siku za nyuma ilikuwa ni kwa sababu nilijitegemea mwenyewe kabisa kutenda ukweli, nilijitegemea mwenyewe kutembea kwa barabara ya wokovu. Sikuwa na nafasi yoyote ya Mungu ndani ya moyo wangu, katika uzoefu wangu sikutenda neno la Mungu, wala sikupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Kama vile tu Mungu amesema: “Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu” (“Njia… (5)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kufunuliwa kwa neno la Mungu huniruhusu kuelewa kwamba waumini wanaofuatilia wokovu hutegemea kazi ya Roho Mtakatifu, wote ni wale wanaoongozwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao hujitegemea wenyewe hawatafanikisha. Katika siku za nyuma, sikumtegemea Mungu kabisa, kumtazamia, wala sikutafuta uongozi wa Mungu. Nilimrusha Mungu kando, na kwa upofu nikafanya chochote nilichotaka kwa nguvu zangu mwenyewe bila matokeo yoyote. Pia nililalamika kwamba kumwamini Mungu na kutenda ukweli kulikuwa kugumu sana. Sasa najua kwamba ni kwa sababu "sikumwamini" Mungu. Neno la Mungu linasema: “Binadamu ana uwezo wa kufanya nini? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe? Mbona Ninasema kwamba Mimi binafsi Nateremka mahali ambapo vita hujiunga? Kile ambacho Nataka ni imani yako, si vitendo vyako” (“Tamko la Kumi” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). “Bora tu uutoe moyo wako kwa Mungu na kutii uongozi Wake, yote yatafaulu. Mbona unadhani ni vigumu sana?” (“Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika Ndio Wanaoingia Katika Uhalisi wa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ukitazama nyuma kwa Waisraeli waliotoka Misri, si ni Mungu binafsi aliyekuwa akiwaongoza? Waisraeli hawakufanya chochote; walipaswa tu kufuata nguzo ya wingu na moto. Njiani, matatizo yote waliyokabiliwa nayo yaliondolewa na Yehova Mungu mwenyewe. Je, si barabara ya leo ya wokovu ni kama ile ya Waisraeli wakikimbia Misri? Mungu hutuhitaji tu kuwa na imani Kwake, kumtazamia Mungu, kupeana moyo wetu mwenyewe kwa Mungu na kufuata uongozi wa Mungu. Kwa njia hii, watu wanaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Mara Roho Mtakatifu anapoanza kufanya kazi ndani ya mtu, ni rahisi sana kwake kutenda kipengele chochote cha ukweli. Kwa sababu ni Mungu Mwenyewe ambaye angepigana na Shetani, ni neno la Mungu ambalo hubadili tabia yetu ya ndani ya kishetani. Hili haliwezi kufanikishwa kupitia kwa kazi yetu. Baada ya kuelewa haya, imani yangu kwa Mungu ilikua kwa upeo mkubwa. Ingawa sasa bado nina kuingia kwa juu juu sana tu katika vipengele mbalimbali vya ukweli, naamini kwamba almradi naendelea kumwinua Mungu na kumtegemea Yeye, Mungu ataniongoza katika ukweli wote na hatimaye nitafanikisha wokovu!

Asante Mungu kwa kunifungua na kwa uongozi Wake, kuniruhusu nielewe kweli kwamba hekima kubwa mno ni kumwinua Mungu na kumtazamia katika kila uzoefu wangu. Ni kwa njia ya kumwinua Mungu na kumtegemea Mungu tu ndipo mtu anaweza kupata uzoefu wa kazi ya Roho Mtakatifu. Mtu anaweza kutenda ukweli kwa urahisi na kufuatilia wokovu na kazi ya Roho Mtakatifu tu. Wakati huo huo, Mungu alinisaidia kutambua mkengeuko wangu wa mauti kwa njia yangu ya kumwamini Mungu—kukiri imani yangu kwa Mungu kwa mdomo wangu, lakini nikikosa Mungu katika uzoefu wangu. Katika siku za nyuma, nilijitegemea mwenyewe kuitembea barabara ya wokovu, nilijitegemea mwenyewe kufanya chochote nilichotaka kufanikisha. Miaka kumi ya majaribio ilithibitisha kuwa nilikuwa kwa njia ya kushindwa. Kuanzia sasa na kwendelea, niko radhi kuacha njia yangu ya zamani ya kumwamini Mungu na njia ya kupata uzoefu wa Mungu. Nitatenda ukweli kulingana na njia mpya ya kupata uzoefu wa Mungu, kupitia mwongozo wa Mungu kutembea njia iliyobaki. Nitamtegemea Mungu kutenda neno Lake, kuelewa ukweli, na kuamini kwamba Mungu kwa hakika ataniongoza katika uhalisi wa ukweli.

Iliyotangulia:Mateso na Maafa Yalinisaidia Kukua

Inayofuata:Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Unaweza Pia Kupenda